Header Ads Widget

Responsive Advertisement

MARIOO


Image result for walter photography



SURA YA KWANZA
Ilikuwa pale maeneo ya bahama mama kimara jijini Dar es Salaam, katika moja ya chumba cha mazoezi ambacho kipo chini ya uongozi wa sheli ya BP, inayotoa huduma ya mafuta sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi. Isaack na Tito walikuwa bize na mazoezi ya kubeba chuma huku kila mmoja akitaka kuonesha ubabe wake mbele ya mwenzake. Isaack alikuwa pandikizi la mwanaume aliyeenda hewani, mweupe kwa rangi na mwenye sura ya kuvutia. Kwake mazoezi yalikuwa sehemu ya ratiba ya maisha yake kama ilivyo katika ratiba nyingine.
Urafiki wa Isaack na Tito ulianzia utotoni kwani walizaliwa na kukua pamoja katika mtaa wa MSEWE na walipofika umri wa kwenda shule, walipelekwa pamoja shule ya msingi MLIMANI ambako walisoma pamoja hadi kuhitimu darasa la saba. Isaack hakupenda sana shule hata darasa la saba alimaliza kibahati bahati tu, kwani kuna muda alitoka nyumbani vizuri akiwa amevalia sare za shule lakini alipofika njiani, alibadili na kuvalia nguo za nyumbani ambazo alikuwa amezificha kwenye begi lake la madaftari na kutokomea mtaani, ambako alicheza na kusubiri muda wa kutoka shule ulipofika, kisha kuvalia nguo zake za shule na kurudi nyumbani na wenzie waliotoka shule kama vile naye ni miongoni mwa waliotoka shule kumbe laa!
Baada ya kuhitimu elimu ya msingi, Isaack hukuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari , jambo lililomfurahisha sana kwani alishapanga akilini mwake kwamba hata angechaguliwa kuendelea, yeye asingeendelea na kama wazazi wake wangemlazimisha basi angetoroka na kuelekea anapopajua yeye. Wanasema ukitembea na mwizi basi na wewe utakuwa mwizi lakini kwa Tito hii ilikuwa tofauti, kwani pamoja na urafiki na ukaribu aliokuwa nao kwa Isaack, bado haikumfanya yeye kutopenda shule. Alikuwa akifanya vizuri sana katika masomo yake na hata walipomaliza darasa la saba, yeye ni miongoni ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari katika shule ya sekondari ya AZANIA BOYS, japo wazazi wake wanaamua kumpeleka kusoma nchini UGANDA kwa kuhofia labda mtoto wao atafuata mkumbo wa rafiki yake na kukataa shule. Hivyo kwa mara ya kwanza toka utoto wao, marafiki wale walitenganishwa na umbali wa kijiografia.
Kuondoka kwa Tito kuelekea masomoni nchi jirani ya UGANDA, kulimwacha rafiki yake mpweke sana, kwani walizoeana sana na walikuwa wakifanya mambo mengi pamoja. Wiki ya kwanza toka Tito aondoke, Isaack alikosa raha kabisa. Alikuwa wa kujifungia ndani na asiyesema na mtu yeyote. Sanasana alitoka nje ya chumba chake kula na kurudi ndani, ambako alilala na mara nyingine kulia. Baada ya muda kupita Isaack alianza kuzoea ile hali na hata akaanza kutoka kujichanganya na marafiki zake wengine, japo hakuwa na ukaribu nao kama alivyokuwa karibu na Tito lakini alikuwa hana cha kufanya kwa wakati ule zaidi ya kukubaliana na ukweli kwamba rafiki yake kipenzi hayupo na hakujua angerudi lini.
Ilikuwa jioni siku ya jumamosi, wiki mbili toka Tito aondoke. Isaack alitoka nyumbani kwao mitaa ya MSEWE na kuelekea viwanja vya mpira vya BARUTI ili kupoteza mawazo na kujichanganya na marafiki zake wengine, ambao walipenda sana kucheza mpira wa miguu mida ya jioni katika viwanja tofauti tofauti vya nyumbani. Alipofika katika viwanja vile, alikuta vijana wengi wakifanya mazoezi na wengine wamezunguka uwanja wakiangalia kinachoendelea, wengine walikuwa wamekaa na wapenzi wao na wengine walikuwa wakivuta bangi hadharani bila woga wowote.
Pamoja na utukutu wake wote, Isaack hakuwahi kuwa na mwanamke wala hakuwahi kuvuta sigara wala bangi. Alitafuta kivuli na kukaa peke yake huku akiangalia marafiki zake ambao kwa muda ule walikuwa wakipasha misuli kujiandaa na mchezo wa kirafiki kati ya vijana wa MSEWE na wale BARUTI.
“Niambie kichaa wangu, mbona umekaa peke yako kama mwanga? Jichanganye na wana kule au kama una mawazo nenda mitaa ile kapate dawa”. Alisema kijana mmoja akimwambia Isaack ambaye alikuwa bize akiangalia wenzake wakisakata kabumbu uwanjani. Wala hakuangaika kumjibu, aliendelea kuangalia wenzie wakifanya mazoezi. Alijikuta akivutiwa na mpira hata akawa anashangilia na kidogo akaanza kuchangamka na kusahau juu ya rafiki yake kipenzi.
Muda wa kupasha uliisha na timu za pande zote mbili ziliingia rasmi kwa ajili ya mechi ya kirafiki, ambayo ilikuwa kivutio kikubwa kwa watazamaji waliokuwepo pale uwanjani na hata kwa wapita njia waliokuwa wanapita, baadhi yao walisimama kuangalia jinsi vijana wadogo wakisukuma mpira. Isaack alishindwa kuzuia mihemuko yake na kujikuta akishangilia kwa nguvu huku akiita jina la rafiki yake waliyempa jina la utani MESSI kwani walikuwa wakimfananisha na mchezaji wa Barcelona, kwa uwezo wake wa kupachika magoli nyavuni.
Kwa mara ya kwanza toka Tito aondoke, kidogo siku ile ndiyo Isaack alianza kurudi katika hali yake ya kawaida kwani upweke aliokuwa nao ulipungua kama siyo kuisha kutokana na kujichangaya na vijana wenzake. Aliahidi nafsini mwake kwamba ataanza kufanya mazoezi na wenzake japo yeye hakupendelea sana mpira wa miguu kama ilivyo kwenye ngumi, lakini aliahidi kwamba atakuwa anaungana na wenzake ili kufanya mazoezi na kupoteza mawazo.
SURA YA PILI
Nyumbani kwa kina Isaack baba yake alikuwa peke yake sebuleni akiangalia taarifa ya habari ya saa moja usiku kupitia moja ya kituo cha luninga cha channel ten. Pamoja na macho yake kutazama luninga, mawazo yake hayakuwa pale kwenye luninga bali yalikuwa juu ya kijana wake Isaack, ambaye ndiyo kwanza amemaliza darasa la saba lakini hataki tena kuendelea na masomo ya sekondari. Baba yule aliwaza sana juu ya mwanawe kwani yeye alipenda kuona mwanae anasoma hadi kumaliza elimu ya juu, ili ndiyo hivyo penye miti hapana wajenzi.
“Hivi huyu mtoto nitampeleka wapi? Mbona anataka kunipa presha mapema namna hii? Hapa cha kufanya ni kumpeleka japo VETA labda akiwa dereva tunaweza kusaidiana kusimamia hii biashara ya daladala na mimi nikapata muda wa kupumzika. Maana na umri wenyewe umeenda, atashirikiana na kaka yake nami nitafute kitu kingine cha kufanya. Hawa watoto wa siku hizi… yani ni tofauti na wale wa enzi zile, yani kwa sababu wanaona wanakula na kulala basi wanaridhika kabisa, enzi zetu tulitamani kusoma ila wazee wetu hawakuona umuhimu wa elimu ila siku hizi toto linapata nafasi ya kusomeshwa ila ndiyo hayataki kusoma… mh kweli kuwa uyaone”. Mzee Mbiru alikuwa akiwaza na kuwazua.
Wakati anamalizia kuwaza mara Isaack anaingia. Alisalimia na kupita kuelekea chumbani kwake, ila kabda hajafungua mlango wa chumbani baba yake alimuita na kumtaka aketi katika moja ya sofa pembeni yake. Alikaa bila ubishi na kumsikiliza baba yake ambaye alianza kwa kumfokea kwa ukali “wewe sa hizi ni saa ngapi? Nimeshasema nyumbani kwangu huwezi kurudi muda unaotaka, ukijiona umekuwa nenda kapange chumba ili ujiamulie muda wa kurudi”.
Isaack alikaa kimya bila kujibu chochote kwa baba yake ambaye alionekana kuwa mwenye hasira sana. Ni kweli kati ya watoto wa mzee Mbiru, ni Isaack pekee aliyekuwa na tabia tofauti na wenzake kwani alikuwa mvivu sana asiyependa kujituma kama ndugu zake waliomtangulia, yeye kwake kila kitu aliona tabu. Alipenda tu kukaa na kuangalia luninga tena chumbani kwake ili asitumwe. Tabia ambayo ilimfanya atofautiane kabisa na kaka yake pamoja na mdogo wake, ambaye pamoja na umri mdogo aliokuwa nao alionekana mtoto mwenye bidii ya masomo na hata siku ambazo hakuna shule, NIM alijishughulisha na shughuli mbalimbali pale nyumbani.
“Nimekuita hapa ili uniambie unataka kufanya nini, maana toka umemaliza shule umekaa tu shule umesema hutaki hata nikikupeleka nitatupa tu pasa yangu. Sasa useme mwenyewe unataka kufanya nini au kama umeridhika kuja ukute chakula mezani ule na kwenda kulala useme, ila ujue miaka inakwenda na hautabaki kuwa mdogo siku zote… na sisi wazazi wako hatutaishi milele kuwaletea chakula na mahitaji mengine, kuna wakati utafika na sisi tutatakiwa kuwategemea nyie au utakuwa na familia yako ambayo itakutegemea kwa kila kitu kama nyie mnavyotutegemea mimi na mama yenu leo, kwa hiyo unatakiwa ujue kwamba maisha siyo lele mama”.
Isaack alikuwa kimya muda wote akimsikiliza baba yake ambaye hasira zake zilionekana kupungua na alikuwa akiongea kawaida. “Baba mimi kweli shule sitaki nataka ubondia… naomba unipeleke pale URAFIKI kuna academy ya ubondia hata kaka wa rafiki yangu anaendaga…”.
“Unasemaje! Yani shule hutaki unataka ubondia! Unataka kuwa jambazi au? Na hayo mawazo umeyatoa wapi? Sasa sikupeleki ubondia wala mieleka utaenda shule ya VETA, tena jumatatu ujiandae mapema tuondoke wote…usitake kunipangia kama vile unajua hela inavyotafutwa… jumatatu ujiandae mapema muda ninaotoka kwenda kazini, twende wote ukachukue fomu na kama hutaki basi utafute pa kwenda mapema kwa sababu hapa kwangu itakuwa ndiyo mwisho wa wewe kukaa”.
Isaack aliondoka akiwa mnyonge na kuelekea chumbani kwake, ambako alijitupa kitandani na usingizi ukamchukua bila hata ya kula chakula cha usiku.
***
Mzee Mbiru alikuwa alinyanyuka kwa hasira na kuelekea chumbani, ambapo alianza kumgombeza mkewe. “Unaona kazi uliyoifanya kwa huyo mwanao? Nilikuambia unaharibu watoto, ona sasa madhara ya kulea watoto kama yai… toto halitaki shule kwa sababu ya uvivu na kudekezwa, linaona maisha ni rahisi kwa sababu ya kufanyiwa kila kitu… mimi sifugi wajinga nyumbani kwangu kwa sababu kwetu hakuna wajinga wajinga namna hii, labda kafuata damu ya huko kwenu. Kaongee nae kabisa kesho ajiandae nampeleka VETA na kama hataki utafute pa kumpeleka maana hapa ndo itakuwa mwisho wa yeye kukaa”.
“Mume wangu ukisema hivyo unakosea…ina maana mimi ndiyo sipendi maendeleo ya mtoto? Kila jambo baya chanzo ni mimi tu humu ndani… hakuna hata moja zuri kwangu? Kama unaona sijui kulea basi kaa ulee mwenyewe maana mi nishachoshwa na gubu na dharau zako… yaani umeona kwetu ndiyo wajinga ? kama ulijua ni wajinga kwa nini ulikuja kuoa? Ukiona hivyo na wewe ni mjinga ndiyo maana umeona katika ukoo wa wajinga”.
Mama yake Isaack alikuwa akiongea kwa jazba huku akitokwa na machozi, lakini mzee Mbiru hakujali alimshika na kumpiga kisawa sawa hadi hasira zake zilipoisha. Isaack alikurupushwa usingizini kwa kelele za mama yake aliyekuwa akiomba msaada baada ya kipigo cha mumuwe, ambacho yeye ndiye alikuwa chanzo cha yote. Alitoka mbio na kumgongea Zaituni (dada wa kazi) ili aweze kwenda kumsaidia mama yake aliyekuwa analia kwa maumivu makali.
“Nimekuambia leo ndiyo mwisho wa hii ndoa, huwezi kunipiga kama umenizaa… nimeshavumilia vya kutosha, sitaki tena bora niondoke”.
“Uondoke una pa kwenda maskini wewe… familia yako yote inanitegemea mimi. Utaenda wapi? Wewe kaa hapo usubiri kuletewa, kama hujui nimekuoa wewe na familia yako”.
Mzee Mbiru alikuwa akimtolea mkewe maneno yale, huku akivaa chati ambalo alivua ili kumshughulikia. Alitoka nje na kumwacha mkewe katika maumivu makali ya mguu. Zaituni na Isaack waliingia chumbani na kumkuta mama yao akiwa chini na waliposema wajaribu kumnyanyua walishindwa kwani alikuwa analalamika maumivu ya mguu. Kuona vile Isaack alitoka mbio na kwenda kuomba msaada kwa marafiki wa familia yao, wazazi wa Timo ili waje kumsaidia mama yao.
Ilikuwa usiku mishale ya saa nne na robo hivi, Timo aliingia ndani mbio bila hata kubisha hodi. Alikuta watu wamekaa sebuleni wakiangalia igizo katika luninga, kulingana na presha aliyokuwanayo hakuweza hata kusalimia alijikuta tu karopoka “ Mama yangu anakufa!”.
Kwa sababu siyo mara ya kwanza kwa jambo lile kutokea, mama yake Timo alitoka mbio na kwenda kwa shoga yake ambaye amekuwa akipigwa mara kwa mara. Alimkuta bado yupo chini akigaagaa kwa maumivu na yeye bila kupoteza muda, alimpigia mumuwe aje na gari ili wamkimbize hospitali kwani hali aliyomkuta nayo ilikuwa tofauti na vipigo vya siku nyingine.
“Pole shogangu, huyu mwanaume atakuja akuue… siku hizi ndoa hazivumiliwi mama! Ukiona maji ya shingo bora kujiondokea tu maana utakuja ufe huku unaona, we huoni wanaume wanavyochinja wake zao? Sikushauri kuvunja ndoa yako lakini bora uondoke ili unusuru roho yako kuliko kuja kufa na kuacha watoto wakiwa yatima. Bora wajue wana mama hata kama hawaishi nae kuliko kubaki bila mama kwa uzembe na vipigo vya baba yao”.
“Yani huyu mwanaume ni mbwa, eti kanipiga kwa sababu ya Isaack kukataa shule… anasema mimi ndiyo chanzo. We uliona wapi mzazi wa dunia ya leo akafurahia kumwona mwanawe akiishia shule ya msingi? Si basi tu watoto wanaamua kueleleza wazazi wao!”
“Haya shoga yangu hebu nyanyuka tukupeleka hapo ARAFA DISPENSARY… baba Timo kashafika.” Mamake Timo alimwambia huku akimsaidia kunyanyuka pale alipokuwa .
SURA YA TATU
Mzee Mbiru alikuwa LATEMBA BAR akilewa kama kawaida yake, akishampiga mke wake huwa hajali kama kamuumiza wala nini. Yeye huenda baa na kulewa mpaka usiku mkali na kuamua arudi au asirudi nyumbani. Mara ya mwisho alimpiga mke wake na kuondoka ila baada ya majirani zake kumpeleka hospitali ,aligundulika amevunjika mbavu mbili za upande wa kulia jambo lililosababisha kulazwa katika wodi ya mifupa MOI pale Muhimbili, na aliporudi nyumbani pamoja na kwamba mke hakuwepo yeye aliendelea na shughuli zake kama kawaida kama vile hakuna kilichotokea.
Pale ARAFA DISPENSARY baada ya kuwafikisha , baba yake Timo aliamua kumuacha mke wake na rafiki yake ambaye bado alikuwa analalamika maumivu kwa ajili ya vipimo na kwenda kumtamfuta mwanaume mwenzake, kwani alijua kijiwe chake. Alipania kumweka chini kama mwanaume mwenzake na jirani yake kwani aliona sasa amezidisha kipimo cha unyanyasaji kwa mkewe.
“Huyu jamaa sijui anavuta bangi? Hivi anawezaje kumpiga mke wake kiasi kile halafu akamuacha ndani peke yake na kuondoka! Kweli wanaume tunaitwa katili lakini huyu mwenzangu sasa amezidi… leo lazima nimwambie kama mwanaume mwenzangu kama amemchoka mwenzake amwache aende kuliko kumtesa namna hii”. Mzee Koola alikuwa akiwaza huku akitembea kwa miguu kutoka pale ARAFA kuelekea LATEMBA kwani ilikuwa kama hatua kumi tu.
Kama vile alijua ile kufika tu pale LATEMBA, alimkuta mzee Mbiru amekaa kaunta peke yake akiwa anamimina safari kama vile hakuna kilichotokea. Alipofika, alinyoosha moja kwa moja hadi pale kaunta ambapo alimsalimia rafiki yake yule , urafiki uliosababishwa na watoto wao.
Mbiru aliitikia huku akishindwa kuzuia mshtuko alioupata baada ya kumuona jirani yake, kwani ni mara chache sana Koola alienda baa hivyo alijua tu alikuwa pale kumfuata yeye na hakika walishajua kama alimpiga mke wake.
“Karibu jirani… dada msikilize jamaa anakunywa nini…”. Alisema Mbiru huku akijisogeza ili mwenzie akae lakini cha kushangaza Koola alikuwa kavimba kwelikweli.
“Asante jirani ila mimi siyo mkaaji… nataka nikung’ate sikio kidogo, hivyo kama hutojali naomba tusogee pembeni ambako hakuna kelele. Niwie radhi sana kwa kukutoa kwenye starehe yako ila sitachukua muda wako”.
Walisogea pembeni karibu na jiko la kuchomea KITIMOTO, ambako hapakuwa na watu wengi na maongezi yakaanza. Kwa sababu Mbiru alishapata chupa kadhaa za safari, haikuwa rahisi sana kuongelea masuala ya familia yake. Kwanza alikuja juu na kumwambia rafiki yake asimuingilie katika masuala ya familia yake, ila baada ya Koola kumtishia atapiga simu polisi kumripoti kwa ukatili anaomfanyia mkewe mara kwa mara, ndipo alikuja chini na kukubali kuongea kwa nidhamu.
“Rafiki yangu nimekuwa kimya muda mrefu juu ya suala la wewe kumfanya mke wako kama ngoma ya mdundiko… ila nadhani damu ya mkeo itanililia nisipochukua hatua mapema kwa maana huko unakoelekea sasa ni kumuua kabisa…hivi unawezaje kumpiga mwanamke mzuri vile! Hujui kuna wengine wanatamani kuwa na mwanamke kama wako ila hawajampata…
“Okey… kwa hiyo unataka kuniambia unamtamani mke wangu! Nimeshajua njama zako unataka nimuache ili umchukue… sasa nakuambia hivi yule ni mke wangu na nimemlipia mahari… usifikiri nitamuacha… hiyo sahau yule hana pa kwenda nimemuoa yeye pamoja na ukoo wake wote.”
“Sasa ndugu yangu naona huko unakoenda siyo kabisa… mi nimtake mke wako nimpeleke wapi wakati na mimi nina wa kwangu? Hapa nimetolea tu mfano kwamba wakati wewe unampiga mke wako na kumnyanyasa, kuna wengine wanammezea mate na kutamani wapate hiyo nafasi ya kummiliki kwa hiyo kama unajidanganya kwamba hana pa kwenda subiri siku akisema imetosha ndiyo utajua kama ana pahala pa kwenda ama laa! Naona utakuwa huwafahamu vizuri wanawake… ni wavumilivu sana ila siku akikuambia imetosha ujue hawatanii”.
“Nikuambie tu kwamba Isaack alikuja nyumbani akilia na kutuambia mama yake anakufa, na mke wangu alipoenda ndipo akanipigia niende kumchukua na hivi ninavyokuambia nimewaacha hapo ARAFA wanampatia maatibabu… unawezaje kuwa na roho ya ukatili namna hiyo… sawa umempiga lakini unaondokaje na kumuacha mwenzio katika maumivu makali namna ile?”
***
Mzee Mbiru alikuwa kimya kama vile kamwagiwa maji ya baridi, kumbe ubabe wote kwa mke wake ila hakuwa na ujanja kwa mwanaume mwenzake. Mashavu yalikuwa yanachuma kunde kwa aibu iliyompata. Hata kunyanyua uso wake kumwangalia rafiki yake ilikuwa mtihani.
Kuna msemo kwamba “safari moja huanzisha nyingine” ila kwa siku ile safari moja ilizima nyingine, kwani safari ya mzee Koola pale ilizima safari ya kukata mti panda mti. Ilibidi hata ile bia iliyokuwa imeshafunguliwa aiache mezani na kuongozana na mwenzake kwenda ARAFA DISPENSARY kumuona mke wake.
Maneno ya rafiki yake yalimpenya mpaka moyoni na kujikuta akijutia uamuzi wake aliochukua juu ya mke wake mara kadhaa, alifikiria kauli ya rafiki yake iliyosema “usijidanganye unaposema hana pa kwenda, kwani siku akisema basi ujue ndo ushamkosa”. Alikumbuka siku ile mke wake alisema kauli kama ile kwamba hawezi kupigwa kama ngoma kila siku, pombe yote ilimuisha ghafla. Alihofia ile kauli kwani ni mara ya kwanza mke wake kuitamka toka waoane, alijiuliza hivi ni kweli mke wake alimaanisha au hasira tu?
“Inawezekana huyu jamaa anamchukua mke wangu nini? Usikute wameshapanga kwamba aniache… mbona nampiga kila siku hajawahi kusema maneno ya leo? Na jamaa kasema mwanamke akisema basi ujue ndiyo imetoka… kuna mchezo hapa”. Mbiru alikuwa akiwaza na kuwazua, alijiuliza maswali na kujipa majibu yeye mwenyewe. Kumbe pamoja na kumtesa mke wake bado alihofia kuachwa… inastajaabisha sana!
Walifika ARAFA na kuindea mapokezi ili kujua nini kimejiri kwenye vipimo. Muuguzi wa zamu aliwaelekeza chumba walichokuwepo na kufika walishangaa kumkuta mgonjwa akiwa amevishwa hogo dogo kwenye viungio vya mguu mmoja wa kushoto, ambao kwa maelezo ya daktari alisema mguu ulikuwa umeteguka, mfupa ulihama na kwenda pembeni hivyo alimfanya kuurudisha kwa nguvu na kumfunga hogo ili uweze kurudi pahala pake.
Mbiru kwa aibu ilibidi atoke nje kwani hakuwa na cha kuongea. Alienda mapokezi na kuulizia jinsi ya kufanya malipo na yule nesi alimtaka asubiri aende kwa daktari kuchukua jalada na aliporudi alimpa hesabu nae akalipa pesa yote iliyodaiwa.
SURA YA NNE
Ilikuwa majira ya saa kumi na moja alfajiri, Isaack alikuwa tayari ameshajiandaa tayari kuongozana na baba yake ambaye jana yake alimwambia ajiandae aondoke nae ili wakachukue fomu kwa ajili ya kujiunga na chuo cha ufundi cha VETA. Pamoja na kwamba Isaack alishakataa kusoma, alijiona kama mkosaji baada ya mama yake kupigwa kwa ajili yake hiyo aliona ni bora aende shule ili kurudisha amani miongoni mwa wazazi wake ambao kila mara wamekuwa wakigombana kwa ajili yao.
Chumbani kwa mzee Mbiru, alikuwa yeye peke yake akipiga pasi nguo zake tofauti na siku nyingine ambazo mkewe ndiye alikuwa anafanya kazi hiyo. Mke wake alikuwa katika moja ya vyumba vya wageni amelala kwani baada ya kurudi kutoka hospitali, hakutaka kabisa kumwona mumewe kutokana na hasira ambazo bado alikuwa nazo kufuatia kichapo alichopewa jana yake.
Mzee Mbiru kwa mara ya kwanza toka amuoe mke wake, alihofia kumpoteza kutokana na maneno ya jirani yake mzee Koola, maneno ambayo yalikuwa yakijirudia kichwani kila dakika iliyopita. Alijipa moyo na kuondoka kuelekea katika biashara zake kwa kuanzia VETA ambapo alimchukulia Isaack fomu ya kujiunga na ufundi umeme wa magari na kumtaka arudi nyumbani kwa ajili ya kujiandaa na kuanza shule kwani wenzake walishaanza kusoma yapata kama wiki moja hivi.
“Upitie kwa yule fundi wangu mwambie akupime suruali mbili za rangi ya bluu, we mwambie tu ni za uniform za VETA ye ataelewa… tena umuambie zina haraka mi nitampitishia hela nikirudi jioni. Sawa?”
Isaack aliitikia kwa kichwa huku akianza kuondoka kuvuka barabara ili apande daladala kurudi nyumbani. Cha kushangaza baada ya kufika nyumbani alimkuta mama yake akifungasha nguo zake kwa kushirikiana na mama yake mkubwa yaani dada wa mama yake ambaye alikuwa akiishi TABATA MATUMBI.
Baada tu kupigiwa simu kwamba alikuwa amepigwa na kuvunjwa mguu, Neema aliamua kuja asubuhi na mapema kumwona mdogo wake ambaye amekuwa akipigwa na kunyanyaswa na mume wake toka wafunge ndoa.
“Yesu! Kwa hiyo amekuvunja kabisa mguu ili usitembee ukae tu ndani? Sasa nakuambia hivi utakuja ufe kwa ujinga wako… leo hapa utaondoka ama kwa lazima au kwa hiari ila hatuwezi kuona unakufa tukakuacha .” Neema alikuwa akiongea kwa hasira baada ya kuingia na kumuona ndugu yake akiwa kitandani na hogo mguuni. Wakati maneno yote yakimtoka, mdogo wake alikuwa akilia kwa uchungu na kumwambia “nimechoka mimi… siwezi tena kuvumilia hii ndoa bora kufa tu.”
“Kufa? Kwa nini ufe kabla ya siku ulizopangiwa na Mungu kuisha? Kila mtu lazima afe lakini pale muda ukifika huwezi kukaa hapa upigwe kama ngoma halafu useme unataka kufa…na hatuwezi kuruhusu huu unyama uendelee, leo ndiyo mwisho maana hapa lazima tuondoke wote. Nimeongea na kaka mkubwa aje na usafiri kwa ajili ya kubeba vitu hapa lazima tumwache yeye na nyumba yake tu lakini vitu vyote tutasafisha ili ajue siyo kwamba huna ndugu… tuliamua kukaa kimya kwa kuheshimu ndoa ila sasa naona anataka kutupanda kichwani. Sasa leo anatakiwa akirudi akute nyumba inamwangalia ili ajifunze adabu.”
Isaack kama kawaida yake aliingia chumbani kwake na kujifungia . Alijitupa kitandani na kujikuta akilia kwani alimpenda sana mama yake hivyo kitendo cha mama yake kufungasha na kuondoka kilimtia simanzi. Alijua fika hata kama angetaka kuondoka na mama yake, baba yake asingekubali hivyo alijiona mkosaji sana. Alichukia ukali wa baba yake ambao alikuwa akiufanya kwa familia nzima kuanzia kwa watoto mpaka kwa mama yao ambaye sasa alikuwa amechoka na alikuwa akifungasha ili aondoke.
Baada ya kukaa chumbani kwa muda aliamua kutoka na kumfuata mama yake chumbani na kumkumbatia kwa nguvu huku akilia “mama usituache peke yetu… kama unaondoka tuondoke wote…”. Isaack alikuwa akilia mfululizo na kumfanya mama yake kuacha kufungasha na kumkalisha chini.
“Sikiliza mwanangu, kuondoka kwangu haina maana siwapendi ila naenda tu kujiuguza nikipona nakuja. Isitoshe nitakuwa nakuja kuwaona kila mara… hivyo acha kulia. Najua wewe na mdogo wako bado ni wadogo na mnahitaji malezi yangu ila kwa sasa hivi mama yenu nahitaji kupumzika kidogo… ukinimiss utakuja kunisalimia kwa mama yako mkubwa sawa?”
“Sasa NIM akirudi kutoka ziara nitamwambia nini? We mwenyewe unajua ni kwa jinsi gani amekuzoea… si atakuwa analia kila siku? Kwa nini usimsamehe tu baba? Najua mligombana kwa ajili yangu ila si nimeshakubali kwenda shule?
“Isaack we bado mdogo, mambo siyo rahisi kama unavyofikiria. Najua ni kiasi gani unaumia mama yako kuondoka ila usijali akipona atarudi, sawa baba?” mama yake mkubwa aliamua kuingilia maongezi ya mama na mtoto, ila Isaack hakuelewa ndo kwanza alikuwa amezidisha kilio.
***
Ilishahitimu majira ya saa sita kasorobo, Neema na mdogo wake wakisaidiana na Zaituni walishamaliza kufungasha vitu vyote walivyotaka kuondoka navyo. Neema alipiga simu kwa kaka yake kumjulisha kwamba walikuwa tayari wakisubiria gari ili waweze kuondoka mahali pale kabla mzee Mbiru hajafika kwani wote walijua ukorofi wake. Kipara ambaye ni kaka mdogo wa Neema hakutaka kuja moja kwa moja kumchukua dada yake na hii ni kutokana na mila na desturi zao hivyo alichokifanya ni kumwagizia yule mwenye gari na kumpa namba ya simu ya dada yake ili waweze kuwasiliana ili awafuate.
Kutokana na nyumba yao kuwa karibu na kituo cha basi cha KONA haikuwa ngumu kwa yule dereva kufika, hivyo alifika na kazi ya kupakia vitu ilianza. Vijana aliokuja nao walikuwa wazoefu hivyo haikuchukua muda mrefu kumaliza, mama yake Isaack aliiacha nyumba yake kwa mara ya kwanza toka aolewe, na kumwacha Isaack na Zaituni huku akimsisitiza awaangalie wanawe vizuri. “Dada naomba uniangalizie wanangu eee… NIM akirudi kutoka ziara naomba unisaidie kukaa nae vizuri nitakuja kuwaona jumapili, sawa?”
Zaituni hakuwa na namna zaidi ya kuitikia, japo alikuwa na mawazo ya kuachiwa nyumba peke yake na mama mwenye nyumba kuondoka. Alikuwa mdogo kwa umri kwani hata darasa la saba hakuwa amemaliza ila mama yake aliamua kumwachia aende mjini kutafuta kazi ili aisaidie familia yake, hivyo toka aanze kazi takribani mwaka na nusu sasa hakuwahi kuona mshahara wake. Bosi wake alikuwa akiutuma nyumbani kwao Iringa moja kwa moja. Alichoambulia yeye ni nguo na mahitaji mengine ambayo bosi wake alimnunulia kila alipowanunulia wanae. Hii ilimfanya ajione miongoni mwa watoto wa nyumba ile kwani mama yake Isaack aliishi nae vizuri kama alivyoishi na wanawe.
Ilikuwa usiku wa saa tatu, mzee Mbiru alikuwa akiingia kutoka kazini. Alishikwa na butwa alipoingia chumbani kwake na kukuta chumba kikimuangalia. Alichokuta ni nguo zake tu ambazo zilifungwa katika furushi moja na kuwekwa sakafuni. Hapakuwa na kitanda, godoro wala kabati la nguo kama alivyozoea kupakuta. Alipata mshtuko wa hali ya juu hata kujikuta akikaa juu ya lile furushi la nguo zake.
“Yeto! Hivi naota au ni kweli? Huyu mwanamke kumbe alikuwa hatanii? Atakuwa ameenda wapi sasa…siyo bure atakuwa amepata mwanaume wa kumjaza maneno. Mbona siku zote nampiga na hajawahi hata kuhama chumba! Leo kumpapasa tu kidogo amefungasha na kufungasha?” mzee Mbiru aliwaza na kujiuliza maswali mengi ambayo hayakuwa na majibu kisha kutoka nje na kuondoka kuelekea kwa jirani yake mzee Koola.
Koola na mke wake walishangaa kumuona Mbiru usiku ule kwani haikuwa kawaida yake. Walilmkaribisha ndani ila cha kushangaza mzee Mbiru alionekana mwenye hasira kupindukia. “Usijifanye mtakatifu naomba uniambie umemficha wapi mke wangu maana jana uliniambia maneno ambayo hayakuniingia akilini. Mi siyo mtoto najua tu wewe unajua mahali mke wangu yupo.”
Maneno ya mzee Mbiru yaliwaacha mdomo wazi Koola na mkewe kwani hawakuelewa alikuwa akimaanisha nini. Baada ya kuona hawamuelewi, mke wa Koola aliamua kumuuliza mzee Mbiru alichokuwa anamaanisha ila kabla hata hajamalizia kusema alichokuwa akitaka kusema, mzee Mbiru alimkata kauli.
“Shemeji samahani siongei na wewe, naongea na huyu mwanaharamu anayejifanya mwaminifu sana kumbe ni malaya tu. Muulize alianza lini kutoka na mke wangu na sasa ameona haitoshi kuiba ameamua kumtorosha. Bora yangu mimi mlevi nakesha baa ila siyo malaya kama huyo mumeo anayejifanya yuko pembeni yako muda wote kumbe anakung’ong’a tu.”
“ Shemeji naona sasa umeenda mbali mno, hayo unayosema una ushahidi nayo au unasema tu kwa sababu umepewa mdomo wa kuongea? Nakuheshimu sana naomba usinifanye nikuvunjie heshima kwa ajili ya vitu vidogo,” Muda wote wakati Mbiru akijibishana na mama yake Timo, Koola alikuwa kimya tu akimwangalia Mbiru kwa mshangao kwani katika wazee wa ule mtaa aliokuwa akiwaheshimu, basi naye alikuwa miongoni mwao ila kwa siku ile alikuwa akielekea kuivunja heshima iliyodumu kwa miaka yote toka wahamie mahali pale.
SURA YA TANO
Ilikuwa siku ya jumatatu majira ya saa 2:00 asubuhi, Isaack alikuwa ameketi katika darasa la wanafunzi wasiopungua hamsini wakimsikiliza mwalimu wao aliyekuwa akitoa somo juu ya umeme wa magari. Isaack alikuwa kimya kama mwenye kusikiliza, lakini ukweli ni kwamba hakuwa darasani kimawazo bali kimwili tu. Siku ile kwake ilikuwa kama adhabu tu kwani hakuwa anapenda kabisa maisha ya darasani, alichowaza yeye ni kuwa dereva na siyo fundi wa magari. Kuja kwake pale ilikuwa kama kuwaridhisha tu wazazi wake na alidhani kwa kufanya vile angeweza kuinusuru ndoa ya wazazi wake lakini alishachelewa kwani mama yake alishaondoka na kuwaacha.
Pamoja na umri mdogo Isaack aliokuwa nao, alikuwa ni mwenye mawazo ya kiutu uzima kwani aliwaza namna ya kupata pesa ndiyo maana alitaka kujua udereva ili atafute kazi na kujitegemea. Kabla ya ndoto yake ya ubondia kuingiliwa na baba yake, Isaack alijua atawekeza nguvu zake kwenye ngumi ili kujiajiri kwa kutumia kipaji chake, ila baada ya kukataliwa na baba yake kwenda shule ya masumbwi, aliamua kuwa dereva ili aweze kupata kazi haraka au hata kusimamia magari ya nyumbani na kulipwa mshahara kama ilivyokuwa kwa kaka yake.
Aliendelea na shule kwa shingo upande ila nguvu kubwa alielekeza kwenye kujifunza kuendesha gari zaidi ya ufundi. Kutokana na wepesi aliokuwa nao katika kujifunza, na mwili mkubwa kuliko wenzake, mwalimu wake alimpenda sana na kumtumia sana kwa kazi za nje ya chuo.
Ilikuwa jumamosi, na kama ilivyo ada siku ile mwalimu wao aliamua kuitumia kwa mazoezi ya vitendo. Wanafunzi waligawanywa katika makundi ya watu kumi na kila kundi kupewa mkufunzi mmoja wa kuwasimamia na kuwaelekeza. Ilikuwa zamu ya Isaack kuelekezwa namna ya kuondoa gari, cha kushangaza hata kabla ya kupata maelekezo ya namna ya kuondoa gari, Isaack alimwacha mwalimu wake kashikwa na butwaa pale alipongia kwenye lile gari aina ya LAND ROVER 109 na kuliwasha na kuanza kuzunguka pale uwanjani.
Pamoja na kuonesha uwoga, mwalimu alitahidi kuficha uwoga wake na kuonesha ishara ya kumtaka asimamishe gari, lakini Isaack hakufanya vile kama mwalimu wake alivyomuagiza. Aliendelea kuzunguka ule uwanja kwa ustadi kama vile dereva mpaka pale alipoona ametosheka ndipo akashika breki taratibu na kupangua gia mpaka pale alipofika namba moja na kusimamisha gari kwa ustadi wa hali ya juu. Mwalimu badala ya kukasirika na kumkemea Isaack, yeye alijikuta akipiga makofi mfululizo na kuwashangaza wanafunzi na wakufunzi waliokuwa pale uwanjani, kwani walimjua kwa ukali na msimamo wa kufuata sheria na maelekezo yake.
“Safi sana kijana, toka nianze kufundisha sijawahi kuona mtoto jasiri kama wewe, nilikuwa nataka damu changa kama hii ambayo ina uthubutu na kujiamini naona baada ya miaka kadhaa nitapata mrithi katika hii taaluma”. Mwalimu alimwambia Isaack wakati akishuka kutoka kwenye lile gari huku akimpa mkono.
“Haiwezekani kukaa tu darasani wiki mbili ndiyo uwe dereva mzuri namna hii, ulishawahi kuendesha gari kabla?”
“Hapana sijawahi kuendesha, ila huwa namwangalia sana baba na kaka wakati wanaendesha gari.” Alijibu Isaack wakati wakitembea na mwalimu wake kuelekea sehemu ya kubadilisha nguo kwa ajili ya kujiandaa tayari kuondoka kurudi nyumbani baada ya siku ile kuwa imeisha kwa namna ya pekee.
Siku ile kwa Isaack ilikuwa ya furaha sana kwani siku zote alitamani sana kukalia usukani ila alizuiwa na baba yake kwa kigezo kwamba umri wake bado ulikuwa hauruhusu. Alijiona kama ndoto yake imetimia kwa asilimia sabini kama siyo mia na kuahidi nafsi yake kwamba ataongeza bidii katika kujifunza zaidi ili aweze kuwa dereva mzuri kumshinda kaka yake ambaye alikataa kumfundisha kuendesha gari pale walipobaki wawili kwa kisingizio kwamba baba yao alishasema mpaka afikishe miaka 18.
Tokea ile siku, alijikuta akipenda shule na kuelekeza mawazo yake shule na hata kusahau juu ya mama yake ambaye toka aondoke ilishatimia mwezi mmoja. Alikuwa mchangamfu na mwenye furaha tofauti na siku za nyuma ambapo alikuwa ni kijana wa kujifungia tu ndani. Kutokana na furaha aliyokuwa nayo, alianza hata kushirikiana vizuri na jamaa zake pale ndani akiwemo dada Zaituni ambaye ndiye alikuwa kama mama kwa wakati wote toka mama yao aondoke kwani ndiye aliyehakikisha wanakula, kufua nguo na kuhakikisha usafi wa nyumba unafanyika.
Mzee Mbiru alifurahi sana kuona kijana wake akirudi katika hali ya furaha kwani ilimpa sana mawazo kuona watoto wake wakiwa na huzuni. Kitendo cha Isaack kwenda shule bila kusukumwa na mtu kilimfurahisha sana baba yake na kuanza kuwa karibu na mwanae kupanga maisha kama vile alikuwa na mtu mzima mwenzake.
“Mwalimu wako alinipigia simu leo mchana, anasema unafanya vizuri sana darasani.” Kama ukiendelea hivyo unaweza ukamaliza mapema kabla ya miaka miwili.” Mzee Mbiru alimwambia Isaack wakati wakiwa mezani wakipata chakula cha usiku.
“Kweli baba? Kumbe naweza kusoma chini ya miaka miwili! Sikuwa najua kabisa kama wanaofanya vizuri wanamaliza mapema. Kuanzia kesho nitazidisha bidii ili nisome muda mfupi nianze kazi…”.
“Mwanangu kila kitu kina wakati wake… kazi utafanya mpaka utachoka ila sasa ni muda wa kutengeneza maisha yako kwanza. Kufanya kazi siyo shida ila bado una umri mdogo ningependa uandae hiyo kazi yako ije kuwa na manufaa makubwa siyo unafanya kazi ya kukuingizia pesa za madafu… soma kwanza upate ujuzi wa kotosha hata ukija kuanza kazi basi iwe kazi ya kipato cha kutosha.”
“Sasa baba kwani si umesema mwalimu kasema nafanya vizuri na kama nikiendelea hivi nitasoma chini ya miaka miwili? Nikimaliza nataka leseni nianze kazi.” Mbiru hakutaka kumkatisha Isaack tamaa, alimtaka amalize kula na kwenda kulala mapema kwa ajili ya kuamka mapema asubuhi ili asichelewe chuo.
***
Mbiru alimaliza kula na kukaa pale sebuleni akisubiri kuangalia taarifa ya habari ya saa nne, kwani ya saa mbili ilishampita kutoka na kuchelewa kufika nyumbani kwa sababu ya foleni. Hivyo baada ya kumaliza kula aliamua kukaa pale ili aweze kuangalia yaliyojiri duniani na Tanzania kwa ujumla.
Alikuwa mwenye mawazo mengi juu ya mke wake ambaye toka aondoke, mwezi ulishakatika. Alifikiria cha kufanya ili kumrudisha mke wake lakini kutokana na jeuri aliyokuwa nayo, aliona kwenda kumuomba mkewe msamaha ni sawa na kujidhalilisha hivyo aliona bora kufa na tai shingoni.
“Hivi kweli mimi Mbiru na ndevu zangu zote nikampigie mwanamke magoti kumuomba msamaha? Haiwezekani hata kidogo si nitaonekana nimechanganyikiwa! Mwache tu akae huko akichoka atakuja mwenyewe.” Mzee Mbiru alikuwa akiwaza peke yake pale sebuleni, mara usingizi ulimpitia bila hata kuangalia taarifa ya habari aliyokuwa anaisubiri.
Ilikuwa majira ya saa 11:00 alfajiri, Isaack alikuwa akitoka kuelekea bafuni ili kujiandaa tayari kwenda chuo. Alishangaa kukuta runinga ikiongea wakati ule na kushangaa imekuwaje Zaituni anaangalia runinga asubuhi yote ile! Alishangaa kumkuta baba yake akiwa amelala fofofo katika sofa huku akiwa amevalia kaptura na fulana kama alivyokuwa jana yake wakati wanakula wote mezani. Isaack alisimama na kumwangalia baba yake na kujikuta huruma inamuingia, kwani alijua fika kwamba kwa usiku ule baba yake aligeuka chakula cha mbu pale sebuleni.
“Baba, baba…baba …amka kumekucha.” Isaack alimuamsha baba yake taratibu ili asimshtue. Mbiru aliamka na bila kusema chochote aliingia chumbani kwake na kujiandaa tayari ili kuondoka katika biashara zake lakini kwanza alimpitisha Isaack pale VETA na yeye kuendelea na safari. Siku ile ilikuwa mbaya sana kwa mzee Mbiru kwani alijisikia vibaya sana pale mwanae alipomkuta amelala sebuleni.
Tofauti na siku zingine ambapo Isaack huongea na baba yake wawapo njiani, siku ile kila mmoja alikuwa kimya njia nzima mpaka anashuka na kumuaga baba yake ambaye alimuambia akitoka ampigie simu, kwani kulikuwa na uwezekano wa kutoka mapema katika shughuli zake ili kama itawezekana ampitie ili waweze kurudi wote.
SURA YA SITA
Baada ya mwaka mmoja kumalizika, Isaack alikuwa tayari ni fundi mzuri wa umeme wa magari na pia dereva mzuri sana. Mwili mkubwa aliokuwa nao ulimsaidia na kumfanya aonekane mkubwa machoni pa watu wengi aliokutana naolakini ukweli ni kwamba ndiyo kwanza alikuwa na miaka 17 tu.
Kutokana na kujifunza kwake haraka, badala ya kusoma miaka miwili Isaack alisoma mwaka mmoja tu na kutunukiwa cheti daraja A katika fani ya udereva na ufundi umeme. Alifurahi sana kwani alijiona mwenye bahati ya pekee. Maisha yake yalibadilika sana na alijiona mtu mzima sasa siye yule aliyekuwa anamlilia mama yake wakati anaondoka. Mwalimu wake alimtaka aendelee kwa ngazi ya diploma ili aweze kuwa na elimu zaidi na kumudu ushindani wa kazi mtaani, lakini Isaack aligoma kabisa kwa kigezo kwamba tayari alishapata alichokitaka.
“Mwalimu, mimi shida yangu sana iliyonifanya mpaka kuja kusoma hapa VETA nilishakuambia ni kutaka kujua udereva, ila nakushukuru kwa juhudi zako nimeweza pia kuwa fundi mzuri. Hivyo mi naona hapa suala lililobaki na kutafuta tu leseni ili niweze kupata kazi kwa sababu nimeshakuwa dereva mzuri tu.”
“Sawa najua yote hayo maana ulishaniambia unataka tu kujua udereva, ila maisha ya siku hizi yana changamoto sana. Ili ushindane na soko la ajira lazima uwe na fani zaidi ya moja tena uwe na elimu ya kutosha ndiyo maana nakuambia chukua diploma kwa sababu huko mtaani wenye fani kama yako wako wengi sana, kitakachokufanya uwe na uhakika wa kazi ni cheti chako kwa sababu wengi wao wana cheti tu na kama ilivyo kwenye ajira zetu za kibongo hawaangalii uzoefu sana kikubwa na elimu… katika kutafuta kazi mtu wa diploma atakuwa na nafasi kubwa kuliko yule mwenye cheti. Kwanza bado wewe ni mdogo sana una harakia wapi? Tuliza akili usome kwanza. Mbona kama ni hela utazichoka mwenyewe?
Mwalimu alitumia muda mrefu kumshauri Isaack aweze kubadili mawazo yake na kuendelea na shule , lakini juhudi zake ziligonga mwamba kwani Isaack alisimamia msimamo wake ule ule kwamba hataki tena kusoma. Yeye alitaka tu kupata leseni ya udereva ili aweze kuendesha gari bila kuogopa sheria za nchi ambazo haziruhusu mtu chini ya miaka 18 kuendesha chombo chochote cha moto.
Ilishahitimu majira ya saa nane mchana, Isaack alimpigia baba yake kumjulisha kwamba alishatoka darasani na alikuwa akimsubiri yeye ili kama amemaliza shughuli zake aweze kumpitia ili warudi wote nyumbani. Alikuwa mwenye furaha sana tofauti na asubuhi yake kutokana na habari alizopewa na mwalimu wake, kwamba alikuwa amefanya vizuri katika mitihani yake ya vitendo hivyo kumfanya ahitimu masomo yake kabla ya muda uliokuwa umepangwa kuisha.
Mbiru hakuchukua muda mrefu sana kufika pale VETA, kwani alikuwa maeneo ya keko magorofani katika moja ya baa akipata chakula cha mchana. Hivyo alimalizia tu kula na kuwasha gari lake tayari kumpitia kijana wake, ambaye kwa siku za usoni wamekuwa marafiki wakubwa tofauti na zamani ambapo Isaack alikuwa mtoto wa kukaa na mama yake muda wote iwe jikoni iwe varandani, ila toka mama yao alipoondoka ukaribu wao uliongezeka sana. Mbiru alijua labda kwa sababu kijana wake alishafikia umri wa mtu mzima ndiyo maaana wamekua karibu.
“Umekula?” mzee Mbiru alimuuliza Isaack wakati akiondoa gari tayari kuanza safari ya kuelekea mitaa ya UBUNGO MSEWE ambapo ndipo makazi yake yalipo.
“Hapana baba, nitakula nyumbani. Niliona leo nimemaliza mapema nikaona bora nikale tu nyumbani … hata hivyo sina njaa sana nilikula mihogo ya kukaanga na juisi asubuhi.”
“Naona chuo kimekufanya kijana mzuri sana, kama ukiendelea hivi basi utakuwa na maendeleo sana baadae kwa sababu kila anayejituma hafi maskini.” Ukimaliza niambie unataka kufanya nini ila usiniambie masuala ya ubondia…”
“Nilitaka tukifika nyumbani ndiyo nikuambie … mwalimu amesema ukipata muda jumatatu uende ila amenipa matokeo yangu. Amesema kutokana na maendeleo mazuri na kujifunza kwangu haraka, naweza kuishia hapa na nikapata cheti sawa na wenzangu waliosoma miaka miwili.”
Mbiru alishangaa na taarifa za mwanae kwani hakujua kama alikuwa na uwezo mkubwa kiasi kile. Kwanza alijua labda alikuwa akimdanganya kwa kisingizio cha kuacha ufundi ila aliamini kutokana na ile barua aliyompatia.
“Hebu ifungue niisome maana nyie watoto hamchelewi… inawezekanaje usome miezi kumi na mbili kozi ya miezi 18? Kwa akili gani haswa ulizonazo wewe?”
Isaack aliifungua ile bahasha na kumpatia baba yake ambae alikuwa akiendesha gari, na tayari walishafika kwenye mataa ya buguruni wakisubiria kuruhusiwa. Aliisoma ile ripoti na kujihakikishia kwamba kila kitu alichosema mwanae ni ukweli. Alifurahi sana kwani alilmdharau mwanae kwa sababu toka alivyokuwa shule ya msingi alikuwa siyo mpenda shule.
Taa ya kijani iliwaka kuashiria kwamba waliruhusiwa kuondoka. Mbiru alikanyaga mafuta kunyoosha na barabara ya TABATA ili akatokee ubungo maji. Njiani Isaack alimwambia baba yake lengo lake la kupata leseni ili aweze kuwa dereva kamili, na baba yake bila hiana alimhaidi kuwa angemfanyia mpango kwa rafiki yake ambaye alikuwa traffic pale kituo cha osterbay.
***
Mnamo saa kumi kasoro jioni, mzee Mbiru na kijana wake Isaack walikuwa tayari wanaingia nyumbani kwao mitaa ya KONA ambapo mzee Mbiru aliegesha gari na kuondoka kuelekea LATEMBA BAR bila hata kuingia ndani, kwani alishaanza kunywa bia tokea akisubiri simu ya Isaack kule keko, hivyo kitendo cha yeye kuingia ndani ni sawa na kuzima moto ambao ulishawashwa.
Isaack yeye kwa upande wake aliingia ndani na kujitupa kitandani, kama ilivyo kawaida yake alipenda sana kulala. Aliutandika usingizi kuja kushtuka tayari ilishajiri majira ya saa kumi na mbili jioni, alichokifanya ni kuingia bafuni kuoga na kuondoka kuelekea uwanja wa mpira wa jirani, ambapo vijana wengi wa eneo lile walipenda kukutana jioni kubadilishana mawazo na kupata dawa kwa wale watumiaji.
Kama kawaida yake, Isaack alijitenga na kukaa peke yake akisikiliza mziki kwenye simu yake kwa kutumia headphone zake hivyo kumnyima fursa ya kujichanganya na mazungumzo ya wenzake ambao walikuwa wakiongea na kucheka pamoja baada ya mazoezi ya mpira.
“oya niambie… inakuwaje mwanangu? Kitambo sana baharia wangu sijui umefichwa wapi…sijakuona toka ile mechi ya siku ile kule baruti ulisafiri nini ?”
Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Evans alikuwa akimsemesha Isaack, ambaye alivua foni sikio moja ili asalimiane na rafiki yake ambaye walisoma wote pale MLIMANI kwani wote walikuwa kati ya watega shule. Kama wasemavyo wahenga kwamba ndege wafananao huruka pamoja ni kweli kabisa kwani kutoa Timo, aliyefuatia kwa marafiki wa Isaack ni Evans ambaye walitoroka wote na kuzurura mpaka pale muda wa kurudi nyumbani ulipowadia.
Evans hakuweza kumaliza hata darasa la saba kwa sababu ya kukamatwa na mwalimu wa nidhamu akimgeuza kinyume na maumbile mwanafunzi mwenzake wa darasa la tano hivyo kufukuzwa shule na ndiyo ukawa mwisho wa elimu yake.
Siku ile pale uwanjani alikuwa na kundi kubwa la vijana waliomzidi umri hata mara mbili. Walikuwa na misokoto ya bangi kila mmoja akionesha uhodari wake katika kujaza moshi mapafuni na kutoa nje kupitia puani.
“Test mwanangu utoe nishai.” Evans alikuwa akimpatia Isaack msokoto wa bangi ili ajaribu kuvuta lakini Isaack alimkatalia na kumwambia hatumii.
“Acha ushamba mwanangu, ushakua mkubwa wewe toa nishai mdomo zege ukutoke. Unafikiri sijui kama mpaka leo hujawahi kutongoza? Unapitwa mwanangu maisha yenyewe mafupi kula ujana bado mapema.”
“Ah… unazingua mwanangu, unataka mpaka nikuchapie dadako ndo uniheshimu au? Isaack alinyanyuka kwa hasira pale na kuanza kuondoka akaamwacha Evans akiendelea kuongea maneno ambayo yaliwaacha midomo wazi vijana ambao walikuwa pale uwanjani wakivuta bangi.
“We nini unajifanya mtakatifu wakati chakula tu? Au umeacha siku hizi… eti unichapie dada yangu! Wakati na wewe unachapwa labda uje kwangu nikuchape kwanza halafu ndiyo na wewe ukamchape sister angu. Umesahau chipsi za bure kwa mudy? We nini bwana tena nikikuona umemsogelea dada yangu ujue nakuacha uchi… mtaa mzima utajua ulichokuwa ukifanyiwa na mudy muuza chipsi. Evans alikuwa akiongea kwa nguvu lakini aliyekuwa akiongea nae alikuwa akitokomea katika kigiza ambacho kilikuwa kishaanza kukolea na kuwaficha watenda maovu waliokuwa uwanjani wakivuta bangi bila woga wowote.
SURA YA SABA
Isaack alirudi nyumbani na moja kwa moja kama kawaida yake alielekea chumbani kwake ambako alijifungia na kuanza kulia. Alikumbuka maneno ya Evans na kujikuta akilia mfululizo. Alikumbuka uovu aliofanyiwa na mwalimu wake wa hesabu ambaye alijifanya anataka kumsaidia hesabu kumbe alikuwa na lengo lake.
Ilikuwa siku ya ijumaa asubuhi majira ya saa nne, miaka mine iliyopita ambapo mwalimu Koleo alimuita Isaack ofisini kwakwe kwani alikuwa amefeli sana hesabu.
“Wewe ndiye Isaack Mbiru?”
“Ndiyo mwalimu, shkamoo mwalimu”.
“Marhaba, keti… nimekuita hapa kwa sababu naona matokeo yako ya hisabati ni mabovu sana, una shida gani? Naomba kuanzia kesho jumamosi uwe unakuja tuition na wenzako ili niwafundishe sawa? Ukirudi nyumbani leo uwaambie wazazi wako mwalimu mkuu msaidizi amesema unatakiwa uwe unakuja shule jumamosi ili kupata masomo ya ziada kwa ajili ya kujiandaa na mitihani ya darasa la nne.sawa?”
“Sawa mwalimu, nitakuja” Isaack alimwambia mwalimu wake na kunyanyuka kutoka ofisini akimwacha mwalimu akimkodolea macho. Aliporudi nyumbani jioni aliwaambia wazazi wake nao wakakubali wazo la mwalimu. Walimruhusu Isaack kuanza kwenda shule jumamosi lakini walichokosea hawakufuatilia kama kweli mtoto alienda shule ama laa.
Ilikuwa jumamosi asubuhi ya saa tatu muda ambao, ndiyo Isaack aliambiwa afike pale shuleni Mlimani. Alijua watakuwa wanafunzi wengi ila cha kushangaza hawakufika hata kumi. Aliingia darasani ambako alimkuta mwalimu alishaanza kufundisha.
“Tutaonana jumatatu, ila Isaack nifuate ofisini.”
Isaack alimfuata mwalimu ofisini na alipoingia tu mwalimu alifunga mlango na kuanza kumpapasa na kisha kumvua kaptura yake. Isaack ambaye alikuwa darasa la nne tu alifanyiwa kitendo ambacho kilimfanya aichuke kabisa shule. Hata aliporudi nyumbani hakuweza kusema chochote kwa wazazi wake kwani mwalimu alimtishia asimwambie mtu chochote kilichotokea, na endapo angesema basi angekula bakora. Kutokana na umri mdogo aliokuwa nao Isaack alikaa kimya ila aliona suluhisho la mambo yote ni kutokwenda shule, hivyo alianza kutoka nyumbani na nguo mbili. Alivaa nguo za shule kama kawaida, lakini njiani alivua na kuvaa nguo za nyumbani na kuingia mtaani, kwa lengo la kumkwepa mwalimu katili bila kujua hata mtaani walikuwepo watu kama walimu.
Siku moja katika kuzurura kwake, njaa ilimuuma na ndipo wenzie wakashauri waende kwa Mudy muuza chipsi wakamsaidiea kumenya viazi kwa ujira ambao walilipwa chipsi. Baada ya kumaliza kazi ya kumenya viazi walipewa chipsi lakini Isaack aliwekewa mshikaki na kununuliwa soda. Toka siku ile Isaack akawa anaenda kushinda kwa Mudy kwa kujua kwamba atakula na kunywa mpaka muda wa kurudi nyumbani ufike.
Isaack alimzoea sana Mudy na kumuona kama kaka yake, hivyo ilifika kipindi wakaenda hadi nyumbani kwa Mudy maeneo ya Mpakani. Huko ndiko Mudy alimgeuza Isaack chakula chake mpaka ilifika mahali Isaack akazoea na kuona kama ni sehemu ya maisha yake. Ilifikia kipindi Isaack akawa anahitaji kukunwa na hapa ndipo haswa walipojuana na rafiki yake Evans ambaye tabia yake ilikuwa kuwageuza watoto wenzake.
Evans na Isaack walizoeana sana kwa sababu kwanza wote walikuwa watoro wa shule, na walitumia muda mwingi kukaa mitaroni ambako ndiko walikofanyia uchafu wao.
Isaack alikuwa chumbani akiyakumbuka yote aliyopitia katika umri mdogo, mambo ambayo hakutaka kabisa yajirudie kichwani kwake lakini kutokana na kujichanganya mara moja aliona kama dunia inaenda kumuacha uchi muda si mrefu. Alilia sana na kutamani ile iwe ndoto lakini haikuwa ndoto bali kweli tupu. Kweli ambayo ilimtesa kadiri miaka ilivyozidi kwenda.
Alishtushwa na hodi iliyokuwa ikigongwa mlangoni kwake na dada yake Zaituni, aliyemtaka atoke akale chakula cha usiku lakini alichoweza kumjibu ni kwamba ameshiba. Zaituni aliendelea kugonga ili afunguliwe mlango na alipoona haufunguliwi aliamua kufungua na kuingia ndani, ambako alimkuta Isaack akilia huku macho yamemevimba haswa.
“Vipi unaumwa? Mbona macho mekundu unalia nini!”
Isaack hakuweza kujibu chochote, alijikuta akimkumbatia Zaituni na kuanza kulia kama mtoto.
“Kwani una nini? Sijawahi kukuona katika hii hali… ngoja nikampigie baba aje akupeleke hospit…”. Kabla hata Zaituni hajamalizia kusema neno hospitali, Isaack alimdaka midomo yake na kujikuta akimla denda. Zaituni alishikwa na butwaa asijue cha kufanya na mwisho alianza kutoa ushirikiano na wote wakajikuta katika ulimwengu wa mahaba mazito yalitochipuka ghafla na kuamsha cheche katika miili yao michanga iliyowaka kama moto wa kifuu.
Si Isaack wala Zaituni aliyewahi kupenda hapo awali, wSote walikuwa bikra kwa aina yake. Zaituni alikuwa bikra kwani hakuwahi kabisa kukutana kimwili na mwanaume na Isaack alikuwa bikra kwa maana hakuwahi kumuingilia mwanamke lakini yeye alishawahi kuingiliwa kinyume na maumbile na hata kumfanya kujiona kama mwanamke japo alijitahidi kuficha ile hali ili watu wasijue.
Kwa mara ya kwanza Isaack alimuingilia mwanamke, jambo ambalo hakuwahi kuliwaza katika maisha yake. Yeye aliwaza kuwa na maisha mazuri ili aweze kuishi maisha mazuri. Kwanza hakujiamini kama angeweza kumuingilia mwanamke kwa sababu kitendo cha yeye kuingiliwa kinyume na maumbile kilimuathiri na kujiona mdhaifu na mwenye aibu mbele ya wanawake ambao pamoja na umri mdogo aliokuwa nao wa miaka 17, tayari kuna wadada walishaanza kumzengea na wengine kudiriki hata kumtongoza bila woga.
Kwa Zaituni ilikuwa kama kuokota dodo chini ya mpera, kwani ni muda mrefu alikuwa akimtamani Isaack ila alishindwa kumwambia. Alifanya kila njia ya kumjali lakini Isaack alikuwa kama kipofu asiyeona.
Alikuwa amelala juu ya kifua cha Isaack ambaye alikuwa kalala fofofo kwa uchovu wa kupanda katika kilele kirefu cha mlima usiokuwa na jina. Zaituni ambaye alikuwa na maumivu kiasi alijizoa kutoka pale kitandani, na kuvaa nguo zake na kutoka nje ya chumba cha Isaack kabla mzee Mbiru hajarudi kwani ilikuwa ndiyo mida yake ya kurudi.
Zaituni alikuwa binti mdogo lakini aliyefundwa akafundika, hivyo alichokifanya kabla ya kutoka alitoa shuka ambalo lilikuwa na zawadi aliyokuwa ameitunza miaka yote kwa ajili ya mume atakayemuoa, lakini zawadi ile aliitoa bila kutarajia kwa mtu ambaye hata hakujua kama atakuwa mume wake. Zawadi ambayo kwao ni kosa kubwa kama utaolewa bila kuwa nayo.
***
Ilikuwa saa saba usiku, Isaack alishtuka kutoka usingizini na kujikuta akiwa uchi kama alivyozaliwa. Alikuwa na shuka lililokuwa limemfunika nusu tu ya mwili wake. Alirudisha kumbukumbu zake nyuma na ndipo akakumbuka mechi aliyoicheza muda uliopita. Hakujua alitoa wapi kule kujiamini. Alijiona mshindi sana kwani hakuwahi kufikiria kupanda kifuani kwa mwanamke, ila siku ile alipanda tena alikuwa yeye ndiyo mzinduzi. Alihofia kesho yake angemuangaliaje dada yake wa kazi usoni, lakini upande mwingine ilikuja sauti ya kujipa moyo ikimuambia “wewe ni mwanaume wa shoka , huna haja ya kuogopa”.
Alikuwa na njaa sana kama vile hajala mwaka mzima, hivyo alijivuta kutoka pale kitandani na kutoka kuelekea sebuleni, ili akaangalie chochote cha kutia mdomoni arudi kulala. Alifunua hotpot na kupakua chakula ambacho bado dada hakuwa ametoa kuhifadhi katika jokofu kwa sababu bado baba yao alikuwa hajarudi.
Isaack alikula na kurudi chumbani ambako aliuchapa usingizi kama vile mwanajeshi aliyetoka vitani. Alikuja kushtuka kutoka usingizini kutokana na kugongewa na baba yake mida ya saa sita mchana siku iliyofuatia.
“Vipi aisee, mbona unalala kama boss? Una raha gani mpaka ulale namna hii… hebu fanya haraka jiandae twende shamba… niliwaahidi walinzi nitaenda leo kuwapelekea chakula walinipigia jana hawana unga wala maharage.”
Isaack hakujibu chochote, alitoka na kwenda kuoga na baada ya dakika kumi alikuwa tayari kashajiandaa. Alipita na kumkuta Zaituni anaandaa chakula mezani, wote waliangaliana kwa jicho la wizi bila hata kupeana salamu. Mzee Mbiru alikuwa tayari alishakaa mezani tayari kwa kupata chakula cha mchana ili aondoke kwenda shamba.
Siku zote huwa Zaituni anakaa mezani na kula pamoja lakini siku ile cha kushangaza aliwaacha Isaack na baba yake mezani wakila na yeye kwenda kukaa jikoni akila peke yake jambo ambalo halikuwa la kawaida. Mzee Mbiru alishangaa lakini hakutaka kumuuliza kwani alishachelewa alitaka ale haraka aondoke zake shamba ili awahi kurudi.
SURA YA NANE
Walisema wahenga kwamba ukilamba asali lazima uchonge mzinga. Isaack na Zaituni hawakuishia usiku ule bali sasa waliamua kuhalalisha mahusiano yao na kuwa kama mke na mume. Walitumia vema nafasi waliyoipata pale nyumbani. Muda wote ambao walibaki peke yao wao waliutumia chumbani wakifurahia penzi pevu lilichipua mioyoni mwao. Walifurahia maisha yale na kuwafanya hata wamsahau mama yao.
Isaack hakusikia wala kuona mbele ya Zaituni, alijiona mwenye bahati ya pekee kumpata mwanamke wa bure bure tena ndani kwao bila gharama yoyote. Ilimfanya awe mtu wa kujifungia ndani na kufanya mapenzi bila hata kuchoka.
Haikuwa rahisi kwa baba yake kujua wala kuhisi kama kijana wake anamchukua dada wa kazi, kwani toka zamani alikuwa ni mtu wa kujifungia ndani hivyo alijua ni tabia yake bila kujua kama alikuwa mtawaji. Siku zilizidi kwena na Isaack alisharizika kabisa na yale maisha ya kukaa ndani akimsubiri dada amalize kazi na kumfuata chumbani kwake kwa ajili ya kula tunda la mti wa kati, tunda ambalo hakuwahi kulionja hapo awali hivyo lilimzuzua na kumfanya asifikirie kufanya chochote. Hata lile wazo la kutaka leseni lilishapotea akilini mwake, yeye akili yake iliwaza ngono tu. Kuna kipindi alijilaumu kwa kuchelewa kuanza kwani alijiona aliyekosa uhondo.
“Hivi kumbe wanavyosema wakubwa wanafaidi ni kweli? Sijui nilikuwa wapi siku zote…”. Alijiwazia Isaack baada ya kupiga goli la fasta bafuni pale alipomfuata Zaituni bafuni wakati anaoga.
“Isaack naona tuwe makini baba asijue maana itakuwa mwisho wangu wa kukaa hapa. Naomba kama itawezekana uwe mvumilivu, uwe unasubiri mpaka nije chumbani kwako usiku au hata wewe unaweza kuja chumbani kwangu ila mambo ya kunifuata hadi bafuni ipo siku tutakamatwa. Au unataka kunikosa kabisa? We mwenyewe unajua jinsi baba yako mkali naona atanipakia usiku huo huo.”
“Usijali baby dingi hawezi kujua mtu mwenyewe kila akirudi yuko tungi, na akirudi ananyoosha hadi chumbani kwake… kwanza hatumii bafu letu akija tu mi nikimsikia natoka fasta… njoo bwana nipe mambo nifaidi mimi… we ndo mke wangu na mimi ndiyo faza house… unaogopa nini, hata akijua hawezi kukufukuza”. Isaack alijigamba huku akimvuta Zaituni karibu yake na kumgeza kuelekea ukuta ambapo alimuinamisha na kuanza safari ya kupanda mlima kwa staili ya mbwa.
Zaituni alishindwa kujizuia na kujikuta akiimba sauti ya tatu iliyopangiliwa vema jambo lililomuongezea munkari Isaack na kujikuta akijituma kama aliye ahidiwa zawadi nono katika mashindano fulani.
***
Nje ya nyumba ya akina Isaack kulikuwa na fremu za maduka ambayo kuna biashara zilikuwa zikiendelea. Miongoni mwa biashara zilizokuwepo ni mashuka mazuri ya kudarizi yaliyokuwa yakishonwa kwa ufundi mkubwa na dada mmoja aliyejulikana kwa jina la Elifosia, ambaye pamoja na kushona pia alifundisha wanafunzi wapatao watano ambao waliingia kwa kupokezana. Wengine walifika asubuhi na wengine waliingia mchana na kutoka usiku saa mbili.
Toka afungue mahali pale miezi kama sita iliyopita, Elifosia alijikuta akivutiwa sana na Isaack lakini aliona aibu angewezaje kumwambia kijana mdogo namna ile kwamba anampenda? Kama alimzidi miaka michache basi haikuwa chini ya miaka kumi. Hivyo alichokifanya Elifosia ni kumwita tu kwa kigezo cha kumtuma chochote ilimradi tu amuone roho yake iridhike. Isaack hakuwa anajua lolote kuhusu yeye kupendwa na yule dada ambaye yeye alimwamkia kama dada yake, hakujua kabisa kama alikuwa akiutesa moyo wa yule dada.
Ilikuwa siku ya jumapili, siku ambayo Elifosia hufungua peke yake baada ya kutoka kanisani kwani wanafunzi wake wote hupumzika. Elifosia aliamua kutumia nafasi ile kujifanya mpweke hivyo alikuwa akimuita Isaack ili ampe company pale dukani. Isaack kwa upande wake alifurahia kwani hakuwa na pa kwenda kwa sababu aliacha kwenda uwanjani toka siku Evans alipomtania na kumkumbusha mambo ya zamani ambayo kwa upande wake hakutaka hata kuyakumbuka kwa sababu ni kati ya mambo yanayomuumiza na kumtia simanzi katika maisha yake, hivyo kama hakuwa ndani akiangalia sinema au kucheza mchezo wa kwenye simu, yeye alipenda kukaa dukani kwa dada Elly kama walivyopenda kumuita wakiongea hili na lile ilimradi masaa yaende ili arudi ndani kutoa dozi kwa dada yake wa kazi, ambaye alishakuwa mke wake wa siri.
Siku ile dada Elly alishaahidi kujitoa ufahamu na kumwambia Isaack ni kwa namna gani aliutesa moyo wake. Ilikuwa mida ya saa sita mchana dada Elly alikuwa kashafungua duka lake na alikuwa akifanya usafi kibarazani kwake. Alipomaliza alifanya kama anavyofanya siku zote alichukua simu na kumtumia ujumbe mfupi Isaack kumuuliza kama yupo.
Elifosia : Isaack hujambo mdg wangu?
Isaack : sijambo C6, heshima yako.
Elifosia : unafanya nini? Njoo bhana unipe company nipo alone, au una kazi?
Isaack: naja ila nina hamu na kitimoto leo, fanya mishe basi nikafuate…
Elifosia : hayo mambo madogo sana, labda useme kitu kingine my, njoo ukachukue,
Mi mwenyewe nina ubao kinoma toka tulipokula chips jana usiku.
Isaack : pa1 nakuja chap, si unajua sirembi kwenye mdudu? Fasta najimwagia maji nakuja.
Baada ya dakika kama kumi Isaack alikuwa tayari, wakati akitoka nje ya chumba chake alikutana na Zaituni ambaye nae alikuwa akienda ndani kwake wakakutana kwenye varanda.
Zaituni : Mbona umeulamba unaenda wapi hata kuniaga?
Isaack : Nipo hapo nje kwa dada Elly ameniita, si unajua leo yuko peke yake? Ameniomba
Nikamnunulie chakula. Usinihesabie ugali nitakula kwa dada Elly.
Zaituni : Mh we na huyo dada Elly wako siwaelewi… angalia usinase maana siku hizi wamama
Wanapenda viben 10… unaweza kukuta anakupenda anashindwa tu kukuambia.
Isaack : Jiangalie kauli zako wewe, au kutoka na wewe ndo unajifanya ushakuwa mke wangu au
Mama yangu? Usisahau nafasi yako wewe ni mfanyakazi na huwezi kunipangia cha
Kufanya…nipishe nipite bhana.
Zaituni alibakia kashikwa na butwaa kwa yale majibu ya Isaack, kwani hakutarajia kujibiwa vile. Toka aanze kuishi katika nyumba ile hakuwahi kujibiwa kwa dharau namna ile. Alihisi wivu sana moyoni mwake, kwani mapenzi aliyokuwa nayo kwa Isaack hayakuweza kujificha tena. Alitamani kuwa na Isaack muda wote na hata alipotoka alitaka kuagwa, lakini Isaack aliaga pale alipojisikia kufanya hivyo jambo ambalo lilimkosesha raha sana.
Kitendo cha Isaack kuwa na mahusiano na Zaituni kilimfanya kuwa mwenye kujiamini na kujiona mwanaume wa shoka, kwani hapo awali alikuwa mwenye kuogopa wanawake kwa kuhofia labda asingeweza kufanya chochote. Kuna wakati hakujua alikuwa anahitaji mwanaume au mwanamke. Alikuwa akipata hisia za kutaka mwanaume wa kumwingilia alifanya mazoezi sana ili kuipinga ile hali. Ni kweli mazoezi yalimsaidia sana ila kuanzia rafiki yake amtolee maneno yale mbele za watu, aliona hata uwanjani siyo sehemu ya kwenda tena na ndipo alipoamua kuanza kufanya mazoezi katika gym pale BAHAMA MAMA mkabala na sheli ya BP.
****
“Mbona umekawia sana kuja? Umezidi kuwa mtoto mayai… yani muda wote nikikutafuta we umelala. Punguza kulala bhana.” Dada Elly alikuwa akimtania Isaack baada ya kufika pale dukani kwake.
“Sikuwa nimelala sister, amenichelewesha da Zai naona anataka kunipangia nianze kumuaga kila ninapoenda kama vile amekua maza angu.”
“Hata hivyo ana haki ya kuagwa, kwa sa hivi yule ni kama mama yako kwa sababu anakupikia, anafua na kuwafanyia usafi… siyo vibaya ukimuaga ili hata unapoenda ukipata tatizo aweze kujua cha kumwambia baba yenu pindi atakapouliza.”
“Ahhhhhhh amezidi bwana, sasa ina maana hata nikienda msalani niage? Hebu nipe bana hela niende mie nikachukue nyama tuje kula kwanza nishasikia njaa”.
Dada Elly alimpatia Isaack pesa ya kununua kitimoto nae akatoka kuelekea LATEMBA BAR, ambayo ndiyo ilikuwa sehemu maarufu kwa kutengeneza nyama nzuri. Huku nyuma Elifosia alikuwa akiwaza namna ya kumuingia Isaack mpaka amuelewe. Aliona kuwa siku ile ilikuwa siku ya pekee kwani alikuwa peke yake na aliona atumie upenyo ule kwani Isaack alikuwa kashavurugwa ndani kwao hivyo alijua angekaa nae mahali pale muda mrefu.
Hakutaka kabisa kupoteza nafasi ile, alishajitoa muhanga na kusema liwalo na liwe. “ wanasema mtoto kwani nimemzaa? Hata kadi yake ya kliniki sina naanzaje kuwa mama yake… mtoto ni yule wa kumzaa mwenyewe wa mwenzio mkubwa mwenzako” Elifosia aliwaza peke yake na mwisho aliamua kufunguka kwa Isaack kuhusu hisia alizonazo juu yake.
Alishajua udhaifu wa Isaack kwamba ni kijana aliyependa kula bata kama vijana wa mjini walivyopenda kusema, hivyo alijua kwa kutumia pesa yake lazima tu angemnasa na kumuingiza mtegoni. “Huyu nikishampata siku moja tu najua ndo itakuwa basi nimejiomilikisha jumla kwa sababu kwanza nahisi hana girlfriend, angekuwa nae asingekuwa wa kukaa ndani kila siku namna hii. Au ukute mtoto si riziki? Maana kwa uzuri na umbo alonalo haiwezekani awe peke yake… labda kama … ila hawezi kuwa siyo riziki, labda tu hataki kuwa na mahusiano ndo maana anafanya tu mazoezi”.
Elifosia alikuwa akiwaza na kuwazua juu ya kijana mdogo aliyeuteka moyo wake kwa kipindi kifupi, toka aachane na mume wake ambaye alikuwa amezaa nae mtoto mmoja mwaka mmoja uliopita, hakuwahi kupenda wala kuwa kwenye mahusiano na aliahidi nafsi yake endapo atakuja kupenda tena, basi angependa kuwa na mtu mwenye muonekano mzuri na kwenye hili kilio chake kilisikika, kwani haikuchukua muda kumpenda kijana ambaye alikuwa na sifa zote alizozihitaji. Siku ya kwanza tu kumtia machoni alipata hali ya ajabu. Alihisi kama kupigwa shoti mwili mzima na katika kipindi kirefu tangu afanye mapenzi, Elifosia alisikia damu ikichemka akitamani kufanya mapenzi na kijana mdogo aliyejaliwa kila kitu alichokihitaji kwa mwanaume.
Kwanza alikuwa kijana mrefu mwenye umbo linalovutia japo hakuwa anajua thamani ya umbo lake. Alikuwa na kifua kilichojazia vema hata kuwababaisha wasichana waliojua matumizi ya kifua kwa sababu siyo wanawake wote wajuao matumizi ya kifua kama kile. Umbo kubwa alilokuwa nalo lilificha umri mdogo aliokuwa nao, kitu pekee kilichoonesha umri wake ni sura nzuri ya kitoto aliyokuwa nayo, sura aliyoipata kwa mama yake ambaye pamoja na uzuri wake bado aligombana na baba yake na hata kuondoka na kumwacha na baba yake pamoja na msichana wa kazi ambaye hakuwa tena msichana wa kazi, kwani walishaanza mahusiano waliyoyafanya kwa siri kubwa bila baba yao kujua.
SURA YA TISA
Isaack na dada Elly kama wengi walivyopenda kumwita, walikuwa wamekaa ofisini wakila kitimoto huku wakishushia taratibu na soda baridi, huku wakiongea hili na lile ilimradi tu chakula kiweze kushuka. Elifosia alikuwa pale kimwili lakini kimawazo hakuwepo kabisa kwani alikuwa akitalii kwenye mwili wa Isaack ambaye wala hakuwa na habari ya kilichoendelea katika mawazo ya dada Elly.
“Da Elly mbona hauli? We si ulisema una njaa! Naona kama nakula peke yangu… unasemaga ikipoa haiwi tamu kula sasa kabla hakijapoa.”
“Mbona nakula? We kula mimi si unajua nakula haraka haraka? Hivyo nawahi pia kushiba… kula wewe mtoto ukue.”
“Kwa hiyo unaona mi mtoto au?
“Hapana sijakuita mtoto ila si unajua mwili haujengwi kwa tofali? Kula ujenge shavu.” Elifosia na Isaack walikuwa wakitaniana na kuwafanya wote kufurahia siku yao. Elifosia aliona ile ilikuwa nafasi ya pekee kwake kuonesha hisia zake japo bado alihofia vile Isaack angepokea.Kimya kilipita bila kusemezana, Isaack alikuwa anakula huku Elifosia akimuangalia kwa jicho la kuibia.
“Hivi ulishawahi kwenda mziki? Mimi napenda sana mziki lakini siku hizi sina hata company ya kwenda nayo”. Elifosia alivunja ukimya.
“Napenda ila sijawahi kwenda si unajua mzee anazingua? Yani hataki kabisa mambo ya kuchelewa home, saa moja tu anataka uwe ndani sembuse kutoka night?” ila ipo siku nitamchezea mchezo. Mi sa hivi nishakua ila ananiona tu kama mtoto”.
Kama vile alikuwa mwenye kusubiri ile kauli, Elifosia alipata upenyo wa kumshawishi Isaack ili watoke wote siku ile kwa kigezo kwamba alikuwa na hamu ya mziki lakini ukweli ni kwamba alikuwa na matamanio yake ya mwili. Alijua kama angetoka nae angepata nafasi nzuri ya kumsoma na ingekuwa rahisi kwake kumlainisha mpaka awe nae na kama ingeshindikana basi lakini ilimradi alitaka tu kutupa ndoano yake.
“Sawa da Elly nitakupa company leo ila tusiende club ya mbali sana ili iwe rahisi mimi kurudi home. Nitampanga da Zaituni halafu nitatoka ila kabla ya asubuhi itabidi niwe nimerudi ili mshua akigonga asubuhi anikute ndani la sivyo itakuwa msala.”
“Usijali, kwanza siamini kama kweli leo naenda na wewe mziki. usiwaze kuhusu wapi tutaenda ilimradi tu umekubali kunipa company we muda wowote ukitaka kurudi utaniambia mi nitakuchukulia bajaj itakurudisha mpaka nyumbani.” Elifosia aliona kama tayari mtego wake umefanya kazi. Alikuwa mwenye furaha kama vile tayari alishampata Isaack, alitamani kupeleka saa mbele ili jioni ifike aweze kufunga ofisi ili waweze kuwa mahali wao wawili tu.
“Ahsante da Elly nimeshiba kweli, ngoja basi nikalale kidogo ili baadae nisisinzie… si unajua nimezoea kulala mapema?
“Nakujua mtoto wa mama, punguza kudeka yani we ukila tu unaenda kulala. Haya bwana ila nakutegemea usije kuniangusha. Au kama vipi ulale halafu wakati nafunga nikushtue tuondoke wote kwangu ili nikajiandae tutoke pamoja.” Elifosia alitupa ndoano nyingine na kufanikiwa. Isaack alikubali wazo la da Elly na kuelekea ndani kulala kwa miadi kwamba angeamshwa saa kumi na moja jioni, ili ajiandae waondoke wote kuelekea maeneo ya MBEZI TEMBONI ambako ndiyo yalikuwa makazi yake ili akajiandae tayari kwa kutoka wakakae mahali wakisubiri mida ya wanga ili waende mziki.
Elifosia hakuamini macho yake, alijiona mwenye bahati kwani hata kukubaliwa kutoka tu kwake tayari alijiona kama tayari kashampata kijana ambaye alikuwa akiuendesha moyo wake kwa mwendo wa 4G. Hata kufungua ofisi jumapili ilikuwa tu kisingizio ili aweze kumuona Isaack kwani kwake siku kupita bila kumtia machoni, ni kosa la jinai hivyo akamlazimu kufungua ofisi ili apate muda wa kuonana naye japo Isaack hakuwa na habari kwamba chanzo ni yeye.
***
Ndani Zaituni alikuwa amekaa sebuleni akiangalia marudio ya DIRA, Isaack alipitiliza na kuingia chumbani kwake kama kawaida yake akajitupa kitandani. Zaituni alikaa kama dakika tano akaamua kumfuata kwa sababu wakati anatoka walipishana kauli na alihisi alimuudhi hivyo alitaka akamuombe msamaha ili waendelee na mapenzi yao ambayo yalishakolea. Zaituni alikuwa na wasiwasi na hakutaka kabisa kumkosa Isaac na alikuwa tayari kufanya chochote ilimradi tu amuone akiwa na furaha. “Vipi mbona umepita kama hujaniona? Ina maana ndo umenikasirikia au! Mbona unapenda kukasirika kwa vitu vidogo sana? Mi nilikuwa tu nakutania bwana usinikasirikie… si unajua sipendi kukuona ukiwa huna raha?” Alisema Zaituni baada ya kuingia ndani kwa Isaack na kukaa kitandani ambako alikuwa amejilaza.
“Wala sijakasirika ila sipendi kupangiwa, yani mshua anipangie na wewe unipangie sasa mi nitakuwa naishi maisha gani?” Zaituni alishavua nguo zote na kubaki mtupu kama alivyozaliwa. Matiti yake yaliyochomoza kama michongoma kifuani mwake, yalimfanya Isaack ashindwe kujizuia na kujikuta akimvuta karibu na kuanza kutembea na ulimi mwili mzima.
Zaituni alikuwa akitoa miguno ya aina yake, hakuwa na hiana katika uwanja wa sita kwa sita. Alishakuwa fundi na hakuwa na woga kama mwanzo, alimpa Isaack tunda lake lote bila choyo chochote. Walisafiri pamoja katika ulimwengu wa maraha na walipofika walifika pamoja wakiwa hoi bin taabani.
“Sasa leo kuna mahali nataka kwenda baadae na nitachelewa kurudi hivyo kama mshua ataingia room na kunikosa itabidi unisaidie kumpanga sawa?” Isaack alimwambia Zaituni wakati akiwa anamchezea chuchu zake zilizosimama kama miba. Hakutaka kumuambia ukweli kama alipanga kwenda mziki na da Elly kwani tayari alishaonesha kutopenda pale anapokuwa nae, hivyo aliona bora adanganye tu kwamba alikuwa anaenda kwenye birthday party ya rafiki yake.
“Sasa mimi nitamwambiaje? Unajua cha kwanza baba akija anafungua mlango wako kuangalia kama upo ndani. Labda ufunge mlango kwa nje nibaki na ufunguo ye huwa akiona mlango umefungwa haangaiki kugonga anajua tu umelala na hutaki kusumbuliwa. We utafunga mlango halafu acha taa ikiwaka. Ila angalia usije kuta naibiwa?”
“Acha wivu, we ulishaniona na mwanamke? Mi siyo mtu wa madem ungesha waona hapa home.”
“Sawa usijali, nitamwambia umeniachia maagizo nimwambie… kwanza leo jumapili anaweza kuchelewa kurudi. Ila jitahidi uwahi kurudi ili hata akichelewe asubuhi akukute ndani.sawa?” Zaituni alimalizia kusema huku akijitoa mikononi mwa Isaack na kuvaa nguo zake, ambazo alikuwa amezitupa chini. Tayari alishapata dose yake ya jioni kwani walifanya mapenzi kama dose ya panadol kutwa mara tatu .
SURA YA KUMI
Ilishafika saa kumi na mbili jioni, Elifosia alikuwa akifunga ofisi ili aondoke akajiandae kwa ajili ya mtoko wake na kijana aliyeuteka moyo wake. Si mwingine ni mtoto wa kipare, mtoto ambaye alionekana mkubwa kutokana na umbile kubwa alilojaliwa. Isaack alishapigilia pamba kali na alitoka nje na kumkuta Elly akimalizia kufunga.
Nyumbani kwa Elifosia aliishi peke yake, mtoto wake alikuwa akisoma shule za bweni na alikuwa akija mara chache kutembea wakati wa likizo. Isaack alikuwa sebuleni akimsubiri ajiandae ili waweze kutoka. Dada Elly aliamua kupanga vyumba viwili tu vya kuanzia maisha baada ya kuachana na mume wake.
Pale sebuleni palikuwa na sofa moja kubwa, meza ndogo na stuli zake mbili, friji ndogo pamoja na luninga ambayo ilipachikwa vema ukutani na kufanya sebule iwe na nafasi ya kutosha kwani palipangiliwa vizuri. Watu husema ‘simple but sure’ kiukweli palionekana mahali pa mtu mmoja asiyependa mambo mengi ila palivutia sana. Mezani palikuwa na magazeti na majarida mbalimbali ya mitindo na michezo.
Ilimlazimu Elifosia kupita pale sebuleni kwenda nje kuoga na kurudi chumbani kwake kwani hakuwa na choo cha ndani. Isaack alishangaa kuona da Elly kama alivyopenda kumwita, akipita na kanga moja tena iliyoloa na kuacha umbo lake zuri kuonekana vema. Hakuwa na mawazo ya kwamba lengo lilikuwa kumtega bali alijua tu ni mambo ya uzungu hivyo hakutilia maanani suala lile. Aliendea kuperuzi kwenye magazeti ya michezo japo yalishapita muda wake.
“Samahani hata sijakuuliza unatumia kinywaji gani…nisamehe bure, nikupe nini cha kunywa? Kuna Serengeti lite, redds na juice ya nanasi.” Elifosia alikuwa akimwambia Isaack huku akifungua friji ambayo ilikuwa karibu na mlango wa kuingia chumbani kwake.
“Naomba maji tu, bado najisikia kushiba sana si unajua ile nyama ni kama tu nimekula peke yangu? Umenitegea sana leo… yani kilo moja nimemaliza yote! Hapa bado tumbo ziko full”.
“Pole basi kama vipi nikuwekee WINE kidogo kwenye glass ili upunguze shibe.”
“Wine si pombe? Situmii pombe nisije kulewa bure… siku moja nilikunywa konyagi ya mshua acha nilewe… nilishinda nimelala kutwa nzima nikasema sinywi tena”.
“Kidogo tu ya kupunguza shibe, kama ulishawahi kunywa konyagi basi huwezi kulewa wine… mi nilijua labda hujawahi kunywa kabisa kumbe umewahi kunywa ngumu kumeza? Basi kwa wine itakuwa kama unakunywa juisi tu.” Elifosia alikuwa akimtania Isaack huku akimimina wine nyeupe kwenye glasi ya wine na kumuwekea mezani. Wakati akifanya yote alikuwa ndani ya kanga moja tena iliyoloa maji kwani alikuwa ametoka kuoga.
Isaack bila kujivunga, alichukua wine na kuanza kunywa na kwa sababu ilikuwa na utamu utamu alikunywa kama juisi. Ndani chumbani kwa Elifosia, alijikwatua haswa na alipotoka alikuwa kama msichana wa miaka ishirini hivi kama siyo kumi na nane, kwani alivalia kijigauni cheusi kifupi kilicho acha mapaja yake manene nje na kuonesha miguu ya bia iliyojazia vema.
Kitendo cha kutokeza tu sebuleni na kile kigauni, Isaack alitoa macho kama vile kaona mzimu. Alishindwa kujizuia na kujikuta karopoka. “Duh da Elly …um… umependeza… kama siyo wewe vile”.
“Aaaahhhh… acha mambo yako bwana. Mbona kawaida tu labda kwa sababu umezoea kuniona ofisini na suruali kila siku. Ila ahsante.”
Elifosia alikaa na kuchukua bia kwenye friji na kummiminia tena Isaack wine kwani alishamaliza na wote wakaanza kunywa taratibu.
“Mi naona bado mapema sana kama vipi ngoja tuzuge hapa ili tukienda tusikae sana nje, si unajua mida ya mziki ni kuanzia saa nne saa tano?” Elifosia alimwambia Isaack huku akiketi na chupa yake ya Serengeti lite mkononi.
“Sawa da Elly, ila naona kibarua unachotaka kunipa leo ni kikubwa mno maana nitakuwa na kazi ya kulinda usiibiwe maana siyo kwa kupendeza huko! Nitakuwa na kazi ya kuangalia usitekwe na watu wasiojulika.”
“Usiniite da Elly bhana, unaweza tu kuniita Elly. Siku hizi mambo ya kizungu zaidi. Hata mama yako unaweza tu kumwita hata kwa jina lake ukipenda, mambo yanabadilika kweli tofauti na zamani.”
“Kweli? Mi nilijua utaona nimekudharau. Basi kuanzia leo nitakuita hivyo ili nikufurahishe… au unaogopa utazeeka? Si tumeshaambiwa uzee mwisho chalinze? Hapa mjini wote baby au nikuite baby? Nakutania bwana da Elly”
“Naomba usitanie, nitapenda ukiniita baby kama utaiita kutoka moyoni na siyo mdomoni. Hivi una macho ya aina gani? Ina maana huoni kama nakupenda? Nimejitahidi sana kukuonesha kwa vitendo nikijua labda utaona lakini naona macho yako kwenye hili yana upofu… naomba usiendelee kuutesa moyo wangu… NAKUPENDA ISAACK sijiwezi juu yako. Toka siku ya kwanza nilivyokutia machoni yapata miezi sita sasa, ndani ya muda wote huo nimevumilia sana unaweza kuona nimeteseka kwa muda gani… please naomba usiendelee kunitesa… niko tayari kufanya chochote juu yako ilimradi niwe na wewe.”
Isaack alidhani anaota, hakuamini yale maneno aliyoyasikia kutoka kwa Elly, alibaki muda bila kuongea chochote. Alishangaa ilikuwaje muda wote huo aliokaa nae kama dada yake asijue hisia zake, alijiona mjinga sana juu ya mapenzi. “Sasa kama huyu ambaye namuona kama dada yangu ananipenda na siku zote sijaona si wengine wataniona mimi si riziki? Duh!” Isaack alikuwa akiwaza.
***
Safari ya kwenda mziki iliishia pale, Isaack na Elly walikuwa chumbani wakiivunja amri ya sita kwa raha zao. Isaack alijifanya fundi na kusimamia kucha kama wanavyopenda kusema vijana wa kizazi hiki. Alikuwa katikati ya mapaja yaliyojazia vema akizama katika mgodi wa chumvi na kuichimba kwa ufundi wa hali ya juu na kumuacha Elly akilia kilio cha furaha.
Isaack alikutana na mzoefu wa mapenzi, tofauti na vile alikuwa amezoea kati yake na Zaituni, siku ile alikuwa na fundi aliyebobea katika uwanja zilipigwa pasi za kila aina. Kuna muda alibaki ameshangaa asijue la kufanya kwa sababu alihisi kuzidiwa mbio, lakini hakutaka kuonesha udhaifu aligangamala na yeye kujifanya fundi mpaka pale alipohakikisha tayari mpira umeingia golini.
Elly hakuamini kilichokuwa kinatokea, aliona kama yuko kwenye ndoto kama ilivyo kawaida yake. Hakuna siku iliyopita bila kuota akifanya mapenzi na Isaack, hivyo alijua ilie ilikuwa ndoto tu kama siku zingine. Kilichomfanya ajue ile siyo ndoto ilikuwa kweli ni sauti iliyomsemesha. “ Kwa nini hukuniambia kama unanipenda siku zote hizo? Nimekosa utamua huu muda wote huo?”
Elly alishtuka na kujikuta yupo kifuani kwa Isaack ambaye alimkumbatia vema. “Siyo rahisi kama unavyofikiri… mi nilijua unajua na uliamua tu kunipotezea maana vijana wa siku hizi mkijua mnapendwa mnajua kuringa balaa.”
“Kweli sikuwahi kujua, laiti ningejua mapema nisingepoteza muda… kwanza siku zote nilijua umeolewa. Sikujua kama unaishi peke yako.”
“Basi ndiyo umeshajua nakupenda na ninahitaji kuwa na wewe, nitafanya chochote ilimradi usipate shida. Kama upo tayari hapa ni kwako muda wowote utakaojisikia we njoo. Ila nina ombi moja tu kwako… naomba uniambie ukweli kama una mwanamke… sipendi kupanga foleni kwenye mapenzi, nataka nijue kama mimi ni mwizi au vipi.”
Isaack alijishauri kama dakika mbili, alikuwa njia panda kama aseme ukweli kwamba alikuwa akitoka na dada wao wa kazi au la! Mwisho aliamua kudanganya kwamba hakuwa na mwanamke. “Nilikuwa nae ila tumeshaachana. Sasa hivi nipo tu peke yangu niliamua kupumzika kwa sababu wanawake wanazingua sana.”
Mwisho walikubaliana kuanza safari ya mapenzi, kwa sharti moja kwamba wangefanya mapenzi yao kwa siri kwani Elly alihofia umri mkubwa aliokuwa amempita Isaack, lakini pia endapo mzee Mbiru angejua kama mwanae anatoka nae basi hata sehemu ya biashara angemnyang’anya kwani alishamaliza soli ya viatu akimfukuzia ila alimkataa kwa sababu alikuwa akimpenda mwanae na siyo yeye.
Tayari ilishafika saa nne usiku, na wote walikuwa na njaa kutokana na shoo za kibabe walizocheza, waliamua kuahirisha safari ya mziki na kwenda baa ya karibu ambako walikula na kunywa kisha Isaack akarudi nyumbani kwa miadi ya kuja kesho yake kulala.
Maskini Zaituni, alinyang’anywa tonge mdomoni kwani Isaack hakumtaka tena. Alikuwa akimkwepa na kutumia muda mwingi na Elly. Alivalishwa kila aina ya nguo na viatu alivyotaka hata akasahau kutafuta leseni akawa ni mtu wa kulala tu ndani na kubadili channel. Kutokana na tabia ile, vijana wenzie waliamua kumpa jina MARIOO.
MWISHO

Post a Comment

0 Comments