Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Nikwambie Kitu

Related image

My lovely sister, mwanaume bora na sahihi kwako hua hata ha-propose relationship. Siku zote hukukuta ukiwa busy na mambo yako na hukusaidia kufanya vizuri zaidi kwenye hayo mambo yako.
:
.
Ni mfano kama wa bacteria, huwezi jua ni lini wameingia mwilini mwako, nae huingia katika maisha yako from nowhere, utajikuta tu unamiss kuwa karibu nae. Mwanaume alie bora hua haingilii na kuharibu chochote katika maisha yako..iwe kiroho, kimwili na hata kiuchumi!
:
.
Huwa haji kama Boyfriend, huja kama rafiki tu na mwishoe hujikuta mmefika milestone katika mahusiano!
:
.
Hata siku moja hua hatangazi kusudio lake la kukuoa, hua haji na bango kichwani lililoandikwa "NIMEKUJA ILI NIKUOE". Wanaume waoaji huwa hawana mbwembwe kabisa.
:
.
Uliza yeyote yule aliyepo kwenye ndoa iliyo na furaha, atakueleza namna walivyofahamiana na huyo mume wake....
:
.
Mwanaume sahihi ni yule ambae unamiss uwepo wake..ni yule mwanaume ambae ukiwa peke yako unawaza kwamba "I wish he was here, he would have..... " My beloved sister huyo ndio mwanaume sahihi kwako!
:
.
Sio yule ambae ukiona anakupigia simu mapigo ya moyo yanaenda kasi kwa hofu, sio yule ambae kila mkiwa pamoja lazima mgombane kwa issue ya usaliti, sio yule ambae kila mkigombana kidogo anatishia muachane, sio yule ambae kila siku unalilia na kubembeleza mahusiano...that's not your man. Huyo ni mwanaume wa mwanamke mwingine.
:
.
Mwanaume sahihi kwako huja na impact chanya kwenye maisha yako, huacha alama katika maisha yako ambayo hauwezi kuisahau, sio kuisahau kwa maumivu, la hasha..ni alama inayoakisi mapenzi, faraja, na matumaini! :
.
Look around your circle and you will see this guy. He is already within reach .
Nimemaliza dia kazi kwako kama umenielewa sema #noted

Post a Comment

0 Comments