Header Ads Widget

Responsive Advertisement

NILIFANYA BIASHARA YA VIPODOZI NA MISUKULE




"NILIFANYA BIASHARA YA VIPODOZI NA MISUKULE"
Mara tu bbaada ya kumaliza kidato cha nne Angel aliwaacha wazazi wake Shinyanga na kwenda Dar es salam kukaa kwa shangazi yake.
Angel alivyokua na rika la miaka kumi nane alikua na kijiuso kidogo, macho makubwa ambayo kila wakati yalionekana kama yanatoa machozi, Alikua ana pua ndogo nyembamba chini ya pua hiyo kulipangika safu mbili za midomo ambayo haikutulia kwa kutabasamu kila Mara.
Urembo aliokua nao Angel miaka ile hauwezi jirudia ni saw a alichezea shilingi Chooni.
***
Dar aliishi na shangazi yake maeneno ya Msasani osterbay, mboga tatu kwao haikuwa tabu kama ilivyo sifa ya eneo lile.
Ushamba wa huko alikotok ulimjaa akawa hatoki ndani kama mwali anayesubiria kuolewa.
Jogoo wa shamba hawiki mjini lakini anaweza kulijua jiji kwa kupitapita,Angel mwaka mmoja wa kukaa Dar alikua ashaanza kubadilika tabia, mule ndani pakawa ni kituo cha kulalia tu atokapo kuzurura kwenye jua kali pasipo sababu.
Urembo aliokua nao ANGEL hakuna mwanaume atakayempita asigeuke nyuma kumuangalia wanaume wakaanza kumjua na kumpigia misele ya kila namna ila kitu kilichovutia kwa yule binti hakukurupuka kuparamia mpenzi.
Mwishoni alijikuta anampenda kijana mtanashati na mwenye kazi nzuri ya afisa msaidizi wa mawasiliano katika kampuni ya AIRTELL pia yule kijana aliona ni bahati ya kupata msichana wa ndoto yake.
Kila mmoja alionesha hisia na upendo kwa mpenzi wake si ANGEL wala PATRIC mpenzie.
Upendo wao ulimea katika kipindi cha miezi mitano maamuzi ya Angel kwenda kumtambulisha Patrick kwa shangaze yake wakayafikia hawakuchelewa jambo lile Shangazi wa Angel alilikubali bila kipingamizi
"Nafurahi wanangu kuwa na maamuzi ya busara, kwani mngekua kimya nisingemjua mkwe wangu, siwezi kataa uhusiano wenu najua mmependana na kufanana kabisa ilimradi Patrick ufanye mpango wa haraka umuoe Angel" ni maneno aliyowaambia siku hiyo jambo ambalo waliliweka kichwani kila mmoja akifikiria wataoana lini.
Haikuwa changamoto kubwa katika mahusiano yao changamoto ilikua kwa Angel ambaye kwa kipindi chote kile hakuwa na kazi ya kufanya zaidi ya vibarua vya hapa na pale kama kuwafulia wahindi magagulo yao.
Siku moja akiwa na Patrick aliamua kuongea kuhusu kazi ambayo itamletea faida kubwa ili wajikimu katika maisha kama wakifunga ndoa
"Mpenzi," alita Angel akiwa kamshika mkono Patrick wakitembea katika fukwe za coco beach.
"Niambie mke wangu mtarajiwa" aliitikia Patrick kwa sauti ya mahaba na ya upole.
"Maisha ya kufanya kazi za vibarua yamenishinda miaka inaenda wala sioni faida yake" alilaalmika Angel
"Mh sasa tutafanyaje?"
"Tufanyaje, naomba mtaji nifungue hata biashara"
"Angel unajua biashara inahitaji moyo kuna kupata na kukosa faida na hasara, kustahimili uvumilivu wake unaweza" aliluza Patric baada ya wazo alilitoa Angel kumkaa kichwani
"Baby najua, ndio maana nimekwambia nataka biashara"
"okay unapenda kufanya biashara gani?"
alifikiri angel kabla ya kujibu swali lile
"Biashara nzuri ninayoina ni kuuza VIPODOZI" alijibu
"Vipodozi? hiyo ina kazi nzuri ya biashara?"
"Ndio mpenzi" Siku zote mwanaume huwa dhaifu kwa mwanamke Patrick hakuwa NA njia ya kukwepa swala lile.
"Sawa nimekuelewa nitaenda kukopa bank nikifungulie duka la vipodozi katika soko la Kariakoo" Angel aliposikia vile aliruka na kumkumbatia Patrick asiamini maneno yake.
Baada ya wiki kadhaa kupita jitihada za Patrick kukopa bank zikafanikiwa.
Hakutaka kuupoza ule mkopo moja kwa moja aliacha kazi zake siku hiyo na kuanza kulisaka soko la kariakoo kutafuta Frame nzuri ya biashara.
Siku hiyo ilikua ni ya bahati kwake alikua frame iliyokua katikati ya soko lile mtu anahama hiyo hiyo ndio aliioda akapangisha.
Baada ya kufanya vile alimfanyia Angel surprise ya kumuonesha akimwambia mzigo wa vipodozi ashaagiza baada ya siku kadhaa utatua bandarini.
Furaha aliyokua nayo Angel siku hiyo haikua ya kawaida akiona maisha yanaenda kuwa mazuri. Jambo zuri atakalofanya angel hakusita kumtaarifu shangazi yake kwani bado alikua anaishi kwake.Shangazi yake alimpa baraka tele hasa kwa Patrick aliyejitolea kumsaidia.
Wiki mbili baada ya Frame kupangishwa Angel alikua ndani ya duka likiwa limesheni vipodozi vya aina mbali mbali hasa mafuta ya lotion ya kujipaka.
Kariakoo kuna biashara ya namna zile nyingi na ushindani uliokua katika soko lile yahitaji ujasiri.
Angel alikua anauza bidhaa zake kwa kusua sua sana hakutegemea kama itakua vile yeye alizani ukifungua duka basi siku hiyo hiyo bidhaa zote zitanunuliwa.
Miezi kadhaa kupita faida aliyokua anapata kwa mwezi ni ndogo kuliko ukiangalia wafanya biashara wenzake walileta bidhaa mpya kila mwezi yeye yapata miezi mitatu vipodozi alivyoanza navyo ni vile vile.
"Mpenzi hii biashara sikujua kama ni nzito hivi tangu nianze napata visenti vya kula na kuvaa tu faida haionekani" ni siku moja akiwa kitandani alimuandikia Patrick massage.
"Hee mara hii ushaanza kulalamika?, biashara ndivyo ilivyo mwanzo mgumu lakini ukizidi kumuomba mungu ipo siku utauza mamia kwa mamia, kumbuka bado mkopo hatujaurejesha, usivunjike moyo mpenzi" yalikua ni majibu ya Patrick akijitahidi kumfariji Angel.
Walichart sana usiku ule kuhusu MAPENZI yao lakini Angel hakukublia kabisa kuona biashara yake inaenda namna ile.
"Hapana kesho lazima niende kwa Mwajuma, anieleze anafanya nini mpaka anauza vile" Alongea kimoyo moyo Angel.
Mwajuma alikua ni rafiki wa Angel hakupishana sana kiumri ila Mwajuma aliionesha ana umri mkubwa isipokua mwili ndio uliomfanya alingane na Angel. Walikutana kariiakoo nae akiwa ni mfanya biashara ila si ya vipodozi kama Angel.
Yeye alimiliki maduka zaidi ya matatu ya nguo za kike na kiume akiwa anapata wateja wengi na kuingiza faida kubwa. Urafiki wao ulianza siku moja Mwajuma alienda kwenye duka la Angel kununua vipodozi wakajuana na angel ndipo alipoanzisha urafiki.
Kesho yake Angel alitoka nyumbani kwa shangazi yake akiwa na mawazo ya kumuona Mwajuma aeleze kile anachotaka.
Baada ya kufika dukani kwake alifungua nakusubiri mda uende ili amfate mwajuma kwani biashara yake haikua mbali na kwake.
Lakini ilitokea kama Bahati siku hiyo Mwajuma alienda dukani kwa Angel.
"Shoga angu Yale mafuta si yamenishiia nimekuja kununua mengine" alijitamba mwajuma aliyekua mzuri wastani mwili ulioja kwa kuridhika na hela, kavaa viatu vya mchuchumio funguo ya gari kaitumbukiza katika kidole cha mwisho.
Angel alipomuona alimchangamkia zaidi ya siku zote.
"eh! tena nilikua nampango wa kuja huko kwako shost" alidakia Angel
"Kuna nini tena shoga, au unahisi natembea na bwana ako?' mwajuma alikuabl ni mtu wa utani sana kwa Angel licha ya urafiki wao.
"Njoo kwanza tukae nikueleze vizuri"
"mhh haya"walikubaliana wakaa kwenye viti pamoja.Angel hakujua aanzaje kumuuliza Mwajuma lakini mwishoni alipiga moyo konde.
"Mwajuma tumekua marafiki kwa mda mrefu, kwa hiyo asinifikirie vibaya" alianza kwa kujihami Angel.
"usiogope Angel wewe endelea" Angel alikaa vizuri akashusha sauti yake chini.
"Shost, naona mwenzangu unauza kama unagawa bure yani wateja hawapungui dukani mwako,lakini angalia Mimi tangu nianze wewe ndio mteja wangu mkubwa, nisubiri mafuta yaishe ndio uje kununua,Kwa hiyo chonde chonde naomba siri ya uuzaji wako kama kanisani niende au kama msikitini niingie nimuombe huyo mungu uliyemuomba wewe" alipomaliza kusema vile Mwajua alicheka sana kiasi kwamba alinyanyua miguu juu.Angel hakutegema kwamba Yale maneno yatamchekesha mwajuma, alijua labda ndio atakamsirisha.
"Angel ni hilo tu" aliuliza mwajua akipunguza kicheko.
"Ndio shosti hilo sio dogo"
"Ushamuomba mungu mara ngapi?" mwajuma alianza kumuuliza maswali
"Mara nyingi tu"
"umepata mafanikio gani toka umuombe?'
"Ndio kama haya kidogo kidogo" alinung'unika Angel
"Hivi una fikiri hakuna njia nyingine zaidi ya kumuomba mungu?'aliuliza mwajuma swali lilomtatiza Angel
"una maanisha nini kusema hivyo?"
"usiwe kama umekuja mjini Leo, usifikiri hapa kariakoo kila mtu anafanya biashara kwa kumtegeme mungu, njoo nikupe siri ya mafanikio yangu" mwajuma alimvuta Angel sikio nakulisogeza kwenye midomo yake.
"Siri ni kwenda kwa mganga tu" Angel alichoropoka katika mdomo wa mwajuma kwa mstuko, maishani mwake hakuwahi kwenda kwa mganga wala kuwaza vile.
"Kwa mganga?' aliuliza kwa nguvu mpaka mwajuma alimziba mdomo.
"Shiiip bibieee, isiwe nongwa habari ndio hiyo, kama unahitaji kuwa kama mimi hiyo ndio siri yangu, na kwa uzuri nakupeleka mpaka kwake" alifoka Mwajuma. Swala lile lilikua ngeni kwa Angel ataanzaje kwenda kwa mganga. Alibaki ameduwaa asijue ajibu nini.
"Embu nyanyuka unipe mafuta niende zangu, wewe endelea kujifikria ukizani mafanikio yanakusubiri" alisema mwajuma akinyanyuka ndipo angel nae alinyanyuka na kwenda kumtolea mwajuma mafuta yake.
"shost bye,ukipata jibu usisite kuja kunieleza nipo wakati wowoate maana najua hapo nimekuacha njia panda" Mwajua alikua ni mtu wa kuongea mpaka anaondoka licha ya Angel kuwa kimya.
Siku hiyo mchana iliisha akiwa anawaza maneno ya mwajuma kwenda kwa mganga.
Ilipofika usiku akiwa kwa shangazi yake alitamani kumwambia lakini alisita.
Alichukua simu ili amueleze Patrick habari zile nayo ikawa vile vile moyo ulisita.
Kazi ikawa kwake yeye na nafsi zake kujibizana kwenda au kutokwenda usiku kucha akijigalaza kitandani asioate jibu mpaka usingizi ulipomchukua.
Siku iliyofata akiwa dukani kwake nafsi ya kukubali kwenda ikashinda hakutaka kusubiri alimtafuta mwajuma dukani mwake na kumueleza kuhusu nae ampeleke kwa huyo mganga.
Mwajuma hakuwa na hila alikubali na kumueleza asichelewe hiyo safari waende kesho yake wazo ambalo Angel aliliafiki.
Bila ya Patrick wala shangazi yake kujua asubuhi ya kesho yake aliamka saa kumi na moja akimdanganya Shangazi yake anaenda kuchukua mzigo wa dukani huku Patrick asijue.
Walikubalina na mwajuma kukutaa moroco kwani yule mganga anaishi Tegeta na mwajuma yeye anaishi Kinondoni.
Sehemu waliyoahidiana walikutana na safari ya kweda kwa mganga ikaanza wakitumia gari ya Mwajuma.
Kwa mganga walipofika Angel akielekezwa na mwajuma alieleza shida yake mganga bila kujali alimkabidhi dawa ya kuvutia wateja lakini kwa mashart makuu matatu.
"Kwanza Akishaisindika ile dawa dukani mwake siku zinazofata akifungua duka muda wa kufunga uwe saa moja usiku na atakapofunga asirudi nyuma kulifungua.
Sharti la pili hela atakazopata asizipeleke Bank wala kwenye taasisi yoyote ya kuhifadhi hela ajeengee kabati ndani ya hilo duka ahifadh huko
Tatu asifungue duka lingine atumie hilo hilo moja ndani ya miaka miwili, akitaka kuajiri ajiri lakini sio nje ya hilo duka."
Angel alikubali yale mashart bila kipingamizi wakarudi safari yao ile dawa iliyotakiwa aizindike ndani ya duka SAA moja usiku wa siku hiyo.
Angel mchana wa siku hiyo hakuwa ametulia akihangaika mda ukimbie aiweke ile dawa. Mpaka SAA moja ilipofika alikua ashatembea vya kutosha mule dukani.
Wiki moja baada ya kuweka dawa hali ya duka la angel ikabadilika ghafla wateja wakaanza kumiminika makumi kwa makumi akiuza zaidi laki tano kwa siku angali mwanzoni alikua anauza hata elfu hamsini haifiki.
Mafanikio yake hakuacha kumueleza Patrick hasa alipotaka aagiziwe mzigo Mara mbili pale dukani kwani vitu vinaenda isivyo kawaida.
Patriki akiwa hajui kilichotendeka alimshukuru muumba wake akimwambia Angel ni mungu alisikia kilio chao hivyo hawana budi kumshukuru lakini si kwa angel aliyetumia ushirikina.
Ikapita mwezi, miezi sasa Angel akawa ni maarufu kariakoo nzima kwa biashara ile, Patricki akijisifu kupata mpenzi mchapakazi lakini kitu kilichomtatiza ni kuwa alipomuuliza Angel anaweka hela bank gani alionekana akikwepeshaa maswali Yale.
Kitendo cha Patrick kuanza kumuuliza maswali Angel kikamfanya Angel aone kwamba Patrick anataka kumuingilia katika biashara yake akaanza kupunguza upendo taratibu zile SMS walizokua wanachart usiku zilififia kama kibatari kilichokosa mafutà.
Patrick alipompigia au kutuma SMS mchana alijibiwa
"Samahani mpenzi, niko bize na wateja" akimpigia usiku au kutuma SMS navyo alijibiwa
"Samahani mpenz nimechoka sana nahitaji kulala" kitendo ambacho Patrick kilimkasirisha na kuona siku moja amuendeee huko huko dukani na ni afadhali asingeenda kwani alikuta wateja wanatoka na kuingia akisubiri amalize huyu anakuja mwingine mwishoni alikata shauri.
"Angel kwanini usifunge duka tuongee maana siku hizi ata weekend hautaki kupumzika mpenz"
"Hivi Patrick una akili? yani Mimi niache hela nikusikilize wewe utanipa nini zaidi ya kugombana, naomba ondoka nitakutafuta kwa mda wangu, ukiwa wewe hapa unaleta gundu wateja hawaji" maneno ya siku hiyo yalikupasua ngoma za Patrick asiamini yule angel alimuomba mkopo wa mtaji ata badilika vile hata kabla nusu ya mkopo haujarudishwa.
Alijaribu kila namna akiona ni utani mwishoni Angel alitaka kupigia simu polisi ndipo Patrick aliondoka kwa machungu sana.
Hela zikamjaza kiburi Angel hakukumbuka wazazi wake alitumia hela zike kuruka viwanja na mwajuma pamoja namatajiri wa kike.
Swala lile Patrick alilipeleka kwa shangazi yake Angel na kumueleza jinsi angel alivyobadilika.
"Pole sana mwanangu at a Mimi naona Angel alivyobadilika kwani siku hizi anakuja usiku wa manane kalewa nikuuumuliza ananitukana sijui kapatwa na nini"
Walimjadili sana wakamkalisha Angel chini na kumuleza lakini jeuri ya pesa akawapuuzia alipomuona Shangazi yake anamzingua aliondoka kwa shangazai yake bila kuaga akiwa na kila kitu chake kwa kiburi alienda kununua nyumba kubwa ya mamilioni huko Masaki mwisho akanunua na gari Kali ya kutembelea kwa duka lile lile moja.
*****
Yapata mwaka NA NUSU sasa Angel hana mawasiliano ya shangazi yake wala Patrick wazazi wake nyumbani shinyanga wanalilia shida Ila yeye alijivinjari akiwa na haja humtafuta mwanaume yeyote anayempenda nakutoa haja yake.
Duka limesheheni vipodozi mpaka vingine vikawa vinatolewa nje nakuingizwa aliajirivwafanyakazi wawili ambao aliwalipa mshahara mzuri.
Hakuna anayejua siku ya ajali yake,
Ilikua siku ya jumanne Angel akiwa katika duka lake baada ya wafanyakazi wake kuondoka alikua anahesabu hela za siku hiyo ili aweke kwenye gala lake lilikua mule ndani.
Alifanya haraka haraka kwani ilikua yapata saa mbili kasoro na ilitakiwa duka lifungwe saa moja.
Alipomaliza kuhesabu alizihifadhi sehemu anayoijua yeye kisha akatoka nje haraka na kufunga duka.
Aliliendea gari yake iliyopaki pembeni akataka atoe funguo afungue mlango alipopapasa kwenye mkoba hakukuwa na ufunguo wa gari zaidi ya zile za duka alizoshika mkononi
Alijipiga sachi kila sehemu akiangalia nyuma kama kadondosha lakini haukuwepo mwishoni alikumbuka kaufungia ndani ya duka.
Alirudi tena dukani akiwa na funguo za duka akaanza kufungua duka akisahau mashart mengine ya mganga.
Alifanikiwa kufungua lakini alipokuja kunyanyua macho kutazama mule dukani la hasha hakuamini macho yake.
Alikutana na watu wa kutisha wamejaa mule dukani kama wateja. wale watu walifanan na misukukule, wakishika vile vipodozi vya mule dukani na kuvifanyia mauza uza kama wengine walivipakza vinyesi, wengine walipakaza makamasi.
Idadi ya wale misikule haikuhesabika kila mmoja akishika kitu chake na kuvifanyia vitu vya ajabu.
Angel hakustahimili tukio lile alijikuta anadondonda chini na kupoteza fahamu.
Alikuja kuamka yuko kwenye kitanda cha hospatli alijaribu kujinyanyua lakini alishindwa akajaribu kuongea nayo akashindwa machoni mwake akamuona mwanamke kasimama na bakuli kumtazama vizuri alikua ni shangazi yake aliyemkimbia kipindi kirefu.
Shangazi yake bado alimpenda alipata taarifa za angel kudondoka alienda hosptali aliyolazwa muhimbili.
Madaktari walimuambia Shangazi yake kuwa Angel kapatwa na stroke, iliyomfanya mwili mzima usifanye kazi yani yeye ni wa kugeuzwa, kutolewa kinyesi na anajisaidia hapo hapo kitandani.
Hiyo haikutosha walisema uwezo wake wa kusikia na kuongea itachukua mda mrefu na pia matibabu zaidi yanahitajika aende nchi za nje.
Shangazi yake hana hela wala nini akaanza kufanya mpango wa kitafuta hela lakini duka lake siku ile alipodondoka liliungua lote ghafla,:moto ulisambaa na kufikia mpaka gari yake ikalipuka, kila kitu kilichokua ndani ya duka au gari kiliteketa kwa moto.
Alichunguza marafiki wa Angel akawafata kuwaomba msaada lakini walidai hawana hela wala pia hawakuonekana hosptali kumtembelea Angel si mwajuma wala nani.
Suluhisho la mwisho lilibaki ni kuuza nyumba ya Angel baada ya shangazi, ndugu na wazazi wa Angel kuafikikiana walikubali kuiuza jela zilizopatikana ndio zikampeleka Angel India kutibiwa.
Licha ya kupelekwa India Angel alirudi Tanzania akiwa anasikia kwa umbali na kuonge kidogo, akawa kilema wakutembea na baiskeli.
"Shanga.....zi, Patrick yuko wap" aliuliza siku moja akiwa anasukumwa na baiskeli na shangazi yake wakimsafirisha kwenda Shinyanga kijijini kwani maisha ya mjini katika hali ile ni magumu hasa mtu wa muangalia
"Patrick, bado unamkumbuka?
sasa hivi anaozea jela mwenzako, zile hela alizokopa alishindwa kurejesha akafungwa" Angel aliposikia hivyo akiwa anashusha maudenda kama tahira alianza kulia kwa kumkumbuka Patrick wake.
Alijuta kwenda kwa mganga ule urembo wake ulipotea akawa na ngozi iliyokakamaa kama mzee angali ndio alikua ana umri wa miaka ishirini na tano tu.
Iligundulika kuwa wateja waliokua wanaenda kununua vipodozi kwake walikua wanatolewa kafara kwa mwezi watano na akitolewa kafara anaekwa msukule ndani ya lile duka bila ya wateja wala Angel kujua.
Angel alijutia na kunung'unika moyoni
"KUMBE NILIFANYA BIASHARA NA MISIKULE" Kutoka kwenye ufahari leo hii anatembelea kibaiskeli, kwa kusukumwa, chakula analishwa, kuoga n vitu vyote anafanyiwa hana uwezo wa mwingine.
Wale ndugu aliowatupa ndio wanamsaidia shughuli zote zile. Marafiki aliokua nao anaruka viwanja, gari ya kifahari ama ile nyumba vyote vilipotea kama upepo.
*****MTAKA SABA NYINGI KWA PUPA,HUPATA MINGI MISIBA********mwisho****
UJUMBE: Ni heri mtaji wa elfu kumi unaokuzailishia elfu hamsini ya faida kwa mwezi ya HALALI, kuliko
Mtaji wa elfu kumi unaokuzalishi faida yamilioni kumi kwa wiki kwa HARAMU.
Usiharakie Maisha kama rizki ipo ipo tu japo itacheleweshwa lakini MTUMAINIE MUNGU WAKO. usimtegeme mwanadamu mwenzako.

PATA NAMBA YAKO YA KITAMBULISHO KWA KUPAKUA APP HII BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments