JE TUPO WENYEWE KWENYE ULIMWENGU? Season Finale, Ep 3 (Time Reference..)
Time, nyakati ni kitu cha ajabu sana … tulipo ishia kwenye posti ya mwisho, itahitaji tujue kitu cha maajabu kinacho itwa ‘time’, bila kukijua hicho, hatuwezi kunyanyua mguu mmoja kwenda mbele.
Time ni mada pana sana, huenda siku moja nikaja kuitiririsha hapa, lakini kwa leo nitaigusa kidogo kwa minajili ya mada yetu, ili tuweze kulijibu swali tulilo achana kwenye posti iliyo isha.
Tumeona kuwa kile ambacho kinafikiwa na milango yetu ya fahamu ni pungufu kwa asilimia 99.99..., dhidi ya kile ambacho hakifikiwi na milango yetu ya fahamu kwenye ulimwengu wote.
Ulimwengu wetu tunaugawanya sehemu kuu mbili, ulimwengu wa kiwiliwili, na ulimwengu wa roho. Asilimia 99.99 … % kwa lugha nyepesi tunaweza kuita ndiyo ulimwengu wa roho, na kilicho bakia ndiyo uliwengu wa kiwiliwili.
Hivyo kitu kinacho itwa ‘time’ tunaweza kukigawa kwenye aina mbili hizi za ulimwengu, yaani ulimwengu wa kiwiliwili na ule wa roho.
Time kwenye ulimwengu wa kiwiliwili tunaigawa sehemu tatu, ‘past, present na future. ’Time’, kwenye ulimwengu wa roho haina sifa hizo tatu tulizo taja, inayo sifa moja tu, ‘NOW’.
Neno ‘Present’ na ‘Now’ kama hayana tofauti, lakini kwenye hili la kiumbe kinacho itwa ‘time’, maneno hayo yanayo tofauti, na hapa ‘time’ tunaielezea kutoka kwenye nukta ya multdimensions.
Hivyo tunajaribu kuitohoa ili iweze kueleweka kwenye 3D, ndiyo maana neno ‘present’ na ‘now’ nime yatofautisha ili walau kuweza kupata mwanga wa nini hasa ‘time’ kwenye multdimensions, lakini pia ‘now’ haitoshi kuelezea hasa hiyo nukta kama ilivyo ya ‘time’ kwenye multdimensions, lakini walau itatupa mwangaza.
Mwishoni mwa WWII, Marekani walikuwa wamesha shindwa vita vibaya mno, na walikuwa na kila sababu ya kutaka vita hiyo imalizike.
Hivyo kipindi hicho kukawa na ‘project’ nyingi, kubwa na za siri zilizokuwa zikifanywa kwa lengo la kutengeneza silaha ambayo itawawezesha Marekani kuimaliza vita hiyo.
Moja ya ‘project’ hizo ni ‘Philadeliphia Experiment’ ambayo ilifahamika kama ‘Rainbow Experiment’, lango la mradi huu ilikuwa ni kutengeneza ‘elcotromagnetic’ kuizunguka meli ya kivita, na hivyo kuifanya isiweze kuonekana kwenye rada ya maadui.
Meli iliyotumika kwenye zoezi hili ni meli kubwa ya kivita ‘USS Eldridge’, ilipofika mwaka 1943 mpango ukakamilika na majaribio yakafanyika. Lengo ilikuwa ni kuificha meli hiyo isionekane kwenye rada za maadui, lakini jambo la maajabu likatokea, ‘mazingaumbwe,’ yakawa makubwa zaidi ya matarajio.
Meli ya USS Eldrige, si kwamba ilipotea kwenye rada ya maadui, lakini ilipotea mbele ya jicho la kawaida, na zaidi ilipotea kwenye ‘time frame’ ya Philadelphia, ilitoweka kama kizuka, now you see it, now you not. Kifupi ilitoweka kwenye 3D!
Masaa 24 baadae, meli hiyo ikaibukia Norfolk, Virginia, mamia ya maili kutoka ilipo kuwepo awali! Napo iliibuka ghafla kama kizuka, au utadhani imeshuka kutoka mbinguni. Hivyo kwa masaa 24 meli hiyo ilikuwa kwenye ‘hyper space’ au multdimension, au uwanda wa zaidi ya 3D! Kisha meli ikatoweka tena kutoka Norfolk, na kurudi Philadelphia kama kizuka.
Mradi ulikuwa umefanikiwa kwa lengo la meli kutoweka kwenye rada, lakini ulifanikiwa zaidi sababu meli iliweza kutoweka eneo hilo na kutokezea eneo jingine, kama kufumba na kufumbua.
Lakini mradi ulifeli kwa zaidi ya asilimia 100 kwa upande wa wanamaji na askari walio kuwemo ndani ya meli hiyo wakati ikifanya safari zake hizo za maajabu kupitia ‘uchawi wa mzungu.’
Wanamaji, wafanyakazi na askari wote walikuwa wendawazimu, hao ni wale walio fanikiwa ‘kurudi’ salama, wengine walirudi lakini miili au viungo vyao vimenasa kwenye sehemu ya meli hiyo, yaani mtu anaonekana kichwa tu, sehemu nyingine ya mwili haipo, au mkono tu, au nusu ya kiwiliwili tu, na kuna wengine hawakurudi kabisa, walibaki kwenye ‘hyper space’.
Si zungumzii uchawi, au ushirikina hapa, nazungumza sayansi, tena sayansi ya daraja la kwanza, hamna bao wala ramli hapa.
Ni kama ‘science fiction’ lakini hilo ni kweli lilitokea, fanya utafiti wako binfasi na utalipata hilo na zaidi.
Mwishoni wa miaka ya 1949 mradi wa ‘Project Rainbow’ ulifufuliwa tena. Baada ya kile kilicho tokea hasa kwa upande wa binadam wakati wa majaribio, serikali kwa maana ya bunge la Marekani liliingilia kati na kuufunga mradi huo. Lakini mwishoni mwa miaka ya 1940 dude likaamshwa tena, lakini mara hii wakiwa na lengo jingine tofauti.
The Dream Team
Mara hii wakiwa na timu ileile iliyofanikisha ‘Rainbow Project’, lengo ilikuwa ni kutizama kwanini binadam aliathiriwa na ‘electromagnetic’ kwa kiasi kile na vipi wanaweza kuliepuka hilo, sababu walicho kivumbua kwa upande wa jeshi ni kitu adimu na lazima kiboreshwe na kitumike, lakini kasoro zilizo jitokeza mara ya kwanza zisiweze kujitokeza tena.
Iliwachukia miaka 10 kwa wanasayansi na mainjinia hawa kuja na jibu au suluhisho dhidi ya kile kilicho wapata binadam kwenye jaribio la kwanza la mradi.
Mara hii wakagundua kuwa binadam yoyote, anapozaliwa anakuja na kitu kinacho itwa ‘time reference’, wakati wa ujauzito, roho inapo dumbukizwa kwenye kiwiliwili inakuwa ina fungamanishwa na ‘time’ au nukta ya kuanzia; hivyo kiwiliwili (mind), roho, na time vina fungamanishwa pamoja.
Kumbuka kuwa time kama ilivyo roho inayo sifa za ‘multidimension’, lakini ‘time’ ambayo ina fungamanishwa hapo inakuwa ni ‘time’ yenye sifa za 3D, yaani (Past, present na future).
Lakini pia kama tulivyo sema hapo juu, time ya kwenye 3D, siyo ukweli wote kuhusiana na kiumbe hichi tunacho itwa ‘Time’, bali ni tuna amini hivyo kwasababu ndivyo maumbile yetu yalivyo, lakini si kila unacho amini ni kweli, na hichi ni kimojawapo.
Time ni ‘Illussion’ iliyo jengwa kwenye mazingira yetu haya ya 3D, na kama tulivyo ona, kwenye 3D, time inayo sifa hizo kuu tatu, ambazo kwenye ‘hyper space’ sifa hizo hazipo.
Sasa basi kilicho wapata binadam walikuwepo kwenye meli ile ya kijeshi ni kwamba meli ile ilikwenda kwenye ‘hyper space’ kabla yakuja kutokezea Norfolk, kisha ikarudi tena kwenye Hyper space, kabla ya kutokezea Philadelphia tena.
Time iliyo fungamanisha na ‘roho’ na mind za binadam wale ni 3D, lakini kwenye ‘hyper space’ hakuna 3D, ‘mind’ kiwiliwili cha binadam hao, hakikiweza kumudu hicho; hayo maumbile mapya ya kiumbe kinacho itwa ‘time’, sababu kwenye ‘Hyper space’ vyote present, past na future vipo sehemu moja.
Yaani kwenye HYPER SPACE, wewe unazaliwa, unaenda shule, unaoa, uko kazini, unakufa n.k vyote hivyo ndani ya ‘NOW’, siyo, akili, wala kiwiliwili vinavyo weza kuhimili aina hiyo ya maumbile ya ‘TIME’, hivyo miili yao, ikayeyuka, wengine wakapotelea huko, na wale walio himili na kurudi kamili walikuwa wendawazimu.
Imepokewa kwa Abu ‘Abdir-Rahmaan ‘Abdullaah bin Mas’uud (ra) kwamba:
“Ametuzungumzia Mtume wa Allaah (SAW) naye ndiye msema kweli wa kuswadikika: Hakika kila mmoja wenu katika nyinyi hukusanywa umbo lake katika tumbo la mama yake kama mchanganyiko wa mbegu ya uzazi ya mwanamme na mwanamke kwa muda wa siku arubaini; kisha kuwa kipande cha damu kwa muda kama huo; kisha kipande cha nyama kwa muda kama huo. Kisha hutumwa Malaika akampulizia roho ndani yake na akaamrishwa mambo manne: Kuandika riziki yake, ajali yake, ‘amali yake na kama ni mwema au muovu…” (al-Bukhaariy na Muslim).
Hadithi hiyo inatufundisha kile kilicho gunduliwa kwenye ‘Rainbow Project’ na muendelezo wake, kwamba wakati ‘kiumbe’ anaye itwa roho anapoingizwa kwenye kiwiliwili kuna mambo ambayo yana fungamanishwa naye ikiwemo, ‘Time’, hapo imekuja kama ‘ajali yake’, yaani umri wake au muda atakao ishi mpaka umauti wake; ‘Time.’
Ndiyo utaona mara hii ya pili timu ya wanasayansi, wakagundua kuwa, ‘time reference’ inakuwa pamoja na roho, wakati roho inapo puliziwa.
Utakumbuka huko nyuma tumeona ‘Darwin na wenzake wanakana juu ya uwepo wa roho, lakini utaona hapa kwenye kiwango cha kisayansi, tena wanasayansi wa kiwango cha juu wanathibitisha juu ya uwepo wa roho.
Mradi huu kwenye hatua yake ya mwanzo, mtu kama Albert Einstein, Testla na vichwa vingine, kwenye taaluma ya fizikia, mahesabu, electromagnetic, metafizikia, nk; walikuwepo kwenye mradi huu, hivyo hatuzungumzii wanasayansi wepesi wepesi.
Sasa basi ukisha mjua adui yako, umesha shinda nusu ya vita, wanasayansi wale waligundua shida ni, ‘Time Reference’, ambayo kwenye kiwiliwili na roho ni kama ‘orbit’ za sayari kulizunguka jua. Muda wote sayari hizo zikiwa kwenye ‘Orbit’ zao, zinaendelea kuwa ‘hai’ na salama, na ndivyo kwa binadam, muda atakao kuwa yupo kwenye ‘time reference’ ya 3D, atabaki salama.
Kama nilivyo sema, dunia yetu kwenye uso wa ulimwengu ni kama chembe moja ya chumvi, au kamchanga kamoja! Hapo binadam na vurugu zake zote kwenye uso wa ulimwengu ni kakitu kasicho tajika, kaduchu mnooooo, lakini mbali na yote hayo binadam huyu ame fungamanishwa na ‘network’ ya jiulimwengu lote kupitia ‘time reference’, ambayo ni kama ‘orbit’ yake.
Kuna uwiano baina ya maumbile yetu na baadhi ya vitu vya angani, kama nyota, mwezi n.k. Mathalani watoto wachanga wanaathirika sana na mwezi unapokuwa kwenye vituo flani flani, kwa wale wazazi wanajua haya. Lakini pia watu wazima kuna namna ambayo mwezi unatuathiri unapokuwa kwenye baaadhi ya vituo. Athari hiyo moja ya sababu nyingi ni ‘time reference’, mwili na roho zimefungamanisha na ‘time reference’ ambayo nayo inayo mafungamano na ‘electromagnetic’ za sayari yetu hii, tunayo iita dunia, ambayo nayo umefungamanishwa na ulimwengu mzima.
Time reference ndiyo dira yako sasa kama kiumbe kwenye ulimwengu huu wenye magalaxy, nebula, solar systems, sayari, nyota na kila chungu ya kila tunachao kijua na tusicho kijua kwenye ulimwengu huu.
The cat in the box is dead and alive at the same time (time mystery)
Nukta yako ya maingiliano na ulimwengu huu, kwamba wewe ni sehemu ya ulimwengu huu, ni ‘time reference.’ Ukitoka kwenye hii ‘time reference’, ni kama sayari inapo toka kwenye ‘orbit’ yake, inapotea kwenye ‘space’, na kudhurika huko, hivyo na binadam ili asipotee kwenye ‘hyper space’ orbit yake ni ‘time reference’ ya 3D.
Hivyo kilicho watokea watu walio kuwepo kwenye meli ile ya kivita ya Marekani ni kwamba, walihama kwenye ‘time reference’ ya 3D, na kuingia kwenye ‘Hyper Space’ ambako nako kunazo ‘time’ za aina kwa aina na idadi yake ni ngumu kuzidhibiti, huwenda ikawa na matrilioni kama siyo mazilioni ya ‘time’ tofauti tofauti, na ndiyo maana kuna ambao hawakurudi mpaka leo, kuna ambao viuongo vyao vilibaki huko na walio rudi walikuwa ni wendawazimu.
Kwenye tamthilia ya Lost, kwa wale walio tizama, mtakumbuka baadhi ya matukio yaliyokuwa yanahusiana na ‘electromagnetic’, pamoja na ‘time shift’
Desmond, kwenye tamthilia hii, mwili wake uliweza kuhimili ‘electromagnetic’ kwa kiwango cha juu mno. Hivyo aliweza kuhimili kusafiri kwenye ‘hyper space’ na 3D lakini alihitaji kitu kinacho itwa ‘Constant’ kumfanya asiweze kupotea, anapokuwa kwenye ‘Hyper Space’ na anaporudi kwenye 3D aweze kukumbuka nini kilimtokea kwenye ‘Hyper Space’.
Hicho kinachoitwa ‘constant’, ndicho ambacho timu hii ya wanasayansi walikigundua na ndicho ambacho kinatakiwa kuwepo pamoja na mtu anayesafiri kwenye ‘hyper space’ ili kumu wezesha au kumbakisha na kumbukumbu kama vile yupo kwenye ulimwengu wa 3D.
Wanasayansi hao wakaja na suluhisho la kutengeneza kile kitakacho fahamika kama ‘alternate reality’ au ‘artificial reality’. Hii inatakiwa kuhakikisha kuwa wakati watu hao wakiwa kwenye ‘Hyper Space’, kiwiliwili au akili zao ziendelee kusoma ‘time reference’ ya kwenye 3D, kama vile bado wapo kwenye dunia yetu hii.
Walicho fanya wanasayansi wale ni ‘ku-streaming’ bila kukoma mazingira ya sayari yetu hii, kupitia kompyuta, kwenda kwa watu ambao wako kwenye meli na hivyo kuwafanya wahisi bado wako kwenye ulimwengu wa 3D, wakati wakisafiri kwenye Hyper space.
Hilo lilifanikiwa, … mengi yaliendela baada ya hapo lakini kwa ajili ya majibu ya swali letu haya yanatutosha.
Tururdi mbinguni
Kwenye aya ile ya Quran; (7:172), tumejifunza kuwa tulisaini mkataba na MUNGU MMOJA, lakini kwa sababu tusizo fahamu hakuna kati yetu anayekumbuka kuingia mkataba huo na MUNGU MMOJA, na wengine kufikia kusema hakuna kitu cha namna hiyo!
Lakini hapa tumejifunza kitu kimoja muhimu sana, japo kwa uchache lakini kwa muktadha wa mada yetu; tumejifunza kuwa time ni ‘mystery’, lakini inayo mafungamano mahususi na roho na kiwiliwili chetu. Zaidi kila ulimwengu unayo ‘time reference’ yake tofauti na ulimwengu mwingine.
Mkataba ulifanyika kwenye ulimwengu mwingine ambao ni ‘Hyper Space’ (mbinguni), tulipokuja duniani kwenye uliwengu wa 3D, tuka fungamanishwa na ‘Time reference’ ya hapo. Kimaumbile kama tulivyo ona awali, nukta hiyo ya mkataba inafutika hapa kwenye 3D, lakini haimaanishi kuwa haipo au haijatokea.
Kama tulivyo ona kwenye Hyper Space, wewe ndiyo unazaliwa, ndiyo unakufa, ndiyo unaowa, ndiyo unapata mtoto wa kwanza, ndiyo unapata mtoto wa pili na kuendelea, ndiyo unakufa, ndiyo tunakuzika, ndiyo tunafanya kumbukumbu ya kifo chako na mengine na mengine, yote yanafanyika kwenye nukta moja inayo itwa NOW.
Yote yamesha tokea na yamesha fanyika, tena kwa ukamilifu wake.
Je kuna unalo kumbuka kati ya hayo?
Jibu ni hapana.
Kwanini?
Sababu hiyo ni nukta ambayo kwenye 3D, huwezi kuifikia bila kuihama hii ‘Time referenece’ na kwenda kwenye ‘Hyper Space’ au ‘Hyper Dimensional’.
Ndiyo maana kwenye ile aya, MUNGU MMOJA, anatugusia tutakacho kisema siku hiyo, hatutasema kwamba hatuja saini huo mkataba, bali tutasema ‘tulisahau/ tulighafilika/ tuliyafata tuliyo wakuta nao wazee wetu, lakini hatutakana kuwa hatukufanya hayo makubaliano.
MUNGU MMOJA, kwa Rehema zake ikawa kila zama anatuma mitume, na moja ya mengi waliyo tukumbusha ni huo mkataba, na walikuja na dalili na hoja ambazo zilithibitisha kuwa hawakutumwa na mwingine ila MUNGU MMOJA, hivyo ujumbe wao ni wa kweli na walilo kuwa wakitukumbusha ni la kweli.
Tulikuwa mbinguni, kabla ya kuondoka, tukaona ni vyema, tukalizungumzia hili la 'mkataba' tuliyo usahau, ... nimeweza kuweka sababu za kwa nini tumesahau, na tena kwa kuangalia upande wa sayansi ya roho, kiwiliwili na akili bila kusahau dini kwa ujumla wake ... nadhani nimelijibu vizuri swali hilo ni kwenu nyie wasomaji kutoa dukuduku sasa ...
Next time tunarudi duniani Inshallah ... na tutakutana na ushahidi wa kushikika juu ya kuwepo kwa binadamu mwenye maumbo makubwa kama kimo cha Adam (as), ushahidi juu ya binadam kuishi na Dinosari kipindi kimoja, n.k
STAY HERE, STAY IN NOW ....
See you soon Guys .... Tchaoooo ...
0 Comments