Header Ads Widget

Responsive Advertisement

HUYU MWANAUME ANAKUTUMIA KUMNYANYASA MKE WAKE LAKINI HATAKUOA!

Uko kwenye mah8usiano na mwanaume, ni mume wa mtu, wanaweza kuwa wamefunga ndoa ya kidini au kiserikali au hawajafunga ndoa lakini wanaishi pamoja. Unachepuka naye, kwanza kabisa wakati anakutongoza alikuambia matatizo ya mke wake, alikua anamponda sana, mistari wanayopenda kutumia ni Mke wangu hana akili hatuwezi tukakaa tukapanga kitu cha maendeleo.
Mara anakuambia kuwa mke wangu ni mchafu, hawezi kufanya usafi, ana kisirani, anapenda kulalamika. Kwa kifupi yaani anakutongoza wewe lakini kila dakika anamtukana mke wake, anamdhalilisha kwako mpaka unawaza hivi huyui Babaa lioa mwanamke au Ngurue! Haishii hapo, anakuambia kuwa mke wake ni Malaya, hamtaki, hapendi ndugu zake na ujinga ujinga mwingi.
Anakuambia kabisa kuwa angemuacha lakini shida ni watoto, ana mpango wa kumuacha taratibu. Lakini sasa, kuna tatizo moja tu, huyu mwanaume mkifanya mapenzi, nataka nirudie, mkifanya mapenzi goli lake ni moja tu na yakija mawili ni ya shida sana, lakini saa hilo goli moja haliendi zaidi ya dakika tano. yaani yeye kila saa ni kazi nyingi, mke wangu ananichanganya, mara hivi mara vile, mara mgongo mara kiuno!
Dada yangu, huyu mwanaume hata kama wewe anakuridhisha lakini ana tatizo la nguvu za kiume, labda niseme kuwa, anaamini kuwa ana tatizo la nguvu za kiume, hajiamini hivyo anachepuka kwakua anahisi mke wake anamdharau. Anachepuka ili kuonekana Malaya, mwanaume huyu alishajiaminisha kuwa ili kuwakidume ni lazima kwenda raundi mbili au tatu na kwenda dakika mpaka 30.
Kwa maana hiyo hajiamini, anahisi watu wanajua, watu wanamdharau hivyo anapenda kuwa na wanawake wengi ili kuonekana Malaya na rijali. Tena mwingine anakupa na simu umpigie na kumtukana mke wake, unampigia simu usiku anapokea mke wake yupo. Basi dada yangu huyo mwanaume hamuachi mkewe, hamuachi kwakua anampenda ila anamdhalilisha kwakua yeye hajiamini.
Hamuachi kwakua anajua akimuacha mke wake anaweza kumtangaza na kumdhalilisha, hamuachi kwakua anampenda, hamuachi kwakua anajua kuwa akimuacha akakuoa wewe basi nawewe hutaridhika utamuacha na ataonekana kuwa yeye ndiyo mwenye matatizo hivyo kudhalilika, hamuachi kwakua ana wanawake wengi, hauko peke yako na wote mnaamini kuwa anamchukia mke wake atamuacha, ila imekula kwenu.

Post a Comment

0 Comments