Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Mapenzi ya malkia Altin Can na Tugrul Bey

Mapenzi ya malkia Altin Can na Tugrul Bey

Katika historia yetu, kuna wanawake wengi mashujaa waliohusika kwenye uboreshaji wa jamii, sanaa, elimu na fani mbalimbali kwa kazi zao muhimu walizozifanya.
Lakini kwa bahati mbaya wengi wao hawajulikani kwa majina.
Mmoja wa wanawake hawa mashujaa ni Malkia Altun Can, aliyekuwa mke wa mfalme TuÄŸrul Bey katika utawala wa Selçuklu.
TuÄŸrul Bey alimpenda mkewe Malkia Altun Can kutokana na kazi zake pamoja na mchango wake ulioweka historia katika kulinda taifa la Selçuklu.
Kabla ya TuÄŸrul Bey, Malkia Altun Can alikuwa ameolewa na HarzemÅŸah kwa sababu za kisiasa na kupata mtoto wa kiume aliyeitwa Enusirevan.
Lakini baada ya HarzemÅŸah kufariki, Malkia Altun Can mwenye umri mdogo akawa ni mjane.
Mjane huyo alipendwa na kuheshimika katika jamii kutokana na tabia zake njema, ustaarabu na busara aliyokuwa nayo.
Mienendo yake hasa ujuzi wa kisiasa uliokuwa umemvutia TuÄŸrul Bey, pia ulivutia na kuhamasisha wengi.
Baada ya muda, mahusiano baina ya jamii ya HarzemÅŸah na Selçuklu yakaimarika na TuÄŸrul Bey akapata fursa ya kufahamiana vizuri na Altun Can na kisha kuanza kumpenda. Kutokana na ujuzi wake wa kisiasa aliokuwa nao, TuÄŸrul Bey akawasilisha ombi la ndoa kwa Altun Can.
Malkia Altun Can akakubali ombi hilo la kufunga ndoa na mfalme wa Selçuklu.
Altun Can alikuwa ni mwanamke wa Kituruki aliyeweza kuendesha farasi na kushika upanga. Alikuwa ni mwenye asili ya utamaduni Asia ya Kati, aliyekuwa na ujasiri na uwezo mkubwa wa kumshauri TuÄŸrul Bey katika uongozi wake na kumsaidia popote alipohitajika.
Alikuwa akiendesha farasi na kurushwa mishale pamoja na mumewe katika mashindano. Kwa kifupi, walikuwa na maisha mema.

Jinsi Malkia Altun Can na TuÄŸrul Bey walipozidi kutunza ndoa yao, taifa la Selçuklu nalo lilizidi kuimarika na kuwa na nguvu zaidi.
Hata hivyo, uongozi wowote ni lazima ukumbwe na mitihani ya matatizo.
Katika kipindi hicho, Mmoja wa viongozi aliyejulikana kama Ibrahim Yınal, ambaye alikuwa ni nduguye TuÄŸrul Bey wa kambo akapata fursa na kusaliti taifa la Selçuklu.
Aliungana na viongozi wa Baghdad na maadui wa Selçuklu.
TuÄŸrul Bey aliyesalitiwa, alimwacha mkewe Altun Can kwa familia yake na kuanza kuwaandama wasaliti.
Lakini hakuweza kupambana nao kwa urahisi kutokana na kuchukuwa hatua kwa haraka bila ya mpangilio dhidi ya wasaliti na maadui wake.
Hatimaye akapinduliwa na kuangamizwa mjini Baghdad.
Malkia Altun Can alivunjika moyo baada ya kupokea habari hizo na kuanza kuwaza atakalofanya kwa ajili ya mumewe aliyempenda kwa dhati.
Mtu mwengine aliyeumiza na tukio hilo kama Malkia Altun Can alikuwa ni Khalifa Abbasi.
Khalifa Abbas alikuwa na hofu kuhusu utawala wa Selçuklu kutokana na pengo lililoachwa na TuÄŸrul Bey.
Mwishoni akaamua kushauriana na viongozi wengine wa Selçuklu na kuchukuwa uamuzi wa kumrithisha kiti cha kifalme mtoto wa Malkia Altun Can.

Altun Can Hatun alipinga vikali uamuzi wa kurithishwa kwa mwanawe kiti kilichoachwa na mumewe TuÄŸrul Bey aliyedaiwa kuuawa.
Malkia Altun Can alikuwa na uwezo wa kuongoza na hata kufanya utawala wa Selçuklu kuwa na nguvu zaidi.
Lakini moyo ulikuwa umezongwa na maumivu ya kumpoteza mumewe TuÄŸrul Bey.
Khalifa Abbasi alishirikiana na Altun Can na kuwaandama viongozi wote waliohusika na maadui na kumsaliti mumewe. Vile vile Malkia alijizatiti kuepuka mitego na njama zote za kisiasa alizochezewa TuÄŸrul Bey wakati wa uongozi wa taifa.
Hatimaye akatupwa gerezani kwa kuonekana kuwa tishio kwa uongozi wa mwanawe aliyekuwa Sultani.
Kutokana na ujasiri wake aliokuwa nao, akaunda jeshi na katika jamii ya Türkmen na kuwa amiri mkuu wa jeshi.
Alikuwa mstari mbele na farasi wake pamoja na upanga katika msafara wa kumsaidia mumewe TuÄŸrul Bey.

Baada ya kujipata ana kwa ana na wasaliti, Altun Can alifanikiwa kuwapindua wote.
Kisha akamuokoa mumewe TuÄŸrul Bey aliyekuwa bado yuko hai na katika hali mbaya.
Hatimaye akarudisha utawala wa Selçuklu mikononi mwa mumewe na kulinda kutokana na maadui waliotaka kuuvunja na kugawanya.
Altun Can akawa ni shujaa aliyeheshimika kwa ukombozi wa taifa la Selçuklu kama alivyokuwa mumewe Tuğrul Bey.
Historia inapoandikwa, lazima kutakuwa na kipengele flani kinachohusiana na mapenzi ya dhati ya watu maalum ambayo ni hamasisho kwa watu wengi. Mapenzi ya dhati ni ya kujitolea kwa hali na mali. Hayawezi kukatwa hata kwa ncha ya upanga wala kuvunjwa kwa vita vya kijeshi.
Mapenzi ya Altun Can yalikuwa ni ya dhati mno na yaliweza kuonekana wazi kabla ya kifo chake. Altun Can aliyeugua maradhi yasiyokuwa na tiba, alimuita TuÄŸrul Bey kabla kuaga dunia.
Alimwachia TuÄŸrul Bey wosia huu:
“Baada ya mimi unaweza kufanya chochote kile unachopaswa kufanya kwa ajili ya kumuoa binti yake Khalifa.
Kwa namna hiyo, utakuwa umetekeleza wajibu wako hapa duniani na kesho ahera.”
Je, mapenzi ya dhati ni ile hali ya kumtamani mtu aliyeondoka wakati unapompenda? Mapenzi hudumu milele na milele. Umpendaye anapofariki pia hukumbwa moyoni kutokana na mapenzi ya dhati yaliyoko?
Malkia Altun Can alimwachia mumewe mali zote kama zawadi ya harusi yake na binti yake Khalifa.
Baada ya kuzikwa kwa Altun Can katika mji wa Altun Can Rey, kifo cha kiongozi TuÄŸrul Bey kilifuatia na kurudisha huzuni tena katika jamii ya Selçuklu.


Post a Comment

0 Comments