Header Ads Widget

Responsive Advertisement

HAKIKA ANASTAHILI KUITWA MKE



TOUCHING LOVE STORY.

Jumatano, January 5, 1994, Monduri, Arusha.

Nilihitimu mafunzo yangu ya Jeshi na nikiwa na ari ya kulitumikia taifa langu mama la Tanzania. Nikiwa nasubiri basi kando ya barabara kuu iendayo Arusha, ilipita gari nzuri sana kwa mwendo wa kasi, lakini kufika mbele kidogo ikasimama na kuanza kurudi nyuma na kusimama pale nilipokuwa nimeketi nikisubiri basi. Kioo cha gari kilishushwa na alikuwa ni msichana mrembo katika usukani wa gari lile.

“Vipi brother unaelekea Arusha mjini” aliongea yule mrembo bila hiyana nikamjibu ndio naelekea Arusha. “Basi twende nikupe lifti kwasababu nipo bored sana kusafiri peke yangu” nilipanda garini na safari ikaendelea.

Tuliongea mengi katika gari na nikafahamu vitu vingi kuhusu yeye, kwamba alikuwa ni binti wa mfanyabiashara maarufu wa madini pale jijini Arusha. Sio siri nilivutiwa kwa jinsi alivyokuwa mkarimu kupita maelezo na moyoni mwangu nikaweka bango kuwa huyu anafaa kuwa mke wangu na mama wa watoto wangu. Tulifika Arusha tukaagana na tukapeana anwani za posta na namba ya simu ya mezani za nyumba zetu (kipindi hicho simu za mkononi hazikuwepo).

Ijumaa, 14 januari 1994, Njiro, Arusha.

Binti aliendelea kukaa mawazoni mwangu na nikapanga kukutana nae ili nimweleze yaliyo moyoni mwangu, hakuwa mkaidi nilionana nae na nikamweleza yote ya moyoni mwangu , sio siri moyo wangu ulilripuka kwa furaha baada ya kunikubalia tuwe wachumba.

Hapo ndipo uhusiano wetu wa uchumba ulipoanzia, kusema kweli hali yangu kimaisha ilikuwa duni kulinganisha na maisha ya yule binti lakini wazazi wa yule binti walinikubali nimuoe binti yao kwa kuwa niliwaweka wazi ni jinsi gani nilivyokuwa nikimpenda binti yao, wakanihitaji niwe mvumilivu binti yao asome mpaka atakapomaliza shahada yake ya kwanza (kwa kipindi hicho alikuwa mwaka wa kwanza akisomea udaktari chuo kikuu kishiriki Muhimbili siku hizi MUHAS).

Nimepeleka mbele>>>...Jumatano 13 machi1996

Nikiwa mwanajeshi kamili Jeshi la wananchi, nilipewa waraka uliokuwa ukinihitaji kwenda moja ya nchi zilizopo mashariki ya kati kuungana na jeshi la umoja wa mataifa kutuliza amani (piece keeping) na ningekaa huko mwaka mzima, kipindi hicho mchumba wangu alikuwa mwaka wa tatu bado miaka miwili ahitimu.

Sikufurahia jukumu lile ila kwa kuwa ni la kitaifa ilinibidi niende. Niliagana na mchumba wangu siku hiyo alilia sana kwani alijua ni nini hatima ya vita waweza kuuwa au kuuawa. Nilimuahidi nitakuwa makini na tutakuwa tukiwasiliana mara kwa mara...Nilipanda ndege ya jeshi na wenzangu kumi na tano na safari ikaanza.

Juni 1996.

Wakati nimefika Lebanoni nilikuwa nikiwasiliana nae mara kwa mara kwa barua, ila ghafla mawasiliano yalikatika kwani kila nilipokuwa nikimtumia barua hakuwa akinijibu tena, aliniweka katika wakati mgumu sana na nikahisi tayari ndege wangu kashaota manyoya kapaa
akimbia.

Jumanne, 9 Aprili 1996, Kinondoni, Dar es salaam.

Ajali mbaya sana ilitokea eneo hilo ikihusisha gari kubwa aina ya Lorry liliacha upande wake na kuvaana na gari ndogo, dereva wa gari ndogo aliumia vibaya sana na kupoteza fahamu papo hapo, alikimbizwa hospitali ya taifa Muhimbili na daktari alitoa ripoti kuwa ameharibiwa vibaya misuli yake ya uso hivyo sura yake haitokuwa kama mwanzo tena.

Huyu ndiye alikuwa mchumba wangu alipata ajali wakati akitoka kumtembelea shangazi yake, Alikata tamaa ya mimi kumuoa tena kwa kuwa hakuwa mrembo tena kama zamani ndio maana hakuwa akinijibu barua zangu kwa mwaka mzima,w mama yake ndiye alieniandikia barua kuwa mwanaye amepata ajali na ameharibika vibaya uso hivyo amekata tamaa hataki kuolewa tena.

Jumanne 15, Septemba 1998, Lutheran Church,Arusha.

Sikujali sura yake kuharibiwa nilimpenda kutoka moyoni na ukarimu wake, kujishusha kwake, upendo wake ndio vilinifanya niwe crazy juu yake. Jinsi alivyokuwa akijichanganya na watu usingeweza kudhani kuwa ni mtoto wa tajiri mkubwa. Sura kitu gani? muhimu ni upendo na ningejilaumu kama ningemuacha mama Nicole.

Nilimuoa mpenzi wangu na Mungu ametubariki katika ndoa yetu yenye furaha na amani tele tuna watoto watatu wenye afya na mwaka huu tunatimiza miaka 17 ya ndoa yetu. Amekua nguzo ya familia amekua daraja kubwa katika maisha yetu ya ndoa. She is my mentor! Mipango yangu inafanikiwa kutokana na baraka zake na ushauri wake. SHE IS A WIFE INDEED!

Napenda kuwausia wanaume wenzangu, kama umeaumua kumuoa binti wa watu ni vema ukafanya hivyo kwa moyo mmoja. Usioe kwa vile amekuvutia umbo lake na sura yake eti kisa una wivu wanaume wengine watakupiku. Uoe huku ukijua hujafa hujaumbika. Kumbuka Uzuri wa mwili huisha!

Nanyi wanawake nawasihi na kuwaomba muache kuwa vigeu geu, kuweni na msimamo thabiti katika mahusiano yenu. Msipende material things katika mahusiano bali upendo ndio utawale mahusiano yenu. Nakuhakikishieni mtafika mbali.

Post a Comment

0 Comments