Header Ads Widget

Responsive Advertisement

JERAHA LA HISIA - 4



Simulizi : Jeraha La Hisia
Sehemu Ya Nne (4)

Ghafla akaruka mbali kama aliyepigwa shoti. Akatokwa na yowe kubwa la hofu. Yowe ambalo lilimkurupua Walter kutoka katika usingizi mzito.
Lilian alikuwa kama aliyeona jinamizi.
Jina la Naomi ambaye anaamika kuwa huenda amekufa kutokea katika jina lake hali hii ilizua utata.
Lilian akamshirikisha Walter, naye akapagawa na kujisahau kuwa wote wapo uchi bado.
Haraka Walter akathubutu kumpigia simu Naomi aweze kusema naye lolote.

Simu ya Naomi haikuwa ikipatikana.
Kama alivyohangaika Naomi, Lilianna Walter nao walihangaika vilevile bila kufanikiwa lolote.
Lilian alikuwa wa kwanza kujishtukia kuwa yu uchi baada ya kuyatazama maungo ya Walter.
Walter naye akashtuka. Ghafla ukafuata mchezo wa kugombania nguo, kila mmoja akachagua yak wake na kuvaa.
Wakatazamana usoni pasipo kusema lolote. Aibu zao zilienda zikipungua.
Wakatazama chini kila mmoja akifikiria lake.
Lilian akathubutu kumkabili Walter, hii ni baada ya taaluma yake kumpa majibu kuwa sasa Walter hakuwa yule Walter wa Mbeya, huyu wa sasa alikuwa ana hisia za kimapenzi japo zilikuwa katiuka mashaka aidha ni sahihi ama si sahihi.
Lilian akamfikia Walter, akaketi kando yake.
Aliamini kuwa nguo yake nyepesi kabisa isiyokuwa na kitu ndani italiruhusu joto lake kupenya katika suruali ya Walter.
Hakika ilikuwa hivyo.
Walter akasisimka, hakusema neno lolote.
Daktari alikuwa ameisoma akili yake tayari.
Mara mkono laini wa Lilian ukajizungusha katika shingo ya Walter.
Walter akawa ametulia tuli.
Mara ule mkono ukakosa utulivu. Ukatambaa hapa na pale. Walter akaanza kuhema juu juu.
“Lilian….” Mara akatokwa na sauti ya kukwaruza isiyojiamini hata kidogo. Lilian akajibu kimahaba.
“Mpenziii….” Sauti laini ikatamka.
Mkono wa Lilian ulikuwa ukipima mapigo ya moyo jinsi yanavyokwenda kasi, jina hilo likaongeza kasi ya moyo wa Walter zaidi.
Lilian akajipongeza kwa kuwa mtaalamu wa mambo ya saikolojia na akiolojia.
Walter hakuwa na ujanja tena.
Lilian akaitazama picha ya Naomi ukutani, hisia za chuki juu yake zikajengeka. Akahisi mwanadada yule akishirikiana na dada yake walimuambukiza Walter Ukimwi, na sasa naye ameukamata.
Aliamini kuwa hata kitendo cha Naomi kukimbia huku na kule ni kukwepa aibu ya kukutana na Walter kisha kuweza kujieleza chanzo cha mabaya yote waliyomtendea.
Wabaya sana wanawake hawa…alilaumu bila kufungua mdomo wake.
Kinachongojewa ni kifo tu.
Lazima nife nikiwa nimeifurahisha nafsi yangu….alijisemea Lilian.
Hisia za daktari huyu ambaye aliamini kuwa kwa namna yoyote ile naye ni muhanga wa kifo cha mateso na karaha.
Hisia potofu zikamwandama kuwa ni heri kufa akiwa amefurahia haswaa starehe hii iliyompa tiketi ya kifo.
Lilian akajiona kuwa alikuwa mjinga kutaka kujiua ilihali hata dalili za Ukimwi zikiwa hazijajitokeza.
Wakati akiwaza haya hakujua kama alikuwa akifanya papaso maridhawa katika kifua cha Walter na Walter naye alikuwa amezizima huku mikono yake ikipalangana huku na kule kulifunua gauni la Lilian.

Hisia nd’o kitu pekee ambacho husababisha mapenzi. Hisia kamwe hazizungumziki kwa njia ya mdomo. Hisia husema kupitia moyo kwa njia ya macho.
Mioyo ikizungumza kamwe hakuna cha kuzuia, hata wahusika wasiposema wao kwa wao lakini mioyo yao itasema na hatimaye watajikuta katika majaribu na hatimaye mapenzi ya dhati.
Ni hisia hizi zilinena katika moyo wa Lilian kisha zikanena pia katika moyo uliopondekapondeka wa Walter.
Hisia hizi zikawaleta katika hali waliyopo kimya kimya.
Mioyo ikazungumza ikisema kuwa inahitaji faraja.
Nani wa kusema HAPANA iwapo moyo umesema ndio?
Sasa hapakuwa na hisia za ‘supa shafti’ wala hisia za ‘mvinyo’ sasa zilikuwa hisia halisi. Hisia ambazo zilitwaa jina la Naomi na kulirusha mbali kisha kusahaulika kwa wakati.
Halafu likafuata lile tendo lililowahi kutokea mara mbili hapo nyuma.
Lilian na Walter penzini.
Safari hii walikongojana hadi chumbani.
Kitanda kilekile ambacho Naomi pekee aliruhusiwa kukitandika vyema na kukilalia akiwa na mumewe, sasa alikuwa anaingia mbadala wake.
Dokta Suzi (Lilian).

****

WAKATI Lilian na Walter wakikipa suluba kitanda ambacho siku nyingi kilikuwa hakijapata misukosuko Naomi alikuwa akiangaza huku na kule huku hasira ikifurukuta kifuani mwake.
Wivu ulijikita haswaa katika mahali husika.
Wivu huu ukamjaza hasira, na chuki dhidi ya Dokta Suzi. Lakini bahati mbaya mlengwa hakuwepo.

Naomi hakuwa na uelekeo maalumu lakini lengo lake lilikuwa kurejea mahali alipofikia kisha akiwa chumbani ampigie tena simu Dokta na kisha kujaribu kumchimbachimba kama atagundua lolote kuhusu mahali ambapo mwanamke huyu anamficha Walter wake.
Akiwa anangojea taksi ya kumrejesha mahali alipofikia.
Akasikia sauti ya mwanaume ikimuita. Japo haikutaja jina lakini alimini kuwa yule mtu alikuwa anamuhitaji yeye.
Alitaka kupuuzia lakini akajikuta akijishusha na kugeuka.
Akakutana na mwanaume mwenye kitambi cha pesa, suti yake safi ikiwa imemkaa mwilini. Kwa mtazamo wa haraka Naomi akahisia kama amewahi kumuona mahali.
“Mimi?” aliuliza Naomi baada ya kugeuka.
“Yah ni wewe dada…samahani kidogo…” Mwanaume mwenye kitambi alijibu. Naomi akamngojea.

Mwanaume yule akajikongoja taratibu huku akifanya tathmini yakinifu ya ni kwa namna gani atamchombeza mwanadada huyu.

Jicho lake lililojaa matamanio lilimuona tangu alipoingia katika ofisi ya ushauri nasaha na kupima. Akatamani kumuwahi juu kwa juu lakini akasita na kugundua kuwa njia ile haikuwa nzuri.
Akangoja hadi alipomaliza, wakati Naomi anatoka yeye aliingia ofisini.
Ni hapa ambapo Naomi alimuona kwa mara ya kwanza.

“Jesca…..vipi huu mtambo ulikuwa na ishu gani…..” mwanaume yule aliuliza kwa kunong’ona huku akiinamia meza ya yule muhudumu aliyekuwa peke yake pale ndani.
Muhudumu yule badala ya kujibu, alicheka kwanza. Kisha akamtazama yule bwana mwenye suti.
“Dokta Kibwana mhhhh……hupitwi we mwanaume.” Alimwambia .
“Hiyo mali mpya haki ya nani…..sijawahi kuiona….alikuwa anasemaje huyo.”
“Alikuwa anamtaka Suzi…..bahati mbaya hajamkuta. Nahisi kavurugwa huyo walah.”
“Ehee hao hao waliovurugwa nd’o huwa nawapendaga….kwa hiyo hajampata Suzi nd’o anaondoka hivyo.” Aliuliza Kibwana.
“Nd’o hivyo, lakini kuwa makini, anaonekana mjanja kweli.”
“Nani? Mjanja? …hakuna mjanja mbele yangu aisee tangu Sophia anisumbue wakati siyajui mapenzi nd’o basi tena sitasumbuliwa tena…….ngoja sasa namfata…” alizungumza kisha akamuaga yule muhudumu ambaye alikuwa ameshazizoea tabia za Kibwana. Tabia zilizoibuka baada ya kusalitiwa na mchumba wake, siku mbili kabla ya kumtolea mahari.
Jambo hili likampagawisha. Kibwana akageuka kimatendo, akaanza kuwa dungadunga. Maneno yake matamu yalikuwa ulimbo wa kunasia wasichana ambao alikutana nao eneo lake la kazi.
Hadi kufikia siku hiyo alikuwa ametoa mimba za wasichana sita ambao alikutana nao hospitali akawachombeza na kisha wakamvulia nguo na hatimaye kunasa mimba.
Kibwana hakuwa na mtoto hata mmoja.

Kibwana alimtazama vyema Naomi, akavutiwa na mitikisiko ya nyama zake za paja na juu yake zaidi.
Kama ilivyokuwa kawaida yake kurukia wasichana kwa kuwakamatia hapo hapo hospitali, Kibwana akamuweka Naomi katika hadubini yake.
“Anaonekana mtamu huyo…” Kibwana alijisemea huku mate yakimjaa mdomoni.
“Mambo dada….”
“Poa sijui wewe.” Alijibu Naomi huku akiwa katika mshangao kidogo.
“Ahh kwangu safi tu….ulikuwa unamuulizia Suzi nimeambiwa, yaani ile naingia tu na wewe unatoka. Yule msaidizi wangu amenambia nikaona si haba ngoja nikukimbilie maana Suzi alidai kuwa akija mtu nimsikilize mimi na ni mimi pekee naweza kutoa majibu mazuri.” Alijinadi Kibwana. Alitumia jina la Suzi kwa kuamini kuwa daktari huyo ana ‘kismati’ cha kupendwa na wagonjwa na pia ni daktari ambaye anafahamika sana kwa huduma zake.
Kama maneno ni karata basi Kibwana alikuwa amemlambisha Naomi galasa, huku yeye akiwa na kadi nne mkononi.
Naomi alikuwa anamuhitaji huyo Suzi kuliko Kibwana ambavyo angeweza kudhani.
Naomi akafanya kosa kubwa. Kuutangaza waziwazi mshawasha wake. Kibwana akang’amua kuwa dada yule alikuwa katika shida kubwa.
Kibwana akaanza kuzuga huku na kule kana kwamba anataka kitu ili aweze kumfikisha Naomi kwa Dokta Suzi. Ilihali alikuwa anafahamu waziwazi kuwa Suzi hayupo mkoani Mbeya.
Naomi akagundua kuwa hapo ilihitajika rushwa. Akajaribu kumtajia dau. Kibwana akaruka maili mia.
“Mimi pesa za nini sasa. Nina pesa nyingi na vile sina ndugu nahisi zimekuwa mzigo kwangu. Pesa zinanikera sihitaji kabisa kusikia kuhusu kuongezeka. Zimenitoshja zilizonazo.” Alijishaua bwana Kibwana.
“Sasa tunafanyaje kakangu.” Alijiweka mahali ambapo Kibwana alipahitaji. Mahali hapa palifanana na kibra.
“Hebu njoo huku..” Kibwana akatoa maelekezo. Naomi akamfuata.
Wakalifikia gari aina ya Noah.
Kibwana akalifungua na kuingia katika siti ya mbele, Naomi akaingia siti ya nyuma.
Kibwana akawasha gari wakaondoka kwa mwendo mfupi kiasi.
Gari likaegeshwa mahali tulivu.
Maongezi yakaendelea.
“Kwani wewe una shida gani na Dokta.” Kibwana alimuuliza Naomi.
Naomi akashindwa kutoa jibu sahihi.
Akabaki kujiumauma.
“Nahitaji tu kumuona” hatimaye alijibu.
“Ni ishu ya kiofisi ama…”
“Hapana ni ishu binafsi kabisa…” Naomi alinong’ona
Kibwana akalitazama paja la Naomi kupitia kioo. Akatamani kulishika lakini akahofia msimamo wa Naomi, hakujua kama ni wa kawaida ama wa bei ghali.
Kimtazamo, binti huyu hakufanania na wale wa Mbeya palepale anaokutana nao mara kwa mara.

Naomi alikuwa ameliachia maksudi paja lake.
Baada ya daktari yule kugoma kupokea rushwa ya pesa, changudoa huyu wa zamani alitambua kuwa bwana huyu alikuwa akihitaji rushwa ya ngono ili aweze kupayuka anachokijua.
Ngono kwa Naomi….hilo halikuwa swali kwa miaka kadhaa nyuma. Lakini sasa alikuwa na pete kidoleni.
Alisita lakini akagundua kuwa hakuwa na ujanja wowote ule katika jiji la Mbeya.
Naomi akauvaa uchangudoa wa miaka ile.
Akalegeza macho na sauti, akazidi kukaa vibaya.
Ujumbe bila sauti ukamfikia Kibwana.
Akaruka siti moja na kumfikia Naomi katika siti ya nyuma.
Vioo vilikuwa vimetiwa nakshi ya utepe mweusi usioruhusu kuonekana kwa ndani. Na mahali lilipokuwa limeegeshwa hapakuwa na mipito ya watu mara kwa mara.
Kibwana akajiona amelamba dume. Akaufikisha mkono katika paja la Naomi, mara akatambaa huku na kule.
Tatizo moja Kibwana alidhani Naomi ni kama wasichana waliopita, hakujua kuwa huyu alikuwa mzoefu.
Ulimi wa Naomi ukapenya katika sikio la Kibwana, mikono ikasafiri huku na kule. Kibwana wa watu hoii.
Baada ya muda Kibwana alikuwa anafundishwa tofauti kati ya mapenzi na ngono.
Kama ni chuo nd’o kwanza alikuwa anasaidiwa kuweza kupata walau cheti cha awali. Kibwana hakuwa lolote mbele ya Naomi.
Ni katika kuandaliwa huku Kibwana akajikuta anaropoka kila kitu hata ambavyo Dokta Suzi alimzuia.
“Yule Suzi yule, alikuja kuchukua oooh gari yake huwa anapaki kwangu..huko Uyole…yeeeh Landruiser moja hivi alinunuliwa na bwana yake kwa sasa ni marehemu… huko alikuwa na kijana oooh ye…kijana mmoja simjui sura lakini….nikimuona namjua…..walikuwa wanaelekea Dar….yeees walikuwa wanaenda Dar…..” Kibwana akaropoka kila kitu, Naomi akawa ananasa, muonekano wa kijana uliotajwa na Kibwana ulikuwa muonekano wa mumewe Walter.
Wivu ukampa pigo maradufu lakini alimtimizia Kibwana haja zake.
Wakamalizana Naomi akaondoka zake.
Kibwana akabaki na stori ya kukumbukwa kwa kipindi kirefu katika maisha yake.
Alikuwa kwa mara ya kwanza amefanya mapenzi katika gari, na kwa mara ya kwanza alikuwa amekutana na msichana anayejua ngono.



Kibwana hakutaka kuendelea kung’aa macho mjini, aliendesha gari yake kwa mwendo wa wastani akarejea nyumbani kwake ambapo alikuwa akiishi na mdogo wake.
Alikuta tayari akiwa ameandaa chakula.
Akaanzia kuoga kwanza kisha akajongea mezani na kupata chakula. Mdogo wake alishangazwa sana na jinsi ambavyo kaka yake huyo aliwahi kurudi nyumbani. Kwa kuwa walikuwa wamezoeana aliamua kumuuliza.
“Nimechoka sana tu halafu kuna wajinga wamenivuruga.” Alijibu kwa ufupi huku akielekea chumbani.
Kibwana alikuwa amechoka haswa. Lakini hakuchoka kwa sababu ambazo alizisema, Kibwana alikuwa amechoshwa na manjonjo ya Naomi katika gari muda mfupi uliopita.
Alipokuwa amejinyoosha kitandani alimuwazia binti yule, akaupimia ujuzi wake.
“Hivi ingekuwa kitandani ingekuwaje?” alijiuliza Kibwana huku akijirusharusha hapa na pale katika kitanda chake.
Wakati akiendelea kujirusharusha Kibwana akakumbuka kitu ambacho kilimwondolea uchovu na kumuingiza katika mawazo mapya. Mawazo yanayofurahisha.

Licha ya kuwa aliwahi kubadili wasichana wengi hasahasa baada ya kutendwa na mpenzi wake wa kwanza. Kibwana hakuwahi kuwachoka wasichana hawa.
Misemo ya ‘utachagua mabucha na bado nyama itabaki ileile haikumuingia akilini hata kidogo. Kibwana aliamini nyama inaweza kuwa ileile lakini mapishi yakawa tofauti. Na utofauti huu nd’o uliomfanya asichoke kuwabadili wasichana.
Katika mfululizo huu, Kibwana alifanikiwsa kuwakamata wagonjwa, wauguzi na hata madaktari wenzake wa kike alifanikiwa kustarehe nao kwa siri na kisha wanasahau kama waliwahi kushiriki tendo hilo.

Kibwana na tamaa zake alijikuta akigonga mwamba kwa daktari Suzi. Hapa alijaribu kila mbinu lakini wala Suzi hakubabaika wala kuonyesha dalili ya kumkubalia Kibwana. Kuna wakati Kibwana alimtangazia Suzi kuwa atamuoa. Lakini bado binti yule hakushawishika.
Baada yam bio zake kuishia ukingoni, alibakia kula kwa macho kila anapomuona Suzi kazini.
Ulimbwende wa Suzi, haukumtoa mate Kibwana peke yake, hata madaktari wengine walijaribu kupigana vikumbo lakini mwisho wa siku walikutana katika kijiwe kimoja na kukiri kuwa ‘Dokta Suzi ni kiboko ya viboko’.
Hakuna aliyefanikiwa kumteka kimapenzi.
Baada ya zoezi hili kushindikana ndipo walipojiingiza kimya kimya katika kumtafuta mwanaume ambaye amempagawisha Suzi hadi kumfanya kuwa ngangari kiasi kile.
Cha kusikitisha hata huyo mwanaume mwingine hakupatikana.
Wanaume wa Dar es salaam wakahisi kuwa Suzi atakuwa ana mwanaume mkoani Mbeya ambaye amemkamata daktari huyu akili na wale wanaume wa Mbeya wakiambatana na madaktari waliamini kuwa kwa asilimia zote Suzi alikuwa na bwana jijini Dar es salaam ambaye alikuwa anampa kila kitu. Hivyo kumfanya asibabaike na chochote.

Kibwana aliumizwa sana na hali hii ya kumkosa Lilian (Dokta Suzi). Lakini akaamini kuwa ujuzi wake wa kuchezesha maneno ili kumnasa mwanamke yalikuwa yamefikia pomoni na kama angeendelea zaidi basi angeleta sera za uongo wa waziwazi ambao kwa msichana mjanja kama Dokta asingeweza kumnasa.
Kibwana akasalimu amri akaamua kuishi na Suzi kama marafiki tu.
Urafiki huu ukapelekea Dokta Suzi kuwa na tabia ya kwenda kumtembelea Kibwana na mdogo wake maeneo ya Uyole. Urafiki ukakolea kwa tabia ya Kibwana kumtambulisha Suzi kwa wanawake wake kama dada yake wa pekee.
Dokta Suzi akapata wimbi la mawifi.
Mawifi hawa wakamzidishia asilimia za ukaribu na Kibwana. Hatimaye zile hisia za Kibwana kuwa na Suzi kimapenzi zikakoma.
Hatimaye Suzi akawa anaenda kulala nyumbani kwa Kibwana.
Wakati Kibwana analala na mdogo wake yeye alikuwa analala chumba cha wageni.
Suzi, Kibwana na mdogo wake wakawa kama ndugu wa familia moja. Suzi akasahau kuwa Kibwana alikuwa akimtaka kimapenzi, hatimaye wakawa wanapeana siri mbalimbali.
Daktari akimtongoza Suzi, basi lazima wakutane na Kibwana kwa ajili ya kushirikishana kisha wanamcheka mtongozaji.
Haba na haba hatimaye Dokta Suzi akawa anamshirikisha siri zake kadhaa. Undugu ukazidi kukomaa.
Ulinzi ulioimarika katika nyumba ya Dokta Kibwana ukamshawishi Suzi kuwa anahifadhi gari lake kila anapotaka kusafiri.
Na hata mara hii alipolihitaji gari, hakusita kumshirikisha Kibwana juu ya safari yake ya dharula kuelekea jijini Dar es salaam.

Hisia ni kitu kibaya sana, hisia husinzia katika nafsi lakini kamwe haziwezi kufa.
Hisia zikisinzia unaweza kudhani kuwa hazitatokea tena maishani. Lakiini siku zinapoibuka nd’o muhusika hugundua kuwa alijidanganya kuwa zimekufa.
Ni wapendanao wengi sana hulia na nafsi zao pale wawaonapo wapenzi wao wa zamani wakiangukia katika mikono mingine kimapenzi.
Kamwe huwa hawatangazi kilio chao hadharani, lakini mioyo huwaambia kuwa hisia zilizolala…zimeamka tena.
Hisia haizikwi kamwe, hisia hufa pale ambapo muhusika huacha kuhisi.
Muhusika akipata ganzi ya milele na hisia nazo hulala jumla.
Hisia hufa muhusika akifa.

Siku hii ambayo Kibwana aligundua kuwa dokta Suzi anasafiri akiwa na mwanaume kisirisiri katika gari lake, hisia ziliinuka kwa kasi na kusimama wima kisha zikaanza kuuchapa vibao moyo wake.
Kibwana mpenda vimwana akajikuta anamwaga machozi.
Hisia za kimapenzi kwa dokta Suzi zilikuwa zinaishi na mbaya zaidi zilikuwa na afya tele tena komavu.

Sasa akiwa katika kitanda chake anaijiwa na wazo ambalo alimini kuwa kama kweli litaenda anavyotaka basi lazima afanikiwe kulidaka penzi la Suzi.
Kibwana alimuwaza Naomi na jinsia livyoonyesha kuwa ana shida sana na dokta Suzi.
Heri nusu shari kuliko shari kamili…….
Kibwana akaamua kujaribu.
Akanyanyua simu yake akabofya jina la dokta Suzi. Simu ikaanza kuita.
Mara ikapokelewa.
“Nani huyo…..” sauti ya kiume ilisikika ikimuuliza Suzi. Lakini badala ya kujibu Suzi akakata simu.
Kibwana alijikuta katika hasira kali.
Alijua kabisa kuwa hana mahusiano na Suzi lakini bado hakuweza kuziongoza hasira zake. Hasira zisizokuwa na maana.
Akiwa bado anatafakari mara dokta Suzi alipiga simu.
Kibwana hakutaka kuonyesha hali yoyote ya kutaharuki.
“Mambo dokta….kwema huko?”
“Kwema tu…..nisamehe, nilifika salama sikukutaarifu.”
“Hata usijali sana….ni mambo ya kawaida tu….”
“Ehe nambie za Mbeya? Upo home?” aliuliza Lilian (Dokta Suzi)
“Nipo home…Mbeya kwema sema kuna ishu moja hivi….aaahn upo peke yako?” alihoji Kibwana.
“Nipo peke yangu nambie tu..”
“Unamfahamu Naomi?”
“Naomi?” badala ya kujibu naye aliuliza.
“Ndio, msichana mmoja mnene kiasi, black beauty kimtindo, ana kithembe kwa mbali ……”
“Namjua vipi kwani nawe unamfahamu Kibwana?”
“Unamfahamu vipi?” Kibwana aliuliza kwa utulivu.
“Kibwana jamani amefanyaje?”
“Unamfahamu vipi nimekuuliza?”
“Sikia Kibwana….elewa kuwa ninamfahamu…..elewa tu hivyo siwezi kusema zaidi ya hapo.” Dokta Suzi alijibu huku akiwa ametaharuki sana.
Kibwana akaifurahia hali ya dokta kutaharuki, alijua kuwa mtego wake umekaribia kufyatuka na kumnasa ndege mjanja.
“Anakutafuta..vipi una ishu naye?” Kibwana akamtwika dokta swali zito.
“Ananitafuta? Ooh Mungu ..Kibwana yupo wapi?”
“Kuna baya lolote?”
“Kibwana kwenye simu siwezi kusema lolote.”
“Fanya fasta basi uje Mbeya.”
“Mbeya Kibwana?”
“Basi tukutane Morogoro…..”
“Poa kesho basi……”
“Poa.” Simu ikakatwa.

Lilian alikuwa katika mshtuko wa hali ya juu baada ya kumaliza kumsikiliza Kibwana.
Hakutegemea kuwa Naomi anaweza kuwa na mtandao mpana kiasi hicho hadi kumfikia Kibwana jijini Mbeya kwa lengo la kumtafuta yeye.
Sio kwamba Lilian alimuogopa Naomi sana, hapana. Kubwa alilokuwa akihofia ni jeraha la hisia.
Jeraha lake lilikuwa linapona katika namna ya maajabu makubwa.
Jeraha hili hakika lilikuwa limepata daktari wa kulitibu.
Tatizo alikuwa ni mume wa mtu.
Walter.

Lilian kwa siku chache za kulalaia kitanda kimoja na Walter alijikuta katika farijiko la namna ya kipekee.
Lilian alitambua kuwa yeye ni muathirika na Walter pia ni muathirika hivyo walikuwa sahihi kuwa wapenzi.
Na ladha halisi ya mapenzi aliyoipata kwa kuwa katika kifua cha Walter ilimfanya ajisikie amani.
Sasa anamsikia tena Naomi akiwa hai na anamtafuta.
“Huyu Malaya amejuaje kuwa nipo na Walter?” alijiuliza huku akijifunga kanga vyema kiunoni.
Lilian akalaani sana taarifa hiyo ambayo ilikuwa imemuharibia siku.

Akiwa anapiga hatua kuelekea chumbani mara akapinda kushoto akaingia jikoni. Huko akaketi katika kigoda kilichokuwa pale jikoni.
Pepo mchafu akajisogeza na kuketi jirani kabisa na yeye alipokuwa.
Pepo yule akamnong’oneza Lilian kuwa anahitaji kuingia katika moyo wake, Lilian akasita kisha akamruhusu kuingia moyoni mwake.
Pepo yule aliyeonekana mpole sana wakati anajiweka jirani na Lilian sasa akaianza tabia yake mbaya ya kulazimisha mambo.
Pepo akajivua gamba na kuanza kumwongoza Lilian.
Mara pepo akatoa amri katika moyo wa Lilian.
“Naomi hatakiwi kuonana na Walter…wakionana naye basi na huo nd’o unakuwa mwisho wa penzi lake kwako..si unajua mwenzako ana pete kidoleni……” sauti hii ikapenya katika masikio ya Lilian. Daktari huyu akajaribu kujizuia asipelekeshwe na hisia hizo.
Pepo mchafu bingwa wa kung’ang’aniza akatafuta mbinu nyingine, sasa akachokonoa huku na kule akakutana na jeraha la hisia. Pepo yule akalitonesha.
Hapa akawa amemaliza kila kitu.
Lilian akapagawa, jeraha lile la hisia likaanza kumsulubu.
Kwanini asulubike wakati njia ya kuliponya jeraha hili ilikuwepo??
Lilian akafikia maamuzi ya kukubaliana na pepo.
Akajipanga kumweleza Walter juu ya safari hiyo ya dharula sana.
Lilian akaamua kwenda kukutana na Kibwana ili aweze kumpata Naomi kabla Naomi hajampata yeye.

*****

GARI TATU zilikuwa zote katika barabara ya lami. Gari moja likiwa linaendeshwa na mwanamke na mengine mawili yakiwa yanaendeshwa na wanaume.
Upande wa kwanza mwanaume mmoja alikuwa anatabasamu huku akitikisa kichwa kufuatisha midundo ya muziki uliokuwa ukitoka katika redio ya kisasa iliyofungwa katika gari lake.
Kila mara alikuwa akicheka mwenyewe na kujiona mshindi sana.
Alikuwa akifikiria jinsi atakavyotumia maneno matamu kumshawishi binti wanayeenda kukutana naye aweze kumpa penzi. Baada ya miaka kadhaa hatimaye ile siku ya kuzishusha hisia zake zilizomsulubu kwa muda mrefu ilikuwa imefika.
“Atajua kwa nini niliitwa Kibwana..yaani nikimkamata, duh!! tena yule Naomi keshanipa maujanja mbona huyu Lilian atanikoma…hapa nina hakikisha kuwa nikimpa dozi moja asichomoke tena milele….” Kibwana alikuwa anazungumza kwa sauti ya juu. Hakujali maana alikuwa peke yake katika gari lake.
Upande wa pili, mwanamama alikuwa amepagawa lakini alijipa ujasiri wa hali ya juu ilimradi tu awe makini barabarani. Licha ya ujasiri huo bado alikuwa ana mawazo lukuki juu ya tukio ambalo atalifanya ili kumuweka Naomi mbali na Walter.
Alijiuliza ni kwanini Naomi alikuwa akimtafuta kwa udi na uvumba na ni kwa jinsi gani ameweza kukutana na Kibwana. Maswali haya yalimweka katika utata.
Utata mkuu ulikuwa pale alipofikiria kuwa Naomi hapatikani katika simu. Lilian akahisi huenda Naomi naye amejipanga kimashambulizi.
Gari liliendelea kuitawala barabara ya Morogoro katika mwendo wa kasi.
Lilian alikuwa peke yake ndani ya gari lake aina ya Landcruiser na alikuwa katika safari ya kwenda kukutana na Kibwana mjini Morogoro.
Lilian alimuacha Walter akiwa amelala bado chumbani mwake.
Katika nafsi yake alikiri kuwa jeraha lake la hisia halijawahi kumtesa kama linavyomtesa sasa.
Ilikuwa lazika kulitibu.

Upande wa tatu, mwanamke aliyejitanda kilemba kilichofanana na nguo alizokuwa amevaa alikuwa katika Pajero jekundu, wakikatisha milima ya Kitonga kwa mwendo mkali. Pajero hili halikuwa la kukodi lakini lilikuwa la mtu binafsi, alikuwa na safari yake kuelekea jijini Dar es salaam akahitaji abiria kadhaa wenye haraka ya kusafiri ambao watamsaidia kuchangia mafuta yatakayowawezesha kufika jijini.
Binti mmoja akavutika na safari ile, mkononi alikuwa na tikiti (Ticket) ambayo ilimruhusu kusafiri alfajiri ya siku inayofuata kurejea jijini Dar es salaam.
Lakini tangazo la mpiga debe kulinadi Pajero jekundu lilimvutia, akajifanya yu na mambo yake ya hapa na pale huku sikio lake likiwa wazi kusikiliza pajero likinadiwa.
Taratibu akavutiwa, akajisogeza katika pajero na kuulizia kana kwamba hana haja na safari ile.
Dereva akampa maelezo. Akazidi kuvutika.
“Kuna mizigo yangu hotelini kama tutaipitia hapo sawa..”
“Yaani hata kama itakuwa nyumbani kwako sisi tunaipitia dada…” alijibiwa.
“Unaitwa dada nani vile…” mpiga debe aliyekuwa anamuandikia tiketi hewa yule dada alimuuliza.
“Andika Naomi.” Alijibu yule dada.
“Una jina zuri sana aisee hata hii safari itakuwa nzuri.”
Yule dada akajikita katika gari, baada ya nusu saa wakaondoka, wakapitia hotelini. Akachukua mizigo yake.
Safari ya kuelekea jijini Dar es salaam ikakolea.

Naomi alikuwa na lengo moja tu, kumkomesha dokta Suzi (Lilian) iwapo amejimilikisha mume asiyekuwa wake.
Safari nzima alikuwa kimya, aliongea neno moja moja sana. Akili yake haikuwa hai katika gari lile. Ilikuwa imekufa kabisa. Na ilipofufukia ni maili nyingi mbele.
Naomi alikuwa akiwaza namna ya kumkabili Walter na Lilian.
Moyoni aliomba kimyakimya Walter asijekuwa ameanza maisha katika nyumba yao na mwanamke yule.
Hisia za mapenzi ya dhati juu ya Walter zikatambaa huku na kule katika kuta za moyo wa Naomi.
Hisia hizi zikamzidishia hasira.
Ilikuwa lazima aliponye jeraha lake hisia kwa kulipigania penzi lake.




****

Majira ya saa tano asubuhi gari aina ya Noah iliyokuwa katika uongozi wa Kibwana wa vimwana iliwekwa katika maegesho ya hoteli ya kifahari mji kasoro bahari Morogoro.
Milango ikafunguliwa akatelemka kijana machachali. Akaitazama kwa chati thamani ya hoteli ile, macho yake yakakiri kuwa mbunifu wa mandhari atakuwa ni mtu wa kipekee sana. Tena wa aina yake.
Miti ya matunda mbalimbali ilitia nakshi ya kipekee katika bustani ile.
Ubunifu wa sehemu ya kuegesha magari nao ulikuwa wa aina yake.
Eneo la maegesho lilikuwa kubwa haswaa.
Akiwa bado anasadifu mandhari mara alishangaa mbele yake akifika msichana mrembo, mavazi yake yalikuwa na muhuri. Muhuri ule ulifanana na nembo ya hoteli ile.
Hoteli Nashela.
Na yule dada alikuwa ni maalum kwa ajili ya mapokezi ya awali kabla ya kufikishwa katika mapokezi kuu.
Tabasamu lake pana lilipitiliza midomo ikafunguka.
Alikuwa na mwanya.
Kibwana akajaribu kutabasamu pia.
Yule dada akamuongoza hadi mapokezi.
“Karibu Nashela hotel.” Sauti nyororo ikamnong’oneza.
Akatabasamu tena.
Ana kwa ana na muhudumu wa mapokezi, akasikilizwa haja yake.
Akafanya malipo, akapatiwa chumba.

Baada ya kufanya utalii wa macho katika chumba chake kwa siku hiyo. Kibwana akatwaa mkonga wa simu iliyokuwa pale mezani.
Akatazama namba kadhaa, akaipata namba ya jikoni.
Akaagiza chai ya maziwa na vitafunwa kadha wa kadha.
Akapewa robo saa ya kusubiri.
Kibwana akautumia muda huo kumtumia ujumbe kimwana wake wa siku hiyo. Lilian.
Akamweleza juu ya hoteli hiyo ambayo amefikia, akakumbuka kumweleza na chumba ambacho amefikia.
Lilian hakujibu.

Licha ya kuuona ujumbe wa Kibwana, hakutaka kujibu chochote. Kwanza gari ilikuwa katika mwendo mkali.
Kuachia usukani na kujibu ujumbe ni sawasawa na kuweka rehani roho ambayo haina mbadala wake.
Lilian akaendelea kuendesha kwa kasi lakini makini sana.
Akaupita mzani wa Mikese huku jicho lake likitapakaa katika safu ya milima ya Uluguru.
Alikuwa ameukaribia mji kasoro bahari. Morogoro.
Mji ambao aliamini kuwa anaenda kupata silaha ya kupambana na adui yake namba moja katika kupigania tiba ya jeraha la hisia.

Baada ya dakika kadhaa akaingia mjini Morogoro.
Hakuwa mwenyeji sana lakini haukuwa mji mkubwa wa kumtisha.
Akaegesha gari pembeni kidogo. Akaufungua ujumbe wa Kibwana.
“Kumbe yupo Nashela??” alijiuliza Lilian kisha akaifunga simu akawasha gari.
Alikuwa anaifahamu hoteli ile, mara yake ya mwisho kulala mjini Morogoro alilala katika hoteli ile.

Baada ya dakika kumi na tano alikuwa mapokezi.
Simu ikapigwa, Kibwana akamruhusu mgeni wake kuingia ndani.
Lilian akapiga hatua moja baada ya nyingine, hakuhitaji uongozaji wowote alikuwa anakifahamu chumba hicho kutokana na uzoefu wake wa mara ya mwisho kufika hapo.
Akaufikia mlango, Kibwana aliyekuwa makini kusikiliza hatua zinazojongea pale mlangoni akafungua mlango.
Alikuwa amevaa suruali yake na juu akiwa kifua wazi.
Lilian akaona aibu kidogo kumtazama. Lakini akajipa ujasiri kuwa Kibwana hakuwa na lolote baya la kumfanyia.
Akaingia ndani.
Mlango ukafungwa.
Lilian na Kibwana, ana kwa ana katika mji wa Morogoro.

****

Pajero jekundu, lilithibitisha kuwa ni gari la shughuli pevu. Lilikatisha milima na kushuka katika mambonde bila wasiwasi wowote.
Naomi aliufurahia mwendokasi ule. Mwendo ambao ulimsahaulisha kabisa nauli ambayo alikuwa ameilipa hapo kabla kwa ajili ya kupanda basi siku iliyofuata.
Dereva alikuwa mchangamfu sana, hakuishiwa maneno ya kuwafanya abiria wake watabasamu na wao kujikuta wakizungumza wao kwa wao.
Naomi naye kwa furaha ya mwendokasi ule alijikuta akijumuika na abiria wengine kupepeta midomo.
Maongezi mengi yakasababisha safari nayo ionekane kuwa fupi sana.
Majira ya saa tatu asubuhi, jiji la Dare s salaam lilianza kunukia.
Dereva aliendelea kulitendea haki Pajero lake.
Na hatimaye saa nne na dakika kadhaa abiria wa kwanza akashuka Kibaha, kisha nusu saa baadaye mwingine akashuka Mbezi mwisho.
Foleni za hapa na pale asubuhi.
Majira ya saa tano na dakika kadhaa Naomi alikuwa katika taksi iliyokuwa inampeleka nyumbani kwake.
Kwa wakati ule alikuwa anaishi kwa hisia pekee zilizokuwa zinamtuma chochote cha kufanya mbele yake.
Hisia zilimtuma kwenda nyumbani kwake.
Kadri teksi ilivyokuwa inakata mitaa naye akazidi kuingiwa na vitu viwili kwa pamoja.
Hofu na hasira kuu.
“Nishushe hapa.” Aliomba Naomi.
Kisha akamlipa dereva pesa yake, akaanza kujikongoja kwa mwendo wa miguu. Machoni alijiziba kwa miwani nyeusi.
Mapigo ya moyo yalikuwa kasi sana. Alikuwa katika hofu ya kufumania. Hofu ya kukuta talaka katika ile meza ambayo wakati anaondoka aliacha ujumbe kwa ajili ya Walter.
Sala za Naomi zilikuwa zikimsihi Mungu amuepushie aibu ya kukuta kile chumba chake kikiwa katika utawala wa mwanamke mwongine.
Tena mwanamke mwenyewe ni daktari Suzi.
Naomi hakuwa tayari.
Mara akavutiwa na mzee mmoja aliyekuwa anauza mapanga, majambia na visu vikubwa.
Naomi akamsimamisha.
Akatazama vile visu vilivyokuwa vinawakawaka kwa makali.
Akanunua kimoja.
Si kwamba hakuwa na kisu ndani ya nyumba yake. Hapana.
Aliwaza kuwa huenda nyumba ipo katika utawala wa mwanamke mwingine hivyo alitakiwa kuingia kwa shari.
Ilikuwa ni aidha kuua ama yeye afe akilipigania penzi.
Mlinzi!! Hiki nacho kilikuwa kikwazo kingine.
Vipi ikiwa mlinzi amezuiwa katukatu asimruhusu mtu anayeitwa Naomi asipenye katika mlango wa kuingilia? Naomi alifadhaika kwa kufikiria jambo hili, lakini akapiga moyo konde.
Akalifikia geti, akasukuma.
Waaa. Likafunguka.
Akafanya tabasamu hafifu. Kisha akapiga hatua moja akawa anatazamana na nyumba yake.
Hapa tena akajikuta anakata tamaa. Alihisi nyumba ipo kama alivyoiacha siku chache zilizopita. Ilikuwa imepooza sana.
Mategemeo ya kumkuta mumewe ndani ya nyumba yakafifia.
Akajihisi yu katika mateso ya nafsi na alikuwa akipungua uzito kwa kasi. Licha ya kupungua uzito alikuwa hawezi kupiga hatua moja ya ziada mbele.
Miguu ilikuwa mizito sana.
Akajikaza akajisogeza hadi akaingia katika sebule yake kubwa.
Kama alivyopaacha palikuwa vilevile. Hii hali nayo ikamkatisha tamaa.
Akiwa katika kutembea akahisi kuwa kuna kitu alikuwa amekikanyaga na kikavunjika.
Akaunyanyua mguu na kisha akageuka.
Macho yakamtoka pima.
Alikutana na heleni.
Heleni ya nani? Akajiuliza.
Haikuwa ya kwake…..
Kwa hiyo Walter ameleta mwanamke ndani ya nyumba yangu? Naomi alijiuliza.
Akainama kuichukua ile herein.
Macho yake yakasafiri hadi uvunguni. Akaona chupa tupu ya mvinyo.
Akausogeza mkono wake katika chumba. Mara ghafla akaruka maili moja mbali. Kuna kitu alikiona na kilimshtua zaidi kuliko kumshangaza.
Ilikuwa chupi ya kike.
Mfanowe bikini.
Hata hii haikuwa ya kwake.

Hapa sasa akapagawa. Imani thabiti aliyokuwanayo kuwa Walter ni mumewe na mguu wake ulikuwa katika nyumba yake na mumewe ikaanza kuyeyuka.
Kisu chake akakiona kuwa kilikuwa kinawashwa kufanya kazi moja tu.
Kazi ya kuua.
Akakichomoa kile kisu. Akakitazama kwa makini kama kuna maandishi fulani alikuwa anayasoma. Kisu kilikuwa kinang’ara.
“Naua mtu…” akasema na nafsi yake.
Sasa akapiga hatua moja baada ya nyingine kwa kunyata.
Hakuwa na hofu tena.
Aogope nini wakati kuna mwanamke katika himaya yake anataka kumdhulumu kile anachoamini kuwa kiliumbwa kwa ajili yake.
“Bibi popote ulipo kama jambo hili ninalotaka kufanya ni sahihi basi liache litokee, kama si sahihi nionyeshe usahihi ni upi, yule mume uliyenitabiria ana mke mwingine katika nyumba yangu, nyumba yangu na ninahisi wapo katika kitanda changu, naumia moyo unakufa ganzi, nina haki gani mimi bibi, nina haki gani?....nionyeshe njia sasa” Naomi alisema tena na moyo wake.
Sasa alikuwa amekikaribia chumba kikuu.
Mitikisiko ya kitanda ikamshtua, akakodoa macho.
Ni kweli alitegemea kukutana na hali kama ile katika chumba chake, tayari alikuwa ameona heleni, kisha akaona chupi ya kike aina ya bikini.
Yote haya yalimuaminisha kuwa ndani ya nyumba yake kuna mwanamke. Lakini cha kustaajabisha bado alikuwa na imani kidogo iliyosalia katika moyo wake. Aliamini kuwa huenda heleni na chupi hivyo vyote viliingia bahati mbaya ama ni vya kwake aliwahi kuvisahau katika mazingira hayo.
Sasa anasikia mitikisiko ya kitanda katika chumba chake.
Je na hapa ni kiuno chake aliwahi kukisahau chumbani??
Hapana….
Naomi alikuwa anatetemeka.
Ghafla akakikumbuka kifo cha Maureen jinsi alivyofia katika mazingira ambayo lawama zote zilikuwa juu yake.
Japo si yeye aliyeua, sasa alikuwa tayari kuzichukua lawama moja kwa moja za mauaji.
Naomi alikuwa ameamua kuua.
Akajitikisa kidogo kupima kama alikuwa na nguvu za kutosha.
Kitanda nacho kikaendelea kutikisika kwa fujo. Naomi akakumbuka jinsi walivyokuwa wakifurahishana na Walter katika namna ya kukitesa kitanda kile ambacho kilikuwa imara sana.
Mishindo iliyokuwa inatoka enzi zile nd’o hii alikuwa akiisikia kwa sikio lake mwenyewe akiwa nje ya kile chumba kile.
Walter alikuwa anazini na mwanamke mwingine.
Naomi akautazama mlango kwa makini akafedheheka.
Wawili hawa walikuwa wanafanya uzinzi kwa amani kabisa huku mlango ukiwa wazi.
Akahisi kitu kikimkaba kooni, akakosa pumzi, alipojaribu kumeza mate ili kulainisha hicho kitu.
Akajikuta anatokwa na machozi.
Machozi mazito.
Machozi ya uchungu usiozuilika.
Lile jeraha la hisia likageuka kidonda komavu.
Donda ndugu.
Naomi akajikuta analegea, akaangukia magoti yake.
Chozi zito likatua katika marumaru.
“Waltaaaaaaa………unaniua Waltaaaaa….” Naomi alisema kwa sauti ya juu, akidhani yupo wa kumsikia, kumbe sauti ile iliishia katika moyo wake. Mdomo ulikuwa umefumba.
Naomi akapapasa tena katika koba lake. Akaibuka na kile kisu alichokinunua.
Roho wa kuua kama aina ya kisasi akamvaa.
Akasimama imara, akajifuta machozi.
“Naua…” akasema haya huku akikilamba kisu kile.
Akajiandaa kwa shambulizi la kukivamia chumba.

****

LILIAN alikaa katika kiti, Kibwana akaketi kitandani.
“Naomi yupo wapi?” Lilian (Suzi) aliuliza.
“Usiwe na haraka Suzi..twende hatua kwa hatua.” Kibwana akaanza kumchombeza Dokta.
Papara za dokta Suzi kuruhusu macho yake kuwa na wasiwasi zilimpa nafasi Kibwana kutambua kuwa ni kiasi gani binti huyu alihitaji kujua jambo kuhusu Naomi.
“Nieleze kila kitu kuhusu Naomi ili name nikushirikishe kinachoendelea maana nahisi hili jambo sio dogo dah maana….” Kibwana alisema huku akijaribu kulifanya jambo lile kuwa gumu.
Dokta Suzi akaingia mkenge akaanza kuelezea harakati zake za kutaka kumnyang’anya Naomi mume na kuwa wa kwake, alijieleza kila kitu mbele ya Kibwana.
Kosa kubwa sana…..

Kibwana akautumia mwanya.
“Suzi….nimezungumza na Naomi…kwa kirefu, hatua aliyoifikia ni mbaya sana kwako na kwa huyo mwanaume….yaani mbaya sana ndo maana nikafanya kukutafuta upesi na sikuwa mjinga sana kukufuata hadi huku. Nakupenda sana na ninapenda uendelee kuwa hai.” Dokta Kibwana akamtishia Dokta Suzi.
Ubaya ni kwamba hawa wawili walikuwa madaktari, Kibwana alijua kucheza na Suzi asiweze kujua kama analaghaiwa.
Kwa hili aliweza kumshinda.
“Sasa tunafanyaje Dokta…..” Suzi alimuuliza.
“Njoo hapa…” Kibwana akamuita. Dokta Suzi kama msukule unavyoongozwa naye alifanya hivyo akajiweka pembeni ya ubavu wa Kibwana.
“Unajua Suzi…” Kibwana alianza kuzungumza huku akiutua mkono wake katika bega la Suzi.
Suzi akajifanya hajaguswa na kitu chochote.
Kibwana hakuwa na lolote la kusema, alionekana alichokuwa anahitaji. Alimuhitaji Suzi kimapenzi.
“Dokta…nipe nikupe…..nina mazito ya kukupa, sasa nipe ili nikupe” Kibwana alizidi kuchombeza.
Suzi hakuwa na hisia zozote za kimapenzi na Kibwana.
Hisia zake zote zilikuwa juu ya Walter.
Kibwana alikuwa anahitaji penzi kwanza.
Dokta Suzi katika mtihani.



Suzi alitatanishwa na kauli ua Kibwana….kauli ya nipe nikupe….kauli hiyo ilijawa na sintofahamu. Kiutu uzima tayari alikuwa ameelewa ni nini Kibwana alikuwa anamaanisha lakini kiutendaji hakutaka kuiruhusua akili yake hata kidogo kufanya hivyo.
Kibwana alikaa kimya akimsubiri Suzi aseme neno lakini Suzi hakusema lolote.
“Mbona kimya…kwani kuna mtu anatutazama hapa jamani.” Kibwana alimuuliza Suzi kwa sauti iliyotangaza tamaa iliyopitiliza.
Suzi alimtazama Kibwana kwa jicho lililojaa kiulizi. Mara Kibwana akamshika kifuani Suzi. Suzi akajihisi anadhalilishwa sana.
Akataka kumtoroka Kibwana lakini akahisi kuwa huo si uamuzi sahihi hata kidogo. Alikuwa anahitaji kujua kitu fulani kuhusiana na Naomi ili awe amejiweka katika nafasi nzuri kimapambano.
Suzi akaendelea kukereka na mpapaso wa Kibwana.
Suzi aliamini kuwa akijitetea kuwa ameathirika na gonjwa la Ukimwi kwa jinsi anavyozijua tamaa za wanaume katu asingeweza kuaminika. Pia aliamini kuwa huo utakuwa mwanzo wa kujikita katika hatia ya kufanya mauaji ya maksudi.
Dokta hakuwa tayario kujiingiza katika hatia hiyo. Akafaikiria jambo la mwisho ambalo linaweza kumuepusha na hatia hii.
“Tumia kinga…” alijikuta akitokwa na kauli hiyo. Kauli pekee ambayo kwa wakati ule aliamini kuwa ilikuwa sahihi. Daktari huyu alitambua fika kuna madhara yanaweza kujitokeza licha ya kutumia kinga lakini kwa eneo alilokuwepo na shida aliyokuwanayo huo ulikuwa uamuzi wa mwisho. Huruma ilikuwa inamuongoza Lilian.
Kibwana akakurupuka upesi upesi. Alikuwa amejiandaa kwa kila kitu mzoefu huyu wa mambo.
Akaibuka na pakiti ya ‘kondom’.
Nafsi ikamsuta sana dokta Suzi kwa kitendo ambacho alikuwa amenuia kukifanya. Lakini kabla hajabadili mawazo yake Kibwana wa vimwana tayari alikuwa amemvamia pale na kumwangusha kitandani.
Kibwana akafanya kwa papara kubwa.
Dokta Suzi hakupatwa na hisia zozote wakati wa tendo hilo zaidi ya kukereka maradufu.
Wakati Kibwana anaendelea kurukaruka huku na kule Suzi akajikuta anaingiwa na hisia nyingine tena, Kibwana alikuwa ni mropokaji sana.
Hofu yake ikawa kwamba, bwana huyu anaweza kwenda kumtangazia kila mtu kuwa amezini na yeye.
“Akishaniambia kuhusu Naomi namfanyia kitu ambacho hatakaa asahau maishani mwake.” Dokta Suzi aliwaza. Huku kichwani akiwa na jibu tayari la nini atafanya kumkomesha Kibwana.

****

BAADA ya Lilian kutoweka katika chumba kile akimuacha Walter nyuma, Walter alifikiria mambo kadha wa kadha juu ya maisha yake. Akaifikiria familia yake ambayo ilimsaliti na kumtoroka ikimuacha peke yake duniani.
Akamfikiria na Naomi ambaye alikuwa muhimili pekee lakini sasa naye amefanania na msaliti. Lakini msaliti anayeishi.
Walter hakutaka kumfikiria sana Naomi akajikita katika kuyafikiria mahusiano mapya aliyoyaanzisha na Lilian kwa muda wa hizo siku chache. Mahusiano haya kabla hayajawa mahusiano ya kimapenzi yalikuwa yakimfariji sana Walter.
Walter akaamini kuwa Lilian ni msichana sahihi sana kwake.
Kwanza alionyesha nia ya kulipigania penzi la Naomi ambalo kwa mwanamke mwingine asingejishughulisha hata kidogo.
Lilian alipambana sana hadi jitihada ziliposhindikana.
Akiwa anawaza haya Walter akajikuta anapiga mwayo mrefu.
Hapo akatanabaisha kuwa alikuwa na njaa.
Akaamua kujitoa kitandani, akasimama wima akiwa na bukta yake.
Akafikiria ni nini atakula.
“Mama Kessy sasa hivi tayari ameshachoma chapati sijui..” alijiuliza Walter. Kisha akakumbuka kuwa binafsi hakuwa na pesa katika mifuko yake.
Tangu wanatoka Mbeya ni Lilian alikuwa akimuhudumia.
Akiwa anawaza hayo mara akaiona nguo ambayo Lilian alikuwa ameivaa siku moja iliyopita.
“Hakosi masilesile huyu najua.” Alijipa imani ya kukuta chochote kitu katika mifuko ya Lilian.
Akaitwaa nguo ile. Akaanza kupekue.
Mfuko wa kushoto akakutana na noti nyekundu nyekundu.
Hizi hakuwa na nia nazo alihitaji pesa ndogo tu.
Akahamia mfuko wa kulia.
Akapekua akakutana na makaratasi mawili.
Noti ya shilingi mia tano na karatasi jingine jeupe lililokunjwa.
“Asijekuwa na mabwana wengine” wivu ukamshambulia Walter. Akaweka kando ile pesa na kujikita katika kufunua kile kikaratasi ajue kina nini.
Karatasi ikafunuka bila tabu.
“Nakupenda Walter, nisamehe kabla haujafa.”
Karatasi iliandikwa maneno haya.
Lahaula!!
Walter akatumbua macho, ule ulikuwa mwandiko wa kipenzi chake, kipenzi chake cha dhati Naomi……
Walter akawa kama anayetamani kusema na mtu lakini angesema na nani. Chumba kizima alikuwa peke yake.
Jasho likaanza kumtoka na akajiona waziwazi jinsi ambavyo alikuwa anatetemeka.
Kikaratasi kile kimefika vipi katika mifuko ya Lilian?
Huyu mwanamke kuna jambo ananificha? Amekutana na Naomi mahali halafu ananipaka mafuta kwa mgongo wa chupa? Walter alitaharuki.
Chuki ikajijenga ghafla juu ya upendo kisha ikamtia katika hali ya hasira.
Uongo ni sumu katika penzi, ni heri udanganye hautaumia sana siku ya kuusema uongo wako lakini ole wako udanganywe kisha ugundue kuwa siku zote uliishi katika chumba kimoja na muongo.
Ni heri usihi na mchawi, akikukata ulimi unatambua kabisa nd’o sheria zao.
Lakini muongo hana alama…….muongo hana sheria za kudanganya.
Na madhara ya uongo ayajuaye mdanganywaji.

Walter alijaribu kufuta kumbukumbu zote alizowahi kushiriki na Lilian lakini katu hazikufutika.
Mbaya zaidi alikuwa amefanya naye uzinzi mara kadhaa.
Uzinzi katika kitanda cha Naomi.
Naomi mkewe wa ndoa. Walter akajihisi yu katika dhambi kubwa kupita zote alizowahi kuzifanya tangu azaliwe.
Tena dhambi hii ameifanya kwa mtu ambaye anampenda kwa dhati.
Naomi hakuwa msaliti kama alivyodhani, Naomi aliupigania upendo wake kwa juhudi zote, na hata ujumbe huu aliuandika akiwa katika kuthibitisha kuwa penzi lake lipo hai bado.
Walter akajisikia aibu kuu. Akaghafirika na kujiona hastahili lolote lkatika hii dunia.
“Ama kwa hakika Tanzania hunipendi….Tanzania ungenipenda usingeniliza kila siku…usingeniumiza namna hii..ni mimi wa kutyokwa machozi kila mara, Tanzania unanipa tabasamu la bandia kila siku, unanifanya nifikirie ni tabasamu halisi kumbe ni bandia….” Alilia Walter huku akilaani.
Alikuwa na ulazima wa kulaani. Imani yake kwa Lilian kama mtu sahihi sasa imegeuka kuwa adui mkubwa, Lilian hakuwa na ladha tena katika akili ya Walter.
Amemsaliti na kuwa muongo. Kwanini afiche hisia za Naomi??
Lilian alikuwa ni mnafiki.
Mnafiki ni sawa na muuaji wa kimyakimya.
Lilian alikuwa muuaji.

Iwapo Walter hana cha kumpa nafasi ya kutabasamu katika ardhi yake akajikuta katika shambulizi baya.
Shambulizi hili likampelekea kuwaza mbali sana. Akafikiria kuifuata furaha yake halisi.
Bibi, mama, baba na dada yake mpenzi.
Walter akaamua kujiua ili asafiri na kuwafikia viumbe pekee ambao walikuwa waaminifu kwake na hawakuwa na chembe ya unafiki hadi walipotoweka duniani.
Jicho lake likatua katika vidonge ambavyo hakuwa na haja ya kujua jina lake.
Akakimbia sebuleni na kuvamia jokofu akatoka na mvinyo asioujua jina vilevile.
Akaufungua mvinyo. Akashika vidonge vyote mkononi.
Akakitazama kikaratasi kilichoandikwa na Naomi.
“Naomi….nisamehe..nimekusaliti sana…..”
Alitokwa na maneno hayo.
Kisha kikafuata kitendo ambacho hufanywa na watu waliokata tamaa ama wepesi wa maamuzi.
KUJIUA………
Walter akaugida mvinyo kisha akabwia vidonge……
Mvinyo ulikuwa mkali haswaa.

*****

KITENDO cha Walter kutoweka na kutopatikana kwenye simu kwa muda mrefu kilimshangaza sana. Japo hatimaye aliamua kuzoea bila kuijua sababu rasmi ya Walter kutoweka nyumbani.
Mkewe hakuwa na maelezo ya kutosha, jambo ambalo lilizidi kumfedhehesha.
Kabla hali hii haijatulia linatokea tukio jingine la kushangaza. Naomi naye akatoweka hewani kwa muda wa siku kadhaa.
Namba yake ya simu haikuwa inapatikana.
Utaratibu ambao Naomi alikuwa amemzoesha wa kumpigia simu kila siku zaidi ya mara moja ulikuwa umemwathiri sana.
Sasa ilikuwa bni siku ya tatu na bado kimya kilitanda.
Hali hii ikamtia mashaka Suzi ambaye ni dada yake Naomi. Dada wa pekee.
Hali yake kiafya haikuwa mbaya sana tangu apate tiba mbadala kutoka kwa daktari ambaye wanafanana majina Daktari Suzi.
Lakini licha ya tiba hiyo, zile tabia za wagonjwa wa Ukimwi bado zilikuwa zinamtafuna. Hasira za kushtukiza na tabia ya kupenda kususa.
Suzi alikuwa amechukizwa na tabia hii ya ukimya na sasa alikuwa ameamua kwenda kumlaumu mdogo wake. Tiba ya hasira zake ilikuwa kumlaumu ama kmumtukana muhusika aliyezisababisha
Suzi aliamua siku hiyo kumtembelea Naomi kimya kimya bila kujalisha alikuwa anapatikana kwenye simu ama la.
Asubuhi sana aliamka na kuanza kufanya mazoezi kama ilivyo kawaida kisha akajisafisha mwili wake maliwatoni ,akajitengenezea, chai nzito akastafutahi, akameza dawa zinazohitajika.
Safari ikaanza baada ya kujivika mavazi yaliyomfanya apendeze sana.
Hakuambia mtu yeyote mahali ambapo alikuwa anaenda.

Akaifikia nyumba ya Walter na Naomi akiwa katika hali ileile ya kununa.
Akatazama ardhini akakutana na alama za matairi ya gari.
“Asubuhi yote hii ameenda wapi huyu mtoto…..” alijiuliza Suzi huku akianza kukata tamaa huku hasira yake nayo ikipanda maradufu.
Akaukaza mwendo.
Akaingia ndani kwa kulisukuma geti kisha akaliegesha hovyo bila kulifunga.
Cha ajabu akalikuta gari la dada yake. Walau matumaini kuwa Naomi yupo ndani yakarejea kwa kidogo. Matumaini haya hayakuipeleka mbali hasira yake.
Akafungua kwa fujo mlango wa sebuleni, akiwa amefura, mashavu yalikuwa yamevimbiana kwa ghadhabu kuu.
Akaangaza huku na kule akakutana na chupi katika upande mmoja wa sofa, akaichukua kwa hasira akaanza kuikanyagakanyaga, mwisho akaipiga teke ikaenda uvunguni.
Chupa ya pombe kali nayo ikamkera akaisukuma kwa mguu wake ikaanguka chini.
“Naomiiiii” akaita kwa sauti iliyotawaliwa na amri.
“We Naomiiii.” Akarudia tena.
Aliyeitwa hakujibu chochote.
Alikuwa anakifahamu fika chumba chake ambacho huwa analala na mumewe. Akapiga hatua huku akiwa na imani kubwa kuwa Walter hayupo.
Alipokikaribia chumba akasikia mitikisiko kwa mbali.
“Huyu Malaya kumbe yupo mimi namuita haitiki….” Suzi alijisemea kwa sauti ya chini. Akazidi kunyata kukikaribia chumba kile.
Hakika ndani ya chumba kile kulikuwa na mtu.
Suzi akakivamia kile chumba, mawazo yake yote alitegemea kumkuta Naomi.
Maajabu…..
Hakuwa Naomi..alikuwa ni Walter akigaagaa huku na kule kitandani.
Macho yalikuwa yamemtoka haswaa.
Suzi naye akastaajabu.
Wakawa wakishindana katika kutumbua macho yao.
Hali ya hatari.
Chupa ya mvinyo mkali ilikuwa imeanguka na mvinyo ulikuwa umemwagika chini.
Walter alikuwa anatapatapa huku akinyoosha mikono ya kuomba msaada..sauti yake haikutoka zaidi ya kukema tu.
Suzi hakutegemea kukutana na tukio la namna ile asubuhi ile.
Aliwaza na kuwazua, akatamani kupiga hatua kumkaribia Walter.
Miguu ikawa mizito sana. Akajikaza akamfikia, hakuwa na msaada wowote zaidi ya kumtikisa Walter ambaye hakuwa na haja ya kutikiswa zaidi ya kujitikisa mwenyewe kwa fujo pale kitandani.
Ama kwahakika roho ni kitu cha ajabu.
Haitoki kwa wepesi kama inavyoweza kudhaniwa.
Muhusika hupambana mpaka mwisho kuizuia isitoke lakini mwenye maamuzi anabaki kuwa Mungu.
“Shem…….Guda jamani Guda….” Alilalamika Suzi kwa sauti ya chini.

Malalamiko ya Suzi yalimfikia mwanamama aliyekuwa nje ya chumba cha Walter.
Naomi alisikia malalamiko haya huku mikito pia ikisikika.
Naomi akiwa nje ya ule mlango akawaza kuwa Walter alikuwa anafanya ngono na mwanamke.
Alipolisikia jina la ‘Guda’ moja kwa moja akatambua kuwa muhusika ndani ya kile chumba ni dokta Suzi. Kwani huyu pia alikuwa akimtambua Walter kwa jina hilo.
Hasira ikapanda maradufu.
Kisu kikali mkononi.
Roho ya kuua.



Suzi hakutegemea kukutana na tukio la namna ile asubuhi ile.
Aliwaza na kuwazua, akatamani kupiga hatua kumkaribia Walter.
Miguu ikawa mizito sana. Akajikaza akamfikia, hakuwa na msaada wowote zaidi ya kumtikisa Walter ambaye hakuwa na haja ya kutikiswa zaidi ya kujitikisa mwenyewe kwa fujo pale kitandani.
Ama kwahakika roho ni kitu cha ajabu.
Haitoki kwa wepesi kama inavyoweza kudhaniwa.
Muhusika hupambana mpaka mwisho kuizuia isitoke lakini mwenye maamuzi anabaki kuwa Mungu.
“Shem…….Guda jamani Guda….” Alilalamika Suzi kwa sauti ya chini.

Malalamiko ya Suzi yalimfikia mwanamama aliyekuwa nje ya chumba cha Walter.
Naomi alisikia malalamiko haya huku mikito pia ikisikika.
Naomi akiwa nje ya ule mlango akawaza kuwa Walter alikuwa anafanya ngono na mwanamke.
Alipolisikia jina la ‘Guda’ moja kwa moja akatambua kuwa muhusika ndani ya kile chumba ni dokta Suzi. Kwani huyu pia alikuwa akimtambua Walter kwa jina hilo.
Hasira ikapanda maradufu.
Kisu kikali mkononi.
Roho ya kuua.Naomi akakiweka sawa kisu chake ili aweze kuvamia. Akatumia mguu wake kuusukuma mlango kwa nguvu. Kisha kama anayeigiza filamu za mapigano akakikumba chumba.
Walter akiwa na bukta, mwanamke akiwa na kisketi kifupi huku akiwa katika jitihada za kumpepea Walter na kanga yake.
Mwanamke yule akashtuka na kugeuka.
Jicho kwa jicho, Suzi na mdogo wake wa kuzaliwa tumbo moja. Naomi akaangusha kisu chake chini, hakutegemea kumkuta dada yake katika chumba chake….
Wazo likakivamia kichwa chake, Suzi alikuwa anazini na mume wake, huyo Suzi ni muathirika wa gonjwa hatari la Ukimwi.
Naomi akaishiwa ujasiri, bila kusema neno lolote akalainika na kutua chini kama mzigo.
Ndani ya chumba chao, mtu na mkewe walikuwa matatani. Suzi aliyekuja kwa shari sasa alikuwa amefadhaika, alikuwa na shughuli pevu ya kufanya.
Lakini ataifanya vipi.
Mambo yalikuwa magumu sana.
Haraka haraka akaamua kukimbia nje aweze kupata msaada.
Akatimua mbio, akapita sebuleni lakini hakuweza kwenda mbali zaidi. Akakumbana na mtutu wa bunduki.
“Tulia…” aliamrishwa.
Mkojo ukatoka ulipokuwa umejificha kwa muda mrefu, ukadhani Suzi yupo chooni, ukaanza kutiririka bila soni yoyote. Suzi hakuwahi kuwekewa bunduki mbele yake, sasa alikuwa anatazamana na bunduki, na mtu aliyekuwa na bunduki ile hakuweka tabasamu lolote katika uso wake ambalo lingeweza kumfanya aonekane kuwa aidha ana utani ama vinginevyo.
Kumbe hakuwa mmoja, mara mwingine naye akafika. Alikuwa na bunduki vilevile.
Majambazi…wazo likamjia Suzi. Majambazi hawa walikuwa wamekuja kuivamia nyumba ile.
Bila shaka hataweza tena kuokoa roho mbili ambazo zimelala sakafuni.
Hali tete….mkojo ukaendelea kupenyeza.

****
SAMSONI MASHIMI, alikuwa katika dimbwi la mawazo, mawazo..mawazo ambayo kwa namna moja au nyingine nd’o mawazo yaliyomfanya maisha yake kuwa magumu katika nchi ya Tanzania.
Akiwa amehitimu kidato cha sita, Sam alikuwa mwingi wa habari na kupenda kufanya mambo ilimradi aonekane ameelimika. Alivaa akapendeza na kila jambo aliloshirikishwa alilijibu kutokana na maneno aliyofundishwa na mwalimu darasani.
Mtu alipokosea alimsema kwa kutumia vifungu kadhaa alivyofundishwa katika somo fulani darasani. Akitakiwa kutoa rushwa aweze kupata kazi alipinga kwa kutumia kipengele fulani.
Utata wa Sam ukasababisha akose ajira baada ya kuwa amefeli masomo yake kidato cha sita.
Akakimbilia Dar es salaam kwa ndugu yake. Huku napo akaendelea na hali yake ileile ya kujifanya anajua sana.
Ni kweli alikuwa anasimamia upande sahihi lakini usahihi huu ukamfanya aonekane kama amekosewa sana kuendelea kuwa mtaani badala yake alitakiwa kuwa muhudumu wa kanisa fulani. Kazi za kanisa zilikuwa zinamfaa zaidi.
Miaka ikakatika, ndugu lawama wakaanza maneno ya chinichini, kwa sababu alikuwa mtu wa kuchambua mambo akatambua kuwa tayari alikuwa ameonekana mzigo katika familia aliyopo.
Sam akaamua kuingia mtaani kutafuta kazi kwa udi na uvumba, huku akisahau kujirekebisha tabia yake ya kujifanya anajua sana.
Kazi ya ulinzi nd’o pekee ambayo aliweza kufuzu kutokana na uaminifu wake na u-kiherehere.
Akapangiwa kulinda nyumba ambayo alikabidhiwa kwa bosi mwanamke.
“Naitwa Naomi…” bosi yule alijitambulisha kwa jina lile.
Wakafahamiana mawili matatu, kisha kazi ikaanza rasmi.
Akiwa na miaka thelathini hii ikawa ajira yake ya kwanza, ajira ambayo ilimfanya ausubiri mwisho wa mwezi kwa hamu aweze kujipatia visenti kadhaa.
Hali ilikuwa shwari katika ofisi yake hiyo.
Hapakuwa na mtafaruku kutoka kwa mabosi wake. Aliifurahia hali hii.
Utata wa kwanza aliokumbana nao ni kutoweka ghafla kwa baba mwenye nyumba ile aliyeitwa Walter.
Huu nd’o utata wake wa kwanza kukumbana nao. Sam hakushtuka sana badala yake alifurahia kuongea kila kitu alichokuwea anakijua mbele ya polisi.
Akaaminika….
“Likijitokeza jambo lolote lenye utata usisite kutushirikisha.” Polisi walimpa kauli hiyo. Ikabaki kichwani mwake.
Siku zikakatika bila utata wote kutokea.
Hadi siku ambayo Walter alifika pale nyumbani akiwa na mwanamke mwingine.
Walter hakuwa na wasiwasi wowote, hali hii ilimtia sintofahamu yule mlinzi. Walidumu katika nyumba kwa dakika kadhaa kisha wakatoweka.
Mlinzi alitamani kutoa taarikfa baada ya wawili hawa kutoweka lakini alihofia maswali ya ‘kwanini hukusema alipoingia?’, Sam akaitunza habari hii.
Usiku wawili hawa walikuwa nyumbani pale.
Sam akakumbwa na roho ya kiherehere baada ya kusikia sauti ya muziki ikiwa juu sana, akazuga kuzunguka huku na kule kama anayefanya lindo. Akafanikiwa kupata upenyo wa kuona nini kinaendelea katika sebule ile.
Wawili hawa walikuwa wanasaidiana kuvua nguo.
Sam akavutiwa kisha akajisahau kama ni mlinzi. Akaweka macho yake sawa kutazama Walter na yule mwanamke walichokuwa wanatenda.
“Ina maana ameoa mke mwingine….” Alijiuliza. Huku akiwa na mashaka juu ya kutoweka kwa Naomi.
“Hapa kuna tatizo….si bure” aliwaza hivyo huku mkono wake ukijaribu kuiweka sawa suruali yake ambayo ilikuwa imenyanyuka kutokana na kile alichokuwa amekiona.
Siku iliyofuata Sam hakulaza damu, akajiahidi kwenda kituo cha polisi. Palepale alipochukuliwa maelezo siku ya kwanza.
Bahati mbaya kwa siku hii hakupata nafasi ya kuonana na yule mpelelezi wa kesi ile.
Lakini siku iliyofuata aliweza kuonana naye.
Kama kawaida akamwaga maneno. Askari yule akavutika na taarifa hiyo. Naye akatoa taarifa kwa wakuu wake.
Akapewa gari na askari kadhaa kwenda eneo la tukio.
Huu nd’o uzuri wa jeshi letu, hakuna kudharau adui, hata kama ni mwizi wa kuku lazima afuatwe na kundi la askari.
Njia sahihi kabisa, utajuaje silaha anayotumia? Ama utajuaje lengo lake?
Askari wakiambatana na yule mlinzi walifika nyumbani kwa Naomi na Walter.
Wakaizingira nyumba vizuri.
Vishindo katika nyumba ile vikawaweka sawa bin sawia.
Mara akatoka msichana.
Akaelekezewa bunduki.
Huyu alikuwa ni Suzi na sasa mkojo ukawa unamtoka.
Kizungumkuti…..

“Wewe ni nani na nani yupo ndani?” askari aliyevaa kiraia alimuuliza Suzi.
“Naitwa Suzi ni dada yake Naomi, wameanguka huko ndani….” Alijieleza huku akitetemeka.
Haraka haraka askari wengine wote wakiwa wamevaa kiraia waliingia ndani ya nyumba.
Wakakifikia chumba. Wakakutana na viwiliwili vikiwa vimetulia tuli pale ndani. Hatua za haraka zikachukuliwa, askari wakarejea garini na kuchukua mipira maalumu inayozuia alama za vidole wakajivika mikononi wakawabeba Walter na Naomi.
Safari ya kwenda hospitali.
Suzi alichukuliwa na kuhifadhiwa mahabusu kwanza.
Hiyo nd’o kawaida ya polisi. Haijalishi kama una kosa la moja kwa moja ama la kuhisiwa. Hifadhi yako ni mahabusu.

Wakati hekaheka hizi zikiendelea jijini Dar es salaam, katika mji kasoro bahari Morogoro Lilian (Dokta Suzi) alikuwa amekunja ndita akimuuliza Kibwana juu ya Naomi.
“Tuendelee kidogo basi mpenzi..” Kibwana alimbembeleza.
“Kibwana hayakuwa makubaliano yetu..tumeelewana nipe nikupe…” aling’aka Lilian.
“Sawa mpenzi lakini…” alinung’unika Kibwana huku akimpapasa dokta Suzi.
Ule uamuzi wa Suzi wa kupambana na Kibwana katika hali ambayo hatakuja kuisahau ulimjia tena.
Akatazama huku na kule akakutana na ‘remote control’ ya luninga.
Akaitwaa na kuongeza sauti ya luninga.
Kibwana hakujua maana yake ni ipi.
Mara Dokta Suzi akageuka, uso wake ulitangaza chuki…
“Kibwana unaniambia ama hauniambii nijue moja…”
“We nipe walau eeh dakika kumi tu halafu nakwambia..” Kibwana alitoa jibu la kitoto.
Dokta Suzi akakereka.
Ghafla mkono wake wa kuume ukatua katika korodani za Kibwana, Suzi akazikamata na kuziminya haswaa. Kibwana akakodoa macho yake kwa hofu.
Alipojaribu kufurukuta Suzi alizidi kuminya…..yowe kubwa likamtoka Kibwana lakini Dokta Suzi hakujali.
“Haya sema…” aliamrisha binti yule hapo akiwa yu uchi wa mnyama.
“Sikia dokta, kiukweli hajaniambia kwa nini anakutafuta lakini alikuja kukutafuta…” Kibwana akatoa jibu ambalo lilimwseka matatani. Suzi akageuka mbogo. Kumbe Kibwana hakuna alichojua ametumia mbinu tu kumnasa.
Suzi akazivuta Korodani za Kibwana katika namna ambayo aliijua ni misuli gani na gani ameiweka katika lengo.
Kibwana akatokwe na yowe kuu la mwisho.
Kisha kimya kikubwa kikafuata.
Kibwana ulimi nje……

Uzoefu wake wa miaka kadhaa ulimfanya asiogope kutazamana na maiti ama kitu chochote kinachokaribia kufanana na maiti.
Dokta Suzi alivaa nguo zake haraka haraka, kisha kwa taaluma yake ili kujiweka mbali na tatizo. Akachukua kitambaa na kuufuta mwili wa Kibwana. Alihakikisha kila mahali alipomgusa anamfuta.
Alifanya hivi kuondoa alama za vidole.
“Lazia afe huyu….” Aliapa huku akimtazama Kibwana ambaye alikuwa hayupo eneo lile kifikra.

Suzi hakuwa na muda wa kupoteza. Alipita upesi pale mapokezi bila kumruhusu mtu yeyote kuikumbuka sura yake.
Akaenda katika maegesho, mlinzi akamtambua na kumruhusu kuondoka baada ya kuonyesha kikadi chake.
Alipopewa kitabu cha kuweka sahihi kuwa amechukua gari lake ni hapa alimaliza mchezo.
Kwenye sehemu ya namba za gari, sehemu ambayo aliamini kuwa nd’o pekee inayoweza kumfunga hapo baadaye alibadili namba akaweka namba zilizomjia kichwani mwake.
Mlinzi hakupata nafasi ya kuligundua hilo, kwa mtazamo ilionyesha kuwa hapakuwahi kutokea wizi wa magari katika hoteli ile.
Baada ya hapo, moyo wake ukiwa na amani kabisa alitoweka.
Safari ya kurejea jijini Dar es salaam kukutana na Walter. Lengo likiwa ni kuondoka kwa muda katika jiji la Dar es salaam iwapo Walter ataafikiana naye.

Landcruiser iliishambulia barabara ya lami ya kutokea Morogoro mjini katika namna ya liwalo na liwe, mwendo ule haukuwa wa kawaida kwa jinsia ya kike katika usukani na hata kwa mwanaume pia ulitia mashaka.
Lilian alikuwa katika ghadhabu kubwa, alijua kuwa baada ya muda atakuwa anatafutwa kwa udi na uvumba lakini hii ni iwapo tu Kibwana atapoteza uhai.
Kama asipopoteza uhai basi hata akitafutwa hatatishika kwani atakuwa na sababu ya kujibu kuwa alikuwa katika kupambania utu wake baada ya bwana Kibwana kufanya jaribio la kumbaka.
Lilian aliombea Kibwana asiupoteze uhai wake. Kwani hakutaka kuingia katika mikono ya askari wasumbufu ambao watamuhifadhi rumande kwa siku kadhaa kabla ya kuanza kumhoji kwa maswali yanayojirudiarudia kila leo.
Lilian alitarajia kumweleza Walter kila kitu kuhusiana na Kibwana ili aweze kutumia tukio alilofanya kama ushawishi wa kumwonyesha Walter kuwa anampenda sana.
Lilian katika nafsi yake alikiri kuwa lazima atumie uongo fulani wa kumshawishi Walter kuwa katu Kibwana hakufanikiwa kufanya naye mapenzi.
Haya yote yalipita katika kichwa chake katika mwendo mkali sana kama gari ilivyokuwa inakimbia.
Wazo lililobakia ni kufika Dar akiwa salama.
Hatimaye ikawa hivyo, baada ya masaa mawili gari lilikuwa linazengeazengea kuyapita magari mengine yaliyoendeshwa na wasiokuwa na haraka maeneo ya Ubungo.
Baada ya kufanikiwa kuingia katika barabara iliyokuwa na magari machache hatimaye akaiona barabara ya kuchepuka, alikuwa analifahamu vyema jiji la Dar es salaam. Akaifuata hiyo.
Baada ya dakika nyingine ishirini gari liligeshwa mbali kidogo na nyumba ya Walter.
Lilian alifanya hivi kwa kujiwekea utabiri kichwani mwake kuwa huenda Naomi alikuwa katika nyumba ilea ma namna yoyote ile ya sintofahamu. Akaamua kwenda kwa miguu. Alitembea kwa hadhari kubwa huku akitazama kushoto na kulia.
Umati wa watu waliokuwa wakishangaa hapa na pale ulimfanya asite kuendelea mbele, machale yakamcheza.
Akababaika kidogo kabla ya kujichanganya nakuingia katika kundi la watu wengi wanaume kwa wanawake.
Wote walikuwa wakilitazama geti la kuingilia nyumbani kwa Walter huku mshangao ukiishi katika nyuso zao.
Lilian naye akazuga kushangaa huku akitega masikio yake yaweze kunasa kila neno litakalosemwa.
“Sijui wamekufa wale? Sijui yule dada aliyefungwa pingu kawaua?” mwanamke mmoja alijisemesha bila ujumbe wake kumlenga mtu mmoja.
Moyo wa Lilian ukapiga kwa nguvu sana. macho yakamtoka.
Akatamini kuuliza chochote yule mwanamke akawa amegeuka na kuzungumza na mtu mwingine. Bila shaka walikuwa wakifahamiana.
Kifo…
Ni kitu ambacho Lilian hakutaka asikie kikiwa kimemtokea Walter. Hisia zikanyanyuka wima na kukishambulia kifua cha Lilian.
Mara akaanza kulia. Hali hii iliyomtokea aliitambua kuwa ilimaanisha kuwa hawezi kuishi bila pendo la Walter.
Yule mwanamke amehofia kuwa kuna watu wamekufa katika nyumba ile…..
Nani sasa amekufa? Ni Walter ama?
“Yule pale kamfumania mume wake na msichana mwingine….yaani kibaya zaidi huyo mwanaume alikuwa anawachanganya mtu na dada yake….” Bibi kizee mmoja ambaye mdomo wake ulikuwa umechongoka alitokwa na maneno yale kana kwamba alikuwa na uhakika.
Lilian aliyasikia na haya. Hapa akakumbuka kuwa aliwahi kupatwa na hisia za Walter kutoroka na kwenda Mbeya ni kwa sababu alikuwa katika mahusiano na shemeji yake. Sasa alikuwa anajipongeza kwa kuamini kuwa Walter ni muathirika na anajitambua kuwa yu katika orodha hiyo ya waathirika.
Lilian licha ya kumfikiria Walter kama muathirika bado alikuwa na hisia naye za kimapenzi.
Akiwa katika dimbwi hilo la mawazo mara alimwona mzee kijana mmoja akiwa ameongozana na watu wawili wakiiendea nyumba ya Walter. Hapa sasa umati ukaanza kujisogeza katika nyumba ya Walter, Lilian naye hakubaki nyuma alihitaji kujua ni kitu gani kilikuwa kinatokea. Jicho la Lilian lilimtazama vyema yule mwanaume na kumtambua. Alikuwa ni mlinzi wa nyumba ya Walter, aliingia na wale wanaume wawili kisha geti likafungwa. Kilichoendelea walijua wao.
Baada ya nusu saa wale wanaume wawili walitoka. Mlinzi akabaki ndani.
Akili ya Lilian ikafanya kazi upesiupesi akaitambua hatari ambayo ilikuwa mbele yake. Japo awali alitamani kujiua kwa kuwa tu ameathirika na gonjwa hatari la Ukimwi. Lakini hakutamani hata kidogo kufia gerezani.
Iwapo Walter amekufa kisha nguo zake zikakutwa katika chumba ambacho Walter huwa analala bila shaka atatafutwa na mbaya zaidi hakuwa na kumbukumbu iwapo kuna kitambulisho chake chochote aliacha katika chumba kile.
Hofu ikatanda Lilian akatambua fika kuwa iwapo anahitaji kuendelea kuifurahisha nafsi yake kwa namna yoyote ilikuwa lazima awe mbali na mkono wa sheria.
Lilian akajipenyeza katika kundi la watu waliokuwa wameanza kutapakaa baada ya kumaliza mshangao wao.
Akalifikia geti kwa tahadhari kubwa.
Akagonga mara mbili, mlinzi akafika kuchungulia.
Ana kwa ana na Lilian. Macho ya kitafiti ya daktari yule yakang’amua kuwa mlinzi alipatwa na hofu kuonana na Lilian, japo ilikuwa mara yake ya pili kumwona hakuwa na amani hata kidogo.
“Karibu mama…” Mlinzi alimkaribisha Lilian.
Lilian hakujibu kitu aliingia moja kwa moja ndani.
Alijivika ujasiri huo ili aweze kucheza na akili ya yule mlinzi.
Alipoifikia sebule alimtazama yule mlinzi kupitia katika tundu la funguo mlangoni.
Mlinzi alikuwa anahangaika kubonyeza simu yake.
Lilian akang’amua kuwa wale wanaume wawili walioingia na kisha kutoka na kumwacha mlinzi nyuma walikuwa ni watu wa usalama.
Polisi bila shaka…..
Lilian akajiweka katika tahadhari kubwa, hata kama angeenda kule chumbani hakuwa na jipya la kufanya. Kama maaskari walikitembelea chumba kile bila shaka kila kona watakuwa wamepekua.
Lilian akataka kuondoka eneo lile. Lakini ghafla akakumbuka vitu viwili kwa pamoja. Alikumbuka kitambulisho chake cha kazi. Alikumbuka kuwa wakati akiwa katika kufurahia raha isokuwa kifani na Walter pale kitandani kuna kitu kilianguka chini ya kitanda.
Lilian aliamini kuwa ni kitambulisho chake kilianguka, hakujua ni kwanini anaamini kuwa ni kitambulisho na wala sio pete ama kitu kingine.
Kitambulisho na pete ndo vitu pekee alivyoingia navyo kitandani wakati Walter akiwa katika matamanio na kuanza kumpelekesha bila kuviondoa vitu vile pale kitandani.
Kitu kingine alichowaza ni mlinzi, je hiyo simu aliyopiga hao wapigiwa wapo jirani ama wapo mbali.
Itakuwaje kama watakuwa jirani.
Nitakamatwa kama kuku….aliwaza zaidi.
Ghafla akachukua maamuzi, akakimbilia chumbani, akawa kama mwendawazimu, akakivamia kitanda na kukivuta. Upande uleule ambao alikuwa anasulubishwa na Walter.
Akapapasa, akakumbana na kitu kigumu. Akakichomoa.
Hapana ilikuwa ni kondomu ya kiume ikiwa haijafunguliwa bado….akasonya akaitupa.
Akapapasa tena, akakumbana na kitu kingine. Akakichomoa.
Kilikuwa kitambulisho chake cha kazi.
Lilian akafanya tabasamu hafifu.
Hakutaka kupoteza dakika ya ziada. Akatoka ndani ya chumba.
Wazo likabakia kwa mlinzi wa mlangoni.
Iwapo atakamatwa, ni huyu mlinzi pekee atakuwa na ushahidi wa kumuona ndani ya nyumba ile akiwa pamoja na Walter. Lilian akapapasa katika mkoba wake, akakutana na bomba la sindano.
Ilikuwa kawaida yake kutembea na vifaa kadhaa vya kitabibu.
Lilian akaingiwa na roho mbaya. Akamchukia yule mlinzi aliyejifanya anajua sana kupiga simu.
“Akifanya ujinga tu nami namfanyizia, ngoja…” alijisemea huku akichukua lile bomba la sindano kisha akapachika mdomo wa mbele.
Akaiweka tayari tayari.
Hatua kwa hatua akaanza kutoka nje.
Huku kama alivyotarajia mlinzi alilifunga geti na kumzuia kuondoka.
“Bwege alipigia simu mapolisi huyu…” Lilian aliwaza huku akiwa amehamaki.
Mlinzi hakuwa amejiandaa kwa mapambano bali alikuwa amejiandaa kwa majibizano baina yake na Lilian.
Lilian hakutaka maongezi yoyote. Alichukua upesi ile sindano bila mlinzi kutambua kinachoendelea. Akamvaa mlinzi, akaizamisha bila kusita katika paja lake, yowe likamtoka mlinzi akajirusha mbali na geti lile. Lilian akamchoma tena katika mgongo.
Hapa mlinzi akatafuta pa kukimbilia. Lilian naye akatoka nje.
Alipoifikia gari na kuiondoa, alipishana na gari la polisi.
“Mabwege kidogo wanikamate….” Alisema kwa sauti ya juu kisha akawasha redio garini….
Safari ya kuelekea anapopajua yeye. Hali haikuwa shwari hata kidogo. Kuna vita ya kimya kimya ilikuwa inaendelea. Baada ya kumsulubisha Kibwana, sasa alikuwa amempa adabu yake mlinzi wa getini.
Lilian akabaki na maswali mawili matatu….je Walter amekufa? Na kama amekufa je ni yeye anayesakwa kama muuaji?
Utata.

Gari la Lilian lilipenyeza katika vichochoro kadhaa, alijaribu kuvuta kumbukumbu akaikumbuka nyumba ya Suzi maeneo ya Mtongani. Alihitaji kufahamu kuwa nini kinaendelea walau kwa muhtasari tu…Lilian alimini kuwa kwa patashika hili lazima dada yake Naomi alikuwa anafahamu chochote kile.
Aliendesha gari lake bila kujalisha kuwa ni usiku. Akaendesha hadi nyumbani kwa Suzi. Huku pia aliegesha gari mbali sana, akajisogeza kwa mwendo wa miguu hadi pale nyumbani kwa Suzi.
Alikutana na mwenyeji ambaye haikuwa mara ya kwanza kuonana. Walipoonana walishangaana.
“Dokta….hali si shwari, hupatikani namba zote…tunakutafuta sana.”
Kauli hii ikamyumbisha Lilian, kivipi wamtafute? Kuna nini? Ama askari wamefika hapo kumtafuta?
“Kuna nini?”
“Ni mgonjwa wako….hali ni mbaya…mbaya sana. dokta Suzi ana hali mbaya sana….yupo hospitali….sijui kama atapona. Alisema tukupigie simu anataka kukueleza jambo. Tumekutafuta sana hadi sasa umefika mwenyewe..” alijieleza kwa kirefu yule mtu.
Dokta akmachezwa machale, huenda ni mtego ameundiwa aweze kunasa kiulaini katika mikono ya polisi kwa kesi ya mauaji.
Lakini kwa uzoefu wake katika saikolojia yule kijana alikuwa anasema kweli.
“Yupo wapi?” Lilian aliuliza katika hali ya kutoonyesha mashaka yoyote.
“Yupo Temeke…amefikishwa pale na maaskari sijui wamemtoa wapi hata..lakini hali ni mbaya sana.” alisema kwa kusisitiza yule kijana.
Kusikia kuhusu maaskari, dokta akapagawa. Akachanganyikiwa kabisa, akahisi yule kijana anasema ukweli lakini hajui kuwa ukweli wake unamuingiza matatani yeye.
Lilian akataka kukimbia majukumu yake, mara ile sauti ya mwalimu wake wakati akiwa chuo kikuu ikamrejea kichwani “ Daktari na ajitoe kwa kila kitu kuokoa uhai wa mwanadamu, ikishindikana ni Mungu pekee awe amepanga na si kwa uzembe ama chuki zozote binafsi…ni aheri usiwe daktari kuliko kuwa daktari ambaye mgonjwa anakufia kizembe” maneno haya yakafanya kama shambulizi kali sana. hisia za usaliti wa nasaha za mwalimu wake zikamuandama.
Je aende kutimiza neno la mwalimu wake ili akakutane na maaskari ambao alihisi kuwa wanamtafuta. Ama akimbie majukumu na kujiweka mbali na majukumu??
Akabaki amezizima. Hali tete……..
Sintofahamu ikatawala……..
Mapenzi yalikuwa yamemsafirisha na kumleta katika nchi ambayo hakuwahi kuitegemea, katika nchi hii anajikuta akipata tuhuma za mauaji, mauaji kwa kupigania penzi lakini yanatokea mauaji mengine yanaongezewa, nchi hii ya maajabu ilikuwa nyepesi sana kuingia lakini njia ya kutoka haionekani.
Lilian akatamani muda urejee nyuma asiwe amewahi kukutana na Walter…..lakini muda haukurudi nyuma…..
Hali halisi ilichukuwa nafasi.


CHUMBA kikubwa kisichokuwa na samani ndani yake zaidi ya vitanda vyenye magodoro ya futi tatu kwa sita, kilikuwa kimya sana. ilisikika sauti ya watoto wakishindana kutoa vilio, sauti za mama zao zilisikika zikifanya kubembeleza. Hali ilikuwa tulivu kama sauti za wale watoto zingepuuziwa.
Kitanda kilichokuwa kimetulia tuli ghafla kilipata uhai wake na kuanza kutetemeka kisha kiwiliwili kilichokuwa juu yake kilinyanyuka na kukaa kitako.
Shuka likafunuliwa kisha kiwiliwili kikaketi vyema na kuanza kutafakari. Ni kwa namna gani kiliweza kufika katika chumba hicho ambacho kilikuwa kimetawaliwa na harufu kali ya madawa. Madawa ya wanadamu.
Kiwiliwili kilinyanyua mikono juu na kujinyoosha.
Matiti yakaonekana. Kumbe kilikuwa na jinsia ya kike.
“Nimefikaje hapa sasa…” alijiuliza yule mwanadamu. Alikuwa katika giza kiasi. Akafanya utulivu kwa dakika moja zaidi kabla ya tukio zima la kusafiri kutokea jiji la Mbeya baada ya kumpa mwili wake bwana Kibwana ili aweze kumpa siri juu ya mbaya wake, akafika jijini Dar es salaam mapema sana akiwa na lengo moja tu…kufumania. Alijua fika kuwa atamfumania daktari Suzi akiwa na mumewe wa ndoa, hakika hali aliyoikuta katika sebule yake ilimpa picha ya nini atakachokutana nacho mbele yake, fumanizi la kushtukiza. Japo alimini kuwa mume wake alikuwa na mwanamke mwingine ndani akajilazimisha kuichukulia hali ile kama ya kawaida lakini mambo yakawa magumu…..akajikuta akitetemeka aliposikia mikito katika chumba chake. Bila shaka Walter alikuwa na mwanamke mwingine, pepo wa hasira akamchukua, akachomoa kisu ili afanye chochote kibaya kwa mwanamke ambaye yu katika himaya yake tofauti na matarajio yake ya kumbamba dokta Suzi katika chumba chake anakumbana na bumbuwazi la karne.
Hakika alikuwa Suzi lakini huyu hakuwa dokta Suzi.
Dada yake wa toka nitoke alikuwa akimvutavuta Walter kutoka pale sakafuni. Kitu mfano wa shoti kali ya umeme ukatambaa mwilini mwake akajikuta ananyong’onyea na kisha akapoteza fahamu.
Sasa yu katika vitanda vinanvyofanana.
Naomi aling’amua kuwa alikuwa hospitalini, na bila shaka hakuwa chini ya uangalizi wowote mkali. Kwa mazoea yake alitambua kuwa alikuwa amepewa kitanda apumzike baada ya huduma ya kwanza.
Akili ya Naomi ikatulia kidogo kisha akakodoa macho yake kana kwamba ameona mzimu mbele yake, mzimu wa kutisha.
Naomi alilikumbuka tukio ambalo akili yake ilipambana nalo kisha akazidiwa na kupoteza fahamu. Ni Suzi, dada yake wa kuzaliwa tumbo moja. Naomi akazubaa kama tahira, akajisikia kupungukiwa nguvu mwilini.
“Suzi alikuwa na mahusiano na Walter….fuck…kaniambukiza Ukimwi bwege huyu…” aliropokwa kwa sauti ya chini bila kutarajia.
Kitendo cha kumkuta Suzi na Walter pale zuliani, na zile kelele alizokuwa anazisikia nje ya chumba kabla ya kuamua kuvamia zikamtupa katika hisia mbaya za kumfikiria vibaya dada yake.
“Alikuwa ametoa kanga na Walter alikuwa na Bukta…….chupi ya Suzi sebuleni…..chupa ya pombe…..walilewa kishaa….aah” Naomi aliyasema kimyakimya matukio ya mwisho kupatiliza katika akili yake.
Ni jibu gani linapatikana kwa ushahidi huu, mwanaume na mwanamke kukutwa chumbani wakiwa katika hali ile na kabla ya fumanizi hilo, sebuleni inakutwa chupi ya kike na chupa ya pombe kali.
Naomi akajihisi yu katika ganzi, alikuwa amebanwa na mkojo lakini ghafla ukatoweka. Japokuwa aliwahi kuwa changudoa lakini hali aliyokuwa anateseka nayo dada yake ilimuogofya na kumshukuru Mungu kwa kumweka salama, akajikuta amebadilika jumla hadi siku alipomvulia nguo Kibwana kwa ajili ya kupata siri ambayo itaokoa penzi lake kutoka katika kinywa cha daktari mbaya.
Sasa alikuwa ameambukizwa Ukimwi na dada yake wa kuzaliwa naye tumbo moja, tena kwa kupitia mwanaume ambaye alikuwa mume wake wa ndoa anayetambulika kila mahali.
Huu kwake ulikuwa ni utata. Naomi akajikuta katika hisia za ajabu hisia ambazo zilimsihi kuwa anatakiwa kujiweka mbali na maadui zake.
“Nani adui yangu sasa? Ni Suzi ama ni Walter…..hivi inawezekana walianza muda mrefu eeh…..” alijifanyia mahojiano katika namna ya kipumbavu, kwani wa kujibu maswali haya hakuwepo.
“Siwezi kukaa nyumba moja na Walter…aibu iliyoje hii…amekosa huruma mwanaume yule, kumbe alipotoweka Suzi alikuwa anajua halafu kila siku ananitazama tu ninavyolia mimi…..dada yangu wa damu ananifanyia usaliti kama huu…bora Walter anisaliti huyo si ndugu yangu. Suzi yaani Suzi anayekijua kilio changu katika mapenzi ananifanyia haya kweli….” Naomi alishindwa kuendelea kuzungumza akaanza kulia, kwa sauti ya chini sana lakini machozi yakibubujika kwa kasi kubwa.
Ghalfa akaijiwa na wazo jingine. Akajihisi kuwa atakuwa na amani iwapo tu atakaa peke yake. Hakuhitaji kuwa karibu na mtu yeyote.
Kama ndugu yake wa damu ameweza kumsaliti kimya kimya bila huruma na kufanya uzinzi na mume wake ni nani tena wa kumuamini katika dunia hii? Hakuwepo hata mmoja.
Naomi hakutaka asubuhi ifike. Akajipapasa katika suruali yake, akakuta kadi yake ya benki ikiwa imejishikiza vyema katika mfuko wake.
Akasimama taratibu kama mgonjwa anayueenda chooni. Akauona mlango wa kutokea. Kisha akashuka ngazi mbili tatu akakutana nna mlango wa kutokea. Kadri alivyokuwa anazidi kutembea ndivyo alivyozidi kuimarika. Alipofikia mlango wa kutokea hakufanania na mgonjwa kabisa.
Alikuwa katika kundi la wazima. Alipofanikiwa kutoka nje alikutana na maneno machache.
DR. SUZAN HERBALIST….” Hakuweza kuona maandishi mengine. Akajichanganya mjini. Macho yake yakakutana na mnara wa saa.
Ilikuwa ni saa nne usiku na umeme ulikuwa umekatika mji mzima.
Naomi akaongozwa na hisia zake za ajabu. Usiku ule akaumalizia katika nyumba za kulala wageni.

****

“Amekunywa pombe huyu….hakuna kitu kingine zaidi ya pombe na mshtuko ..kabla ya hapo alikuwa amekunywa dawa za tumbo aina ya fragile ambazo hazina madhara mwilini mwake..” daktari alikuwa anatoa maelekezo kwa wapambe wa Walter. Ambao tayari walikuwa wamepata taarifa za kupatikana kwake.
“na mamaa kule..” kijana mmoja aliuliza, akimaanisha Naomi.
“Yule hana tatizo kabisa, alizinduka na kisha akalala tena, zaidi ya ule mpasuko kichwani ambao tayari nimeufunga hana tatizo jingine..”
“Na yule mwingine. Si walikuwa watatu..yeye vipi?”
Daktari alikunja kunja ndevu zake akifanya tafakari, kisha akanyanyua kichwa chake akawatazama wale vijana.
“Yule hali yake haikuwa nzuri, kuna kijana alifika hapa baada ya kupigiwa simu kutoka katika simu ya yule mwanamke. Alijitambulisha kama jirani yake. Kijana yule alimchukua na kutoweka naye akisindikizwa na wauguzi. Alidai kuwa yule anaye daktari wake maalumu.” Alitoa maelezo haya. Hakuna aliyejali sana. ilhari mpambe wao na mkewe hali zao zilikuwa shwari.

Wakati haya yakitokea katika chumba cha daktari. Wodi ya wagonjwa wa kiume. Walter aligutuka kutoka usingizini na kujikuta yu mwenyewe.
Alihisi kuwa yu jehanamu ama peponi.
Pepo gani sasa hii kuna mashuka?
Mh..Jehanamu kuna vitanda? Lakini kuna joto dah…au jehanamu kweli…
Mawazo haya yalipita katika kichwa cha Walter ambaye wazo lake la mwisho lilikuwa kujiua.
Alitaka kujiua ili kujiweka mbali na Naomi baada ya kufanya usaliti wa kufanya uzinzi na daktari Suzi.
Wakati akiyawaza haya, akayasikia mazungumzo ya watu aliokuwa akiwafahamu.
“Derick naye yupo huku peponi? Mbona sikumbuki amekuja lini?” Walter alijiuliza. Na hapa hakupata jibu. Akatamani kuita kwa nguvu….mara akang’amua kuwa koo lake lilikuwa kavu sana.
Akapepesa macho huku na kule akaona kopo la maji ya ‘uhai’.
“Duh Bahkressa kiboko…hadi mbinguni ana’supply’ maji yake..” maneno haya yalimtoka kwa sauti hafifu.
Mara maneno yale yakatoka na harufu katika kinywa chake.
Harufu hii aliwahi kuisikia mahali, ni wapi? Alijiuliza….akili ikazunguka kwa kasi…aliwahi kuinusa kama ilivyo.
Wapi? Wapi…..ni penyewe hapo hapo…..mbona napasahau sasa….
Lahaula….ni duniani…hii harufu ya duniani, nyumbani kwangu. Ni harufu ya pombe za Naomi….Mungu wangu……nipo duniani bado.
Ni hapo akili ya Walter ilipokaa sawa, akatambua kuwa hakufa. Hakufa bali alifanya jaribio la kujiua na likashindikana.
“Mbona sikufa sasa?” alijiuliza.
“Wewe roho wa namna gani sasa mimi nataka kufa unanilazimisha kuishi..” alilaumu.
Akaweka kimya cha muda mrefu kisha akamkumbuka Naomi, yakajirudia yote ambayo aliyawaza na yakamsababishia kujiua.
Ni lazima angekumbana nayo tena baada ya kurejea uraiani.
Akakumbuka pia alikuwa amefanya jaribio la kujiua. Akaikumbuka sheria ya nchi itakavyomsumbua kwa thubutu yake ile ya kujitoa roho.

Walter akajikuta katika kigugumizi cha maamuzi. Lakini alitambua fika kuwa hakutakiwa kulala zaidi.
Alijiweka kitako kwa tahadhari kubwa sana. akatazama kushoto na kulia kisha akaupima mwili wake akatambua kuwa bado alikuwa na nguvu za kutosha.
Akasimama wima. Kana kwamba akili yake na ya Naomi ilifanana.
Naomi hakuwa tayari kuishi karibu na Walter, naye Walter hakutaka kuishi karibu na Naomi kwa hatia iliyokuwa inamkabiri. Hatia ya usaliti.
Walter akatoweka.
Palipokucha kilikuwa kitimtimu.
Wagonjwa wawili walikuwa wametoweka.
Mume na mke.

ITAENDELEA

Post a Comment

0 Comments