Header Ads Widget

Responsive Advertisement

ALL OF ME



SIMULIZI FUPI - ALL OF ME



Nyota njema huonekana asubuhi, hivyo ndivyo waungwana wanavyosema. Hata mimi nasadiki maneno hayo. Maana Kila siku niamkapo asubuhi huwa naijua kua siku hiyo huwa na furaha kwangu au huwa ya kawaida kulingana na kipato changu nikiingizacho baada ya kufanya kazi usiku kucha.

Wengi huniita Shamira, au Shammy. Ila mimi hupenda kujiita Queen kutokana na muonekano wangu na jinsi ninavyojikubali.

Zamani nilikua naishi temeke mikoroshi, ila kwa sasa nimepangiwa upande mzima na mwanaume anayenimiliki ambaye ni mume wa mtu.

Mbali na ufadhili huo niliofadhiliwa, lakini mimi ni mmoja kati ya ndege aina ya kunguru. Huwezi kunifuga. Hivyo siku zote niliamini kuwa jasiri haachi asili na mimi niliona vigumu kuacha asili yangu iliyonifanya nipate kile ninachokihitaji kwa haraka.

Sijui Idadi ya wanaume niliolala nao mpaka sasa, ila ninachojua kua hakuna mwanaume ambaye aliugusa mwili wangu na kuacha kuurudia. Na hakuna mwanaume ambaye aliijutia laki mbili yake aliyoitoa kwangu kwa usiku mmoja aliolala na mimi.

Kuna waliokua wanalia na kunipigia magoti na kuniambia kua wapo tayari kunioa. Niliwaangalia na kuwacheka. Maana ndani ya moyo wangu sikua na chembe hata ya ukubwa wa mchele ya upendo juu ya mwanaume yoyote.

Bali pesa ndio alikua bwana wangu wa ukweli na nilimpa moyo wangu wote. Na daima nilimuabudu na kumfuata popote pale alipo.

Rangi yangu ya ung`aavu ndio iliokua inawachanganya wanaume wengi. Pia uteke wa kifua changu na umri ndio kumefanya niwafanye watu waathirike kisaikolojia pindi wanionapo kwenye anga zangu.

Hakuna mtu yoyote mtaani kwetu ambaye alikua anijua kazi niifanyayo, zaidi waliniona tu nikibadilisha nguo kila toleo na chumba changu kilitimia kila aina ya urembo unaotakiwa kuwepo kwenye chumba cha mtoto wa kike.

Mtaani sikua na story na mtu wala kumpa nafasi mtu yeyote kunizoea. Hata wanaume waliokuja kunipigia misele, niliwaagalia kwa dharau na sikuwajibu chochote.

Binti maringo ndio jina nililotungwa huko Temeke na mimi nililipokea kwakua ni kweli nilikua na maringo zaidi ya twiga mbugani.

Mpaka nahama huko temeke na kuhamia hapa kijitonyama ambapo ndio naishi kwa sasa, sikuwahi kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mtu yoyote. Ila huyu jamaa ambaye anamiliki maduka ya nguo hapa mjini, niliamua kumpa nafasi nje ya moyo wangu ili mradi tu aweze kunilipia mahitaji yangu niyatakayo bila kuchukua hata senti tano kutoka kwenywe account yangu.

Kwakua nafasi yake yeye ya kuja kwangu ilikua ni mchana peke yake, hivyo hakuweza kunibana kufanya yangu usiku.

Kwakua mchana huwa nautumia kwa kulala, basi kila akija hunikuta nimetulia ndani mtoto wa kike wala sina dalili za kutoka.

Basi moyo wake huburudika na kujiona amepata tulizo la moyo bila kujua kua alipata gume gume lililoshindikana na wazazi mpaka mabazazi.

Mvuto wangu uliwatosha kuwapa darasa masister doo wa mtaa huo niliohamia kwa jinsi nilivyokua nawakimbiza kwa kila kitu.

Kioo changu cha kujiona mwili mzima kiliniambia kua mimi nilikua na umbo jembamba. Lakini kuanzia kiunoni, nilikua na shape ya kibantu na iliyokua pana na kutengeneza hipsi zilitengeneza namba nane ya ukweli. Kibinda cha wastani nilichojaaliwa na Mungu na sio maujanja ya wachina ndicho kilichowaua wanaume wote waliojaribu kuyageuza macho yao kuniangalia.

Nilijua ni jinsi gani nilivyoweza kuwatesa wanaume wenye uchu wa watoto wazuri kama mimi. Wakati mwengine nilikua nafanya makusudi, ili mradi tu kuwachengua wakwara na walozi wa kufanya mapenzi na mabinti waliokua na hadhi ya nyota tano.

Siku moja wakati nipo kwenye shughuli zangu za usiku. Nilimuona mtu akiwa ana chechemea na kuja upande wetu. Mkononi alikua ameshika fimbo Fulani nyeupe huku akiwa haitumii. Alikua amevaa nguo iliyokua imechafuka na matope karibia suruali yote.

Nillimsogelea na kumkuta akiwa ameanguka chini.

“pole,.. umepatwa na nini kaka yangu.” Nilimuuliza baada ya kuingiwa na imani

Baada ya kumuona amelowana na damu mguuni.

“nimepigwa na wezi waliokua wantaka kuiba visenti vyangu.” Aliongea huku akiushikilia mguu wake huku akionyesha wazi kua alikua anaumia.

“pole.. subiri kidogo.” Niliongea hivyo na kumfuata dereva wa bajaji alikua anakesha maeneo hayo na kwenda nae hadi kwa Yule mtu ambaye nilimkuta amekaa pale pale.

“mpeleke hospitali “ nilliongea baada ya kusaidiana na Yule dereva wa bajaji kumuingiza Yule kaka kwenye bajaji hiyo.

Nilimpa huyo kaka shilingi elfu thelathini kama pocket money kama ikilazimika atoe pesa huko hospitalini, kisha nikamlipa shilingi elfu kumi huyo dereva wa bajaji kama nauli yake ya kumpeleka mgonjwa huyo hospitali.

Mimi sikwenda kutokana na kua na miadi na mshefa wangu wa serikalini muda huo ambaye dakika ishirini baadae alinipitia na kwenda kupumzika nae mpaka asubuhi.

Nilirudi nyumbani na kujifungia ndani kama kawaida yangu baada ya kuoga na kujilaza kitandani ili kupunguza usingizi na uchovu niliokua nao. Ilipofika saa saba mchana,alikuja mpenzi wangu na kuingia ndani. Alinikuta nimetulia sebuleni nikifuatilia moja ya tamthilia niipendayo.

“karibu mpenzi wangu.” Nilimpokea kwa bashasha huku nikijiangusha kifuani kwake baada ya kumbusu.

“ahsante… nina njaa, umeandaa nini?” aliniuliza baada ya kuungana na mimi sebuleni.

“hata sijapika mume wangu, leo hii nilivyochoka. Utanisamehe tu wangu.” Niliongea kwa sauti ya kudeka

“sasa wewe ndio unashindia hizo pop cone?” aliniuliza baada ya kuliona bakuli kubwa la pop cone kwenye meza huku pembeni kukiwa na glass kubwa ya maziwa.

“hii ndio nitolee tena, mimi nikiwa peke yangu huwa nakula vitu simple tu kama hivi . hasa mchana.” Nilimjibu na umfanya atabasamu.

“poa, wacha niende hotelini, kisha nitarudi ofisini . nafikiri tutaonana tena kesho.” Alongea na kunyanyuka.

Alitoa wallet yake mfukoni na kukata kiasi cha fedha bila ya kuhesabu na kunikabidhi.

“take care baby.” Nilimuaga na yeye akaondoka zake.

Baada ya tamthilia hiyo kuisha, nilikumbuka kua nilikua na mgonjwa hospitaini. Nilijiandaa na kwenda kwenye hospitali aliyopelekwa Yule kaka. Nilifika na nikaelezea mapokezi juuya mgonjwa aliyeletwa saa saba usiku.

Baada ya kuelekezwa ward aliyolazwa, nilienda na kumkuta akiwa amefungwa ogo mguuni. Ghafla nilishtuka baada ya kuona uzuri wa mwanaume huyo aliyekua kama ananiangalia bila ya kupepesa macho yake juu yangu.

Nilijikuta mapigo ya moyo wangu yamebadilika ghafla. Na hata ile confidence yangu niliyokuja nayo ilipotea kabisa na kujikuta sina usemo juu ya mwanaume huyo.

Baada ya kuelekezwa ward aliyolazwa, nilienda na kumkuta akiwa amefungwa ogo mguuni. Ghafla nilishtuka baada ya kuona uzuri wa mwanaume huyo aliyekua kama ananiangalia bila ya kupepesa macho yake juu yangu.

Nilijikuta mapigo ya moyo wangu yamebadilika ghafla. Na hata ile confidence yangu niliyokuja nayo ilipotea kabisa na kujikuta sina usemo juu ya mwanaume huyo.

Alikua aniangalia muda wote na kunifanya nianze kuona aibu. Mara daktari akaingia na kunikuta mimi pale.

“habari yako binti “ alinisalimia Yule daktari baada ya kuingia pale.

“salama tu .” niliitikia na kumuangalia Yule daktari usoni.

“mgonjwa wako amevunjika mguu…. Ila nyinyi ndio mnapaswa kulaumiwa kwa kumuacha mlemavu wa macho kama huyu kutembea usiku peke yake.” Aliongea daktari maneno yaliyonifanya nigeuze shingo yangu haraka na kumuangalia Yule mtu ambaye macho yake hayakunijulisha haraka kama alikua haoni.

“huyu ni kipofu?” niliuliza kwa mshangao

“si umesema ndugu yako, vipi hujui kama haoni?” alingea daktari na kunifanya niumbuke.

“kusema ukweli dokta, mimi sina undugu nae huyu mtu, ila nilimuona tu kama alikua anahitaji msaada pale alipokua ndio maana nikaamua kuchukua uamuzi wa kuhakikisha anafika hospitali.” Niliongea na kumuangalia Yule daktari ambaye alitabasamu na kunionyesha ishara za kufurahia uamuzi wangu.

“basi ndio hivyo, huyu haoni hapo alipo, ila ukimuangalia ni kama mtu ambaye hana madhara yoyote ya macho… pia alikua anaulizia fimbo yake, umebahatika kuiona?” aliniuliza swali hilo Yule Daktari na kunifanya nishindwe jinsi ya kujibu kwakua sikua na kumbu kumbu za uwepo wa hiyo fimbo.

Baada ya kuongea na daktari huyo, nilitajiwa gharama nilizotakiwa kulipa. Kuanzia vipimo ,tiba pamoja na dawa, ilifikia laki moja na thamanini elfu.

Nilitoka nje na kumpigia mshefa wangu na kumuomba kiasi hicho cha fedha, hazikupita hata dakika kumi, shilingi laki tatu ziliingia kwenye accounti yangu ya simu. Nilitoka na kwenda kweye kibanda cha Tigo pesa na kuitoa hiyo hela.

Nilirudi hospitalini na kuilipa hiyo bili. Baada ya kupewa maelezo ya kutosha kutoka kwa daktari, nilimchukua mgonjwa wangu na kumpeleka nyumbani kwangu ninapoishi.

Nilimshika mkono na kumuweka kwenye moja ya sofa yaliyokuwemo ndani kwangu.

“karibu…. Na pole sana.” Niliongea na kumuangalia mvulana huyo aliyekua mzuri wa sura na umbo pia. Lakini sikujua hata kama alikua anajijua kama alikua na uzuri huo kutokana na tatizo alilokua nalo la kutokuona.

“ahsante… pia nashukuru sana kwa yote uliyoyatenda juu yangu.” Aliongea Yule kaka na kunifanya nitabasamu.

“usijali, kwa hali kama ile uliyokua nayo, niliumia sana na nikajikuta automatically nimeingiwa na imani na kuamua kukusaidia. Ila cha kushukuru Mungu hawajakupa tu ulemavu mwengine.” Niliongea huku nikimuangalia mwanaume huyo kwa saura iliyojaa imani na huruma juu yake.

“ni kweli.. mungu atakulipa dada yangu.” Aliongea na yule kaka.

“unaishi wapi hapa dar?” nilimuuliza swali baada ya kurudi kuchukua kisu na kuanza kukata machungwa yaliyokwisha menywa na muuza machungwa huko barabarani nilipo yanunua.

“nilikua naishi Temeke. Ila kwa sasa sina pa kuishi. Maana toka nilipopoteza macho yangu, bado sijaonana na mtu yeyote anaye nijua. Kiufupi maisha yangu nahisi yamefika mwisho. Maana nimepoteza dira ya maisha yangu na sina msaada toka nilipokua na macho yangu. Nahisi hiki kilema ndio sababu iliyonifanya nikate tamaa ya maisha.” Aliongea huyo kaka na kunifanya nizidi kumuonea huruma.

“kwa hiyo unataka kuniambia kua hukuzaliwa na ulemavu wa macho?” niliuliza kwa mshangao.

“ndiio,.. nimepata huu ulemavu wa macho miezi miwili iliyopita..” Aliongea na kunifanya nihuzunike.

“pole sana… imekua haraka mpaka tumeshindwa kufahamiana kwa majina. Mimi naitwa Shamira, au Shammy. Sijui wewe unaitwa nani?”

“naitwa AMOUR.” Alinijibu kiufupi.

“jina zuri kama wewe mwenyewe.” Nilimsifia na kumfanya atabasamu. Nilijikuta nainjoy kuuona mwanya mdogo wa mvulana huyo uliopambwa na ma dim pose yiliyobonyea mashavuni kwake.

“ahsante.” Alishukuru huku akiendelea kutabasamu.

“unaweza kunihadithia ilikuaje mpaka ukapoteza macho yako?” niliuliza baada ya kuona nahitaji kumjua zaidi ili nijue ni jinsi gani naweza kumsaidia.

“huwa naumia sana pindi niikumbukapo siku niliyopoteza macho yangu. Ila kwakua unahitaji kufahamu ilikuwaje, suna budi kukuhadithia kila kitu…….”

************************

Ilikua siku ya kumbukumbu kwa Amour baada ya kuamka asubuhi kama kawaida yake na kwenda kibaruani kwake. Alikua anamiliki lliblary ndogo Tandika. Kwakua anapoishi ni temeke mikoroshini, hakua na haja ya kupanda gari aendapo kazini au akirudi kutoka kwenye ofisi yake iliyokua inamuingizia hela ya kula na mahitaji mengine muhimu.

Siku hiyo alitembea kwa mguu na kufanikiwa kufika ofisini kwake akiwa salama. Akaenda kwa mama ntilie wa karibu aliyemzoea na kuagiza supu na chapati mbili.

Baada ya kunywa chai, alifungua Liblary yake na kuanza kupiga miziki mbali mbali huku akisubiri wateja watakaokuja kukodisha cd au kuingiza nyimbo kwenye memory card zao.

Siku hiyo haikua nzuri sana, maana wateja hawakua wengi sana. Ilipofika saa tatu, Amour alitaka kufunga ofisi yake, alikuja mteja ambaye alikua na Flash na alikua anahitaji kuweka nyimbo kwenye Flash yake.

“iwe video au audio, mbili ni shilingi mia tano.” Aliongea Amour baada ya kuulizwa bei.

“sawa.” Aliitikia Yule mtu na kuanza kuchagua nyimbo. Walijikuta wametumia masaa matatu na nusu katika kuchagua nyimbo hizo kutokana na kutozijua majina na jinsi walivyokua wana ziangalia kwanza video ndio wanazituma.

Shilingi elfu kumi na tano aliyopewa kwa ajili ya kuijaza flash hiyo iliyokua na ukubwa wa GB 32, ndio iliyomfanya afunge ofisi saa sita na dakika zake.

Alitembea peke yake huku akiangaza huku na huko kuangalia usalama wake. Alitamani apande gari au piki piki, lakini muda huo havikuwepo maeneo aliyokuwepo.

Sehemu yote aliyokatiza kulikua na ukimya uliomfanya azisikie mpaka hatua zake mwenyewe. Alitembea haraka ili awahi kufika. Ila kabla hajafika, alikuta kelele zikiambatana na milio ya risasi ikitokea numa yake.aligeuka nyuma haraka na kukutana na mwanga wa gari lililokua linamfuata yeye kwa kasi ya ajabu. Alijaribu kuruka pembeni, ila gari hiyo ilimgonga na kumuacha akiwa chini amepoteza fahamu.

Asubuhi ya siku hiyo, watu walijazana kushuhudia ajali hiyo iliyohusishwa na wezi waliokua wametoka kuiba keko maduka mawili. Ambulance ilikuja kumchukua na kumpeleka hospitali ya temeke ambapo alipokelewa na kupelekwa ICU kutokana na hali aliyokua nayo. Alipasuka maeneo ya kichwani na damu nyingi zilikua zinamvuja.

Alishonwa nyuzi nane kichwani kutokana na jeraha alilokua nalo. Ila baada ya kufanyiwa huduma hiyo, Amour aliona utofauti kwenye macho yake. Maana aliweza kufumbua likini hakuweza kuona kitu chochote mbele.

“embu fumba kwa kipindi kirefu halafu fumbua tena.” Alishauri daktari baada ya kusikiliza maongeza ya Amour.

“sioni kitu chochote,” aliongea Amor na kumfanya Yule daktari kuja na vifaa vya kupimia macho. Baada ya kumpima, waligundua kua hakua na uwezo wa kuona kabisa katika maisha yake. Walirudi na kumpa transfer kwa ajili ya kwenda kwenye hospitali ya CCBRT kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa macho yake.

Hata huko walimthibitishia kua hataweza kuona zaidi ya kusubiri tu miujiza ya Mungu katika hilo. Amour alichanganyikiwa na kujikuta analia kwa sauti huku akilalamika.

“eeh Mungu, hivi nilipokua na viungo vyangu vyote nilishindwa hata kupata hela ya kodi kwa wakati, halafu leo ndio nimepoteza macho.. nitaishije mie” alilalamika huku analia Amour baada ya kukabithiwa fimbo nyeupe iliyomjulisha kua yeye ni kipofu.

Ugumu wa maisha aliuotabiria ulianza pindi tu aliporuhusiwa kurudi uraiani akiwa mtu ambaye hajui ataanzia wapi hata kupata hela ya kula.

Siku moja akiwa katika kutafuta pa kulala usiku, alikutana na vibaka ambao hawakumuonea huruma. Walimsachi na kumkuta na fedha ndogo sana. Hivyo hasira zao wakazimalizia kwake yeye kwa kumdondoshea mkong`oto wa haja. Alijitahidi kujivuta na kudondoka baada ya maumivu makali kumkabili.

***********************

“ndio ukatokea wewe na kuamua kunisaidia.” Alimaliza story yake na kunifanya nishushe pumzi na kumuangalia mwanaume huyo aliyekua anaonyesha wazi ni vipi alikua anahitaji msaada wangu.

“usijali Amour, nitajitahidi kwa kadri ya uwezo wangu kukusaidia.” Nilijikuta nimeongea hivyo huku moyo wangu ukiwa bado una maumivu ya hadithi ya maisha yake aliyonihadithia.

Nilimuacha sebuleni na kuingia chumbani kwangu na kuchukua simu na kumpigia mpenzi wangu.

“niambie dear” aliipokea kima daha.

“safi tu,.. upo wapi?” nilimuuliza huku nikijifanya nina shida nae.

“nipo kazini muda huu… unanihiji nije sasa hivi?” aliniuliza na kunifanya nicheke.

“nooo… wewe fanya kazi laazizi wangu, ukimaliza nakuomba uje . kuna kitu nahitaji nikuombe tukiwa wote pamoja.” Niliongea na kuonyesha ishara zote za kujali kazi yake.

“hata hivyo nimeboreka sana huku nilipo. Kama vipi mi nakuja muda huu. Au wewe unasemaje?” nilijua tu lazima atakua na kiherehere cha kuja pindi nimuitapo. Kwa sababu ni mara chache sana kutokea kumpigia simu ingawaje ndio mtu anayeniwekea vocha kila siku.

“wewe tu wangu.” Nilimjibu na kukata simu.

Hazikupita hata dakika ishirini, nilisikia mlio wa gari na kunifany a nifungue mlango na kwenda kumpokea huko huko alipokua. Nilipokea mizigo aliyoniletea na kuingia nayo mpaka sebuleni ambapo alishstuka kidogo baada ya kumuona mgeni akiwa amejaa pale sebuleni.

“dear.. huyu ni rafiki yangu, anaitwa Amour. Ni mlemavu wa macho na kusema ukweli anahitaji sana msaada wetu. Maana hana hata pa kulala wala hajui atawezaje kupata chakula na hali yake hiyo aliyokua nayo.” Nilijiwekea uzio kabisa kabla hajaanza kuhisi kitu chochote kbaya kati yetu. Nilimuangalia huku mkono wangu uliomshika kiunoni ukiwa una mtekenye kidogo kwenye mbavu zake.

“kwa hiyo wewe umeamua tumsadie kwa njia gani?.” Aliniuliza kwa sauti ya upole.

“mimi naona sio mbaya kama tukikaa nae hapa.. halafu baadae utamtafutia mfanya kazi kwa ajili ya kumuangalia na kumuhudunia. Hatuwezi kushindwa mpenzi wangu kumsaidia mtu mmoja. Hata Mungu atatusamehe madhambi yetu tunayoyafanya kila siku.” Niliongea na kumuangalia mpenzi wangu huyo ambaye hakua na kauli kwangu.

“sawa… nakuamini na nathamini sana mawazo yako mpenzi wangu.” Aliongea na kunifanya nimsogelee na kumkaribia kabisa huku lipsi zangu nikizikaribisha karibu kabisa na lipsi zake.

“hicho ndicho kinachonifanya nikuone wa pekee kuliko wanaume wote Dear.” Niliongea na kumbusu shavuni.

“okey.. Amour, mimi naitwa Dismas. Nadhani tutaendelea kukutana na kufahamiana zaidi.” Aliongea na kwenda kumpa mkono Amour ambaye alibabaika kidogo katika kuupata mkono wa Dismas.

“kuna la ziada?.” Aliniuliza na kunifanya nitabasamu.

“twende chumbani.” Nilinong`ona na kumpa ishara kwa kuonyesha chumbani kwa mkono.

Alinyanyuka haraka huku akitabasabu, alitangulia chumbani na mimi nikamfuata. Nilimpatia kile kinachostahili kwa wapendanao wawapo faragha. Ila mimi nilikua na hisia tofauti sana. Sikua natoa kwa mapenzi, bali kwa urefu wa mkwanja nitakaoahidiwa na mtu ninayempa huduma hiyo.

Baada ya kumaliza, alienda kuoga na kunijandaa. Alitoka na kumsindikiza mpaka nje na kumfungulia mlango wa gari ili awahi kwa mkewe.

“hivi mama B. akikuambia kua ana kuhitaji usiku huu.. utaumudu mchezo kweli?” nilimtania.

“ataanzia wapi kusema hivyo. Mimi ndio naamua siku za kukutana nae na si yeye.” Alinijibu hivyo na kunifanya nicheke kinafki.

Alifungua pochi na kunipa kiasi cha shilingi laki nne. Nilizibusu zile hela na kurudi ndani. Nilimuangalia kwa madaha na kumsemesha Amour.

“una uchovu nikuandalie maji ya kuoga?” niliongea huku nikimuangalia na kuutathmini uzuri halisi wa mwanaume huyo.

“nipo sawa tu.” Alinijibu na kuabasamu.

“utakula nini nikupikie?” nilimuuliza tena.

“chochote tu.” Alinijibu huku akiendelea kutabasamu.

“haya,… ngoja nikakuandalie.”

Nilitoka na kwenda kutafuta kuku na kumkaanga. Nilikata kachumbari na baadae nikapasha nyama niliokwisha pika na kuihifadhi kwenye friji. Baada ya hapo. Nikatulia jikoni mtoto wa kike na kutoa wali wa kukaanga ulionakshiwa na njegere na kubadili rangi kidogo huku karoti zikileta muonekano mzuri wa chakula changu.

Nilimsogezea bwana mkubwa na kumpelekea mezani. Nilijua kua atapata shida kula mwenyewe. Nilimlisha huku fikira zangu zikinipeleka kwengine kabisa. Kimoyo moyo nilimuomba Mungu kijana huyo afumbue macho ili apate kuniona, huenda akanipenda na kunitamkia hayo maneno. Maana alikua na kila kigezo cha mwanaume niliyekua namtafuta katika maaisha yangu.

Baada ya kumlisha, nilimpeleka kwenye chumba cha wageni na kumlaza baada ya kukitandika kitanda vizuri. Nilikitandika kitanda vizuri wala sikuacha bam hata moja kwenye mikunjo ya shuka. Ila nilidhoofika moyo baada ya kugundua kua niliyemuandalia mazingira hayo hatoweza kuona na kunisifia kwa umahiri wangu wa kutandika kitanda.

Baada ya muda, nilipokea simu ya rafiki yangu wa viwanja akinijulisha kua mida ilikua imefika pia kulikua na mteja aliyekuja kuniulizia. Nilimuacha ngeni baada ya kuhakikisha amelala na mimi nikaelekea kazini.

Nilirudi saa kumi alfajiri nikiwa na shilingi laki tano nilizoziingiza usiku huo baada ya kulala na wateja wangu watatu tofauti.

Nilipofika nyumbani, nilikuta mlango umefungwa, nilishangaa sana kukuta hali hiyo. Maana mimi niliuacha wazi hata kama ikitokea dharula yoyote kwa mgonjwa wangu huyo iwe rahisi kutoka nje. Niligonga malngo taratibu, na haikupita muda mrefu, Amour alikuja kufungua.

“ai jamani,… mbona umeamka mapema hivi?” nilipatwa na aibu baada ya kugundua kua aliisikia simu niliyopigiwa nikiwa nahitajika usiku huo.

“niliona sio vyema kuacha mlango ukiwa haujafungwa kwa usalama zaidi.” Aliongea huku akijitahidi kupapasa na fimbo yake na kurudi kwenye sofa.

“nashukuru..pia..pia..” nilibaki najiunya unya kwa kua nilishajishtukia kwa jinsi alivyoweza kugundua kua sikulala pale nyumbani.

“wewe kapumzike tu Shammy, mimi usingizi umekata.” Aliongea Amor huku akionyesha ishara za kutabasamu. Kwangu iliniuma kwa sababu sikuhitaji hata kwa bahati mbaya agundue kazi yangu ya kishenzi ninayoifanya.

Siku hiyo nilijihisi nimepoteza maksi kwa mvulana huyo ambaye tayari anajua kuwa mimi nina mtu. Pia kiitenddo change cha kutoka usiku na mtu mwengine tofauti na aliyekuja mchana bila shaka kilileta picha mbaya kwa mwanaume huyo. Pia mazingira aliyokuja kudondokea kama alikua anayajua awali ndio kabisa yalitosha kumjulisha kuwa mimi ni kahaba.

Nilipata shida sana katika kuyafikiria hayo na kufanya usingizi wangu wote kuruka na kuwaza ni jinsi gani ninavyoweza kubadilisha mawazo ya Amour ili asiwaze mabaya juu yangu japo kua huo ndio ulikua ukweli wenyewe.

Mbali na uchafu na maringo niliyokua nayo, ila kwa mwanaume huyu, nilikua tayari kufanya chochote kwa ajili yake.

Siku hiyo nilikua mtiifu na kuhakikisha mgeni huyo namkirimu na kukaa nae siku nzima. Usiku niliizima simuyangu na sikua tayari kupokea simu yoyote ili mradi kama ni dili zinipite tu ili niweze kusafisha cheti changu kwa mvulana huyo.

Nililala nyumbani usiku huo wote kwa mara ya kwanza toka nimeanza kazi hiyo ambayo kwangu usiku ulikua na thamani zaidi ya usingizi.

Mazoea yalinifnya nisipate usingizi kwa muda mrefu. Lakini hata hivyo moyo wangu uliridhia kabisa kukosa hizo hela kwa ajili ya Amour.

Asubuhi nilimkuta Amour akiwa ameshaamka na kuangalia Tv. Nilishindwa kumtafsiri kipofu huyu aliyeyazoea mazingira ya nyumba hiyo haraka. Maana alikua anajua ni wapi rimonti ya tv inapatikana na na ni wapi mlango wa kutokea nje ulipo na makomeo yake.

Nilimuandalia chai nzito ya mikate ya mayai pamoja na meat chop nilizoziandaa mwenyewe. Nilichemsha soseji na kumkaribisha chai mvulana huyo aliyeukosha moyo wangu kila nimtazamapo.

Alikaribia na kukaa upande wa pili wa meza ambapo mimi nay eye tukawa tuna tazamana. Mboni za macho yake zilikua kama zinaniangalia, lakini hakukua na mawasiliano na nuru ya macho yake. Hakuna alichojivunia zaidi ya tabasamu ambalo lilinitosha kabisa kuniua mtoto wa mwanaume mwenzie.

Tulikunywa chai huku mawazo yanguyakiwa mbali, nilipaliwa na chai huku kipande cha mkate kikinidondokea kwenye nguo yangu upande wa kufua change. Nilipatwa na mshangao wa mwaka baada ya kumuona kipofu huyo akinyayuka tena bila kuishika fimbo yake na kunisogelea nilipo. Mara aliingiza mkono mfukoni na kutoa leso nyeupe na kunifuta maeneo niliyojimwagia chain a kukitoa kipade cha mkate kilichonidondokea na kurudi kwenye siti yake. Nilishindwa kujua ni maajabu au ni ukweli halisi kama mgonjwa wangu sasa aliweza kuona.

Alitabasamu na kuaniangalia kama vile alikua ananiona na kuichukua fimbo yake na kuanza kupapasa chini na kuondoka zake na kuelekea chumbani kwake. Kusema ukweli sukumuelewa na sikua najua ni kwanini alikua ananiweka mwenzie kwenye njia panda.

Nilijikuta sitamani kutoka ndani mpaka niujue ukweli halisi juu yake. Nilichukua simu yangu na kumpigia mshefa wangu.

“haloo dear.” Niliongea huku nikiwa makini ili asijue utofauti wangu niliokua nao kwa wakati huo.

“safi tu , niambie.” Alinijibu na kunisikilizia .

“leo naenda kwa shangazi yangu wa temeke. Amejifugnua sasa ameniammba nikakae nae mpaka atakapotoka saba.” Niliongea huku nikilegeza sauti yangu kama mtu anayehitaji sana maamuzi yake kwa wakati huo.

“duh!... itakuaje sasa mpenzi wangu, maana wewe unajua kabisa kua mimi hua haupiti usingizi kama ikipita siku sijaiona sura yako.” Alililamika huyo mshefa na kunifanya nibinjue mdomo wangu kwa dharau.

“pole mpenzi wangu, hata mimi natamani sana tungekuwa wote kipindi hiki, ila kumbuka kua hapa DAR tupo mimi na shangazi tu na hakuna ndugu mwengine, sasa unafikiri kuna njia gani nyengine ya kukwepa hapo. Maana leo yeye kesho mimi.” Niliongea huku nikilalamika na kuona kama vile nimelazimika tu kwenda hiyo safari na si mimi niliyeamua kwa matakwa yangu.

“sawa mpenzi wangu… nitakurushia akiba ya kukusukuma hiyo wiki moja.” Aliongea mpenzi wangu na kunifanya nim mwagie mabusu yasiyo na idadi baada ya kunitajia maswala ya hela.

“nakupenda sana my buu buu” niliongea hivyo na kukata simu.

Dakika kumi mbele, nilipokea sms ya tigo pesa iliyonijulisha kua kimeingia kiasi cha shilingi laki tano kwenye account yangu. Nilicheka na kwenda sebuleni kuangalia tv.

Hata hivyo fikira zangu zilirudi nyuma na kunikumbusha kua nilikua nahitaji kujua kua Amour alikua ni kipofu kweli au alikua ananiigizia.

Niliwaza sana ni njia gani nitumie ilimradi niweze kujua ukweli huo ulojificha kwa muda huo.

Baada ya kuwaza na kuwazua, ndipo nilipopata majibu ambayo niliamini lazima yataniletea matokeo mazuri ya puzzle hiyo niliyoamua kucheza.

Nilinyanyuka na kuanza kutembea taratimu kuelekea kwenye chumba cha Amuor. Nilinyata na baada ya kumifikia, niliguna ili asishituke kuniona nimefika pale.

“naweza kuingia.” Niliongea baada ya kuufikia mlango wa chumba chake.

“karibu.” Alinikaribisha na kunifanya niufungue mlango taratibu. Nilimkuta amekaa kitandani huku akiwa kifua wazi. Nilitakakusita lakini nilijipa moyo kwakua alikua haoni, hivyo hakutakua na matatizo.

Niliingia na kwenda kukaa kwenye kiti kilichokua mbali kidogo nay eye.

“niambie.” Aliongea na kutabasamu.

“nilikua najihisi mpweke nilipokua peke yangu sebuleni.” Niliongea na kumuangalia mvulana huyo kimahaba.

“hunishindi mimi. Hata mimi niliuhisi upweke huo baada tu ya kunyanyuka pale kwenye kiti na kuingia ndani. Imekua vizuri zaidi kunifuata huku na kunipa company.” Aliongea maneno hayo huku akwa haniangalii.

“kwani wewe unahisi hii ni sehemu nzuri ya kuwa mimi na wewe?” nilijikuta nimeuliza swali hilo bila kujitambua.

“hata umbali uliopo kati yangu mimi na wewe kwa sasa, unaruhusu upweke kati yetu. Unaonaje kama ukisogea zaidi kutoka hapo ulipo?” aliongea maneno hayo na kufanya moyo wangu ulipuke. Nilihisi kuna kitu alikua ana kihitaji kutoka kwangu.

“mh?..... kwani unajua mimi nipo wapi muda huu?” nilimuuliza ili nipate kujua alikua na upeo gani.

“sina nuru ya kuona, ila nimepewa hisia kali zaidi yako kwa sasa. Naweza kujua ulipo kupiitia harufu yako nzuri ya mwili wako hata kabla hujapaka manukato. Unaonaje ukatoka hapo kwenye kiti na kunisogelea hapa kitandani?” aliniuliza hilo swali na kunifanya nikose la kujibu.

Sikuwahi kumuogopa mwanaume, ila kwa huyu nilikua nasita kabisa na kuona miguu yangu haina nguvu ya kunyanyuka. Ile kufumba na kufumbua, nilijikuta nimeshikwa mabegani kwa mikono miwili huku uso wake ukiwa karibu kabisa na mimi.

Macho yake aliyatuliza na mdomo wake ulianza kuusogelea mdomo wangu taratibu kama ishara ya kua alikua anahitaji kunipiga denda. Niliyafumba macho yangu taratibu, na haikupita hata sekunde, nilianza kusisimkwa na mwili baada ya ulimi wake kuanza kupenya kinywani kwangu huku hisia za mate ya moto yaliyojaa utamu usiokua na sukari ukianza kuyabadilisha mapigo ya moyo wangu.

Sikuweza kumzuia japokua nilikua najaribu kukwepa mashamubulizi hayo ya kushtukiza baada ya kuona mikono yake iliyokosa adabu ikinipapasa kwenye maungo yangu.

Baada ya muda mfupi, nilijikuta nimelegea na kumuachia afanye yale aliyokua amedhamiria kufanya juu yangu.

Baada ya nusu saa, nilijikuta nipo kwenye ulimwengu mwengine huku Amour akiwa pembeni yangu akiachia tabasamu.

“kweli wewe fundi.. nani kakufundisha yote haya?” aliongea na kunifanya nimonee aibu.

“fundi seremala au washi… usije ukan’tangaza bure.” Nilijibu huku nikinyayuka na kwenda bafuni kuoga. Wakati nilipofumba macho yangu huku nikiusikilizia ubaridi wa maji yatokayo kwa kasi kutoka kwenye bomba maalumu la mvua, nilihisi kitu kama mlango unafunguliwa, nilipofumbua macho yangu haraka, nilimuona Amour akiwa ameshafika pale na taulo lake.

“Khaa…!” nilibaki nimeshangaa tu na kumuona akilitundika taulo pembeni na kunisogelea.

“una umbo zuri sana linanoweza kumfanya mwanaume yeyote aliyekamilika akatamani kuurudia mchezo baada ya kumaliza. You’r so beautiful.” Aliongea na kunifanya nipigwe na butwaa.

“hilo umbo langu umelionaje na wewe umenithibitishia kuwa hauoni?” niliongea huku nikiwa nimeliwahi taulo langu na kujifunga.

“nikisema sioni nitakua naongopa. Mimi naona kila kitu. Hata ukitaka nikuambie hilo taulo ulilojifunga ni rangi gani, naweza pia kukutajia.” Aliongea na kunifanya niishiwe nguvu.

Baada ya hapo, alifungulia maji na kuanza kuoga bila kujali kua alikua ananilowesha. Niliutazama mwili wake uliokua na mvuto wa aina Fulani hivi. Hakua na umbo kubwa, bali kifua kidogo ambacho kilikua bado kiteke na six parks zilizojitokeza kila alipofanya kitendo kilichosababisha kukaza kwa mikono yake, alinifanya nimuangalie na kuziacha dharau zangu kando. Mara nyingi hata ninapokua kazini, huwa nakutana na wazee au kama vijana, basi wana vitambi. Wenye umbo kama lake ilikua nadra kuwapata coz hawakua na hela ya kunimudu.

Nilitoka na kuondoka zangu chumbani kwangu. Nilitulia na kuanza kuufikiria ule mchezo uliotokea muda mfupi nyuma. Nilicheka baada ya kugundua kua sikukosea kumpa bure mtu huyo aliyeitumia nafasi yake vizuri.

“ila kwanini aliniongopea kuwa haoni?” nilijiuliza na kunifanya nikae kitako na kuwaza mtiririko wa matukio.

“kama kweli anaona, ilikuaje mpaka daktari alinithibitishia kua Amour haoni?” nilijiuliza hilo swali bila kupata jibu sahihi. Nilitoka na kwenda sebuleni na kumkuta Amour akiwa hana fimbo. Pia alikua amewasha Tv huku akionekana kukifurahia kipindi kilichokua hewani muda huo.

“mbona una makusudi hivyo Amour?” nilijikuta nimeongea hivyo baada ya kwenda sebuleni hapo na kukaa kwenye sofa lililokua karibu na Tv.

“muda ulikua bado hujafika wa wewe kujua kua mimi ni mzima na sina kasoro kwwenye macho yangu. Naweza kuona uzuri wa kifua chako kilichobeba matiti madogo yalinayokaribia kutoboa top yako uliyovaa.” Aliongea Amour na hapo ndipo nilipoamini kua kweli alikua anaona.

“kwanini ulinidanganya kua hauoni?” nilimuliza huku sura yangu ikonekana kua haikua kwenye masihara muda huo.

“ni uzuri wako ndio ulionifanya nitumia njia hii baada ya kuona njia zote nilizozitumia zimefeli kua karibu na wewe.” Aliongea maneno hayo na kunifanya nishushe pumzi.

“nakupenda sana Shammy na nipo tayari kwa lolote ili mradi nihakikishe kua penzi langu linaishi milele.” Aliongeza maneno hayo na kunifanya nibaki nimeduwaa huku nikiwa nimemtumbulia macho bila kuongea chochote. Macho yalimuonea aibu na kunifanya niinamishe uso wangu chini, ila moyo uliniambia kua chaguo ulilokua unalisubiria, ndio hilo limejileta lenyewe.

“haiwezekani Amour. Nadhani hata wewe mwenyewe unafahamu kila kitu kuhusu mimi. Hata hapa ulipo unaishi kwa mgongo wa bwana wangu anayenilea hapa mjini.” Niliongea huku nikiwa nimejikaza ilimradi nisionyeshe udhaifu niliokua nao.

“hakuna kisichowezekana chini ya jua. Mambo yote yanaendeshwa kwa kupanga na kupangua. Ukipanga hili na kulitilia mkazo kwa dhati ya nafsi yako, huwa mara nyingi Mungu hulipitisha hata kama kitakua ni kibaya. Najua kua huyo jamaa uneyemzungumzia yupo upande gani kwako. Ni dhahiri shahiri kua unahitaji hela tu kutoka kwake na si mapenzi ya dhati. Nafahamu ni jinsi gani moyo wako unavyosulubika juu ya utandu wa penzi la dhati ulilo nalo juu mwanaume ambaye hana chochote katika mali zaidi ya moyo pacha unaoendana na moyo wako na kukuhakikishia furaha ya maisha yako. Hela huweza kufanya mengi sana lakini haiwezi kuinunua furaha yako kamwe…. Naomba niliyoyaongea, uyachuje na unipe jibu umeamua nini katika hili.” Aliongea maneno hayo na kunyanyuka.

Nilibaki nikiwa nimemuangalia tu anavyoenda ndani. Kila alichokiongea, hakikubaki nje, kilipita moja kwa moja kwenye halimashauri ya ubongo wangu na kupelekwa kwenye moyo ambao ulifarijika sana kuyasikia maneno hayo matamu ya mwanaume niliyetokea kumpenda sana.

Nilimuangalia tu akiwa anaishia na kuelekea chumbaini kwake. Usiku nilitulia kitandani kwangu na kuanza kuyatafakari kwa kina mambo niliyoambiwa mchana na Amour.

Kusema ukweli siwezi kupindua kwa jinsi ninavyompenda, ila nilikua na wasi wasi juu ya aina ya mapenzi tutakayoyaanzisha mimi na mwanaume huyo. Pia niliamini kua kama ikitokea nikaharibu kwa mshefa wangu, sitokua na njia nyingine ya kuingiza hela zaidi ya kufanya ukahaba. Pia nilijua kua kukubali kua na uhusiano wa kimapenzi ndio itakua mwisho wa biashara yangu ya kuuza mwili.

Nilitafakari sana na kujikuta nimeshindwa kuamua chochote.

Asubuhi nilimuandalia chai na kuondoka kabla hajaamka. Nilimpigia simu rafiki yangu na kukutana nae nyumbani kwake maeneo ya kimara.

“vipi shost asubuhi asubuhi.?” Aliongea rafiki yangu baada ya kunifungulia mlango.

“yaani we acha tu shosti … maana kinachonisibu mwenzio huko nyumbani kwangu ndicho kilichonifanya nije kwako kabla hata sijakunywa chai.” Niliongea na kumfanya rafiki yangu kunikokota mpaka sebuleni. Baada ya kukaa alinibusti nimpe umbea.

“enheee… haya nielezee kinaga ubaga, kipi hicho kilichokusibu shost?”

aliongea shoga yangu na kunifanya nianze kumsimulia kuanzia mwanzo wa kukutana na Amour hadi kufikia hapa tulipo.

“hapo cha kufanya shoga yangu, kubali tu kuwa nae….kama anayajua mautundu kula raha za dunia.” Aliongea rafiki yangu na kunifanya nishangae kidogo ushauri wake alionipa.

“mimi mwenyewe mume wangu akisafiri tu, naruka na shamba boy wangu… sembuse wewe unaishi na handsome wa nguvu,…. Tena mwambie ajifanye kipofu hivyo hivyo kila jamaa akitaka kuja kwako. Hawezi gundua kamwe” aliongeza rafiki yangu huyo na ndipo nilipoona kua kuficha siri hiyo ilikua na uwezekano.

Niliamua kuaga huku nikiwa na jibu la kukubali kuanzisha uhusiano na Amour.

Nilirudi nyumbani baada ya kupitia sokoni na kununua mahitaji ya msingi kwa ajili ya mapishi ya chakula cha mchana. Nilipofika, nilimkuta Amour yupo jikoni huku akikata kata vitunguu. Nilipotupa macho yangu kwenye jiko, niliona sufuria mbili zikiwa jikoni. Sikujua alikua anapika nini muda huo, lakini nilipoangalia saa yangu, ilinisomea kua ilikua saa nne na nusu muda huo.

“wewe tulia, leo nataka nikuonyeshe mapishi ya mchele na mboga zake.” Aliongea Amour ambaye alinisogelea na kuchukua ile mizigo niliyoileta huku macho yake ya mahaba yakiwa ameyatuliza kwenye uso wangu na kunifanya nione aibu kidogo.

Baada ya kuchukua kila kitu,aliendelea na mapishi na mimi nilirudi sebuleni na kuchukua cd moja iiliyokua na full season ya series ya spartcus na kuanza kuangalia part ya mwanzo kabisa ya Blood and sand.

Wakati naiangalia movie hiyo, sikujua kua nilitumia muda gani, ila nilikuja kushtuliwa na Amour ambaye alikuja kuniziba macho na kuutoa mkono wake kwenye macho yangu baada ya sekunde kadhaa. Nilipoyafumbua macho yangu, nilikuta na tabasamu kali kutoka kwa mwanaume huyo aliyekua ananifanyia vitimbi kila dakika.

“chakula tayari mummy” aliongea na kutangulea kwenye meza ya chakula.

Nilistopisha ile movie na kunyanyuka kivivu na kwenda kwenye hiyo meza ya chakula. Nilimkuta amesimama akinisubiri. Nilipofika, alikivuta kiti na kuniruhusu nikae. Baada ya kukaa, alienda kukaa kenye siti iliyokua mbele yangu na kusababisha eyes contact kati yetu.

Alinipa pawa zilizokua zinalingana na idadi ya ma hot pot na kuniambie nifunue kwa ajili ya kupakua chakula.

Poti kubwa kuliko yote ndio nililifungua la kwanza. Nilikutana na harufu ya wali iliyokua inafanana na hiriki lakini hizo hiriki hazikuonekana. Nilikuta karoti zilizokatwa kiustadi bila ya kutegemea mashine kama nifanyavyo mimi. Nilikuta njegere kiasi huku rangi ya vitungu vilivyokua na rangi ya kahawia vikizifi kuufanya msosi huo kuwa na harufu ya ajabu hata kabla sijautia mdomoni. Nilijikuta nimetabasamu huku nikiliendea port la pili bila kupakua ule wali.


Hapo nikutana na kisamvu kilichoonekana kuwa na nazi nyingi. Sikuendelea tena kufungua mapoti mengine, nilipakua chakula na kupakua mboga hiyo kwenye sahani yangu. Nilipofungua poti la tatu, nilikuta mchuzi wa nyama uliokua unanukia viungo ambavyo hata sikujua amechanga nini na nini japokua jikoni kulikua na viungo vya kila aina. Ndani ya mchuzi hakukua na nyama. Hata kabla sijauliza, nilisogezewa kipoti kidogo kilichokua na nyama zilizokaangwa vizuri huku maini yakiwa mengi.

Port la mwisho nilikuta kuku wa kubanika akiwa amerembwa na kachumbari pembeni yake.

Utamu wa chakula cha mwanaume huyo ni ngumu kuelezea, ila nilijihisi kua nilikua nimechelewa sana kujuana na mwanaume huyo.

Baada ya wiki moja kupita, hakuna mtu ambaye aliweza kuzizuia hisia zake kwa mwenzie. Amour aliinitongoz tena na mimi sikuchukua round kutokana na mateso niliyokua nayapata juu yake.

Nilishasahau kabisa kama kuna kitu kama kutoka usiku kwenda popote. Tena baada ya kuona napigiwa simu mara kwa mara, niliamua kubadilisha hadi line ya simu yangu ili mradi tu nisipatikane.

Kwa mara ya kwanza nilianza kujua nini maana ya mapenzi.

Penzi tamu la kijana huyo lilinifanya nione kua yeye ndio kila kitu katika maisha yangu. Sikutaka kufanya siri tena. Hata mshefa wangu alipokuja, nilimbwaga na kumwambia kua simuhitaji tena aendelee na maisha yake pamoja na familia yake.

Kusema ukweli Amour alikua type yangu sana. Uzuri wa kijana huyo ulinifanya nipate sifa kila mahali nilipokwenda. Hawakunisifia mimi tu,, bali walisema kuwa tumependezana.

Tulihama pale tulipokua tunakaa na kuhamia mikocheni ambapo tulipanga vyumba viwili kwa pamoja, yaani chumba na sebule kwenye nyumba mpya kabisa ya kupangisha iliyojengwa na mmoja wa wafanyakazi maarufu. Mimi ndio nilikua nahitajika kulipia kodi na kila kitu kinachohusu huduma yoyote itolewayo pale.

Niliona sio vizuri mpenzi wangu awe mtu wa kushinda ndani na kunitegemea mimi kwa kila kitu. Hivyo nilitoa kiasi cha fedha benk na kumfungulia duka la nguo maeneo ya masasani.

Miezi sita baadae, tulifanikiwa kufungua duka linguine kubwa maeneo ya kinondoni kwa manyanya. Na hilo nilimpa kabisa kwa kila kitu kutumia jina lake.

Dhuruba la mazoea pamoja na hitilafu za mapenzi ndipo zilipoanza taratibu. Mara kadhaa Amour aliona kama mimi namdharau kutokana na kipato nilichokua nacho. Aliona namnyanyasa hata kama nikimlaumu kwa vitendo ambavyo hastahili kutenda kama mpenzi bora.

Nilijitahidi nisimkasirishe mpenzi wangu huyo niliyetokea kumpenda sana kuliko kitu chochote lakini haikusaidia kitu.

Alitumia fedha nyingi pasi na mpangilio wala hesabu. Na hakutaka niongee kitu chochote.

Kukutana nae kimwili ilikua kwa nadara sana na hata tukipata nafasi basi hakua ana perform kama alivyokua akifanya mwanzo.

Nilivumilia na kumuheshimu kama mpenzi wangu aliyenibadilisha kutoka kwenye ukahaba mpaka ujasiria mali na kuona kua yale yote niliyokua nayafanya yalikua ni ujinga tu.

Hali ilizidi kuniwia vigumu baada ya kuanzisha tabia ya kuchelewa kurudi nyumbani huku akiwa amelewa. Kuna siku nyingine hakurudi kabisa.

Matatizo juu ya matatizo yalizidi kuniandama. Maana kila kukicha idadi ya wanawake ambao alikua anatembea nao ilizidi kuongezeka na kunifanya nishindwe kuvmilia. Nilishindwa hata kuona raha ya kuwa wapenzi na uhuru wa nafsi yangu ukaanza kufifia taratibu.

Ilibaki kidogo nizimie kama si kupoteza maisha baada ya watu wa Benk kuja kudai mkopo wa milioni ishirini ulio kopwa na Amour huku maduka yetu yakiwa ndio dhamana ya mkopo huo. Sikujua alienda kufanyia nini hizo hela zote.

Nilichoka nilipomuuliza kuhusu hilo swala.

“kama umenichoka niambie, huwezi kuniuliza nimetumiaje hizo fedha wakati mzigo umeouona dukani.” Aliongea huku akiwa hataki hata kukaa chini.

“milioni ishirini ni hela nyingi sana. Na mzigo nilio uona hauzidi hata milioni tatu. Kwanini unapenda tuwe tunarudi nyuma kila siku badala ya kuendela?.” Niliongea kwa uchungu huku machozi yakianza kuni lenga lenga.

Hakunisikiliza, zaidi alinisonya na kuondoka huku akiacha mlango wangu ameubamiza hali iliyonifanya nishtuke.

Ilipita siku nzima bila kurudi nyumbani. Usiku ulipokua mkubwa, nilipiga simu yake hakupokea. Nalijaribu kupita sana, lakini simu yangu iliishia kuita mpaka kukatika yenyewe.

Siku ya pili yake, alipokea na kunipa majibu ambayo sikuyatarajia kwa mwanaume kama huyo ambaye nimempa dhamana ya maisha yangu angweza kuongea hivyo.

“kwa uliponifikisha panatosha sana Shammy. Napaswa nikushukuru kwa kunibadilishia maisha, so unaweza kuendelea na maisha yako na usahau kabisa kuhusu mimi kipofu wako niliyeona hadi mwangaza wa maisha mazuri. Sikua nakupenda zaidi ya nilivyokua napenda kuona unavyonipa hela zako. Now nina nyumba na duka la nguo. Ila ninachokuomba ni kwamba. Utakapokua unafanyika mnada wa maduka yako, basi usisite kunishtua ili nihudhurie huenda nikaweza kuyanunua na kuyamiliki tena….. nakutakia siku njema.”

Maneno hayo yalinifanya nishindwe kuongea chochote zaidi ya kulia tu mpaka simu ikakatika.

Haikuwa na haja ya kutoamini kua Shammy wa zamani aliyekua akiishi kwenye chumba kimoja temeke yanarudi tena huku nikiwa nimepoteza kila kitu katika maisha yangu.

Maduka na vitu nilivyokua navyo ndani, vyote viliuzwa na kuniacha mtupu huku nikiwa sina hata godoro la kulalia.

Nilirudi kwa shangazi yangu, naye hakunipokea kutokana na kumtenga kipindi nilipokua na hela.

Sikujua nifanye nini, zaidi ya kurejea tu kazi yangu ya ukahaba japokua nilisha badilika na sikua naipenda tena. Ila yote naamini yamesababbishwa na mimi. Kama si Yule niliyemuamini.

********MWISHO**************

Post a Comment

0 Comments