Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Mpenzi Akiwa Si Wa Maana Na Wewe Si Wa Maana





Mpenzi Akiwa Si Wa Maana Na Wewe Si Wa Maana

HUENDA ukawa ni msemo mgumu kidogo, na huenda pia wengine wasiuelewe kwa haraka lakini ukiona mtu hana mwenzi wa maana ni dalili kwa kiasi kikubwa kwamba hata yeye si wa maana.

Wa maana kwa kawaida hufanya mambo baada ya kutafakari na kutafiti kwa kina.
Na ukiona mtu mara nyingi amekuwa ni mwenye kulalamikia wapenzi wake kwamba aaah nilikuwa na fulani, tukaachana kwa sababu alikuwa na tabia mbaya, baadaye nikawa na fulani naye ni wa hovyo, nikawa tena na fulani wa hovyo kabisa, sijui Mungu huyu kwanini ananifanyia hivi..... hii ni dalili mbaya na ni lazima uwe makini na mtu huyo.

  • Ni kwamba unakutana na mtu ambaye tayari alishazaa, labda ni tayari alishakuwa kwenye ndoa, labda tayari alishakuwa kwenye uhusiano na wanaume au wanawake wengi, ni lazima uwe makini sana kabla ya wewe kuamua kama uwe naye maisha au la.

Watu wengi wabaya mara zote huwa ni maarufu sana wa kulaumu wengine, badala ya ukweli kuwa wao ndio wafanyaji makosa, huwatupia lawama walioachana nao kuwa ndio tatizo. Inakuwaje kila siku wao tu ndio wawe wakosaji? Ni uongo wa hali ya juu.

Kwanini uwe makini na mtu ambaye tayari alishakuwa kwenye ndoa au kuishi na mwanamke au mwanaume pamoja au kuwa na wanaume wengi au wanawake wengi katika maisha yake kwa maana ya watatu na kuendelea? Ni kwamba kuachana si jambo rahisi, kwa maana hiyo ikiwa mtu alifikia maamuzi ya kuachana na watu hao, ni kwamba akili yake ina matatizo, ni mtu mwenye kuamini kuwa suluhu ya shida ya kuikimbia, badala ya kuitafutia tiba ili itoweke.

Kitaalam mtu yeyote ambaye alishawahi kuachana hasa kama waliishi kama mke na mume, ni lazima uwe makini sana kuangalia sababu walizoachania. Kama kwa mfano anasema aaah mwenzangu ndio alikuwa mbaya, alikuwa anakwenda kwa wanawake wengine, aaah alikuwa anakwenda kwa wanaume wengine, ni kweli inawezekana ni hulka ya mtu kuendekeza ngono, lakini swali la kujiuliza ni kwanini leo na wala sio jana?
Eeeh ni kwamba kwanini ni leo huyo mwenzi wake anafuata wengine? Wakati mwingine utakuta wengine wana nyodo, kama ni tendo la ndoa, kulipata hadi ubembeleze weee kama unaomba kibarua. Kazi tumbeleze, unarudi nyumbani nako, unaomba weee hadi watu wa chumba cha pili wanasikia leo kuna jamaa anabembeleza nanihiii.

Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa kadri ndoa inavyodumu, ndivyo idadi ya kufanya tendo inapungua, nyodo huongezeka, utasikia mtu anakwambia aaah bwana eeeh jana nimekupa na leo unataka tena kwani mimi ng'ombe....aaah hata ng'ombe huwa anapumzika. Wapo pia wanaume utawasikia wanaongea maneno mabaya kwa wake zao kwa mfano aaaah achana na mimi bwana, nimechoka

Sio sawa. Ni lazima kama wanandoa mjitahidi kuwa na lugha nzuri. Watu wengi wamekuwa maarufu wa kulalamika, lakini ukichunguza sana utaona mabaya mengi yanatokea kutokana na kauli au matendo yetu. Utakuta mtu kwa mfano hata kama labda anakubali mfanye tendo wengine wanatumia kama vile hasira si umesema unataka, haya basi njoo, njoo nataka kuwahi, kama hutaki mi naondoka. Huwezi kufurahia ndoa katika kauli za kipuuzi kama hizi. Ndoa inataka maneno matamu, eeeh si ndiyo ndugu yangu, sio maneno ya kimagumegume, maneno makavu kama dagaa!!! Hainogi. Unapozungumza na mwenzi wako ni lazima kuwe na tofauti na vile unavyozungumza na watoto au ndugu ama mzazi. Kwa mfano kama amelala na umemtengea maji, hutapaswi kumwita ukiwa mbali, bali unamsogolea na kumgusa baba nanihii, maji tayari amka wahi kazini.

Huenda hii kauli ikawa ni ngeni kwa baadhi ya wanawake, hawajui kuwatengea maji, wala mswaki, wala kuwasafishia viatu wala kuwatengea chakula waume zao. Mwanamke ukiwa hivi, jua unakosea. Katika maisha, hata kama si kila siku, lakini unapaswa kufanya kati ya haya, si mbaya pia mume kumfanyia mwenzi wake haya. Mapenzi ni deni, fanya ufanyiwe, mfanyie naye aone na siku moja afanye.

Kanuni ya mapenzi ni kwamba ikiwa umeguswa kichwa, unajisikia raha, ni kwamba hata ukimgusa kichwa pia ataona utamu. Tafakari kwa makini haya, chukua hatua. Msingi wa kuwa na maisha bora yenye furaha katika ndoa ni kuwa makini kwa kila unachofanya.
Kabla ya yote ni lazima uwe makini katika uchaguzi.Siri nyingine iliyo ya msingi sana ni kwamba usikubali kuwa mwepesi wa kufanya mapenzi. Watu wengi wanaokimbilia kufanya mapenzi, ndio wale ambao wanaishia kuachana na wapenzi wengi.

Post a Comment

0 Comments