Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Simulizi ya kweli

****JIFUNZE KUPITIA SIMULIZI HII YENYE MAFUNZO  ITAKUSAIDIA HUKO MBELENI UENDAKO***
Julieth alipata ujauzito miaka 10 iliyopita akiwa bado ni mwanafunzi wa secondary,
Kijana aliyempatia ujauzito akamkana na kuamua kutokomea kusikojulikana.
Kwa kuwa Julieth hakutaka wazaz wake wajue kuhusu mimba aliyobeba akaamua kutoa mimba lakini ikashindikana,
Akajaribu njia zote ili kuharibu mimba lakini bado ikashindikana
Baadae akaamua kutorokea kwa rafiki yake aliyekuwa akiishi mji wa mbali
Akakaa huko mpaka siku alipojifungua.
Siku mbili baadae alikwenda kumtupa mtoto katikati ya msitu na kuamua kurudi kwa wazazi wake.
Siku kama ileile ikiwa ni miaka kadhaa baadae Julieth alikuja kuolewa na mwanaume wa ndoto yake na wakaishi maisha ya furaha na amani
Lakini mpaka wanafikisha miaka mitano ya ndoa yao Julieth alikuwa bado hajapata mtoto
Mume wake akampeleka kwa madaktar ili kujua nini tatizo na madaktari wakasema kizazi cha Julieth hakina tatizo lolote na kuwataka waendelee kuvumiliana.
Walisubiri na kusubiri bila mafanikio yoyote mpaka siku mtabiri mmoja alipowaambia ukweli kwamba Julieth hawezi kupata mtoto kwa sababu ya kile alichomtendea mwanae wa kwanza wa kumzaa.
Mume wa Julieth baada ya kusikia hayo na kujua kwamba Julieth hawezi kumzalia mtoto akaamua kumfukuza nyumbani na kisha kuoa mke mwingine.
--------------------------------------------------------------------
BUSARA YANGU:
-Ewe dada usitoe mimba /usitupe mtoto maana nindhambi mbele za Mungu
-Ewe kijana mwenzangu mwanaume rijali hakatai mimba
Mwanaume rijali hakwepi majukumu bali mwanaume rijali ni yule anapambana mpaka dakika ya mwisho
MWISHO:  Nikupongeze wewe dada/mama uliyekubali kulea mimba yako na hatimaye kujifungua na kumlea mtoto wako hata baada ya mpenzi wako kuikana mimba yeke ama kukuteleleza.
MAOMBI: Ee mwenyezi Mungu tusamehe kwa madhambi yote tuliyotenda pasi na kujua hatima yake.
Turehemu na utuongoze ktk njia zenye kukupendeza wewe tusije kutenda kinyume na mapenzi yako tukaharibu future zetu.
Ungana na mm ktk sala hii kwa kusema *AMEN*
       #Share

Post a Comment

0 Comments