Header Ads Widget

Responsive Advertisement

NI HADITHI FUPI LAKINI YENYE KUTUPA FUNDISHO KWA MAISHA YETU YA KILA SIKU TUKIWA HAPA DUNIANI….

Image result for simulizi fupi za maisha


Naitwa Jose,  naishi Same,  Kilimanjaro. Nina umri wa miaka 36, nimeoa na nina watoto watatu(3).
  Leo nataka nukupe simulizi fupi ya maisha yangu. Nilipokuwa na umri wa miaka 6  mama yangu alifariki dunia na hivyo Baba hakuchukua muda mrefu akaoa mke mwingine.
     Hapo   ndipo maisha yangu yalianza kuvurugika,  huyo mama alinitesa na kuninyanyasa sana ikiwa ni pamoja na kunitumikisha kazi ngumu na kuninyima chakula. Niliogopa kumwambia Baba maana alinikanya nikimwambia ataniua kabisa. Basi  niliendelea kunyanyasika sana kwa muda mrefu.
   Yule mama alifanikiwa kuwa na watoto  wawili (2),  msichana na mvulana.Watoto wale walinipenda sana lakini mama aliwakataza kucheza na mimi. Ilifikia wakati tukaanza kwenda shule,  nakumbuka nilikuwa darasa la pili,  bahati mbaya Baba yangu akafariki kwa ajali ya basi wakati akitoka Mwanza kuja nyumbani.
  Hapo ndipo nilipokata tamaa kabisa ya maisha yangu. Yule mama alizidisha manyanyaso ikiwa ni pamoja na kunifungia ndani siku nzima bila kula. Ila nakumbuka siku moja yule mama alinikataza kula ugali,  ila maskini yule dada yangu(mtoto wa yule mama)  aliumia sana,  akawa akikata tonge anachovya ananipa kwa nyuma,  hivyo hivyo  maisha yakawa yanaenda tu.
   Ila siku moja  mateso yalinishinda maana nilikuwa napewa kazi nyingi hadi nashindwa kwenda shule. Basi niliamua kutoroka nyumbani nikakaa mtaani,  ni kweli baba yangu alikuwa na mali sana lakini ndio hivyo mrithi akisha kuws mtoto huwa ni kama mtumwa tu.
  Maisha yalikuwa magumu mtaani ikabidi nizunguke zunguke mtaani kutafuta kazi ili mradi nipate hata chakula. Nilifanikiwa kupata kwa baba mmoja ambaye alinipatia kazi ya kuuza Karanga mtaani,  sikuwa na jinsi ilibidi nifanye. Ila Mungu alivyo wa ajabu aliibariki kazi yangu mpaka bosi akashangaa,  basi nikapata mtaji kidogo nikawa nauza maji,  biskut,  soda na bidhaa ndogo ndogo kwenye vituo vya mabasi.
Biashara ilizidi kukua sana na baada ya muda nikafungua kioski changu ambacho kilikuwa kwa kasi sana. Nikafunguaa duka  moja,  mawili,  matatu,….. Mwisho wa siku Mungu alinyoosha mkono wake nikajenga shule ya Sekondari na  maisha yakawa mazuri sana.
Siku moja yule mama akaja pamoja na watoto maisha yamewawia magumu,  walikopa Benk na wakashindwa kulipa deni nyumba ikachukuliwa. Kwa kweli ilichukua muda kidogo kufikiri alivyonifanyia,  lakini Mungu alisema tusamehe saba mara sabini, kwani BWANA YESU  angehesabu makosa yetu nani angepona,  basi nililia kwa uchungu sana nukamkumbatia mama na wadogo zangu nikawakaribisha tukaanza maisha ya upendo,  nikawafungulia wale wadogo zangu biashara kubwa basi maisha yakaendelea.
“”FUNDISHO:KATIKA MAISHA ZINGATIA UPENDO NA MSAMAHA BILA KUANGALIA KOSA””.

Post a Comment

0 Comments