Header Ads Widget

Responsive Advertisement

USIMTUKANE MAMBA KABLA HUJAVUKA MTO




 USIMTUKANE MAMBA KABLA HUJAVUKA MTO

Abubakari ni kijana yatima ambaye alizaliwa katika kijiji cha Mwenda kulima wilayani Kahama mkoani Shinyanga. Alibahatika kulelewa na wazazi wake wote wawili kuanzia akiwa mdogo mpaka akasoma na kufikia level ya kidato cha sita,Bahati ya yeye kuendelea kuishi na wazazi wake ilitoweka Mara baada ya wao kufariki dunia Siku chache baada ya yeye kuhitimu kidato hicho cha sita.Walifariki kwa mkupuo Kutokana na ajali ya Basi na hivyo kutoweka kabisa duniani na kumuacha peke yake akiwa hana ndugu yoyote wa karibu.
Ndoto yake kubwa aliyokuwa nayo ndani ya moyo wake ilikuwa ni kusoma kwa bidii hadi kufikia elimu ya juu zaidi itakayo mkwamua hata kimaisha,Lakini ndoto hiyo ilitaka kukatika Mara baada ya yeye kuchaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine kilichopo huko mkoani Morogoro,alichaguliwa kwa kozi ya sayansi ya wanyama (Animal Science) Lakini kwa bahati mbaya hakupewa mkopo wa kumsaidia kimasomo hususani kwenye suala la meals and Accommodation na masuala ya stationary .Si kwamba hakuwa na sifa za kupewa huo mkopo hapana,alikuwa nazo zote lakini Bahati hakuwa nayo.Aliumia sana maana alijua tayari kasha ipoteza furusa la yeye kuipata hiyo elimu ya juu.Hakuwa na mtu au ndugu wa kusema kwamba Labda atamsaidia hivyo roho ya kukata tamaa ilianza kumnyemelea,,marafiki zake aliokuwa nao ambao wote walipewa huo mkopo walianza kumdharau na kumsimanga Abubakari hususani pale anapowaomba msaada wa pesa kidogo za chakula hapo chuoni mpaka ikafikia kipindi wakawa wanamkepa na wakati mwingine kumwambia makavu.
"We dogo sisi tumechoka kukusaidia. Sasa ushauri wetu kwako uko hivi:Rudi kijijini tu ukaanze biashara ya kuchoma mkaa maana hakuna namna,tutakusaidia sawa kwenye hutu tupesa twa chakula lakini je kwenye hayo mamilioni ya karo nani baba yako atakaye kulipia?.Dogo jiongeze LA sivyo yatakutokea puani.Elimu ya juu ina wenyewe bwana,siye Mungu alituandikia barua na kutuambia tutasoma mpaka Oxford na mpaka mwisho wa elimu hii ni kwa sababu tuna nyota tena iliyotukuka.Sasa kwa nyinyi mliokurupuka kuja huku Wakati hata nyota hamna mwaka huu lazima mfe njaa.Sisi wala hatuna shida acha tule mema ya nchi"
Hayo yalikuwa ni baadhi ya maneno ya masimango aliyokuwa akiyapata kwa marafiki zake hao waliokuwa wakijiita kwamba wao ndio wao .Abubakari aliumia sana,uchungu ulimwingia pindi alipokuwa akiwaona Siku zingine walifanya asana na kuja na wasichana mbele yake kwa ajili ya kumwonyesha kwamba wao ni matawi ya juu na ni moto wa kuotea mbali.
"Daah cheki bonge la mtoto huyu jinsi alivyonona,weeee Mungu atupe nini,Mimi Nina bonge la mtoto na nyie machali zangu mna watoto wakali ,ama kweli mwenye nacho atazidi kuongezewa.Sasa machoko kama kina Abubakari sijui watamiliki lini watoto wakali kama hawa.Ile buku tu ya kula chakula cha kina mama ntilie imemshinda sembuse na kumiliki hii mizigo,lazima wapasuke msamba kudadeki zao .Abubakari chali wangu unauona huu mzigo? Hahahaa!! Utaishia kula kwa macho tu na kuzidi kuwatumia ndotoni au kwenye punyeto Lakini kuwa nao karibu ni sawa na panya kugombana na simba,,dogo katembeze tu karanga huko kijijini kwenu maana elimu ya juu imesema haikutaki na ndio Maana hujapewa hata mkopo".
Masimango yalipozidi Abubakari aliamua kukata rufaa kwenye bodi ya mikopo Lakini napo mambo yakazidi kuwa mabaya tu Maana iliishia kuwekwa kapuni na kutotolewa majibu yoyote .Aliendelea kusubiria hatimaye akachoka na kuamua kutaka shauri ya kuahirisha mwaka wa masomo ili akajihangaikie huku na huko kutafuta pesa ya kumsomesha. Alionana na uongozi wa chuo nao Bila hiyana walimkubalia ombi lake. Sasa Wakati anafunganya mabegi yake kurudi nyumbani huko kijijini kwao wengi walimcheka na wengine walisikika wakimsengenya huku wakisema .
"Mwoneni ndugu yenu yamemshinda,si tulimwambia akauze karanga kijijini harafu yeye akajifanya mjuaji dadeki ameshaumbuka sasa!!.Alikuwa anadhani elimu ya juu ni ya kukurupukia ,huku tunatembea under dream. Sasa yeye kama alikuwa anasubilia embe juu ya mnazi naona kashalipata mwacheni akajaribu bahati yake kijijini Labda hata kuchoma mikaa kutamtoa kimaisha, ila elimu ya juu aisahau kabisaaa! Na atuachie sisi tu".
Abubakari alirudi kijijini na kuanza kujihangaikia na kupanga mikakati ya kuanza ili malengo yake yatimie na mwaka unaofuata arudi tena chuoni. Japo hata wanakijiji hususani wale waliokuwa wakimfahamu walianza kumcheka huku wakimkejeli Lakini yeye wala hakuwasikiliza Maana mipango yake aliijua mwenyewe. Basi alimtanguliza Mungu Katika mipango yake yote na baada ya wiki moja kupita alichukua baadhi ya bahasha Zake na kuelekea kwenye shule moja ya Sekondari Kwa ajili ya kuomba kufundisha kwa muda.Kutokana na masomo yake kuwa ya sayansi yaani Chemistry na Biology hakupata shida ya kukataliwa ombi lake,,lilipokelewa na yeye akaanza hiyo kazi moja kwa moja.Hakuwa na muda wa kupoteza alijituma kuwafundisha wanafunzi kwa juhudi zake zote Maana alifahamu hiyo ndiyo siri ya kukubalika na kupendwa na wengi hususani walimu na wanafunzi. Kweli Katika hilo alifanikiwa na akaweza kupendwa na wanafunzi wengi na hivyo kumchochea kuendelea kupewa ruksa ya kuendelea kufindisha pale.Mshahara aliokuwa akilipwa hakuutumia vibaya, bali aliuhifadhi kwenye akaunti yake kila akipokea.Alijiwekea jambo moja zuri sana,yaani kila mwisho wa mwezi akipewa tu huo mshahara wake ni lazima robo tatu yake aihifadhi .Alifungua hadi kijiwe chake cha tuition na chenyewe kikawa kinamsaidia kuzisogeza ndoto zake za kumrudisha tena chuoni.
Baada ya miezi sita kupita, Abubakari alijaribu tena bahati yake ya kuomba tena mkopo Maana aliuamini ule msemo wa "Bahati hubahatishwa". Alikamilisha kila kitu kwa ufasaha zaidi na baada ya hapo akarudi kuendelea na mihangaiko yake ya kila siku.Miezi ilipita hatimaye siku za kurudi chuoni zikawadia,kwa bahati nzuri ndani ya akaunti yake kulikuwa kunasoma kiasi cha Shilingi milioni tatu za kitanzania na hivyo kumhakikishia safari ya kurudi tena huko chuoni. Alifika na kufanikiwa kuanza upya masomo yake kwa mwaka wa kwanza, hii ilitokana na yeye kuahirisha masomo yake kabla hajafanya mitihani yake hususani ile ya mhura.Mungu nae alimsaidia na akawa amepewa na huo mkopo hivyo kumhakikishia kuipata hiyo elimu yake kwa uzuri zaidi mpaka akaamini kwamba kumbe Mungu si athuman.Wote waliokuwa wakimcheka na kumdharau ikiwemo marafiki zake walibaki mdomo wazi na wasiamini kama Abubakari amerudi tena chuoni na wakati walimtabiria kuja kuwa mchoma mkaa au muuza karanga .Kuna baadhi hawakufanikiwa kuingia mwaka unaofuata Maana walifeli na kufukuzwa chuo na mijigambo yao ikawa imeyeyuka ,na kuwapelekea wao wakawe ndo wauza karanga na wapiga debe wakubwa mitaani. Abubakari alizidi kujituma zaidi na zaidi huku akiachane na mambo mengine ya ajabu ajabu tofauti na kujikita kwenye masomo yake tu.Sasa baada ya miaka kama minne kupita baadhi ya marafiki zake walihitimu masomo yao na kurudi makwao kusubiria ajira ,walisubili sana hatimaye ajira zao zikatoka Lakini kwa bahati mbaya wao hawakupata bahati hiyo ya kuajiriwa, sasa walianza kujihangaikia kutafuta kazi na vibahasha vyao Lakini napo waliishia kukataliwa tu na hivyo kuzidi kuzididimiza ndoto zao za kupata kazi serikalini na kuwasaidia kuwa na maisha mazuri. Walijikatia tamaa na kubaki kujilaumu kwa nini waliutumia mkopo wao chuoni Kwa anasa na wasijiwekee hadhina ,waliutumia sana ule msemo wa "TUNGEJUA" Wakati maji yameshamwagika chini.
Matumaini yalizidi kujionyesha dhahili kwa upande wa Abubakari kwani baada ya miaka yake minne ya masomo kumalizika alihitimu kozi yake ya utaaramu wa wanyama na kurudi Kijiji kuendelea na majukumu yake kama kawaida. Sasa baada ya Siku nyingi kupita ajira zilitoka na Abubakari akawa ameajiriwa moja kwa moja kama Afisa mifugo kwenye wilaya moja huko mjini Dodoma. Hivyo Maisha yake yakawa mazuri na machungu yake yote akaanza kuyasahau. Mambo hayakuwa hivyo kwa upande wa marafiki zake Maana wao hawakuipata hiyo bahati bali Maisha magumu ya kusota mitaani yalizidi kuwaandama.Hawakuwa na wakumlaumu Maana walijifanya wajanja wa kumtukana mamba kabla hawajauvuka mto.
===>Sasa hili nifundisho tosha kwa watu wote wanaowadharau na kuwacheka wenzao kwamba wanaishi Maisha ya kifukara tofauti na wao,jambo hilo si zuri Maana kila aliyepewa pumzi ya uhai awe Maskini au kichaa amepewa neema na mwenyezi Mungu na huwezi jua kesho yake atakuwa wapi.Isije kuwa ukamdharau Leo harafu kesho akaja kukuajiri.

Post a Comment

0 Comments