Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Sipingi kuwa make-up ni muhimu ila iwe na mipaka jamani

(KAMA UMEOLEWA/UMEOA TAFADHALI USISOME)

Kuna story za kutisha nyingi sana kutoka kwa wanaume, kuhusu kuamka asubuhi na kujikuta wakiwa wamelala kitandani pembeni ya viumbe wasio watambua baada ya kutoa MAKE UP usoni usiku.

Wanawake wengine hutumia pesa nyingi kila mwezi kununua make-up, na sababu kuu ya kutumia make-up kuzidi mipaka ni kutokujiamini kwa jinsi walivyo, hasa uzuri wao sehemu za usoni.

Wanawake ni kama bidhaa. Pindi bidhaa zikiwa sokoni, hua kuna na ushindani mkubwa wa biashara nzuri nzuri kuuzika. Na mtu yoyote aliekua mfanyabiashara atakwambia kua ni "lazima bidhaa kila siku kuifanya yenye mvuto sokoni" ili ipate wanunuzi.

Haina tofauti na wanawake kwa make-up. Ni lazima waongeze uzuri katika muonekano wao ili wavutie, hususan muonekano wa sura, kwasababu ya kumvutia mlengwa maana ndio kitu cha mwanzo hutazama (japo wengine huangalia mizigo).



Muonekano wa sura mitaani na sehemu za starehe huongopa, tumeshasikia story nyingi za kutisha kutoka kwa wanaume kuhusiana na kuamka asubuhi na kujikuta pembeni ya kitanda kuna mdada amelala asiemtambua. Najua inatisha kama imeshakukuta.

Mfano wa hizo story:

Kuna jamaa dalali wa magari siku moja alikua Club moja hivi, aliwaona wadada wakiwa wamependeza sana. Baada ya usiku wa furaha tele alimuimbisha dada mmoja na wakawa wanapeleka vyombo (tungi, nyagi, bia) pamoja mpaka wakazima. Alipo amka asubuhi, alichokiona pembeni yake kilikua ni cha kutisha. Ilibidi awapigie sim rafiki zake kuwauliza kama aliondoka na mtu sahihi ama laa.

Mwingine alikutana na dada mmoja mrembo maeneo ya beach, akashusha mistari mpaka dada akaingia kilaini, kisha akamuomba waende kuogelea. Walipo zama baharini, na kisha dada kuchomoka, aliona dada kabadilika rangi (rangi imefifia), kope na nyusi hana, mpaka jamaa akashtuka ni kipi kimemsibu yule dada.

Jamaa mwingine alimuona dada mrembo na kuamua kuongea nae, ilikua mwisho wa mwezi, na alikua anataka kujifyatua kidogo ili mwezi uishe viziri kwake, dada alikubali na wakaamua kwenda hotel. Walipofika chumbani dada aliomba taa izimwe na atoe make-up ili alale kwa amani, jamaa aliridhia. Dada aliingia chooni atoe make-up yake, cha ajabu alitumia muda mrefu sana mpaka jamaa akawa na wasiwasi, aliamua kumfuata na kujua kipi kinaendelea kwa ule ukimya. Alichokutana nacho kilimshtua sana, sura alioikuta haikua ile ya yule dada alieongea nae mwanzo, na hata ile shepu iliomvutia haikuwepo. Alijikuta amepiga kelele kubwa, yule dada alishtuka na kuamua kujifungia kule bafuni. Jamaa akasepa bila kuaga!!!

Mfano wa hayo matukio, ni haya











Sipingi kua make-up ni muhimu. Huwapa kujiamini kisaikolojia, kuonekana mzuri ni kujihisi mzuri. Ila iwe na mipaka jamani, mungu anawaona!!! Mtatutoa roho zetu ipo siku


Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook

Post a Comment

0 Comments