Header Ads Widget

Responsive Advertisement

NJIA PANDA'' SIMULIZI FUPI YA MAPENZI

Image result for simulizi za kweli kuhusu maisha


Naitwa Saimon nina miaka 28 tafadhali soma Hadithi yangu ya kweli kisha nishauri...
Nilihamia Mkoani Bariadi kutoka Mkoani Shinyanga katika harakati zangu za utafutaji, Sina Mama wala Baba naishi nikitegemea ndugu ambao kwa upande mwingine na wao wananitazama mimi kama msaada kwao lakini nimebarikiwa kupata marafiki ambao wananisikiza, wananijali na kunishauri vyema katika kuyafikia malengo.
Nilipofika mkoani Bariadi nilifanikiwa kufungua duka la uuzaji wa DVD,VCD,CD, FLASH na MEMORCARD kwa bei ya reja reja na jumla huku nikitoa huduma ya kuwawekea wateja miziki na movie katika vifaa vyao kwa gharama nafuu, Duka langu limetazama na duka la mahitaji ya Chakula kwa bei ya reja reja na jumla pia ambako anauza binti mmoja mrembo aitwaye Grace, Duka hilo Grace alifunguliwa na Kaka zake ili aweze kukizi mahitaji yake katika maisha yake hapo baadaye baada ya kuwa wazazi wao wamefariki pia huko mkoani kigoma.
Haikuwa rahisi kwangu mimi kushawishika kimahusiano maana kila aliyekuwa akinishauri kuhusu utafutaji alinisihi nisiyape mapenzi kipao mbele lakini hisia za mapenzi hutokea Automatic hivyo nilijikuta nimeanza kuvutiwa na Grace na kujikuta amenikaa moyoni kabisa, sikufanya haraka katika kumueleza ila kadri ya siku zilivyozidi kusonga maji yalinizidi kina hivyo niliona ni vyema nimueleza hisia zangu Grace juu yake na sikuwa mbali saana na fikra zake maana yeye pia alikuwa akinitazama kimapenzi richa ya kuwakataa vijana wengi waliohitaji kujisogeza kwake kimapenzi, Grace ni binti wa kiha mwenye uadirifu wa hali ya juu kuanzia mawazi yake mpaka kauli zake katika jamii inayo mzunguka pia yuko tofauti saana binti huyu! Nasema tofauti kwakuwa punde baada ya kuanzisha mahusiano na yeye alijitahidi saana kunishauri kujijenga kimaisha kuliko mapenzi yani mapenzi kwetu yalichukua nafasi ndogo saana, maelewano kati yetu yalizidi kukomaa mpaka tukafikia hatua ya kufungua akaunti ambayo tulihakikisha tunahifadhi elfu 20 za kitanzania kila siku! Nilipohitaji penzi Grace alinipatia na hakuwa mzembe kwakweli maana burudani nilyoipata sikuwahi kuipata kabla, maisha kwangu niliyaona mepesi saana maana nilipata mwanamke wa aina niliyokuwa nikihitaji.
Siku moja nikiwa nyumbani katika chumba nilichokuwa nimepanga alipita rafiki yangu kunisalimia ambaye alikuwa akihusikia katika mambo ya Afya na mkononi alikuwa ameshika vipimo vya VVU,nilimuomba anipime na hakusita alinipima pia nilipata furaha saana baada ya kuonekana niko salaama lakini nilimuomba rafiki yangu apite kesho mchana nitakuwa na Shemeji yake ili atupime kwa pamoja! Siku iliyofuata mchana rafiki yangu alipita na alibahatika kunikuta na shemeji yake, japo sikuwa nimemtaarifu Grace alikubali kupima lakini hakukawia alitoka kwakuwa alihitajika haraka dukani na Kaka yake hivyo aliniambia nichukue majibu kisha nitamjulisha ila sikutaka kuamini mara baada ya majibu kuonesha kuwa Grace ni muathiriki lakini nilimficha juu ya majibu yake! Nilitafuta siku nyingine nikamuita rafiki yangu akatupima tena kwa pamoja mimi na Grace lakini bado alionekana ni muathirika na hatukumuweka wazi pia mpaka alipokuja kuona mabadiliko ya mimi kutokumzingatia saana kimahusiano, alipouliza juu ya mabadiliko yangu sikumficha ilinibidi nimuweke wazi Grace kuwa anaishi na maambukizi ya VVU! Hakuamini hata nilipo muonesha vielelezo vya majibu yake hivyo alinishika mkono mpaka maabara tukapima kwa pamoja lakini bado ilionesha kuwa Grace ni muathirika na mimi nipo Salama ikiwa tayari nimeshiriki na yeye kimwili zaidi ya mara tatu, nilitafakali ila sikupata majibu juu ya upatikanaji wa maambukizi hayo kwa mpenzi wangu ambaye nanamtazama kama mke mtarajiwa hapo baadaye. Ndugu zake walinishukuru kwa kuwafanya wajue jambo hilo maana sio Grace tu hata wao walionesha kutokujuwa jambo hilo kabla na wameniacha niwe huru kwa maamuzi yeyote kwakuwa walikuwa wakitambua mahusiano yetu!
Grace analia kila akiniona maana tayari nimeonesha dalili za kumuepuka, haikuwa kwangu tu bali hata mbele ya Kaka zake Grace alitishi kujitoa uhai zaidi ya mara nne pale nilipotaka kumuacha na ameahidi kuwa tuwe tayari kuandaa mazishi yake endapo nikijaribu kumuacha kwa njia yeyote maana haoni faida ya kuishi bila mimi kwakuw bado ananipenda na kunihitaji sana pia haelewi ni jinsi gani yamemfika maambukizi haya ila kwakuwa imetokea hana budi kukabiliana nayo! Hata mimi bado nampenda tena saana, nakumbuka mchango wa mawazo yake katika kupiga hatua kwenye maisha yangu nakumbuka pia hata mchango wa fedha zake pindi nilipokwama lakini nahofia kukwamisha ndoto zangu huku nikiwa na ndugu wanao nitegemea pindi nitakapo ishi na maambukizi haya, kwa sasa nina mpango wa kuhama Bariadi kimya kimya nikaanze maisha kwingine bila Grace kujua ili nimuepuke lakini nahofia pia juu ya uhai wake maana amesema nikijaribu kumuacha kwa njia yeyote basi mimi na Kaka zake tuandae mazishi yake Grace! 

Post a Comment

0 Comments