SIMULIZI; MKE WANGU MSHAMBAMSHAMBA LAKINI NI WADHAHABU!
Nakumbuka ilikua ni Tarehe 12 mwezi wa nane mwaka 2007, siwezi kuisahau, ilikua ni siku ya jumapili, siku ambayo nilipaswa kuwa na familia yangu. Lakini kama kawaida yangu nilichagua marafiki, kulikua na sherehe ya kikazi ofisini kwetu na kila mtu alikuja na mwenza wake kasoro mimi. Kama kawaida yangu sikwenda na mke wangu, nilimuona mshamba mshamba hivyo nilienda na Mariam, mchepuko wangu wa muda mrefu.
Yeye alikua ni mwanafunzi wa chuo pale UD akiwa mwaka wa tatu. Nilianza naye mahusiano tangu akiwa mwaka wa kwanza baada ya kuwa anajitolea pale ofisini kwetu wakati wa likizo. Kweli nilimpenda na kwakua alikua msomi tofauti na mke wangu ambaye aliishia kidato cha nne niliona anafaa zaidi kwangu.
Baada ya ile Sherehe nilirudi nyumbani, si kwasababu nilikua na hamu ya kumuona mke wangu hapana, nikwakua nilisahau ATM Card yangu nyumbani hivyo nilienda kuichukua. Nilifika na kumkuta mtoto wangu mkubwa amekaa sebuleni analia, alikua ameshikilia simu ya Mama yake akinipigia, nikweli niliona Miss Call nyingi za mke wangu lakini nilijua ni wivu wake wa kijinga.
“Wewe kwanini uanchezea simu ya Mama yako?” Nilimuuliza kwa hasira kwani nilijua yeye ndiyo alikua ananisumbua. “Mama ndiyo kaniambia nikupigie anaumwa…” Nilistuka kidogo na kwenda chumbani alikokua mke wangu, kweli alikua kalala, nilimsogelea mwili ulikua unawaka Moto, nilimuuliza tatizo nini lakini alikua hawezi kuongea vizuri.
“Nipeleke Hospitali mume wangu nakufa…” Aliongea kwa shida, pale nilichanganyikiwa kidogo, kwani sikua na mpango wa kukaa nyumbani siku ile. Nilimuangalia tena nijiridhishe kwani nilihisi anaigiza baada ya kumpiga mchana wake alipoona meseji za mapenzi katika simu yangu na kuanza kulalamika, nilimuambia akusanye kila kilichochake aondoke, nilihisi kua hataki kuondoka ndiyo maana anajifanya kuumwa.
Kabla sijawaza nini chakufanya simu yangu iliita, ilikua ni Mariam, niliiipokea na palepale alianza kulalamika kuwa namchelewesha kama sitaki kwenda basi nimuambie wengine wanamsubiri. Pale nnje niliacha Gari yangu, Mariam alikua nnje pamoja na wafanyakazi wenzangu. Nilienda kuchukua ATM kwani mimi ndiyo nilikua mnunuaji na walikua wananisubiri.
Nilimuambia nakuja, nilirudi chumbani na kuchukua ATM yangu (tulishatengana chumba na mke wangu), niliingia chumbani kwake na kumnyanyua, alinyanyuka kwashida, nilimuona anaweza kusimama. Nilimkokota mpaka nnje. “Mke wangu anaumwa, tumpitishie hapo Hospitali kidogo…” Niliwaambia lakini niliona wote mood zilibadilika, waliamnza kulalamika ni mambo gani hayo kama sitaki kutoka si niwaambie.
“Sasa hapa atapanda wapi huoni gari imejaa?” Mariam aliniuliza kwadharau, alionekana kukasirika zaidi. “Wanawake nawafahamu, huyo kaona unatoka analeta wivu wake!” Rafiki yangu mmoja aliongea na wote wakacheka, walianza kunitania kama siwajui wanawake, nilijikuta kama nataka kuwaamini hivi. Nikiwa ninawaza nini chakufanya na mke wangu, nilikumbuka nina namba ya Tax, nikampigia alipokuja nilimpa elfu ishirni na kumuambia ampeleke mke wangu Hospitalini.
Mke wangu aliniomba niende nayeye nakumbuka nilimjibu “Kwani mimi ni Daktari, unafikiri nitafanya nini kama nikienda au ni kweli unaigiza ili tusitoke!” Nilimjibu kwa hasira huku nikipanda kwenye Gari. “Huo ndiyo uanaume sasa!” Rafiki zangu walinisifia wote tulicheka kwa pamoja, mbele ya mke wangu Mariam alinikumbatia na tukaanza kunyonyana denda. Hakikua kitu kipya mke wangu alijua nachepuka na mara kibao nilishamfanyia dharau hizo.
Tuliondoka na nilizima simu siku nzima, siku iliyofuata sikurudi nyumbani, nililala kwa Mariam shemu ambayo nilikua nimempangishia. Haikua mara ya kwanza, sikujali hata kama mke wangu yuko Hospitalini wala kuuliza alikua anaendeleaje. Jioni nilirudi kwa Mariam na tukaanza kunywa, ndipo nilimkumbuka mke wangu na watoto, nilikumbuka kuwa Dada wa kazi nilishamfukuza hivyo kama mke wangu atakua amelazwa basi watoto watakua wenyewe.
Kidogo nilipata huruma na nilitaka kwenda kuwacheki. Nikiwa nimelewa kidogo niliingia kwenye Gari, lakini nikiwa njiani nilitaka kugonngana na Lori la mizigo ambalo sikuliona kutokana na Pombe, wakati nikilikwepa niligonga kwenye Tela lake, sikujua kilichoendelea mpaka masaa 28 baadaye. Nilinyanyuka nikiwa Hospitalini, nilikua nimekatwa miguu yote miwili.
Nilifikishwa pale nikiwa na hali mbaya sana, nilikua nimevunjiaka mbavu sita, bega na miguu ilikua imesagikasagika na hawakua na namna zaidi ya kuikata. Rafiki zangu walikua pale kunipa moyo, nilanza kulia kama mtoto, Mariam alikuja na muda wote alikua naalia tu. Mke wangu bado nilikua sijamuona, alikua hana taarifa kwani nayeye alikua amelazwa Hospitalini, alikua na Typhod.
***
Kutokana na kazi niliyokua nikifanya na muda niliotumia Hospitalini na kupoteza miguu sikuweza kuendelea tena na kazi. Niliachishwa kazi baada tu ya kutoka Hospitalini, nilikaa Hospitalini kwa miezi mitatu mpaka kuruhusiwa. Hapo ndipo niliona thamani ya marafiki na thamani ya mke. Mariam alikuja siku ya kwanza tu baada ya kusikia nimepata ajali, alilia na kulia kisha akaondoka na sijawahi kumuona tena mpaka leo naandika kisa hiki.
Kutokana na kazi niliyokua nikifanya na muda niliotumia Hospitalini na kupoteza miguu sikuweza kuendelea tena na kazi. Niliachishwa kazi baada tu ya kutoka Hospitalini, nilikaa Hospitalini kwa miezi mitatu mpaka kuruhusiwa. Hapo ndipo niliona thamani ya marafiki na thamani ya mke. Mariam alikuja siku ya kwanza tu baada ya kusikia nimepata ajali, alilia na kulia kisha akaondoka na sijawahi kumuona tena mpaka leo naandika kisa hiki.
Kumbuka huyu ni mwanamke niliyekua nikimpenda kuliko mke wangu, nilikua nikimlipia ada ya Chuo, nimempangishia nyumba na kumfanyia kila kitu kama mke wangu. Tulishaweka mipango ya kuoana na kila siku nilikua nikitafuta sababu tu ya kumuacha mke wangu, nilikua nikimpiga mke wangu kwa makosa yangu, akinifumania akiongea ni kipigo.
Mara kadhaa nilishamuambia kuondoka na watoto wake kwani siwataki na mambo mengine mengi kibao lakini alivumili. Mke wangu alipata habari za kupata ajali siku mbili baadaye, ni baada ya kupata nafuu na alipoambi watu alikuja kuniona. Nilimuona namna alivyokua anaugulia, hakua sawa lakini alinijali na kuja kunihudumia mpaka natoka Hospitalini, alinisaidia kunyanyuka, kunisukuma kwenye kiti cha magurudumu, kunisafisha na kila kitu.
Hakujali mambo niliyomfanyia mara ya mwisho, hakujali kua siku naondoka mbali na kuwa niliacha kumpeleka Hospitalini lakini mchana wake nilimpiga na kumuambia akusanye kila kilichochake nikirudi nisimukute ili tu kuishi na Mariam. Nilikua nikimuangalia naona aibu kwa kukumbuka mambo ambayo nilimfanyia na namna mabavyo hakujali kitu chochote.
Marafiki walikuja mwanzoni lakini kila siku zilivyokua zikienda walikua wakipungua, mpaka natoka Hospitalini walishapotea wote, na nilipofukuzwa kazi sikuwaona kabisa, hata simu zangu walikua hawapokei kwani waliona kama ninawapigia ili kuwaomba fedha. Mke wangu alisimama na mimi na kila mara nilipotaka kuomba msamaha alinizuia na kuniambia kuwa alishanisamehe ni Shetani amenipitia.
Kazi kubwa kwangu haikua kupona kazi kubwa ilikua ni maisha baada ya mimi kupona, sikua na pesa kabisa, pesa nilizokua nimelipwa kama mafao baada ya kuachishwa kazi ziliishia katika matibabu hasa matumizi kwani mke wangu alikua hafanyi kazi. Ndugu ambao wengi nilikua nawasaidia hata wale wa tumbo moja ambao kila siku nikilalamika kuhusu mke wangu walikua wakiniambia nimuache walikimbia kabisa.
Kama marafiki zangu nao walikua wakija kuniona mara moja moja kuacha elfu kumi na kutokomea. Kazi kulikua hamna siajiriki, mke wangu nilishamkataza kufanya kazi kwa sababu ya wivu, mara kadhaa alifungua vibiashara lakini nilimkataza na kumuambia kuwa ananidhalilisha mimi na pesa zangu, alipokua akiniomba mtaji nilikua nikimtukana na kumuambia hana akili za kufanya chochote atanipotezea pesa zangu.
Baada ya ajali sikua na namna mke wangu ilibidi kuanza kufanya biashara, alikua akipika vitumbua na maandazi na kuzunguka mjini kuuza baadaye alipika na sambusa. Kwakua sikua na kazi na mikono ilikua inafanya kazi nilimsiadia kwa kila kitu, sasa hivi tumeweza kufungua Mgahawa wetu mkubwa tu, tuna mabanda matatu ya Chips, tumeweza kujenga nyumba mbili na magari matatu vyote hivyo vikiwa ni juhudi za mke wangu.
Nizaidi ya miaka kumi sasa tangu hili jambo kutokea, bado niko na mke wangu na tunaishi vizuri. Nimeandika kisa changu kwani nilitaka kuwaambia wanaume wenzangu wenye tabia kama zangu kua, kuna watu wapo karibu na wewe, wanakusifia na kujifanya kukupenda kwakua tu wanapata kitu flani kutoka kwako. Watu wengi tunaowaita marafiki wanasababu za kuwa karibu na sisi siku sababu hizo zikiondoka nao wataondoka.
Hao wote unaokunywa nao Bia leo hawatabaki na wewe siku ambayo utakosa hela ya kununulia Bia, watakuvumilia mwanzoni kisha watarudi na kuanza kukusimanga na kukutenga kabisa. Huo mchepuko wako upo kwakua unauhudumia na si uanaume wako, siku ukishindwa kuuhudumia basi utaondoka na mwisho wa siku utarudi kwa huyo mkeo ambaye unamuona takataka leo, hivyo mtumze leo ukiwa na nguvu kwani hujui ni lini utadondoka.
0 Comments