Header Ads Widget

Responsive Advertisement

AHADI YA MILELE



 AHADI YA MILELE
Miaka kumi na mbili iliyopita binti huyu pichani aitwaye Dear alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na kijana mmoja wakiwa na umri wa miaka 18.
Walipendana sana na kuapiana kuwa wasingesalitiana na kuja kuishi kwa pamoja kama mme na mke baada ya kuhitimu masomo yao.
Binti akatoa wazo kwa kuwa yeye hana imani na wanaume, kwani wengi huwa na tabia za kusaliti mahusiano basi waape kwa kitumia Biblia na kofuli.
Wazo hili kijana alilipokea kwa furaha na binti akafurahi sana kuona yule kijana amekubaliana nae kuwa ataapa kwa njia hiyo kama ishara ya kuwa hawatasalitiana na kupendana kwa dhati.
Wakaondoka wakiwa na biblia na kofuli yao mpaka kwa mzee mmoja aliyeaminika kwa busara na kumweleza adhma yao naye kabla ya kuwakubalia ombi la kuwa shahidi wao akawauliza,


" Je ni kweli mmeamua kuapa kwa kutumia Biblia na kofuli hii kuwa mnaufunga uhusiano wenu kuwa wenu tuu na mnakubali kuwa hamtasalitiana milele?"
Wote wakajibu ndio.
"Je mnatambua kuifunga kofuli hii na ufunguo kuniachia mimi na kofuli kwenda kuitupa mbali mjue kamwe hamtaifungua tena na matatakiwa kuwa pamoja kwa namna yoyote ile?"
Wakasema tumeafikiana.
Mzee akawaongoza kwa sala na kuwaomba waishi kama walivyokubaliana na kisha kuifunga ile kofuli.
Wale vijana wakarudi majumbani kwao na kuendelea kuishi kwa furaha na amani huku kila mtu akiwa na kiu ya kuonyesha zaidi upendo kwa mwenzake.


Miaka ikaenda wakahitimu chuo na kijana akapangiwa kazi kijijini sana na kukawa na matatizo ya usafiri na binti kwa kuwa alipangiwa mjini akawa kila mara akimtembelea kijana na kijana akienda mjini pia.
Miaka ikaenda hatimaye taratibu wakaanza kupunguza mawasiliano baada ya kijana kuhamishiwa mbali zaidi na binti akabadili namba na kuanza mahusiano na boss wa kampuni yake na kisha wakaoana.
Kijana akafanya kazi kule kijijini kwa kujituma na kuweka fedha ili aweze kuja mnunulia pete nzuri ya uchumba na harusi yao ije kufana na waishi vizuri bila kujua kuwa keshaolewa.
Baada ya kujiandaa vya kutosha akaanza kuomba uhamisho ahamie mjini na alipofika mjini akapata habari za mkewe kuolewa na wamehama mji ule.
Kijana aliumia sana na kisha akaamua kuondoka kwenda mbali kuanza maisha mapya akiwa na huzuni sana.
Maisha ya furaha yakamwishia yule binti kwani hakupata mimba wala dalili na kila alipofanyiwa uchunguzi akaonekana yupo safi.


Furaha na amani ikaanza kumpotea katika familia yake na baadae mambo kuwa mabaya zaidi kabla ya kuanza kutembelea kila kibanda kilichoandikwa mganga wa jadi akihisi kafanyiwa mchezo.
Baada ya kwenda kwa njia hizo zote bila mafanikio akawa hana jinsi zaidi ya kuwa mtu wa kulia na kuhuzukika kila mara.
Siku moja akiwa ndotoni akaonyeshwa Biblia na ile kofuli akakumbuka kuhusu nadhiri yake na yule kijana. Akaanza kumtafuta yule kijana amwombe msamaha na baadae akampata.
Baada ya kumwambia kijana huku akimwomba msamaaa kijana akasema mimi sina tatizo ndio maana sikuoa ili nikuone na uje uniruhusu kwa kulingana na agano letu.


Na kilichobaki hapa ni kumtafuta mzee kwani kofuli mimi nilimkabidhi mama yangu na analo kwani niliamini mama ambaye ni mwanamke kama wewe angenirekebisha kama nikikosea na ajue siri yangu na wewe ili azidi kunipa hekima na busara ya kuwa na wewe, je na wewe funguo ya akiba uliweka wapi?
Binti akasema niliipoteza nilipoanza mahusiano na mme wangu.
Wakaenda kwa mzee na kusikia kuwa alishafariki, kijana akampa kofuli bila ufunguo na kumwomba binti ampe ruhusa akaoe.
Binti akakubali na kijana akaoa na sasa ana mke na watoto wawili lakini yule binti mpaka sasa kashaachika zaidi ya ndoa nne akikosa amani kwa kuvunja agano lake na kijana yule.




Dada na kaka zangu kumbukeni
1. Kamwe usimwahidi mtu kumpa mambo makubwa maishani na hali wewe huna uwezo

2. Kamwe usimwambie mwanamke unampenda wakati humaanishi

3. Usitumie vitabu vya dini kufanikisha mipango yako ya ulaghai wa mapenzi

4. Kamwe usiwahusishe watu kukusaidia kushuhudia uongo ili kumpata mwanamke...
Hawa ni viumbe ambao kwa asilimia kubwa sisi wanaume ndio huwafanya waumie na kila mwanamke katili, jambazi, kahaba na wengine lazima wana hadithi iliyowafanya kuwa hivyo na ilisababishwa na mwanaume

5. Usijaribu kufanya ahadi yoyote ili kumpata mwanamke ukiapa kwa jina la Mungu kama huamini
Ukishindwa kutekeleza huishia kukosa furaha maishani mwako na kuwa kama dada yetu.

Post a Comment

0 Comments