Header Ads Widget

Responsive Advertisement

JINI ALIVYOHARIBU NDOA YANGU



Katika maisha kila mtu anapitia mikasa mbalimbali na hakuna mtu yeyote anayeweza kujua hadi pale yeye mwenyewe anapoamua kuweka wazi kupitia gazeti hili tunawaletea upande wa pili wa maisha ya msanii maarufu wa filamu nchini Frolah Mvungi ambaye kwa mara ya kwanza anatuletea na kutuhadithia upande wa pili wa maisha ambayo mimi na wewe hatujui ila tutafahamu mara baada ya kusoma mkasa huu ni jinsi gani alinusurika kupoteza maisha baada ya kutupiwa jini na wabaya wake ambalo lilimuendesha karibu kupoteza uhai wake karibuni wapenzi wasomaji


 Nikiwa natoka zangu mazoezini kwani tulikuwa tunaifanyia mazoezi movie    ya   nilipokuwa narudi nikiwa kabisa nakaribia nyumbani nilihisi kama kuna kitu kilikuwa kimeniingia ndani ya mwili wangu kwani haikuwa hali ya kawaida kutokea,sikujali sana niliendelea na safari yangu huku nikiwa na mawazo kadha wa kadha ni kitu gani ambacho kilikuwa kimeniingia katika mwili wangu,nilipokaribia nyumbani moja kwa moja niliingia chumbani kwangu na kuendelea na shughuli zangu kama kawaida,nikiwa nimetoka kuoga mara nikaanza kuhisi vitu tofauti katika mwili wangu huku vikiwa vinanizidia uwezo yaani vikawa vinaniendesha na kunipeleka peleka mara nikajikuta nipo nje ila kwa bahati nzuri nilikuwa nimevaa suruali ya kitambaa,nilianza kupiga makelele mara nilipotoka kwa nje na kila mtu alikuwa ananishangaa ila wale wapangaji wenzangu walinifata na kunichukua na kunipeleka hadi kibarazani,nilikuwa 

naongea maneno ambayo hata mimi kwa kweli nilikuwa siyaelewi kwani nilikuwa naongea kimasai tuu kila m tu aliyekuwa pale alikuwa ananishangaa kwa kweli haukupita muda sana mara walikuja majirani ambao tulikuwa tumepanga nao na kuwaita walokole ambao moja kwa moja walianza kazi ya kuniombea na kunifanyia maombi,waliniombea sana ila sikuona mafanikio yeyote hadi pale alipokuja ustadh naye kubahatisha bahati yake,alikuja akanishika sikio la kulia na kuanza kunifanyia kisomo,alifanya sana kisomo ndipo kidogo yakatulia sasa nikaanza kudai kuwa ninahitaji damu ya m tu,nilikuwa nikipiga kelele sana kuwa nataka damu hakuna aliyekuwa tayari kunisaidia kwa lolote,kumbuka kuwa muda wote huo mimi sijielewi ni kitu gani kilikuwa kinanitokea katika kichwa changu nikiwa bado naendelea kupiga kelele mara nilikichukua kisu na kujichoma nacho katika,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Nikiwa  ndio natoka mazoezini nimechoka nilichukua tax ambayo 
ilinipeleka hadi nyumbani nilishuka na kuingia ndani nikamkuta mpenzi wangu{h baba}akiwa kapumzika katika kochi alinipokea kwa makiss motomoto na kuni huge kabla sijaingia chumbani ambapo nilibadilisha nguo na siku hiyo niliamua mimi mwenyewe kumuandalia chakula mzee japo house girl alikuwepo.Nilipomaliza kuandaa nilimuita mzee na tukaanza kula huku tukipiga story mbalimbali za hapa na pale ili kusogeza muda uende kidogo nilikuwa nahitaji nilale mapema kwani kesho yake nilikuwa nahitaji kufanya video ya filamu mpya na ilikuwa asubuhi hivyo sikuhitaji kuchelewa kulala.Asubuhi na mapema niliamka na kuelekea mazoezini huku nikimuacha mzee kapumzika,nilijitahidi ili niwahi shooting hata hivyo nilichelewa kidogo nilikuta wenzangu wameshaanza tayari

 kufanya shooting mi nilipofika nikaigiza sehemu yangu kisha nikawa rest room ambapo huwa tunabadilisha nguo na kadhalika.Nikiwa narudi zangu nyumbani baada ya kumaliza kazi ya siku hiyo kwa bahati nzuri au mbaya njiani nilikutana na mtu mmoja ambaye mpaka leo hii sijamuelewa na yeye ndiye sababisho la mimi kuwa hivi hadi leo hii,nikiwa narudi njiani nilikutana na kaka mmoja hivi bishoo bishoo baada ya kuniona aliniita kama vile ananijua,mimi sikuweza kwenda niliingia ndani ya gari langu na kuanza safari ila kwa maajabu kwa mbele alinitokea tena akinisimamisha kwa mara ya pili.Nilipofunga breki alikuja hadi pale kwangu mlangoni na kuniambia 
kuwa ameona wengi ila amenichagua mimi na hivyo ananiomba nimuelewe kwani kaona wengi sana warembo ila moyo ndio umenichagua mimi aliongea sana hadi akapiga magoti chini akionyesha kila dalili ya kunihitaji ili awe nami,tatizo moja ambalo yeye hakuwa akilijua ni kuwa tayari alikuwa amechelewa mimi nilikuwa tayari yupo  mtu ninayempenda na hata kama asingekuwepo nisingeweza kuwa na uhusiano wa mapenzi kumkabidhi moyo wangu mtu ambaye simfahamu hata mara moja.Nilimsukuma kwa nje kisha nikaendesha gari kwa nguvu hadi nyumbani kwani sikuhitaji tena aniwahi hata kama akikodi pikipiki ya kunifatilia.Nilifika nyumbani na moja kwa moja nikaingia ndani kujipumzisha nikikiwaza kile kituko ambacho nilikuwa nimetoka kukutana nacho,kwangu kilikuwa ni kitu cha ajabu sana kwani sikuwa na wazo sikutaraji kukutana na kitu kama kile kilikuwa ni

 kama miujiza fulani hivi kwa upande wangu.Sikutaka kufikiri sana nilienda bafuni kujiogesha maji kabla sijarudi ndani na kuanza kufanya shughuli zangu za hapa na pale.Mda ulikuwa tayari umeshaenda nakumbuka ilikuwa ni jioni nikiwa nimetoka zangu kuoga nikarudi kitandani kujipumzisha huku nikiwa tayari nimesahau mambo ya yule mtu ila cha ajabu eti nilipofika pale kitandani niliona amekaa katika dressing table yangu,nilishtuka kupita kiasi kwani ni kitu ambacho mimi binafsi nilikuwa sijakitegemea hata kidogo.Pale pale nilianza kumuita Hamisi{h baba}ambaye kwa kipindi hicho alikuwa amekaa kibarazani akiangalia kipindi cha mcheza kwao.Cha ajabu nilipogeuza kichwa tu kukirudisha tena hakukuwa na mtu na mda huohuo h baba alikuwa anakuja kwa kasi zote”vipi my love kuna kitu tofauti?””hapana kuna kijana nilikuwa nimemuona amekaa pale””aaaah mama watoto mbona pale hakuna mtu wa aina yoyote yule?””that’s serios my love mimi nimemuona alikuwa amekaa pale”mchumba wangu hakuweza kuniamini kwani alijua labda tu nilikuwa naweweseka kutoka usingizini au na mawazo ya kitu flani kwani yeye alidai muda woote alikuwa amekaa pale sebuleni na hakumuona mtu wa aina yoyote kupita.Sikuwa na jinsi tena nilichofanya ni kujichukua na kuanza kujisogeza tena kitandani huku nikiwa na hofu kidogo kwani ile hali haikuwa ni ya kawaida

.”Usiniue tafadhali nakuomba usiniue tafadhali””hapana wewe ni lazima ufe kwa sababu hautaki kuwa na mimi lazima ufe””usiniue chochote kile ambacho unaona unastahili kukipata tafadhali chukua ila uhai wangu nakuomba sana uniachie usiniue”haukupita mda yule mtu alichukua kile kisu na kunichoma nacho katika tumbo langu ambalo ndani yake nilikuwa na ujauzito wa miezi miwili au mitatu hivi na baada ya hapo damu nyingi zilikuwa zinanitoka kutoka katika kila sehemu yangu ya mwili kila upande damu zilikuwa zinanitoka kwa wingi sana,mara nilishtuka kutoka usingizini huku nikipiga kelele sana hadi h baba akaamka na kuniuliza kwani nina nini?,sikumficha nilimwambia kila kitu kilichotokea na jinsi ambavyo nilivyoota kutoka katika usingizi hata yeye alianza kuwa na wasiwasi sasa juu ya kile kitu ambacho kinanikumba.Kwa kawaida usiku huwa natoka mara mbili hadi tatu kujisaidia haja ndogo na baada ya kumhadithia nilijisikia haja nikaenda kuitikia wito wa hawa.Cha ajabu nilipofika nilijiskia hali mbaya zaidi ila nilipokuwa nataka kujisaidia haja ilikuwa wala haitoki nilijitahidi ila haikutoka na kipindi nilipokuwa nimeshakata tamaa ilianza kunitoka na haikuwa kama kawaida bali safari hii ilikuwa ikinitoka damu,kila 


nilivyokuwa najisaidia damu ilikuwa inanitiririka sana hadi nikashangaa nikamuita mchumba ngu aje kuona ila alipofika ni yaleyale kwani haikuwa damu bali ilikuwa ni majimaji tu kama ya haja ya kawaida,misukosuko bado iliniendelea kuniandama na kwa upande wangu nilikuwa nashindwa kujua nini cha kufanya hata ile furaha ambayo nilikuwa ninayo mda mwingi sasa ilikuwa inanitoweka na sasa nikawa mimi ni mtu wa huzuni na majonzi mda wote kila saa nilikuwa nawaza tu,niliondoka saa tano kuelekea kufanya video ya filamu ya Total love ambayo nilikuwa nimefanya na Wolper nilijitahidi kuwa katika hali ya kawaida japo ilikuwa ni ngumu huku nikiwa na mawazo sana.Nilifanikiwa kufanya ile filamu kwa usalama hadi namaliza ila maajabu bado yalikuwa yanaendelea siku hadi siku.Nikiwa natoka zangu kazini narudi nyumbani tukiwa katika zile foleni za ubungo kulikuwa na mtu mmoja alikuwa anauza maji na mimi nilikuwa ninahisi kiu sana hivyo sikuwa na budi kumuita na kununua maji na baada ya kumpa kijana hela yake yale maji yalibadilika na kuwa damu nilitupa huko kumuangalia yule kijana aliyekuwa ameniuzia alibadilika na kuwa ndiye yule ambaye ameniambia kuwa eti ananipenda nilimshangaa sana kwa kweli na kwa bahati nzuri taa zikawa tayari zimesharuhusu nikaondoka nikimuacha yeye akinipungia mkono huku akinipiga busu kwa ishara ya mdomo.Nilikasirika sana na nikaapa kuwa lazima nimkomeshe kwa tabia yake hii nitafanya chochote hata ikibidi nitumie nusu ya akiba yangu kusafiri kuliko adha nayoipata kama hii.Nilipokaribia nyumbani nilifunguliwa geti na kuingia ndani huku mawazo yakiwa yanazidi kunizidia juu ya yale yote yanayonikumba kwa sasa,niliamini maisha ni mitihani na huu ni mmoja katika mitihani ambayo binadamu inabidi apitie.Baada ya kupata ushauri kutoka kwa baadhi ya marafiki zangu na mchumba wangu walinishauri niende

 kwanza kwa mama yangu nikamuelezee yake yote ambayo yanayonisibu.”Dah sasa dada florah hii hadithi yako ni nzuri sana kwa kweli unajua kuna baadhi ya watu najua watakuwa hawawezi kuamini kama hii ni historia yako””haa haa kaka Tajiri unajua ni kutokujua tu sisi wote ni binadamu na kila binadamu katika maisha yake huwa anapitia mengi sana tangu kuzaliwa kwake hadi anaingia ndani ya kaburi ila kwa sisi maarufu watu wanatuona kama vile ni tofauti hivyo mtu anakuwa ni mgumu kidogo kuamini ila kutoamini kwao hakuwezi kufanya ukweli kuwa uongo””mmmh haya dada yangu tuendelee na na uhondo”basi nilianza kufanya mipango na safari ya kuelekea kwa mama ili nipate kumuhadithia yale yote yaliyokuwa yananisibu,mama yangu anakaa maeneo ya kimara ni mwendo kama wa nusu saa hivi,baada ya siku mbili nilikuwa njiani nikielekea nyumbani kwa wazee wangu baada ya kufika nilimuhadithia mama kuanzia mwanzo hadi mwisho jinsi mambo yote yanavuonitokea.Mama aliniambia kuwa kesho yake anifate na twende kwa mtaalamu mmoja tukaangalie labda ni kitu gani ambacho kinachonisibu yawezekana kuna kitu ambacho nimetupiwa

.Mimi binafsi sikutaka na sikupenda mambo ya kwa waganga ila mama aliniambia kuwa kutokuamini kwako hakufanyi kutokuwepo mambo hayo na kama nahitaji kupona sina budi niende ili nipate pona.Ilinibidi nipate tu kumsikiliza mama yangu kwani yeye ni muongozo katika maisha yangu na kila anachokisema sina budi kumsikiliza na kukifata.Siku ilipofika mimi na mama yangu tulifanya safari na kuelekea kwa mtaalamu huyo ambaye alikuwa anakaa bagamoyo.Tulipofika pale kwa yule mtaalamu alikuwa na chumba kimoja hivi kikubwa sana ambacho alikuwa anakitumia kwa shughuli zake binafsi.Baada ya muda alikuja na sisi tukaanza kumuelezea mwanzo hadi mwisho jinsi ilivyokuwa na mara moja akachukua kioo na kuanza kuangalia,mimi nilikuwa na hofu sana kuwa inakuwaje mtu huyu anakuwa na uwezo wa namna hii yaani anakuwa anaweza kukichukua kioo na kungalia mbali kabisa kila kitu 

kilichotokea,aliniambia kuwa mimi nimetupiwa jini mahaba na sababu ni kuwa kuna mtu ambaye alikuwa ananipenda na mimi nikamkataa sasa ndio ameamua kunifanyia hivi na amenitumia jini la kimasai.Alimvuta yule mtu hadi pale na ni kweli alikuwa ni mtu ninayemfahamu na ni msanii mwenzangu ambaye ana jina tu ila sipendi kumuweka wazi kuwa alikuwa ni nani ila mwenyewe akisoma hapa atakuwa tayari ameshajijua bila wasiwasi.Aliniambia kuwa yule ni jini alikuwa anajigeuza na kuwa kama mtu ila alikuwa I jini na nia na madhumuni ni kuubadilisha moyo wangu nisinywe nisilale nisile bila kuniona hata chochote kufanya iwe tabu.Alisema yule msanii wala hana nia mbaya ila tu ni jinsi ambavyo ananipenda ndio kaamua kufanya hivyo na ameona kwa kawaida ameshindwa ameona ni heri atumie njia tofauti ili afanikishe lile ambalo alikuwa analihitaji kutoka kwangu,mimi nilishaamini kwa sababu ni kweli alikuwa ananifatilia yule msanii na alikuwa ananitaka yule mganga alikuwa anazidi mwanaume hapo ndipo nilipoamini kuwa kumbe kweli kuna baadhi ya waganga wanaona na wanajua nini wanakifanya.Yule mganga aliyekuwa anafahamika kwa jina Ramadhani Hassani kwa hakika alikuwa ni 

mtaalamu kwa kuangalia tena sana,aliniambia kwa leo angenipa dawa  tu ya kunipunguza makali kwa muda wa siku mbili hizi ila kazi ya kumtoa huyo jini aliniambia siku inayofaa kumtoa ni siku ya jumanne
 asubuhi au mchana kwani atakuwa anatawala zohari{masaa haya wanayajua wenyewe wataalamu}.Mimi na mama yangu tuliamua kurudi nyumbani huku nikiwa na mawazo kibao hivi haya yote ni kwanini yananitokea mimi tu kwa hakika nilikuwa nashangaa sana haya maajabu ya kila siku.Nilipofika kwa mama wala sikukaa sana moja kwa moja nilirudi nyumbani kwangu kwa ajili ya kwenda kupumzika kwa mihangaiko ya siku hiyo.Nilipofika nyumbani nilimuelezea kila kitu mchumba wangu na kwa kweli namshukuru mungu kwani alinipa moyo na kunifariji sana ndio maana nasema yaani huyu mwanaume hapana kwa kweli anajua kuni handle na kunifariji sana pindi napokuwa na matatizo.”Owk unajua dada frolah story yako nimeipenda sana ni nzuri na ya kuvutia kwa wapenzi wasomaji na naamini watajifunza mengi sana kupitia story hii””usijali kaka na mimi ndicho nahitaji wape wapate somo kupitia kwangu”basi baada ya h baba kunifariji niliondoka pale na kumfata yule mwanaume ambaye ameniroga na nilimwambia wazi kuwa watu mapenzi huwa hawayalazimishi hata kidogo na penzi la dhati huwa haliendewi kwa mganga,kipindi chote kipindi namwambia alikuwa amejiinamia tu kwani hakuwa na jibu la aina yoyote kuashiria ni kweli na yeye anahusika kwa asilimia zote 


kisha baada ya kumpa ukweli niliondoka zangu”alijisikiaje baada ya kumwambia ukweli?””hakuwa na la kusema ila alikuwa anaona aibu tu kaka tajiri””owk na wewe wala haukuogopa kumfata kwake na kumpa ukweli je angekudhuru na chochote kile?””kwa kweli hata mimi sijielewi ule ujasili mimi niliupata wapi,kwani nilikuwa najiamini sana japo nilikuwa nipo peke yangu””owk”siku huwa hazidanganyi na mda huwa haurudi nyuma nakumbuka vizuri sana ilikuwa ni jumapili zikiwa zimebaki siku mbili tu kabla  ya kwenda kwa yule mganga nilianza kuhisi mambo ya ajabu kipindi natoka kuigiza filamu ya steve nyerere akiwa na maunda suka filamu ya My son,nilipokuwa narudi nikiwa kabisa nakaribia nyumbani nilihisi kama kuna kitu kilikuwa kimeniingia ndani ya mwili wangu kwani haikuwa hali ya kawaida kutokea,sikujali sana niliendelea na safari yangu huku nikiwa na mawazo kadha wa kadha ni kitu gani ambacho kilikuwa kimeniingia katika mwili wangu,nilipokaribia nyumbani moja kwa moja niliingia chumbani kwangu na kuendelea na shughuli zangu kama kawaida,nikiwa 

nimetoka kuoga mara nikaanza kuhisi vitu tofauti katika mwili wangu huku vikiwa vinanizidia uwezo yaani vikawa vinaniendesha na kunipeleka peleka mara nikajikuta nikajikuta nipo nje ila kwa bahati nzuri nilikuwa nimevaa suruali ya kitambaa,nilianza kupiga makelele mara nilipotoka kwa nje na kila mtu alikuwa ananishangaa ila wale wapangaji wenzangu walinifata na kunichukua na kunipeleka hadi kibarazani,nilikuwa naongea maneno ambayo hata mimi kwa kweli nilikuwa siyaelewi kwani nilikuwa naongea kimasai tuu kila m tu aliyekuwa pale alikuwa ananishangaa kwa kweli haukupita muda sana mara walikuja majirani ambao tulikuwa tumepanga nao na kuwaita walokole ambao moja kwa moja walianza kazi ya kuniombea na kunifanyia maombi,waliniombea sana ila sikuona mafanikio yeyote hadi pale alipokuja ustadh naye kubahatisha bahati yake,alikuja akanishika sikio la kulia na kuanza kunifanyia kisomo,alifanya sana kisomo ndipo kidogo yakatulia sasa nikaanza kudai kuwa ninahitaji damu ya m tu,nilikuwa nikipiga kelele sana kuwa nataka damu hakuna aliyekuwa tayari kunisaidia kwa lolote,kumbuka kuwa muda wote huo mimi sijielewi ni kitu gani kilikuwa kinanitokea katika kichwa changu nikiwa bado naendelea kupiga kelele mara nilikichukua kisu na 

kujichoma nacho.Kile kisu nilijichoma nacho katika mguu wangu wa kushoto na damu zikaaanza kuruka ila cha ajabu sikuwa nahisi maumivu ya kitu chochote katika mwili wangu na mbaya zaidi nilitoka na kuanza kuinyonya ile damu yangu mimi mwenyewe ilikuwa ni ajabu sana,waliniwashia udi ubani na dawa za aina mbalimbali ndipo nilipotulia na kuanza kuongea nilikuwa nimepandisha kichwani,aliitwa mmasai na kuanza kumuuliza yule jini wa kimasai ni kitu gain anataka kutoka kwangu?ndipo aliposema kuwa alikuwa ametumwa na kijana mmoja alimtaja jina{yuleyule niliemfata}kuwa alikuwa ananihitaji na yupo tayari kuwa na mimi kwa hali yoyote hivyo yeye katumwa kwangu aje ili anichukue na kunipeleka kwake kwa amri.Watu waliokuwa pale wengine walikuwa ni wataalamu na walianza kumwambia kuwa mimi tayari kanipata aache fujo na muda si mrefu atanichukua na tutaenda kwa yule jamaa.Hapo sasa ndipo yule jini alipotulia na kuanza kushuka nikiweka kichwa kwa mbele na kuondoka zake na mimi ndio nikawa nimerudiwa na fahamu kamili.Kila kitu kilichotokea nilisimuliwa na majirani kwa hakika nilijuta hata kwa nini nilizaliwa katika hii dunia yale maisha yangu yote yameharibika kwa ajili ya mtu mmoja ambaye yeye kwa mapenzi yake ndio ananisababishia matatizo kama haya niliumia sana moyoni mwangu ila sikuwa na la kufanya ilinibidi nivumilie tu hizi siku mbili hadi pale nitakapoenda kwa yule mganga.

Nilikutana na vikwazo vingi sana ambavyo siwezi kuvizungumzia vyote ila miongoni mwa hivyo ni kile ambacho kuna siku nikiwa nataka kwenda kuoga katika swimming pool ile kabla sijaingia aliingia panya na hapohapo nikaona amepigwa na shoti ya umeme hadi kufa na kukauka kabisa yaani ina maana yale maji yalikuwa yametegeshwa shoti ya kimaajabu sana na ningeingia tu ndio ingekuwa mwisho wangu tayari hata leo hii mimi nisingekuwepo mwandishi wangu.Hiki kitu kwa kweli sitakisahau katika maisha yangu,mapenzi ni mazuri sana ila pia yana umiza sana kaka yule kijana kweli alikuwa ananipenda ila mimi tayari nipo na mtu mwingine na ninampenda kwa dhati siwezi kumuacha sasa nitafanyaje unadhani kweli si kosa lake ni moyo,pia mimi sina kosa kwani tayari nishampata mwingine.Jumanne ilifika na nikaanza safari ya kuelekea kwa mama ili twende kwa yule mganga aende akamtoe alituagiza twende na mbuzi wa rangi nyekundu na vitambaa kadha wa kadha nimpelekee kwake.

Post a Comment

0 Comments