Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Sultan Feruze anajitetea mbele ya Sultan, Sehzade Mustafa anachinja mtu


Leo tuanze kuwaangalia walinzi wa Mustafa wakiendelea na msako wa nyumba kwa nyumba, katika msako huo wanafanikiwa kumkamata mtu mmoja wakimtuhumu kuhusika na njama za kumuua Mahmet, Hurrem akiwa pembeni ya Mehmet, Sultan Suleiman anafika na kumshika begani huku Hurrem akiushikilia mkono wa Sultan lakini akiendeleza maneno yake ya chuki dhidi ya watu wengine akihisi kwamba hayo yote ni njama ya Mustafa na mama yake, lakini Sultan anampinga.
Mahdervan hana raha kuhusiana na tukio hilo anazungumza na Mustafa baada ya kumwona naye akiwa haelewi kilichotokea ni matokeo ya nini, anaona kwamba hawezi kukwepa lawama kwa kuwa tukio limetokea mbele yake na ameshindwa kulizuia licha ya kuwa na ulinzi wa kutosha, lakini wanafarijiana mtoto na mama wanakumbatiana.
Hadija Sultana anamsubiri kwa hamu Ibrahim Pasha akitaka kumlaumu kwa alichokiona kwa Niger, lakini Ibrahim anafika na kumkumbatia ila anapotaka kutoka Hadija anamwita Ibrahim na kumhoji kuhusu alichoshuhudia, Ibrahim anakasirika anaondoka.
Rostima anafika kwa Niger Kalfa lakini anazidi kumjaza huzuni kwani analia muda wote anatoka nje Rostima anamkumbuka mama yake alivyofariki akimuacha bado mdogo aliyekuwa akihitaji malezi yake, anakumbuka alivyochukua kidani cha mama yake na kukitunza hadi sasa na bado hajampata mtu wa kumvisha.
Chozi la Hurrem linamdondokea Mahmet jichoni linamshtua na kuanza kurejesha fahamu zake. Sultana anafika na kumwona Sehzad Mahmet akizinduka. Lakini anachosema kinamuumiza Mustafa, anasema walikosana lakini wakati Mustafa anaondoka, alimwona mtu akimlenga na mshale akaamua kumwokoa kwa kujikinga yeye dhidi ya kaka yake, Mustafa anafurahia mno kusikia wema huo kwani licha ya utu aliuonyesha lakini pia unasaidia kuondoa sintofahamu za kwamba huenda ilikuwa njama ya kumuua Sehzade Mahmet. Mustafa anasogea pembeni anawaza
nani aliyetaka kumuua, akiwa katika mawazo hayo Sultan anafika anazungumza naye anamtaka awe mwenye kutenda haki kwa kila mtu. Niger anazungumza na Ibrahim Pasha lakini Pasha anaonyesha kutokutaka mazungumzo yao yaendelee wala kukutana mara kwa mara kwa kuwa hataki kumfedhehesha mke wake, Hadija Sultana.
Jaji Mkuu anafika kwenye klabu cha pombe anamkuta mlinzi mmoja akiwa amelewa anamtoa akitaka kufanya mapenzi na muuzaji wa ngono wakati anatoka naye nje, anawaona Ibrahim Pasha na watu wake wa karibu katika klabu hiyo anawaacha anaondoka zake anamchukua yule askari hadi kwake anazungumza naye.
Rostima baada ya kujifikiria aliyoelezwa na mama yake kabla hajafariki, anaamua kumpenda kweli Niger anarudi ndani anamfurahia Niger anataka kumbusu Niger anashangazwa na mabadiliko hayo anamkwepa. Sultan Suleiman anaaga watu wake kwa ajili ya safari lakini akiwa katika hatua ya kuagana Mihrima bado anazungumza na mwandishi wa mashairi wanapoagana mwanamashahiri huyo, anampa zawadi Mihrima ili amkumbuke daima katika maisha yake.
Mihrima anaaga huku akiwa na furaha wakati wanataka kuondoka Hurrem anashtukia jambo kwa mtoto wake anamwona mwanamashairi akitokea mstuni anahisi wanazungumza, Hurrem anaporudi Ottomani katika hali ya kustaajabu anakutana uso kwa uso na Feruze, Feruze anamdhihaki Hurrem kisha anakwenda moja kwa moja hadi kwa Sultan anamkumbatia wanazungumza, Hurrem anamwita Sumbula anamkaripia kwanini Feruze bado yupo Ottoman wakati walishapatana aondolewe hapo.
Majigambo ya kumuumiza Helena yanaanza kwa Fatuma Hatum anapomuona Mustafa akizungumza na Hellena anamleta mtoto ili apate kuzungumza na Mustafa, Hellena anatoka anawaacha lakini Mustafa hamfurahii Fatuma Hatum.
Hurrem anafika kwa Rostima wanazungumza anamlaumu kwanini hakumuua Feruze lakini anajibiwa kwamba Feruze ana alama muhimu kwao anamuonyesha na namna itakavyowasaidia kupitia Feruze, Hurrem anafurahia. Hurrem anatumia nguvu anamteka tena Feruze anampeleka gerezani.
Mtukufu anapewa taarifa kwamba Feruze ametekwa na Hurrem anakasirika anamfuata Hurrem huku Hurrem akiwa ametuma watu wamlete akiamini Sultan atakuja kwake, Sultana anawakutanisha Feruze na Sultan anampekua kuhusu alama aliyonayo Sultan anashangaa muda wote huo hakufahamu kwamba ana alama hiyo.
Sultan anamuhiji Feruze anamgeukia anashindwa kujibu chochote.
Sultan anaondoka kwa hasira anamwita Ibrahim Pasha usiku akiwa amelala na Hadija anamfokea kuhusu Feruze, Ibrahim naye anakwenda kwa Feruze na kumfokea kwa kuficha nembo yake na uhalisia wake.
Hurem wote wanazungumzia kuhusiana na Feruze kufungwa gerezani, Hadija anapata taarifa hizo anakwenda moja kwa moja kwa Hurrem. Ibrahim baada ya kuzungumza na Feruze anarudi kwa mtukufu na kumweleza alichoelezwa kisha walinzi wanampeleka kwa mtukufu na kumuacha huko.
Cha kushangaza Sultan anamtaka hadi Ibrahim Pasha atoke nje abaki yeye na Feruze, Feruze anapojaribu kumsogelea Sultan, Sultan anamzuia kwa kumuonyeshea mkono wake anamtaka arudi nyuma asimsogelee kisha anaanza kuzungumza naye.
Feruze anajitetea mbele ya Sultan Suleiman lakini mwisho Sultan anatoa uamuzi wa cha kufanya kwa Feruze, Hadija Sultana naye anakasirishwa na Feruze anaruhusu apelekwe gerezani.
Wakati hayo yakitolewa kwa Feruze, Mustafa na jeshi lake wanagundua kwamba aliyerusha mshale uliokuwa na lengo la kumchoma Mustafa alikuwa ni yule mfanyabiashara aliyekuwa amemchumbia Hellena wanamkimbiza polisi wanamkamata Mustafa anashikwa na hasira anakamata upanga wa mmoja wa walinzi wake anamchinja mfanyabiashara huyo kisha wanaondoka zao.

Post a Comment

0 Comments