Header Ads Widget

Responsive Advertisement

INATOSHA - 5



Simulizi : Inatosha
Sehemu Ya Tano (5)


Ilipoishia jana..

Nilishangaa kwa mara nyingine tena Gervas akimfuata Jammy nakumkumbatia kisha bada ya pale Gervas alinifuata na mi nakunikumbatia,
"Levina...? Nakupenda na Jammy nawapenda sana"
"hata sisi Gervas tunakupenda...!"

Songa nayo sasa…

Maisha yaliendelea kupendeza zaidi kwani kwa sasa tulikuwa tukiishi kama wanandugu tena wale wa damu na siyo wachumba tena,niliishi mi Gervas na Jammy huku mfanyakazi wa ndani alitusaidia kwa kupika chakula,hata inapofka muda wa kulala huwa kila mmoja anachumba chake,
Nakumbuka siku moja ambayo ilikuwa ni sikukuu tulitengeneza chakula kizuri nakuwaalika marafiki,hivyo tulisherekea vizuri kwa kunywa nakucheza muziki na hata ilipofika muda wakulala kila mmoja alilala kwake,kwa upande wangu nilikuwa nimelewa sana kiasi chakuamua niwahi kulala,lakini mkojo ndio tatizo kubwa nilikuwa nalo hivyo kila baada ya muda nilikuwa ni mtu wa kwenda chooni kukojoa na kwa kipindi hiki nikasahau njia ya kuingia chumbani kwangu nakujikuta nikiingia chumba cha Gervas bila kujua,na nilipoingia nilijisogeza mpaka kwenye kitanda chake kwakuwa taa ilikuwa imezimwa Gervas hakuweza kunigundua kiurahisi kwanza alikuwa kapitiwa na usingizi, hapo hapo
Nilianza kumpapasa kuanzia shingoni mwake huku nikishuka mpaka kifuani mwake hakika nilivimisi vitu vingi kwa Gervas,nilijihisi kama pombe yote imeniisha kwani niliendelea kumshika shika Gervas bila ya yeye kushtuka,mpaka nikafanikiwa kumvua nguo,hivyo nikaanza kumchezea viungo vyake vingine vya mwili akashtuka,
"nani...? Toka hapa toka...?"
Gervas alikuwa ameshtuka nakuanza kupiga kelele hapo hapo nikamyamazisha,
"ssshhh...! nyamaza Gervas usiku sasa hivi..."
Alinielewa nakulegea huku akionesha kukubaliana na mimi kwa kitendo nilichokuwa nakifanya kwake,
Nilivua nguo zake zote kisha nikazivua na za kwangu nakuendelea na yetu. Nilifurahia sana siku hiyo. Nilikumbuka maisha ya nyuma kati yangu na Gervas, Nilikumbuka mapenzi yake ya nyuma. Hakika ilikuwa ni siku iliyojirudia katika maisha yangu.

****************
Asubuhi na mapema mfanyakazi wa ndani alikujaa mpaka chumbani kwangu kuniamsha.
"Dada.., chai tayari,nenda ukanywe sebuleni,wenzako wakina Gervas wanakusubiri..."
Nilishusha pumzi nakutoka kitandani. Nikachukuwa mswaki wangu nakuingia bafuni baada ya hapo nikachukua gongo langu la kutembelea nakuacha kibaiskeli changu huku nikiongoza moja kwa moja mpaka sebuleni, aibu kubwa ilinishika pale nilipowakuta Jammy akiwa na Gervas wanakunywa chai,
"Levina...,yani bado ulikuwa umelala tu mpaka sa hivi...?"
"...ujue jana nililewa sana hata nilivyopatapata usingizi sikujitambua kwani jana sherehe iliishaje..."
"tuliwasindikiza wageni wote mpaka nje,kisha tukanywa sana kila mtu akaenda kumalizia kunywa chumbani kwake...."
Nilitoka pale nakwenda kuoga,kisha baada ya hapo nikajiandaa vizuri huku nikijisogeza sebuleni kunywa chai,
tulikunywa chai lakini kila nikimwangalia Gervas aibu kubwa inanishika nabaki naguna huku nakuangalia chini.

~ BAADA YA MIEZI 4 ~

Mazoea ya kuishi kama ndugu yalituteka sana,hakuna hata siku moja tuliogombana wala kufanyiana kitu chochote cha ajabu,
Siku moja nikiwa njiani ndani ya gari nikielekea mabibo nilikuwa mimi,Gervas,na Jammy pamoja na dereva, siku hiyo kulikuwa na foleni sana ikatubidi kutumia njia ya mkato ya kupitia Ubungo ili tuweze kutokea Mabibo mara gari yetu kwa bahati mbaya ikakutana uso ka uso na lori aina ya fuso kitendo hicho kilifanya upande mmoja wa dereva uharibike vibaya,
"Gervas...,Gervas...? Jammy..., Jammy...?"
Maskini dereva alikuwa ameshapoteza maisha huku Jammy akiwa hajielewi wala kujitambua ikanibidi niombe msaada fasta nakuwakimbiza hospitali na Tax lakini kabla hatujafika hospitali,
"Jammy...! Jammy..., Jammy amka Jammy...?"
Nililia kwa uchungu sana huku nikiwa siamini kama nimempoteza Jammy kwani kiukweli alikuwa hata hapumui,na tulipofika tu hospitali walimpeleka moja kwa moja mpaka monchwari yeye na dereva na kisha Gervas wakampeleka chumba cha wagonjwa mahtuti 'ICU' kwani na yeye alikuwa hajitambui kabisa,
Nililia sana huku nikiomba mungu japo Gervas apone kuliko kuwapoteza wote,nilisisimka sana,nakutetemeka nikijiuma uma huku nisielewewe chakufanya nakutamani hata ingekuwa ni ndoto tu,
"Dada unaitwa nani...?"
Aliniuliza nesi mmoja aliyekuja huku akionesha kuwa kuna habari amezileta,
"naitwa Levina.., vipi hali ya mgonjwa wangu huko...?"
"mbona unaharaka hivyo...?"
"yeah...,ndio mimi,vipi anaendeleaje...?"
"Tumejitahidi kwa kila uwezo na tunasikitika kukwambia kuwa Gervas ameumia sana upande wa kwenye mbavu zake ila chakusikitisha ni kwamba tumemkata mkono mmoja hivyo..."
"ooh my god...! Gervas wangu au..?"
"Ndio huyo huyo pole sana dada yangu..."
Nilikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa nikaongoza moja kwa moja mpaka chumba alichokuwepo Gervas na nilipoingia tu nilikutana na jopo la madokta huku Gervas akiwa kawekewa
Dripu na mirija ya kupumulia,nilijihisi nina mikosi tena mikubwa mno maishani mwangu Levina mimi.
Niliganda pale hospitali huku nikisubiri japo Gervas aweze kutoa hata macho nami nipate kuondoka kwani nilikuwa bado sijiamini amini kama kweli Gervas yupo hai tena.
"...dokta lakini si atapona tu...?"
"yeah..,usijali mgonjwa wako atapata nafuu tu.."
Madokta walinipa moyo sana hivyo sikuwa na jinsi zaidi ya kurudi nyumbani nakujua taratibu ya mazishi ya dereva na Jammy itakuwaje.

¤¤¤¤¤¤¤¤¤
Ndani ya kama siku mbili tulikuwa tumeshamzika Jammy na dereva taksi. Watu hawakuwa wengi sana,nilipewa pole na majirani waliokuwa wakinifahamu huku wengi wao wakinipa rambi rambi zao.
Maskini Gervas hakuwepo kabisa kwenye msiba kwani alikuwa hospitali akiugua,siku hiyo hiyo baada tu ya msiba sikutaka kabisaa kupoteza muda ikanibidi kwenda kumuangalia nakujua taratibu zinakwendaje huko hospitali,
Nilikodisha teksi mpaka hospitali ya 'Hindu Mandali' pale posta ambapo ndipo alipokuwa amelazwa Gervas na nilipofika tu niliongoza moja kwa moja mpaka kwenye wodi niliyoelekezwa nakumkuta,lakini kwa sasa hali yake kidogo ilikuwa tofauti na siyo kama mwanzo nilivyomuacha kwani hata ile mirija yakupumulia ilikuwa haipo tena hivyo alikuwa akibadilishiwa dripu tu,
"Gervas...?"
"ndio Levina umekuja? Kuniona...?"
"ndio nipo hapa kwa ajili yako nakukujulia hali pia..."
"na Jammy ndio hataki kuja kuniona kabisa...?"
Nilisisimka ghafla nakuanza kutetemeka huku meno yakiumana na vidole kushikamana kwani kiukweli Gervas hakuwa anajua lolote kuhusiana na kitu kilichotokea na kwa yeye kumbukumbu zilikuwa bado hazijamrudia vizuri juu ya tukio lililomtokea.
Ikanibidi nimdanganye japo aridhike.
"Jammy yupo na amekumis sana..."
"mbona hujaja naye sasa...?"
"nilimwacha akikuandalia mtori hivyo baada ya kama lisaa atakuwepo hapa kukuletea..."
"nitashukuru sana,kumbe kweli bado mnanipenda..?"
"ndio tunakupenda nakukujali sana Gervas..."
Nilimdanganya nakumlazimisha japo ale chakula nilichomletea cha viazi vya kusagwa pamoja na juisi, akanywa na kisha baada ya hapo nikamwacha apumzike huku nikimsisitizia kuwa Jammy atamletea chakula kingine.

~ BAADA YA SIKU TANO ~

Gervas aliendelea kuweka chuki zaidi kwa Jammy ambapo alijua bado yupo nyumbani na hataki kuja kumjulia hali, ilikuwa ni kazi ngumu kwangu kumwambia kama kweli Jammy kafariki kwenye ile ajali kwani ningemletea Gervas matatizo makubwa sana ikizingatia bado Gervas anaumwa nakumbukumbu hazijamrudia vizuri.
Nakumbuka niliongea vizuri nadokta aliyekuwa anamtibia Gervas na akaniahidi kesho yake asubuhi nije kumchuka Gervas nakufanya malipo yote aliyokaa pamoja na gharama za operesheni ya mkono aliokatwa.
Hivyo ilipofika kesho yake nilikuwa nahamu kweli nirudi kuishi na Gervas nyumbani kwangu hivyo nikafanya kujiandaa fasta nakuongoza mpaka hospitali na nilipofika nilifika mpaka pale kwenye kitanda alichokuwa kalazwa Gervas napo sikumkuta,kijasho chembamba kikaanza kunitiririka huku nikijipa moyo huenda wamempeleka kujisaidia hivyo nikakaa kwenye kitanda chake nikimsubiri,nilikaa kama dakika kumi sikuona chochote zaidi yakushuhudia mgonjwa mwingine akiletwa nakulazwa kwenye kitanda akichokuwa kalazwa Gervas huku nikinyanyuka pale nakuwapisha,
Hapo hapo akili yangu ikanituma niongoze mpaka ofisi ya dokta kumwangalia napo nilipofika sikumkuta Gervas.
"Dokta...? Gervas yuko wapi...? Gervas wangu yuko wapi..?"
Nilikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa na sikutaka kumwelewa kabisa dokta.
"ameshakuja kuchukuliwa..."
"na nani sasa...? Na nani...?"
Nilijikuta nikilivuta koti ka dokta kwa nguvu zote huku nikiwa na machungu yakutokujua Gervas amepelekwa wapi,
"...calm down mama..!,calm down...!"
Nilimwachia koti lake nakumtaka aniambie ukweli Gervas yuko wapi.
"walikuja wanaume wawili na Mmama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Jamila au Jammy nakumpa pole sana mgonjwa nakumuomba msamaha kwa kutofika tangu alipokuwa kalazwa, huyo Gervas alionesha kuwafahamu hao watu kwani alikuwa akicheka nao na pia yeye mwenyewe Gervas ndiye aliyeamua kuwa wamlipie gharama za pale kisha wakaondoka naye..."
"...n o o o o o o o o o Dokta Jammy alishafariki...!,wamekudanganya hao...!"
Nilitoka haraka haraka uku nikitembea kwa gongo langu moja kuelekea kwenye taksi nakuongoza kwanza mpaka nyumbani kwangu huenda wamempeleka nyumbani kwangu na nilipofika mpaka ndani sikumkuta mtu yeyote hivyo nikatoka tena mpaka getini na nilipofika getini tu,
"mamaaaa uwiiih....!"
"Gervas...? Gervas...?"
Gervas alikuwa kabadilika rangi ya mwili wake kabisa mithili ya mtu aliyenyeshwa sumu,alikuwa kalala pale nje ya geti,
Ile nataka tu kumshka ili nimnyanyue,
"hapo hapo...! usiinuke,uko chini ya ulinzi kuanzia sasa..."
Sikuweza kugeuka nyuma ili nimjue ni nani aliyeniweka chini ya ulinzi na nilitazama mbele ambapo macho yangu yalikutana moja kwa moja na gari lenye namba 'PT 3005'
hapo hapo akili yangu ikanituma ni gari ya polisi hivyo nikainua mikono juu kuashiria nimesalimu amri japokuwa sikujua kosa langu haswa.
Watu waliokuwa wamevalia mavazi ya kipolisi takribani sita huku wakiwa wameshika silaha za moto mikononi mwao walinisogelea karibu wakitaka kunikamata.
“ Levinaaaaaa… Levina usikubali wakukamatee haoooooo…!!!”
Ilikuwa ni sauti ya Gervas akinisihi huku sauti yake ikionesha kukwaruza kwaruza. Nilibaki nikitoa macho yangu kuwatizama ambapo askari mmojawapo alimgeukia Gervas na kukoki bunduki yake kisha kuanza kummiminia risasi Gervas. Niliumia moyo sana kumshuhudia Gervas wangu akiteketezwa kwa risasi mpaka kufa. Damu nyingi zilimtoka maeneo ya usoni na kifuani. Wale watu hawakuwa na huruma hata kidogo ndio kwanza wakaendelea na safari ya kunifuata eneo nilipo.
Nilitumia macho yangu kuangaza huku na kule nakuona upenyo.Nikajibiringisha kurudi nyuma ya geti nakubamiza geti. Kilichofuata niulianza kusikia milio ya risasi mfululizo ikipigwa eneo la geti, Mungu ndiye pekee aliyeniokoa kwani risasi nyingi. Nilikuwa nikizishuhudia zikipenya masikioni mwangu. Haraka haraka huku nikihema kwa juu juu nikajikongoja na magongo yangu ya kutembelea, Nikazunguka nyumba kwani niliamini nikiingia ndani watafungua geti na wakinipata wataniteketeza. Ndani ya muda mchache nilikuwa tayari nimezunguka ndani ya nyumba na tayari akili ilinituma kuupanda uzio nakutokea upande wan je. Sikuweza! Sikuweza kwakuwa nilikuwa sina uwezo kwani miguu yangu haikuwepo. Nilikuwa ni mlemavu. Nikakimbilia mpaka katika banda la mbwa . Haraka haraka nikawafu ngulia mbwa kisha nikaingia katika banda la mbwa. Nikajificha!
Kilichoendelea nilisikia milio ya risasi uku mwa wakionesha kufoka,niliamini wale majambazi wanamalizia hasira kwa mbwa wangu. Nikabaki nikijikikunyata mwenyewe kwa woga. Nikiwa bado nimezubaa peke yangu bandani. Mara,
“ Huyu hapa mpumbavu, huyu uku bandani tumepata!”

Maskini jambazi mmoja wapo alikuwa yupo mbele ya macho yangu, mbele ya banda langu la mbwa nilipojificha. Akarusha bunduki yake pembeni kisha akaanza kulifungua banda kwa lengo la kunitoa..
**********************************************
::: Inamaana Levina amekamatika?? Je atasalimika hapo?? Na ni kina nani hao waliofanya mauaji ya Gervas??

:::: Mwisho wa INATOSHA. Kumbuka bado Simulizi hii inaendelea na Sehemu ya Mwisho kabisa inaitwa.. NIACHE NA MOYO WANGU… ambayo ni Part 3 na ya mwisho kutoka SITAKI TENA… itakujia hivi karibuni hapa hapa

MWISHO

Post a Comment

0 Comments