Header Ads Widget

Responsive Advertisement

MSAMBWANDA !!



Mke wangu alisajili line mpya bila Mimi kujua,Jina lake Jenifa Godson.
Jana usiku nimerudi home akaniomba Tshs 10,000/= akasuke nywele nikamwambia sina ila nakupa Tshs 7,000/=
Wakati tumelala,message ikaingia katika simu yangu "Hi,my Love!",Nikatoka nje(toilet) nikamjibu,"We ni nani?"
MESSAGE:
"Ni mimi Jen Msambwanda" kusikia sambwanda, Mshipa wa "Samsing" ukanicheza!
MIMI:
Jen Msambwanda wa wapi tena?
MESSAGE:
"Buana baby,nawe,si pale unapokulaga kila siku?"
MIMI:
"Oooh,kumbe unaitwaga Jenifa!Namba yangu umeipata wapi?
MESSAGE:
Nimepewa na rafiki yako DJ Tipwili.
Nakupenda sana handsome, sema huwa naogopaga kukwambia.Fahamu mi sijiwezi juu yako,yaani kila ukija kula, natamani usiondoke,nikwambie yaliyomo moyoni mwangu,Unanitesa mwenzio!"
MIMI:
Ooh,Jamani pole mpenzi!
Hata Mimi nilikuwa nakupenda,yaani kila nikiona hilo "tako",nahisi mzunguko wa damu ku-change! I love you too Honey!
MESSAGE:
Basi mpenzi,Nikuombe kitu?
MIMI:
Aaah,sema tu.
Message:
Naomba Tshs 50,000/-
MIMI:
Nakutumia sasa hivi.(Nikatuma)
MESSAGE:
Wow!
Asante mume wangu,haya rudi ndani tulale.Ni mimi mkeo Mama Kiduku hapa!
‍♂‍♂‍♂
Basi mwenzenu leo nimezuga zangu mlinzi nipo nje hata ndani sitaki kwanza hakuna hata feni alafu mbu wengi Acha awake mwenyewe !

PATA NAMBA YAKO YA KITAMBULISHO KWENYE APP HII BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments