Header Ads Widget

Responsive Advertisement

NIMEPOTEZA DIRA YA MAISHA YANGU



Niliolewa na mwanaume mpole sanaaaaaa miaka mitano iliyopita, yaani nikisema mpole ni mpole kweli, hakunifatilia hata siku moja, hakuniuliza nini wala nini, alinipa uhuru wa kutosha, nikiaga naenda mahali anasema nenda, hata kama narudi saa nane usiku atanifata tu maana hakuwa akipenda niendeshe gari usiku hata siku moja, nikirudi na taxi ananifokea sana,,,, mafuta ya gari niliwekewa kila safari, vocha niliwekewa, alinikuta fresh from collage so hata kazi sikuwa nayo, akanitafutia kazi,baada ya ndoa, nikapata, na nikaanza.
Kuna kipindi akawa ananiambia niache gari ana feel proud kutembea na mimi kwenye gari, kifupi alinijali sana, sana sana,,,,,,,, sasa ile care yake ndio ninayoikumbuka hadi leo hii, wamama, wadada, wanandoa, kama una mwanaume anakujal mshikirie vizuri sana.
Si kwamba alikuwa si mtaalam katika mambo ya kitandani la hasha alikuwa ni mjuzi na mtundu, siku wahi kumfumania hata mara moja, na alikuwa muwazi sana kwangu, ofisini kwao walinijua, alipenda kunitambulisha kila kona,,,, kuna kipindi alienda South Africa kikazi kwa muda mrefu ikawa kila baada ya miezi kadhaa ananitumia nauli naenda, siku zingine anakuja yeye hadi aliporudishwa huku, ni upendo wa ajabu.
Baada ya kuoana siku moja aliamua twende kwetu kijijini akapaona palivyo, akasema atanisaidia kujenga, alivunja nyumba ile iliyokuwepo na kumjengea mama yangu kijumba kidogo cha kumtosha mwenyewe, akamuwekea mashamba, hadi leo namkumbuka. Kwao yeye alikuwa amezaliwa peke yake, mama yake alifariki wakati amemzaa tuu, akasema anamlea mama yangu kama mama yake, hana dada wala kaka wa kuzaliwa tumbo moja, wako wa ndugu wengine tu.
NATHIBITISHA KWA KINYWA CHANGU, COMPANY ULIYONAYO INAWEZA KUBADILI MSIMAMO NA KUSHUSHA AU KUZIDISHA HESHIMA YAKO,,, company niliyokuwa nayo mimi ilikuwa ni ya kupunguza heshima kwangu na ndio iliyoniponza, sitaki kuiongelea sana hilo maana wengi rafiki zangu wako katika mitandao hii hii, ila kifupi tu, nilifanya ujinga mno, naujuita hadi kesho.
Nikiwa na rafiki zangu tuliandaa mtoko kwenda Bagamoyo kutembea lakini tukapanga tusiwaambie waume zetu ukweli, tudanganye maana wengi wasingekubali tukapanga safari tukasema uongo kwamba ni safari za kiofisi,( mume wangu hakuwa akinifatilia ofisini kabisa) basi nikamwambia ni safari ya kikazi tunaenda Bagamoyo, yeye ofisini kwake ni boss fulani, so anaweza kuondoka muda wowote bila swali, basi akasema nitakufata, sitawasumbua nitakaa hotelini tu, wewe ukimaliza kikao chenu utanikuta chumbani, nakumbuka siku hiyo nilichukia sanaaa, yani sanaaaa nilichukia nikamwambia hapana tunalala wawili wawili, akasema basi sawa nenda.
Alinipa hela ya kutosha nikaenda na rafiki zangu tulikuwa group ya watu wanne tu, watatu tumeolewa mmoja bado, basi kufika Bagamoyo tulihv fun sana almost three days, nikiwa kule nikakutana na kijana mmoja ambae alinipenda sana (Naomba kuficha jina,,,, tumpe KELVIN) basi alikuwa amekuja na marafiki zake wengine ambao nao nafikiri nao walikuja ku enjoy maisha,, sasa kila jioni tukiingia buffet tunakutana nae, akaanza kunitongoza nikagoma, akamfata mmoja wa rafiki zangu akaomba namba yangu ya simu akapewa, nilishangaaa usiku akanipigia simu, nikakataaa, rafiki zangu walinisisitiza sana nimkubali, kijana mzuri, handsome, nikasema no, ninae mume wangu, simtaki huyu,,,,, siku tunaondoka akaja na diary moja nzuri sana kwenye gari yetu, akaniuliza “ unaondoka”?? nikasema “ndio, unataka nini??, akasema “don’t be dry like this” akanipa diary yake niichukue kama kumbukumbu, nikakataa.
Nilipofika mjini mume wangu alinifata, akanipokea akaniambia tu mke wangu toka uende huko, nimekuwa mpweke sana,, wakati huo sikujua kama alipiga simu ofisini ku-confirm kama ni kweli niliondoka,,, akaambiwa nimejaza AD na sio kwamba nimesafiri kikazi,,, kumbe ukweli aliujua, nashangaa mwanaume huyu hakuniuliza chochote akakaa kimya tu, ila niliona mabadiliko fulani, kwani tulipokuwa kwenye gari alikuwa ananiangalia sanaaaaaaaa,,, nikimtazama na mimi anageuka anaangalia pembeni.
Nikamuuliza vipi? akasema nilikumiss tu mke wangu,,,, tukafika home nikaoga nilikuwa nimechoka. Usiku Mume wangu akataka tufanye tendo la ndoa, nilikuwa nimechoka nikamwambia nimechoka, hakujibu wala kusema chochote akasema pole mama, akageuka akalala nami nikalala. Asubuhi mapema akaniambia tena “naomba mke wangu nilikumiss sana” nikamwambia “nachelewa kazini, nitampa jioni” akasema “sawa”, tukaondoka, kila mtu na gari yake, kufika ofisini HR hakuniambia chochote kama aliwasiliana na mme wangu aliniuliza tu, umepona? Nikasema ndio akasema karibu tena, basi kazi ikaendelea,,,,,, baada ya siku nne tu akaja yule kaka ofisini kwangu na alielekezwa na mmoja wa hao best zangu, alipofika nilishangaa nikamuuliza “nini kimekuleta hapa?” akasema “tuongee kwenye gari” basi nikaingia, jamani ni kama nililogwa naweza sema kweli tena, kama hamtaamin basi ila naamini ALINIROGA HUYU KAKA, maana alipokua akiongea nikaanza kumpenda,,, nilizidi kumpenda kupita kiasi nikaanza kuona uzuri wake, nikaanza kumcompare na Franco wangu, naona huyu amemzidi kila kitu.
Akasema tuagane ndani ya gari yake ilikuwa full tinted akanivuta tuka kiss ile yenyewe, aisee nilikuwa kama nimepigwa short, nilitetemeka moyo ukaenda mbio sana akapitisha mikono yake kwenye mapaja yangu ...isingekuwa maendeo ya kazi dadhani tungefanya mapenzi ndani ya gari yake siku ile ile, nae alikuwa ameshapoteza Network tokea pale nikaanza kumpenda kupita maelezo.
KUMBUKENI CHA KWANZA FRANCO KUGUNDUA KUWA SIO MWAMINIFU ILIKUWA NI KUSEMA NAENDA BAGAMOYO KIKAZI, WAKATI OFIS HAIJUI NA NILIAGA NAUMWA,, SO HII ILIKUWA YA KWANZA ALIGUNDUA NA HAKUSEMA KITU
Niliporud Nyumbani mume wangu akasema anaomba tutumie gari moja tu, moja tupaki, atakuwa ananipeleka kisha ananirudisha, nilifunguka sana siku hiyo nikamwambia sitaki, nini maana ya kuwa na magari mawili kwanini alininunulia la nini wakati alijua anaweza kunipitia, akasema nimeamua tu, mke wangu nini shida kwani, wewe nakupeleka nakurudisha kama una issue zako nitakupeleka nakuacha ufanye mimi naondoka badae nakufata nikakataa akasema sawa.
Usiku wake tulifanya mapenzi na kusema kweli tulifanya hasa. Ila yeye mimi ndo alikuwa yuko serious mimi nilikuwa namuwaza kelvin tu,. Wakati tunaendelea niliona kabisa hayuko kawaida, anafanya tu ili mradi tu atimize haja zake,, nikamuuliza kuna shida gani akasema hakuna shida yoyote. Alimaliza haja zake kujihudumia , kisha akatoka hakusubiri nimsafishe huyo akainuka kwenda kuoga. Kuna vitu alikuwa ananifanyia mwanzoni mwa ndoa yetu nikaona hafanyi tena kazi yake ilikuwa ni kutimiza haja zake.
Wakati huo nikawa nimeshaanza mahusiano na kelvin,,,,,,, mahusiano yangu mabest zangu waliyajua vizuri sana, siku ya bith day yangu nilipotoka nikamkuta Kelvin ananisubiri nje akanichukuwa kunipeleka hotel moja hivi iko sinza, nzuri sana nikakaa kama nusu saa wakaja mabest zanu na keki,,,, nilibaki nashagaa, nikiwa hapo mume wangu alinipigia simu kuuliza niko wapi,, nikakimbilia chooni kupokea simu, akauliza uko wapi mama? nikasema Muhimbili nimekuja kumuona mama yake rafiki yangu anaumwa, akasema mbona sauti ina mwangwi? na kumetulia hivyo, nikasema niko chooni najisaidia, akasema mbona hukuaga? nikasema sorry, ilikuwa urgently,… alichosema ni kimoja tu,,, KUWA MAKINI NA MAAMUZI UNAYOTAKA KUYAFANYA, akakata simu.
Nilikaa hapo bila hofu kabisa mbaya Zaidi nikisema nawahi nyumbani kwa Mr, wananiuliza unamnyonyesha? Kaa ule raha hapa,,,, nilikaa kweli hadi saaa mbili, nikiwa hoi, akawa ameanza kunipa pombe ninywe, nilishindwa kwakweli nikaanza kunywa wine tu ambazo nazo sikuwa nikitumia zamani, siku ya birthday Kelvin alinikazania sana anipe zawad ya sex, kweli pale baada ya kuondoka wenzangu tulichukuwa chumba tukafanya Sex haraka haraka, cha ajabu nilikuwa naenjoy sana penzi lake kuliko la Franco,, kisha tukarudi home,,, nafika home tu namkuta mume wangu kaka kibarazan ila kaka wa getin wakati anafungua aliniambia tu dada leo shemej ana hasira hasira sana sijui kwanini, (kijana wa getini ni ndugu yangu so yuko huru kwangu sana ) nikamuuliza kakuulizaje? akasema alisema tu ikifika saa nne hujaja nisifungue geti atakuja kukufungulia yeye.
Tumejenga nyumba ya ghorofa basi ile naingia naongea na mlinzi kumbe yuko ghorofani ananiangalia atu mie sikumuona maaan niusiku na amekaa kwenye kona, badae ndio kaka akaniambia umeona anavyokuangalia yule kule juu, ndio nikamuona, alipoona nimemuona tu akarudi ndani,,,,,, naingia sebuleni tu nae anashuka ngazi, akanifanta akanikumbatia akasema nikupokeee hand bag,,,,, kisha twende dinning kuna gift yako,,,, tukaenda hadi dinning, nikakuta kuna keki, akamuita dada aandae sahani alete cha champagne, basi nikajikausha kama sio mie nikafurahi ili awe na Amani, nikashangaa mbona hasira nilizoambiwa anazo sizioni tena,,,, basi tukakata keki tukala, akaniiimbia wote na kina dada na kaka wa mlangoni kisha wakasambaa, tukapanda juu kulala, ile nafika juu tu akaniambia nina gift yako ingine,,,,,, njoo tukae hapa tuongee kidog nikupatie zawadi,,, tukae sebule ya juu, ambayo inatazamana na chumba chetu,,,,, nikamwambia nisubiri basi nakuja,
Basi niliiingia ndani nikachukua simu nikamu sms Kelvin asinipigie maana nimefika nyumbani, hakujibu chochote kile, basi nilitoka nje nikaakaa seblen na tauro langu, mume wangu akasema mbona hukuniaga ulipoenda na sio kawaida yako??? Akasema mbona hukuniambia wakati huwa unaaga, nikamwambia mgonjwa alizidiwa nikachanganyikiwa akasmea,,, KUWA MAKINI NA HAYO UNAYOTAKA KUYAFANYA, akanifata akaniambia nakupenda sana,,, jitahidi uniheshimu, usiniumize,,,nikasema sawa, akaniambia, chukuwa zawadi yako pale kwenye kikabati cha vitabu,,,, nikaenda nikakuta simu nzuriiii ya HTC ONE rangi ya gold, Niliruka sanaaaa sana nikamkumbatia, akafurahi akaniambia basi tufanye mapenzi pale seblen sikujivunga nafuraha ya simu tukafanya,,,,ila kuna kitu alihisi, maana alipoanza tu akaniangalia usoni, hapo hapo akawa mpole, , akanitazma usoni akaniuliza unaenjoy nikasem yes, you? Akasema me too ila nashangaa kwanini nimeishiwa nguvu ghafla.
Nilistuka nikamuuliza unawaza nini akasema nothing, nashangaa tu, Saa nane usiku naamka niende washroom Mr hayupo kitandani, nikastuka, nikaenda washrum hayupo, nikatoka sebule ya juu hayupo, nikaja kumchungulia namuona sebuleni ya chini amekaa anaangalia movie, amevaa tauro tu,,,, nikashuka hadi chini, nikamuuliza unashida gani usiku huu watu wamelala wewe unaangali tv, akasema niache sina usingizi, kucheki pembeni yuko na simu yangu,,, moyo ukafanya paaaaaaaaaaaaaaa.
Nikamwambia mbona umekaa na simu yangu, akasema SINA MIPAKA JUU YA SIMU YAKO MKE WANGU,,,,, nikataka kuichukuwa kwa nguvu akasema usipende kutumia nguvu, sana utaumia,,, chukuwa simu hii hapa nenda kalale, nikakuta anakunywa wine ,, alikuwa anaangalia CD moja ambayo nilitamani kila mtu angekuwa nayo inaitwa FIND A SECRET,,, nzuri sana sana sana,,,,,,,,,nikamwambia okay uliichukuwa yanini, akasema kama nataka lipiza basi nienda na yakwake.
Sikumjibu nikarudi ndani, nikaanza kupekua sms, sikukuta sms hata moja, nikajipa moyo sikujua kumbe kelvin alikuwa alirudisha majibu na alinisifia Sanaa tuliposex, mume wangu akajifowadia sms ile maana siku ananiacha kanisani aliionyesha na akasema anazo sms zote maana alienda (mtandao kapuni by admin) AKAPRINTIWA SMS NA RAFIKI YAKE, ambazo tulikuwa tunatumiana, basi nilipojiridhisha tu nikalala usingizi hauji nikasema au katuona?
Nilipitiwa na usingizi nikalala, hali ilianza kubadirika hapo, simuelewi kabisa mwenzangu, anauchuna tu, haniulizi chochote ni kama ndani ya miezi sita niko na kelvin mambo moto moto,, kuna siku akanaimbia mke wangu nataka kukutoa
nikamwambia wapi? Akasema nahitaji kuongea na wewe omba ruhusa kazini WAAMBIE UNAUMWA TENA,,,, nahitaji kwenda na wewe Zanzibar,,, mh nikastuka hiyo tena imetoka wapi? Nikamuuliza niwaambie tena kwani nishawahi kuomba ruhusa ya kuumwa, akasema ah nilikosea kuongea tu, don’t mind, we omba ruhusa, niliomba tukaenda hadi Zanzibar, tukafikia hotelini, lakini safari ile ilikuwa ni kuongea tu,,,,,,, alinisihi nitulie, kama kuna shida niseme, kama kuna tatizo tuongeee ananipenda sana,, yani aliongea kupita kiasi, nikasema sema kwani kuna nini, najikausha akasema ah moyo tu hauna Amani, tukaenjoy kidogo akaninunulia madraya ya mkono ya kutumia mwenyewe nisiende salon, yani kila kitu hao tukarudi dar, kufika tu ugomvi ukaanza na kelvin kwa simu, anasema kwanini niliondoka bila kumwambia, nikamwambia nilikuwa na mume wangu, na ilikuwa ghafla, na nilikuwa so tight nisingeweza kabisa kuongea na simu, akachukia akaanzak utuma sms za ajabu ajabu tukiwa tumekaa seblen niko busy na simu, yangu, sina hili wala lile, Franco akasema wife,,,, SIKU NIKIGUNDUA UNANIDANGANYA, NITAKACHOKUFANYA HUTOSAHAU MAISHANI KWAKO,,,, nikamwambia kwani nini, basi nikazuga hapo kimoyo moyo nikasema ntakuwa makini Zaidi.
Tulikaa kama miezi miwili Amani ikiwepo kabisa nyumbani kwangu, japo sio sana, tukawa tumepanga twende kwa mama yangu, tukamsalimie yuko Kigoma, tukaenda na mume wangu hadi kigoma nashangaa nimefika kigoma Kelvin ananipigia simu nae yuko Kigoma eti alinifata nikasema siwezi kukuona akasema no, lazima tuonane, basi nikadanganya kuwa naenda kwa dada yangu mkubwa, Mr. aniruhusu niende tu, akasemea mie nimekuja kwenu,,,, wewe ndio mwenyeji wangu, unaniacha na huyu mama naongea nae nini? Kuna mipaka mimi kwenda kwa ndugu zako hadi uende peke yako? Nikasema hakuna, nilichokaa maana nilikuwa nimemuelekeza kelvin aje maeneo hayo, namimi huku Mr. akanibana twende wote ikabidi nimwambie kelvin asije.
Sijui hadi leo, mme wangu aliisomaje ile sms maana nilikuwa nikituma tu naifuta, wakati tunarudi dar akaniuliza vipi, mbona ulimzuia mwenzio, kuja kwa dada yako, nikasema nani? Akasema ah,,ACHANA NAYO HAYO, NIKASEMA NO, NIAMBIE UNAMAANISHA NINI? AKASEMA yaache tuendelee na mengine,,,, akaanza kuongea mengine, nilistuka kidoog ila mwenzangu akawa sawa tu, tulipofika dar, ugomvi ukaanza na Kelvin kwanini nilimzimia simu, ugomvi mkubwa sana,,, nikaaendelea kuchelewa nyumbani.
Kuna siku nilipigiwa simu na mama akanaimbai Suzy una nini nyumani kwako? Maana mumeo kaniambia niongee na wewe, nikamuuliza kuhusu nini kasema wewe UNAJUA NIONGEE NA WEWE, nikamwambia mama hakuna kitu acha nitayamaliza kama yapo,,,, usiku nikamuuliza mme wangu uliongea na mama akasema Yes nilikuwa namsalimia tu namjulia hali nilikosea? Akasema no hukukosea KABISA UKO SAWA.
KUNA SIKU INGINE TENA NILIKUWA NIMELALA.......MIDA KAMA YA SAA NANE HIVI USIKU NIKASTUKA NINI. SIJUI NIKAKUTA MWENZANGU HAYUPI KITANDANI..
NIKASTUKA NIKAINUKA KWETU MADIRISHA YAKE NI MAKUBWA SANA NA HUWA SITUMII.AC MAANA UPEPO WAKE MKUBWA SANAAA BASI HUWA NAKUNJA PAZIA TU KWAHIYO.MWANGA HUPENYA NDANI NIKAONA KWENYE KONA KABISA MUME WANGU AMEKAA JUU YASOFA KAINAMISHA KICHWA CHINI. NILIINUKA NIKAWASHA TAA NIKAMFUATA NIKAMUULIZA ANA NINI.MBONA SIMUELEWI....KABLA HAJAJIB.MACHOZ YAKAANGUKA NIKASTUKA NIKASEMA FRANCO....ARE YOU CRYING????KUCHEKI KOCHI LIMELOWA KWA MACHOZI NA MAFUA ANALIA BILA KUTOA SAUTI.....NIKAMUINUA KICHWA NIKAONA MACHO YAMEMVIMBA NI KAMA MTU.ALIEQNZA KULIA ZAMANI SANA.
NIKAMSOGELEA NIKAMUULIZA UNA NINI BABA??? PLEASE TELL HAKUJIBU KITU CHOCHOTE AKANISUKUMA AKASHUKA NGAZI KWENDA CHINI..NIKAWA NAMFATA AKANIGEUKIA AKANIONYESHA KIDOLE TU.....ISHARA NISIMFATE.......NIKABAKI NIMESIMAMA.
HAKUNIJIBU AKATAKA KUNISUKUMA NIKAMWAMBIA NO....KAMA KUNA KITU TUONGEEE PLEASE KULIA SIO SOLUTION..AKASEMA HIV...NIJIBU MASWALI NITAKAYOKUULIZA...NIKASEMA SAWA AKAANZA...KWANINI UNATEMBEA NJE YA NDOA?,,BASI NIKARUDI JUU NIKAKAA USINGIZI UKAKATA KABISA......NIKASEMA NO....NAMFATA NIKATOKA NIKAENDA SEBULENI CHINI NIKAKUTA HAYUPO ILA MLANGO UKO WAZI..NIKASHUKA HARAKA NIKATOKA NJE NIKAMKUTA AMEKAA ANALIA HUKU AMENG'ATA KIDOLE...NIKAMFATA NIKAMKUMBATIA..NIKAMWAMBIA NAKUPENDA
MOYO ULIFANYA PAAAAAA NIKAJIKAUSHA NIKASEMA NINI WEWE? AKASEMA SIRUDII SWALI HATA MOJA MAANI UMESIKIA.......LA PILI.. NIPE SABABU ZA KUFANYA HIVYO...NA TATU NIFANYE NINI UMUACHE KELVIN..WAKAT HUO ANAONGEA ALIKUWA NA HASIRA SANA....MACHO MEKUNDU SANAAA MISHIPA KICHWANI IMESIMAMA ANANG'ATA MENO..ANAJIPIGA KICHWANI.......AKASEMA NIPE MAJIBU YA MASWA YANGU HUKU ANANITAZAMA USONI.
NIKASEMA HAYO NI MAWAZO YAKO..SINA MTU MIMI.......KWA MARA YA KWANZA TOKA NIOLEWE ALINIZABUA KIBAO KIMOJA KIKALI..AKASEMA KWANINI UNATEMBEA NJE YA NDOA..KWANINI HURIDHIKI..WHAT IS SO SPECIAL KWAHUYO JAMAA YAKO..AKANIZABU KINGINE..NIKAKIMBILIA NDANI NIKAPANDA NGAZI HARAKA MAANA ALIKUWA ANANIKIMBIZA.
Nilipofika ndani nikapanda ngazi haraka haraka akanifata mie napanda moja moja yeye mbili mbili kabla sijafika hata mlangon akanivuta akanishusha chini akasema leo nakuuwa........siwezi penda mwanamke nikampa kila kitu anachotaka kisha anisaliti alinipiga sana pale chini..salama yangu ni kijana wa getini kuja kuniokoa maana nilipiga kelele kama nimekalia moto.......hakuongea aliponipiga nikaokolewa akaenda kwenye wine space akakaa huko akaanza kunywa wine...huku analia sana.....nikaingia chumbani nikaanza kulia asubuhi kufika nikamkuta kalala palepale juu ya meza ya wine sikumsemesha kitu nilivaa nikaondoka kwenda kazini....sijui aliamka sangapi..ila mida ya mchana akanipigia simu sikupokea..akapiga nikakata akatuma sms pokea simu mke wangu siku pokea.
Niliporudi jion kaka wa getin akasema shem nae kaondoka sasa hivi toka asubuhi alikuwa analia tu. Kaja rafiki yake wameondoka ....sikujibu kitu nikafika......kidogo ikaingia sms kwamba nimfate samaki samaki kule mliman city nikasema siji....sijakaa sawa akamtuma mtu anifate nikaenda kufika akaniomba radhi sana mbele ya rafiki Zake kwa kunipiga...yeye mwenyewr anajutia kwanini alinipiga aliomba radhi sanaaaaaa nilimshangaaa kukuta anakunywa pombe wakati alikuwa hanywi nikamuuliza Franco..when did you started this....yesterday.......and its because of you...basi aliomba radhi na wenzie wakanisihi nimsamehe tukarud home.....that day tulifanya sana mapenzi na mke wangu...lakini bado niseme kweli Kelvin aliniroga jaman..wakati tuko kwenye raha na mume wangu nikawa nakumbuka mapigo ya Kelvin......hadi alipotimiza haja zake.
Za mwizi zilifika ambazo had leo sijui aliijuaje hotel niliyokuwa nimeenda kulala na Kelvin....nawaza had leo nakaribia miaka miwili toka nimeachika sijui alijuaje Franco. Ilikuwa jumamos Kelvin akaniambia kuwa ameninunulia kiwanja Mkuranga niende akanikabidhi....hakusema kama nitalala huko sikujipanga kuaga chochote ..nikamwambia Franco naenda kwenye chama kikaoni huko mbagala akasema sawa nenda.....nikaondoka kufika huko tukakaa baa moja hiv tukala..akaenda kunionyeaha hicho kiwanja nikakitazama tulipomaliza kukiona akasema twende kwenye kituo chake kimoja cha mafuta mbele ya Mkuranga. Wakati huo ilikuwa saa 12 jioni......nikamwambia si unajua natakiwa kurudi home akasema yes hatukai sana....tulipaki gar yangu nyumbani kwake kawe tukaondoka na gari yake. I was confortable coz ilikuwa full tinted ukisema uchungulie ndan unajiona sura yako unavyochungulia ndan huon kitu
Kufika huko tukatembelea kituo chake nikapaona....Kelvin. alikuwa hajaoa kabisa so nilikuwa free kwake..akaniintroduce kwa wafanyakazi wake kama mkewe mtarajiwa..bad enough nilikuwa nikikutana na kelvin tu ananiambia toa mapete pete yako..na kuna siku alitaka kuzitupa alisema hazipendi ikawa ugomvi basi nikawa nazivua....baada ya hapo akaniambia anafeel joto nimsindikize kuoga hotel moja hivi na akasema tufanye mapenzi hawezi niacha nami kuonesha ushirikiano wa kiwanja kile nikaenda ila kwa makubaliano tukimaliza tunarudi nyumbani ..siku nzima sikuwa nimeongea na wale mabest zangu hata mmoja... tukaenda hotelin hukohuko Mkuranga
Tukiwa hotelini pale akaniambia leo huondoki..simu hii hapa mpigie mumeo sema unavyosema leo tunalala wote.nikalia sanaaaa akanipokonya funguo za mlangon..akasema siku nikisikia mume wako kafa ntafurah sana..hana hadhi ya kumiliki mtoto mzuri kama wewe.......nililia haniruhusu akagoma.....basi mida ya saa mbili simu ikaita kucheki ni mme wangu.......nikafungua madirisha ili mwangwi utoke nikapokea nikamwambia nimepitia msibani kuna rafiki yangu kafiwa ........akachekaaaaa akasema okay kwahiyo hurudi?nikasema naweza kuchelewa sana..akasema haya mke wangu. Nakupenda nikamwambia nakupenda pia. Akakata simu.. hapo nilikuwa na hofu sanaaaa.
Nikiwa hapo tulikuwa tumeagiza kuku wa kuchoma nje. Nikasema hatuendi kula nje walete chumbani..basi nilikaa ndani kama saaa moja baada ya kuongea na Franco akapiga tena akasema nipo hapa ulipo naomba nikuone Mara moja... Nikaastuka akasema tena unakuja au Mimi niie?.....sauti ile ilikuwa kama MTU Amalia.......pembeni nasikia MTU anamwambia Franco utaharibu sasa....nikakata simu.
Nikamuuliza klevin Franco anasema yupo hapa nilipo kuna MTU yeyote ulimwambia tutakuwa hapa Leo? Kelvi. Akasema bwege Huyo muongo anakutishia tu..mie sikumwambia MTU ila niliongea na na Rachel asubuhi nikamwambia Leo nakuja kukupa KIWANJA ila sikusema nitakuja hapa.
Simu ikaita tena nikapokea akasema Mke WANGU. Nipo nje....unakuja au nije? Ila sauti yake kama anabana kilio....nikakata simu bila kujibu... Jamani sitasahau Siku hiiiii huwa nalia sanaaaaa hapa pia nalia nimekumbuka mbali Ghafla simu ya chumbani kwetu ikaita.....wote tukaogopa kupokea.........kidogo mlango wa chumban ukagongwa.
Mlango ulipogongwa kelvin akauliza nani? Wakati huo Mimi Niko hoi jasho linanitoka..mwili unaishiwa nguvu..nikaombaaaaaa nikasema Mungu wa uzima nitetee kwenye hili naahidi nikitoka salama sitakutenda dhambi tena..nikasahau kama MUngu hasikii maombi ya mwenye dhambi.
Kama mnakumbuka nilikuwa kwenye purukushan za kutaka kumkimbia kelvin tulipofika..moyo haukuwa na amani kabisa Siku hiyo kelvin aliuchukua ufunguo ili nisitoroke akawa nao mlangon kukabaki hakuna kitu chochote cha kuzuia ufunguo mwingine kupita....tukasikia sauti ya muhudumu ikisema Mimi muhudumu fungua mlango Kelvin akamfokea....kwann unasumbua wateja?.... hii sheria ya wapi hii ya kumuarisha mteja afungue mlango?...hakujibiwa...nikasikia nyayo zikitembea kama zinaondoka vile moyo ukarelux.
Baada ya dk tano tu nikasikia mlango unafunguliwa ndio nikaju kumbe na hotel huwa wana funguo spair....oh pssaaa naumia zaidi mazingira niloyokutwa Nayo I'm crying kila ninapokumbuka haya mwenzenu roho inaniuma sana mimi Nikiwa uchi kabisa nimekaa kwenye kona ya kitanda nimeshikiria MTO..kelvin akiwa uchi kabisa ameganda kona ya kitanda hajui afanye ninii akashika simu anaacha anainuka anakaaa anaangalia pa kukimbilia....mwisho akasema niingie uvungu wa kitanda.....room tuliyochukua INA vitanda vya box vile vikubwa sana havina uvungu akatoa godoro ili niingie kupitia chaga za kitanda..ndipo mlango ulipofunguliwa nikiwa nimesimama natafuta pa kuitetea ndoa yangu
Alianza kuingia shemeji yangu ambae in askari ila alivaa kiraia badae akafata Mume WANGU mpenzi Franco.....ambae alipofika mlangon aliganda tu.... Alishikilia mlango tu akinitazama Mimi na kelvin..huku machozi yanamtoka..kamasi zinamwagika.....akaniangalia...shemeji akanitazama akasema hapa ndio msibani? Kabla sijajibu kitu Shem alinipiga kibao kimoja kupitia Kitako cha bastola yake nikakwepa kikanichana mgongon juu ya bega. Nikakimbilia kwenye godoro Juuu kwenye kona ya kitanda nikakaaa Shem akamvamia kelvin akaaanza kumpiga vichwa. Manager wa hotel akafanya kazi za kuzuia huku akiniambia mama vaaa taulo.......wakati huo Franco amesimama tu mlangoni anatetemeka hadi unaona kabiaa anatetemeka...jasho linamtoka..badae akavua sandals alizokuwa amevaaa akasimama pale pale..muda wote huo ananitazama Mimi tu.
Yule muhudum na meneja walifanikiwa kumtuliza shemeji yangu...Shem akanifata akaniita KWA jina langu Mimi ............(hide the name) akaniuliza umefanya nini? Mbona familia yetu ilikuamini na kukupenda sana.....imekuwaje umefanya hivi?....kilikupata ninii shemej yangu. Shem nae anaongea kwa kuliaa kabisa..akasema unataka ummalize Franco ukoo wake ufe?maaana kabaki peke yake..hana dada wala kaka (shem ni Mtoto wa babake mkubwa Franco)
Ghafla nilianza kuishiwa nguvu....kuanzia miguuuni ganzi ikaaanza kupanda kuja mapajani badae kwenye vidole na mikono mwisho nikasikia kizunguzungu nikakosa nguvu nikalegea kabisa na kuangukia kitandani style ya ubavu KWA kulala..nasikia ...naona. Lakini sijui nilipatwa na kitu gani sikuweza kunyanyua mdomo..sikuweza kutikisa hata kidole kimoja mapigo ya moyo yalibadirika nalia machozi hayatoki kabisa yamekata ila jasho linanimwagika kama maji.
Namuona kelvin anavaaa nguo lakini damu zinavuja puani sana badae muhudumu namuona anavyonifunika tauro shemej anaongea Kilugha na Franco kumsihi asiwe vile alivyo nikasikia akimwambia tamka chochote moyo upumue..usiwe hivyo utakufa? Ongea chochote maana toka ameniona pale alisimama mlangon hakutamka neno lolote lile ni machozi na kamasi vinamtoka Mimi niipo naona lakini siwez Fanya lolote.........sina nguvu na ulimi kama umekatwa...sikuwahi kupata mstuko wa aina hii toka nimezaliwa..ingekuwa sio fahamu kuwepo naona ningekuwa nimekufa
Nakumbuka Franco alisogea mbele akanitazama KWA upole akaniambia sikustahili haya mke WANGU........sina nilipokosea mke WANGU kustahili adhabu hii......naaapia kama niliwah kutembea nje ya ndoa toka nimekuoa Basi nife kifo cha mateso.............kwanini uliamua kufanya hivi......nini kilikusibu mke WANGU.......akalia sanaaaaaaa kisha akasema UTANIKUMBUKA........Akakainuka akatoka shemeji akanitazama akasema weweeee....bahati yako.......haya endeleeni wakatoka wakatufungia mlango
Alipoondoka kelvin alinitazama alikua amechanika mdomo na jicho moja lilikuwa jekundu sanaaaaaaa akaniambia pole......sikuweza kujibu alivaaa yeye akanivalisha nikiwa kitandani badae akampigia simu rafiki yangu mmoja aje yeye pia aliogopa KWA hali niliyokuwa Nayo' maaana mie sijui nini kilinisibu ni kama nimepooza.
Badae walikuja watu wawili wakaanza kuninyoosha KWA kunipia piga misuli KWA mbaliii nikahisi ufahamu ila koo lilikuwa linauma na ulimi bado haukua ukinyanyuka vizuri......wakanibeba hadi kwenye gari KWA kujikongoja nguvu zimeisha kabisaaaa tukaenda hadi kwa rafiki yangu ilala.....nguvu zikaaanza kuja taratibu sana nikaweza kuongea macho yakaaanza kutoka sasa nalia kama nimefiwa nawaza narudije kwa Franco niliumia sana.
Badae Kelvin alituacha kwenda hospitali akatibiwe majeraha badae alipiga simu nipelekwe wakanicheki na Mimi nikapelekwa wakanishona nyuzi NNE tukarudi nyumbani KWA rachel wakawa wananifariji.....Ilipita Siku mbili nikamfata aunt yangu anipeleke kwangu Nilimueleza kila kitu.......alinisema sanaaaaaa nimewatia aibu...ila tukasema nisimwambie mama kwanza tukaenda wawili kufika tukaingia tukamkuta amelala anaangalia movie sebleni akatupokea vizuri tu .........akamkaribisha aunt akampa juice na mimi akanimiminia akanikaribisha ..nilipata faraja sana badae akasema anataka kutoka so tuseme tulichofata...aunt akajieleza sanaaaaaaaa lakini Franco alianza kulia akasema shangazi niko tofauti na baadhi ya wanaume..Mimi ni mpumbavu kuliko woote ndio maana binti yako ameweza kunichezea hivi...mama yangu alikufa nilipozaliwa .nimekosa upendo wa mama nikaweka upendo WANGU wote KWA mke WANGU......nilimpa kila anachotaka mke WANGU...alibadirikia ghafla .. Muongo..msiri.. Sijui alikosa nini..akashindwa kulinda upendo WANGU....
Alieleza mengiiii jinsi Alivyokuwa akinifatilia anasema pale alielekezwa KWA njia ya simu. Alisaidiwa na best friend wake Yuki mtandao wa.................... .(jina kapuni)......pia yule Shemeji YANGU alisaidia kujua niko wapi kwa system yao wanayotumia huko kazini kwao ndio MANA walifika anasema yeye aligundua siku nyingi nachepuka na hakutaka kuambiwa alikuwa akinionya tu labda nitaacha mwisho akasema hataniacha hadi athibitishe so Hatanisamehe kamwe.
Alieleza sana jinsi inavyotumika kunikamata na imlicost sanaaaaa. Basi alisema nikiendelea kumuona hapa nitazidi kuumia nitamfanya kitu kibaya hatasau mtanipa kesi.. Shangaz kama mmemchoka Mtoto wenu mwacheni hapa ila kama mnampenda naomba nendeni nae. Alikataaa kabisa nikamfata kwa magoti akagoma akasema ana hasira niondoke zikiisha ataniita..tukaondoka na aunt........kesho yake nikapigiwa simu na mchungaji kanisani tulikokuwa tunaabudu niende ofisini kwake.....nilienda nikiwa mpole nimevimba macho KWA kuliaa nikammkuta Franco nae yupo huko na yule shem WANGU askari aliekuja nae Mkuranga.
Akaeleza KWA Mchungaj kisha akasema nilimchukulia hapa...mkatubarikia hapa....namuachia hapa...tukitoka hapa atafute pa kwenda.... Kama kutakuwepo na anachodai aende mahakamani nitakutana nae huko na nitamlipa anavyodai.... Nguo zake nimeshusha KWA mama aggy ( ni mama anaefanyaga USAFI kanisani na ofisini KWA pasta).akaniachia funguo za gar yake...badae akasema na gari nakuachia vingine atafanya kelvin..kama tulisaidiana nae vingine basi na huduma achangie..na mwambie akutafutie pa kuishi..akujengee.......ukija nyumban utatoka maiti.
Pasta alimsihi sanaaa Franco aliondoka bila kujibu chochote....pasta akasema hana jinsi ila atazidi kuongea nae lakini pia kwa sheria za kanisan kwetu lazima nitengwe nipewe adhabu KWA dhambi ya uzinzi.
Nilirudi kwa shangazi akasema tumpigie mama simu tumueleze mama alilia sanaaaaaaaaaaaa Alinisema sana akampigia Franco aongee nae Franco alikataa aa akamwambia mama too late and am. Sorry sihitaj maongez juu yake. Mama alikuja toka kwake tukaenda KWA Franco......tukaambiwa kachukua Likizo kaenda kupumzika South Africa.. Na hiyo safari ilikuwa twende wote na yeye alikuwa ameniambia nifanye research tufikie hotel gani nzuri..ameenda peke yake..nikaaanza kulia
Ulipita mwaka ..mzima nikiwa Kwa kelvin baaada ya Franco kunikataaa.... Mungu akaniadhibu tena kelvin alienda kuoa UK na alioa kwa siri....nilijua baada ya ndoa yake.......nilikuwa kama kichaaaa. Nilisikia kuna mdogo wake Franko amefariki ......nikaenda msibani na rafiki zangu nikaoneshwa msichana anaeishi na Franco kwa sasa... Franco kanisani kahama sijui anasali wapi kifupi haeleweki maaana nilijua nitamuona kanisan tu...mbaya zaidi binti Huyo nilikuwa namjua alikuwa jirani yetu na alikujaga kumsaidia aunt yake vikazi vya ndani baada ya kutoka kijijini nikasema poor Franco......ameenda kukachukua kasichana kadogo kias hiki?? Aliponiona msibani alistuka ila hakunisemesha lolote ndugu baadhi walinipokea wengine walinichunia.
Najipa moyo iko Siku nitarudi kwa Franco WANGU tu!HIVI NDIVYO NILIVYOACHWA NA FRANCO....WAAMBIE WASHEE ILA MAENEO MUHIMU YAFICHE KABISA KWA USALAMA WANGU..ITAWASAIDIA..KAMA MME WAKO ANAKUPENDA ...MUHESHIMU MIE HAPA NIMEPOTEZA DIRA YA MAISHA YANGU.. FAMILIA NZIMA IMENIDHARAU MAMA KILA AKINIONA ANANISEMA....KIWANJA CHA KELVIN KIPO TU..NIMEPANGA NYUMBA YANGU NAISHI. NAKULA....LAKIN BADO SIJAKIDHI HAJA YA MOYO WANGU NAJIULIZA IKO SIKU FRANCO ATARUDI KWANGU?????? MUNGU ANAJUA

Post a Comment

0 Comments