Header Ads Widget

Responsive Advertisement

QUEEN REPLACED ... pt 2



Clinton alisimama kama muwakilishi wa wapenda vita, wauwaji, waporaji na kila kila baya unaloweza kulirikodi kwenye historia ya dunia.
Trump alisimama kama malaika, mpingaji wa yote Clinton anayo yawakilisha, anaye taka kubadilisha njia ambayo umma umeupita kila uchao.






Vyombo vya habari kote duniani, wasomi, watu maarufu kwa kiasi kikubwa waliona nguvu iliyo nyuma ya Clinton, na hakuna anayetaka kucheza kamari na akashindwa, hivyo mahala pa kuweka pesa yako na ushinde ulikuwa ni upande wa Clinton.



Lakini imekuja tofauti!


Je wananchi wameshinda?


Au ni aina nyingine ya mbinu na mpango wa kuendelea kuwafanya walimwengu wajinga?



Trump tangu mwanzo wa safari hii alikuja tofauti sana, sizungumzii kipindi cha kampeni, lakini nyuma kabisa kwenye miaka ya 80 alipokuwa ananyanyuka kibiashara, alipoulizwa swali juu ya sera za Marekani na nini anaweza kufanya kuibadilisha, alionekana yupo tofauti kabisa, na amekuja hivyo mpaka amekuwa rais mteule.

Amekuwa kinyume na chama chake, na sera zake ni kinyume na sera za mambo ya nje za Marekani kama ulivyoona kwenye hiyo vidio hapo juu.


Lakini mfumo wa utawala na siasa za Marekani wenye nguvu si wanasiasa. Hillary alipokea pesa nyingi kwa maana ya michango kutoka kwa mashirika na taasisi ambazo zimekuwa zikifanya hivyo zama zote za uchaguzi, na kila mgombea aliye shinda aliwasikiliza kwanza mabwana wakubwa waliyo muwezesha kufika hapo, mabwana wakubwa ambao inasemekana wana mtazamo na malengo na mipango tofauti dhidi ya walimwengu wote. Kama ulivyo muona Trump na kumsikia kwenye hiyo vidio hapo juu akithibitisha hilo la wanasiasa kununuliwa.





Trump naye alipokea vijisenti hivyo kupitia chama chake, au kwake moja kwa moja, ingawa havikuwa vinono kama vya Clinton. Je ni kusema atasimama dhidi ya ‘mfumo’?





Swali hili linaonesha ni namna gani jamii imesukwa na mfumo kiasi haiwezi kuona njia tofauti na hiyo ya mfumo. Tuliona kuwa Hillary ndiye atakaye shinda sababu tumesukwa kuona hakuna jema litakalo kuja ile ubaya, kiasi cha kutamani ubaya, na ikawa ni maajabu Trump aliposhinda dhidi ya Hillary, hakuna aliyeona hilo linakuja.



Ispokuwa wale wale ambao tuludhani wanataka Hillary ashinde ndiyo waliona kuwa Trump atashinda, au ndiyo waliotaka Trump ashinde, tizama hiyo katuni ya simpsoni hapo juu. Ilitolewa nadhani ni mapema mwaka 2016 kama siyo nyuma kidogo.


NI SHIDDAH!!
Kwa taarifa tu ni kuwa simposoni na katuni nyingine na pia filamu nyigni za Hollywood zimekuwa zikitumika sana kuwaambia walimwengu mambao yatakayo kuja miaka kadhaa baadae, na hii ikithibitisha kuwa matukio mengi ya kihistoria na makubwa duniani yalisha pangwa kitambo.






Je ni saikolojia hiyo hiyo inayo tuongoza kuona kuwa Trump hawezi kufanya chochote sababu ‘mfumo’ unazo nguvu mara milioni kushinda yeye?



Ukitizama historia ya ‘mfumo’, kwa wale ambao tunaamini juu ya kuwepo kwa mfumo, kutokana na kuwepo kwa viashiria na doti za kutosha zinazo chora picha ya ‘mfumo’ kwenye maisha na matukio ya kila siku kutoka ya kijamii, kiasiasa, kiuchumi na kidini.



Mfumo huu ni wa muda mrefu kuliko kama ilivyo historia ya binadam mwenyewe kwenye sayari hii. Iwe unaitazama historia yake, kidini, au kiuchumi, au kijamii na hata kiasiasa, kote huko pana onekana uwepo wa mikono ya siri inayo amualia matakwa na muelekeo wa sayari hii na mustakbali wa vilivyomo.


Kennedy alisema hivyo, kuhusu ‘mfumo’ huo, na moja ya kauli zinazo hesabiwa kupelekea kifo chake.



Lakini lengo kuu la mfumo kutokana na nukta tulizo weza kuzi onganisha kwa wale ambao tunao amini juu ya kuwepo kwa mfumo huo ni kusimamisha (1) Serikali moja ya dunia nzima, (2) Mtawala mmoja wa dunia nzima (3) Dini moja kwa binadam wote (4) Sarafu moja kwa dunia nzima. Zaidi kuhusu malengo na mipango hiyo tizama posti hii_ http://salimmsangi.blogspot.com/2013/05/tunaendelea-na-safari-lakini-leo.html





Utaona kuwa ‘mfumo’ huo si kwamba tu ni mpango wa zaidi ya milenia kadhaa wa kadha, lakini pia umegharimu mamilioni ya roho za watu, matrilioni ya dola za Marekani, maelfu ya mipango na mikakati, sera na sheria, vita na majadiliano mpaka umefika hapa. Kilicho nyuma ya historia ya ‘mfumo’ hata kidogo huwezi kukilinganisha na Trump. Mfumo na Trump ni kama Nyangumi vs Kambare.





Narudia kujiuliza, ni wananchi wameshinda au ni mbinu mpya ya adui yule yule kwenye vita vile vile?



Kivitendo demokrasia imeshindwa.
Demokrasia imeshindwa kuwapatia wanachi mtu sahihi atakayesimama kama kiongozi wao. Demokrasia imeshindwa kuleta majibu sahihi na mikakati dhidi ya matatizo yanayo wakabili wanachi kote duniani.



Matatizo mengi tuliyo nayo sasa ni kutokana na mfumo unao tumika kutatua matatizo hayo. Hii si kwa Marekani tu, lakini kote duniani. Ukitazama katika nchi zetu zinazo endelea ndiyo imekuwa balaa zaidi.



Ni mjadala mwingine mpana kuzungumza ni vipi demokrasia imeshindwa. Lakini ikiwa vyama viwili vinavyo shiriki kutoa mgombea na hatimaye raisi wa nchi; vipo juu ya wananchi; yaani wananchi hawana lolote kwenye vyama hivyo zaidi ya kadi ya uanachama, unafikiri ni vipi vyama au wagombea wao wataweza kuwasikiliza wananchi?



Unapo ichambua siasa ya Marekani utaona wanachi wanatakiwa kuwapigia kura wagombea ambao ni vyama ndiyo vimewapa baraka ya kushika bendera ya kugombea uraisi; siyo wananchi.



Lakini vyama hivyo wawezeshaji wao wakubwa ni walewale maadui wa wananchi. Au ni watu wachache wenye matakwa yao binafsi ambayo wanatumai yatatimizwa na wagombea pindi watakapo ingia madarakani, hivyo wana wahonga wagombea kabla ya uchaguzi kwa kutoa michango mbalimbali kusaidia kampeni zao. Mahitaji ya hao wachache ndiyo yanayo tengeneza sera na sheria za nchi.



Sasa Trump naye ameingia madarakani kwa mfumo huo huo, ni vigumu kunishawishi kwamba atakata tawi la mti alilokalia.


Mfumo ulioshindwa, demokrasia, ndiyo uliyomuingiza madarakani, je tunaweza kutatua tatizo kwa akili ile ile iliyotumika kutengeneza tatizo? HAPANA.



Pamoja na ushahidi wa kihistoria ambao una msimamisha Trump kama mtu tofauti na mfumo ulivyo, mtu ambaye kwa muda mrefu sana amekuwa akizikosea sera za nje na za ndani za Marekani, na ambaye aliitamani nafasi hiyo ili aweze kufanya mabadiliko, ni vigumu kusema this time people won?




Hadithi ya Mussa kulelewa ndani ya nyumba ya Firauni na baadae kuja kuwa sababu ya maangamizo ya Firauni, katika kipindi ambacho tayari Firauni alikuwa na taarifa juu ya kutokea kwa mtu atakaye uangusha ufalme wake, na akaamrisha kila mtoto wa kiume atakaye zaliwa kwenye nyumba ya myahudi achinjwe, kama mbinu ya kukilinda kiti chake, lakini alikuja kumlea Mussa (as) ndani kwake, na aliyo yahofia yakatokea! Huo ulikuwa ni mpango wa Muumba Mtukufu, lakini huwezi niambia kuwa Trump ndiyo Mussa aliyelelewa ndani ya nyumba ya Firauni, bali bado kwa asilimia nyingi naona, ni mbinu za kivita zimebadilishwa, and Time will tell.

PLAY HII VIDIO, NA WEWE UWE HAKIMU







To be continued Inshallah ..

Post a Comment

0 Comments