Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Wanaume mpooo!!! UNANGOJA,JIBU,! NIPE MUDA.

Related image


Ni pale unapoangaika nae sana,majibu nipe muda,nafikilia.
Kesho,imekuwa miezi mpaka miaka.
Kisingizio nafikilia.
Kesho nafikilia.
Mwezi nafikilia.
Mpaka mwaka.
Bado unajipa moyo.

CHA AJABU
Shida zake anakuhusisha,anaomba msaada wako.
Ndio ushapenda unangoja majibu,ila ni kesho kesho siku zinaenda.
Na unatumika,vocha,pesa ya Saloon na huduma zingine Zote.

IPO HIVI.
Si kwamba hana majibu ya ndio au hapana.
Tatizo kwanza huna nafasi kwake bali kuna mtu amemuweka moyoni nae kama aeleweki.
Anachoifanya ni kukuweka wa akiba,huyu akiteleza anajishikiza kwako,,Mwanaume huu ni utapeli km wa cheni ya bandia na noti ya bandia.

Shiida ni tamaa,anakula huku na huku,kuachilia upande mmoja anaona kukosa woote.
Tamaa ya vitu,pesa na anaweza kuwapanga foleni wanaume hata wa3 wa4 na amjuani,mmoja amepewa nafasi wa3 wangoje,wampe muda na vyao anakula.

HITIMISHO.
Mwenye mapenzi ana maamuzi ya papo kwa papo hata kama ni kungoja sio miezi,hata akisema sipo tayari ni upendo,anauelezea uhalisia wake,apendi kukupotezea muda,pokea hata kama una maumivu,vumilia kubali kistarabu.
Ustarabu wako ni moja ya sifa kwake,usishangae kupokea kwako kwa busara kwa mtu wake akajichanganya nafasi ikarudi kwako,inatokea.

Wanawake kwa wanaume,kama huna nia nae mwache ajitafutie lidhiki yake mbele ya safari,umjali,umpendi,umthamini,tamaa tu ya vitu,ya mwili,waachieni wenye upendo wa dhati wawatumie kwa haki,halafu wanazuga kuwa na wiiiivu saaana kumbeeee zuga tu.

Kama huna malengo naye usile vyake.. Kama utafanya kula vyake afu huna nia naye maana kuna wengi sana wanaumia leo kwa sababu waliwanfanyia wengine unyama.. MAANA MALIPO NI HAPA HAPA DUNIANI.
mabinti mpo?

Post a Comment

0 Comments