Header Ads Widget

Responsive Advertisement

SIRI YA MWANAMKE MJANE




Kuna mjane mmoja mwenye watoto wawili hapo kisiwani Zenj aliweza kukaa na wanaume wawili bila matatizo yoyote kwa zaidi ya miaka minne. Zaidi aliweza hata kuwafahamisha wanaume hao kuwa wanakula chungu kimoja, bila ya tatizo lolote... Akiwa ni mjane katika umri mdogo hii ni baada ya kutwangwa talaka na mumewe, mjane huyo kwa jina la Zuhura(sio jina lake halisi) alijikuta akifanya mapenzi na mume wa mtu kwa jina la Bakari(sio jina lake halisi). Walikutana katika moja ya baa mashuhuri hapo kisiwani na ni Zuhura ambae alianza kumchokoza Bakari, baada ya kumpa ofa ya bia kadhaa kabla ya kumwomba kukaa nae katika meza moja. Jioni hiyo ndani ya baa hiyo kulikuwa na rusha roho na kama kawaida ya wasichana/akinamama/akinadada wengi visiwani humo uitumia siku kama hiyo kurusha vijembe kwa mahasimu wao. Hata baada ya kwisha kwa rusha roho a

Zuhura ambae alikuwa akitamba muda wote wa rusha roho, alimwomba Bakari afuatane nae usiku huo. Bakari alishindwa kufanya hivyo kwani mama watoto wake alikuwa akimsubiri nyumbani kwake. Hivyo siku hiyo ya kwanza ilikwisha kwa mapenzi mepesi kati yao, na kupanga kukutana tena siku ya pili katika baa hiyohiyo. Hivi ndivyo Zuhura alivyoweza kukutana na Bakari. Akiwa amezungukwa na warembo watatu, kijana Franko(sio jina lake halisi)alionekana mwenye furaha tele mbele ya wadada wale watatu. Meza yao ilikuwa imesheni aina kadhaa za bia zilizokuwa zimeshafunguliwa na zile ambazo zilikuwa zikisubiri kufunguliwa. Akina dada wale ndio waliokuwa wametala meza ya Franko na muda wote waliweza kuteka karibu kila mnywaji katika baa hiyo kwa vicheko vyao visivyokwisha. Ilikuwa ni wazi kuwa kila mtu alitamani kuwa katika meza hiyo. Pembeni ya meza ya Franko, alikuwa amekaa msichana mmoja ambaye kila mara alikuwa akimtupia macho Franko, hakuwa mwingine bali ni Zuhura. Kadili muda ulivyokuwa unakwenda ndio meza ya Franko ilivyozidi kupungukiwa na watu hadi akabaki msichana mmoja tu ambaye nae alionekana kuwa amelewa vya kutosha. Muda si mrefu msichana huyo wa mwisho nae alijiondokea zake na kumwacha Franko akiwa peke yake. Hali hii ilimfanya Franko kumkaribisha Zuhura katika meza yake, na bila kinyongo Zuhura alikaribia. 

Baada ya maongezi ya hapa na pale Franko na Zuhura walionekana kama ni watu ambao wanajuana kitambo, hii yote ilitokana na uwezo mkubwa wa Zuhura katika maongezi ambayo yalitawaliwa na kuwakandia wale wasichana watatu waliokuwa na Franko awali. Hata walipotosheka na unywaji wao Franko aliongozana na Zuhura nyumbani kwake. Huu ndio ulikuwa mwanzo wa mapenzi yao. Franko akiwa ni bachela na Zuhura akiwa ni mjane. Zuhura alipenda zaidi maisha aliyokuwa akiishi Franko, kwani aliweza kupata faragha bila tatizo kuliko kwa Bakari. Bakari akiwa ni mume wa mtu iliwalazimu kukutana katika nyumba za wageni katika faragha yao. Zaidi Bakari hakuwa mtu wa kutoka kila siku kama Franko, ambae kila siku jioni alikuwa akionekana katika baa mbalimbali. Muda ulivyozidi kwenda Bakari alijikuta akimpenda zaidi Zuhura kiasi cha kwenda kumtambulisha kwa mama yake. Hatua hii iliongeza kasi ya mapenzi yao kwani sasa waliweza kukutana kwa mama yake Bakari na kumaliza shida zao pasipo usumbufu wa kwenda kwenye nyumba za wageni. Ni katika hatua hii Zuhura alimkaribisha Bakari nyumbani kwao na ikiwa ni ruhusa kwa Bakari kwenda kwa Zuhura ambae alikuwa akiishi na baba yake. Kwa upande wa Franko hakuwa na shida sana na kuonana na mrembo wake Zuhura, kwani hata asipokutana nae baa, hujua kuwa Zuhura anatakwenda kulala kwake. Na iwapo inatokea tatizo la Zuhura kushindwa kwenda kulala kwa Franko, taarifa hutolewa mapema. Maisha haya ya Zuhura na mabwana wawili wasiojuana yalikwenda vizuri tu kwa muda mrefu. Bakari akitamba na Zuhura katika rusha roho huku Franko akitamba nae katika muziki wa dansi na madisco.

 Zuhura ambae alikuwa na marafiki wengi katika baa aendazo aliweza kuwaambia rafiki zake wasijaribu kamwe kutoa siri yake. Aliweza kuwanyamazisha kwa kuwapa ofa nyingi za bia. Marafiki hao kwa wakati tofauti walitambulishwa kwa Bakari na Franko. Walikuwa ni wahudumu wa baa walioanzisha kuvujisha siri ya Zuhura, hii ni baada ya Zuhura kufuruliza kwenda kwenye baa moja akiwa na Franko leo na kesho akiwa na Bakari. Kipindi hiki mkewe Bakari alikuwa amesafiri na Zuhura kwa mara ya kwanza aliweza kwenda kulala kwa Bakari, huku akipangua ratiba ya kulala kwa Franko kama kawaida yake. Siri hii iliwekwa wazi akiwa na Bakari ambapo walikorofishana na kila mtu kutimka kivyake usiku huo. Hii haikuishia kwa Bakari tu kwani siku iliyofuta Franko nae alifahamishwa hilo akiwa peke yake na hata Zuhura alipofika alimkuta Franko asie mjua. Hali haikuwa nzuri kabisa kwa Zuhura kuwapoteza wapenzi wake wawili kwa mpigo. Akitumia uwezo wake mkubwa wa kuongea, taratibu aliweza kumshawishi Bakari kuendelea na mapenzi yao. Kwa upande wa Franko aliwatumia zaidi marafiki zake wa kiume ambao walikuwa ni marafiki wa Franko vilevile kumrudisha katika himaya yake. 

Haikuchukua muda mrefu kufanikiwa kuwarudisha wanaume wale na kuendeleza libeneke. Na hata aliporudi mkewe Bakari tayali Zuhura alikuwa amekwisha mrejesha Bakari katika himaya yake kama hapo awali. Baada ya tafrani hiyo, Zuhura aliweza siku moja kuwakutanisha Bakari na Franko na kunywa nao vilivyo, siku hiyo ilikwisha kwa Zuhura kwenda kulala nyumbani kwake akiwaacha Bakari na Franko wakiendelea na vinywaji vyao kama sio maadui. Hii iliwashangaza watu wengi sana waliokuwa wanajua alichokuwa akifanya Zuhura. Gumzo la wanaume hao kukutanishwa katika meza moja pasipo kutokea aina yoyote ya ugomvi lilidumu kwa muda mrefu kwa waendaji wa baa hiyo, huku wengi kama mimi kushindwa kuelewa ni kwa namna gani aliweza kuwakutanisha pasipo aina yoyote ya ugomvi. Leo hii Zuhura ameolewa tena na amepata watoto wawili zaidi na bado anakutana na Bakari na Franko katika muda aupendao.

Post a Comment

0 Comments