Simulizi : Nini Hatima Ya Maisha Yangu Sehemu Ya Tatu (3)
Nilijiuliza maswali mengi juu ya ile picha lakini sikupata majibu, Niliitoa ile picha kwenye ukuta na kuianza kuiangalia vizuri na kwaumakini, maana nilikuwa siamini kama kweli yule alikuwa ni jomba Denis. Wakati nikiwa naishangaa ile picha. Nilimuna yule mzee amerudi huku akiwa ameshikilia matunda kwenye mikono yake.
Yule mzee alianza kunishangaa, baada ya kunikuta nikiwa nimeshika ile picha."Samahani mzee unamfahamu huyu" Nilimuuliza yule mzee huku nikiwa namkabidhi ile picha."Sasa mjukuu wangu nitawezaje kuweka picha ndani kwangu ya mtu nisiemjua" Alinijibu yule mzee huku akitabasam.
Yale majibu ya yule mzee yali dhihirisha kuwa ni mtu anaemfahamu Mjomba. Tena si kumfahamu tu bali na kumjali, maana hata ile picha ilikuwa imetengenezewa vizuri na kuwekwa mbele ya kile chumba. Yule mzee alichukua kiti na kusogea karibu yangu huku akiwa ameshikilia maepo mawili na kunipatia moja.
"Mzee samahani kwa usumbufu. Naomba uniambie wewe ninani na kwanini umeamua kuniokoa, na huyu mtu kwenye picha unamjuaje, maana unaonyesha kumjali na kumthamini?" Nilimuuliza yule mzee ili nimfahamu kiundani maana yeye alionyesha kunifahamu pamoja na kunijali.
"Mjukuu wangu mimi ni Babu yako najua sirahisi kuamini kutokana na kutonifahamu na nikipindi kirefu sana, maana mimi nilikuacha ukiwa mdogo sana. Na mama yako ni mwanangu wa kwanza, na huyo unaemuona hapo kwenye picha ni mwanangu wa pili".
Aliongea yule mzee huku akitokwa na machozi, kitendo kilichopelekea na mimi kuanza kutokwa na machozi, ndipo nilipogundua kuwa yule alikuwa ni Babu yangu. Ambae sikuwahi kumuona wala kufikiri, kama nina Babu hapa duniani.
Kile kitendo kiliniumiza sana maana karibia ndugu zangu wote walikuwa katika mateso, nilimwangalia yule mzee pamoja na yale machozi yaliokuwa yakimtoka, ndiyo hasira zilivyo kuwa zikizidi kunipanda, maana nilijua anaefanya haya ni Baba mkubwa."Pole Babu kwa yalio kukuta, lakini Babu kunakitu kinanichanganyakwenye akili yangu" "Kitu gani mjukuu wangu" "Babu nakumbuka mara ya mwisho nilikuwa chini ya mti huku nikiwa nina hali mbaya sana kitendo kilichopelekea mimi kupoteza fahamu, lakini nilipokuja kushtuka nikajikuta nipo kwenye kakichaka huku nikiwa si hisi maumivu yoyote na pale nilipokuwa na kidonda palikuwa na kovu tu".Nilimuliza Babu ili kujua nini kilinisibu. "Ni story ndefu sana mjuku wangu, ila nitakueleza angalau kwa ufupi" Aliongea Babu huku akiwa anafuta machozi na kuendelea kuongea."Kipindi ukiwa kwa Baba mkubwa wako mimi pamoja na mdogo wako na mjomba wako, tulikuwa tukijua maana kuna mtu yupo pale ambae alikuwa akitupa taarifa zote kuhusu wewe, yote yaliokuwa yakifanyika tulikuwa tukipewa taarifa. "Kipindi walipo kuja kukuchukua na kukuleta hapa, mimi sikuwepo tulikubaliana watakuacha hapa ili nije nikukute hapa, kutokana na kumbukumbu zako kupotea" Aliendelea kuongea kwa shinda kutokana na kwikwi ya kilio. "Mimi nilipofika hapa nilijua utakuwepo maana nilijua hauwezi kwenda popote, nilikupofika nilishangaa kukuta hakuna mtu, ndiyo nikaamua kuanza kukutafuta. Ndipo nilipokukuta ukiwa upo kando ya mti, huku ukiwa unatokwa na mapovu na sura yako ikiwa imebadilika rangi. Nilipokuangalia niligundua kuwa ulikuwa umegongwa na nyoka mwenye sumu kali, ndiyo nikaamua kukupa huduma ya kwanza, huku nikiwa sina mtumaini ya wewe kupona maana ulikuwa kwenye hali mbaya sana kutokana na ile sumu kuwa imesambaa mwilini" Kiukweli niliposikia vile nilianza kuona mwili unabadilika na kuanza kutetemeka kwa hasira niliokuwa nayo. "Nilijitahidi kadri ya uwezo wangu lakini ilishindikana. Nilikuwa nikiamini ipo siku utaliona jua japo sikuwa na huakika, huku siku zilizidi kusonga hatimaye na wiki zikatika huku hali yako ikiwa haionyeshi dalili ya kupona, hadi nikakata tamaa na kutokana na mapigo yako kutoonyesha dalili ya kudunda ndipo nilipo kuweka kwenye kile kichaka ili kuandaa kaburi la kukuzika kwa kuamini ulikuwa umesha poteza maisha."Yale maneno ya Babu yangu yanilishangaza."Inamaana nilikuwa sijitambui siku zote hizo, kweli nimeamini Mungu anamakusudina mimi. Lakini mbona ananipitisha kwenye majaribu magumu namna hii" Nilijikuta naongea mwenyewe kwa sauti ya juu huku machozi yakinitoka.Tulikaa pale na Babu huku nikiwa sijui hatima ya maisha yangu, lakini babu alikuwa akinisihi nimuombe Mungu kwa kila jambo huku akiwa ananiambia nisihofu kuhusu ndugu zangu wapo salama.Tulikiwa pale kwenye kale kajumba huku tukiwa tumejipumzisha tulisikia sauti za watu wakiwa wanaongea. Nilishituka maana toka nimeanza kukaa pale sikuwahikuona mtu wala kusikia sauti ya mtu zaidi ya babu yangu.
Zile sauti zilinishtua sana, sio mimi tu hata Babu yangu nae alionyesha kushangazwa na lile tukio. Niliwaza huenda wakawa ni watu wa Baba mkubwa japo sikuwa na huakika. Dhidi muda ulivyokuwa unaenda ndiyo zile sauti zilivyo kuwa zikizidi kusogea karibu na masikio yangu.
Nikiwa nazidi kujiuliza zile sauti ni zakinanani na wamekuja kufanya nini, ndipo nilipomuona Babu yangu akiwa kama mtu aliechanganyikiwa. Kile kitendo kilinishangaza sana, nipoona vile nikaamua kumuuliza Babu. "Babu kuna nini mbona unaonekana mtu mwenye wasiwasi" Nilimuuliza Babu baada ya kumuona akiwa katika hali ya kiutofauti sana.
Lakini chakushangaza badala ya kunijibu nilishangaa ananivuta mkono, na kuniingiza ndani ya kijishimo ambacho kilikuwa kule ndani ya kile kijumba. Aliponiingiza ndani ya kile kishimo yeye alitoka, na kuniambia nisijaribu kutoka wala kuongea neno lolote, mpaka atakapo rudi.
Yale maneno ya Babu yangu yalinishangaza sana, maana sikuona sababu ya mimi kunificha na kuniambia nisitoke. Sikuwa na kipingamizi nilikaa pale huku nikiwa najiuliza."Nikwanini amenificha na kuniambia nisitoke na nisiongee neno lolote"
Nilijiuliza bila kupata jibu, ndipo nilipoamua kutoka na kutaka kujua nini kilikuwa kinaendelea, na wale watu ni wakina nani na kwanini wapo pale na nikwanini Babu hataki mimi nitoke. Nilizidi kujiuliza maswali yasiokuwa na majibu, huku nikiwa nazidi kujisogeza karibu na mlango wa kile chumba, ili kuchungulia nje ambapo wale watu walikuwepo.
Nilishangaa na kutaka kuzimia baada ya kuwaona watu wa Baba mkubwa wakiwa wamesimama na Babu yangu. Kiukweli nilishangaa sana na kustaajabu maana sikutegemea kitu kama kile kwa mtu ambae nilimuona tegemeo kwangu.
Kiukweli nilianza kuona kama naota lakini haikuwa ndoto, nilimuomba Mungu tukio lile ndoto tena ndoto iliofika ukingoni. Lakini sikuweza kubadilisha kitu, ukweli ulibaki pale pale. Wakati nikiwa nashangaa mara niliona Babu yangu anarudi ndani mbio, huku wale watu wakiwa wamebaki pale pale. http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Kile kitendo cha kumuona Babu akiwa anarudi ndani, niliona kama ndiyo ameagizwa kuja kunichukua na mimi sikupenda kitu kama kile, nilipomuona anakuja nirudi hadi kwenye kile kishimo, alichokuwa ameniacha na kuniambia nisitoke.
Alipoingia nilijifanya sijui kitu na nilikuwa nimedhamiria kumuuwa kama atakuwa anataka kunidhuru, lakini alipoingia alienda moja kwa moja kwenye sanduku lake la nguo, na kutoa mfuko mweusi na kutoka nao nje.
Nilishangaa ni kitu gani alichokuwa ameenda kuwapatia, nilipoona sipati majibu ya kujitosheleza ndipo nilipoamua kutoka kwa mara nyingine tena, ili kuangalia nikitu gani walikuwa wamepewa na Babu yangu.
Babu aliwapatia ule mfuko na wale watu waliondoka. Sikujua ni kitu gani walikuwa wamepatiwa na Babu yangu, japo nilikuwanatamani kujua ni kitu gani. Lakini ilinibidi kukaa kimya, nilirudi pale Babu alipokuwa amenificha.
Aliporejea ndani alinikuta pale pale alipokuwa ameniacha. Hakunisemesha kitu zaidi ya kuniambia nitoke, nami nilitoka bila kuonyesha dalili ya kugundua kitu chochote. Nilikuwa na maswali mengi ya kumuuliza Babu yangu juu ya wale watu, lakini nilijua muda wake hauja fika, utakapo fika nitamuuliza.
Siku zilikatika huku miezi nayo ikiwa inazidikusonga, huku tukiwa tupo pale pori, nilikuwa tayari ni muwindaji hodari pale porini, huwezi kuamini uwezo niliokuwa nao.
Babu alikuwa bega bega na mimi japo mimi sikuwa namuamini asilimia mia ila nilikuwa nakaa nae huku najihadhari, Siku moja tukiwa tumetoka na Babu kwenda kuwinda. Tulifanikiwa kupata tulichokuwa tukikihitaji na kuanza kurudi sehemu ambay tulikuwa tukiishi, tukia njiani tulishtukia kuwaona watu watatu wakiwa wanakuja upande tulikuwa tupo.
Nilipowaona wale watu sikushtuka wala kuogopa, lakini kwa upande wa babu alionekana kushtuka na kuonyesha wasi wasi mkubwa, huku akiwa anatetemeka. Kiukweli nilikua nimebadilika na nilikuwa sio yule John wa zamani aliekuwa muoga, sasa nilikua mtu mwingine hata wakati mwingine Babu yangu aliekuwa akinishangaa nilivyo badilika.
Niliendelea kusonga mbele huku nikiwa nimebeba mzigo wangu. nilipopiga hatua kadhaa nilisikia sauti ikiniita nyuma yangu. Niliposikia ile sauti nilishtuka sana maana aliekuwa nyuma yangu ni Babu yangu, lakini sauti ile haikuwa ya Babu yangu ilikuwa ni sauti ya msichana. Niligeuka haraka ili kujua ninani alikuwa akiniita. Nilipogeuka nilishangaa kumuona mdogo wangu Sophia.
Kiukweli nilifurahi sana huku machozi ya furaha yakianza kutiririka. Nilimkimbilia mdogo wangu na kumkumbatia, huku wote tukitokwa na machozi ya furaha. Kiukweli sikuamini kama nimekutana na mdogo wangu, ambae nilimpoteza kwa kipindi kirefu.
Wakati nikiwa nimemkumbatia ndogo wangu, huku nikiwa siamini amini kama kweli nimekutana nae kwa mara nyingine. Nilisikia sauti nyuma yangu. Nilipogeuka sikushtuka nilipowaona wale watu wa Baba mkubwa wakiwa nyuma yangu.
ENDELEA................ Kile kitendoha kuwaona wale watu wa Baba mkubwa maeneo yale kilinishangaza sana, nilianza kuwaza pengine Babu yangu ndiyo alikuwa amewaita kuja kutukamata maana nilianza kumtilia mashaka toka siku ile alivyonificha na kuniambia nisitoke.
Niliwaza mengi huku nikiwa nimemshika mkono mdogo wangu ili endapo likitokea la kutokea nikimbie na mdogo wangu maana wale watu walikuwa wana miili mikubwa.Lakini chakushangaza nilimuona Mdogo wangu anawasalimia wale watu kwa kuwapa mikono huku wakitabasamu.
Nilianza kuona kama naota tena ndoto isiyokuwa na maana. Sikutarajia kitu kama kile, maana wale watu walikuwa ni maaduizetu wakubwa. Kiukweli nilikuwa kama mtu alie lala na sehemu isiyo julikana."
Kaka hawa unaowaona ni watu Baba mkubwa waliokuwa wakipelekeshwa na kutumikishwa, nakufanya vitu ambavyo hata mnyama waliokuwa na Akili hawawezi kufanya vitu kama walioku wakifanyishwa hawa"Aliongea ndogo wangu kwa kuniondoa wasiwasi. Baada ya kugundua kuwa wale watu si watu wabaya, ndipo nilipo wasalimia.Tulirudi hadi pale tulipo kuwa tukiishi na Babu yangu.
Tulianza mikakati ya kumzibiti Baba mkubwa huku tukiwa na wale watu wake. Tukiwatupo kule porini tulikuwa tukijifunza mafunzo mengi kama kuastola" na mambo nengine mengi.
Kiukweli nilijiona ni mtu tofauti sana maana mafunzo niliokuwa nikiyapata yalikuwa ya hali ya juu, kitu hambacho kilinisaidia kufahamu kwaharaka vitu vingi ni kutokana na Mimi kuwa mshapu. Tulizidi kujipa mazoezi makali huku wengne wakiwa wametangulia na kuanza kutupa taarifa juu ya kinachoendelea kwa upande wa Baba mkubwa.
Tukiwa tumekaa na Babu tukiwa tunapiga story za apa na pale, huku ndogo wangu akiwa anaandaa chakula. Ghafla simu ya Babu yangu iliita, alipoipokea nilishangaa kumuona Babu anaangua kilio kikali kilichonifanya kushangaa.
Nilipomuona Babu yangu ameachia cm huku akiwa kama mtu aliechanganyikiwa hali ilionifanya kuingiwa na hofu. Niliamua kuichukua ile cm ili nijue nini kilikuwa kinaendelea.
Nilipoiangalia ile cm ilionyesha bado ipo hewani, ndipo nilipoiweka masikioni mwangu ili kuzungumza na yule aliempigiaBabu. Kiukweli hata mimi zile taarifa nilizo zipata zilinishtua sana.
Yale maneno niliyasikia kwenye cm niliona kama nipo kwenye ndoto, lakini haikuwa ndoto. Nilibaki nimesimama pale huku nikiwa simu yangu nimeiweka kwenye sikio. Kiukweli nilikuwa nimechanganyikiwa, haikuwa rahisi kuamini.
"Kaka kuna nini? mbona mpo hivyo" Aliongea mdogo wangu na kunifanya nishtuke kutoka kwenye dibwi la mawazo juu ya zile taarifa nilizozipata."Mdogo wangu Mjomba Denis hatupo nae tena" Nilimwambia mdogo wangu na kushindwa kuendelea na kuanza kulia.
Kiukweli zile taarifa zilimshtua kila mtu, hata nilivyo mwambia mdogo wangu zile taarifa alionekana kushtushwa sana. Niliona hali inaanza kuwa mbaya huku tukiwa tunazidi kupungua bila kutekeleza kile tulichokuwa tuna hitaji kukifanya.
Kiukweli ilikuwa pigo kubwa sana kumpoteza Mjomba wetu kipenzi, hasira zilizidi kunipanda juu ya Baba Mkubwa. Lakini haikuwa na budi kukubaliana na jambo lile. Tulijipanga sawa sawa huku tukiwa tunajiandaa kwenda kufanya mashambulizi makubwa, tena mapambano ya ndugu kwa ndugu. Tulipo jiandaa na kujiweka sawa tuliamua kwenda kuanza kutekeleza kwa vitendo, huku tukiwa tunapata taarifa kwa wale watu wa mwanzo walioenda na mjomba.
Tulitembea kwa kutumia miguu kwa umbali mrefu, na sehemu nyingine ilikuwa inatulazimu kupita kwenye maji kutokana na ufinyu wa njia. Haikuwa rahisi kutoka kwenye lile pori. Hiyo ni kutokana na kuwa na wanyama wakali, ambao muda wowote wangeweza kutudhuru. Tulitembea kwa kujihadhari na wanyama wakali pamoja na wadudu wenye sumu kali hadi tukafanikiwa kutoka katika lile pori.
Kile kitendo cha kutoka kule porini kilinifanya nifurahi, maana sikuwa na amini kama ningeweza kutoka kule porini nikiwa salama. Tulitembea hadi tulipoiona barabara kubwa ambayo ilikuwa imewekwa lami, tuliifuata ile barabara huku tukiwa tunaangaza angaza pengine tutaweza kupata usafiri.
Tulitembea kaumbali kidogo ndipo tulipoona piki piki zikiwa zimepaki pembezoni mwa barabara. Tulisogea pale kwenye zile pikipiki ili kujua kama wanaweza kutupeleka tulipokuwa tunaenda. Kiukweli sikuwa nafahamu nipo wapi japo mdogo wangu alionyesha kufahamu ile sehemu.
"Samahani kaka unaweza kutupeleka Mikocheni" Aliongea mdogo wangu na wale vijana waliitikia. Safari ya kwenda Mikocheni ilianza. Wale vijana walikuwa wanakimbiza piki piki kwa mwendo wa kawaida, tulizidi kusonga mbele huku tukiwa bado hatujafika tulipokuwa tunaenda.
Tulipokuwa tunazidi kusonga ndipo nyumba zilivyozidi kuongezeka, hatimae tulianza kuona magorofa, na nyumba za kifahari. Kiukweli Dar ilikuwa imebadilika kwanzia mazingira hadi miundombinu. Tulizidi kusonga mbele, nilitamani kusimama angalau kuosha macho kwenye yale majengo ya kifahari. Tulipofika mbele kidogo mdogo wangu aliwaamuru wale vijana wasimame.
Wale vijana walitii na kusimamisha piki piki zao. "Shingapi kaka" Aliuliza mdogo wangu baada ya kushuka kwenye pikipiki. "Tupe elfu kumi kumi" Aliongea mmoja wa wale vijana na kunifanya nishangaae. "Elfu kumi kwa kila mtu ama?" Niliuliuliza baada ya yule kijana kusema tuwape elfu kumi kumi. "Ndiyo. Kila mtu elfu kumi kumi. Mbona bei ya kawaida, ingekuwa mwingine angewachaji elfu kumi na tano hadi elfu ishirini" Aliongea yule kaka na kunifanya niendelee kushangaa, maana ile hela ni bei ya kupanda basi kutoka Arusha hadi Dar na chenchi unabaki nayo.
Mdogo wangu hakuwa na maneno sana alichofanya aliingiza mkono mfukoni na kutoa noti tatu za elfu kumi kumi na kuwapatia wale vijana. Wale vijana waliondoka na kutuacha tukiwa tumesimama pale. Mdogo wangu alipoona wameondo ndipo alipoanza kusonga mbele huku mimi na Babu yangu tukiwa tunafuata nyuma. Mbele kidogo tuliona nyumba nzuri ambayo ilikuwa na geti kubwa, kiukweli ile nyumba ilikuwa nzuri. Nilimuona mdogo wangu akiwa anasoea kwenye geti la ile nyumba. Alipofika alianza kugonga mlango, baada ya dakika chache geti lilifunguliwa na sisi tukaingia.
Naweza kusema ile nyumba ilikuwa ya kipekee kutokana na muonekano wake. Kiukweli ile ilikuwa mara ya kwanza kuingia kwenye nyumba nzuri namna ile. Tulipoingia mdogo wangu aliingia hadi ndani huku sisi tukiwa tunamfuata nyuma. T Yale maneno niliyasikia kwenye cm niliona kama nipo kwenye ndoto, lakini haikuwa ndoto. Nilibaki nimesimama pale huku nikiwa simu yangu nimeiweka kwenye sikio. Kiukweli nilikuwa nimechanganyikiwa, haikuwa rahisi kuamini.
"Kaka kuna nini? mbona mpo hivyo" Aliongea mdogo wangu na kunifanya nishtuke kutoka kwenye dibwi la mawazo juu ya zile taarifa nilizozipata."Mdogo wangu Mjomba Denis hatupo nae tena" Nilimwambia mdogo wangu na kushindwa kuendelea na kuanza kulia.
Kiukweli zile taarifa zilimshtua kila mtu, hata nilivyo mwambia mdogo wangu zile taarifa alionekana kushtushwa sana. Niliona hali inaanza kuwa mbaya huku tukiwa tunazidi kupungua bila kutekeleza kile tulichokuwa tuna hitaji kukifanya.
Kiukweli ilikuwa pigo kubwa sana kumpoteza Mjomba wetu kipenzi, hasira zilizidi kunipanda juu ya Baba Mkubwa. Lakini haikuwa na budi kukubaliana na jambo lile. Tulijipanga sawa sawa huku tukiwa tunajiandaa kwenda kufanya mashambulizi makubwa, tena mapambano ya ndugu kwa ndugu. Tulipo jiandaa na kujiweka sawa tuliamua kwenda kuanza kutekeleza kwa vitendo, huku tukiwa tunapata taarifa kwa wale watu wa mwanzo walioenda na mjomba.
Tulitembea kwa kutumia miguu kwa umbali mrefu, na sehemu nyingine ilikuwa inatulazimu kupita kwenye maji kutokana na ufinyu wa njia. Haikuwa rahisi kutoka kwenye lile pori. Hiyo ni kutokana na kuwa na wanyama wakali, ambao muda wowote wangeweza kutudhuru. Tulitembea kwa kujihadhari na wanyama wakali pamoja na wadudu wenye sumu kali hadi tukafanikiwa kutoka katika lile pori.
Kile kitendo cha kutoka kule porini kilinifanya nifurahi, maana sikuwa na amini kama ningeweza kutoka kule porini nikiwa salama. Tulitembea hadi tulipoiona barabara kubwa ambayo ilikuwa imewekwa lami, tuliifuata ile barabara huku tukiwa tunaangaza angaza pengine tutaweza kupata usafiri.
Tulitembea kaumbali kidogo ndipo tulipoona piki piki zikiwa zimepaki pembezoni mwa barabara. Tulisogea pale kwenye zile pikipiki ili kujua kama wanaweza kutupeleka tulipokuwa tunaenda. Kiukweli sikuwa nafahamu nipo wapi japo mdogo wangu alionyesha kufahamu ile sehemu.
"Samahani kaka unaweza kutupeleka Mikocheni" Aliongea mdogo wangu na wale vijana waliitikia. Safari ya kwenda Mikocheni ilianza. Wale vijana walikuwa wanakimbiza piki piki kwa mwendo wa kawaida, tulizidi kusonga mbele huku tukiwa bado hatujafika tulipokuwa tunaenda.
Tulipokuwa tunazidi kusonga ndipo nyumba zilivyozidi kuongezeka, hatimae tulianza kuona magorofa, na nyumba za kifahari. Kiukweli Dar ilikuwa imebadilika kwanzia mazingira hadi miundombinu. Tulizidi kusonga mbele, nilitamani kusimama angalau kuosha macho kwenye yale majengo ya kifahari. Tulipofika mbele kidogo mdogo wangu aliwaamuru wale vijana wasimame.
Wale vijana walitii na kusimamisha piki piki zao. "Shingapi kaka" Aliuliza mdogo wangu baada ya kushuka kwenye pikipiki. "Tupe elfu kumi kumi" Aliongea mmoja wa wale vijana na kunifanya nishangaae. "Elfu kumi kwa kila mtu ama?" Niliuliuliza baada ya yule kijana kusema tuwape elfu kumi kumi. "Ndiyo. Kila mtu elfu kumi kumi. Mbona bei ya kawaida, ingekuwa mwingine angewachaji elfu kumi na tano hadi elfu ishirini" Aliongea yule kaka na kunifanya niendelee kushangaa, maana ile hela ni bei ya kupanda basi kutoka Arusha hadi Dar na chenchi unabaki nayo.
Mdogo wangu hakuwa na maneno sana alichofanya aliingiza mkono mfukoni na kutoa noti tatu za elfu kumi kumi na kuwapatia wale vijana. Wale vijana waliondoka na kutuacha tukiwa tumesimama pale. Mdogo wangu alipoona wameondo ndipo alipoanza kusonga mbele huku mimi na Babu yangu tukiwa tunafuata nyuma. Mbele kidogo tuliona nyumba nzuri ambayo ilikuwa na geti kubwa, kiukweli ile nyumba ilikuwa nzuri. Nilimuona mdogo wangu akiwa anasoea kwenye geti la ile nyumba. Alipofika alianza kugonga mlango, baada ya dakika chache geti lilifunguliwa na sisi tukaingia.
Naweza kusema ile nyumba ilikuwa ya kipekee kutokana na muonekano wake. Kiukweli ile ilikuwa mara ya kwanza kuingia kwenye nyumba nzuri namna ile. Tulipoingia mdogo wangu aliingia hadi ndani huku sisi tukiwa tunamfuata nyuma. Tulipofika ndani tulishangaa kumkuta.angaa kumkuta.
Tulishangaa kumkuta Mjomba Denis akiwa ameketi kwenye mmoja ya sofa yaliokuwa pale kwenye ile nyumba. Haikuwa rahisi kuamini kama kweli aliekuwa pale ni Mjomba Denis. Hakuna alieamini kama yule aliekuwa pale alikuwa ni mjomba Denis, maana tarifa tulizopata kuhusu yeye ni kwamba alikuwa amepoteza maisha. "Mbona mnanishaa sana, nini tatizo?" Aliuliza Mjomba Denis baada ya kuona tunamshangaa kwa muda mrefu. Lile swali lilikuwa gumu kwa kila mtu pale. Chakushangaza badala ya kumjibu mjomba, tulimuona Babu anaanza kucheka huku akicheka hadi machozi yakawa yanatoka.
Kile kitendo kilitushangaza sana, hadi nikaanza kuona kama naota yaani mtu ambae alikuwa wakwanza kutokwa na machozi, baada ya kupata taarifa za kifo cha Mjomba, leo hii yule tuliepewa taarifa kuwa amepoteza maisha tunamkuta ameketi huku akiwa anafurahaa. Nilijiuliza bila kupata jibu. Babu aliendelea kucheka hadi mjomba Denic kuanza kulalama, maana haikuwapo na sababu ya kucheka namna ile. Kile kitendo kilimkera hata mdogo wangu Sophia japo hakuweza kufanya lolote kwakuwa yule aliekuwa akicheka alikuwa ni mtu mzima, tena Babu yake ivyo ilikuwa ngumu kumkalipia na kuamua kukaa kimya.
Baada ya kuona Babu anazidi kucheka bila sababu za msingi. Tuliamua kuketi chini endapo atamaliza basi ndiyo tufanye kile kilichotuleta. Dakika chache mbele tulimuona Babu anaanguka chini na kimya kikatawala, Tulivyoona hivyo tulijua bado anaendeleza vituko vyake. Kila mtu aliendelea na mambo yake, mdogo wangu alikuja na kunichukua na kunipeleka katika chumba nilichotakiwa kupumzika. Kiukweli kile chumba kilikuwa cha aina yake, kila upande niliokuwa nauangalia ilikuwa najiona. Hali ya hewa ya pale kwenye ndani ilikuwa nzuri sana, nilijihisi nipo peponi.
Kitanda na vitu vilivyokuwa pale ndani vilikuwa vikivutia sana pale ndani. Haikuwa mara ya kwanza kuona nyumba kama ile ama kuona vitu kama vile, ila kwenye ile nyumba ilikuwa tofauti sana. Hata kipindi nikiwa kwa Baba mkubwa hali ilikuwa safi ila kwa pale kwenye ile nyumba ilikuwa ina utofauti mkubwa sana. Nilijitupia kitandani na kuanza kugala gala, kile kitendo cha kugala gala pale kitandani kilinikumbusha kipindi nilipokuwa na Debora katika nyumba ya Baba Mkubwa. Nilizidi kuwaza mengi juu ya msichana niliempenda, huku nikiwa kwenye kile kitanda kizuri hadi nikawa nimepitiwa na usingizi.
Nikiwa katikati ya usingizi mzito ulioambatana na mchoko wa kutembea muda mrefu bila kupumzika. Ndipo nilipomuona binti aliejiinamia chini huku akiwa anatokwa na machozi. Nilipomuona yule biti huku nikiwa sijaiona sura yake nikaamua kumsogelea na kumgusa bega la kushoto. ndipo yule biti alivyonyanyua uso wake. Kiukweli alikuwa biti mrembo kupindukia, nilimwangalia mara mbili mbili. Kwa uzuri aliokuwa nao ulinifanya nishindwe kuongea kitu chochote na kubaki nikiwa namshangaa. Kiukweli uzuri wa yule dada ulikuwa ni uzuri wa namna yake. Nikiwa nazidi kumshangaa yule mrembo huku nikiwa najiuma uma nilishtukia yule Dada ananyanyuka na kuanza kuondoka bila hata kunisemesha.
Nilipomuona anaondoka sikuwa na lakusema japo nilikuwa nahitaji japo kujua hata jina lake ila kutokana na uoga wangu juu ya uzuri wake kwa kuhisi atanielewa aje ndivyo vilivyo nifanya nishindwe kumpata mrembu yule. Ile sehemu aliokuwa ameketi ndipo niliamua kwenda kuketi na mimi huku nikiwa namfikiria mrembo huyo. Nikiwa nimejiinamia huku nikiwa namuwaza yule mrembo, ndipo nilivyo hisi kuna mtu mbele yangu. Nilipo nyanyua kichwa kutazama yule aliekuwa mbele yangu. Nilishtuka kumkuta yule mrembo akiwa kasimama mbele yangu huku akiwa ameshkilia kisu kwenye mkono wake wa kuliwote
"Wanaume nawachukia sana na nahisi wewe utakuwa mfano kwa wanaume wote" Aliongea yule mwanamke huku akinyanyua kile kisu na kunichoma kifuani damu zikaanza kunitoka, zilitoka damu nyingi huku yule mrembo akiwa ananiangalia bila hata huruma, nilimuangalia yule Dada aliekuwa mzuri wa sura huku roho yake ikiwa tofauti na uzuri aliokuwa nao. "Kaka? kakaaa?" Nilikurupuka kutoka kwenye ndoto, ndoto ambayo sikujua mwisho wake nini. "Kaka Babu toka amelala jana hajaamka mpaka sasa kalala vile vile" Aliongea mdogo wangu na kunifanya kukasirika sana maana mimi nilikuwa kwenye ndoto ambayo nilihitaji kujua mwisho wake nini. "Sasa kama kapenda kulala mpaka sasa hivi si yeye mimi nifanyaje. Vitu vingne unatakiwa kufikiria. wemwenyewe uvifahamu vituko vya Babu alafu unakuja kunisumbua sumbua" Niliongea kwa hasira hadi mdogo wangu akaanza kunishangaa hiyo ni kutokana na kunikatisha ndoto yangu. "Kaka unajua Babu nimemwamsha lakini hajaamka, na hata nilivyo jaribu kumtingisha sikuweza kufanikiwa kumwamsha. Lakini mwili wake umekuwa kama ukuni maana mwili wake wote umekauka sijajua tatizo nini" Aliongea mdogo wangu na kunifanya nishtuke. "Amefanyajeee?"
Aliongea mdogo wangu na kunifanya nishtuke na kukurupuka kitandani. Nilitoka mbio hadi sebleni alipokuwa Babu. Nilimkuta Babu akiwa amelala kama alivyo anguka jana. kile kitendo kilinishangaza sana maana halikuwa hajajigeuza hata upande mmoja, nilimsogelea na kumgeuza upande wa pili ambapo sura yake ingeweza kuonekana. Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firahuni, hakuwa Babu yule niliekuwa namfahamu. Kiukweli nilishtuka sana nilihisi naota ndoto za mchana, siyo mimi tu ambe nilishtushwa na lile jambo hata mdogo wangu nae alionekana kushtushwa na lile jambo.
Niliona kama mauza uza maana kwanzia nguo, vitu ,asilimia kubwa ya muonekano ulikuwa ni wa Babu ila kwenye upande wa sura ndiyo nilichanganyikiwa. Sura ya yule mtu ilikuwa ni kijana ambae kwa haraka haraka anaweza kuwa na miaka 25-35, haikuwa rahisi kuamini kitu kama kile. Mwili wake ulikuwa umekakamaa. Muda wote huo mjomba tulikuwa hatujamuona hata tulivyo mfuata chumbani napo hakuwepo hata simu yake haikuwa hewani. Tulizunguka nyumba nzima kumtafuta mjomba bila mafanikio. Kile kitendo kilizidi kunitia hofu.
"Mbona mnanishangaa?" Nilikumbuka sauti ya mjomba kipindi tulipotoka kule porini na kuja hapa, sauti ya mjomba ilikuwa imebadilika sana, haikuwa sauti ya mjomba yule niliekuwa namfahamu. Hata taarifa za kifo chake zilikuwa za kutatanisha sana. Niliwaza mambo mengi kwa wakati mmoja huku nikiwa nazidi kukumbuka matukio ya nyuma. Huku nikiwa sijui lolote nilishtukia watu wawili wanadondokea mbele yangu wakiwa wamevalia nguo nyeusi, huku makoti yao yakiwa marefu usawa wa magoti. Haikuwa rahisi kufanya jambo lolote maana tayari tulikuwa wale watu walikuwa wamesha tuzibiti kwa kutukamata mikono na kutukandamizia ukutani. Kile kitendo kilikuwa ni kitu cha haraka tena cha kushtukiza, uwezo na nguvu walizokuwa nazo wale jamaa hazikuwa za kawaida.
Hivyo ilikuwa ngumu kujikomboa, hakuna hata mmoja aliebahatika kuona sura za wale watu, au kuwatambua kirahisi. Tulifungwa kamba mikono na miguu bila kupewa nafasi ya kuwatambua wale watu. Baada ya hapo tulisogezwa hadi sebleni, tulipofika sebleni tuligeuzwa upande ule alipokuwa amelala yule mtu. Tulishangaa kumkuta Baba mkubwa akiwa amekaa kwenye sofa lilokuwa karibu na yule mtu. Kiukweli niliogopa sana hadi nikahisi haja ndogo kutoka, maana hakuna mtu liekuwa namuogopa kama Baba mkubwa. Kile kitendo kilinishangaza sana kwakuwa hakuna mtu aliekuwa anafahamu kama sisi tulikuwa pale. Nilishindwa kuelewa nini kinaendelea maana jambo lile lilikuwa jambo la ghafla, sikutegemea kitu kama kile.
"Si mlikuwa mnanitafuta mniuwe? aya niuweni sasa" Aliongea Baba mkubwa huku akiwa anamgeuza yule mtu aliekuwa ameanguka pale chini. "Nawapongezeni sana kwa kujitahidi kupunguza watu wangu, mkafikiri mtaniweza. Ila niwaambie kitu, Mmechelewa" Alizidi kuongea Baba mkubwa huku nikiwa sielewi anamaanisha nini. "Mlifikiri mkimuuwa huyu na kumbadilishia nguo, mkazani mimi nitawaacheni ninyi muendelee kuwamaliza watu wangu" Kiukweli yale maneno yalizidi kunipa maswali mengi juu ya yule mtu tuliemkuta amelala pale Babu alipokuwa na kuvishwa nguo za Babu. Nikiwa nawaza kuhusu uwepo wa yule mtu kwenye ile nyumba, huku mavazi yake yakiwa ni ya Babu yangu.
Nilishtukia Baba mkubwa. Ananyanyuka na kumfuata mdogo wangu. Alipomfikia alinigeukia na kuniambia. "Wewe na mdogo wako wote, mtakuwa marehemu muda siyo mrefu. Aliongea Baba mkubwa na huku akiwa anatabasamu. "Na kama mtakuwa marehemu itakuwa imenipunguzia kero ya kusumbuliwa na vitoto vidogo kama nyie. Kama wazazi wenu walinishindwa, nyie mtaniweza" Alizidi kuongea Baba mkubwa na kunifanya hasira zikaongezeka mara dufu, tena pale alipo kuwa anawataja wazazi wangu ndiyo hasira zivyozidi kuniongezeka.
Mpaka wakati huo sikuwa na jua Babu pamoja na Mjomba wapo wapi. "Kabla hamjaondoka kwenye hii Dunia nataka angalau kamechi cha kirafiki na mdogo wako, maana akifa mtoto mzuri namna hii bila kupata mechi nae itakuwa kosa kubwa sana" Aliongea Baba mkubwa huku akiwa anashika shika kifua cha mdogo wangu.
Kile kitendo kilinishangaza sana. Mwanzo nilikuwa naona kama utani lakini ilikuwa tofauti. Kiukweli sikuamini kama ipo siku Baba mkubwa angekuja kufanya kitendo kama kile, cha kinyama tena kwa ndugu yake wa damu. Sikuamini kama kweli Baba mkubwa alikuwa akiongea kwa kumaanisha. Nilishangaa anamvua mdogo wangu nguo zote na kumwingilia kimwili bila ridhaa yake. Kile kitendo kilikuwa cha kinyama, tena chakuzalilisha. Yote hayo yalifanyika mbele ya macho yangu. Nilijaribu kujitoa mikononi mwa wale watu, ili nimsaidie mdogo wangu, lakini sikufanikiwa zaidi ya kuambulia ngumi, vibao, na mateke. Mdogo wangu alilia sana hadi ikapelekea mdogo wangu kupoteza fahamu. Baada ya kupoteza fahamu Baba mkubwa hakuridhika, aliwahamuru wale watu wake waendelee kumzalilisha mdogo wangu mbele ya macho yangu.
Kiukweli Baba mkubwa alikuwa na roho tofauti na wanadamu wengine, alikuwa ni zaidi ya mnyama. Sikuweza kuvumilia kile kitendo alichokuwa anafanyiwa mdogo wangu. Hasira zilizidi mara dufu hadi nikaanza kuona kizunguzung. Nilitoka mbio na kuwaruki wale watu Kabla hata sija wafikia nili shtukia kitu kizito kinatua kichwani mwangu, maumivu makali yalifuata huku macho nayo yakakosa nguvu mwili nao ukakosa nguvu, na kuanza kuona kiza kingi, sikujua nini kiliendelea. Nilipo kuja kushtuka nilijikuta nipo kwenye kitu kama shimo. Lakini lile shimo lilikuwa tofauti sana, maana lilikuwa linageuka kama vile nipo ndani ya maji. Sikujua nipo wapi kwa wakati huo, nilijitahidi kutafuta pakutokea lakini sikufanikiwa. Kadri muda ulivyokuwa unakwenda ndivyo nilivyokuwa nazidi kuona lile shimo linapinduka..
Nilivyokuwa najipigiza kwenye lile shimo ndipo nilipogundua kuwa nipo ndani ya pipa na si shimo, ni kutokana na milio ya kujipigiza. Nilishindwa kuelewa nimeingiaje kwenye lile pipa na sikuwa najua nipo wapi kwa wakati huo. Hata nilipo jaribu kuvuta kumbukumbu sikuweza kukumbuka chochote, hiyo ni kutokana na kupigizwa pigizwa ndani ya lile pipa. Nilizidi kubaki ndani ya lile pipa huku nikiwa sijui mchana wala usiku. Njaa nayo haikuwa mbali, kiu nacho hakikusita kuwa karibu na njaa. Sikuwa na uwezo wa kufanya lolote lile, hata nilipojaribu kutoboa lile pipa ilishndikana. Nilituma kila aina ya mbona ili kujitoa kwenye lile pipa lakini sikufanikiwa.
Kiukweli nilikuwa nimechanganyikiwa. Haikuwa rahisi kuomba msaada. Hiyo ni kutokana na nguvu kunishia, njaa niliokuwa nayo ilikuwa haielezeki, hewa nayo ilikuwa nzito tofauti na apo awali. Nililia sana huku nikimuomba Mungu anitetee katika lile janga, maombi yangu hayakufika mbali, kelele, kilio na machozi yangu, hivyo ndivyo vilivyokuwa rafiki yangu. Hali ilizidi kuwa mbaya. Nilijitahidi kupaza sauti kwa nguvu zote, lakini sikufanikiwa kupata msaada. Nilivyoona hakuna msaada nilianza kumuomba Mungu, iwapo kuna sehemu nilifanya yasiyo mpendeza anirehemu ili nisiwe mmoja kati ya wale walio mchukiza.
Nilijipa moyo wa matumaini japo nilikuwa nimekata tamaa lakini kutokana na zile kelele nilijua lazima ningepata msaada. Nilijikaza kwanguvu zote na kuanza kupiga kelele za kuomba msaada, nikiwa najua zile kelele zilikuwa ziki wafikia wale waliokuwa wakifurahiya. Nilikaa muda mrefu huku hali yangu ikizidi kuwa mbaya kusubiri pengine kungetokea msaada, lakini sikuona mtu zaidi ya kuendelea kuzisikia sauti zao wakiwa wanashangili, huku miziki, tarumbeta na vingine vingi vikisikika. Kweli niliamini ule msemo usemayo "Siku ya kufa nyani miti yote huteleza"
Nilimuomba Mungu nikiwa najua dhahiri nitakufa kwakuwa hakukuwa na msaada, baada ya hapo hali iliendelea kuwa mbaya. Nilikitamani kifo maana nilikuwa nimesha iona Dunia chungu, niliomba maombi ya kila aina lakini sikuona mabadiliko. Nikiwa tayari nimekata tamaa ya kuishi, huku nikiwa sitamani tena kuishi tena kwenye hii Dunia, nilisikia sauti kama za watu wakiwa wanapiga kelele za kushangilia. Huku wengine wakipiga vigele gele, miluzi, firimbi na kila aina ya shangwe. Zile kelele hazikuwa mbali maana zilikuwa zikisikika vizuri na kwasauti kubwa tofauti na ukiwa mbali.
Taratibu nilianza kupoteza matumaini ya kuishe, ni baada ya kupiga kelele bila kupata msaada. "Nani kaniweka humu? na nikwanini? au kuna kitu nimemkosea Mungu. Ee Mungu nipunguzie adhabu, niwangapi wanakula na kunywa huku wakiwa wanadhambi tele Mungu wangu nisaidie kunitoa katika hili janga" Nilijikuta naongea mambo mengi tena mengine yasiyo husika, huku machozi yakinitoka. Hali ya kiza kuongezeka kwenye macho yangu, tokea apo sikujua nini kiliendelea. http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Nilikuja kushtushwa na sauti ya hooni ya gari. Nilikurupuka pale nilipokuwa nimelala. Nilishangazwa na mazingira ya lile eneo, haikuwa rahisi kutambua nilikuwa wapi. Nilipo angalia mazingira ya kile chumba nilishangazwa sana na kile chumba, kilikuwa chumba cha namna yake, nilizidi kushangaa yale mazingira maana hali ya pale ndani ilikuwa tofauti sana. Nilipotaka kunyanyuka ili niende kuchungulia dirishani ili kujua ni wapi.
Nishangaa kuona mpira mdogo, uliokuwa unapitisha maji na kuingia mwilini kwangu.Kile kitendo kilinishangaza sana, nilipoangalia vizuri ndipo nilipogundua kuwa nilikuwa hospital. Nilizidi kushangaa maana sikuwa nafahamu nini kilimetokea apo kabla. Nilishindwa kuelewa ninani kanipeleka pale. Nilikaa pale kwa muda ndipo nikasikia mlango unafunguliwa. Mlango ulivyo funguliwa nilijifanya nimelala, yule mtu alinisogelea hadi pale nilipokuwa. Alipofika pale nilipokuwa nimelala alinigusa kwenye paji la uso wangu.
Yule mtu kwa haraka haraka niliweza kumgundua kuwa ni mwanamke, hiyo ni kutokana na harufu ya marashi niliyo kuwanikiyasikia. Nilifumbua macho baada ya yule mtu kutoka nje. Sikuwa nafahamu ninikinaendelea, nilijaribu kuvuta kumbukumbu juu ya uwepo wangu pale, ila sikuweza kufanikiwa kukumbuka nimefikaje kwenye kile chumba. Kumbukumbu zangu zilikuwa mwisho pale nilipokuwa ndani ya lile pipa, lakini kuhusu kile chumba sikuwa nakumbuka chochote. Dakika chache mbele mlango ulifunguliwa, aliingia mzee wa makamo huku akiwa ameambatana na msichana mrembo, alivalia nguo za docta.
Nilipowaangaliawale watu sikuwa namfahamu hata mmoja. "Hawa ni wakinanani? na wamekuja kufanya nini hapa?" Nilijiuliza maswali mengi kwa wakati mmoja bila kupata jibu kamili. "Kijana habari yako. Unajisikiaje?" Aliniuliza yule mzee baada ya kunifikia. Nilishndwa kimjibu yule mzee na kubaki nikiwa namshangaa yule mzee. "Kwa jina naitwa Mzee Solomon na huyu unaemuona hapa ni mwanangu wa pekee anaitwa Naomi. Alijitambulishayule mzee huku akiwa amesimama sambamba na mwanae.
Nilizidi kuchanganyikiwamaana sikuwa najua kinachoendelea.Waliniacha pale huku wakinipa pole, baada ya muda mchache alikuja yule msichana alikuwa na yule mzee akiwa kavaa yale mavazi yake ya hospital. Alinitolea ile dripu na kuniambia nimfuate, sikuwa na kipingamizizaidi ya kumfuata yule msichana. "Karibu mjukuu wangu. Pole sana kwa yaliyo kukuta" Nilikaribishwa baada ya kufika sebleni, nilipoangalia ni nani alienikaribishanilishangaa sana kumuona yule bibi tulie kutana nae porini kipindi chanyuma.
Kile kitendo kilinishangaza sana. Niliwaza pengine nimemfananisha lakini haikuwa hivyo. "Karibu kijana jisikie upo nyumbani na huyu unaemuona hapo ni Bibi yangu" Nilijikuta nikiduwaa kwa yale maneno, maana yule Bibi nilikuwa nikimfahamu kama Bibi yangu, na hata ile siku tulipo potezana tulikuwa kwenye harakati za kutoka kule porini huku kila mmoja wetu akiwa na kiapo cha kulipiza kisasi kwa Baba mkubwa. Kutokana na hali ya pale nyumbani kwa yule mzee ilikuwa rahisi afya yangu kurejea, hiyo ni kutokana na kupata chakula kizuri na mahala pazuri pa kulala tofauti na hapo awali. Niliishi vizuri na ile familia huku nikiwa natamani kujua nini kiliendelea kwa mdogo wangu maana, sikuwa nafahamu mdogo wangu yupo wapi na nini kilimkuta. ******** Siku moja tukiwa tunaangalia Tv tukiwa tunapata chakula cha jioni. Kuna taarifa zilikuwa zinarushwa kwenye Tv za mfanya biashara maarufu, akiwa anaonekana anatoa misaada kwa watoto wa mitaani ahalimaarufu kama chokoraa.
Nilivyo iangalia sura ya yule mfanya biashara nilishtuka kukuta ni Baba mkubwa, huku akijifiku kuwa na roho ya kipekee ya kujali watoto wasiokuwa na wazazi. Kile kitendo kiliniuma sana na kunifanya hasira zilizokuwa zimejificha, maana ni mtu alie niulia wazazi wangu tena kikatili. Kitu kingine kilichokuwa kikizidi kunipa hasira ni kile kitendo cha kumwingilia mdogo wangu kimwili bila ridhaa yake, huku akiwaamuru walizi wake kumfanyia uchafu mdogo wangu, huku angali akijua kuwa yule ni kama mtoto wake. Nilishindwa hata kula kile chakula. Hasira nilizokuwa nazo zilikuwa hazielezeki, nilijitahidi kuendelea kula lakini nilishindwa, ndipo nilipoamua kuelekea chumbani kwangu huku nikiwaacha Bibi na Baba wakiwa wameduwaa na kile kitendo cha kuacha chakula na kuondoka bila kuaga. http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ "Kijana nini kimetokea na mbona umeacha chakula mezani umekuja kukaa huku mwenyewe. Nini kinakusumbua mwanangu maana, hata mazingira niliyo kukuta hapo mwanzo yalikuwa mazingira ya kutisha?" Aliniuliza yule mzee baada ya kuingia kwenye chumba changu. Nilishndwa kumficha kitu chochote maana yeye ndiye mtu pekee alieonekana kunijali katika hii Dunia. Aliumia sana na alinihaidi atanisaidia ili niweze kumpeleka Baba mkubwa polisi, japo mimi sikuwa na nia ya kumpeleka polisi, nia yangu ni kumuuwa kabisa tena ikibidi kumuuwa kikatili kama alivyo uwa familia yangu. Maisha yaliendelea huku siku zikipita nikiwa nipo na ile familia yenye upendo. Ni takribani miaka miwili tayari ilikuwa imepita bila kuonana na ndugu yangu yeyote, niliamini pengine watakuwa wameuwawa na Baba mkubwa. Nilizidi kuamini hivyo kutokana na kutowaona wala kusikia taarifa zozote kuhusu wao.
Siku moja tukiwa na tumeenda kumpokea mtoto wa mzee. Naomi alikuwa mtoto wa kipekee katika familia ya mzee Solomon na kwakipindi chote hicho alikuwa akiishi nchini Marekani akiwa anamalizia masomo yake. Kiukweli Naomi alikuwa ni msichana mrembu huku rangi yake ya chocolate iliyokuwa inamfanya uzuri wake kuzidi. Mzee Solomon ni mtu muhimu sana kwangu, alienilea kwa upendo na kunifanya kama mwanae. Safari ya kwenda uwanja wa ndege ili wadia. Tulipofika uwanja wa ndege wa mwalimu julius kambarage nyerere tulimkuta Naomi akiwa na begi lake la kuburuza huku akiwa amevalia miwani kwenye uso wake. Nilimchukua Naomi hadi ndani ya gari na safari ya kwenda nyumbani ilianza. Tukiwa njiani tulikuwa tukipiga hadithi za hapa na pale, huku nikijitahidi kuweka mazowea na Naomi ili kuzoweana vizuri. Tukiwa tunazidi kupiga story huku mwendo wa gari ukiwa wa wastani, tulishtukia magari mawili yenye rangi nyeusi kutokea mbele yetu na kutoka watu walio valia nguo nyeusi na kuanza kusogea kwenye gari tulilokuwa tumo….
Kile kitendo kilinishangaza sana. Nilijiuliza maswali mengi juu ya wale watu huku nikijaribu kujiweka sawa kwa lolote litakalo tokea. Nilivyoangalia vizuri wale watu sikuweza kubaini hata mmoja, na dhidi walivyo kuwa wengi ndiyo ilikuwa siyo rahisi kukimbia maana tayari walikuwa wamesha fika kwenye gari tulilokuwa tumepanda. Walivyofika kwenye gari letu wali tushusha na kutuambia tupande viti vya nyuma.
Kitendo bila kuchelewa tuliingizwa viti vya nyuma, huku wawili wao wakawa wamepanda mbele. Walivyopanda waligeuza gari na wale wengine walirudi kwenye magari yao. "Nyie ni wakina nani? Na mnafanya hivi kwaajili gani? Na ni nani aliwatuma kufanya hivi?" Naomi aliuliza baada ya kuona kuwa wale watu walikuwa wanatupeleka mahala tusipo pafahamu. Lakini hawaku tujibu kitu chochote zaidi ya kukanyaga mafuta. Nilishindwa nifanye nini maana mbele kuna gari na nyuma vile vile kuna gari. Nilijiuliza pengine bado Baba mkubwa alikuwa akinifuatilia na kama ni Baba mkubwa, basi itakuwa ndiyo mwisho wangu pamoja na Naomi. http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Kiukweli nilitokea kumuogopa sana Baba mkubwa, hiyo ni kutokana na mambo alionifanyia katika maisha yangu ikiwepo la kuniulia wazazi wangu pamoja na ndugu zangu. Kutokana na wale watu kuwa wengi huku tukiwa hatujui tunaelekea wapi, tulitamani kujitetea lakini ilikuwa ngumu sana. Dakika chache mbele tulifika kwenye nyumba iliokuwa kama pango, tukiwa tunachungulia katika vioo vya gari tuliona jumba ambalo lilikuwa bado halijamalizika.
Tulivyo zidi kusonga mbele tulianza kushangaa baada ya kutokea mbele sehemu iliokuwa mfano wa hotel ya kifahari. Wakati huo Naom alikuwa bize na cm yake. Kitu kilichokuwa kinatushangaza kwa wale watu ni kuto kutugusa wala kutunyang'anya kitu chochote ikiwemo simu na vitu vingine.
Baada ya muda kidogo tulifanikiwa kuingia kwenye nyumba ya kifahari sana, nyumba ile ilikuwa ya namna yake. Tulipelekwa hadi ndani ya ile nyumba huku tukiwa bado hatujui tunapelekwa wapi. Tulipofika ndani nilishangaa kumkuta mzee Solomon, akiwa na Bibi huku upande wa pili kukiwa na mjomba na mdogo wangu.
kile kitendo kilinishtua na kunishangaza maana sikutegemea jambo kama lile. Nilifurahi sana kuwaona ndugu zangu ila kitu kilicho nipa maswali mengi ni kuhusu mzee Solomon na Bibi. Kwa wakati huo Naomi alikuwa ameduwaa tu kama mtu alipigwa na bumbuwazi.
Tulikaribishwa vizuri huku Naomi akizidi kumuuliza maswali mengi Baba yake. Hata mimi nilikuwa na maswali mengi kichwani kwango ila niliamua kukaa kimya maana niliona pengine si wakati muafaka wa kuuliza maswali. Usiku wa siku hiyo sikuweza kupata usingiza hata kidogo.
Niliwaza vitu vingi juu ya maisha yangu ya baadae pamoja na ndugu zangu. Asubuhi ya siku hiyo tulijumuika pamoja kupata kifungua kinywa, ila nilikuwa na maswali mengi hadi nikakosa nianzie wapi nimalizie wapi. "Mjomba nini kimetokea maana toka jana nimekuwa na maswali mengi juu yako, maana hata siku ile tulivyo kamatwa na Baba mkubwa hatukufanikiwa kuwaona na hata Babu sijamuona mpaka sasa"
Nilimuuliza mjomba baada ya kuona kimya kimetawala, maana kipindi tupo kule tulikuwa wote wanne na ndiyo maana nilitaka kufahamu nini kinaendelea.
Yale maneno yalionekana kumshtua Mjomba. Alikaa muda kidogo na kuniambia nipate kifungua kinywa kwanza mambo mengine yatafuata. Baada ya kupata kifungua kinywa ilibidi nimtafute mjomba, ili kupata kujua nini kiliwasibu kwa kipindi chote hicho. Mjomba bila kunificha alimiambia kila kitu.
Kumbe hata Babu nae hakuwa mtu mzuri kwa upande wetu, na hata siku ile tulipokamatwa na Baba mkubwa ilikuwa ni kutokana na Babu. Na kwakipindi hicho chote Babu ndiye alikuwa akimpatia taarifa zote Baba mkubwa.
Niliamini ule msemo usemao "Kikulacho kinguoni mwako" Maisha mapya yalianza huku tukiwa tukiishi na Mzee Solomon na mwanae Naomi. Maisha tuliokuwa tukiyaishi yalikuwa maisha ya upendo na furaha, haikuwahi hata siku moja kutoka kwa Mungu familia yetu ikawa na malumbano, au ugomvi baina ya mtu na mtu. http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ ******* Siku moja majira ya jioni tukiwa tunaangalia movie na mdogo wangu pamoja na Naomi. Tukiwa tunazidi kufurahiya movie, kwa mbali tulisikia sauti za watu wakilumbana kama mtu anaedaiwa. Tulitoka ili kwenda kujua nini kimetokea. Tulivyotoka nje tulimkuta mzee mmoja aliekuwa akituhumiwa kuwa ni mzulumati, mzee yule alionekana kuwa mnyonge kiasi cha kumuonea huruma.
Wakati hayo yanaendelea tulishtukia gari linatokea upande wa pili, likiwa katika mwendo mkali sana.
Kitendo bila kuchelewa lile gari liliacha njia na kumvaa yule mzee, pale pale yule mzee alipoteza maisha. Lakini kutokana na yule mtu kushusha kioo cha gari na kuiona sura yake ndipo nilipo mtambua yule mtu ninani.
0 Comments