FREEMASON NA ALAMA ZA SIRI ZA MIKONO Pt. II
Tunaendelea pale tulipo ishia ....
Alama ya ‘Entered Apprentice’ au daraja la kwanza au First Degree kwa Blue Lodge,au pia inafahamika kama daraja la kwanza kwenye blue degree, inayo fanywa na mwanachama wa daraja hilo, wakati anapoingizwa kwenye jumuiya, alama hiyo, kama inavyo oneshwa na picha hapo chini, huelezea au kuelekeza wakati mwanachama anapo chukua kiapo chake kwa mara ya kwanza ndani ya hekalu la kimasonia kukubali kujiunga na jumuiya hiyo.
“Mkono wangu wa kushoto unaishikilia Biblia na mkono wangu wa kulia upo juu ya Biblia”
Hivyo ni kwa mwanachama ambaye imani yake ni ile ya Kikristu, mwislam atafanya hivyo kwa Quran, na wengine kulingana na vitabu vyao vya kidini.
Utaona hapa mwanachama anaapa kwa kutumia kitabu cha dini yake, kwa vile katika Blue degree, yaani daraja la i,ii, na iii, mwanachama haambiwi kama freemasoni ni dini mpaka atakapo fika daraja la 18, lakini wengi wao hawavuki daraja la iii, na hivyo utawakuta freemason wengi hawakubali wanapo ambiwa kuwa wapo kwenye mtandao unao muabudu shetani, kama nilivyo sema kwenye posti zingine, hawa ni MAUWA mazuri kwenye ukuta wa nyumba chafu ya dhambi.
Katika daraja hilohilo, yaani daraja la kwanza, mwanachama huonesha alama nyingine kama inavyo onekana kwenye picha hii hapo chini.
Alama hii ambayo nayo hutambulishwa kwa mkono vilevile huwa na maana ifuatayo.
Alama hii hufanyizwa kwa kupitisha kiganja cha mkono wa kulia, kwa haraka mno, kwenye shingo.
(Ishara hii huwa tunaiona mtaani kwetu kila mara ambapo inapotokea mtu anamtishia mwenzake kumchinja)
Alama hii inaelezea adhabu ambayo mwanamasonia ataipata endapo atakwenda kinyume na jumuiya aliyo jiunga nayo, jumuiya ya kimasonia.
Mwanamasonia wakati wa kuchukua kiapo hicho kwa kutumia alama hiyo ya mkono huwa anasema, au kumaanisha maneno haya.
“Koromeo langu likatwe katikati, ulimi wangu uvutwe nje wote, na mwili wangu uzikwe kwenye mchanga mbaya wa ufukweni mwa bahari, ambako mawimbi yanapiga mara mbili kwa masaa ishirini na nne, ikiwa mimi nitakiuka miiko ya kuingia kwenye daraja hili la kwanza”
Hicho ni kiapo kwenye daraja la kwanza kabisa. Rais Kennedy aliuwawa kwa kukatwa koromeo lake kwa risasi, wakati wa jua la utosi, alikiuka miiko ya kimasonia, ingawa hakuna ushahidi kama alikuwa ni freemason, ispokuwa kunayo ushahidi kuwa aliwapinga. Kifo cha Steven Kanumba hata kidogo, hakioneshi aina ya mauwaji yanayo fanywa na freemason endapo utakiuka miiko yao, na kama nilivyo elezea, Kanumba hakuwa Freemason na wala hakuna ushaihid wa kushikika kama alikuwa ni freemason, zaidi ya maneno ya mtaani.
Bado tukiwa kwenye daraja la kwanza, kuna kile kinacho fahamika kama, BOAZ,
Hapa ni pale mwanachama mpya anapo anza kutambulishwa kwa wanachama wenzake, kunayo namna fulani ya kushikana mikono na wanachama wenzake. Aina hii ya kushikana mikono ataitumia hapo kama utambulisho, wa kutambulishwa, lakini pia katika maisha yake ya kila siku kama freemason na hata atakapo panda madaraja mengine, ataendelea pia kuitumia aina hii ya kushikana mikono na freemason wenzake, kama njia ya kutambulishana baina yao na wenzake.
BOAZ ipo kama inavyo onekana kwenye mchoro huo hapo.
Mwanachama atalibonyeza DOLE GUMBA lake, Kwenye NAKOSI ya kidole cha shahada (Index finger), naye mwanachama mwenzake atafanya hivyohivyo.
Mwanachama mpya, atakapo kuwa anafanya hivyo, atasema meneno yafuatayo kwa mwanachama mwenzake, ambaye ni ‘Worhipful Master’, hichi ni cheo cha juu sana ndani ya hekalu la kimasonia.
Mwanachama Mpya au yule anaye andaliwa kuwa mwanachama, akiwa amepiga magoti kama ishara ya kuwa tayari kupokea digirii ya kwanza, ataambiwa maneno haya na Worshipful Master ambaye atakuwa na msaidizi wake.
“Mimi sasa hivi ninaweka mkono wangu wa kulia kama ishara ya urafiki, udugu na upendo, na nitafanya hivyo kwa kukushika mkono na kutamka maneno. Maneno haya utatakiwa kuyatamka, kila unapo fanya ishara hii kama ambavyo yatakavyo tamkwa mbele yako na msaidizi wangu.”
Kisha Worshipful Master atamgeukia msaidizi au mtu wa daraja la chini yake, wakiwa mbele ya MWANAMASONIA MTARAJIWA, ambaye bado kapiga magoti na wataanza kubadilishana maneno yafuatayo, kama somo kwa Mtarajiwa mwanachama aliyopo mbele yao.
VIFUPISHO:
WM: Worshipful Master na SD: Senior Deacon (Msaidizi au aliyechini ya WM)
WM: Ndugu unayenifuata kwa daraja.
SD: Worshipful Master.
WM: Natanga
SD: Nafanya siri
WM: Unachofanya siri ni nini?
SD: Siri zote za kimasonia, ambazo zinafichwa na alama hii ya mkono. (Kisha hapo, mwanachama mtarajiwa, anaoneshwa ishara ya BOAZ)
WM: Hiki ni nini?
SD: Mshiko wa mkono.
WM: Wa nini?
SD: Wa - Enterered Apprentice (Daraja la kwanza)
WM: Je huo mshiko unajina?
SD: Unayo jina.
WM: Je utanipatia hilo jina?
SD: Mimi sikupokea, wala sitalitoa.
WM: Ni vipi sasa, utaliweka jina nilielewe.
SD: Taja herufi zake au ligawe kwa usawa.
WM: Taja herufi zake na anza.
SD: Anza wewe.
WM: Anza wewe.
SD: A
WM: B
SD: O
WM: Z
WM: (Akimuambia mwanamasonia mtarajiwa): “BOAZ, ndugu yangu, ndilo jina la mshiko huu, na lazima litolewe kwa utaratibu wake, kwa kulitaja kwa herufi au kwa kuligawa nusu kwa nusu. Unapo litaja kwa herufi daima anza na herufi, ‘A’.
Blair na Papa, wanajua nini wanacho fanya, hiyo ni BOAZ
Papa John na kiongozi wa Israeli, tizama mahali ambapo Sharon ameweka kidole gumba chake, ni juu ya index finger ya Papa John. Wanajua wanfanya nini.
Unaona ni wapi kidole gumba cha huyu ambaye kamshika Bush mkono kilipo wekwa? Jinsi kiganja cha Bush kilivyo kaa, nacho kinatoa nafasi kwa kidole gumba chake, kufanya hivyo hivyo, B-O-A-Z.
Papa Paul VI, naye ndani ya mjengo, kwenye picha ndogo inaonekana vyema namna wote wawili, wanavyo vibonyeza vidole vya shahada vya kila mmoja wao, kwa kutumia vidole gumba vyao.
Kama kawaida ... BOAZ
Wakubwa wawili, kutoka kona tofauti za dunia, wenye mitazamo tofauti ya siasa, uchumi na dini, lakini hapa wanatambuana kwa alama ya siri ya kushikana mikono, jicho la kawaida haliwezi kuona hilo, inaitwa B-O-A-Z.
Unawaona tena hapa, nadhani mimi na wewe tunawafahamu watu hawa kama maadui, Blair na Ghadafi, lakini hapa vizuri kabisa wanasalimiana kwa kutumia, salam maalum, siyo ASALAMALYKUM, WALA TUMSIFU YESU KRISTO, NI B-O-A-Z.
Hii hapa haihitaji maelezo anayeonekana kwenye picha, aliwahi kuwa raisi wa Urusi, halafu akawa waziri mkuu, halafu tena amerudi kuwa Rais wa nchi hiyo ... nadhani unamfaham.
HATA KWENYE MIKUTANO YETU NA WAANDISHI WA HABARI, PALE TUNAPO PEANA MIKONO, KAMA ISHARA YA UPENDO NA UPATANISHI, BADO TUNATUMIA ALAMA YETU YA SIRI Y BOAZ.
Alama hii ya BOAZ hunaswa na kamera au na jicho la anaye fahamu nini kinaendelea, au kinyume chake, utaona ni mshiko wa mkono wa kawaida tu.
Itaendelea ....
0 Comments