Header Ads Widget

Responsive Advertisement

FADHILA



SOMO KUHUSU FADHILA

Alipopokea tu tuzo zake hivi karibuni, Ronaldo alisema, "Shukrani zimwendee Alberto Fantrau." Kisha akasema:
"Naam mimi ni mchezaji bora na mafanikio yangu yote yamesababishwa na rafiki yangu Alberto"

Watu walitazama na kusema, "Huyu Fantrau ni nani?"

Kisha Ronaldo aliendelea kusema: "Tulicheza pamoja katika timu ya vijana.Watu wa sporting Lisbon walikuja kutazama, walituambia kuwa mshambuliaji ambaye angefunga magoli mengi zaidi watamchukua.

Siku hiyo tulishinda 3-0. Nilifunga goli la kwanza na kisha Albert alifunga 2 kwa kichwa. Na kisha goli la 3 lilikuwa lililovutia kila mtu. Alberto alianza kutokea kwa pembeni, kisha akajikuta uso kwa uso na kipa, alimpunguza kipa na kujikuta yeye na goli tu kias kwamba ilikuwa auskume tu golini mpira. Wakati huo nilikuwa nakimbilia upande wake. Na badala ya kufunga , Alberto aliamua kunipasia mpira na mimi nikafunga. Hivi ndivyo nilivyojikuta katika Sporting Lisbon Academy. Baada ya mchezo nilikwenda kwake, nikamwuliza "kwa nini ulifanya hivyo?" Naye akajibu, "Kwa sababu najua kwamba wewe ni bora kuliko mimi"

Waandishi Walipenda kujua zaidi, walianza kuchunguza na waliweza kukutana na Alberto Fantrau kumwuliza kama hadithi waliyoambiwa na Ronaldo ni kweli, na aliihakikishia, akiongeza kuwa kazi yake kama mchezaji wa mpira wa miguu ilimalizika baada ya mechi ile wakati ilikuwa nafas ya pekee kuwa mchezaji mahiri kama angeajiriwa na sporting lisbon. Badala yake amejikuta akibaki mtaani bila ajira.

Hata hivyo, waandishi wa habari, waliangalia nyumba yake ya kifahari na Mercedes benz anazomiliki wakamuuliza Alberto "huna ajira yoyote je ni jinsi gani unaweza kuwa na nyumba na gari la kifahari? Hauonekani kuwa na kipato cha kumiliki hivi vitu" jibu la Alberto: "Hiyo yote? ni Ronaldo

Maadili ya hadithi hii:
Hebu tujiulize swali lifuatalo: Je! Wangapi wetu tumefanya kitu kama Ronaldo na Alberto? Kwa kinyume chake, wengi wetu tunaonyesha kinyume cha hadithi hii inayoonyesha ubinafsi na msamaha kwa wenzi wao.

Marafiki! Hebu tusaidiane ili tuwe na fahari ya mafanikio ya ndugu / dada / marafiki / jamaa zetu
Na tunapomsaidia mtu kufanikiwa, huyo wa mwisho hawapaswi kamwe kusahau wale ambao wamechangia katika mafanikio haya katika maisha yake.
Na juu ya yote, hatupaswi kamwe kusahau kwamba Mungu anaangalia na kutuhukumu kwa Upendo,

Post a Comment

0 Comments