Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Uvaaji wa magauni mafupi, vimini, kikaptula

Mko poa walimbwende,

Ngoja niwape darasa kidogo, kimsingi uvaaji wa nguo fupi kwa wanawake pia ni fasheni ya mjini nazungumzia gauni fupi,kimini au kikaptula(kichupi) ila nazungumzia zaidi vimini na magauni mafupi.

1/Mazingira yanaruhusu?
Kabla hujavaa kimini au gauni fupi jiulize kwanza unaenda ofisini,sehemu ya ibada,starehe au kitaani tu au utapanda daladala? Ukijiridhisha wewe jipigie tu kimini chako.

2/Una miguu?
Kuvaa tu kinguo kifupi wakati una miguu mibaya ni sawa na kujidhalilisha tu kama unajijua unatembelea mikono usivae vazi hili.

3/Kiatu kirefu ndio mwake
Ili utoke bomba na gauni fupi au kimini hakikisha unavaa kiatu kirefu, lakini kimini pia kinaweza kuvaliwa na flat shoes kikaeleweka utaonekana wa kijanja.

4/Epuka kuinamainama
Ukivaa vazi fupi kamwe usitake kuinama unaweza kujikuta mali zako zinabaki nje.Njia bora wakati unaokota/kuchukua kitu ni kuchuchumaa tu.

5/Kaa kwa staha
Wakati wa kukaa hakikisha unapishanisha miguu badala ya kuachanisha au kuitanua, utakaa uchi !!!!!

6/Uvaaji wa kaptula fupi/kichupi
* Huvaliwa chumbani au sehemu ya starehe
* Inapendeza ukivalia top au blauzi
* Hakikisha miguu yako ipo soft
  
  
  
  
  
  
  
  
  
  
  
  
  
  
  
  
  
  
  

Post a Comment

0 Comments