Header Ads Widget

Responsive Advertisement

NONDO KWA WANAUME




SIMULIZI FUPI : NONDO KWA WANAUME

Baada ya kupata ajali ya gari, na kutolewa jicho moja huku uso wake ukiwa umeharibika Anna aligopa hata kutoka nnje achilia mbali kutoka na mumewe kwenda sehemu za starehe.

Mumewe alijaribu kumuonyesha mapenzi yote lakini bado Anna alikua na wasiwasi na mwili wake, kwani watu waliokua wakimsifia kwa uzuri wake sasa walikua wanamuonea huruma.

Siku moja mumewe alimlazimisha kutoka, ilikua ni katika chakula cha jioni cha wafanyakazi wenzake ambapo kila mmoja alipaswa kuja na mwenza wake. Anna alikataa sana lakini mumewe alimuambia nilazima waende.

John alikua anampenda mke wake na kwake hakuna kitu kilichokua kimebadilika. Anna kwa shingo upande alijitahdi kujipamba na kuvaa miwani nyeusi ili kuficha joicho lake bovu.

Kama alivyotegemea katika kile chakula, walikua wakimuonea huruma kumuuliza maswali ya kejeli huku wa kikonyezana na kucheka chinichini. Anna alijisikia vibaya, alikula kwa shida na alitamani kuondoka pale.

Muda flani aliamua kwenda msalani, akiwa huko huku nyuma wafanyakazi wenzake na John walianza kumtania, wakimuuliza maswali ya kejeli kwamba wanaishije, wanatesekaje na shida anazopata kuwa na mwanamke kama yule.

Walimtania John na kumuambia kwanini asitafute mwanamke wa maana anayeendana na hadhi yake wakimuita Handsome, walimuambia hata kama anampenda angekmuacha nyumbani lakini si kuongozana naye katika shughuli za maana kama zile.

Walivuka mipaka mpaka kuuliza kama bado wanafanya mapenzi, walicheka na wake zao nao kuongea maneno ya kejeli. Anna alirejea na wote walinyamaza kimya, alijua walikua wanamsema lakini alijikaza kulia kwasababu ya mume wake.

Baada ya kumaliza kula kabla ya kuondoka, John alimsogelea mkewe, alimvua ile miwani ili jicho lenye chongo lionekane vizuri. Kisha alimbusu mdomoni na kumuambia.

“Nakupenda sana mke wangu…” Hapafu akaendelea. “Wakati umeondoka hapa rafiki zangu hapa walikua wanauliza kama kuna kitu kimebadilika, kama bado nakupenda tena na kama tunaishije, walikua wanakucheka chinichini eti kwakua unachongo.

Niliwashangaa kwakua sisi tuna amani kuliko hawa, vicheko vyetu na matabasmu yetu si yakonafiki…” Aliwageukia rafiki zake. “Ally mke wako hana chongo, lakini sijui kama humridhishi au la kwani anatembea na Bosi hapa, muda mrefu tu.

Hata lile gari alilokudanganya kuwa kachukua mkopo hakuchukua mkopo ni bosi alimnunulia, wote tunajua hapa kasoro wewe. Lakini wote pia tunajua kuwa umezaa na yule binti wa masijala pale ofisini.

Fred wewe kila siku unachelewa kurudi nyumbani kwakua mke wako anakelele, unajifanya kunywa pombe ili kuficha maumivu kuwa mkeo anakupiga kila siku na hata ule mkono uliovunjika haikuwa ni ajali ya bodaboda bali mkeo alikusukumakwenye ngazi.

Bosi na ubosi wako wote lakini mkeo anachezewa na vijana pale ofisini, wote hapa wanajua na wanakusanifu tu unavyojifanya kidume na wake za watu wakati wako hata humridhishi, wale wote anaowaita kaka zake ni mabwana zake.

Shemeji, hembu muambie mumeo hapa kuwa yule mtoto wenu wa kwanza hata si wake ni mtoto wa yule Mzee alofariki juzi, ukajifanya kulia kana kwamba ni ndugu yako kumbe ni Baba wa mtoto wenu wa kwanza. Usijali hawezi kukuacha wote tunajua anakutegemea wewe nyumba ile umejenga wewe akikuacha anaondoka na begi tu!

Ndiyo mke wangu ana chongo, angalau inaonekana lakini nyie mioyo yenu inamashimo kabisa, mnaishi maisha ya shida kwenye ndoa na kujifanya kujichekesha hapo. Kabla ya kujifanya mnatuonea huruma hembu anzeni kujionea huruma nyinyi kwanza na ndoa zenu za kuigiza.

Mke wangu twende tuwaache na maumivu yao na Bosi jumatatu tunakutana kazini, hunifanyi chochote!” John alimkumbatia mkewe na kuondoka, wakaingia kwenye gari na kwenda zao akiwawaacha wafanyakazi wenzake wakingaang’aa macho tu.

MWANAUME wa kweli siku zote atasimama upande wa mkewe kwani ni wajibu wake kumtetea pale anapodhalilishwa na si kuwa sehemu ya udhalilishaji.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments