WAO NI AKINA NANI?
FREEMASON NI AKINA NANI?
Swali hili limekuwa likiulizwa na mimi binfsi mara kadha tangu na baada ya kuanza kuchapisha makala zangu kwenye gazeti la Mtanzani, nimekuwa nikiulizwa swali hili. Ni swali ambalo muulizaji hulidhani ni jepesi tu na lenye majibu ya haraka haraka, lakini ukweli ni tofauti kabisa.
Kwanza kubaliana na mimi kuwa tunao freemason wa aina mbili kote duaniani. Kuna jumla ya wanamasonia wanao karibia milioni sita kote duniani, ambao kama nilivyo sema tunaweza kuwagawa katika makundi mawili tu.
Kundi la Kwanza ni Freemason wanao onekana (Visible Freemason)
Kundi la Pili ni Freemason wasio onekana (Invisible Freemason)
Asilimia tisini na tani mpaka tisini na nane (95-98%) ya freemason wote duniani wapo kwenye kundi la pili 'Visible Freemason' na Asilimia tano mpaka mbili (2%) ya freemason wote ni Invisible freemason.
Hivyo basi mpaka utakapo yaelewa makundi haya mawili ya kimasonia ndipo utakapo weza kuja na tafsiri sahihi au definition ya freemason.
Definition au tafsri inayotumika kwa sasa kuhusiana na freemason sehemu mbalimbali duniani imeegemea kwenye kundi la kwanza la Visible Freemason. Tafsiri hiyo ni sahihi kabisa lakini tafsiri hiyo siyo ukweli wote kuhusiana na freemason.
Tafsiri nyingi kuhusiana na freemason zinawataja kama (1) kikundi au taasisi au jumuiya (2) Ambayo asili yake ni kutoka kwa wajenzi wa zama za kati Ulaya (4) Ambayo sasa inawakaribisha wanachama ambao hawana taaluma ya ujenzi kujiunga (5) Aambayo inajihusisha na shughuli mbalimbali za kijamii.
Hayo kwa uchache utayakuta kwenye tafsiri nyingi za sasa kuhusiana na freemason, lakini kama nilivyo sema huo siyo ukweli wote kuhusiana na freemason.
Ukitaka kuwafahamu freemason vyema, watizame kama mfano wa jengo zuri lililo nakshiwa vizuri. Jengo linapokamilika kujengwa, hufatiwa na kupakwa rangi na kutiwa nakshi mbalimbali. Visible Freemason ni kama nakshi juu ya jengo, ni kama mauwa mazuri kwenye ukuta wa jengo, halafu Invisible Freemason ndiyo haswa jengo lenyewe. Hivyo ni wazi utafanya makosa makubwa ya kimsingi utakapo litafsiri jengo kwa mujibu wa mauwa yaliyo chorwa juu ya ukuta wake, ni lazima tukwangue mauwa yale, rangi yenyewe, halafu ndipo tutakapo kuta jengo lenyewe limejengwa na kitu gani, juu ya kitu gani na muhimu kabisa kwa madhumuni gani.
Hivyo basi Visible Freemason wanatumika kama ngao dhidi ya Invisible Freemason, lengo na kazi yao ni kuyafinika yale ambayo yanafanywa na Invisible Freemason.
Jesse Jackson, huyu ni mfano mzuri wa Visible Freemason
Nadhani huyu sote tunamjua, Mtanzania, freemason ambaye naye anawakilisha kundi la VISIBLE FREEMASON.
Mazzini na Mwenzake Pike vinara wawili katika ulimwengu wa kimasonia, hawa ni Invisible freemason. Pike na mwenzake Mazzin wanatajwa katika maandishi mengi kuwa ndiyo waandishi wa mapinduzi makubwa Ulaya pamoja na vita vya I na II vya dunia na pia vita vya III vya dunia vinavyo andaliwa hivi sasa.
Hivyo basi wakati visible freemason wakiwaficha ngugu zao Invisible freemason kwa kuchangia madawati, vifaa vya hosipitali, miundo mbinu na kazi mbalimbali za kijamii, kaka zao Invisible freemason nyuma ya mapazia ya kiza kwenye mahekalu ya kimasonia wanapanga na kutekeleza njama za kusimamisha utawala wa kishetani juu wa wanadamu wote.
Jumuiya ya kimasonia inayo madaraja 33 au 33 degrees, lakini asilimia 98 ya freemason wote duania hawavuki daraja la 3 ambayo pia ni maarufu kama blue degrees. N a wengi kati yao hawa asilimia 98 hawafahamu kabisa juu ya kuwepo kwa Invisible freemasoni.
“Umasonia kama zilivyo dini zingine zote … unaficha siri zake isipokuwa kwa wateule, wajuzi na wenye hekima na inatumia maelezo ya uwongo ya nembo na alama zake kuwapotosha wale ambao wanaostahiki kupotoshwa ili kuficha ukweli, ambao ni nuru na (kutumia maelezo hayo) tunawaweka mbali na nuru hiyo” (Albet Pike, Morals and Dogma, uk. 104-5, 3rd Degree)
Pike hapi kaweka nukta moja ya msingi kuwa Umasonia ni dini, ni dini ya nini, nitalijibu swali hilo baadaye kwa urefu wake, ila ni dini ya kishetani kwa kifupi. Freemason kama jengo la shule lengo lake ni kuuficha ukweli Fulani kwa watu Fulani, ambao hawa ni lile kundi la freemason wanao fahamika, ambao wao ni kama mauwa mazuri juu ya ukuta usio fahamika asili yake ni nini. Wateule wachache kama alivyo sema Pike ndiyo makhususi siri hizo na mambo yake ya maajabu wanafunuliwa wanapo yafikia madaraja ya juu kabisa.
Mathalani mwana masonia ambaye anaona kuwa dini yake labda Ukristo au Uislamu ndiyo sahihi na hawezi kuziacha basi huyu atabakizwa katika ile sehemu ya jumuiya inayoonekana, huyu atakuwa ni mauwa kwenye jengo la kimasoni, huyu atakuwa ni yule freemason anayo julikana na wanajamii na wala hafichi umasonia wake, na wapo wengi hawa tunawaona kila mahala. Huyu hatofanikiwa kuufahamu ukweli labda autafute mwenyewe binafsi lakini si ndani ya hekalu la kimasoni, huyu ni katika wale ambao Pike anasema wanastahiki kupotoshwa. Lakini mtu huyu atajihisi anafahamu kuwa anaujua ukweli kumbe la hasha, sivyo hivyo.
Utakumbuka Milton Copper kwenye kitabu chake 'BEHOLD A PALE HORSE' ametuambia kuwa daraja la 33 limegawanyika sehemu mbili, hivyo mtu huyu anaweza kafikishwa mpaka daraja 33 lakini akawa ni miongoni mwa wale wanaofaa kupotoshwa, hivyo hatoujua ukweli daima.
Hivyo freemason ni jumuiya ambayo inawagawanya wanachama wake katika makundi mawili, kundi la wale wanao faa kuambiwa kila kitu na wale ambao wanastahiki kupotezwa, hawafai kuambiwa kila kitu.
Freemason kutokana na kazi zao kuna mahala utawasikia wakifahamika kama BABILON BROTHERHOOD, BIG BROTHER, AU ILLUMINANTI, lakini majina haya siyo ya kwao, majina haya yanakuja kutokana na aina fulani fulani za shughuli zao chafu za kimataifa walizo pata kuzifanikisha au wanazo lenga kuzifanikisha na shughuli hizo asili yake ni za kale zaidi kuliko freemason yenyewe.
Freemason imekuwa ikitajwa kwenye maduara ya majina hayo hapo juu na mfano wa hayo si kwavile wao ni 'WACHEZAJI MAHIRI' kwenye mchezo mzima, bali zaidi kutokana na ufahamu finyu wa asili ya matukio hayo na freemaso wenyewe. Freemason katika hili duara la matukio makubwa na mazito ya kidunia kitu kidogo mno, au ni sehemu ndogo sana kwenye duara la nyuzi 360.
0 Comments