Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Kwanini Wasichana Wanakukimbia ?

Image result for kukimbia mapenzi

FAHAMU KWANINI WASICHANA HUWA WANAKUKIMBIA


1. Wakikosa attention yako. Wasichana hupenda pale
wanapofahamu kuwa unawasikiliza na unafahamu nini wao
wanahitaji. Kama kutakosekana mawasiliano mazuri na
atagundua hilo atauona uhusiano huo haumtimilizii haja
zake. Hata kama kila kitu kinaenda sawa. Msikilize
anapoongea. Kama akiona hapati penzi analolihitaji
atatafuta mwingine ambaye yupo tayari kumtimizia.


2. Kumuheshimu. Msichana huwa anajitoa sana awapo
katika mahusiano hivyo anategemea mvulana uheshimu
hata kwa chochote kidogo anachokufanyia. Mfanye
agundue kuwa umeheshimu kile ambacho amekufanyia.


3. Usaliti. Unaposaliti inamaanisha kuna kitu hakipo sawa
katika mahusiano yako hata kama una uwezo wa
kushughulikia lakini wewe unaona njia sahihi ni kutoka nje
kuwa na mahusiano na msichana mwingine ukidhani ndio
unarekebisha. Pale msichana wako akikukamata unamsaliti
fahamu hawezi kuvumilia naye atakuacha.


4. Ukosefu wa hisia za kimapenzi. Msichana hupenda
kuona kuwa wanapendwa wanathaminwa na wapenzi wao
wanawajali sasa wakiona kuwa hakuna conection ya hisia
za kimapenzi kutoka kwa mvulana wake huona kuwa
hakuna mapenzi ya kweli katika uhusiano aliopo


5. Hawapendi kusikia kuhusu mapenzi mara kwa mara
wasichana hupenda kutumia muda mrefu na wapenzi wao
bila kusikia neno la kuwataka wafanye mapenzi kama ukiwa
nao na ukawataka kimapenzi mara kwa mara watakuwa
wanakuavoid hata utakapokuwa ukiwagusa.


6. Unapomcontrol sana
msichana humpenda mvulana atakayemlinda na kujiona
yupo sehemu salama sio kumdhibiti kufanya mambo yake
mengine anapenda uhuru kwa ujumla

Post a Comment

0 Comments