Header Ads Widget

Responsive Advertisement

KAMA NDOA YAKO INA AMANI ACHA KUTAFUTAMATATIZO YA NDOA!

Kuna wanawake wenye matatizo ya ndoa, na kuna wanawake ambao wanaafutra matatizo ya ndoa. Sasa nakuambia daa yangu, acha kuhangaika kutafuta matataizo ya ndoa ambayo hayapo! Acha! Acha! Acha! Acha! Mume wako anakujali, anahudumia familia, anahudumia watoto, hujawahi kumuona akichepuka, hajawahi kuongea na wanawake mbele yako lakini unafanya upuuzi huu;
(1) Unaanza kukagua simu yake na kila mwanamke unayekutana naye unaanza kumfuatilia kudhani kuwa anachepuka naye na wakati mwingin ekuwapigia simu kujua wao ni nani mbona wanaongea sana na mume wako! Ni upumbavu acha!
(2) Akiwa online asipojibu meseji zako unaanza kutukana na kusema kuwa anakudharau alikua anachart na wanawake wengine. Huo ni ujinga siku akiahza kuchart nao hata hutaongea.
(3) Unampigia simu anakuambia nitakutafuta baadaye unanuna kwakua kasahau na kusingizia alikua na watu wengine.
(4) Unamfuatilia ofisini kwke, kuuliza kila mtu anayemjua, au kuna mtu umemuweka ili kumfuatilia awe anakupa taarifa za mume wako, huo ni upumbavu na niamini nikikuambia unachoambiwa ni uongo.
(5) Anarudi nyumbani unamkagua mpaka unamnusa nguo kujua kuwa kama ana harufu tofauti ili ujue kama anachepuka, acha huo ujinga.
Iko hivi acha kuwa na kisirani cha kutokumuamini, kama mwenza wako hajawahi kukuvunjia heshima acha kumchunguza. Hicho kisiarani ulichonacho ni kwakua hujapigwa matukio, siku huyo mwanaume akikupiga matukio hutahangaika. Yaani sikua aklikuchoka hutakua na haja ya kushika simu yake, wanawake zake watakua wanakupigia simu wanakutukana.
Siku akichoka huo wivu wako wa kipumbavu hutakua na haja ya kutuma watu wamfuatilie, hapana wanawake zake watakua wanakuja hapo kwako kukutukana, atakua anakuletea watoto pamoja na hicho kisirani chako utamtibua. Acha huo ujinga, naandika kwa hasira kwasababu naongea na watu ambao wanapuiigwa wanatolewa vizazi ila na nyie wenye ndoa nzuri mnaanza kuniboa kwakua mnazivunja kwa vitu vya kijinga kama hivyo!
Nimemaliza, wakunielewa wamenialewa, wale ambao wanasema mimi nimeshindwa kumfuatilia nasubiria mnitafute mkishamaliza kumfuatilia kwamba mmekundua nini na mmefaidika nini? Wanaume hawapendi visirani, na mwanaume akichepuka kwakua una kisirani ni hatari zaidi kuliko kuchepuka kwakua yeye ni Malaya!
NB; Kama una hizi tabia soma kitabu changu cha “Ndoa Yangu Furaha Yangu” jifunze kuwa na amani kabla ya ndoa yako kuharibika!

Post a Comment

0 Comments