Header Ads Widget

Responsive Advertisement

SAFARI YANGU KWAKO




 Safari yangu kwako

Nafurahi sana kuunganika na wewe katika safari hii. Najua umejiuliza kwa muda mrefu bila kupata majibu. Unajua ni safari gani? Safari ambayo niliitoa kwa mara ya kwanza hata na wewe ukasisimka sana nakuomba iendelee. Unaikumbuka? Safari iliyonitoa machozi mengi sana na hata hapa ninapoiandika safari hii kwako bado machozi yananitiririka. Sina maana nitaacha kusafiri la hasha! Nipo na wewe na nataka tuwe wote safarini. Tuanze kwa kusafiri.
Wengi wanasema safari inaweza kumfanya mtu kufikia kujiua kwa kunywa sumu hata kujinyonga. Na wegine wanakuwa na wivu wa safari hii. Lakini kwa sisi ambao tumefanikiwa kusafiri japo kidogo tunaifurahia sana huku tukicheka kwa pamoja tukipeana pongezi. Embu endelea kufumba macho yako. Tazama safari inavyomtesa rafiki wako wa karibu, ndugu yako. Tazama sebuleni kuna kikao cha usuluhishi juu ya safari hii ambayo kwa wengine inakuwa na utata. Tazama yule anashindwa kupata usingizi nakuongea kila muda kwenye simu kisa anafurahia yupo safarini . Vidole vyake vinamuuma kwa kubonyeza ovyo simu yake kutuma ujumbe mfupi huku akiifurahia safari kwa kila majibu ya meseji yakirudi lakini mwisho wa siku huyo huyo analia sana nakuilalamikia safari kuwa ni mbaya, inamilima na mabonde na inautesa moyo wake. Safari ambayo kwako wewe huwa inakukumbusha ulivyoumia wakati unaianza. Hasira zinakushika kwa kupotezewa thamani yako ya ujana. Najua umeshavuta picha vya kutosha, inamaana mpaka hapo hujaelewa ni safari ipi nazungumzia..? kama bado tazama hii.
Patricia Emmanuel, alitamani sana siku moja naye asafiri kama mimi na wewe tulivyokuwa ndani ya safari. Akauchukia sana ujana wake kwakuwa hakuwa akijua nini maana ya safari.Ushawishi wa marafiki zake juu ya kuingia katika mtandao wa facebook ukaonekana kumuingia sana akilini. Marafiki zake wakampa maneno matamu na hata kumtamanisha kwa safari na kumwambia kuwa atakapokuwa facebook ataifurahia sana safari. Kwani anaweza kuanzisha safari na mwanaume yeyote amtakaye. Patricia akatamani sana kusafiri. Usingizi kwake ukawa shida huku akiitamani siku naye asafiri. Hakuwa na kompyuta nyumbani kwao lakini kutokana na utamu wa safari alioukuta facebook akajikuta pesa yeyote anayoipata nikukimbilia intaneti ili mradi aone utamu wa safari. Akaenda sehemu wanazopiga picha akapiga picha nzuri sana kisha akairemba katika ukurasa wake wa mbele wa facebook. Kila mwanaume akalilia safari na yeye. Utamu ukamzidia Patricia akajikuta anasafiri na kila mmoja aliyemtumia ujumbe mfupi facebook. Shukrani akazipeleka mpaka kwa wale waliomshawishi afungue akaunti facebook nakuwaandikia ujumbe kwenye kurasa zao.
“Naipenda safari. Sasa nimejua nini maana ya safari..”
Safari ikawa ndefu kwa Patricia. Wapo ambao walidandia safari yake, Patricia hakujali hata kila mmoja akasifiri naye. Leo hii Patricia analalamikia safari mbaya nakudai hakuna cha maana alichopata. Hivyo anasimama anataka ashushwe hataki tena kusafiri. Safari sasa imekuwa chungu mbele yake. Safari imemgombanisha na marafiki zake hivyo hataki kusikia neno safari. Taarifa za Patricia juu ya kuiacha safari yake sasa ikawa imemuingia vilivyo Charles masikioni kwake. Akaguswa sana na safari alioiacha Patricia. Akamtafuta Patricia kila pande alipo akampata nakisha kila mmoja kuhadithiana safari zao zilivyokuwa. Wakaapa kamwe hawatajiingiza katika safari nyingine mpaka kila mmoja atakapooa ama kuolewa. Urafiki wao ukaendelea kuwa mzuri bila ya kusafiri popote. Charles na Patricia wakamrudia mwenyezi Mungu. Ikawachukua miezi mitatu tu kuhudhuria kanisani na kufanya maombi ya mara kwa mara sambamba na vikao vya kanisa. Hatimaye uzalendo ukawashinda baada ya kuvumilia kwa muda mrefu wasisafiri huku udenda ukiendelea kuwatoka kanisani kuona baadhi ya waumini wakifurahia safari na wenzao. Charles ndio alikuwa mtu wa kwanza kukata tiketi ya kusafiri. Akamfuata na Patricia na kisha kumnong’oneza.
“Turudi kwenye safari yetu. Nataka tusafiri tiketi hizi hapa..”
Patricia akaonesha kusisimkwa kwa mwili. Mawazo yake yakamrudisha mbali sana. Enzi zile ananyeshewa na mvua na kwa uchovu wa safari nakulowana. Akakumbuka mvua hiyo akiwa safarini na mwanaume wake wa kwanza ikamfanya kuteleza kwenye tope zito nakukasirika sana kitendo cha mwanaume wake kumcheka kwa kuanguka. Akakumbuka lile tukio kwa jinsi alivyokuwa na hasira wa ile safari akaiona chungu. Lakini mwisho mwanaume wake akamfuata na kumbusu kisha akavua shati lake nakumfunika huku nalo likiwa limelowa chakari. Akahisi joto kutokana nakuendelea safari huku mvua ikimnyeshea. Utamu wa safari akaufurahia. Sasa leo hii akajikuta akimjibu Charles kwa msisimko ule ule.
“Tiketi umesema unazo..?”
Charles akajibu kwa kutumia kichwa kisha akaonesha tabasamu pana kwa Patricia huku akimpa tiketi.
“Nipo tayari kusafiri na wewe Charles usiniache..”

Charles akafarijika sana moyoni mwake. Akahisi moyo umetawaliwa na ubaridi mkali. Ndoto yake kubwa siku zote ilikuwa ni kusafiri na mwanamke ampendaye. Mwanamke ambaye angempikia chakula nakula wote. Mwanamke ambaye watazaa naye watoto nakufurahi pamoja. Sasa Charles akili ikamrejesha mpaka chumbani kwake. Akawaza kama amejipumzisha kwenye kitanda huku Patricia yupo mgongoni mwake akimfanyia mesaj. Akawaza siku ya kufurahia safari yao wakiwa kanisani.
“Charles gari lenyewe si hilo hapo limefika tupande twende..??”
Charles akawa bado hajielewe elewi kwa bumbuwazi ya safari yake na Patricia. Bado akawa anaona kama ndoto. Kwa jinsi Patricia alivyoumbika kamwe akajiona hawezi kuwa na bahati ya kusafiri naye. Wakapanda basi wote pamoja tayari kwa safari. Njia nzima ikawa ni furaha kwa Patricia na Charles. Furaha ya kusafiri pamoja. Ile hali ya kusafiri na kila mmoja katika facebook Patricia akaiweka moyoni mwake. Akahaidiana na moyo wake kuwa kamwe hatokuja kumfanyia Charles na kifo tu ndio kitawatenganisha safari yake na Charles.

******

Safari ilikuwa ndefu sana kwa Patricia na Charles. Sasa wakawa wameshashuka kwenye basi. Walipofika tu nyumbani kwa Charles, Patricia akawa mtu wa kwanza kuinama mpaka miguuni kwa Charles na kumvua viatu kisha soksi zake. Charles akafurahi sana. Tabasamu kubwa akalitoa na kisha kumbusu Patricia.
“Safari yetu ilikuwa nzuri sana. Ila bado tu wasafiri Patty”
“Ndio Charles. Unaniahaidi nini katika safari hii..?”
“Nakuhaidi kukupenda. Kuwapenda ndugu zako. Kukuheshimu nakukujali wewe pamoja na wazazi wako..”
“kweli Charles..??”
“Ndio Patty..!!”
Patricia akasisimka mwili wote. Maishani mwake alizoea kusafiri safari fupi fupi. Safari ambazo mara nyingi alikuwa akisafiri na wanaume mbali mbali wa facebook na hata mtaani mwao. Kamwe hakuwahi kuonja utamu wa safari ndefu. Charles pekee ndio aliomuhaidi kusafiri naye safari ndefu. Safari ambayo kamwe hatoijutia maishani.
“Nakupenda sana patty..?”
“Nakupenda pia..”
“unanihaidi nini na wewe patty wangu..?”
“Mhh..!! mimi nitakuwa wa kwanza kufanya kila ulitakalo. Kuanzia kukuamsha kwenda kazini asubuhi mie nitakuwa mtu wa kwanza kuamka. Utakuwa ukikuta maji bafuni nimeshakutayarishia asubuhi na mapema kabla hujaamka. Ukiriudi kazini utakuwa unakuta tayari nimeshakutayarishia chakula. Nitakupokea vizuri. Nitakupeleka mpaka chumbani kwetu nakukuvua nguo kisha nitakuvalisha taulo halafu tunaelekea bafuni kukuogesha. Amini utaipenda safari yangu kwako..”
“Mpaka nimesisimka Patty. Nakupenda sana. Enhh kingine..?”
“kingineeeee..!!!, Nitakuwa nakupa moyo kwenye wakati mgumu kama vile matatizo ya misiba mbali mbali. Nitahakikisha nakuzalia watoto wazuri na kuwalea kwa maadili mema. Pia napenda sana surprise hivyo nitakuwa nakufanyia kila mara kama vile katika siku yako ya kuzaliwa nitakuwa nikikumbusha. Hata nikipata ujauzito nitakufanyia surprise kukuambia. Siku yetu ya kwanza kuanza safari nitakukumbusha kuanzia tulipokutana mpaka tukawa wacha Mungu na ndipo ukanikatia tiketi hii. Siku za kuzaliwa watoto wetu. Na hata kukutafutia zawadi mbali mbali kwa kila kizuri utakachonifanyia..”
“Nitafurahi sana na safari. Wewe ndio msafiri wangu wa maisha Patricia..”
“sawa nakupenda sana charles pliiz usiniache katika safari yetu hii tulioanzisha..”
“Nakuhaidi sintokuacha na kukata tiketi kwa mwingine..”

Patricia akajiona ni mtu mwenye bahati duniani. Bahati ya kumpata mwanaume mzuri sana kisura na hata kimawazo. Mwenye kujua nini maana ya maisha. Baada ya miezi mitatu tu ya safari yao, Charles akaanza kubadilika. Zile ahadi alizohaidiana na Patricia akazidharau. Kazi akafukuzwa kutokana na uzembe wa kwenda kazini akiwa bado yu mlevi. Patricia akajitahidi sana kumfariji kwa kumpa moyo atafute kazi sehemu nyingine lakini jitihada zote zikashindwa kufanikiwa kutokana na Charles kutotilia maanani. Maisha yakawa magumu sana kwa Partricia. Zile surprise alizomuhaidi kumfanyia mumewe zikageuka kuwa sumu. Uvumilivu ukamshinda kutokana na Uchungu wa safari. Kamwe alipenda kusafiri na mumewe muda wote akirudi kazini lakini mumewe akawa anadai amechoka hataki habari za safari. Patricia akawa kama yatima asyejiweza hata kwa nauli ya kukata tiketi tena. Hakubahatika kupata hata mtoto kutokana na kushindwa kusafiri mara kwa mara na Charles wake. Akafikiria sana maisha ya nyuma walivyokuwa na Charles kabla hawajaianza safari yao. Sasa akawa anaijutia kwa mara ya pili baada ya ile ya kwanza facebook. Uvumilivu wa miaka kadhaa bila ya kusafiri ukamshinda. Akawa anamtoroka mumewe Charles kila akitoka kwenda kwenye mishughuliko yake basi na yeye nyuma anatoka. Abdul ndio akawa msafiri wake wa pembeni. Patricia akajiona anafaidi safari na Abdul kuliko alivyo na Charles. Safari ikawa imemnogea Patricia mpaka akajikuta anabeba ujauzito wa Abdul. Akataka kuhamia kwa Abdul lakini ikashindikana kutokana na vitu viwili. Kwanza abdul alikuwa akiibia safari ambayo si ya kwake. Abdul alikuwa na safari na mkewe wa ndoa. Na kila mara walikuwa wakisafiri na mkewe hivyo kutokana na tamaa tu ya kusafiri nje ya ndoa akajikuta amesafiri na Patricia.
Woga ukaanza kumtawala Patricia. Patricia akawa njia panda. Njia panda hajui ujauzito aupeleke wapi. Ujauzito ukaanza kukuwa taratibu bila ya Charles kujua. Abdul akaikimbia safari ya Patricia. Akamtukana sana Patricia kwa kuwa mzembe safarini hata kipindi cha hatari hakumtaarifu hadi amepata ujauzito. Abdul akajitoa rasmi kwa safari na Patricia na kugeukia safari yake na mkewe wa ndoa.
Baada ya miezi minne mabadiliko ya mwili ya Patricia yakaanza kubadilika taratibu. Mwili ukanenepa sana. Tumbo likaanza kujaa sambamba na miguu kumvimba. Kichefu chefu cha mara kwa mara kikamtawala Patricia. Wasiwasi ukaanza kujijenga kwa Charles ambaye alikuwa na muda mrefu kutokusafiri na Patricia. Hasira kali zikamjaa Charles kwa kujiona mume bwege. Akaamua kulitoa duku duku lake moyoni.
“Huo ujauzito umeupata wapi mke wangu..?”
“Ni wako Charles. Na niliupata siku nyingi ila nilitaka kukufanyia suprise kabla hujagundua lakini kwa kuwa umegundua haina haja tena ya kukwambia..”
Patricia alijibu kwa kujiamini huku akiyachezesha macho ya wizi kwa Charles. Charles alijua fika ujauzito si wa kwake kutokana na tetesi za mtaani kuwa mkewe anatembea na Abdul. Alichokifanya ni kumshika mkono Patiricia mpaka hospital kupima huo ujauzito utakuwa wa nani..

***************


:::: Najua wasafiri tu wengi sana katika hii safari. Na kama haijawahi kukuta safari hii basi itakukuta lazima. Patricia ameamua kusafiri na Charles. Na Charles akabadilika. Unavyodhani Safari itakuwaje kwa Patricia huko mbeleni..

:::: Nadhani umeshajua maana ya safari, kama bado utaelewa tu hii safari ninayomaanisha.. tuendelee kusafiri..

Post a Comment

0 Comments