Header Ads Widget

Responsive Advertisement

FREEMASONRY ILIANZIA WAPI Part III


FREEMASONRY ILIANZIA WAPI Part III


Hata hivyo kulikuwa na madhehebu mengine ya watu walio fahamika kama Essenes, hawa nao walikuwa ni Wayahudi, mafunzo yao hawa nayo yanakuja kuwa ni sehemu muhimu ya mafunzo na muongozo kwa Illuminati na freemasonry katika historia yao yote. Essenes katika picha hii wana uzito wa kipekee, kwa vile ni kutoka kwao ndiyo freemasonry wanajivunia walivyo navyo. Ingawa Essene walipatikana Palestina zaidi lakini mafunzo yao yalienea mpaka Egypt. Essene hawa walikuwa ni moja kati ya madhehebu makubwa matatu ya Kiyahudi katika dini hizi za kipagani, wengine walikuwa ni Pharisees na Sudducees. Essene walitambulika kama warithi wa mafundisho ya Chaldea, elimu ya nyota ya wa Misri, na elimu ya tiba ya wa Persia wa kale, wali fananishwa na makuhani wa Magi kutoka Persia.





Kwa msaada wa mitume waliofuata hekalu lilijengwa upya, lakini likaja kubomolewa tena kwa mara nyingine na Wayahudi kubakizwa kwenye dini za kipagani za watu wa Roma.


Hivyo mafunzo haya ya kipagani yaliwatoa kabisa Wayahudi katika imani ya Mungu Mmoja na kuwaingiza katika imani za kishirikina ambazo ndani yake shetani aliabudiwa waziwazi.
Quran nayo ikalitaja hili kuhusiana na Wayahudi na athari waliyo ipata baada ya kutekwa na kupelekwa Babyloni.




“Na wakafuata yale waliyo zua mashet'ani kuuzulia ufalme wa Suleiman. Na wala Suleiman hakukufuru, bali mashet'ani ndio walio kufuru, wakiwafundisha watu uchawi, na yaliyo teremshwa kwa Malaika wawili, Haaruta na Maaruta katika mji wa Baabil (Babiloni). Wala hao hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni mtihani; basi usikufuru. Wakajifunza kwa hao wawili yale ya kumfarikisha mtu na mkewe. Wala hawawezi kumdhuru mtu ila kwa kutaka Mwenyezi Mungu. Na wanajifunza yatayo wadhuru wala hayawanufaishi. Na hakika wanajua kwamba aliye fuata haya hatakuwa na fungu lolote katika Akhera (maisha baada ya kifo). Na hakika ni kiovu mno walicho jiuzia nafsi zao laiti wangelijua.”( Quran2: 102)
Kutoka kwa mungu Mithra aliyeingizwa Ugiriki na Wayahudi kutoka Babyloni mpaka kuundwa kwa madhehebu ya Mithra ambayo yatabakia kama dira ya Illuminati katika zama zitakazo fuata, kote huko familia za Illuminati zilikuwa ni sehemu ya ukuaji huo. Ukoo wa nyumba ya Commagene iliungana na ile ya Herod Great, pamoja na familia za watu wa Siria wakiwemo makuhani na wachungaji wa mungu Baal pamoja na familia ya Julius Caesar. Waliyafuata yale madhehebu ya Mithra wakaichanganya na mafunzo ya maajabu kutoka kwenye Kabbala na kutengeneza kitu kipya chenye mchanganyiko wa maajabu ya kichawi na elimu za nyota. Dini hiyo ikafuata ile mila ya dini ya Kibabiloni ambapo wafalme waliabudiwa kama mfano wa mungu jua, mungu Mithra katika haya madhehebu yaliyo toholewa akawa kwenye umbo la binadamu naye akaabudiwa kama Alexander the Great ambaye pia alimuwakilisha mungu Jua.
Mafunzo haya yalishika mizizi ndani ya mashariki ya kati vilivyo, hata Uislamu ulipobisha hodi kwa mara nyingine Mashariki ya kati na kuanza kuimeza miji mmoja baada ya mwingine, haikusalimika na mafunzo haya ya kipagani.
baadhi ya wafasiri hasa wa zile kazi za Magi, Mithra, Essene waliacha dini yao ya Kiislam na wengine walichanganya mafunzo ya Uislamu na yale ya Upagani na hapo ukawa mwanzo wa kuundwa dini mpya ndani ya dini ya Uislamu, dini ya kisufi, walijiita kuwa ni Waislam lakini hawakuwa na chochote cha kufanania na Uislamu zaidi ya mavazi yao. Mafunzo haya yalikwenda yakaingizwa katika dini nyingine ya Kishia ambayo nao pia walishatoka kwenye Uislamu kutokana na mhimili wa mafunzo yao, lakini kama walivyo Sufi nao wanajiita kuwa ni Waislam, kupitia kwa Ismailia dhehebu jingine la dini ya Shia kazi hizi au mafunzo haya zikawafikia Knights Templar ambao wakazipeleka Ulaya na kutengeneza Scottish Rite Freemasons. Wakati Knights Templar wanazichukua kazi hizi tayari zilikuwa kwenye maudhui sawa na ya Freemasons tunao waona leo. Egypt kulikuwa na mahekalu ya kimasoni hata kabla ya Ulaya, kulikuwa na madaraja 3 mpaka 10. Hivyo Freemasons na asasi nyingine za siri zilizokwenda kwa majina tofauti zilikuwa zimeshaota mizizi Mashariki ya kati kwa karne nyingi kabla aina hii ya maarifa haijapiga hodi katika nchi za Ulaya. Preure de Sion na Knights Templar walipotengeneza Scottish Rite Freemasons wakaipatia madaraja 33. Lakini waliita ‘Ancient and Accepted Rite’ akiwa na maana kuwa walicho kiongezea juu ya kile cha mababu wa Freemasons wa Egypt kimekubalika. Ile ya Egypt ilikuwa ikifahamika kama, ‘Ancient and Primitive Rite’, hii ndiyo baba na babu wa Freemasons zote tunazo ziona leo duniani.



Nembo na muhiri wa Knights Templar.


Knights Templar nayo hadithi yao ilikuwa ikivutia mno, wao walijinadi kuwa kazi yao ni ulinzi kwa mahujaji wa Kikristo walio kuwa wakifika hapo kwa ajili ya ibada hiyo, lakini iliwachukua miaka 20 baada ya vita vya msalaba wao kuchukua dhima hiyo, na kwa muda wa miaka 10 walikuwa wapo tisa (9), unaikumbuka nambari hii niliitaja huko nyuma wakati mfalme Agrippa alipokutana na wenzake kuasisi Mysterious Force?





Alama kuu ya Knights Templar, ambayo inatumika mpaka hivi leo, utaiona kwenye vazi la Papa, na pia utaiona kwenye bendera ya Uingereza.


Jamaa hawa tisa walikuwa bize kuchakura chakura na kutafuta kitu fulani au masalio ya namna fulani katika kaburi alilozikwa mfalme Agrippa na katika hekalu la mara ya pili la Wayahudi ambalo lilibomolewa na Titus mnamo mwaka 70 AD.








ASKARI WA KNIGHTS TEMPLAR


Kwa muda wote huo walikuwa wakichimba chimba katika maeneo ya masalio ya hekalu hilo, kwa miaka yote hiyo kulikuwa na kitu ambacho walikuwa wakikitafuta. Mpaka leo hakuna anayefahamu kinagaubaga kuwa nini hasa Templar walichokipata katika hekalu hilo, ila hakuna maswali wala shaka kuwa kuna ambacho walikipata, kitu chenye thamani kubwa, kitu kilicho ibadilisha historia ya Templar tangu hapo. Inasemekana waliipata hazina ya mfalme Suleiman ambayo si Nebuchadnezzar II wala Waroma waliofanikiwa kuipata. Inasemekana kuwa hazina iliyo kuwepo kwenye hekalu hilo ni tani 65 za fedha (Silver) na tani 26 za dhahabu. Mengine ambayo yanadhaniwa yalichukuliwa na Knights Templar kutoka kwenye hilo hekalu ni nyaraka na maandishi mengine muhimu kuhusu Yesu na familia yake



KIKARAGOSI KINACHO ONESHA PICHA YA JACOB DE MOLAY


Baada ya hapo Templar walirudi Ulaya.
Baada tu ya kupata baraka za Papa, utajiri waliokuwa nao, pamoja na aridhi na mamia wakijiunga kutoka katika familia za kifalme na watu kutoka katika familia tajiri na huku wakitoa mali zao kwa Templers ikawa ni sababu ya wao kuweza kumiliki aridhi sehemu mbalimbali za Ulaya kama Uingereza, Portugal, Spain, Germany, Italy, Austria Ufaransa na kwengineko. Baada ya kipindi kifupi tu Templers wakawa karibu kabisa na kanisa la Romani kiushawishi na kiutajiri pia. Mwaka 1139 Papa Innocent II aliifanya jumuiya hii ya Templar huru juu ya wafalme wote, na kwa wazee wa baraza za kifalme, aliyeruhusiwa kuwaingilia shughuli zao ni Papa peke yake na ndiye msimamizi wa shughuli zao mpaka hivi leo
Mtandao huu wa Tampler ukazidi kupata nguvu, walifanya walivyotaka, walikuwa ni wataalam wa tiba na madawa ya miti shamba, ndiyo waasisi wa benki na ndiyo watu wa kwanza kutumia hundi, na watozaji wa riba kubwa katika biashara zao, katika sehemu kubwa ya Ulaya wakawa ni watu wenye ujuzi mkubwa wa mambo ya benki, walifanya kazi ya kusafirisha fedha za wafanyabiashara kupitia kwa watu wao waliko Ulaya, wafalme wa nchi nyingi waliwakopesha Templer kiasi kikubwa cha fedha, yote haya ilikuwa ni mbegu ya kuzaliwa kile tunachokiita ubepari na mifumo ya benki. Templar hawakutakiwa kulipa kodi, walijihusisha pia na mambo ya ujenzi na wakaruhusiwa kujenga makanisa yao wenyewe, ambayo yalikuwa ni ya maajabu kwa utaalam wa mahesabu na elimu ya hali ya juu ya maumbo iliyotumika ambayo watu wengine hawakuwa na maarifa nayo
Mnamo mwaka 1296 wazo lilitolewa kuwa Jumuiya ya Knights Templar na ile ya St. John ziungane, kiongozi wa Templar, Jacques de Molay alilipinga wazo hilo. Aliyekuwa mfalme wa Ufaransa Philip IV na ambaye alikuwa amewakopesha Templar kiasi kikubwa cha fedha na alitaka kuwa mwanachama wa jumuiya hii yenye nguvu na ushawishi mkubwa lakini akakataliwa na hivyo akafikiria namna ya kuivunja vunja jumuiya hii, ikumbukwe si Papa wala mfalme Philip IV aliyekuwa na sauti juu ya Tampler.
Mfalme akaweka majasusi kufuatilia ajenda za jumuiya hii na haikuchukua muda akatambua kuwa Templar waliojiita watumishi masikini wa hekalu la Mfalme Suleiman, na wanajeshi masikini wa dini ya Kikristo na wanao tumia nembo ya wapanda farasi wawili juu ya mgongo wa farasi mmoja kuonesha umasikini na undugu wao; kumbe wao ni watu matajiri, wenye nguvu kubwa za kijeshi na kiuchumi na wanao tishia ufalme wake, wao ni wafuasi wa dini ya mashetani, wanashirikiana na wachawi, wanavitumia vitabu vichafu vya kimila kutoka Babyloni, Kabbala na Talmudi kufanya mambo ya nguvu za giza, wanawafundisha wanawake kutoa mimba, wanatoa kafara za watoto wachanga na wanafanya ngono kinyume cha maumbile. Tarehe 22 Septemba 1307 mfalme akatoa amri ya kukamatwa kwa Templar wote, amri hiyo ilitolewa katika mfumo wa barua iliyofungwa ikapigwa muhuri juu na amri ya kuwa barua hiyo isifunguliwe mpaka jioni ya tarehe 13 Oktoba 1307, barua hiyo wakapewa viongozi wote wa kiserikali waliyo chini ya utawala wa Philip IV, na pia viongozi wa kifalme wa nchi zingine walipewa barua hiyo.
Ijumaa ya tarehe 13 Oktoba 1307 ilikuwa ni siku mbaya kwa Templar, bado tarehe 13 Oktoba inaadhimishwa na Freemasonry kama siku mbaya kuliko. Kati ya Templar 3200 ni 620 tu ndiyo waliokamatwa wengine walifanikiwa kutoroka.





JACOB DE MOLAY ANACHOMWA MOTO AKIWA HAI, Mpaka leo freemasonry wanalipiza kisasi juu ya kifo cha kiongozi wao huyo kwa njia mbalimbali.


Knights Tampler walikimbilia Scotland, walipokelewa na mfalme Robert the Bruce ambaye alikana kuitekeleza amri ya mfalme, hii ni kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa ni mfuasi wa Tampler. Kutokea hapo Scotland Tampler wakazizika shughuli zao, chini kwa chini kama mto wa chini ya aridhi uelekeao baharini, Templer walianza kuikamata Ulaya na koo mbalimbali za kifalme huku wakisubiri fursa nzuri kujitokeza upya, lakini wakiwa na jina jingine tofauti na lile la awali.
Unakumbuka hadithi ya Black Death, walikuwepo watu waliyo itwa masoni, baada ya zahama la Black Death, masoni walianza kuwapa uanachama wale wasiyo kuwa masoni, yaani wasiyo kuwa na taaluma ya ujenzi kuwa wanachama katika jumuiya hii, watu mbalimbali walijipenyeza ndani ya masoni kwa sababu mbalimbali, lakini pia kwenye kona fulani yenye kiza totoro, watu fulani walio funika nyuso zao, ambao walikuwa wakifahamika kama Tampler, wakaona fursa waliyo kuwa wakiisubiri kwa muda mrefu, hatimaye imefika, Tampler wakajipenyeza ndani ya Masoni.
Ajenda ya Knights Templar ilikuwa kuichukua jumuiya ya kimasoni ambayo kipindi hicho ilikuwa ikihusika na mambo ya ujenzi kwa kutumia elimu ya siri iliyo fahamika kwa wajenzi wa jumuiya pekee. Kwa sababu kipindi hicho jumuiya hiyo ilikuwa na hali ngumu kiuchumi ilitumia fursa ambayo Knights Templar waliona faida yake kwao, kwani hawakuhitaji uwe mjuzi katika ujenzi bali ulipe ada tu ya uanachama. Walikuwa na hamu kubwa ya kufahamu nini kilicho nyuma ya kazi za ujenzi za jamaa hawa, na kwa vile masoni walikuwa wamejijenga mpaka nje ya England, ingewapatia fursa Knights Templar kujitanua chini ya kivuli cha wamasonia na wakati huo, huo wakisubiri wakati muafaka wa kuitumia masoni kama pazia la kufichia ajenda yao kuu. (kutoka kwenye kitabu ambacho Salim Msangi anakiandaa)
Walio ingia ndani ya Masoni, walikuwepo Francis Bacon, halafu akaja mwana mahesabu na mwana kemia Robert Moray
Msomi mwingine mkubwa katika nyanja ya Alchemy, nyota na uchawi Elias Ashmole akajiunga ndani ya hekalu la kimasoni, halafu akaingia mwana Kabbala Robert Boyle ambaye naye alikuwa na taaluma ya kemia na fizikia, na pia kipindi fulani nyuma alikuwa ni grand master wa asasi ya siri cha Prieure de Sion 1654 mpaka 1691, kikundi hicho ndiyo baba wa Knights Templar ambao nao kwa sasa walikuwa wanajipenyeza ndani ya masonia, baba na mwana. Halafu Sir Christopher Wren mjenzi na mjuzi wa taaluma ya nyota, jamaa huyu ndiye aliye fanisi hekalu la St.Paul na pia alichora ramani ya kulijenga upya jiji la London baada yakuharibiwa na moto mkubwa mnamo mwaka 1666. Isaac Newton akawa mwana jumuiya mnamo mwaka 1672, kama alivyokuwa Boyle, Newton naye alikuwa ni grand master wa Prieure de Sion kutoka 1691 mpaka 1727
Bwana wakubwa hawa katika ulimwengu wa kisayansi, wakiwa ndani ya hekalu la kimasoni wakaanza kuigeuza sayansi kichwa chini miguu juu kwa faida za kisiasa na kwa malengo ya jumuiya za siri walizo toka, wakatengeneza nadharia ya inayo julikana kama Materialist, maarufu kwa lugha yetu kama sayansi ya Darwin na sasa inakwenda kwa jina la Humanist, sayansi na nadharia hii, ina kataa kuwepo kwa roho, nadharia hii inasimamiwa vilivyo na vikundi vinavyoitwa wasimamizi wa haki za binaadam, chini kabisa ya nadharia hii ni kukataa kuwepo kwa Mungu, wanadai kuwa ulimwengu umejitengeneza wenyewe na kifo hakihusiani kabisa na kuwepo kwa Mungu.
Mwaka 1717 Templers wakajitokeza tena Ulaya, idadi yao imekuwa kubwa mno na nguvu yao imeongezeka na wako tayari kutengeneza kitambulisho kipya. Kitambulisho kitakacho waacha huru na matendo yao ya karne zilizotangulia na wakipewa nguvu na watwana pamoja na masultani wa England. Na jina walilolichagua litajulikana na wengi lakini litafahamika na wachache.... hili jina jipya..... ni....... FREEMASONRY.......

Post a Comment

0 Comments