Header Ads Widget

Responsive Advertisement

FREEMASON NA ALAMA ZA SIRI ZA MIKONO PART I


FREEMASON NA ALAMA ZA SIRI ZA MIKONO


Kama ambavyo tutakavyo ona Freemason na wenzao wanaabudu miungu wengi katika majina mengi tofauti, katika kutekeleza ibada hizo au kuonesha utii kwa miungu hao, maadui zetu wamechagua njia mbalimbali, alama mbalimbali zikiwemo hizi zinazo fanyizwa kwa kutumia viungo vya mwili.





Freemason wote wa YORK RITE, SCOTTISH RITE, SKULL & BONES, na katika kila asasi ya siri za kishetani kwenye mstari huu wa Illuminanti, wanayo aina fulani ya kusalimiana na aina fulani ya alama zinazo fanyizwa na mikono yao, alama hizo huwa na maana mahususi kwa wanachama.


Kwenye buku rejea la freemason (Masonic Encyclopedia) imeandikwa hivi,


“Mkono ni muhimu sana kwa freemason ... kwani sababu na lengo la kupokea utambulisho hufanya kwa mkono.”







MWANACHAMA KATIKA ROYAL ARCH AU SEVENTH DEGREE, UNAWEZA KUIKUZA HII PICHA NA KUSOMA KILE KILICHO ANDIKWA CHINI YAKE.


Alama hizi za kimasonia, ni lugha ya kimataifa baina yao, huizungumza baina yao na huelewana bila kujali utaifa wao. Manfred Adler, kwenye kitabu chake alicho kiita The Freemason and The Vatican, amesema kuwa ni kweli kabisa freemason wanawasiliana kokote ulimwenguni bila kikwazo cha mipaka baina ya nchi zao kwa kutumia alama mbalimbali. Amendika kwamba, kutokana na tafiti zilizofanywa na ‘United States Senate Committee’ ambayo ilikuwa ikiwachunguza CIA, amendikwa kwamba,


“Asilimia tisini ya taarifa za siri, zinatangazwa, zinapitishwa, zinatumwa kwa kupitia kwenye vyombo vya habari, kama vile magazeti, kwa msaada wa maneno yaliyofungwa kama code na picha”






Huyu jamaa natuambia kuwa kutokana na utafiti huo ni kwamba maadui zetu taarifa zao, hawazifichi kokote, wanazituma waziwazi kupitia kwenye vyombo vya habari, kupitia kwenye taarifa ya habari tunayo tizama, magazeti tunayo soma, taarifa tunazo soma, lakini hatuoni chochote, kwa vile lugha wanayo tumia, ni ngeni kwetu. Msomaji wa habari au mgeni kwenye kipindi fulani cha Luninga, anaweza kufanya kitu ambacho mtazamaji anaweza kudhani ni makosa, bahati mbaya au kioja, lakini walio kusudiwa wakaupata ujumbe wao vyema.



Moja ya filamu za kimasonia waigizaji wake wapo mbele ya Washington monument, ambao ni mnara wa kimasonia, wenye maana pana sana na ambao utaukuta katika kila mji mkubwa duniani ulioshikiliwa na freemason.


ITAENDELEA ......

Post a Comment

0 Comments