Header Ads Widget

Responsive Advertisement

FREEMASON NA ALAMA ZA SIRI ZA MIKONO PRT IV


FREEMASON NA ALAMA ZA SIRI ZA MIKONO Pt. IV
“JACHIN”
MSHIKO WA UTAMBULISHO KWA MFUASI WA DARAJA LA PILI







Mwanamasonia atamshika mkono mwanamasonia mwenzake, kama watu wanavyo salimiana kawaida, na kisha atalibonyeza dole gumba lake kwa nguvu kwenye nakozi ya pili, na masonia mwenzake naye atafanya hivyohivyo dhidi yake.


Kisha maneno ambayo WM na SD walibadilishana awali yatafanyika mpaka kufikia kwenye hatua ya kutaja jina la mshiko huo, ambalo nalo litatajwa kwa herufi au kwa kuligawa mara mbili.




SD: A
WM: J
SD: C
WM: H
SD: I
WM: N


Kisha WM, ATASEMA MANENO HAYA KUMUAMBIA MWANAMASONIA ANAYE TARAJIWA KUINGIA DARAJA LA PILI, “JACHIN, NDUGU YANGU NDILO JINA LA LA MSHIKO HUU. NA LAZIMA SIKU ZOTE LITOLEWE AU KUTAMKWA KWA UTARATIBU HUU, KWA KULITAJA KWA HERUFI ZAKE AU KULIGAWA MARA MBILI, NA UNAPO LITAJA KWA HERUFI SIKU ZOTE KUMBUKA KUANZA NA HERUFI ‘A’.


ALAMA YA MKONO KATIKA DARAJA LA TATU (MASTER MASON DEGREE)





Wakati mwanachama anapo chukua kiapo kwa ajili ya kuingia daraja la tatu, mikono yake yote miwili anaweka juu ya kitabu cha imani ya dini yake, (Biblia, Quran n.k), lakini pia kunakuwepo na alama kuu za kimasonia, yaani Bikari na Kipima pembe ambavyo navyo mwanachama ataweka mkono juu yake.


ALAMA KWA MASTER MASON







Alama ya Master Mason inalenga kuonesha adhabu ambayo mwanachama ataipokea endapo atakwenda kinyume na miiko ya jumuiya katika daraja hilo. Anapoweka alama hiyo baada ya kuchukua kiapo, huwa anaamanisha au kutamaka maneno haya,


“Mwili wangu ukatwe vipande viwili sawasawa, utumbo wangu utolewe na kisha uchomwe moto mpaka uwe majivu ambayo yatawanywe kwenye kona nne za dunia”


Alama hii yenye kuashiria kiapo cha kutisha, hufanyizwa kwa ishara ambapo mwanachama, hupitisha kiganja cha mkono wa kulia, kutoka kushoto kuja kulia na kwa kutumia dole gumba lake, kwa haraka sana, baina ya tumbo na kiuno chake.


TUBALCAIN


MSHIKO WA MASTER MASON






Mwanamasonia, atasalimiana kwa kushikana mikono na masonia mwenzake, kama salamu ya kawaida, kisha atapaswa kuweka dole gumba lake la mkono wa kulia, kwenye nafasi iliyopo baina ya nakozi ya pili na ya tatu, na atabonyeza kwa nguvu kwa kutumia dole gumba lake katika huo uwazi, na masoni mwenzake naye atafanya hivyohivyo.


KUMBUKA KATIKA HATUA ZOTE HIZO, KUTOKA KWA MWANACHAMA MTARAJIWA, MPAKA MWANACHAMA ATAKAPO KUWA ANAPANDA DARAJA MOJA BAADA YA JINGINE, MWANACHAMA HATOKUWA AKIFANYA HIZO ‘HANDSHAKE’ BALI WM na SD, NDIYO WATAKAO KUWA WAKIFANYA KWA MAANA YA KUMUELEKEZA, MTARAJIWA WAO NINI CHA KUFANYA, ANAPO ATAKIWA KUFANYA HICHO CHA KUFANYA, KATIKA WAKATI MAALUM, SEHEMU MAALUM NA MTU MAALUM.
HIVYO BASI, MAJIBIZANO KAMA YALIYO TANGULIA AWALI, BAINA YA WM na SD, YATAENDELEA NA KUFIKIA HATUA YA KUTAJA JINA LA AINA HIYO YA ‘HANDSHAKE’ NALO LITATOLEWA KWA KANUNI ILE ILE, KWA HERUFI AU KULIGAWA NUSU KWA NUSU.





KISHA BAADA YA HAPO WM atamgeukia mtarajiwa na kumuambia hivi “TUBALCAIN, NDUGU YANGU, NDIYO JINA LA MSHIKO HUU, (HANDSHAKE)

WANAO FANYIA KAZI 'HANDSHAKE' ZA KIMASONIA KATIKA KAZI ZAO ZA KILA SIKU ... WATU WA KWELI .... WATU WENYE MAJINA MAKUBWA... WATU WENYE MAJUKUMU MAKUBWA KITAIFA NA KIMATAIFA ... WATU WA 'WATU' .....




KUTOKA TEHRAN MPAKA CNN .... HATUACHI UTAMADUNI WETU ...


WAKUBWA WA DUNIA ...


VIONGOZI WA KIDINI ....


MUGABE NA WALE ANAO WAITA NI MAADUI ZAKE ....

OBAMA ENZI HIZOOOOO ....

Post a Comment

0 Comments