Header Ads Widget

Responsive Advertisement

UCHAWI WA UKWENI



Kwenye maisha kuna mambo mengi sana ambayo yanatokea,mambo hayo yanaweza kuwa ni mabaya au mazuri,lakini kama ni mabaya mengi yanatokea pale tu ambapo tunazembea mambo fulani
Kilichompata huyu anasema hatakisahau maishani mwake,anasema ni kutokana na uzembe wa kudharau alichaombiwa na mama yake,hebu jikaze usome kisa chake ......
Nimetokea kwenye familia maarufu sana hapa nchini,lakini nimekulia kwenye maisha ya tabu sana kutokana na msimamo wa aliyeisababisha familia yetu kuwa maaruku wa kutotaka kuifanya familia hii kuwa matajiri kwa njia za kifisadi
Kwasababu hiyo mama yangu alitoka kwenye moa ambao alizaliwa na kuja Mwanza ambako ndiko alikutana na baba yangu,kwa baba yangu nilifanikiwa kuzaliwa mimi tu na baada ya hapo mama yangu alirudi kwao na kuniacha kwa baba yangu ambako niliishi nae hadi nilipofikisha umri wa miaka 15 ndipo mama alikuja kunichukua na kunipeleka kwao,alikozaliwa yaa ni kwenye ukoo wao
Niliishi kule na maisha yalikuwa mazuri kwani tulikuwa tunapata mahitaji mengi kutoka kwenye familia ya babu yangu ambae alikuwa anajiweza sana kiuchumi,masha yaliendelea nilipelekwa shule kwaajili ya masomo ya sekondari lakini nilishindwa kuendelea baaya ya mama kuolewa na bwana mwingine na kuhama pale ambapo tulipokuwa tunaishi
Baba aliyemuoa mama alikuwa tayari ameshazaa na mama watoto wawili wakati mimi niko kwa baba hivyo kuifanya familia yetu kuwa ya watoto watatu na baada ya baba huyu kuamua kuishi na mama ndipo tulihama kutoka pale ambapo tulikuwa tunaishi

Tulipohamia maisha yaliendelea lakini hayakuwa mazuri sana na ndipo niliamua kujiingiza katika kutafuta pesa kwa kuanza kufanya biashara ndogondogo,nilifanya biashara kule tulipokuwa tunaishi na baadae niliamua kuhamia Jijini Mwanza na niliendelea na biashara zangu
Baadae nilipata taarifa kuwa dada yangu aliyenifuata amepata mchumba na ataolewa siku sio nyingi,niliambiwa kuwa mchumba ambae dada alimpata alikuwa ni wa kutokea wilaya ya sengerema na kwa kabila alikuwa ni Mzinza,baada ya mwezi mmoja dada aliolewa na kuhamia sengerema kwaajili ya kuanza maisha
Mume aliyemuoa dada hakuwa na kipato kikubwa sana lakini pia walikuwa wanaishi nje ya mji wa sengerema kwenye kijiji kimoja hivi ambacho ukitokea jijini Mwanza ukiwa unaelekea sengerema kutokea kamanga kiko njiani tu
Baada ya mwaka mmoja dada alijifungua mtoto wake wa kwanza na masiha yaliendelea,nami niliendelea kupambana na masiha,baada ya miaka mitatu dada alijifungua mtoto wa pili,baada tu ya kujifungua dada alianza kuugua sana na ilifikia kulazwa mara kadhaa kwenye hospitsli ys rufaa Bugando na nilikuwa naklwenda kumsalimia kila nilipoweza na mama pamoja na baba [baba yangu wa kufikia] walikuwa wanakuja sanasana



Mungu alileta neema yake na dada alipona na kurudi nyumbani kwa mumewe,lakini alipopona tu mtoto wake mdogo nae alianza kuugua,hapo ilikuwa ni miezi 8 tangu ajifungue,mtoto yule aliugua sana na kufikia kuwa katika hali mbaya sana,ilibidi mama aende hadi nyumbani alikokuwa anaishi dada ili akajaribu kuangalia kilichokuwa kinamsumbua mjukuu wake kwani walishalazwa sana hospital bila mtoto kupata nafuu yoyote ile
Mama aliwasili kwenye kitongoji ambacho dada alikuwa anaishi na mumewe na kukaribishwa,mume wa dada alikuwa anaishi na familia yake pale pale alipokuwa akikaa kwani kulikuwa kuna nyumba zaidi ya 4 na moja ndio dada alikuwa akiishi na mumewe
Mama alipofika alikaribishwa kwa bashasha sana,alikaa na kusalimiana na wazazi wenzie na kujadiliana nao mawili matatu na baadae alikwenda kuongea na mwane ambae wakati huo alikuwa yupo jikoni akipika chakula kumuandalia mama yake,kabla ya kuongea sana mama aliomba kumuona mjukuu wake na alioneshwa alipokuwa amelazwa

Mama baada ya mama kumuona yule mjikuu,dada ananiambia kuwa alikuja haraka sana jikoni na kumwambia dada ajiandae kesho warudi kwao mama ili akamtibu mtot,dada alimshangaa sana mama lakini dada alimuambia hawezi kuondoka tu bila kwenda kuzungumza na mumewe ambae kwa wakati huo alikuwa hayupo pale nyumbani
Mumewe dada alikuja jioni kidogo kwani ilikuwa ni kama saa kumi na moja hivi,dada alikwenda kumuambia mumewe kuwa mama mkwe wake amesema anataka amchukue mjukuu wake akamtibu kwao,mumewe dada aliposikia vile alionesha kustuka kidogo lakini alimkatalia sana dada wazo la mama,dada alimkwenda kumuambia mama kuwa mumewe amekataa kumtoa mwanae hapa,mama alionesha kukerwa sana na hali ile lakini alikaa kimya

Baada ya kula chakula mama alimuita dada na kuanza kumueleza kuwa mwane alikuwa amefanyiwa mambo ya kie nyeji yaani uchawi na akicheza atampoteza,hivyo mama alikuwa anataka ampeleke kwa wataalam ili apone,dada alimshangaa sana mama na kumkatalia alichokisema na kumalaumu mama kwa kitendo chake cha kuamini sana ushirikina,mama hakutaka sana kubishana na dada lakini alimuambia kuwa ameona mengi na yule mtoto alipomuona tu alijua tatizo la mtoto
Basi walilala lakini usiku mtoto alisumbua sana na kulipokucha alikuwa na hali ambayo haijulikani na baadae alianza kubadilika rangi na kuwa wa kijani na baadae alianza kuzimia ilifanywa mipango ya kutafuta gari ili wamkimbize hospital na gari ilipopatikana mtoto alikuwa tayari ameshakata roho
Hadi hilo tukio linatokea ilikuwa ni majira ya saa 5 asubuhi,nilijulishwa msiba huo na bahati mbaya nilikuwa imesafiri na kwenda mkoani singida kwenye biashara zangu,niliwaambia kuwa nitajitahidi kufika kama nitafanikiwa kuwahi mazishi
Mipango ilifanywa na maziko yalipangwa siku inayofuata saa 6 mchana,walikusanyika wanakijiji na msiba uliendelea,usiku ulipofika dada alilala na mama ndani lakini wanakijiji wengine walioweza walikaa nje na walioamua kulala walilala hapo hapo

Usikuwakati dada na mama wamelala ndani walianza kusikia wakiangukiwa na vitu ambavyo hawavijui,walipowasha kibatari na kuangalia waliona ni vipande vya ugali ambao umetoka kupikwa muda mfupi uliokwisha,walitazama milango na kuona imefungwa walitazama juu kwenye bati na waliona hakuna mtu na mabati yaliyokuwa yameezeka nyumba yalikuwa vile vile
Dada alimuangalia mama kwa mshangao hawakusema kitu,cha ajabu wale wageni wengine ambao ni akina mama waliokuwa wamelala nao walikuwa wamelala fofofo na hawakuona kile kitendo na kilichowashangaza mama na dada ni kitendo cha wao tuu kuangukiwa na vile vipande vya ugali,yaani eneo walilokuwa wamelala wao tu ndio lilionekana limeangukiwa na vile vipande vya ugali na sio eneo lingine lolote lile
Walikubaliana kulala na hali ile iliendelea kwa muda na ilikwisha alfajiri ilipokuwa inakaribia,kesho yake mama alimuambia dada kuwa wakimaliza mazishi ataondoka na kama atataka aongozane nae lakini pale halali tena
Nilifanikiwa kufika siku ya mazishi na nilifika wakati ndio wanamalizia kuzika,niliwasalimia ndugu na jamaa na mama aliniita na kunieleza ambacho nimeshaeleza hapo juu,niliposikia hayo nilihamanika kidogo maana haya mambo ya uchawi sijayazoea,baada ya mazishi mama na dada waliondoka lakini kwa mzozo mkubwa kwani mume wa dada hakuwa anataka hilo litokee

Ilibidi nami niongozane na mama na dada kwani niliona kubaki pale ni kama kubaki kwenye kisiwa huku kisiwa hicho kiezungukwa na maji na wanyama wakali

Tuliondoka na kuvuka Feri salama na kufika jijini Mwanza na mama na dada walipanda gari kurudi nyumbani kwa akina mama,lakini kabla ya kuondoka mama alinisihi sana nisije nikaendas pale kwenye ile familia kwani sio watu wazuri hata kidogo.nilimkubalia mama na nilibaki na mihangaiko yangu

Ilipita miaka miwili huku nikiwa tayari nimeshasahau ile tukio na biashara zangu nilikuwa nazifanyia eneo la Kamanga kwenye feri ya kuvukia kwenda sengerema,nilikuwa napanga viatu vya mitumba kwenye kibaraza na nilienbdelea vizuri na masiah yangu hayo
Siku moja alikuja jamaa yangu moja ambae alikuwa anaishi sengerema na kuniambia kuwa kuna jamaa walikuwa wanataka viatu kama pea 8 hivi na walikuwa wanatoa hela nzuri,aliniambia kuwa jamaa wale wapo sengerema na ingekuwa vyema ningewapelekea vile viatu,niliona ni dili zuri na nilifungasha mzigo wangu na kwenda sengerema

Nilifanikiwa kufanya biashara na wale jamaa na nilipata hela nzuri tu,nilimalizana nao saa 1 usiku na nilimpatia kitu kidogo yule jamaa yangu na nilianza kufikiri mahali pa kulala.nilifikiri kuhusu kutafuta nyumba ya kulala wageni lakini niliona kama ni kutupa hela tu,nilikumbuka pale kwa yule shemeji yangu ambae alikuwa amemuoa dada miaka miwili iliyopita,nilikumbuka lile tukio lakini nikajipa moyo kuwa yale yatakuwa yamekwisha na niliamua kwenda kujaribu kulala hapo
Kutoka sengerema hadi pale kwa shemiji ilikuwa ni kama dakika 5 tu kwa boda boda na gharama yake ni shilingi 1000,nilipanga kuwa kama wataonekana kuniletea ngumu nitakwenda kulala kwa kaka wa huyu jamaa yangua ambae anaishi jirani na hapa kwa huyu shemeji yangu kwani kuna ka umbali kama kilomita moja hivi,sikutaka kulala kwa huyu jamaa yangu kwani yeye alikuwa ana chumba kimoja tu na alikuwa ana mke
Nilipanda boda boda na kufika kwa shemeji yangu,nilipokewa vizuri tu na kukaribishwa ndani,sikupata tabu sana ya kujitanbulisha kwani shemeji yang alikuwa ananikumbuka,nilikaribishwa ndani na niliingia huku nikiwa na egi kangu lililokuwa na viatu ambavyo nilikuja navyo kwaajili ya kuviuza
Nilikaa muda kidogo na shimeji alikuja kwaajili ya maongezi mawili matati na nilimuambia shida yangu na aliniambia hakuna shida nitalala na kesho nitaedelea na safari yangu ya kurudi Mwanza
Kilikuja chakula na tulikula na baadae nilioneshwa pa kulala,niliambiwa kuwa nitalala na mzee mmoja ambae nae alikuwa amekuja pale kusalimia na niliambiwa kuwa huyo ni babu yao

Kabla ya kulala walikuja mule chumbani na kukaa na kuanza kuongea na yule mzee ambae niliambia kuwa ni babu yao,mimi nilikuwa nimejilaza kitandani chali nikiwa nimevua shati na kubaki na "singlendi",nilikuwa nimevaa trucksuit na nilikuwa nimevua viatu nimebakiwa na socks

Shwmwji alikuwa amekaa upende ambao mimi nilikuwa nimeweka kichwa pale kitandani na mdogo wake shem alikuwa amesimama mlangoni
Waliendelea kuongea,lakini kadiri maongezi yalivyokuwa yanaendelea mimi nikiwa niejilaza pale kitandani nilianza kujihisi tofauti,nikiwa naendelea kustaajabu vile nilivyokuwa najisikia bila kusema kitu baada ya muda nilisikia mwili wangu ni mzito sana hadi nilikuwa nashindwa kunyanyua mguu
Niliendelea kustaajabu,kwa namna nilivyokuwa nimelele pale kitandani nilikuwa natazama paa la nyumba ile na ghafla kwenye paa nilionaa kimekuja kitu kama screen na picha za watu zilijitokeza na kilichonistua ni kuwa nilikuja kuona picha ya mama pamoja na dada yangu kwa wakati tofauti,kufikia hapo nilijua kuwa kuna shida hapa
Mwilini mwangu sikuwa na uwezo wa kunyanyua mguu wala mkono,lakini kichwa kilikuwa na uwezo wa kunyanyuka na hata macho yalikuwa yanaweza kugeuka,nilijaribu bila mafanikio kunyanyuka pale kitandani,niligeuka kumtazama yule mzee ambae niliambiwa kuwa ni babu yao na nilimuona akiendelea kuongea tu bila kuniangalia,nilipomkazi macho nilimuona akianza kubadilika na kuota mapembe halafu yanapotea

Unaweza kuona kama ni hadithi hii lakini yote haya yametokea mbele ya macho yangu,nilimkumbuka sana mama na onyo lake la mimi kutokuja hapa na nilijisikitikia huku nikiwa sina la kufanya

Nilijitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu wote lakini ilishindikana kunyanyuka pale kitandani,ulipita muda kama wa nusu saa nikijaribu kunyanyuka bila mafanikio,lakini ghafla nilikuja kushtukia nimepata nguvu na nilikurupuka pale kitandani na kusimama,shemeji alikuja na kutaka kunizuia lakini nilimtandika ngumi ambayo ilimpeleka hadi kitandani na kuanguka,shemeji mdogo alipoona hivyo alinipisha pale mlangoni na nilitoka nje na kusimama pale kibarazani
Baadae nilichuchumaa na kubaki pale kwa muda,nilipokuwa nimechuchumaa nilikuwa nawasikia ndani wakiongea,nilitazama saa yangu ya mkononi niliona kuwa ni saa 4 usiku,nilitafakari kidogo na baadae nilirudisha mawazo yangu kule ndani,nilimsikia yule mzee alisema kuwa naonekana ni mgumu sana lakini nitakiona huko ninakotaka kwenda
Niliwaza kidogo kuhusiana na mzigo wangu kule ndani lakini nilijisemea hapa ni kuokoa maisha yangu kwanza,niliondoka kwa minajili ya kwenda kwa yule kaka wa jamaa yangu ambae alinileta huku kwaajili ya kuuza viatu,kama nilivyosema kutoka hapo na kwahuyu ndugu sio mbali ni kama kilometa moja hivi
Nilianza kutenbea kutoka pale usiku ule,kulikuwa na giza sana na kila mtu alikuwa amelala,nilianza kuiacha nyumba ile na kutokomea kwenye barabara iliyokuwa inakwenda kwa yule ndugu,nilitembea kaama kwa dakika 2 hivi na ghafla niliona mtu kasimama katikati ya barabara,nilisita kidogo na niliendelea mbele kama namfuata,nilipomkaribia na kwa msaada wa mwanga wa mbalamwezi niliweza kumuona kiumbe yule,alikuwa ni kama binadamu lakini ni mweusi sana na alikuwa na macho makubwa sana kama mtu ambae anakodoa macho

Niliogopa sana lakini nilijisemea sina jinsi ilinibidi niendelee tu,nilikikaribia kile kiumbe na kilisogea mbele zani,kilivyokuwa kinasogea sio kama vile binadamu anavyopiga hatua bali kilikuwa kama vile kina matairi miguuni,yaani kilikuwa kinaserereka tu,mara kirukie kwenye mti mara kinisogelee mara kiende mbali kidogo,hali hiyo iliendelea kwa muda na kile kiumbe kilitoweka
Nilitembea sana na nilipokuja kuangalia saa niliona ni saa 6 usiku,nilistuka kwani kutoka nilipotoka hadi ninakokwenda hakuna umbali wa kunifanya nitembee kiasi hicho,nilikagua njia na mazingirz na nikagundua kuwa bado niko kwenye njia ile ile tu,lakini kwanini sifiki? sikupata jibu
Nilitazama ninakoenda na niliona paa la nyumba ninayokwenda kwani kwa msaada wa mbala mwezi lilikuwa linawaka sana,niliangalia nilipokuwa na nikagundua kwa mwendo wa kawaida mtu anatumia dakika 10 tu kuifika apale na nilijipa moyo kuwa nimekaribia
Nilitemba sana bila hata kuikaribia nyumba ile na baada ya kama saa moja hivi nilifika kwenye kijimto ambacho ukikivuka tu unafika kwa yule mdugu,nilipofika kwenye kile kijimto nilikuta kundi kubwa sana la mbwa,nilisita na kusimama huku nikiwaangalia sana wale mbwa
Nilisimama pale kama dakika 10 hivi na kuamua kuendelea na safari yangu,niliwakaribia wale mbwa huku moyo ukinidunda sana na nilipowakaribia sana nao walianza kunifuata huku wakionesha hasira,nilijisemea moyoni liwalo na liwe,niwaendea wale mbwa huku nikiaangalia kama kuna upenyo wa kukimbia lakini sikuona kutokana na miiba mikubwa iliyokuwa imeota pembeni mwa ka barabara kale



Wale mbwa waliponisogelea walitoweka na kuibukia nyuma yangu,niliwapuuza na kuendelea nasafari,niliukaribia mti mmoja mkubwa sana uliokuwa pembeni mwa barabara na nilianza kusikia kelele nyingi sana kama za watu wako kwenye harusi,nilipiiza na kuendelea mbele
Nilitembea tena kama saa moja bila kufika huku zile kelele ambazo nimeziacha kwenye ule mti zikiendelea
Nilipoangalia saa niliona ni saa 8 usiku na dakika kama 20 hivi,nilishangaa sana,yaani umbali wakutembea kama dakika 15 tu natembea masaa matano bila kufika!!
Niliendelea na safari yangu huku nikijisemea kuwa sirudi kabsa kule nilikotoka kama kufa bora nifie huku huku,nilifanikiwa kuikaribia ile nyumba na niliona kuna kundi kubwa na fisi wakinijia kwa kasi ya ajabu sana huku wakionekana wana uchu na mimi nilisimama nao walisimama,niliwaangalia nao walikuwa wananitazama tu nilipoangalia kwa makini maana sasa woga ulikuwa unaniishia niliona wale fisi wana macho kama ya binadamu na hata mmoja nilikuona akiwa na umbo kama la binadamu lakini alikuwa ana miguu minne

Niliamua kuendelea kuiendela ile nyumba ambayo niliamua kuiendea,wale fisi walisimama pale pale na nilipowakaribia waliyeyuka machoni pangu na nilifanikiwa kufiuka nilipokuwa nakwenda

Niligonga mlango sana bila mafanikio,lakini wakati naendelea kugonga nilisikia zile kelele zikihamia pale kwenye ile nyumba,sikujali niliendelea kugonga kwa nguvu hadi nilihisi nitavunja ule mlango
Niligonga sana na hatimae nilifanikiwa kusikia mwenyeji wangu akiitikia ndani,aliuliza ni nani na nilimtajia jina langu na alikuja kufungua,kutazama saa yangu ilikuwa inanionesha ni saa 9 na dakika 24 usiku,nilikaribishwa na kuingia ndani,mwenyeji wangu alimuamsha mkewe na kuja kuniuliza kulikoni
Niliwasimulia kilichinipata na walinishangaa sana kwani ile familia inasifika kwa ulozo maeneo yale na inaogopwa sana,niliwaambia kuwa nilikuwa nimekwenda pale kwa dharula tu lakini waliniambia kuwa nisije nikarudia tena
Nilipewa sehemu ya kulala lakini usingizi haukuja kabisa,nilikaa macho hadi kunakucha na nilikuja kujishangaa kwa namna ambavyo nilikuwa nimepauka na kuchafuka vumbi kwani nilikuwa natembea peku yaani bila kuvaa viatu kwa muda wote ule
Nilianza kusikia maumivu ya mwili kwa purukushani za jana,lakini nilijisemea kuwa ni lazima nitarudi zangu Mwanza,lakini wenyeji wangu waliniambia kuwa kitendo cha kuacha nguo na viatu vyangu inawezekana wakanifanyia kitu cha ajabu,nilikata shauri kuvifuata vitu vyangu asubuhi ile
Nilijisemea kama wamenishindwa usiku mchana hawata niweza,nilianza safari na mwenyeji wangu na baada ya dakika 12 tu tulifika,nilishangaa sana kwa kitendo cha kutembea masaa 6 usiku kwenye safari fupi kiasi kile
Nilipofika tu niliwakuwa shemeji yangu na watu wengine wa pale wakiwa nje,waliponiona walikimbia wote na kuiacha nyumba wazi,sikuwajali,niliingia ndani na kukuta vitru vyangu viko pale pale nilipoviacha jana yake na nilichukua na kuondoka zangu

Nilisindikizwa na mwenyeji wangu na kwenda kupanda gari na kurudi Mwanza,niliapa sitokwenda tena huko hata kama iweje kwani naona kama Mungu ananipenda sana na kuanzia hapo nikiambiwa kitu na mtu mzima namsikiliza kwa makini sana!

MWISHO

Post a Comment

0 Comments