Header Ads Widget

Responsive Advertisement

SMART WIFE, IMEKUWA RAHISI MNO KUKUPENDA.

Ilikua ni asubuhi, alifungua macho yake taratibu.
Akanyosha mkono kumgusa mkewe. Hakukuwa na mtu. Mkewe alikua ameshaamka.
Akamsikia kwa mbali mkewe akiimba wimbo huu..
"🎼🎼Nionapo amani kama shwari, Ama nionapo shida; Kwa mambo yote umenijulisha, Ni salama rohoni mwangu. Saalama rohooni, Ni salama rohoni mwangu.🎼🎼🎶🎼🎤
Mume aliposkia mkewe akiimba akageuka upande wa pili wa kitanda kivivu huku akitabasamu.
Akamshukuru sana Mungu. Hii ni aina ya ndoa ambayo siku zote alimuomba Mungu awe nayo: Kumuoa mwanamke ambae amezama katika upendo wa Mungu.
Taratibu akafanya sala ndogo palepale kitandani. Akamshukuru Mungu kwa kumpa familia yenye furaha. Kichwa cha nyumba lazima aiombee familia yake.
Baada ya sala fupi akaamka. Akavaa suruali yake ya mazoezi na kisha akavaa fulana ambayo kwa mbele imeandikwa kwa kiingereza "Love conquers all". Fulana hiyo alinunuliwa na mkewe.
Akatoka chumbani na kufuata sauti ya mkewe iliyokua ikiimba, ilionekana kutokea jikoni.
Mkewe alikuwa akiendelea kuimba...
"🎼🎼🎵Ingawa shetani atanitesa, Nitajipa moyo kwani Kristo ameona unyonge wangu, Amekufa kwa roho yangu. Salama rohoni, Ni salama rohoni mwangu🎼🎼🎵🎤.
Mume nae huku akielekea jikoni akadakia ubeti uliofuata na kuimba...
"🎼🎼Dhambi zangu zote, wala si nusu, Zimewekwa msalabani; Wala sichukui laana yake, Ni salama rohoni mwangu. Salama rohoni, Ni salama rohoni mwangu🎼🎼🎤"
Mke akageuka na kutazama, akamuona mumewe akiingia jikoni huku akiimba..mke akatabasamu. Lile tabasamu zuri la kumuua mtu...!
Mume akamkumbatia mkewe kwa nyuma na kwa pamoja wakaimba...
"🎼🎼🎵Ee Bwana himiza siku ya kuja, Panda itakapolia; Utakaposhuka sitaogopa Ni salama rohoni mwangu..Salama rohoni, Ni salama rohoni mwetu🎵🎵🎙"
Wakaimba kwa pamoja huku wamekumbatiana wakinesa huku na huku.
Mke akageuka kumtazama mumewe usoni.
"Umeamkaje Partner wangu katika kuabudu" Mume akamsalimu mkewe.
"Nimeamka salama my honey. Umelala salama?" Mke akajibu.
"Ndio nililala salama. Umeamka saa ngapi? Sijakusikia ukiamka." Mume akashangaa
Mke akainyosha vizuri fulana ya mumewe, "Baby, ulikua umechoka sana. Usingenisikia navyoamka. Hata hivyo sikutaka kukuamsha leo ni weekend. Unahitaji kupumzika."
"Vipi kuhusu wewe? Unapumzika saa ngapi? Maana usiku umenipa haki yangu tena kwa mechi ya kibabe. You drive me crazy my wife" Mume akasaili.
"Hahaaa Sweetdarling unavituko sana. Kwa Mwanamke kazi hua haziishi"
"Kwaio unafanya nini sasa hivi?" Mume akauliza.
"Si unaniona namenya magimbi. Naandaa breakfast. Sio muda mrefu nimemaliza kuosha vyombo" akamjibu mumewe.
"Watoto je?" Mume akauliza.
"Dorah yuko nje anacheza huku akisubiri kifungua kinywa. Jayden ameenda kwa jirani kuchukua kitabu chake cha hadithi za watoto" Mke akajibu huku akiendelea kumenya magimbi.
"Mume akazungusha mikono yake na kumshika kiunoni mkewe na kumgeuza amtazame usoni."
Akambusu mdomoni na kumwambia, "Unajua ni nini nakipenda kutoka kwako?"
"Nini?" Mke akauliza.
"Unavyoabudu. Napenda sana unavonyenyekea kwa Mungu. Napenda namna unavyoguswa na upendo wa Mungu. Napenda namna unavyo-surrender kwa Mungu na kuabudu kwako ndiko kunakufanya uwe mama na mke wa mfano.
Unapoabudu inakua rahisi kukupenda zaidi, unavyoabudu unakua una amani. Amani yako inaleta mood nzuri ndani ya nyumba. Unapoabudu unakua mrahisi mno wa kusamehe. Unapoabudu unakua mtiifu na mnyenyekevu mbele za Mungu hatankwa mimi mumeo. Tunapoabudu pamoja tunakua tunaendana, uwepo wa Mungu unatamalaki nyumba yetu kwa sababu Mungu hukaa mahala penye sifa.
Tunapoabudu tunapata ufumbuzi wa matatizo yetu na Mungu anatupigania. Tunapoabudu matatizo hayatutafuti na hata kama yakitupata Mungu anatupa ujasiri wa kukabiliana nayo. Siku zote naamini, kwa sababu wewe ni mtu wa kuabudu basi kukupenda imekua rahisi mno na upendo juu yako unakuja naturally tu" Mume akamwambia mkewe.
Mke nae akambusu mumewe mdomoni na kumwambia.."Ni namna gani nimebarikiwa kuwa na mume ambae ni co-worshiper wangu. Wote kwa pamoja tumejenga hema ya BWANA katika nyumba yetu. Kuabudu kwetu kunamleta Mungu karibu yetu. Naupenda sana huo moyo ulio nao Mume wangu."
Mtoto wao wa miaka saba akaingia jikoni huku akiiimbia, alipowaona baba na mama yake akawakumbatia na kuwaambia "Nawapenda baba na mama"
Mama na baba wakacheka.
"Ona namna kuabudu kunavovutia. Asante sana mke wangu kwa kuwalea vema wanangu katika mazingira ya kumjua Mungu, wazazi wengine ni mwiba kwa watoto wao. Watoto hawana hata uthubutu wa kuwakaribia."
Akambusu shavuni mkewe..
"Nakupenda mume wangu. Ngoja nimalizie kuandaa breakfast."
"Nikusaidie kufanya nini?" Mume akauliza.
"Labda unisaidie kupika mayai..na tukimaliza kupika na kupata breakfast ile zawadi niliyokupa usiku nakupa na leo tena..leo si weekend... Mke sina mamlaka juu ya mwili wangu bali wewe mume wangu unayo; hali kadhalika nawe mume, huna mamlaka juu ya mwili wako, bali mimi mkeo. siwezi kukunyima haki yako, i'm all yours!!!
"Oh oh oh mke wangu okey I am on it" mume akajibu huku akichukua flying pan fasta fasta..
"🎼🎼Tufani inapovuma Sana moyoni mwangu, Huona pa kujificha Mkononi mwa Mungu.
Hunificha, hunificha Adui hatanipata, Hunificha, hunificha, Mkononi mwake🎸🎤🎼🎼.
Wote kwa pamoja wakawa wakiimba wimbo wa tenzi ya rohoni huku wakipika tabadamu ikiwe imesheheni nyusoni mwao..mke anapika magimbi, mume anapika mayai.

Post a Comment

0 Comments