Header Ads Widget

Responsive Advertisement

FREEMASONRY ILIANZIA WAPI Part II


FREEMASONRY ILIANZIA WAPI Part II


Kuna vyanzo vingi vinavyo elezea kuwepo kwa freemasonry Kabbala ya 1717, vyanzo hivyo ni vingi, vinahitaji muda na uyakinifu ilikuweza kutofautisha baina ya almasi na vipande vya vioo. Kuna vilivyo andikwa kwa nia nzuri tu, kuna vilivyo andikwa kwa ajili ya kupotosha, na kuna vilivyo andikwa na wale wasio fahamu wanacho andika, lakini wote wakijaribu kuthibitisha au kukanusha kuwepo kwa freemasonry kabla ya 1717.


Katika mtandao wa Bible Beliver, wameweka hadithi moja nzuri sana ya namna ambavyo freemasonry walivyo kuwepo kabla ya 1717, napo hapo nitaiangalia kwa uchache sana, kwa urefu hadithi hii unaweza kuitizama mwenye hapa. http://www.biblebelievers.org.au/masonry2.htm


Hadithi yenyewe inazungumzia habari ya mwaka 43, kipindu kifupi sana baada ya Yesu/Kristo (Issa Mwana wa Mariam Rehma ya Mungu iwe juu yao wote) alipo paishwa kwenda mbinguni. Ulitokea mtafaruku baina ya waumini wa dini za kipagani na dini aliyoiacha Yesu. Jamii ilikuwa imechanika chanika mno. Baba anamakana mwana, mwana anamkana baba, mama na baba hawaelewani, dada na kaka na ndugu wengine halikadhalika. Uadui mkubwa umeletwa na kile kilicho onekana kama ‘dini mpya’.


Waliyo zikataa ‘dini mpya’ alikuwemo mtu aliyeitwa Mfalme Herod Agrippa II, anatajwa kama alikuwa ni kibaraka wa dola ya Roma, na Wayahudi walinyanyasika vibaya kwenye mikono yake, hasa pale walipo itikadi kuwa Yesu ni mtume wa Mungu Mmoja na wao wanayafuata mafundisho yake.





Mfalme Herod Agrippa II
Mfalme Herod alisimama mbele ya baraza la Jerusalem na kulihutubia juu ya zahama au kisu kilicho ichana jamii yao, juu ya mafundisho ya ‘dini mpya’ na namna gani watasimama dhidi ya dini hiyo, na wafuasi wake na mafundisho yao, ili nyumba za Jerusalem zisalimike na ‘balaa’ lake.


Katika baraza hilo mfalme alikutana na watu tisa tu (9), hii namba itizame na ikumbeke vizuri, tutakutana nayo huko mbele na kasha nitakueleza maana yake hasa nini. Waheshimiwa tisa walio kuwepo kwenye baraza hilo ni Herod Agrippa II, Moab Levy, Adoniram, Johanan, Jacob Abdon, Antipas, Solomon Aberon, Ashadi Abia, na Hiram Abiud.


Mfalme Agrippa akawambia kwanza hakubaliani na Yesu kwamba ndiye Kristo, kwa vile yeye na wenzake na mababu zao kunayo Kristo mwingine waliyekuwa wanamngojea, ambaye ndiye atakuwa KING/Mfalme wa Jerusalem, na sasa hivi kiti chake kipo kinamngojea, kama tunavyo jua harakati hizi za kuwa na kiongozi mmoja duniani kote, serikali ya kiongozi huyo itakuwa ni Jerusalem na hapo tumemuona Agrippa miaka hiyo akizungumzia kitu hicho, hicho, na leo hii tunawaona freemasonry wakiandaa makazi ya mfalme huyo, na kumbuka kwenye hadithi ya Mtume Muhammad (s.a.w) kuwa Dajjali, Mpinga Kristo, au huyo Kristo ambaye Mfalme Agrippa anayemtaja, atauwawa katika eneo linaloitwa ‘Baab Lud’ leo panajulikana kama Tel Aviv, hapo ndipo Dajjali atakapo uwawa, kwa vile ni ndani ya Jerusalem ndipo atakapo taka kusimamishia dola yake na ukitizama matukio ya kiulimwengu leo ndicho hasa Illuminati wanacho kiandaa, kitu cha mfalme mwenye jicho moja.










Kazi ya Nikolai Bodarevsky, 1875, ikimuonesha mtume Paulo akihukumiwa mbele Mfalme Agrippa.


Agrippa akaendelea kuliambia baraza lake kuwa na hicho alicho kuja nacho Yesu mababu zake walishapambana nacho kabla yao na wao akina Agrippa wataendelea kupambana na hicho mpaka mwisho. Alicho kuja nacho Yesu si kingine bali dini ya Mungu Mmoja. Hivyo basi Agrippa kwa ushawishi wa Hiram Abiud wakaanzisha kile walicho kiita ‘Mysterious Force’ kama anavyo elezea mwenyewe.
“Tutawafanya waamini kuwa jumuiya yetu ni ya kale kwa kutumia alama za zana za ujenzi zilizo tumiwa na ndugu yetu Hiram Abiff kulijenga hekalu la Suleimani (Solomon) kama vile nyundo, bikari, kampasi n.k vyote vya mbao kama alivyo kuwa navyo Abiff. Katika jumuiya yetu tutaweka madaraja (degree) madaraja hayo yatakuwa thelathini na tatu kama ulivyo umri wa Muongo, mzushi aliyejiita Massehia. Kila daraja tutalipa jina na tutatengeneza nembo zingine. Yote haya ni mawazo yangu pamoja na mawazo ya ndugu zetu Hiram na Moab. Maana ya ndani ya nembo hizi haitafichuliwa itabakia kuwa ni siri kati yetu sisi watu tisa tulioanzisha jumuiya hii. Kwa watu wengine watakao jiunga nasi katika jumuiya yetu hii, inatosha kwa wao kujua kuwa hivi ni vifaa vya ujenzi vya enzi na enzi, hivyo wataamini kuwa jumuiya yetu imeanzishwa tangu wakati wa Suleiman.”
“Mimi kutokana na nguvu zangu kama kiongozi nawa zawadia kila mmoja heshima ya kuwa katika daraja la 33 (33 degrees) daraja la juu kabisa katika jumuiya yetu.... na kwa sababu ndugu yetu Hiram Abif ni yatima wa Baba, tangu utotoni mwake hakuna aliyemjua ila mama yake mjane na pendekeza pia jumuiya yetu kuitwa “Mjane” (The Widow) kutoka sasa na kuendelea sisi waasisi tutaitwa watoto wa mjane (The Sons of the Widow), na kila mshirika atajiita mtoto wa mjane mpaka mwisho wa dunia kwani tunaamini kuwa jumuiya yetu itaishi mpaka mwisho wa dunia.”


Maneno hayo yalitamkwa muda mchache baada ya Yesu kupaishwa kwenda mbinguni, na maneno hayo yameweza kusimama dhidi ya muda, dhidi ya kila janga lililoikumba dunia yetu tangu, na leo tunawaona watu au jumuiya ambayo inawiana 100% na maneno hayo, tunawaona freemasonry.
Lakini kama alivyo sema mfalme Agrippa, kuwa hiyo ‘dini mpya’ mababu zao walishapambana nayo, hivyo akimaanisha kuwa kabla ya Yesu kuna wengine walikuja na ujumbe sawa na huo, yaani mitume wengine kama Daud, Musa na wengineo (Amani ya Mungu iwe juu yao) na walipingwa na mababu wa akina Agrippa na wenzake, kwa maana mababu hao tayari walikuwa na dini au mfumo wao wa kuishi tofauti na huo ulioletwa na mitume wa Mungu Mmoja, hivyo basi utaona kuwa Freemasonry haikuanzia kwa Agrippa, bali kwa mababu kabla yake.
Hadithi yenyewe iko hivi,
Utakumbukwa kwamba, katika wafuasi wa dini ya Mungu Mmoja, ambao walipata shida sana kutokana na jeuri yao na kiburi ni Wayahudi, kuna wakati waliadhibiwa na mfalme katili mpaka nyumba yao ya ibada ikateketezwa na wakachukuliwa kwenda utumwani Babyloni. Walipokuwa huko mawasiliano ya kiroho yalikatwa, na kwa kipindi kirefu sana watu hawa wakawa chini ya ibada mbalimbali za kimila na kishetani.
Wayahudi waliotokea utumwani Babyloni na dini ya kimila iliyobeba mafunzo ya Kabbala walikuwa wakidhaniwa kuwa ni wafuasi wa dini ya Chaldea Magi. Watu wa Persia walikuwa ni wafuasi wa dini ya Zoroastrian ambayo Magi walikuwa ni wachungaji wa dini hiyo, hivyo Wagiriki walidhani kuwa hawa Wayahudi ni wachungaji wa Magi. Dini hii ya Magi asili yake inasemwa kuwa ilikuwa ni dini ya Mungu Mmoja lakini baadaye ikachanganya na mafundisho ya kibabiloni na kuharibiwa. Dini hii ikawa imejikita zaidi katika sanaa na elimu ya mambo ya nyota, inasemwa makuhani wao ndiyo wa mwanzo katika karne ya 6 BC kuifanikisha elimu hii ya mambo ya angani, misingi yake ikawa ni kuabudu nyota. Elimu hii nyota ikaenda sambamba na ile hadithi ya kufa na kufufuka kwa mungu










Mchoro huu unaonesha uharibifu kwenye hekalu la kwanza la Wayahudi, ambapo baada ya hapo walikamatwa kama watumwa na kupelekwa Babyloni.


Mungu wa watu wa Persia alifahamika kama Mithra ambaye alikuwa sawa na Baal wa Babyloni, mungu huyu wa Persia alitukuzwa kwa nguvu na sifa zote za kichawi. Dola hii ya Persia ilivyo zidi kupanuka , mafundisho ya Magi nayo yakatapakaa kila ambapo dola hiyo iliingiza mguu au ilikuwa na mahusiano na watu husika. Wagiriki walizipokea tamaduni hizi na zingine mfano wa hizi na kuzitafsiri kwenye lugha zao. Wagiriki wanatajwa kuwa wao ndiyo wa mwanzo kuiweka Kabbala kwenye maandishi wakati kabla ilikuwa ni aina ya fasihi simulizi. Baadaye mafundisho haya yalichukuliwa na Waislam walioacha mafunzo sahihi ya dini ya mdomo mnamo karne ya saba na kuanza kuzitafsiri kazi hizi katika lugha ya Kiarabu na kisha kupelekea kuundwa kwa dini mpya ya Usufi ambayo mafunzo yake yalikuwa sawa na yale ya Kabbala na Zoroastrian zaidi, nao walijiita Waislam lakini imani yao, matendo na mafundisho yao hayakufanana chochote na Waislam. Kama tutakavyo kuja kuona Wasufi ndiyo walio wapatia Knights Templar mafunzo haya nao wakayapeleka Ulaya ambapo matokeo yake tukawapata Scottish Rite Freemasons







Baada ya nyumba ya ibada kubomolewa kabisa na Nebuchadnezzar , Wayahudi walikamatwa kama watumwa na kupelekwa Babyloni. Mchoro huo unaelezea safari hiyo ya kuelekea Babyloni.


Hivyo Kabbala asili yake ni Babyloni lakini si huko ilipo anzwa kuwekwa kwenye makaratasi, bali ni Ugiriki na watu wanao tajwa kufanya zoezi hilo ni Pythagoras na baadaye Plato ambaye kwa muda mrefu tena kimakosa alikuwa akitajwa kuwa ndiye muasisi na mtunzi wa Kabbala, lakini la Hasha, Kabbala ni kubwa kushinda Plato mwenyewe, na hata leo inasemwa kuwa asili ya kitabu hichi ni Babyloni lakini hajulikani mtunzi wake ni nani ndani ya hiyo Babyloni ila hakuna shaka kuwa mafunzo haya haikuwa kazi ya binaadam bali Mashetani wenyewe.


Usikose sehemu inayofuata kwenye mtiririko huu, ...


maoni, maswali, michango vyote vinakaribishwa ..

Post a Comment

0 Comments