Header Ads Widget

Responsive Advertisement

INATOSHA - 1

INATOSHA - 1



*********************************************************************************

Simulizi : Inatosha
Sehemu Ya Kwanza (1)

‘’Sirudi tena jamani, sitauwa tena, sitaki tena… Sitaki tena. Ni bora nife tu sasa hivi..’’
Nilikuwa na jazba sana mpaka nikachomoa ile dripu lakini sikuweza kufurukuta kutokana na zile pingu zilizoshikana na kitanda, nilishangaa napigwa vibao na maaskari huku Happy akiwa mmoja wapo kunirushia mateke.

Songa nayo sasa…


Nililia sana bila kupata hata lepe la usingizi pale hospitali ya 'LIGULA' huku nikizungukwa na mapolisi wakisaidiana na manesi, pingu nilizofungwa mikononi na miguuni huku zikishikana na kitanda zilitosha kunithibiti kutokufanya vurugu ya aina yeyote,
"Mungu wangu...! Mungu wangu...! mbona umeniacha...? Kwanini wajitenga mbali nami...! Kwanini wanikimbia nyakati za shida na matatizo...?"
Ni kati ya maswali niliokuwa nikijiuliza sana akilini mwangu huku nikimlaumu sana sana mwenyezi Mungu aliyeniumba nakujiona ni mkosaji hapa duniani tena yule aliyetengwa kuanzia na jamii mpaka mbinguni.

~ BAADA YA SIKU 3 ~

Bado nilikuwa katika wakati mgumu,machozi niliyolia tangu juzi kwa sasa yalikuwa yamenikauka pia na sauti ilikuwa imeisha,niligomea hata chakula nilipoletewa pale hospitali,hakukuwa na mtu yeyote niliyomfahamu labda angenitetea la hasha! zaidi yakuzungukwa na jopo la madaktari tena wale wanaotibu magonjwa ya akili.
"Nooo...! Nooo....! Nimesema mimi mzima,mzima dokta niacheee...?
Niacheni jamani...?"
Walinishika kwa nguvu wakisaidiana na mapolisi huku wakionesha kuwa wanataka kunipima akili,nilishawashtukia dhamira yao na nilijitahdi kuwa mkali lakini ilishindikana mpaka wakafanikiwa kunipima akili,na baada ya muda madaktari kama wawili hivi waliondoka na chombo nisichokuwa nakifahamu vizuri kisha wakarudi tena.
"huyu siyo mgonjwa wa akili hata kidogo...!"
Aliongea mmoja wa wale maaskari huku akisisitizia kuwa sikuwa nasumbuliwa na matatizo ya akili hivyo nimeua kwa makusudi, maneno hayo ya madaktari yalionesha kuwahudhi sana maaskari pale pale bila hata yakujua nikwanini,wakachukuwa yale makaratasi kwa dokta kisha.
"Twende we muuaji...! twendee..! embu kamanda Msofe...!"
"naam mkuu...!"
"....embu mfungueni hizo pingu tumpelekee Dar es salamu leo leo 'then' tutajua jinsi kesi yake itakavyokuwa huko mbeleni."
Ilikuwa ni sauti ya mkuu wa kitengo cha maaskari akiongea na makamanda wenzake huku wakitilia mkazo kuwa nipelekwe Dar.

********
Kweli nimeamimi usilolijua ni kama usiku wa giza, sikuwa nafahamu kama Gervas,Jammy na Omari wamezikwa au la! Nilijihisi ni zaidi ya mtu aliyechanganyikiwa. Ndani ya masaa Manne nilikuwa katika gari aina ya 'LandCruiser' la polisi huku nikiwekwa siti ya nyuma chini ya ulinzi mkali wa maaskari wawili waliokuwa wamenielekezea bunduki zao kichwani mwangu huku tukianza safari ya kuelekea Dar tukitokea kituo kikubwa cha polisi pale Mtwara.
Uso wangu bado ulikuwa umejaa simanzi kubwa haswa kwa upande wa kichwani kwani muda wote kilikuwa kikiniuma sana bila ya kupata dawa yeyote ya kupunguzia maumivu. Safari ilizidi kuwa ndefu huku tukivuka majumba na mapori mbalimbali,ukimya uliotawala ndani ya gari niliokuwamo ilikuwa jibu tosha kama hawasafirishi maiti basi itakuwa ni mtuhumiwa na mtuhumiwa mwenyewe ni Levina mimi wala si mwingine.
"Afande Stan.. imetimia saa ngapi sasa...?"
"Ehh muda umekwenda kweili, tayari ni saa 4 kasoro...!"
"basi kumbe tuna uhakika kwenye saa kumi na moja tunaingia jijini Dar es salaam.."
"Enhh kama mwendo wetu utakuwa hivi hivi tuna imani tutafika muda huo"
Ilikuwa ni sauti ya mmoja wa wale askari akizungumza na mwenzake kuhusiana na mwenendo mzima wa safari yetu, baridi kali nilioanza kulisikia ambalo kwa sasa lilikuwa likipenyeza kupitia katika mikono yangu huku likiniacha kutetemeka mwili mzima nakufanya zile pingu zicheze cheze zenyewe kwa kutingishika.
Hatimaye tukafika katika pori kubwa nahisi itakuwa ni mkoa wa Pwani Pwani hivi,gari likasimama kisha kilichofuata..
"afande Stan..?"
"naam mkuu.."
"Huyu mwanamke muangalie vizuri asiwazidi ujanja, na tunatoka kwa kupokezana kwenda kujisaidia.."
"sawa mkuu.."
Pale pale akili yangu ikachemka nakufikiria ni jinsi gani nitawatoka wale mapolisi,nikiwa najiuliza uliza mara likapita lori aina ya 'Fuso likapiga sana honi kwa sauti ya juu kwani gari yetu haikuwa imepaki vizuri, mwanzoni nilitamani sana kuchoropoka kinguvu na kuamia kwenye lile lori lakini kama nafsi ikaniambia nisubiri hivyo nikavuta pumzi lile lori likasimama kidogo nakuongea na maskari kisha likaendelea na safari yake na hapo hapo wale maaskari wakawa tayari wamemaliza kujisaidia hivyo tukaendelea na safari yetu, tulienda umbali si mkubwa sana kama kilomita 20 mara gari yetu ikasimama kisha kilichofuata,
"....Afande,umewaona washenzi wameanza mchezo wao..?"
"Hawampati mtu hawa tena naona wanacheza na chombo cha dola.."
Kiukweli kulikuwa na kamba nadhani ni ya chuma iliyokuwa imeziba katikati ya barabara kisha mbele yetu zilikuwepo gari zimetanda huku ikiwaonesha watu kwa mbaali waliovalia mavazi meusi japo haikuwa rahisi kuzitambua sura zao, pale pale risasi zikaanza kurindima juu kwa juu nakufanya nijikunyate huku wale maaskari wakiwa bega kwa bega kuhakikisha bunduki zao haziwekwi mbali na mimi nisije kuwakimbia,woga ulizidi kunitanda tena haswa pale zile risasi zilizokuwa zikiendelea kupigwa nje ya gari niliokuwamo.
"Afande Stan..?, Marwa hawa jamaa wako wengi sana, hivyo hapo abaki moja na huyo binti sisi tuendelee kupambana nao,na wewe Afande Joshua hakikisha unawapigia simu makao makuu sasa hivi wajue kinachoendelea.."
Ilikuwa ni sauti ya mmoja wa wale maaskari ikiwaamrisha wenzake, wakiwa bado wapo katika mazungumzo mara lile kundi la majambazi likawa tayari lipo nje ya gari letu wanataka kuingia na tayari askari mmoja wa kwetu alikuwa ameshauliwa.
"toka nje..! toka njee puuumbaaavu..! mnajifanya eti vijiaskari pumbaaavu..,tokaa...!"
Tayari maaskari wakwetu walikuwa hawana tena ujanja huku akitoka mmoja mmoja na kila aliyetoka hapo hapo alikuwa akikutana na risasi, hadi tukabaki wawili mule ndani ya gari,mara mlango ukafunguliwa kwa nguvu kisha yale majambazi yakamtoa askari nje nakumdubukizia bunduki mdomoni na kisha wakamfyatua hapo hapo akafa na kilichokuwa kinafuata ni zamu yangu kutoka ndani ya gari kwani lile jambazi lilishaniona sura yangu kipindi linamtoa yule askari wa mwisho.
"Toka mwenyewe binti..? Uko wapi...?"
"Mimi hapa...! Jamani lakini mimi sio Polisi...!"
Hawakunielewa chochote zaidi ya kunivuta nje kwa nguvu, nilipiga sana kelele lakini haikusaidia kitu,walifanikiwa kunitoa nje kisha kilichofuatia ni kupigwa vibao vikali huku wale majambazi wakiitana pale.
"Tunakupiga na lazima tukuue kwa kuwa wewe ni mpumbavu japo hatujui kosa lililokufanya ukawa hatiani na hawa wapuuzi...."
"Nawaombeni mniachie huru jamani...!"
Maneno yangu ya huzuni na upole hayakusaidia chochote zaidi ya kuchochea hisia za wale majambazi na kuwafanya waendelee kunipiga huku wakinisukuma huku nakule nikiwa bado na pingu zangu mikononi,damu nyingi zilianza kunitoka puani na mdomoni kwa mateso niliyokuwa ninayapata,wale majambazi hawakuridhika wakanisogeza pembeni pembeni na kale kapori kisha wakanivua nguo zangu kwa kuzichana chana mithili ya ile filamu ya 'Yesu' alipochaniwa chaniwa nguo zake, pale pale wakaanza kuniingilia kwa zamu wanavyotaka,niliumia na kuteseka sana moyoni,hasira kali zilinijaa haswa kila nikifikiria kuwa haya yote ameyasababisha Gervas.
Waliniumiza sana mpaka nikapoteza fahamu na nilipokuja kuzinduka nilijikuta niko pale pale porini tena nikiwa uchi wa mnyama huku damu nyingi zikiwa zimenigandia mwilini,nilijitahidi japo kusimama lakini nikashindwa hivyo nikaanza kutambaa huku nikitafuta japo vipande vya nguo zangu maeneo ya pale napo nijizibe lakini sikuviona,nilitambaa taratibu mpaka kwenye barabara ya lami, sikuweza kushuhudia gari lolote likipita zaidi ya lile gari la polisi waliouliwa kuwa pembeni yangu,ghafla mwanga mkali ulioashiria kuwa kuna gari inakuja,hapohapo nikainua mikono yangu juu na pingu zake hivyo hivyo huku nikiwa uchi wa mnyama nikiomba msaada japo lile gari lisimame,lakini haikuwa hivyo kwani lilinipita tena kwa kasi ya ajabu.
"Mungu wangu...! Mungu saidia...!"
Nilijishangaa napata nguvu za ajabu na hapo hapo halmashauri yangu ya kichwa ikafanya kazi fasta,nikaaza kufanya ule mchezo niliowahi kuufanya kule mpakani enzi zile,taaratibu nikajisogeza mpaka karibu na mwili wa askari yule aliyekuwa mkubwa wao kisha nikamsachi mifukoni nakumkuta na bastola ikiwa nipamoja na funguo zilizoonesha ni za pingu zangu,haraka haraka nikaanza zoezi la kujaribu kuzifungua zile pingu mpaka nikafanikiwa,furaha kubwa ikaanza kutanda mwilini mwangu,kwani nilisisimka sana hapo hapo bila kupoteza muda nikamvua nguo mmoja wa mwili wa wale askari waliokuwa wamekufa na kuzivaa ikiwa ni pamoja na kofia yake bila kusahau namba zake za uaskari nikazibandua nakuziweka mfukoni mwangu kisha nikaingia ndani ya lile gari lao nakuliwasha huku nikiendelea na safari ya kuelekea Dar nisijue itakuwaje huko mbele.

************

Umati mkubwa ulioonesha kuwa ni maandamano kwani walikuwa takribani mia tano hivi huku wachache kati yao wakishika bendera zilizoonesha huenda ikawa ni maandamano ya chama fulani na kwa kipindi hiki walikuwa wakiandamana tena kwa vurugu kali zilizosababisha baadhi ya watu kuuliwa na siyo hivyo tu bali hata kupotea kwa watoto na uharibifu mkubwa wa magari na vitu mbalimbali,kutokana na maandamano yale yalisababisha hadi kufungwa kwa barabara ya kuingilia Dar hii inayotokea Mtwara, ilinifanya kulisimamisha gari langu ili wapite,lakini haikuishia hapo kwani hasira zao kubwa zilikuwa ni kwa mapolisi hivyo walivyoiona gari niliokuwa nayo hi ya polisi walinifuata na kulizunguka kisha wakaanza kulitupia mawe huku na kule huku wakilivunja vioo,
"Toka nje..! Tokaa mpumbavu mkubwa wee, ndio mnajifanya wenye nchi siyo...! Leo ama zetu ama zenu..., tokaa husikii...?"
Ilikuwa ni moja ya sauti kati ya wale watu waliokuwa wakiandamana huku akiniamrisha kutoka nje,sikuwa na jinsi yakufanya ili waniamini kuwa mimi siyo polisi kutokana na mavazi niliyovaa yalioonesha dhahiri nitakuwa ni polisi tu wakati sivyo,
Nilitetemeka huku mchozi ukinitoka,
"Aaah bora nife tu Levina mimi..., mateso.., mateso kila kukicha sasa basi inatosha....!"
Nilijisemea kimoyomoyo huku nikifungua mlango wa gari nakutoka nje,nilipotoka tu nikainua mikono yangu miwili juu kuashiria najisalimisha lakini hawakunielewa zaidi yakuanza kunishambulia tena hata bila ya kujali mimba niliokuwa nayo,
"Ua kabisa..., muueni..., pigaa...! leteni na tairi tumchome kabisa...."
"Jamani mie sio polisi..!"
"Unasemaje...?"
"Mie sio polisi...!"
"Na hizi sare ulizovaa za unesi au...? mpumbavu kabisa wee...!,naona huyu anahitaji tumkaushe,haya leteni mafuta fasta...!"

*************

Nilikuwa sina tena ujanja Levina mimi kwani walinipiga sana tena kwa mateke maeneo ya tumboni huku wakinirukia huku na kule wakigombania nguo zangu,waliniaibisha na kunidhalilisha mbele ya umati wa watu kwa kunivua nguo zangu huku nikibakiwa na nguo ya ndani tena yakiume ile niliyomvua yule askari kulee,nililia sana kwa maumivu niliokuwa nayapata,nilikuwa sijiwezi mpaka nikawa najikokota tena kwa kutambaa huku wakinimwagia mafuta na wengine wakinitupia tairi la gari tayari kwa kuniwasha lakini kabla hawajaniwasha mara..subiri Majaliwa, usiwashe kwanza
moto, Jamani eeh...!"
"Eeeh....?"
"Huyu siyo askari kweli...!"
"N i i i n i i...?"
"Ukweli ni kwamba..."
Kabla hajamalizia kuongea mmoja wa wale watu akawa tayari kawasha moto hivyo ukawa unanisogelea huku nikiukimbia tena kwa kuelekea kwa yule mtu aliyesema kuwa mie siye
askari nadhani atakuwa aligundua kitu kwani mikononi mwake alikuwa na ile suruali aliyonivua huku akishikilia kitambulisho hapo hapo halmashauri yangu ya kichwa ikanituma kuwa itakuwa nikitambulisho cha yule askari niliokuwa nimemvua nguo zake.
"Njoo dada, njoo...!"
aliníita yule kaka huku akinikumbatia kwa nguvu..
"niueni mimi...?,nimesema niueni..?"
Yule kaka aliendelea kukasirika na kuropoka kwa nguvu nakufanya ule umati wa watu unyamaze kwa muda na kumtolea macho yule mwenzao.
"Embu oneni...! hiki ni kitambulisho nimekipata ndani ya suruali ya huyu
dada na kinaonesha jina la 'Emmanuel Swai' na hata picha ya hapa sio ya huyu dada..."
Wale watu wakawa wameamini na hapo hapo nikastaajabu kurushiwa khanga ya mmoja wa wale watu ambaye
ni wakike na ilikuwa ni ya chama chao hivyo nikajifunga nakuungana nao huku nikisahau yote yalionitokea muda mfupi uliopita,tukaendelea na safari ya kuandamana barabara yote
huku mie nikijikongoja taaratibu kwani nguvu zilinipungua mara nikashangaa
gari za polisi takribani sita zikisimama mbele yetu na hapo hapo wale mapolisi
wakafyatua bunduki zao juu ili kutawanya watu,tulikimbia huku kila mmoja akitafuta njia yake,sikuwa
mwenyeji wa ile sehemu lakini nilipita vichochoro nisivyovijua huku na kule kisha nikapitiliza kwenye nyumba nisiyoifahamu na hapo hapo nikaingia ndani ya ile nyumba huku nikipokelewa na mama wa ile nyumba kwani alikubali palepale kunihifadhi kutokana na zile vurugu hivyo nikawa ndani kwake tena sebuleni kimya huku yule mama akihakikisha milango yote ameifunga kwa ufunguo, nikiwa bado nipo mule ndani huku nachungulia kwa nje kupitia dirishani mara hodi ikapigwa,
"Mama Rajabu...?, Mama Rajabu fungua...!"
"Aabe mume wangu..,naja kukufungulia...!"
Maskini alikuwa ni mume wa yule mama tena kumbe ni askari Polisi kwani alikuwa amevalia mavazi ya kipolisi tena akiwa hoi kwa kipigo alichokuwa amekipata toka nje,nikiwa bado namshangaa yule askari mule ndani huku nikitetemeka nakujificha sura yangu kwa kutumia mikono hapo hapo nikageuza shingo yangu nakuelekezea macho yote nje kupitia dirishani mara...
"Nooo...! Nooo..! Msimuue jamani..."
Niliishiwa nguvu nakujikuta naropoka bila yakujua kuwa nipo himaya ya watu tena hatari sana,nilishindwa kuzuia hisia zangu nakujikuta nikitamani kutoka kwani kiukweli nje alikuwa yule kaka aliyeniokoa muda si mrefu nilivyotaka kuuliwa pale kwenye
maandamano na kwa muda huu alikuwa akishambuliwa na maaskari,
"We mama Rajabu huyu nani..? Na
anafanyaje hapa...?"
"Mume wangu ni vurugu ndizo zimemfanya umkute hapa huyu binti..."
"Haya we binti,nimesema toka nje,hapa kwangu sikutaki sawa..! Nyie ndio wakorofi wenyewe tunaowatafuta..."
Sikujua kumbe zile kelele zangu zilimkera sana yule mzee mwenye nyumba pia na khanga nilizovalia zilikuwa jibu tosha kuwa na mimi ni mmojawapo wa waanzisha vurugu za
kile chama,haraka haraka yule mzee alichomoa pingu zake nakunifuata kwania ya kunifunga.., niliingiwa na moyo wa kijasiri ghafla nakujikuta nawahi lango la kutokea na nilipofika nje tu yule mzee aliachana na
mimi hivyo kazi ikawa ni moja tu ya kujinusuru juu ya hawa mapolisi wanaotuliza ghasia,

**********
Nilikuwa mtu wa kutembea hatua mbili tatu kisha najibanza kupitia viuchochoro,sikuweza kuyajua vizuri
maeneo haya hata kidogo na pia mfukoni sikuwa na hela yeyote ya kununua japo biskuti kwani njaa ilianza kunizidia Levina mimi,
"Simama hapo hapo ulipo...! Ukigeuza tu shingo nakufyatua mshenzi
mkubwa wee...!"
maskini nilikuwa katika wakati mgumu kwani nilihisi nimewekewa bastola kichwani mwangu huku sauti ya kiume nikiiskia ikinifokea, nilianza kunyong'onyea huku nikikata kabisa tamaa ya kuishi nakutamani ni bora nijiue mimi mwenyewe kuliko kuwa tena mikononi mwa polisi,
"nisameheni jamani mimi sijaua...?"
"Embu kaa chini haraka...?"
moyo ulizidi kunipasuka kwani kwa upande wa mbele yangu umati mkubwa wa watu ulikuwa ukinishangaa huku wengine wakinicheka,hasira zilinizidia mpaka ile njaa niliokuwa nikiiskia ilikata,nilijihisi kama mkojo unataka kunitiririka kutoka mwilini mwangu kwani kijasho kilichokuwa kinanitoka dhahiri kilichochea hisia za mkojo,
"haya ruka kichura chura kuelekea mbele, 1 2 3..."
Ikanibidi nitii tu ile amri ya yule mtu kwani bado sikuweza kugeuka nyuma
toka alivyonitishia anataka kunifyatua,ila kwa muda huu sikuweza kuvumilia kuiskia sauti yake mpaka
nijionee kwa macho yangu mwenyewe hivyo harakaharaka nikageuza kichwa changu nyuma nakumtolea macho,
"mpumbaavu mkubwa wee....?"
nilitamani nicheke kwani kiukweli alikuwa ni chizi la mtaani likijifanyisha kuwa ni polisi eti mpaka likanishikia chupa ya soda huku likiniwekea nyuma ya kichwa changu,
"kumbe ndio mana watu walikuwa wakinishangaa huku wengine wakinicheka....?"
Ni kati ya maswali niliyojiuliza moyoni mwangu huku nikijichekea kimyakimya nakuondoka taratibu
huku nikimwacha yule chizi akinikimbia nakufanya ule umati wa watukucheka kwa sauti ya juu,nikiwa
bado nataka kutoka pale mara macho yangu yakakutana uso kwa uso na kundi la mapolisi lililokuwa bado linatuliza ghasia na walipoona kundi lawatu pale nilipokuwamo iliwachochea kuja kwa kasi hivyo tukatawanyika tena kwa spidi zote haikuishia hapo tu kwani hawa mapolisi walikuja kwa
dizaini tofauti,walitupa mabomu ya machozi nakufanya kila mmoja wetu asiweze kuona mbele, "simameni wenyewe,nimesema simameni....?"
Ilikuwa ni moja ya sauti ya wale maaskari waliokuwa wakinitaka kusimama lakini haikusaidia chochote kwani nilizidi kusonga mbele,nilitembea mita chache
nikashindwa tena kuona mbele kutokana na macho yangu kuingiliana na yale mabomu ya machozi hivyo
nikawa mtu wa kukisia ninapokwenda,ilifika sehemu nikatulia huku nikihema kwa nguvu mara
nikasikia tena sauti kama za maaskari,
"wamekimbilia huku huku, mwaga mwaga..."
maskini Levina mimi nilimwagiwa maji ya kuwashwa mwili wote hadi ukawa hautamaniki nakujikuta nikishindwa kuona mbele na zile khanga kuzivua huku nikitapatapa huku nakule
nikiendelea na safari ya kukimbia nisipopajua...
"Ooh My God...! Uuh uuh uuh uuh huuuuuuu...! hapa wapi....!"
"tulia kwanza..., enhe unaitwa nani...?"
Akili yangu ikaja kukumbuka baada ya muda kuwa niko katika mikono salama,kwa mavazi aliyokuwa amevalia dhahiri husiti kusema kuwa ni mtumishi wa kanisani tena kama siyo kanisa la anglikana basi atakuwa ni mmoja kati ya masista wa
kanisa la Romani katoliki kwa jinsi muonekano wake ulivyo,alikuwa kavalia gauni refu huku maeneo ya
karibu na shingo yake yakiwa na kaalama cheupe kuashiria kuwa atakuwa ni msaidizi wa kanisani,
"naitwa Amina Samuel George..."
nilijitahidi kumdanganya ili nisiweze kujulikana maeneo ya pale,
"binti uko sehemu safi na salama na wala usiwe na hofu yeyote juu ya maisha yako..."
"sista...?"
"enh niambie binti....!"
"eti hapa nimekujaje kujaje...?"
tulikuokota baada ya zile vurugu zilizokuwa zinatokea juu ya maandamano ya chama chenu.. kabla hajamalizia kusema nilimuwahi na kujitetea,
"lakini mi sikuwa mmojawapo...?"
"usitie shaka kwa hilo,ila ulikuwa ukiwashwa sana na maji yale
waliokuwa wamekumwagia wale askari wa kutuliza ghasia.."
"Ooh ahsanteni sana, sasa hapa ni wapi....?"
"upo katika kanisa la Mt. Yohana kongowe hapa...!"
"inamaana hapa ni Dar...?"
"ndio kwani we ulitokea wapi..?"
Nikiwa katika maongezi na yule sista mara mtu mmoja akatokea aliyeonekana huenda akawa ni mchungaji.,
"Sista Zanita..! huyo binti kazinduka...?"
"ndio Pandre..."
"Ooh,ni jambo jema na la kumshukuru Mungu kuwa kanusurika kwenye zile vurugu pale nje.."
Moyo ulinilipuka ghafla nakutamani kama ningeokoka tu palepale nakumrudia mwenyezi mungu labda huenda nikaepukana na hii mikosi inayoniandama kila siku. Kuanzia siku hiyo nikawa mtu mtakatifu tena yule aliyekuwa anaishi karibu sana na shirika la utawa (mashirika ya dini ya kikristo.) Ndani ya siku mbili tu nikawa si Levina yule unayemjua wewe,kwani nilibadilika sana kuanzia mavazi mpaka mwenendo na kwa muda wote huo nilikuwa mtu wa ndani ya lile shirika kwani muda wote ilikuwa nikusaidiana
na masista katika kazi za mule ndani ikiwa ni pamoja na usafi,niliwahadithia nusu ya story inayohusu maisha yangu japokuwa zile sehemu nilizowahi kufanya mauaji niliwaficha hivyo wakanionea sana huruma sehemu za mateso ambazo nimewahi kuzipitia,pia niliwadanganya hapa nilipo sina hata makazi hivyo wakashawishika nakuamua kunipa kakazi cha kupika chakula pale kanisani na pia niwe nasaidiana na wenzangu katika kutengeneza vyakula vya watawa na mapandre.


**********
Niliyazoea mazingira yote ndani ya wiki mbili tu,upole na unyenyekevu niliouonesha ilikuwa jibu tosha kuwa nimekubaliana na maisha ya pale,ile akili ya kukumbuka mapolisi wala mauaji niliyoyafanya hapo nyuma niliyasahau kabisa na hata habari juu ya Gervas na Jammy kama walizikwa au la sikutaka hata kulijua ila kitu kilichokuwa kinaniumiza nikuhusiana na miradi yangu niliokuwa nimeiacha
kipindi cha nyuma, sikuwa najua kama yule Mama ndiye atakayekuwa bado
anaisimamia au la.


~ BAADA YA MIEZI 2 ~



Mimba ilianza kunisumbua ukiachana na tumbo lililokuwa tayari limeanza kunitoka. Maumivu mengi nilianza kuyapata hadi ikafika kipindi utendaji wangu wa kazi ukaanza kunipungua,hasira za hapa na pale ndizo zilianza kuwafanya uongozi wa pale kanisani kuniweka kikao mara kwa mara nakunisihi nibadilike
nisiendekeze hali yangu hii ya uvivu. Ilipofika asubuhi sikutaka kabisa kutulia nilichokifanya nikuchukuwa kila kilicho changu ikiwa ni pamoja na vijipesa kidogo nilivyokuwa nimejiwekea nakuanza safari ya
kuondoka pale nikijifanya kama naelekea dukani then nikanyosha moja kwa moja mpaka nikajikuta nimefika stendi ya mabasi ya mbagala hapo ndipo akili ikaanza kuchemka nakujitambua kuwa nipo maeneo ya mbagala,sikutaka kuchelewesha muda kabisa na nilichokifanya nikupanda daladala iendayo kariakoo ambapo itakuwa rahisi kufika nyumbani kwetu kurasini, kila mwendo wa safari ulivyokuwa unazidi ndivyo mapigo ya moyo yalipokuwa yakinibadilika nakufanya nisijiamini kabisa kama ni Levina mimi au mwingine kwani kiukweli nilikuwa nimebadilika sana kuanzia kimatendo mpaka kimavazi,
"Konda..? Konda..?"
"unasemaje wewe..."
"shusha hapo., shusha hapo hapo...!"
"watu wengine bwana.., mmezidi kusinzia sana utafikiri gari mmekodi,ona sasa umepitilizwa kituo na ukome huko...!"
nilishuka kwa kunywea kwani siri kubwa nilikuwa nayo moyoni na ilinibidi kushuka kituo kisichokuwa changu kwani macho yangu yaligongana na kama yule mama niliyemuachia mali zangu,hivyo moyo ukaanza kunilipuka sana huku nikimkimbilia na nilipomfikia karibu aibu kubwa ilinijaa kumbe hakuwa yule mama niliyemdhania hivyo nikanyong'ea nakuendelea na safari,sikutembea umbali mrefu mara..
"simama hapo hapo ulipo..! Ole wako ukimbie..!"
ukweli walikuwa ni mapolisi na mmoja kati yao sura yake haikuwa ngeni machoni mwangu,hivyo Levina mimi sikuwa tena na lakufanya zaidi yakujisalimisha kwao kwa kuinua mikono juu kisha wakanifunga pingu nakunipiga vibao huku wakionekana kukasirishwa sana na kitendo cha mimi kutafutwa kwa muda mrefu..
"Fala wewe..! Ulidhani hapa Dar hatutakukamata enh? Na leo utaelezea
kwanini umewaua wale polisi waliokuleta huku Dar..!"
"sikuwaua mimi jamani..ni majambazi..!"
"hakuna ni wewe..embu twende huko.."
Nilichukuliwa na safari yakuelekea kituo kikubwa ikaanza japo sikupajua ninapopelekwa.

Nilipokuja kuzinduka tayari nilikuwa narudishwa gerezani,kitu kilichonifanya nishtuke ni tumbo la uchungu ambalo lilikuwa likiniuma na kunivuta sana haswa kwa maeneo ya kitovuni ndipo palikuwa pakiniuma sana.
"Uuhh...! Uhh....! Hapa ni wapi...? Nauliza hapa ni wapi....?"
"...yani kuua uue sasa hivi unazinduka nakujifanya hujui ulichofanya...? Si ndio...?"
"...nisameheni jamani aiyaaa...! iyaaaa...! iyaaaa....! Levina mimi naozea jela uwii...!"

********
Nakumbuka ilikuwa mida ya saa tatu za asubuh huku nikipandishwa kizimbani tena kwa mara ya pili nakusomewa mashtaka yangu juu ya mauaji niliyofanya,yule mama niliokuwa nikiishi naye alikuwepo huku akitoa machozi yaliochochea hisia zangu nakunifanya nitamani japo kumumuuliza kuhusu miradi yangu lakini ilishindikana kwani nilikuwa chini ya ulinzi mkali,nilikuwa nikitetemeka mdomo huku meno yangu yakiumana.
Hatimaye jopo la mahakimu likiongozwa na mawakili waliojitokeza angalau kunisaidia kesi yangu japo haikusaidia kitu, nakujikuta nikisomewa mashtaka yangu na kisha kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani,nilishindwa kuzuia uchungu nilionao nakujikuta nikizimia na kupoteza fahamu zangu zote.

***********************************

:::: Kila panaposhia ni kama inavyoendelea.. Levina kahukumiwa kifungo cha maisha gerezani. Hana msaada wowote kwa sasa.. maisha yake yatakuwaje?? Nini Mwisho wa hii Simulizi kali na ya kuvutia..??

::: Hii ndio INATOSHA… Mwendelezo wa SITAKI TENA ni zaidi ya ile ya kwanza ni nzuri kuliko.. Kamwe usithubutu kuikosa hata siku 1..

ITAENDELEA

Post a Comment

0 Comments