Header Ads Widget

Responsive Advertisement

NILIPONZWA NA HURUMA YANGU


SIMULIZI FUPI - NILIPONZWA NA HURUMA YANGU

“Wakaanza kunipiga bila huruma .Mwizi huyu piga …piga…Huyu alinipiga teke,yule akanipiga ngumu,huyu akanipiga kipepsi ,mwingine akaja na gongo na kuanza kunipiga nalo .Walinishanbulia sana kama wachezaji wanagombania mpira wa kona na kila mtu alinipiga sehemu aliyochagua yeye bila kujali maumivu nitakayoyapata.Mara askari wa mgambo wakafika wakiwa ndani ya gari lao nyuma wakifuatiwa na difenda ya polisi wa kutuliza ghasia(FFU).Wamachinga wa hapo boma wakaanza kukimbia hovyo hovyo kujinusuru na kipigo na mali zao zisikamatwe na wanamgambo waliokuwa katika operesheni safisha jiji .Wale watu ambao walikuwa wananipiga wakanisukumizia kwa mgambo waliokuwa wanakuja kuwakamata na mimi niliposukumwa cha kwanza kuangalia ni mali zangu zilizoko mfukoni hama zipo au lah.Nikajipekua kila mfuko na kukuta pochi ya hela na vitambulisho pamoja na simu hazipo.

Nikaanza kuangaza huku na kule sehemu hiyo kuangalia kama vitakuwa vimedondoka huku muda huo huo wamachinga wengine wakiendelea kukimbia na kunipiga vikumbo mara kwa mara.Mgambo waliponifikia wakajua na mimi ni mmoja wa wamachinga nikiwakimbia .Aise nilipigwa ngwala hiyo nikajikuta nimedondoka chini nimelala chali .Sijakaa sawa wakaanza kunipiga na magongo yao .Nikajitahidi kuwaeleza kuwa mimi si mmachinga wala mwizi lakini wapi wao ndio kwanza wananiongeza kipigo.Nikainulia juujuu na kutupwa ndani ya difenda huku mwili wangu ukiwa umepasuliwa pasuliwa na damu kutoka na nguo zangu kuchanika ovyo ovyo.”Juma aliuwa anamsimulia bosi wake mzee Kisaka mkasa uliomkuta miezi miwili iliyopita uliomfanya kukamatwa na askari wa mgambo.

*************
Bosi yaani sijui nisemeje ,siku ile niliyokamatwa ilikuwa Ijumaa na siku hiyo mvua kubwa ilinyesha na kusababisha madhara makubwa kwa wananchi.Nilifanikiwa kuachiwa polisi siku ya Jumatatu baada ya kumwomba askari mmoja ampigie simu rafiki yangu ndipo alipokuja na kuniwekea dhamana na kuwajulisha kuwa mimi sio mwizi wala machinga .Niliporudi nyumbani nilichokiona nikajikuta nakaa chini na kuanza kulia kama mtoto mdogo.Nyumba yangu ilikuwa imebomoka kutokana na mvua ile na maji kusomba mali zangu zote zilizokuwepo ndani kutokana na mimi kujenga nyumba eneo lenye mteremko .Nililia sana mpaka nikapoteza fahamu nilipokuja kuzinduka nilikuwa hospitali dripu zikitiririka kuingia mwilini.

Nikiwa pale kitandani nikaanza kukumbuka matukio yote yaliyonisabanishia mimi kupoteza fahamu.Nikakumbuka nilipo kutana na Rashid pale boma kota barabara ya Kawawa mbele ya ofisi y mkuu wa mkoa ambapo wamachinga wanauza bidhaa zao jioni.Mimi ndie niliyekuwa wa kwanza kumuona Rashid na yeye aliponiiona tu akabadili njia kwa kunikwepa akiwa na mwanamke wake.Mimi nae nikamuwai kwa mbele kwa kufuata ile njia ambayo yeye anapita tukakutana uso kwa uso.
”Kwanini Rashid unaniona na kubadili njia kwa kunikimbia?”Nikamuuliza.
“Kwani we ni nani ,mbona sikufahamu?”
Aha Rashid leo unifahamu?”Nilimuuliza vile huku moyo wangu ukiniuma sana.
”Rashid kumbuka nilikukopesha shilingi milioni ishirini kwa ajili wewe uanzishe biashara kutokana na wewe kukosa ajira ya kuajiriwa nikakushauri ujiajiri.Au kwa sababu fedha hizo nilikukopesha bila ya kusainiana mkataba ndo maana unaamua kunizurumu?Kumbuka fedha hizo nilikopa benki kwa ajili ya kununulia gari lakini nilipokuona maisha yako ni magumu nikaamua kukupa, leo unanikana Rashid?Rashid kweli unijui?Nilitegemea kuwa ukifanya biashara na kupata mafanikio ungenirudishia fedha zangu ninunulie gari lakini wewe ndo kwanza unaponda starehe na wanawake!Wanawake hao mbona mwanzo hawakukupenda ulipokuwa huna hela lakini leo wanawake kibao wanakutaka kutokana na fedha ulizonazo. “ Niliongea kwa uchungu sana moyoni.
“We jamaa acha kunipakazia mbele ya mpenzi wangu,umetumwa nini?Mimi na wewe tumeonana wapi mpaka unipe hizo hela?”Rashid alinijibu kwa nyodo na dharau na kuamua kuanza kuniita “Jamani tapeli huyu anataka kututapeli .“Rashid aliongea vile na kuanza kunikwida shati akiendelea kuniita tapeli kwa sauti kubwa.

Wamachinga waliokuwepo hapo kusikia neno tapeli na jinsi walivyo na hasira za kupambana na mgambo walikuja mbio mbio walipotufikia wakaanza kunipiga bila ya kuuliza sababu.Nilopojitetea na kupambana nao ikawa ni kosa kubwa,wakapandisha hasira na kuanza kuniita mwizi .Wamachinga wakajaa na kila mtu akawa anagombea kupata nafasi ya kunipiga, Rashid na mpenzi wake kuona hivyo wakaondoka kimya kimya wakiniachia msala wa mimi kuwa mwizi.”

****************
Machozi yakawa yananitiririka mashavuni nikiwa nimelala pale kitandani huku dripu zikiendelea kutiririka kuingia mwilini.Fedha za mkopo wa benki nimedhulumiwa,nyumba yangu imekombwa na mafuriko,kipigo nimepigwa aha nikajikuta nalia kwa sauti mpaka watu wote waliokuwemo wodini mle wakashituka na manesi kuitwa kuja kunitizama hali yangu.
Niliporuhusiwa kutoka hospitali baada ya siku tatu ,nilienda kuishi kwa rafiki yangu yule aliyeniwekea dhamana polisi.Baada ya wiki moja nikaenda kuripoti kazini kwangu na kukabidhiwa barua ya kufukuzwa kazi sababu ikiwa ni upotevu wa shilingi milioni hamsini ndani ya idara yangu ya fedha mimi nikiwa kama mhasibu msaidizi.


Ndipo kijana wako alinikuta ninalia kama mwanamke aliyefiwa na mumewe kipenzi pale stendi ya posta mpya.Alinibembeleza ninyamaze, akaamua kunipeleka nilipokuwa ninaishi kwa rafiki yangu .Aliniomba nimueleze kilichosababisha mimi kulia vile,nikamweleza kila kitu.Alisikitika sana na kuniambia atanitafutia kazi na baada ya mwezi akanileta kwako ambapo wewe ni baba yake.Nipokuwa naishi kwa rafikiyangu tulikuwa tunafanya uchunguzi wa kwanini nifukuzwe kazi bila ya kushitakiwa kwa upotevu wa fedha kama walivyodai ,tukagundua kuwa Rashid alimuonga bosi wa pale shilingi milioni tano anifukuzishe kazi ili nishindwe kulipa mkopo wa benki nifungwe jela.

Na sasa hivi ninavyokusimulia nimepewa taarifa kuwa Rashid amepata ajali ya gari baada ya kuliovertake loli la mafuta na kumbe hakuliona loli la mizigo lililokuwa linapita upande wa pili na kugongana uso kwa uso na gari la Rashid kudumbukia mtoni na kufariki hapo hapo katika mlima kitonga akiwa anatoka Mbeya kuja Dar es salaam.Na Yule bosi wangu alienifukuza kazi ameukumiwa kifungo cha miaka ishirini jela kwa upotevu wa shilingi milioni themanini baada ya ukaguzi wa mahesabu wa ndani na wa nje kufanyika na kugundulika umegushi nyaraka nyingi za uongo pamoja na mihamala ya matumizi yake binafsi.Hama kweli niliponzwa na huruma yangu.”Alisema Juma.

Juma sasa hivi amepewa nyumba mpya ya kisasa,magari mawili ya kutembelea,bima ya afya bure na kampuni ya mzee Kisaga akiwa kama mkurugenzi wa fedha.Nyumba na magari aliopewa anakatwa kidogo kidogo katika mshahara wake na riba yake ni ndogo ukilinganisha na mikopo ya mabenki.Miezi sita ijayo Juma anatarajia kumuoa mchumba wake Fatuma aliyeko masomoni mkoani Morogoro katika chuo kikuu Mzumbe akiwa mwaka wa mwisho akisomea sheria.
MWISHO.

Post a Comment

0 Comments