Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Kisa cha binti wa kazi

Mama mmoja aliishi na mumewe vizuri,alishika mimba na kufikiria kutafuta mfanyakazi wa ndani, hivyo alienda kijijini na kumchukua binti mmoja aliyekua mpole tu.
Yule mama aliishi na binti huyo kwa muda mrefu, na muda mwingi binti huyo alikua akimlelea mtoto wa yule mama kama wake.
Baada ya miaka minne, mtoto akiwa anasoma shule, huyu mfanyakazi wa ndani alikua akifatilia maisha ya huyu mtoto na kwenda kumchukua kila siku shule. Mtoto alimpenda sana huyu mfanyakazi.
Siku moja, huyu mama akiwa anarudi nyumbani na gari, alipofika getini akamuona yule mfanyakazi wa ndani amesimama na kijana wa jirani yao, yule mama hakupenda kitendo hicho.
Binti alivyomuona mama amerudi, alikimbia ndani na kumuaga yule mwanaume. Alivyoingia ndani alimkuta yule mama akiwa na hasira sana na kuanza kumwambia “sijakutoa kwenu uje kufanya mapenzi hapa, nimekuleta uje kufanya kazi basi..”.
Yule binti wa kazi akamwambia mama kua yule mwanaume ni mpenzi wake na alitaka amuoe na yeye yuko tayari.
Ila mama alitupilia mbali hoja ya binti huyo na kumpiga marufuku kuonana na huyo kijana.
Binti hakuishia hapo, alienda na kuongea na baba wa nyumba na kumwambia kua kuna kijana amempenda na alitaka kumtolea mahari na kumuoa, yule baba alifurahi na kumwambia ni sawa, lakini mama alikataa kabisa.
Binti alifikiria sana kwanini mama anamkataza asionane na mpenzi wake lakini hakupata majibu.
Siku nyingine tena yule mama aliwaona yule dada wa kazi na yule mvulana wamesimama sehemu, sasa yule mama alichokifanya akasubiri wameagana, kisha baadae akaondoka na kwenda mpaka kule kwa jirani anapokaa huyo mvulana na kumsema aachane na huyo binti maana hakuja mjini kufanya mapenzi na iwe mwanzo na mwisho kuonana nae.
Yule kijana baada ya kufanyiwa hayo, alikata mguu kuonana na yule binti na ile mipango yake yote akaifuta kabisa.
Binti aliumia sana kwa kitendo alichokifanya huyo mama. Na ghafla asubuhi yake, alishtukizwa kuona begi lake limeandaliwa na yule mama kisha mama akamwambia leo tunakurudisha nyumbani kwa tabia zako mbaya na tutaleta mfanyakazi mwingine.
Wakati yule binti akiwa hana hili wala lile ikasikika hodi, na alipokelewa dada wa kazi mwingine, kisha yule mama akaanza kumwambia yule binti ajiandae apelekwe stand ya mabasi.
Binti alimuangalia na baba, lakini baba alikua upande wa mama, basi kwa huzuni kubwa ya kumkosa mtu aliyetaka kumuoa, binti alijiandaa na kupandishwa bus la kurudi kwao kijijini.
Zilipita siku tatu, yule binti akaenda shuleni kwa mtoto wa yule mama, akawahi kipindi anatoka ili amchukue mtoto kabla ya yule dada mpya kuja kumchukua.
Binti alimchukua mtoto shuleni na yule mtoto alikua hajui chochote kuhusu kufukuzwa kwa huyu dada, basi wakawa wanarudi njiani na yule dada akamnunulia juice na ice cream.
Wakafika nyumbani kisha yule binti akagonga mlango, yule dada mpya akafungua mlango na kushangazwa kumuona kumuona yule binti aliyefukuzwa siku ile, akamwambia ” wewe si ulirudishwa kwenu?” , yule binti akamjibu “nimemkuta huyu mtoto anazurula huko nikaamua kumrudisha nyumbani” kisha akaondoka zake na kuwaaga.
Yule mtoto akaingia ndani na haikuchukua dakika mtoto akaanza kutapika, yule binti mpya akiwa haelewi hili wala lile, mtoto akaanguka na kuanza kutokwa na damu mdomoni, binti alipiga kelele kwa msaada na majirani wakaja pale na kugundua kua mtoto amepewa sumu. Wakamuwahisha hospitali na kuwataarifu wazazi wake.
Lakini walivyofika hosipitali mtoto alifariki dunia. Na kutokana na maelezo ya yule binti mpya wote wakajua kua yule binti wa zamani ndo kampa sumu mtoto wao.
Kabla hawajaenda polisi kuanza kumtafuta yule binti. Mama alipokea ujumbe wa mesage usemao “niliwapenda nyie kama familia, lakini hukutaka mimi nipendwe na mtu mwingine, nilimlea mtoto wenu kama wangu, nilimfuta kinyesi na kumuogesha, nilimpeleka shule na kumrudisha, lakini hukuona hata huruma kwamba nimempata mtu aliyekua na malengo na mimi ya kunioa na alikua na malengo ya kuniendeleza kimaendeleo, lakini wewe ukaamua kuniumiza kwa kunipotezea mwanga wangu na furaha yangu. Basi na mimi nikaona nikuondolee kitu ukipendacho, na msijihangaishe kunitafuta maana hata mkija kwetu mtakuta msiba wangu. Bye” .
Yule mama alichanganyikiwa na kujafibu kuipiga ile simu lakini asiipate, wakaenda polisi na kumtafuta na kuambiwa kua yule binti alifariki dunia.
Majonzi yalitanda sana na maumivu ya kila namna.

Post a Comment

0 Comments