Header Ads Widget

Responsive Advertisement

NIMEIPATA FURAHA YANGU. - 3

Related image


Simulizi : Nimeipata Furaha Yangu
Sehemu Ya Tatu (3)

kuwasha moto kwa shangazi ambaye hakuwa na roho ya huruma hata chembe alitupiga sana hadi muda mwingine tulikuwa tukizima hasa hasa Rhodina ule upendo aliokuwa akiuonesha pindi wazazi wetu wapo ulifutika.

Nakumbuka siku moja shangazi alitupiga sana hadi tukawa tumezimia kwa muda mrefu hali iliyopelekea kumzika Rhodina nyuma ya nyumba angali akiwa hai , nilikuja kuzinduka na kujikuta peke yangu ndipo nilipoanza kumtafuta Rhodina lakini sikumpata nililia sana na kwenda kujikunyata nyuma ya nyumba nikiwa huko nalia ndipo nilipoona mchanga mbichi ukiwa umechimbuliwa , moyo ulinisukuma kwenda kutazama mahala hapo sikuamini macho yangu nilipoona gauni la Rhodina likiwa limeachia achia katika michanga nilianza kufukua haraka sana kweli dada Rhodina alikuwemo ndani ya shim....."
"What? Are your serious ( Nini unauhakika?”) Rodrick alijikuta akipigwa na mshangao mkubwa sana hata mikono yake ilishindwa kuandika. "Mwanangu pole sana," nae mkuu wa gereza alisisimkwa na habari hiyo.

"Sikuwa na nguvu za kumtoa Rhodina ndani ya shimo hilo kutokana na utoto wangu hivyo nilichukua kamba ngumu ya ngo' mbe na kumfunga nayo Rhodina katka miguu yake kisha nilitafuta ngo' mbe aliyekuwa mpole na kumfunga kamba shingoni nilianza kumswaga ......" alikatishwa. "Je shangazi na ndugu zako walikuwa wapi?" Mkuu wa gereza alimuuliza Rhoda aliyekuwa akilengwa lengwa na machozi. "Walikuwa ndani……….. kitendo cha ngo'mbe kutembea kilimfanya Rhodina aanze kutoka ndani ya shimo huku akiwa bado amezimia japo nilijua kuwa alikuwa akiumia sana kuvutwa lakini sikuwa na njia yeyote ya kumuokoa namshukru sana ng' mbe huyo kwa kumuokoa dada yangu Rhod....inaaaa ali..chu...kaaaa!" Rhoda alishindwa kuendelea baada ya kukumbuka tukio zima alianza kulia sana hali iliyopelekea kukosa maelewano tena.

Japo walijitahidi kumtuliza lakini hakutulia. "Rhoda mama pole sana!" Rodrick aliyatamka maneno hayo huku akitoa leso na kumpatia Rhoda aliyekuwa bado akilia huku kamasi nyepesi zikichuruzika. "Ahsa...nte..!" "Usijali chukua tu!" "Ha..paana!" Rhoda hakutaka kuchukua leso hiyo kutokana na kukosa imani kwa binadamu. alendelea kuyafuta machozi yake kwa sketi yake chakavu. "Nahakikisha kukusaidia hadi mwisho Rhoda " Rodrick aliongea huku akitoa tabasamu dogo macho nayo yalikuwa yakiutazama uso wa Rhoda katka tazama hiyo alijikuta akiutambua uzuri wa Rhoda mwili ulitetemeka. "My God she is so quety( mungu wangu ni mrembo sana) Rodrick alijikuta akiwaza hayo na kuachia tabasamu jingine kwa Rhoda , ambalo halikupokelewa na Rhoda zaidi ya machozi .
" Rhodina alikuwa amechubuka sana karibia mwili wote nilimfungua kamba na kuanza kumpulizia pumzi mdomoni lakini nikiwa sifahamu kama kweli angeweza kupona kabisa.

"Je uliwezaja kuwa jasiri kiasi hicho?" Mkuu wa gereza aliuliza huku naye roho ya huruma ikianza kuchukua nafasi kwa haraka sana. Rhoda aliendelea "Sijui ni mungu ndiye alikuwa akifanya kazi na siyo mimi , baada ya kumtoa Rhodina ndani ya shimo nilianza kumpulizia pumzi kifunia huku nikilia japo nilikuwa nikijitahidi sana lakini haikusaidia roho iliniuma sana nilianza kuona picha ama mwili wa Rhodina ukiwa ndani ya jeneza akiwa amefumba macho.Picha hiyo niliifananisha na ya wazazi wangu pamoja na bibi siku chache zilizokuwa zimepita!"
"Kwanini hukwenda kumuita shangazi yako ama majilani!?" "Rodrick shangazi alikuwa hapatani na kila mtu mtaa ule na hiyo ilichangiwa na wao kututetea sisi .............sikuwenda popote ikabidi nikae kusubili lolote lile na nilipanga kama Rhodina angekufa nami ningejiua tu lakini katika kukaa huko nilishtukia Rhodina akipiga chafya sikuamini dakika chache alifumbua macho na kuniita nililia kwa furaha sana.

Baada ya miezi miwili kupita Rhodina alikuwa amepona kabisa ndipo shangazi Martha alimpoleta tena Ngariba ......... “Ggariba ndo mtu gani?" "Kaka ngariba ni mtu anayekeketa wanawake," Rhoda alijibu swali hilo na kuendelea.
"Tulikataa tena ndipo alipoamua kutufukuza ndani na alidai kuwa tusipofanya hivyo siye sio wanawake waliokamilika na ili uwe mwanamke kamili lazima ukeketwe kwa ajili ya kuolewa , tulipozidi kugoma kufanyiwa hivyo shangazi alitufukuza nyumbani kwake lakini Rhodina alikataa kuondoka hali iliyopelekea kufungiwa katika zizi la ng' ombe tukiwa tumefungwa na minyororo kama mbwa us......," alikatishwa. "Wewe binti acha kuong'opa!" "Mkuu sitanii hebu tazama alama hii," Rhoda aliwaonyesha kovu kubwa lililokuwa katika kiwiko cha mkono lililokuwa limesababishwa na mnyororo.
"Pole sana Rhoda," hata Rodrick alishindwa kujizuia alijikuta akitaka kulia ila alijikaza kiume
"Tulilala zizini na kushi......," Rhoda alishindwa kuendelea alilia tena wote wawili walimtuliza sana hata mkuu wa gereza alimfungulia pingu katika mikono yake ilichukua dakika kama kumi na tano ndipo walipoendelea tena .
"Tuliendelea kulala na kushinda zizini zaidi ya wiki moja huku tukiwa tumekula siku tano tu tena mlo mmoja sikumuelewa shangazi yangu huyo alikuwa na roho gani kilio na machozi ndiyo kilikuwa faraja yetu muda mwingine tulitamani nasi kufa tu ndipo siku moja shangazi alipotuleta chakula alisahau kutufunga minyororo hapo hapo tulitoroka na kuanza kukimbia tusikokujua japo ilikuwa usiku lakini hatukujali.
Usiku huo tulilala porini hadi asubuhi na kesho yake tulianza kuifuata njia iliyokuwa mbele yetu bila kujua wapi tulikuwa tunaelekea tulishtukia tukifika Tarime mjini ambako hatukukaa sana kesho yake tulipanda gari lililokuwa likielekea musoma mjini tukiwa na lengo la kwenda kwa baba mdogo aliyekuwa akiishi nyumbani kwetu ...." Rhoda alikatishwa tena na Rodrick aliyekuwa akiendelea kuchukua maelezo.
"Je shangazi yako huyo yupo?" "Sijui sijawahi wasiliana naye toka kipindi hicho." Aliendelea. "Sikuamini tulipofika kwa baba mdogo aliyekuwa akiishi katika nyumba ya baba , hakuonyesha furaha hata kidogo hata kukaa kwenye makochi yaliyokuwa yetu hatukuruhusiwa tulikuwa tukilala kwenye banda lililokuwa la ng'ombe japo mali zote zilikuwa za baba lakini hatukuambulia chochote tukawa wafanyakazi wa ndani ile ahadi aliyoitoa ya kutuendeleza kimasomo ilifutika mateso yalipotuzidia sana tuliamua kutoroka baada ya kuiba elfu kumi ambayo tuifanya kama nauli kutoka musoma hadi huku mwanza tukiwa hatuna ndugu yeyote yule wala hatukuwa tukijua chochote kuhusu mwanza.
Tuliishi mtaani zaidi ya mwaka mmoja tulilala mtaani huku tukisumbuliwa na adha za mtaa ndipo tulipokuja kuchukuliwa na mama mchepuko." Rhoda alieleza mengi sana hadi mazigira ya kifo cha Rodina hali iliyopelekea hata mkuu wa gereza kuahidi ushirikiano na Rodrick .
"Aise hili limtu linapiga simu na kukata harafu halipatikani tena na linadai kuna mtu anatoka Trime ana magendo tulifatilieni," alionge Afande Issack kwa rafudhi ya kikurya na kuwafanya baadhi ya askari waliokuwemo ndani ya kituo hicho kidogo cha Bunda kuanza kutoa taarifa sehemu mbalimbali za eneo hilo.
"Oyaaa! Vipi mbona naona vijana wako wamezagaa kila kona?" "Kweli?" Upande wa pili wa simu ulijibu kwa mshangao. "Ndio watoe bhana nina mzigo mkubwa sana watanizingua!" mama mchepuko alikuwa akiongea na mkuu wa askari mkoa wa mwanza , ambaye naye alikuwa mmoja wa wauzaji wazuri wa bangi na mirungi na alikuwa akimtumia mama mchepuko kumuingizia mizingo hiyo ila alichokuwa akifanya ni kumuwekea usalama wa kutosha .na huyo huyo ndiye aliyekuwa amempatia mavazi ya jeshi la polisi.
"Kwani wewe uko wapi?" "Ndo naelekea seregeti." "Oky subili kama dakika tano!" Aliongea mkuu huyo kabla ya kukata simu moja kwa moja alimtafuta Ocd wa Ramadi na Magu baada ya kuongea nao mara moja ilitolew amri ya askari kutolikagua ama kulisimamisha gari aina ya Suzuk T 567 BSS hali iliyopelekea baadhi ya askari polisi waliokuwa mle barabarani kuondoka kwa hasira.
"Hili linchi basi tu rushwa haitaishaga! Uaweza ukakuta mkubwa wa nchi ndo anayeingiza magendo na kutueleza eti mali ya serikali!" Alisikika mmoja wa askari polisi miongoni mwa wale waliokuwa wakiondoka.
"Hiii! Unauliza? Tena .....,." alisita kuendelea baada ya kuliona gari alilokuwemo mama mchepuko likija eneo hilo na kuwapita bila kusimamishwa hali iliyopelekea wao kwa wao kuanza kurumbana.

Saa tatu kamili za usiku gari aina ya Suzuki ilionekana ikipaki mbele ya nyumba kubwa na ya kisasa geti lilifunguliwa na gari hilo liliingia. ”Pole sana." "Ahsante sana." Yalikuwa maongezi kati ya mama mchepuko na mkuu wa polisi baada ya mazungumzo hayo mama mchepuko aliondoka kuelekea kwake ilemela.
Hamis ambaye muda wote alikuwa macho kuangalia nini kitatokea katika taarifa aliyoitoa alishangazwa kuona lango likifunguliwa na mama mchepuko aliingia na kuufanya moyo wake ukudunda sana . "Honey vipi mbona umepoa sana?" Aliuliza mama mchepuko baada ya kuona mabadiliko makubwa kwa Hamis. "Niko sawa tu,"alijibu na kuondoka huku kichwa chake kisokotwa na mawazo lukuki .
"Huyu mwanamke hatari kawakwepaje polis kesho naenda kwa miguu yangu hii polisi ala!" Hamis alizidi kukiwazisha kichwa chake usiku huo akiwa ndani ya shuka.

******
"Nakushukuru sana Rhoda nipe siku mbili nitakuja kukuona tena," alisema Rodrick huku akikusanya kusanya vitu vyake kisha aliagana na bwana Hashimu na kuondoka.
Baada ya kutoka hapo Rodrick alielekea kwake Buswelu maana kichwa chake kilikuwa kimebondolewa na mawazo juu ya Rhoda .
"Itabidi niende mpaka Zanzibar kumtafuta Andrew na nikirudi nitaelekea polisi kutafuta ile kesi yake aaaah! Nimesahau kuuliza tarehe ya kesi yake ya mwanzo!" Kwakuwa alikuwa na namba ya mkuu wa gereza hakusumbuka mara moja aliitafuta. "Niambie mwanangu." "Mzee hivi tarehe ya hukumu ya yule binti ilikuwa lini?" "Aaaah! Nipe dakika tano nikaangalie kwenye faili lake!" Simu ilikatwa baada ya dakika tano Rodrick alikuwa ameshapewa jibu.
****
Ilikuwa ni jumatano tulivu sana katika uwanja wa ndege wa mkoa wa mwanza watu mbalimbali walikuwa wakitembea huku na huko na wengine wakiingia ndani ya uwanja huo kwa lengo la kusafiri ama kupokea wapendwa wao miongoni mwa watu hao alikuwemo Rodrick aliyekuwa akisafiri kuelekea dar na kisha Zanzibar . Kwa mwendo wa taratibu aliingia sehemu la kukaguliwa na kufuata utaratibu kisha aliingia ndani ya ndege na kukaa katika siti iliyokuwa haina mtu . "Habari yako ndugu !" Sauti ya kusalimia ndiyo iliyovuruga mawazo yaliyokuwa yakijirudia rudia juu ya Rhoda ndani ya kichwa chake. "Naamu mkuuu habari zako?" "Nzuri !" Alijibu mtu huyo huku akikaa katika siti moja na Rodrick "Sijui ndugu unaelekea wapi?" " Zanzibar ila nitaishia kwanza dar na kesho yake asubuhi nitaondoka." "Okay unafanya kazi huko?" "Mimi naitwa Rodrick sijui mwenzangu nani?" baada ya Rodrick kujibu swali aliingiza utambulisho. "Naitwa Marick." "Okay nashukru kukufahamu Marick.
"Naelekea dar es salaam kufatilia kesi ya mtoto mmoja hivi niliyekuwaga nimedhamiria kumsaidia ila nilijikuta nikipata matatizo miaka kama miwili iliyopita." Ilibidi Dr marick amsimulie Rodrick kisa chote ambacho kilimuumiza sana Rodrick . "Huyo binti kwani amefungwa wapi?" "Nasikia Butimba japo sijawahi kwenda kuonana naye." "Okay sawa namie naelekea Zanzibar kuonana na mtu ..........!" kabla hajamalizia sentesi yake alikatishwa na sauti ya muhudumu wa ndege.
"Abiria tunawaomba mfunge mikanda na muwe watulivu ndege imepoteza uelekeo hivyo kuweni wavumilivu sana tuna wasiliana na watu wa misaada maana hapa tupo sehemu mbaya sana!" Sauti hiyo ilimchanganya kila mtu ndani ya ndege hiyo . Dakika tatu ndege hiyo ilianza kushuka kwa kasi kuelekea usawa wa bahari ya Hindi kukiwa hakuna matumaini kwa rubani kuiongoza tena.


Baada ya Rhoda kumpatia habari yote mwanasheria Rodrick ambaye amejitolea kumsaidia Rhoda kwa hali na mali , na baada ya kutoka gerezani hakutaka kupoteza muda anapanga safari ya kwenda Zanzibar kumtafuta Andrew kijana alieshuhudia mauaji ya Rhodina lakini akiwa angani uelekeo wa uwanja wa ndenge wa mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndege inapoteza uelekeo kutokana na sababu ambazo hazikufahamika kwa haraka na kuifanya ndege hiyo kuanza kushuka kwa kuelekea usawa wa bahari ya Hindi hali iliyopelekea kila mtu ndani ya ndenge hiyo kushikilia moyo wake . Mama chepuko bado hakamatiki kutokana na ulizi aliojiwekea kupitia vyombo vya dola ambavyo vinamshikilia kila sehemu na kufanya aendelee kuingiza bangi na watoto wadogo Kwa lengo la kuwafanyisha biashara ya ngono Je nini kitaendelea ?.

SONGA NAYO.

"Maweee!" Ilisikika sauti hiyo kutoka kiti cha nyuma kabisa ndani ya ndege tena kwa sauti kubwa na kuwafanya karibia abiria wote kugeuka nyuma huku hofu mioyoni mwao zikipungua na hata baadhi yao walianza kumcheka mwanamke huyo aliyekuwa akilalamika kuyapoteza maisha yake siku ya kwanza kupanda ndege. Kutokana na maneno hayo hata rubani ndani ya ndege hiyo aliyekuwa alifahamika kwa jina la Japhet alijikuta akipata ujasiri wa ajabu sana , japo mwanzo alikuwa amekata tamaa na kuiruhusu ndege hiyo kushuka baharini. Alijaribu kuiongoza kukata kona kabla ya kuirudisha juu huku huruma ikimuingia kutokana na maneno ya mama huyo.
"Maweee leo ndo nimepanda ndege chonkaaaa naenda kufaaa kwaheri mwanangu koku , mganyizi na nyakato!" Mama huyo wa kihaya aliendelea kupayuka maneno hayo yaliyoifikia vyema ngoma ya masikio ya Rubani Japhet. "Noooo ! Acha niwaokoe ,mungu nisaidie!" Alijikuta akiwanza maneno hayo huku ajijaribu kuokoa maisha ya watu hao japo kona ilikuwa kali sana na ya kushtukiza hali iliyoipelekea ndege kuyuba sana kabla ya kutulia na kuifuata barabara yake ya kawaida.

"Mungu ni mwema sana tumeokoka kufa .....!" Sauti nyororo ya msichana ilisikika ikitoka katika kipaza sauti ndani ya ndege hiyo ndiyo iliyowashitua abiria wengi waliokuwa wamenogewa na vituko vya mama wa kihaya na kutega vyema pina zao ili kunasa mawimbi ya sauti kutoka katika kipaza sauti hivyo.
"Sababu za ndege kupoteza mwelekeo ni kukatika mawasiliano kati yetu na idara ya anga Dar es salaam kutokana na mvua kubwa iliyoukumba mji huo muda mchache na hadi sasa bado hali ni mbaya kwa jiji hilo hivyo tutaenda kutua kiwanja cha ndege Kia ahsanteni sana kwa uvumilivu wenu." Sauti hiyo ilikatika lakini ikiwa na ujumbe wa kufurahisha kwa abiria wote.
Siku hiyo kila mtu alimuomba mungu na wale ambao huwa hawamjui mungu nao waliabudu kwa muda . "Ahsanteni sana kwa kuchangua shirika letu la ndege na karibuni tena,".taarifa hiyo iliashiria kuwa ndege hiyo ilikuwa imetua katika uwanja wa kilimajaro abiria wote walianza kutoka huku wakiwa hawaamini kama kweli walikuwa wamepona.
"Mimi ikiwezekana kwa leo hii nitaondoka na basi." "Hapana Rodrick kuna jamaa zangu huwa wanahelkopita ambayo inafanya safari za huku mpaka dar es salaam wacha niongee nao tuone," yalikuwa ni maongezi kati ya Dokta Marick na Rodrick wakitoka ndani ya uwanja huo na kuzifuata tax zilizokuwa maeneo hayo.
“Heee! Tuna dakika kumi na tano tu za kuwa hapa na siti zipo mbili tu kama mtaweza wahini," ulisika upande wa pili wa simu ya Marick. "Oky tunakuja mida hii hii" Dokta marick aliongea huku akifungua mlango wa tax iliyokuwa eneo hiyo. "Wakubwa wapi ?" "Flights air claft fasta" "Buku kumi tu!" "Dogo acha kahawa twende !" Marick aliamru na gari hiyo ilitoka kwa kasi kuelekea huko. .Kwakuwa hakukuwa mbali walitumia dakika saba tu walikuwa eneo hilo walimlipa dereva tax huyo na kuielekea helkopita iliyokuwa teyari ikizungusha mapanga yake. "Poleni sana!" "Ahsante!" Wote walijibu huku wakikaa katika siti na dakika tatu helkopita hiyo ilianza kuyakata mawingu.

"Tunashukru sana kwa msaada wenu!" Marick alitoa shukurani hiyo baada ya kuikanyanga aridhi ya Dar es salaam huku mvua ilikuwa ikiendelea kuiadhibu aridhi ya mji huo. "Nashukru sana Dokta Marick!" "Usijali Rodrick," wote waliagana na kila mmoja kuelekea alikokuwa akikujua.

"Hivi kweli muda huu naweza nikaenda Zanzibar?" "Eeeeh! Kuna Azam Mv inayoondoka saa kumi na sasa ni saa nane na nusu." "Okay! Nipeleke basi." Aliongea na dereva tax aliyemchukua uwanja wa ndege wa mwalimu nyerere. Japo alikuwa amechoka sana hakutaka kupoteza muda roho ya huruma dhidi ya Rodha ilikuwa ikimsumbua sana . akiwa ndani ya meli hiyo ndipo alipotafuta chakula kisha alipitiwa na usingizi kilichokuja kumshtua ni kelele za forodhani baada ya meli kutia nanga.mishale ya saa mbili usiku.
Kwakuwa hakuwa na mizigo zaidi ya kibegi kidogo tu kilichokuwa na nguo chache alitoka na kuziendea tax zilizokuwa zikifanya kazi hapo. "Nipeleke hotel yeyote ile ambayo ni nzuri." "Pouwaaa!" Alijibu kijana huyo kwa lugha ya kihuni huku akitia ufunguo wa gari kabla ya kuliwasha. “Eeeeeh!,Andrew nipo Zanzibar tuonane kama itawezekana?" "Aaaah! " "Tafadhali nakuomba nitakulipa kiasi chochote cha pesa na isitoshe mimi mgeni hapa!" Maongezi hayo yalipenya vyema masikioni mwa dereva tax na kumfanya aingiwe na tamaa ya pesa "Acha nimpeleke kitaa chetu kwanza " aliwaza kijana huyo huku akiandika ujumbe mfupi katika simu yake na kuwatumia vijana wenzake bila Rodrick kujua chochote.

******
Usiku mzima Hamis hakupata usingizi kutokana na mzingo wa mawazo juu ya mama mchepuko. "Sina ushahidi kwa sasa maana hata mabinti keshawatoa aaaah! Au nikashitaki kesi ya mauaji ya Rhodina!" Aliendelea kuwaza kisha aliiruhusu miguu yake kumpeleka sebuleni lakini kabla hajafika vizuri sebuleni alista kidogo baada ya kusikia jina lake likitajwa katka maongezi kati ya mama mchepuko na mtu mwingine kupitia simu . Alihisi miguu ikishindwa kusimama kutokana na maongezi hayo.


"Yaaani hata usijali mkuu huyu huyu ndiye nitayemtumia kuingiza huo mzigo." "Kweli?" "Hana faida kwangu huyu wanaume mimi siangalii mtu ninachoangalia mimi pesa tu afande je hiyo itakuwa lini ili nianze mpango wa kumleta na madawa yanapesa sana daaaa!" Mazungumzo hayo yote aliyasikia vizuri Hamis ila alijikaza vizuri na kutokeza sebuleni.
"Vipi mbona asubuhi sana wapi mwenzangu?" "Naelekea hapo nitarudi baadae ," Hamis alijibu huku akifungua mlango na kutoka nje kulielekea geti. "Tutamchoma dawa ya usingizi na kumpakilia madawa tumboni kisha tunamsafirisha hadi ...." maneno hayo yalizidi kukichanganya kichwa cha Hamis kila alipopiga hatua kuelekea asikokujua. "Sijui niende polisi ila sina ushahidi na wamesema siku tatu mbele wananikamata daaaah! Sikumjua mtu huyu lakini nitapambana nao tu," Hamis alizidi kutawaliwa na lundo la mawazo na kuzidi kuchanganyikiwa sana hadi inaingia mchana alikuwa bado hajielewi hivyo alidhamiria kurejea nyumbani.
"Ndiyo afande huu mzigo nitautunza vizuri sana." "Haya mimi naondoka," Hamis aliyekuwa amejibanza dirishani aliyasikia vyema maongezi kati ya mama mchepuko na mkuu wa polisi mkoa wa mwanza hadi kitendo cha wao kukabidhiana mzingo. "Yes kesho polisi hahaha!" Alicheka na kuingia ndani kupitia mlango wa nyuma.
******
"Huyu jamaa mbona ananiangalia sana?" aliwaza Rodrick baada ya kushtukia mchezo wa dereva tax huyo kupitia kitendo chake cha kumtazama kila wakati kupitia kioo cha ndani. "Bro hebu simama kidogo!" "Aaaaah! Hii sio sehemu salama bhana," alijibu dereva huyo huku akiongeza mwendo wa gari kitendo hicho kilimfumbua macho Rodrick na kuzisoma alama za nyakati. "Mungu wangu! Huyu ni kibaka mmmmh! Mungu utanisamehe kama itatokea nimeua!" Rodrick aliwaza hayo huku akipeleka mkono wake katika kiuno chake ambako palikuwa na bastola.
"Kwa usalama wako tu simamisha gari haraka sana!" Aliamuru huku mdono wa bastola ukiwa umekilenga kisogo chake hali iliyopelekea kiwewe cha hali ya juu kwa dereva huyo. "Oky..ok...mkuuu nasimamishaaaa!" Aliyatoa maneno hayo huku akitetemeka sana . "Ulikuwa unata......!" "Triiiii! Triiiiii! Triiiii!" Mlio wa simu ya Rodrick ndio uliochangia kukatisha sentensi yake , haraka haraka aliitoa mfukoni na kuipikea bila kuangalia mpigaji.
"Nani?" "Andrew uko wapi?" Upande wa pili wa simu ulijibu na kumfanya Rodrick kuchanganyikiwa sana kutokana na hali iliyokuwa ikimkabili pili ugeni wa mji ule. "Sikia shika simu hii mwelekeze wapi tulipo mpuuzi sana!" Bila hiyana kijana yule aliongea na Andrew na kisha Rodrick alimuaru ampeleke eneo alilokuepo Andrew .kisha walimuacha aende zake.
"Naitwa Rodrick natokea mwanza!" Rodrick alianza utambulisho baada ya kuona hali ya msituko kwa Andrew wakiwa ndani ya tax kuelekea Viviana hoteli. "Ndiyo yule nilikuwa naongeaga naye toka mwanzo ?" "Eeeeh! Ni mimi." "Mmmmmh!" "Usiwaze sana mimi ni mtu salama kabisa."
Hakuna alieongea hadi walipofika hotelini hapo .Walishuka na kuchukua chumba.
"Najua hunifahamu ila naitwa Rodrick Steven nimwanasheria anayeshughulikia kesi ya marehemu Rhodina alieuawa tarehe 25-12-2000 majira ya saa tisa ama kumi na mwanamke mmoja anaefahamika kwa jina la Regina ama mama mcheouko, hiv.....!". Rodrick hakumalizia sentesi yake alikatishwa.
"kwahiyo mimi nikusaidieje!" Andrew aliyekuwa amekaa juu ya kochi chumbani mle aliongea huku akinyanyuka na kuanza kutembea tembea kwa dharau. "Kaka msaada wako ni kuisaidia mahakama ushahidi utakaomuweka Rodha huru!" "Kiaje labda?" Safari hii aliuliza huku akiwa ameinamia kochi kwa nyuma. "Rhoda amefungwa kifungo cha maisha Butimba hivyo nakuomba ukamuokoe tafadhali , kwakuwa ulishuhudia kwa macho yako mtu aliyehusika katika mauaji ya binti Rhodina!"
Rodrick aliongea kwa upole zaidi ili tu Andrew amuonee huruma ,. Kwa mkono wake wa kulia alitandaza kiganja na kuufuta uso wake. "Huyu hapa mtumie." "Aaaah! Hata hamu sina tena niliyekuwa namtaka umemuua!..Mamaaaa.. mamaaa umemuaaa Rhodina! Na pesa sihitaji sihitaji."
Ilikuwa ni kumbukumbu katika kichwa cha Andrew siku ya tukio miaka kadhaa iliyokuwa imepita picha ya Rhodina akiwa amekufa ilianza kukisumbua kichwa chake achilia mbali kilio cha Rhoda baada ya kusikia kifo cha dada yake.
"Rhodrick!" Andrew aliita huku akikaa kwenye kochi uso wake ukijawa na huruma. "Nipo radhi kushirikiana nawe !" Jibu hilo halikueleweka mara moja kwa Rodrick hali iliyopelekea kuuliza mara mbili mbili.
"Nitamtetea Rhoda ila naomba usalama wangu kwa mama mchepuko." "Nakuhakikishia utakuwa salama na tukifika tu mwanza kitu cha kwanza ni kwenda polisi kufungua kesi upya na kupewa kibali cha kumkamatia basi tunasubili kesi!" "Hapo sawa."
Waliongea mengi kisha Andrew aliagana na Rodrick wakiwa na miadi ya kukutana kesho yake uwanja wa ndege kwa safari ya kurejea mwanza tena .
Usiku mzima Rodrick hakupata usingizi kutokana na furaha ya ushindi uliokuwa mbele yao. "Abiria wote mnaosafiri kuelekea Dar es salam kwa leo hakutakuwa na ndege ya kwenda huko kutokana na mvua kubwa zinzoendelea kunyesha," lilikuwa ni tangazo lililowakaribisha akina Rodrick na Andrew uwanjani hapo. "Sisi hayatuhusu hayo!" Walifuata taratibu zote kisha waliingia ndani ya ndege wakisubili safari yao iliyokuwa na furaha sana.
"Triii! Triii!," ulikuwa ni mlio wa simu ya Rodrick ambao hata yeye ulimshtua kwani hakujua kama hakuizima alipoingia ndani ya ndege haraka haraka aliipokea. "Rodrick upo wapi hali ya Rhoda ni mbaya sana....tiii.. tiii" simu ilikatika na alipopiga haikupatikana tena .
"Vipi?" "Mkuu wa Gereza amenipa habari mbaya kuhusu Rhoda " wote waliishiwa nguvu na wakawa na hamu ya kufika mwanza mara moja.



Gari la mkuu wa Gereza la Butimba aina ya Nisan ilionekana ikitoka ndani ya Gereza la Butimba huku nyuma kukiwa na mtu aliyekuwa amefunikwa gubi gubi kuanzia kichwani hadi miguuni , dalili za wazi wazi zilionyesha mtu huyo alikuwa amekufa au alikuwa katika hali mbaya sana.

"Hata sielewi maana Rodrick hapatikani tena nimempigia amekata simu!"
"Duuuh! Sasa tufanyeje?"
"Acha tumpeleke hospitali kwanza," yalikuw maongezi kati ya Hashimu ambaye ni mkuu na msaidizi wake .wakiwa ndani ya gari hilo kwakuwa Butimba magereza na Hospitali ya jeshi la Butimba haikuwa mbali walijikuta wakitumia dakika tano tu.

Hata kabla gari hilo halijasimama tayari manesi wawili walikuwa wakivuta kitanda cha matairi manne alimarufu kama kachela kwa ajili ya mgonjwa huyo.
"Anavuja damu puani," nesi mmoja aliongea kwa sauti ya chini.
"Shoga isijekuwa Ebo..!"
"Mmmh!" Japo walikuwa wakiongea tayari walijikuta wakiwa ndani ya chumba cha daktari.
"Nani jina na umri?"
" Rhoda Jackson miaka 20 na ni mfungwa," mkuu wa Gereza alijibu huku akiwa na wasiwasi juu ya afya ya Rhoda.
"Alianza lini?"
"Dokta mtibu kwanza hayo nitakueleza baadae!"
"Oky nipe nafasi ya kufanya kazi yangu," mzee Hashimu hakuwa na hiyana alinyanyuka na kuanza kutoka nje lakini kabla hajafika nje simu yake iliita.

"Mkuu yule mgonjwa toka kagera amefariki na kuna wafungwa wengine watano hali zao mbaya sana!" Simu ilikatwa.
"Mungu wangu nini tena!" Mzee Hashim aliishiwa nguvu hata ile supu aliyokuwa ametoka kunywa ilikauka tumboni mwake taratibu alikaa katika benchi lilokuwa eneo hilo.
"Mzee" sauti toka chumba cha daktari ilisikika katika ngoma za masikio yake baada ya dakika arobaini na tano.
"Mzee !" alianza kuongea daktari baada ya mzee Hashim kuingia chumbani humo.
"Mgonjwa wako anadalili ya maabukizo ya ungonjwa wa Ebola!"
"Mmmmh!"
Mkuu wa Gereza aliishia kuguna tu maana hata yeye alikuwa akihisi hilo.
"Kuna maswali ya kunijibu je kuna mtu yeyote aliyekuwa akidhaniwa kuwa na virusi hivyo hapo gerezani?"
Swali hilo lilimfanya mzee huyo kukikuna kichwa chake kilichokuwa na nusu nywele kutokana na upala , kumbukumbu ya haraka ilirejea siku tatu nyuma.

"Mimi naumwa kichwa sana na hata mwili wote unauma achilia mbali homa!" ilikuwa taarifa kutoka kwa mfungwa mmoja aliyekuwa ametolewa kagera na ni huyo huyo ndiye aliyekuwa amefariki muda mfupi uliopita .
"Ndiyo."Akajibu kwa kujiamini kabisa moyo wake ukizidisha wasiwasi sana.
"Sasa sisi hapa hatuna tiba ila tayari ameshapata huduma ya kwanza na tunalazimika kumpeleka Bugando na tayari nimeshatoa taarifa hizo wew rudi gerezani ukatoe taarifa hizo na utambatana na daktari atakaeenda kutoa maelezo ya ugonjwa huu."
Japo alikuwa akiongea maneno hayo lakini naye alikwa ametandwa na woga dhidi ya gonjwa hilo.
"Jamani tumewaiteni hapa kuna tatizo kubwa sana liloikumba kambi yetu hii ya gereza !" Mkuu wa gereza bwana Hashim alianza kuongea baada ya wafungwa wote kukaa na kutulia.
"Hapa Gerezani kumetokea na ugonjwa hatari sana wa Ebola ambao ndio uliosababisha kifo cha Debora na maambukizo mengine kwa wafungwa sita wa kike ," aliendelea.
"Hapa mbele yenu kuna daktari ambaye atatuelezeni maana ya ugonjwa huu na dalili zake
huyu hapa!" Alimaliza kuongea na kumpa nafasi daktari
"Ugonjwa wa Ebola ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi kinachoitwa ebola," alianza kutoa darasa linalohusiana na ugonjwa huo mara baada ya kuwasalimia kisha aliendelea.

"Kirusi hiki kinapatikana kwa wanyama waishio polini hasa hasa maeneo ya joto hususani nchi za Afrika mfano wa wanyama hao ni sokwe popo na n.k.
Kuna aina tano za Ebola ambazo majina yake yanatokana na eneo na mazingira mfano hapa gerezani kunakirusi kinachoitwa Bundibugyo kutoka nchini Uganda hicho ndicho kilichosababisha kifo cha Deborah,ugonjwa wa Ebola una ambukizwa kwa :
Kugusa damu na majimaji kutoka mwilini mwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa huo.
Kugusa maiti ama mwili wa mtu aliyekufa na ugonjwa huo .
Dalili zake.
Homa Kali ya ghafla " alipotaja dalili hiyo wafungwa walianza kujikagua kagua Kwa kujigusa miili yao.
aliendelea
"- kulegea mwili.
Maumivu ya misuli.
Muumwa kichwa hizi ni dalili za mwanzo kabisa na nyingine ni vidonda kooni , damu kutoka sehemu zenye matundu kama puani , mdomini , sehemu za siri kwa wanawake , sehemu ya haja kubwa , machoni na n.k. Hii husababishwa na kupasuka kwa misuli mwilini.
Tiba , Ebola haijapatiwa tiba yeyote hadi sasa ila huwa kunachanjo ambayo humsaidia mgonjwa kwa asilimia kubwa sana.
"Pia daktari huyo aliwafahamisha wafungwa jinsi ya kujikinga na ugonjwa huo . Baada ya somo hilo daktari aliondoka na kuwaacha wafungwa wakiwa na elimu ya kutosha dhidi ya ugonjwa huo .
Mkuu wa gereza aliamru amri itolewe kwa watu kutotembelea hapo .
"Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kuhusiana na ugonjwa wa Ebola uliotokea katka mji wa mwanza , inasemekana tayari mfungwa mmoja amepoteza maisha yake kutokana na ugonjwa huo na zaidi ya wafungwa watatu wanashukiwa kupata maambukizo hayo , pia imetolewa amri ya wakazi wa mwanza kutotembelea gerezani hapo , endelea kusikiliza radio free Afrika kwa habari zaidi," ilikuwa ni taarifa za kushtua sana katika masikio ya Rodrick aliyekuwa ndani ya tax akiwa na Andrew wakitoka airpot kuelekea mjini . haraka haraka alichukua simu na kumpigia mkuu wa gereza la Butimba.

"Shikamo mzee," alisamia baada ya simu kupokelewa.
"Rodrick ulienda wapi?"
"Eti kunani ni tena ?"
"Njoo kwanza Bugando hataka sana." Mzee hashim alikata simu na kumfanya Rodrick kuchanganyikiwa zaidi.
"Vipi Rhoda amekufa?"
"Andrew sijui dereva tupeleke Bugando hospitali" Rodrick hakuongea tena hadi tax hiyo iliposimama nje ya hospitali ya Bugando bila kuongea chochote alimlipa dereva tax na kushuka kisha kuliendea geti la hospitali hiyo huku mapigo ya moyo yakiongezeka.
"Rodrick," sauti ya mzee Hashimu ndiyo iliyoizuia miguu yake na ya Andrew kupiga hatua wote walisimama kisha mzee Hashim aliwafuata ila Rodrick alipomtazama vizuri aligundua kuwa alikuwa akilia hali iliyozidi kumstua zaidi.
"Rhoda yuko wapi ?" Aliuliza lakini swali kwa Mzee huyo ambaye hakulijibu zaidi ya kumtazama Tu.

"Mzee Rhoda yuko wapi?"Rodrick aliuliza tena swali hilo huku mapigo ya moyo wake yalizidi kuongezeka , miguu nayo ilishindwa kusimama vizuri kutokana na wasiwasi aliokuwa nao kuhusu Rhoda .
"Nifuate !" Mzee Hashim aliongea huku akiondoka eneo hilo na kutoka kabisa ndani ya hospitali hiyo.
"Je unafahamu nini kilichotokea hapa mwanza na kwanini Rodrick uliondoka bila kuangana na Rhoda?" Aliuliza mzee Hashimu mara baada ya kukaa katika moja ya sehemu ya watu waliokuwa wakipumzikia kabla ya kuruhusiwa kuingia ndani ya hospitali eneo hilo hilo la hospitali.
"Usiniambie kuwa Rhoda amekufa!"
Aliuliza Rodrick huku akiwa ameyatoa macho yake mithili ya mjuzi aliebanwa nyuma ya mlango
"Noo! Rhoda yupo ila yuko katika hali mbaya sana."
"Tatizo nini?"
"Ebola!"
"Mungu wangu!" Ilibidi mzee Hashim amuelezee habari yote inayohusiana na ugonjwa huo .
" Mimi nilienda Zanzibar kumfatilia mtu ambaye aliyaona mauaji ya Rhodina na ndo huyu hapa.”
"Karibu sana kijana."
"Ahsante…. je tunaweza kwenda kuonana naye?" Andrew aliongea huku akiwa ameshasimama tayari kwa safari ya kuelekea alikokuwa Rhoda.
"Kwanza poleni sana !" Dokta Moses aliongea baada ya wote kuingia ndani ya ofisi yake.
"Yanini inamaana Rhoda amekufa ???"
" Kijana tulia yupo hai!"
"Aaaah! Nipeleke kwanza nikamuone ndiyo hapo nitaamini?" Rodrick hakutaka kuridhishwa na maneno matupu alitaka yaendane na vitendo hali ambayo Dokta Moses hakupendezwa nayo na aliona ni karaha sana na ili kuitoa karaha hiyo aliamua kukubaliana na ombi la Rodrick.

"Sasa inatakiwa aende mmoja mmoja na lazima tukupatie mavazi maarumu."
"Haina shida Dokta!". Haraka haraka Dokta Moses aliwaletea mavazi na kutoa darasa dogo kuhusiana na ugonjwa huo ambao ukiupuzia tu lazima ukupitie .
"Haya twendeni !" Wote watatu waliongozana hadi eneo ambalo Rodha alikuwa ametengewa ambalo halikuruhusiwa mtu yeyote yule kufika kule bila kuwa na kibari.
"Hakikisha hukosei chochote sawa?" Moses alizidi kumsistiza Rodrick aliyekuwa wa kwanza kuingia humo.

Taratibu mlango ulifunguliwa na Rodrick alianza kupiga hatua kuelekea katika kitanda cha Rhoda aliyekuwa hajielewi kwa chochote kutokana na kupoteza fahamu kadri alivyozidi kupiga hatua kukielekea kitanda hicho ndivyo mwili wake ulivyozidi kupata hofu sana .
"Rhoda mpendwa amka sasa!"Ndilo neno la kwanza kabisa alilolitamka polepole baada ya kukifikia kitanda cha Rhoda.
"Mungu wangu anaongea!" Dokta Moses aliongea baada ya kuiona midomo ya Rodrick ikicheza cheza kupitia vioo vilivyokuwa vimewekwa kwa ajili ya baadhi ya watu kumuona mgonjwa wao. .
"Mungu usimchukue Rhoda , epusha roho wa mauti , epusha baba katika jina la mwanao yesu kristo najua baba wewe ndo mwenye mamlaka na mtu huyu ukipanga hakuna wa kupangua , ukisema afe na kweli atakufa ila baba naomba umpatie nafasi nyingine ya kuishi tena mtazame baba toka mtoto anapitia mateso ya kila namna baba niwakati wake sasa kuwa huru naomba baba utende kuanzia sasa akapokee uponaji katika jina la yesu kristo Amina " ilikuwa ni sala fupi kutoka kwa Rodrick akiwa amesimama karibu kabisa na kitanda alichokuwa amelazwa Rhoda.
"Nitakupigania ili haki yako ionekane hata kama utakufa!" Alitamka hayo kwa uchungu sana huku akipiga hatua za kutoka nje."
Baada ya siku tatu tangu Rhoda alazwa hali yake ilikuwa bado haijategemaa japo damu zilikuwa hazivuji tena , mashine za kupumlia nazo alikuwa ametolewa ila fahamu zilikuwa hazijamrejea.
Siku hiyo ya tatu ambayo ilikuwa jumapili Rodrick alidamka mapema sana na safari yake ilikuwa bugando , alifika na kupitiliza moja kwa moja katika eneo alilokuepo Rhoda bila mtu yeyote kumuona ama kufahamu na kuingia ndani ya chumba hicho bila hata kuwa na vifaa vya kuepusha maambukizi endapo lolote lingetokea.

"Rhoda!,Rhoda !"Rodrick alimuita huku akimtigisha tingisha hali iliyopelekea Rhoda kushtuka na kumtazama Rodrick kwa macho yenye kuhisi usingizi singizi Rodrick hakuamini kama kweli aliyekuwa akimtazama alishindwa kujizuia kutoa chozi la furaha lililoambatana na busu la mdomoni kisha aliinama na kumkumbatia akiwa vile vile bila kuvaa vazi la kuzuia maambukizi.

"Wewe Kijana!" Dokta Moses hakuamini kumkuta Rodrick akiwa ameukumbatia mwili wa Rhoda aliyekuwa na maambukizo ya virusi vya ebola.
"Toka njeeeeee,"Dokta moses alitoa amri hiyo huku akiwa amekasirika sana bila hiyana Rodrick alitoka na kumuacha Rhoda akiwa anamsindikiza kwa tabasamu changa.
"Wewe boligo ulikuwa wapi mpaka mtu anadiriki kuingia ndani ya chumba hicho?”
"No...miss..nisamehee ....nilikuwa nipo!"
"Upooo? Wapi na ole wako mtu huyu awe amepata madhara utajileza vizuri!" Dokta Moses alimfokea mlizi na kuondoka kuelekea usawa aliokuwepo Rodrick.
"Kijana mbona hivyo unachezea maisha yako?'
"Hapana Dokta ilinibidi nimsalimie tu ila usijali nipo salama tu ,waliagana kisha Rodrick alirejea nyumbani kwake alikokuwa akiishi na Andrew kwa kipindi hicho.
"Vipi hajambo?"
"Daaah! Leo anaendelea vizuri sana kesho nitakwenda polisi kufungua kesi na ikiwezekana tunaenda kumkamata mama mchep......" hata hakumalizia sentesi yake alihisi mwili wote ukiishiwa nguvu kichwa kilianza kumgonga sana hali iliyopelekea kukaa juu ya kochi maana alikuwa amesimama toka alipoikanyanga sebule hiyo huku akiwa ameinamisha kichwa.
"Vipi bro?"
"Aaaah! Kichwa kinauma sana," japo alikuwa ameinama lakini hiyo haikumnyima nafasi Andrew kuona michirizi ya damu iliyokuwa ikianza kutoka puani hali iliyomshitua Andrew
"Rodrick nini hicho?"
"Kipi?"Akauliza huku akiishanga damu iliyokuwa ikichuruzika na kudondokea juu ya kochi alilokuwa amelikalia.


Taratibu Andrew alinyanyuka katika moja ya sofa pale sebuleni na kuanza kumsogelea Rodrick ila kabla hajamfikia alikumbuka kitu.
"Ugonjwa wa ebola ni hatari sana maana maambukizi yake ni ya haraka sana na moja ya dalili kubwa na ya haraka sana ni kutokwa na damu sehemu zilizo wazi kama vile puani na hii inasababishwa na mishipa ya damu kupasuka , hivyo ukimuona mtu wa namna hiyo hutakiwi kumsogelea kabisa la sivyo nawe utaambukizwa!" Ilikuwa ni kumbukumbu siku tatu nyuma iliyokuwa ikitolewa na dokta Moses.
"Uuuuuuuh!" Aliishia kushusha punzi ndefu iliyoashilia kuchoka akili yake.

"Naondoka wacha niende zanzibar bara hakunifai tena mie!" Mawazo hayo yaliambatana na kitendo cha kuelekea chumbani kwake kukusanya kila kitu chake na kuanza kutoka lakini alipofika sebuleni roho ya huruma ilianza kumshawishi baada ya kumuona Rodrick akiendelea kugugumia kwa maumivu.
"Na..naakuombaaa usiniache....baado...unasa...fari....ya ...kumuokoaaaa.....Rhoda...., na...tambuaaa....kila nafsi....itaonja...mauti hivyo usiogope kufa .....hakuna atakaye baki ....na ukifa unatoaaa msaada .....wewe ni shujaaaa.......nakuomba unipeleke hospitali sasa hivi nikaaagane na Rhoda, najua tayari nina Ebola ila sijutii hata kidogo......, nilijitahidi kwa uwezo wangu ku...kum......"Rodrick hakumalizia sentesi yake alizimia hali iliyozidi kumchanganya zaidi Andrew.

"Aaah! Hapana sifi kijinga!" Alichukua begi lake na kuondoka sebuleni hapo akiwa anakimbia kama mwizi.
"Boda! Bodaaa nipeleke airpot fasta bei gani?"
"Elfu hamisini tu!"
"Aaaah! Poa twende," Andrew alikaa kwenye boda boda na safari ikaanza lakini dakika tatu alikumbuka kitu alichokiacha nyumbani kwa Rodrick.

"Kila nafsi itaonja mauti hata kama sio kwa ebola ....tambua una kazi mbele…" Kichwa chake kiliyakumbuka maneno ya Rodrick.
"Hebu geuza nimesahau kitu nyumbani!"
"Kweli?" Japo boda boda aliguna lakini aliigeuza boda na kurudi.
"Shika hii nenda!"
"We vipi?"
"Nenda bhana." Andrew aliongea huku akisukuma geti na kuingia ndani
"Mungu wangu !" Alihamaki baada ya kumkuta Rodrick akiwa bado anavuja damu tena ilikiwa imeongezeka .
"Halooo mzeee Hashim kunatatizo!”
"Lipi?" Ilibidi Andrew aelezee kila kitu huku akiwa anatetemeka mwili wote .
"Nakuja sasa hivi nilikuwa Bugando !"
"Uje na ambulance kabisa Rodrick ,..."
"Kafanya nini?”
"Wewe njoooo !"
"Sawa nipe dakika kumi !" alikata simu na kutoa habari katika eneo husika kisha gari lilitolewa na safari ya kuelekea buswelu ikaanza kwakuwa gari hizo huwa hazina kizuizi chochote ilijikuta ikifika buswelu ndani ya dakika kumi na tano tu na hiyo ilichangiwa na ubovu wa barabara kutoka nyakato national hadi buswelu la sivyo isingetumia dakika hizo.
"Ilikuwaje?"
"Dokta mimi amefika hapa akawa .....!"
"Oky kumbe Rodrick dokta Moses alishangaa kisha aliwaeleza kile kilichotokea muda mchache baadae uliokuwa umepita kisha alianza kumpatia huduma ya kwanza haraka haraka kisha safari ya kuelekea bugando kwa ajili ya matibabu .
"Hatuna haja ya kujiuliza nini tatizo lake."
"Lakini mgempima kwanza !"
"Haina haja huyu ana ebola dalili zote zipo wazi!" Alisema Dk.Moses na mzee Hashim kisha alianza kuandaa dawa za kudhibiti maabukizi zaidi.
"Triii! Triiii! Triii!" Ilikuwa ni simu ya Rodrick ikiita
"Mzee baba yake anapiga."
"Lete niipokee !"
"Naomba niongee na mwenye simu."
"Mzee mwenzangu kuna tatizo." Ilibidi mzee Hashim atoe maelezo kuntu ambayo yangekuwa sahihi ndani ya masikio ya mzee Steven .
"Nakuja na ndege ya saa kumi!"Baada ya kutoa taarifa hiyo alielekea muhimbili kuonana na dokta Harun ambaye alikuwa amesomea magonjwa hayo.
"Kweli anaumwa?"
"Ndio na hata juzi nilisikia taarifa hiyo ya kuibuka gonjwa hilo ndani ya mkoa wa mwanza hivyo naomba twende na ikiwezekana tumlete huku!"
"Hakuna shida maadam leo jumapili nitafanya hayo." Baada ya maongezi hayo mzee Steven alirejea nyumbani kwake huku kichwa chake kikiwa kinakwanguliwa na mawazo.

"Jamani kaka yenu anaumwa na nilichoambiwa anaumwa ni ebola!" Alitoa taarifa hiyo katika familia yake hali iliyopelekea kila mtu alitoa chozi ,
"Nitaenda kumchukua aje huku!"
"Sawa baba!"
Saa kumi na nusu ndege ilikuwa ikitafuta mahali pazuri pa kutua katika kiwanja cha ndege cha mjini mwanza kilichopo ilemela.
Haraka haraka mzee Steven na doktar Harun walishuka na kutoka nje , kisha waliingia ndani ya tax iliyowapeka bugando .
"Tupo nje."
"Tunakuja!" Aliongea mzee Hashim huku akiwa anatoka nje ya hospitali hiyo mbio mbio kuwapokea wageni hao.
"Kama mlivyopewa taarifa mtoto wenu amepata maambukizi ya ugonjwa wa ebola!"
"Dokta tunaweza kuondoka nae !"
"Haina shida !"
"Je yule binti aliemuambukiza anaendeleaje !?" Mzee steven alizidi kuuliza
"Hali yake kiasi inaridhisha!" Haraka haraka taratibu zilifanyika za Rodrick kusafirishwa akiwa katika uhifadhi mkubwa sana ili naye asiambukize wengine kisha safari ya kuelekea airpot ilianza ili kuiwahi ndege ya saa kumi .na mbili jioni.
"Kijana utabaki katika nyumba ya mwenzio kwa muda." Mzee Steven alitoa maelezo hayo kwa Andrew aliyekuwa ameambatana nao kisha walimuingiza ndani ya ndege akiwa hajitabui na kugonja safari.
"Piiiiii! piiiiiiii!" Ilikuwa ni gari ya wagonjwa ilikuwa ikipiga ving' ora kutoka katika uwanja wa ndege wa Dar es salaam kuelekea muhimbili ambamo ndani ya gari hilo alikuwemo Rodrick , baba yake na dokta Harun majira ya saa mbili usiku.

Kwakuwa taarifa zilikuwa zimeshafika muhimbili Rodrick alifikishwa moja kwa moja katika chumba maarumu na vipimo vilichukuliwa ili kujiridhisha zaidi .
"My God ?( mungu wangu? )” dokta Harun alishtuka baada ya kuona majibu ya Rodrick haraka haraka alichomoa baadhi ya dripu na kumchomekea zingine kisha alitoka huku akiwa anawaza sana jinsi ya kutoa taarifa hiyo kwa ndugu zake waliokuwa wamefurika hospitali hapo.


Miguu ya Dk. Harun ilizidi kuishiwa nguvu kila alipopiga hatua kuelekea ofisini kwake.
"Dokta enaendelea mwanangu!" Ilikuwa ni nisauti ya mama yake Rodrick ambayo ilisababisha ngona za masikio yake kufunguka
"Njooni ofisini tafadhali !" Hata kabla hajamalizia sentesi yake ndugu zake wote walikuwa wameshanyanyuka na kumfuata .
"Mmmmh!" Alianza kuguna dokta kabla ya kuongea , kisha alivua koti lake jeupe la kazi na kulitundika sehemu maalum na kuketi katika kiti kilichokuwa nyuma ya meza kubwa hofisin humo .
"Tueleze baba!"
"Mama tulia mwanao atapona tu!"
Aliongea dokta Harun huku akipeleka mikono yake katika moja ya karatasi ya majibu ya Rodrick na kuwatazama mmoja baada ya mwingine.
"Ngooo! Ngoooo!" Zilikuwa kelele za kugongwa mlango katika chumba alichokuemo dokta Harun
"Pita."
Nesi aliyekuwa amevalia mavazi meupe na kikofia kidogo kichwani chini akiwa na raba nyeupe zilizosindikizwa na soksi nyeupe alisimama mbele ya dokta Harun na kumkabidhi majibu ya x- ray kisha aliondoka.
"Kwanza poleni sana kwa kuuguliwa !..... " alianza kuongea huku akisoma soma majibu yaliyotoka katika chumba cha mionzi
"Mmmmh!
"Kiufupi Rodrick hana virusi vya ebola hata kidogo kutokana na majibu niliyoyapata muda huu.” Aliongea dokta Harun kisha aliwatazama wote.

"Acha utani mzee mwenzangu! Haiwezekani mtu akawa anatoka damu puani na hizo ni dalili za wazi kabisa za ugonjwa huo , mwanza penyewe walitueleza kuwa ana ebola hapana nenda ukarudie tafadhali," aliongea mzee Steven huku akiwa amesimama.
"Steven tafadhali kaa nikueleze," dokta Harun alizungumza kwa upole sana.
"Kwanza naanza kwa kutoa lawama za asilimia elfu kumi kwa madaktari wa mwanza kwa kosa walilolifanya la kumtundikia dawa za kuzuia virusi vya ebola bila kufanya vipimo kwanza ,......!" alianza kueleza hivyo na kila mtu humo ndani alikuwa kimya.

"Nasema hayo kutokana na majibu niliyoyapata hapa , mwanenu anasubuliwa na tatizo la kupasuka mishipa ya damu chini ya koo pamoja na mishipa inayounganisha sehemu za uso na eneo la masikio ambayo inakuja kuungana na ile ya pua , hii ni mishipa midogo midogo sana na huwa haina madhara sana ila yeye ilileta madhara kiasi kutokana na kukosa usingizi kwa muda mrefu na ilionekana alikuwa na msongo wa mawazo sana."
"Hivi kweli unayosema ni kweli?"
"Ndio hata majibu ya x- ray haya hapa."
"Je hizo dripu za ebola alizokuwa ametundikiwa hazina madhara?" Aliuliza dada yake mkubwa aliyekuwa akifahamika kwa jina la Pamela.
"Mmmh hapana maana dawa zenyewe ni dripu za maji ya chumvi chumvi ambayo pia ni mazuri kwake katika kuziba mishipa iliyoachia .
"Lakini mimi sina imani na.......!" Mama yake hakumalizia sentensi yake alikatishwa na simu ya mume wake iliyokuwa ikipiga kelele.
"Baba Rodrick anaendeleaje?"
"Wewe nani?"
"Andrew kutoka mwanza yule kijana uliem..."
"Aaah ! Nimeshakukumbuka anaendelea vizuri !"
"Kweli anaebola?"
"Mwanagu hana hivi kweli walimpima huko?"
"Sijui hebu subili niongee na dokta moses maana namba zake ninazo." Alikata simu na kumtafuta dokta moses.
"Eeeh! Haba huyu hapo nimemuunganisha ongea naye.”
"Habari yako dokta mimi ni dokta Harun kutoka Dar es salaam."
“Aaah! Nishakukumbuka vipi huyo kichwa gumu anaendeleaje?"
"Kwanza dokta hutakiwi kutamka neno hilo pili huo udaktari wako wa kutoa dawa bila kipimo uliotoa wapi?"
Aliuliza kwa hasira isiyokuwa na kificho.
"Si dalili zilikuwa zinaonyesha tu."
"Sasa nitakuadhibisha kwa kupotosha watu na inawezekana hata huyo binti hana ebol......" Hata hakumalizia vizuri simu ilikatwa na kubaki akiongea na Andrew .
"Dokta kama kweli mwanetu hana ebola turuhusu twende kumuona ."
"Haina shida twendeni sote ." Wote walinyanyuka na kuelekea katika chumba alichokuwemo Rodrick bila hata kuvaa mavazi yeyote.
"Pole sana baba," Mama yake alitoa maneno hayo baada ya kufika ndani ya chumba cha Rodrick.
"Na hizi dripu za damu je?"
"Lazima atundikiwe ili kurejesha damu iliyopotea."
Kwa kiasi kikubwa familia hiyo ilipata amani hata waliporudi tena nyumbani mioyo yao ilikuwa na amani sana .
Mlango wa chumba namba 256 ulifunguliwa na mzee steven akiwa na mkewe ambamo ndani ya chumba hicho alikuwemo Rodrick siku ya pili yake saa 12:00 asubuhi.
"Waooooo! baba unaendeleaje?" Mama yake alifurahi baada ya kumkuta Rodrick amefumbua macho ila alikuwa haongei kutokana na oparashen ndogo aliyokuwa amefanyiwa chini ya ulimi.
"Atapona tu wala msijari ila dokta wa mwanza lazima awajibishwe kabisa na tayari nimeshamripoti!" Dokta Harun aliwafariji wazazi hao.

******

Ugonjwa wa ebola uliokuwa umeanza kuua wafungwa katika gereza la butimba na kulazimika kuzuiwa watu kutembelea hapo , taarifa hizo zililifikia shilika la Afya duniani na kulazimika kutoa misaada ya haraka sana ndani ya mji wa mwanza ambako hata wakazi wake hawakuruhusiwa kutoka wala wageni kuingia.
"Je yule mgonjwa alianza kuumwa ugonjwa huu yuko wapi?"
Aliuliza dokta collin mzee wa kizungu mfupi na mnene kiasi baada ya kutoa chanjo kwa wafungwa wote akiwa katika chumba cha mkuu wa gereza hilo, kwa lugha ya kigereza.
"Yuko bugando"
"Vipi hali yake?"
"Bado sana hata uhakika wa kupona haupo !"
"Duuuh! Niruhusu nimpeleke marekani kama hutojari na ataondoka na askari magereza!"
"Haina shida."
Kesho yake taratibu zilianza kufanyika za kumsafirisha Rhoda na afande Marry, siku tano kila kitu lilikuwa sawa na safari ilikuwa kesho yake .
"Ufike salama Rhoda." Mzee Hashim alimuaga Rhoda ambaye alikuwa hajitambui tena kutokana na hali kubadilika tena katika kiwanja cha ndege cha mwanza akiwa na askari magereza Marry.
Hakuondoka hapo hadi alipohakisha ndege hiyo kutoka marekan inaanza kuseleleka kabla ya kupaa ndipo alipogeuza shingo kuanza kuondoka lakini alishtuka baada ya kuhisi akiguswa begani.
"Rodrick?"
"Naaaam. Rhoda anaendeleaje?"
"Aaaakh! Khooo! Khoooo!" Alijikuta akishindwa kuongea na kuishia kukohoa huku akiwa na maswali kibao dhidi ya Rodrick

"Mama mimi kesho naenda mwanza!"Alisema Rodrick siku moja baada ya kutoka hospitali ya muhimbili akiwa amekaa juu ya kochi huku mkononi akiwa na glass ya juice ya embe.
"Lakini mwanangu mbona hali yako haijakaa vyema tulia kama wiki hivi ndo uende!" Mama Rodrick aliongea huku anafuta futa kabati.
"Hapana kuna mtu naenda kumshughulikia mama mimi nimeshapona kabisa si unaona!" Aliongea Rodrick huku akinyanyuka na kuanza kuruka ruka ili hali mwili wake ulikuwa bado dhaifu sana ila alifanya hivyo kumridhisha mama yake aamini kuwa mwanaye yuko salama.
"Kwa yule mwanamke aliekuambukiza? Eeeh!"
"Mmmmh! Mamu lazima.....!"
"Hakuna cha lazima hapa kaa mbali naye nisikuone tena na kesho huondoki alaaaa!" Alifyatua maneno hayo na kuondoka sebuleni hapo na kumuacha Rodrick akiwa hana raha.
"Nitakupigania hata kama umekufa " alijikuta akikumbuka maneno aliyowahi kuyatoa siku chache hospitali ya Bugando siku chache. 
"Nooo! Lazima niende mwanza tena leo hii tu!" Alinyanyuka na kuelekea chumbani kwake kisha alitoka akiwa ameficha hati yake ya kusafiria.
"Mama naenda kariakoo mara moja,"
"Haya uwahi kurudi!"
"Airpot!" Aliwaza Rodrick akiwa anafungua geti na kutoka nje kisha alichukua tax iliyompeleka kiwanja cha ndege kisha alisafiri hadi mwanza ambako anajikuta anapishana na Rhoda akiwa anapelekwa marekani kwa matibabu zaidi.

******


ITAENDELEA

Post a Comment

0 Comments