Header Ads Widget

Responsive Advertisement

MY STORY; MUME WANGU AMENIACHA ANADHANI NILITAKA KUMUUA!

Mwaka jana mwezi wa 9 nilipigiwa simu na mwanamke ambaye simjui, alianza kwa kuniuliza mimi ni nani mbona nampigia simu mume wake usiku. Nakumbuka mume wangu alikua kasafiri kikazi, aliniaga hivyo, lakini nilikuja kugundua kuwa alikua hajasafiri kikazi bali alikua kwa mwanamke wake. Mimi ndoa yangu ina miaka 7, huyo dada alijitambulisha kama mchumba wa mume wangu na kuniambia kuwa mume wangu alishajitambulisha mpaka kwao.
Kwanza nilishtuka, kidogo nimtukane lakinia likua akiongea kistaarabu kuwa mume wangu alimdanganya kuwa hajaoa lakini alishangaa kuwa anaona picha zangu wakati alimuambia kuwa kuna mwanamke kaza anaye lakini hawaishi pamoja. Aliniambia mambo mengi kuhusu mume wangu, namna wlaivokua wanachepuka, jinsi walivyopanga mipango mingi na namna ambavyo mume wangu alimuumiza.
Kusema kweli niliumia sana, mume wangu alikua kaniumiza, kwani nilimuamini sana. Tuliongea sana na yule dada kiasi kwamba baad aya hapo tulikua marafiki, aliniambia nimfuatilie mume wangu vizuri kwani anahisi kuwa ana mwanamke mwingine ndiyo maana kabadilika. Ghafla tukawa kama marafiki, ingaw anilikua simuamini lakini tulikua tunachart sana, akawa ananiambia mambo mengi sana ya mume wangu amabyo mimi nilikua siyajui.
Aliniambia kuwa mume wangu anajenga sijui wapi, akanitumia na picha za nyumba, akaniambia kuwa mara nyingi akisafiri anaenda kwa wanawake zake. Nilitaka kumuambia mume wangu lakini aliniambia kuwa kama nikimuambia mume wangu lazima atakataa, aliniambia nilazima tufanye kitu, tupange mipango ili mimi na yeye tumfumanie mume wangu na mwanamke mwingine na kumuambia kuwa tumeujua ukweli. Wazo lake lilikua sawa, aliniambia kuwa kwakua mume wangu hapokeis imu zake tena na hataki waonane basi mimi ndiyo nifuatilie simu zake na kuona madudu yake.
Mimi nilikua sina password ya mume wangu, alinipa nikawanafuatilia nyendo zake, kweli mume wangua likua kapata mwanamke mwingine na walikua wanakutana mara kw amara. Kila nilichokua nakiona kwenye simu ya mume wangu nilimuambia, tulichart tangu kipindi hicho mpaka mwakajana mwisho ndiyo aliniambia kuwa tupange kumfumania mume wangu. Mume wangu aliaga kuwa anaenda safari ya kikazi Mwanza.
Nakumbuka ilikua ni tarehe mbili, lakini kiuhalisia alikua anachart na huyo mwanamke wake kuwa anaenda Bagamoyo na hoteli alitaja. Yule mwanamke aliniambia anaifahamu hiyo hiteli kwani mume wangu anampelakaga sana, alinishauri kuwa siku hiyo mimi niongozane naye ili kwenda kumfumania, alikua anafahamu nyendo zote za mume wangu, sheemu anazopita, kula na kunywa. Kweli siku hiyo tulipanga, tukaenda Bagamoyo.
Hakuniambia kitu chochote zaidi ya sisi kwenda kumuona mume wangu na kumfumania ili tumkomeshe yeye na mwanamke wake. Kweli tulienda mpaka kwenye ile hoteli, kuna watu alikua anajuana nao, akatoa pesa kidogo mpaka tukaruhusiwa kuingia, tukaenda mpaka kugonga kwenye chumba cha mume wangu. Lakini wakati anagonga anajifanya mhudumu sijui yule dada alipotelea wapi! Ghafla walikuja vijana watatu kama mabaunsa hivi.
Ile mume wangu anafungua mlango kuchungulia waliukanyaga mlango, wakamvamia mume wangu na kuanza kumpiga. Kweli mume wangu alikua na mwanamke mwingine, walimpiha mume wangu sana, mpaka nikamuonea huruma, hawakuishia hapo, walimvua nguo, wakamchukua video na kutaka kumuingilia kinyumke na maumbile. Hapo nilishindwakuvumilai, nikaanza kupambana nao huku nikipiga kelele, walipoona kuwa kelele zimezidi walimuachia mume wangu na kukimbia.
Lakini tayari walishamuumiza mume wangu sana, watu walikuja mume wangua kachukuliwa na kupelekwa hospitali. Ile natoka namtafuta yule dad ahapatikani, namba yake haipo hewanzi. Kusema kweli nilichanganyikiwa, nilienda hospitalini kumuona mume wangu lakini hakutaka kuniona, alikua kakasirika akisema kuwa nataka kumuua kwasababu ya wivu wa kijinga. Kusema kweli sikua naelea chochote, mimi nilijua kuwa tunaenda kumfumania mume wangu basi kumbe mume wangu aliamuia kunifanyia vile.
Nilirudi nyumbani nikiwa nimechanganyikiwa, sikumuambia mtu yoyote, baada ya siku mbili mume wangu aliruhusiwa, aliporudi nyumbani alichukua Mabegi yake na kila kitu chake akaondoka, hakutaka tena kukaa na mimi, aliniita muuaji, nilijaribu kumuelezea lakini hakunisikiliza, alikua ananiambia kama niliweza kumpeleka watu ili wamuue kwanini nishindwa kufanya mimi mwenyewe. Mume wangu aliondoka aliwapigia simu wazazi wangu kuwa ameshaachana na mimi hivyo waje kuchukua mtoto wao.
Alikaa kama wiki mbili hivi bila kujua kuwa yuko wapi na nini iimetokea, aliwaambia ndugu zake kila kitu, walinipigia simu kunitukana na kuniambia kuwa hawanitaki. Mama yangu alikasirika, baba yangu alikasirika zaidi, kila mtu alikua ananiona kama mnyama kutaka kumuua mume wangu. Nilijaribvu kuomba msamaha lakini mwezi wa pili tarehe 1 mume wangu alikuja na kunipa talaka yangu akiniambia kuwa hanitaki tena.
Kibaya zaidi Kaka yule mwanamke ambaye aliniambia kuwa tumuumbue mume wangu naona sas ahivi yuko bize kumpost mume wangu nakumtakia pole. Kaka namuona tu kwenye mitandao instagram lakini simu yake haipatikani. Ninampenda sana mume wangu, pamoja na mapungufu yake lakinia likua anajali familia na hakuwahi kunionyesha kuwa anachepuka na kunidharau, nashindwa hata nianze wapi maisha bila mume wangu, kila mtu ananiona mnyama wakati si kweli kwamba nimejaribu kumuua mume wangu.
MWISHO

Post a Comment

0 Comments