Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Hadithi ya kusisimua "baba"

Tulizaliwa wawili Mimi na Dada yangu Rose....

wakati Fulani mama alipata kunisimulia kuwa walikuwepo ndugu zetu katika ukoo wetu ambao walikufa na tukabaki sisi na baba yetu ...

maisha yalikuwa mazuri sana ingawa Mara nyingi baba Yetu hakutulia nyumbani na kuna wakati mdogo wangu Rose alirudi nyumbani wakati wa likizo na kumaliza likizo yake bila kumuona baba! hata hivyo maisha yalikuwa mazuri kwani zile siku ambazo baba alikuwepo nyumbani hadi majirani walijua kuwa Mzee amerudi! hakika tulikula bata.. nakumbuka nyumbani walikuwepo wafanyakazi Wa shamba na wale waliohusika na kuchana mbao porini...

nakumbuka kila Mara nilipokuwa nikiwapelekea mahitaji walinipongeza kwa kuwa na baba mzuri..

"Mzee wako peace sana" nakumbuka sana kauli hizi Mara nyingi..

wakati Fulani Rose alikuwa akiniambia kuwa baba hafai maana anakaa nje ya nyumba yake kuliko kukaa na sisi hata hivyo Mimi sikuona shida yoyote kwani nilijua baba yupo anatafuta kwa ajili Yetu...ingawa nami ilifikia hatua nikammisi baba!

baba Yetu alikuwa na utaratibu Wa kutufanyia sherehe kwenye birthday zetu....na hata hawa wafanyakazi Wa shamba pia nakumbuka alisema siku moja "kwakuwa hawa watu Wa shamba tunao humu ndani basi nao tutawafanyia sherehe.. na kwakuwa hatujui siku zao za kuzaliwa basi tuwatafutie tarehe yao.."

"basi iwe julai mosi" nakumbuka Rose alidakia kwa furaha na baba akaipitisha tarehe hiyo na kweli kila julai mosi wale wafanyakazi Wa baba walifanyiwa sherehe pamoja na kupewa zawadi kila mwaka...

siku hiyo nakumbuka nikiwa narudi chuo nilimkuta mama akiwa sebuleni akaniambia kuwa wakati Wa kuachana na baba umefika! niliduwaa na moyoni nilifurahi kwani hata Mimi nilishamchoka Mzee..

"baba gani hakai nyumbani kwanza" nilijisemea

"baba yenu ananipenda lakini wazee wamemkataa"na inabidi awasikilize...mama aliongea..

nilingia chumbani kwangu na kuwasha redio kwa sauti hakika nilifurahi sana kwani nilijua sasa nitapata baba mwingine atakayetujali sana..

wiki moja baadae baba alirejea toka safari zake na baada ya kuongea na wafanyakzi wake wa shamba na kuwaaga alisema hatawaacha hivi hivi na pale pale alitoa nusu mshahara kwa wale wafanyakazi Wa kupasua mbao na kusema hiyo itakuwa posho yao kabla ya mshahara!!

kisha baba alitugeukia sisi wanae..alianza na Rose ambaye alitaka tu apewe usimamizi Wa shamba la mibuni..

baba akamwambia si kupewa usimamizi Bali anampa lote liwe lake! Rose alikimbia na kumkumbatia baba kwa furaha!
"haya zamu yako " baba aliongea kwa furaha akitabasamu...
nilitumia dakika kadhaa kumtazama baba nilikumbuka zile nyakati nilipobaki nyumbani na familia huku baba akiwa huko ..nilikumbuka kipindi mama akiwa mgonjwa na Mimi na rose tukamkimbiza hospitali tukiwa na majirani..ndio baba alituachia pesa za kutosha lakini kwanini alifanya vile??..
kwa ujasiri na kujiamini nilisimama..
"sitaki chochote mwanaharamu mkubwa wewe ulituacha wenyewe wewe ukila mitaa huko unadhani hela ni kila kitu..."

"wewe Mtoto umerukwa na akili?" mama alidakia..

"mwache aongee mke wangu mwache" baba aliongea tena akitabasamu...

"sitaki chochote nitabaki nikimlea mama na mdogo wangu we ondoka tu"

nilisema nikiondoka..
hata hivyo baba alitabasamu na kucheka kwa sauti halafu aksema msemo wake alioupenda sana Wa "ni upepo tu utapita" huyu Mtoto atanikumbuka...

mama aliguna tu..

hata hivyo baba aliniachia vitu vingi ikiwemo nyumba tatu na miradi yote ya kuchana mbao...kisha akasepa zake....

miezi miwili baadae..


nikiwa chuo mwaka Wa tatu nikasikia mama ameolewa tena...hakika nilifurahi na nilikimbilia chumbani kwangu kumpigia simu mdogo wangu Rose..
"ni kweli kaka baba yetu Wa sasa hivi hatoki ndani kabisa"

"were kweli really"? niliuliza kwa furaha..

"lakini pia hakai sebuleni kabisa labda wakati Wa chakula au taarifa ya habari" rose alisema..


siku zilipita na nikafanikiwa kurudi nyumbani nikiwa nimefaulu vizuri...nilitegemea kwa matokeo haya lazima Mzee anipe nafasi nzuri..

wakati nafika nyumbani nilishangaa kupewa maji tu...na mama..sikustuka sana maana nilijua mama ataniandalia soda au juisi.. muda ulipita na jioni nikamuona baba..

"hujambo..habari za chuo?...lete vyeti vyako" Mzee huyu aliongea akiwa siriasi ..

"baba hata sijakaa hatujaongea unataka vyeti?" nilifoka

aisee kumbe nilikosea sana maana nilishtukia nikipewa kibao na teke la maana nikaangukia meza ya chakula..

"Mimi sijaribiwi usidhani Mimi ni kama yule baba yenu aliyepita...""
siku hiyo hatukulala nyumba ilijaa vilio..
kesho yake baba akatangaza kuwa hakuna tena kuajiri watu shambani wote hadi mama tutakuwa tukienda asubuhi na kurudi jioni
hata ile posho ya kusafirishia mbao na nauli ya kwenda shamba baba akafuta ..

alidai kuwa hakuna umbali Wa kukodi bajaji badala yake tutembee tu..


zile birthday za kila tarehe moja July baba akafuta kimya kimya maana mwezi ulipita hivi hivi..

"Rose unasemaje mdogo Wangu? nilimgeukia Rose wakati tukirudi nyumbani jioni moja..

Rose hakujibu kitu akaanza kulia kwa kwikwi..


*MWISHO*

Post a Comment

0 Comments