Header Ads Widget

Responsive Advertisement

TUKIO LILILOMTOA MACHOZI




SIMULIZI FUPI : TUKIO LILILOMTOA MACHOZI

Katika maisha kuna majaribu sana haswa ya nani atakuwa wa kufa na kuzikana katika ndoa nijambo ambalo limefichwa sana.
Kuna rafiki yangu kipenzi sana (wa kiume) nimekuwa nae na tumeishi wote na kuanza shule moja primary mpka tulipo itimisha masomo yetu chuo kikuu cha UDSM kwa upande wa telecommonication engneering kilichokuja kututenganisha ni ofisi za kazi tu.
Ndg zanguni kipindi tunasoma tulisoma katika maisha magumu sana kwani wazazi wetu hawakuwa na uwezo nakumbuka kipindi tunafaulu kwenda 4m1 marangari boys ilibidi tushare vitu ili twende shule na pia kipindi tunaenda 4m5 pugu napo tulitumia kushare vitu ila tutimize lengo letu kutokana na hali halisi ya kiuchumi ktk familia zetu.

Basi baada ya kumaliza shughuli zetu za masomo tukaanza maisha ya kijitegemea ikifika wakati wa kuoa tulikuwa na wakati mgumu sana kuwa yupi ndio chaguo halisi kabla ya hapo baba yake rafiki yangu alimuita kabla hajaanga dunia tulienda wote alituachia hosia kuwa "wanangu chondechonde mkikosea kuoa mtajuta mpaka mauti yanawakukuta mfanya vyote msije kosea kuoa" ni kauli amabayo kila Mara wazazi wangu wananiambia pia kwel rafiki yangu akampata binti mmoja wakaanza mahusiano wakafika kipindi cha kuoana wakafanikiwa kufunga ndoa maisha yakaendelea vizuri wakafanikiwa kupata mtoto ss mama mzazi wa kijana alikuwa kijijini kiukwel kijana akatengeneza kwao alikozaliwa kwa mama yake vizur basi bwana yule mke wake alikuwa hapendi... siku zikaenda kijana akamwita mama yake aje akaye naye, mama alikuja baadae akaondoka akawa anakuja anaondoka ss basi yule mama yake umri ukawa umesogea na pia akauguwa ikabidi mwanae amlete kwake kwa matibabu na kupumzika kwa muda kidogo ikagundulika mama alikuwa anasumbuliwa na kisukari na presha ss ikabidi vyakula vya mgonjwa wa kisukari viwepo na madawa ss basi mke wa rafiki yangu akatokea kuchukia sana kwann huyu mama kakaa hapa ss manyanyaso yakaanza kwa hyo mama alikuwa hapewi huduma ya vyakula vilivyokuwa vinatakiwa, anatengwa kiukwel ni mambo mengi aliyofanyiwa hyo mama.

ss mama wa rafiki yangu alikuwa anaogopa kusema kwa kuofia kuwa mwanae akijua ndoa inavunjika alivumilia ijapo kuwa alikuwa anang'ang'ania kurudi kijijini akidai kapona mtoto wake alikataa cn kwani ndio mtoto wake wa pekee... siku zikaenda mama ikifika muda wa kula mchana analishwa stooni (kwenye store) na kombe la plastiki na chakula ambacho hakifai kabisa kwa mgonjwa wa kisukari wakati rafiki yangu kila siku ya mungu alikuwa anaacha pesa ya chakula cha mgonjwa na pesa ya matumizi ya nyumbani... ikafika wakati majirani hawakupendezwa na ile hali waliyokuwa wakimkuta yule mama ikafikia hatua majirani wakaanza kumwambia yule mwanae yanayomkuta mama yake na pia alikuwa na mtoto wa miaka minne hivi naye baba yake akija jioni mtoto anaanza kusema ss jamaa alikuwa anachukulia ni maneno ya majirani na mtoto akawa anapuuza wakati huo mama ananyanyasika na afya yake inazidi dhohofika kila wakati.

Ss basi rafiki yangu alikuwa akiwaza sana juu ya hayo mambo yalimuumiza kichwa cn akimpeleleza mama yake mama yake anakataa kwa 100%... siku moja ikabidi aage anasafiri kapata safari ya kikazi kwel akaacha pesa yakutosha cn ya mgonjwa kwa mke wake na matumizi ya nyumbani akaondoka lengo lake ni kufanya fumanizi zikapita siku mbili hvi mida ya mchana hakarudi gafla nyumbani na akurudi na gari kwani walikuwa wamezoea honi ya gari nikwel aliwakuta wanakula mezani mke wake na dada wa kazi na mwanaye akauliza je mama yuko wapi mtoto akasema anakula stoo kwenda kiukwel alichokikuta mama yake anakula na akiangalia wenyewe wanavyokula machozi yalimtoka ndipo akanipigia simu nikaenda kiukweli wanawake cjui .... yule mama alikuwa anakunywa uji usio na sukari na chakula kibaya na pia katelekezwa store mchafu sana jamaa alimwangalia mke wake wakati machozi yanamtoka aliongea hii kauli " mke wangu asante kwa haya uliyoyafanya kwani asinge kuwa hyu uliyemtelekeza store usinge nipata kanilea kwa kuuza karanga za kupika na mahindi na mihogo iliyokaushwa ( udaga) ndio maana nimefika hapa nilipo" akamnyanyua mama yake na kwenda naye mezani alichokifanya alimwambia mama yake achukuwe begi lake la nguo tukaondoka tukaelekea kwangu mm sina Mke ila nilikuwa naishi na Mdogo wangu Wa kike kipindi tunaondoka aliongea hvi " sitakufukuza kaa na mwanao Nyumba hiyo hapo na kila kitu nimekuachia" wakati analia sana ikabidi mwanamke abebe mtoto waende kwao wakafunga Nyumba mama yake yule rafiki yangu akalazimisha kurudi kijijini kwanza baada ya cku mwanamke akawaeleza wazazi wake ss wazazi walipagawa sana wakaanza kubembeleza jamaa amsamehe alichokuwa akiwajibu mm hajanikosea kabisa ikabidi mama yake Mzazi aje kunusulu hyo ndoa kwani ilikuwa inaenda kuvunjika mama yake kijana alichokifanya alienda ukweni akamchukuwa Mkwe wake na mtoto wakaenda kijijini as baba zake mwanamke na mama yake na ndg zake wakaenda huko kijijini rafiki yangu alikataa kabisa mama yake akatoa kauli 1 akamwambia " kama mm ndio nimebeba mimba yako nimekulea tokea damu mpka miezi tisa nimekuzaa chumbani usipo kuja na kurudiana na mkeo tafuta mama yako na nikifa usikanyage kwenye msiba wala kaburi langu" rafiki yangu alikuwa na wakati mgumu sana ikabidi tuondoke mpaka kijijini yule mwanamke wake aliomba msamaha na kusimulia yote aliyokuwa anayafanya kwa hyo mama kiukwel iliniuma sana nikawa najiuliza kwanini wanawake wanafanya hivi ili iweje? Kwa faida gani?


Pia nikikumbuka yaliyonikuta within 1 week mwanamke anabadilika na kusababisha ndoa kutokufungwa kwa usaliti kwel nikifikilia story ya rafiki yangu na nikiunganisha na yaliyonikuta nabaki kuwataza wanawake kama wanaume wenzangu kiukweli " Kilichonifanya niandike huu uzi nimekuwa nikipitia mada mbali mbali kuhusu mapenzi ndoa uchumba leo nimevutiwa na maada ya mwandishi mmoja anaitwa AKILI UNAZO kaandika juu ya wanawake na wadada na kutaja hayo mambo nahisi yako kumi au saba.

Wanandg wenzangu kwanini wenzetu wanafanya hvyo nini zaidi kinachosababisha unyanyasaji kwa wakwe zao kwann lakini kama kuna mtu yalishamkuta hatueleze na wadada na wanawake mtueleze nn tatzo?

Post a Comment

0 Comments