Header Ads Widget

Responsive Advertisement

SIMULIZI; NILIMKARIBISHA KATIKA BIASHARA YANGU, AKANIZALISHA NA KUNIFUKUZA!

SIMULIZI; NILIMKARIBISHA KATIKA BIASHARA YANGU, AKANIZALISHA NA KUNIFUKUZA!
Mwaka 2014 ndiyo nilikutana na huyu Kaka, mimi ni darasa la saba nayeye ndiyo alikua amemaliza chuo, mimi nilikua nafanya biashara, nilikua na duka dogo nauza vyombo. Tulizoeana na kujikuta tunakua wapenzi, yeye bado alikua anahangaika kutafuta kazi lakini baada ya kuwa wapenzi na kuona hana kazi aliniambia aje awe anakaa dukani kwangu pale ili kuangalia maisha, kwakua nilikua nampenda nilimruhusu.
Alikua anakuja dukani ananisaidia kuuza, ingawa halikua duka kubwa sana lakini alikua anajituma. Baadaye mwaka huo huo nilipata ujauzito, aliniambia kipindi hicho hana kazi lakini atahudumia akipata kazi, alikubali kwenda kujitambulisha kwetu na mimi alinitambulisha kwao. Akaondoka kwao na kuhamia kwangu tukawa tunaishi kama mke na mume wakati tukisubiri apate pesa ya mahari kwani aliniambia haitakua vizuri kwa mimi kujitolea mahari mimi mwenyewe.
Biashara ilikua inaenda vizuri, duka lilianza kuwa kubwa, kutokana na ufinyu wa sehemu tulitafuta fremu nyingine tukafungua duka kubwa la vyombo. Nilipojifungua nilienda kwetu, yeye ndiyo akawa anasimamia duka, alikua akinitumia matumizi na kunijali, nilirudi na kuendelea na biashara na katika kipindi hicho tulinunua kiwanja na kuanza kujenga taratibu, yeye ndiyo alikua anasimamia kila kitu. Mwaka 2016 nilipata ujauzito wapili, hapo aliniambia kua ni pumzike nikae nyumbani.
Aliniambia napata kila kitu hivyo sina haja ya kujisumbua, nilikubali kutokana na hali yangu ya ujauzito, mwezi wa kumi nilijifungua lakini nilipotaka kurudi tena dukani alinikataza kwa kuniambia kua mimi nikae nyumbani. Hataki watoto wake kulelewa na dada wa kazi, tuligombana sana mpaka akatishia kuniacha akisema kama namnyanyasia mali zangu basi ataondoka na kuniachia kila kitu. Kwakua nilikua nampenda sana nilikubali kuacha kwenda dukani akawa anasimamia yeye kila kitu.
Hapo ndipo nilanza kuona uchungu wamahusiano, kwanza suala la kufunga ndoa hakua akitaka, kila siku ilikua ni matusi, nikimshauri kitu ananiambia nitamuambia nini wakati mimi darasa la saba, alikua akinitukana, akiwaambia ndugu zangu masikini na kila kitu cha matusi. Kabla ya kuwa naye mimi ndiyo nilikua nasaidia ndugu zangu, nilishaanza kuwajengea wazazi wangu na ilibaki finishing tu.
Lakini baada ya kuacha kwenda dukani alikua akinipa pesa ya chakula tu hata nguo za watoto ilikua shida, nikimuuliza ananiambia ile biashara ni yake, alinikuta nina kaduka tu kakapandisha kwa kutumia akili zake za kisomi hivyo hawezi kuhudumia familia ambayo haina shukurani. Manyanyaso yalizidi, alikua anafanya kila kitu kimyakimya, mwaka 2017 mwezi watatu nilikuja kugundua kua ana mwanamke mwingine ambaye alikua akimleta mpaka dukani, nilipoongea aliniambia lile ni duka lake.
Siku moja nilienda dukani kilazima kwani alikua hataki niende, nilikutana na yule mwanamke tukagombana mpaka kuitiana Polisi, mimi nilikamatwa na yeye alikua upande wa yule mwanamke akisema tumeenda kuwafanyia vurugu. Niliwambia duka ni langu lakini kumbe alsihaabdilisha kila kitu, makaratasi ya leseni yalionekana kamuandika yule mwanamke wakati mwanzo kila kitu kilikua chakwangu.
Huwezi kuamini nilikaa ndani siku moja na baadaye akaja kunitoa, aliniambia hataki usumbufu na kusema yeye ni mtu wa hadhi sana na hawezi kuoa mwanamke wa darasa saba na kama nataka niondoke. Aliniambia sina chake kwangu kwani hatukuoana na kama ninataka basi atanipa mtaji kidogo wa kaunzia maisha, alinipa laki tano ambayo niliikataa kisha akanifukuza katika nyumba tuliyokua tukiishi.
Nilirudi nyumbani nikiwa nimechanganyikiwa, ndugu walinipokea lakini walinilaumu sana kwani mimi ndiyo nilikua tegemeo lao, sikua na namna kwani nilisikia kashaanza kuuza vitu, viwanja tulivynunua na nyumba tuliyokua tukijenga aliiuza. Kila nilipojaribu kumpigia simu niliishia matusi tu. Kwabahati nzuri nilikua nakusoma tangu zamani, nilijilaumu kwanini sikukutafuta ukanishauri kuhusu mchumba wangu ila niliona kwangu mambo yako vizuri hawezi kunigeuka.
Nilikupigia simu nikakuambia hali yangu, uliniambia niemshachelewa na kama katika ile biashara kamuandika mwanamke mwingine basi pamoja na kwamba kisheria tunaweza kuonekana kama mke na mume lakini hakukua na mali za kugawana. Uliniambia nilazima kuanza maisha kwani kama niliweza kutafuta pesa mwanzoni basi naweza kutafuta tena. Sikua na mtaji mkubwa, nilikua na kama laki tani tu tena ambazo ilikua ni ada ya mdogo wangu lakini alilazimika kurudi shule za serikali kwani mimi ndiyo nilikua namsomesha na sikua na kitu tena,
Uliniambia niwaache watoto kwa Mama yangu kwania alinifukuza nao kisha nirudi mjini kutafuta maisha. Sikutaka kurudi Dar kwani nilikua naumia sana nikimkumbuka yule Kaka. Nilienda Mwanza na kuanza kufanya biashara ya vyombo, nilikua nazungusha kwa watu kisha nikatafuta kakibanda mjini, nilikua nikiuza kila kitu kuanzia vyombo mpaka nguo lakini mwisho nilifanikiwa katika nguo. Nimehangaika sana tangu hiyo mwaka jana mpaka mwaka huu ndiyo nimeweza kufungua duka langu mwenyewe.
Kwakua Dar kuna sehemu nilikua nanunua na nafahamika basi kuna sehemu nyingine nilikua napata bidhaa kwa mali kauli, umenisaidia sana Kaka kusimamia biashara yangu. Sijarudi kama zamani lakini biashara imesimama na naweza kuendesha maisha yangu. Yule mwanaume kule alipo baada ya mimi kuondoka mwanamke amekua akitumia pesa hovyo hivyo, kuna wafanyakazi wananipigia na kuniambia wana miezi karibu sita hawajalipwa.
Wanasema tayari kashampa mimba na kila siku yeye anachojua ni kuchukua pesa, mwanaume naye anachukua mpaka duka linakaribia kuisha, wanagombana kila siku kila mmoja akimuona mwenzake kama ndiyo anafilisi duka. Juzi yule Kaka kanipigia ananiomba msamaha, ananiambia alifanya makosa na amejifunza. Nimemuuliza kuhusu huyo mwanamke mwingine si ana mimba yake na duka si alimuandika yeye akasema hamna shida anataka kuchukua kila kitu chake na kuhamishia mtaji kidogo alio nao dukani katika duka langu la Mwanza.
Ananiambia kajutia na sasa hivi yuko tayari kuja kwetu na kama ni ndoa basi tufunge ili tulee watoto wetu. Nawaza sana Kaka kuhusu hili kwani nikiwaangalia wanangu bado wadogo, bado wanamhitaji Baba yao, lakini nawaza hivi nikweli kabadilika au, ana mwanamke mwingine ambaye bado wanaishi naye na ana mimba yake je kweli atamuacha au? Wazazi wangu hawataki kumsikia lakini mimi bado nampenda, kwakua wewe ndiyo ulinisaidia katika matatizo yangu ya mwanzo nimeona nikuambie ili unishauri nifanye nini?

Post a Comment

0 Comments