Header Ads Widget

Responsive Advertisement

TETEMEKO LA MOYO - 4

Image result for adrian mcdonald photography

Simulizi : Tetemeko La Moyo
Sehemu Ya Nne (4)

Muonekeano wa yule binti baada ya kutufikia na kuanza kuzungumza nae niliona vyema hakuwa anahamini ambacho anakiona mbele yake kamwe sura yake ilionekana imeshikwa na mfadhahiko mbele ya macho yangu hivyo niliongea na dakika chache na kutuacha pale mimi na juma tukiendelea kuongea jambo. Juma akanitupia swali, swali likaleta dhahama kwenye kichwa changu.
ENDELEA.

“Vipi Eddy unamkumbuka yule mdada?”
Aliniuliza juma, nikatafari kidogo lakini sikuwa na jibu, nikaamua kumkabili Juma.
“Hapana mimi nimeshangaa tu, akinishangaa na kunipa pole kwa yalinikuta ila nahisi ile sura si ngeni machoni mwangu” niliyatoa maeno yale huku nikimtazama kwa makini Juma. Kabla ya kuibuka na jibu lilionifanya nijione mjinga.
“Wapi wewe yule ni Rose rafiki yake mkubwa na Irine,” alisita kidogo Juma huku akinitazama na mimi nikimtazama katika mfadhaiko.
“Hivyo pale alipokuona ameshikwa na aibu msichana mbaya sana ndugu hafai hata kidogo ndugu ,na kwambia simpendi huyu msichana si mimi tu watu hawamkubali hata kidogo hapa chuo unavyoona.

Maneno yale ya Juma yaliniiingia kwenye kichwa changu akili ikaaanza kumtafuta,,, “Rose!!! Rose!!!”, kama dakika kadhaa nikakumbuka yeye ndio alikuwaga msaada kwangu mpaka kujenga mazoea na Irine. Nikaikumbuka vizuri siku ya kwanza kuonana na Irine kule cafe area yule msichana ndio alikuwepo pamoja na wenzake wakipiga domo pale karibu na meza nilipokaa mimi. Oooh!.. aiseeeh!... Juma nimemkumbuka huyu manzi" nilizungumza kwa kuhamaki. “Basi ndugu yule msichana hafai hata kidogo hafai kaka hata kwa kulumagia…. acha mimi na kwambia acha babu!!! mwone vile vile mnafiki tu yule asikuambie mtu ninavyokuambia unavyomuona huyo Irine wako si bure tabia zote unazozijua mbovu yule mdada ndio atakuwa anahusika si ndio rafiki yake mkubwa siku hizi wamekuwa hawafai hata kidogo lecture gani asiyewajua hawa we kaulize” Juma aliongea kwa msisitizo sana yale maneno yake.

Yaliniiingia vilivyo kwenye ubongo wangu, hapo tena hata hamu ya kutaka kujua habali za Irine ziliniisha kabisa. Ingetokea wapi?, sikutaka kuutesa moyo wangu kabisa kama Mungu amenipangia kunipa basi hata nipa lakini si kwa majalibu haya alionipatia yanatosha kabisa, nilisema na moyo wangu.

Wakati huo, tulizungumza kwa kina na Juma na nilimweleza juu ya hatima yangu katika masomo. Uzuri Juma alikuwa rafiki mzuri sana kwangu hakunivunja moyo alinifaliji, nichukulie hali ile ya kawaida tu nisifikirie kitu kibaya umri wangu bado tu ulikuwa ukiruhusu kizuri sasa nipo na ninafuraha tele na mwenye afya hiko ndio kikubwa pia hakusita kunipa ushauri juu ya wanawake. Niweze kuwanao mbali kabisa na kama hivyo nitashindwa basi niangalie mwanamke wa kuanae na si wanawake wote tu. Nilimwelea vyema na kumwahidi nitazingatia yale yote aliyoniambia.

Hakika Juma alikuwa rafiki mwema sana kwake, kuhusu yote siwezi kumpa lawama yeye najilaumu mwenyewe na nafasi yangu.
Muda nao haukuwa rafiki sana kwetu, baada ya zaidi ya lisaa nikiwa naendelea mazungumzo. Mida ya kipindi kwa upande wake Juma ilikuwa ikiwadia hakuwa na jinsi ilimbidi tu aende na kutuacha mimi na Criss tukiangalia njia ya kutokea ndani ya chuo. Tulipiga hatua kwa dakika kadhaa huku nikitafakari yale niliyokutana nayo ndani ya chuo kile nikiwa nimeinamisha kichwa na kukata hatua.

Hamadi ile na nyanyuaa kichwa kwa mbali niliona kitu,kilifanya mapigo yangu ya moyo yaende mbio hata nilipojaribu kuizuia hali ile nilishangaa nikishindwa kujizuia. Moyo nilihisi maumivu makali kweli, taswira ile niliyokuwa nikiiyona japo kwa mbali ila haikuwa ikileta hali ya kawaida ndani ya moyo wangu, ilieta mfahahiko kwa kiasi hata ule uchangamfu niliokuwa nawo hapo awali njiani mule ulipotea.
Sura ya Irine mboni zangu ziliweza kusawili kile nilichokuwa na kiona na afadhari angekuwa yeye hata hakuwa peke yake mwanaume yule aliyevyokuwa anakikimatia vizuri kuino cha Irine ambaye licha ya yote ila nilishangaa tu roho inauma mbaya usiombe ndugu kitu ukiwa unakipenda haijalishi ikiwe kimekutenda namna gani ila bado tu kitabaki ndani ya moyo na kama kidonda ukikigusa basi kina shituktuka. Kweli niliumia sana kwa siku hiyo, na kupoteza furaha yangu.

Hata hali ya kuendelea kupita njia ile ilinishinda kabisa miguu yangu ilijikuta inabadilisha njia huku mikono yangu ikikosa nguvu hata kuishika mikono ya mdogo wangu Criss.
Nilijivuta taratibu sikutaka kuungalia hali ile niliyoina kwenye mboni ya macho zangu muda mfupi, niliendelea kufakamia ardhi taratibu huku kichwani mwangu jambo lile lilikuwa likinirudia ndani ya kichwa change. Hapo sasa maneno ya juma yalianza kuingia vizuri kwa mara nyingine ndani ya kichwa changu nakuamini alikuwa sahihi asilimia zote haikuwa haja tena wakupinga maneno yake hata kidogo unayapingaje? kwanza alikuwa sahihi kabisa Juma kwa kile alichokuwa anakiongea. Hapo niliamini hata ule msemo wake ya kuwa kama kunavitu duniani hapa havipendeki basi ni viumbe vinaitwa wanawake.

Mawazo hayo yote yalikuwa yananigonga nikiwa njiani kurudi
Nyumbani, hata tulivyoingia nyumbani siku jua nilishaanga tu nipo ndani nimeshika kidaftari ambacho kilikuwa kama kijitabu nilichonunua wakati tulipokuwa India na kuanza kuandika mambo yote kuanzia pale nilipoona na yule binti basi kuanzia hapo niliendelea kuandika tu hata sikujua hali ile ilikuwa ikitokea wapi?.

Haki walifanya jambo ambalo sikulitegemea kabisa, kama wangelifaya kwa upande wangu, ni vile walivyokuwa wakinitizama kwa dharau kiasi cha kwamba , nilihisi uwenda kuna kitu nimekifanya kibaya dhidi yao, lakini nikakumbuka si kuwa na wafahamu labda wao ndio walikuwa wakinifahamu. Sikutaka kuisumbua akili yangu nilipuuzia, nikiongoza kule kwenye ofisi ya mkuu wa chuo.
Lakini sasa ofisi ilinipokea katika namna ya aina yake, macho yangu yaliweza kuona lile kwa uzuri kabisa, ni kweli niliona.
***********
“Aahhh! nani tena?” , haraka nilijitoa ndani kuelekea nje baada ya kusikia sauti ikiniita jina langu. Haikuwa ya mwingine, ilikuwa sauti ya mjomba. Nilishangaa ujio wake katika mshangao ambao tiyari nilikuwa na majibu nao.
“Karibu anko”, nilimkaribisha kabla ya kumsalimu, wakati huo akikaribia ndani na kuketi katika moja ya sofa. Punde mjomba aliniuliza habari za mama, nikamwambia yakuwa ametoka kidogo, kauelekea kwenye mikutano yao. Hivyo alikubaliana nami na maneno yangu, tuliendelea kukaa pale sebuleni wakati huo, nilikuwa nimempatia maji kama alivyokuwa, ameniagiza. Aliendelea kunywa taratibu huku kinywa chake kikionekana na mengi ya kusema lakini, katika namna ambayo nilikuwa najua sipaswi kujua kutokana na tabia yake mjomba.

Nilikuwa Kimya tu huku sauti ya runinga kidogo ikifukuza kimya kile, kabla yakufukuzwa kwa mazungumzo yetu sasa, tulizungumza sana na mjomba kwa wakati ule, mazungumzo ambayo mjomba aliyatawala sana. Ilikuwa juu ya masuala yangu ya shule, hakuchoka kunisisitiza niendelee kusoma iliniweza kufaulu mtihani wangu, huku akinipa mifano mingi mingi kuhusu maisha. Nami nilikubaliana na maneno yake kwa kiasi kikubwa. Aliendea mbali zaidi na kunikanya kuhusu mahusiano katika namna moja ama nyingine nami nilikubaliana nae kabisa na hata asingeniambia habari za mahusiano kwa upande wangu moyo wangu, haukuwa tiyari kabisa kujihusisha ndani ya dhahama hiyo. Ni kweli tangia hapo nyuma sikuwahi kupenda na kuhusu wanawake nilikuwa nikisikia tu kwa watu na kamywe sikuwahi kujua uzuri wa viumbe hivyo zaidi ya mabaya ya viumbe hivyo labda vingenifanya niwe mfuasi kama wa viumbe hivyo kama binadamu wengine. Hivyo pale maneno yake mjomba kuhusu wanawake kwangu niliona hayana tija hata kidogo.

Mazungumzo yetu yalianza kukatishwa na njaa kali iliyoanza kuchachafya tumbo langu, japo nilijitahidi mwanzoni kujizuia lakini hali ilionekana kuleta ugumu upande wangu. Nilijua wazi mama asingeweza kurudi na kufikia kupika, hivyo ilinibidi niandae chakula cha haraka. Akili yangu ikafikiria kwenda kuchukua samaki wa kukaanga ambao hawakuwa wanakaanga mbali na maeno yale ya nyumbani. Hivyo nilivyomaliza kutaarisha ugali. Nilichepuka haraka kwenda kuchukua samaki ambao niliona wangefaa kabisa katika kuridhisha tumbo langu na hata la mjomba. Kuhusu mama sikuwa na shaka nae mara nyingi hakienda kwenye vikao vyao huwa akirudi hanaga mpango wa kula.
Kweli nilifanikiwa kuridhisha tumbo langu baada ya dakika kama kumi, hapo walau maneno ya mjomba yaliweza kupenya vizuri kwenye masikio yangu kwa mara nyingine kuliko hata awali. Wakati tukiendelea kuzungumza baada ya kumaliza kula, hakupita muda mrefu hatimaye mama alirejea kutoka mkutanoni na kukuta ujio wa mjomba machoni mwake.
Sidhani kama mama alikuwa anategemea mjomba angekuwa pale kwa nyakati ile. Maana ilikuwa ajamaliza hata siku tatu alikuwa amerejea tena. Mjomba alionekana ana mengi yakuongea katika kinywa chake.

Sikutaka kuendelea kukaa pale, baada ya kuzungumza kidogo na mama huku akinipatia maagizo ya kwenda sokoni kwa muda ule, alikuwa kama anajua kuwa nisingeendelea kukaa kusikiliza maongezi yao.
Taratibu niljitoa ndani, miguu yangu ikiongoza soko lilipo, dakika chache tu zilinifanya nifike eneo lile, nilichukua nilichokuwa na miigizwa na kurejea nyumbani. Wakati huo nilikutana na maongezi yalikuwa yakiendelea kati yake mama na mjomba, sikutaka kuyafatiria. Nilijitoma ndani ya chumba changu baada ya kumkabidhi alichokuwa amenituma.

Nilijibwaga juu ya kitanda nikiwa katika tafakuri kidogo, ni kweli tafakuri ile ilinitoa pale nilipokuwa na kunipeleka mbali zaidi, katika namna ambayo sikudhani kama ingenipeleka mbali. Na kili wazi ndugu msikilizaji, mawazo ni kitu kibaya sana, hakika ni ubaya ambao uwezi kuoona katika jicho la kawaida tu. Mwili wangu ulikuwa pale kwenye kitanda lakini akili haikuwa pale kabisa, hata nusu saa, lisaa linipita nikwa pale pale juu ya kitanda, huku nikiwa nimeyakodoa macho yangu juu tu.
Naikumbuka siku ile, ndio haikuwa imenipotea, naam!. Mawazo ya shule yalinijia nikiwa kitandani pale. Haswa nilikumbuka siku ile, nilivyoletewa habari za kupendwa na msichana, hakika hakuwa kazi ndogo katika kutuliza mzuka wangu. Hakuna aliyetegemea uwenda ningezipokea habari zile katika mtazamo wa namna ile, mtazamo ulijaa chuki ndani yake. Na si hivyo tu aina ya msichana mwenyewe ndio ilifanya watu wa nione wa ajabu kweli. Na kili alikuwa msichana ambaye hakuna mwanafunzi wa kiume wa shule yetu asingependa kuwa nae, Mungu alikuwa amekijalia kiumbe hicho, mwili wa wastani, usiochukizwa kwenye macho ya wapenda ngono. Lakini kwangu hakupata nafasi walau kumtazama mara mbili mbili na kubadili msimamo wangu. Ilikuwa bahati nzuri tu kwake siku hiyo naweza kusema maana lilishia juu juu baada ya fikra zangu tu, kuamua kulipoteze jambo lile, huku nikitoa onyo kali kwa msichana yule.

Sasa lilikuwa limejirudi jambo lile nikiwa kitandani pale, akili yangu ilikubaliana yakuwa nilikuwa sahihi kabisa katika lile, tofauti hata nilivyokuwa nikidhani. Nilisonya mara mbili kabla ya kuamka na kutikisa kichwa changu, huku nikionya kisinilitee kumbukumbu ambazo hazikuwa na faida kwangu.
Ni muda huo, ambao nilisikia sauti ya mama ikiniita na mimi kujitoa ndani, kiuvivu kwenda kumsikiliza. Hakuwa na jipya sana ilikuwa kama nilivyokuwa nikidhani ya kuwa ilikuwa nyakati ya kutumwa tena. Ndio lazima ingekuwa hivyo maana hapakuwa na mtu wakumsidia kazi pale nyumbani walau dhahama hiyo ya kutumwa tumwa isingekuwa kwangu.

Nilijitoa kusikiliza wito, katika nyakati ambazo tiyari juu lilikuwa likielekea kuondoka kwenye uso wa dunia.
Wakati huo macho yangu yalikutana na tabasamu pana la mjomba kuliko kawaida, ni hilo tabasamu ambalo lilikosekana nadhani kwa kipindi kirefu kwake. Macho yangu yalipigwa na kama bumbuwazi, kabla ya kukili sasa mjomba alikuwa ni yule ambaye niliyokuwa nimezoea, katika siku za nyuma. Moyo wangu ulifarijika sana, nilitamani kuendelea kumwangalia lakini sauti ya mama ilikuwa imeshapita ikiniagiza dukani kuendea chumvi.
*********
Siku hiyo ilikuwa tofauti sana, nilitegemea ningeweza kurejea mapema nyumbani, kutokea dukani kwa Mangi, lakini nilikuatana na wateja kadhaa ambao walikuwa na mengi mahitaji hivyo ilinisubirisha sana, ubaya akili yangu hakunishungulisha kuliendea duka lingine, na pale nilipokumbuka umbali wa kuendea duka lingine mwili wangu ulinyongonyea na kuendelea kusubiria pale pale. Mvumilivu hula mbivu baada ya dakika kama kumi hivi nilipata nafasi ya kuhudumiwa.
Nilirejea nyumbani, nyumba ilinipokea katika namna ambayo sikuitegemea.


Kweli sikutegemea kabisa. macho yangu hayakuweza tena kumuona mjomba, ni muda kidogo tu alikuwa ameshaaga na kuondoka, pasipo hata matarajio yangu.
Taswira ya mama tu ndio ilinipokea baada ya kuumulizia mjomba, kumbe muda mfupi tu alikuwa ameendoka. Sikutaka sana kujishughulisha na habari zake, wakati huo akili yangu ilishaanza kukumbuka kuhusu kitabu cha kaka Eddy hivyo nilimuaga mama na kuingia ndani, kutokana na tabia nilikuwa nimejizoesha muda wote wa kukaa ndani mama alishaizoe tabia ile hivyo, hata aikumfanya uwenda kuhisi kitu ambacho muda wote kilikuwa kinanifanya niwe ndani.

Nijitoma ndani, nikiwa na shauku kubwa sasa, taratibu niliwasha feni na kulifukuza joto katika namna iliyoleta faraja kwenye mwili wangu huku nikiwasha taa kulifukuza giza ambalo lilianza kutaka kushamili ndani ya chumba changu, kufanya macho yangu kuwa katika ubora wa hali ya juu. Mikono yangu hakuchelewa kupambana kule nilipokuwa nimekiifadhi kitabu kile. Muda mchache macho yangu yalianza kupambana na maandishi yale, ambayo yalionekana kunipa shauku ya kuliona jambo, muda ambao ulionekana si mrefu.
************
Kibao kilikuwa kimeendikwa maneno yalikuwa yamesomeka closed yaani kumefungwa ndio yalipambwa nje ya mlango wa ofisi ile, ambayo sikuwahi kutegemea uwenda kungekuwa kumefungwa kwa muda kama ule, niliangalia saa yangu ilionesha vyema ilikuwa sasa tano kasoro, kwa muda kama ule nilijua wazi uwenda hakuwa mbali muhusika wa ofisi ile ambaye ni mkuu wa chuo kile.
Akili yangu haikuniupa kutoka eneo lile, niliamua kujisogeza kidogo na kuketi kwenye moja ya viti vilivyokuwa nje ya ofisi ile. Ambavyo havikuwa mbali sana na dirisha la ofisi ile. Wakati huo sikujua kukaa kwangu eneo lile kungeleta dhahama kubwa sana kwa upande wangu, dhahama ambayo sikuwahi kuitegemea uwenda ingenitokea katika siku ile ambayo ilikuwa ni moja ya siku muhimu sana katika maisha yangu ya kuipata elimu kwa namna moja ama nyingine.

Niliendelea kusubiri kwa muda kidogo kabla ya ngome za masikio yangu, kuanza kupitiwa na sauti ambazo hakika hazikuwa mara ya kwanza kuzisikia, ni sauti hizo ambazo zilikuwa zinanifanya ni furahi kuwa na mwanamke aitwaye Irine nikiwa ndani ya jambo ambalo wapenzi wote katika hii dunia, wanalipa kipaumbele na kurifurahia kuliko mambo yote. Mwanzoni nilihisi uwenda masikio yangu hayakuwa vyema kupokea sauti ile, lakini nilipojisogeza vizuri kwenye dirisha lile sasa sikuwa na haja ya kubishana na sauti zile, ziliendelea kupenya vizuri huku zikiuacha mwili wangu katika namna isiyoelezeka kibaya zaidi ni hata yale maneno ambayo mara nyingi Irine alikuwa akipenda kuyatamka tukiwa kwenye zoezi hilo, niliyasikia vizuri ya kimtoka huku sauti ya kugumia ya kumkuu wa chuo kile ilikuwa ikitoka. Nilijiuliza mara mbili mbili huku nikiwa siamini ya kile nilichokuwa nakisikia. Maswali mengi yalijengeka kichwani mwangu kabla ya kunitoka neno la kizembe katika hali ambayo hata mwenyewe ilikuwa ngumu kujisikia, ni hilo neno ambalo lilikuwa likiomba eti asiwe Irine wangu, nilijitamani kujicheka lakini kicheko kilikuwa mbali, na hata kingekuwa karibu na mimi hakika kingekuwa kicheko kilichojaa uchungu ndani yake.

Uvumilivu ulinishinda nikiwa pale, niliamua kujitoa mahali pale, kwa miadi ya kurudi kwa muda mwingine, sikutaka kuendelea kusikiliza sauti zile, nilijitoa kinyonge kuliko hata nilivyokuwa nikitegemea. Wakati huo kwa mbali kelele za wanafunzi ambao walikuwa uwanjani nilikuwa na pambana nazo, sauti ambazo zilinikumbusha vicheko vya wale wasichana ambao akili yangu sasa ilihusinisha na lile tukio, na kukili uwenda walikuwa wanajua maana ya vicheko vyao, ambavyo mwanzoni niliwatoa akili sasa nilijiona uwenda mimi ndio nilikuwa sina akili. Japo niliampa kutojihusicha na msichana huyo lakini, nguvu ya penzi ilikuwa ikininyanyasa.

Kweli ilininyanyasa katika kiwango cha juu sana, miguu yangu ilitetemeka njia mule, nikipambana na ardhi ambayo niliona muda si mrefu ilikuwa inataka kunidharisha, katika namna ambayo sikuwahi kuitegemea, na hata nilipojikaza bado nilishindwa. Niliamua kujitoma ndani ya darasa moja ambalo lilionekana liko wazi, taratibu niliamua kuketi kwenye moja ya kiti ambacho kilikuwa kimejitomea kimeza kidogo mbele yake. Ambacho kiliupa hifadhi mwili wangu punde nilipojiweka kwenye kiti, baada ya kukisogeza karibu nami, nilijiinamia chini kwa muda kidogo lakini hatimaye fikra zangu zikasiliti kile kiti huku ikijenga taswira ya mkuu yule wa chuo, na Irine wangu. Kabla ya kupingana na kile nilichokuwa na kisikia kwenye dirisha la ofisi ile, ya kuwa hakuwa Irine wangu, roho ya kupingana na lile ilianza kunitawala huku nikitamani kwenda kuhakisha juu ya lile. Ukweli ilinisumbua niliamua kujitoa haraka.

Ajabu sasa, bora ningeiamua kubaki kule kule, nisingehitaji ushahidi wa kile. Masikio yangu yangetosha kuwa shahidi kabisa. Maana macho yangu sasa yalikumbana na dhahama ile, ni kweli alikuwa Irine, macho yangu yaliendelea kupambana na mwanamke yule punde alipokuwa akijitoa kwenye ofisi ile ya mkuu wa chuo, utadhani hakuna kilichokuwa kinaendelea ndani yake. Nikiwa nimesima kwa mbali kidogo lakini umbali ambalo ulikuwa ukiniwezesha vyema kuona vizuri kile kilichokuwa mbele yangu, na uzuri Irine hakuwa mgeni kwangu.
Nguvu ziliniishi na hata hamu ya kuendelea kubaki ndani ya chuo kile hakuwepo kabisa, miguu yangu ilishageuza njia ya kurejea nyumbani huku akili yangu ikiwa nzito kuliko kawaida, mwili ukiendelea kupambana na maumivu ambayo hayakuwa ya mchezo hata kidogo. Mawazo mengi yakiwa yanakikabili kichwa changu nikiwa ndani ya daladala nikirejea nyumbani. Alimanusura nipitilizwe sehemu ya kituo cha nilipokuwa na shuka.

Hali yangu haikuwa sawa hata niliporejea nyumbani, siku nzima kwangu ilikuwa mbaya, ijapokuwa nilijitahidi kuificha sana mbele ya mama ambaye kwa upande wake siku hiyo alionekana kama anajambo ngumu linamkabiri hivyo hakujihusisha sana na mimi na hata mdogo wangu Criss siku hiyo si kumkuta nyumbani, alikuwa amekuja kuchukuliwa na mjomba, ambaye nilipata taarifa zake punde nilipoona kuna tofauti kidogo ambayo hapo awali haikuwepo pale nilipoamua kumuliza mama ambaye alikuwa akiendelea kujishughulisha japo kiuvivu uvivu, ni kama alikuwa anajua uwenda jambo zito lilikuwa linakwenda kutokea katika familia yetu, ni kweli ni kama alikuwa anajua lakini alikuwa tiyari amechelewa. Roho yangu haikuwepo tena dunia, kwa muda ule, maana nilipojitoma ndani, sikuona faida ya kuishi katika dunia. Dunia ambayo katika jicho la kawaida niliona hainitaki kabisa, Kiukweli niliamua kufanya maaumuzi haya, huku nikimsihi Mungu.

ITAENDELEA

Post a Comment

0 Comments