“unajua kabisa kuwa hivi sasa usiku umeshakuwa mkubwa na muda mwingi tulikua macho. Huoni kama mwenzako nimejawa na uchovu?” aliongea Diana huku akionyesha wazi kuwa alikua anatetea wazo lake la kwenda chumbani.
“kama wote tumejawa na uchovu, ni bora tungeenda nyumbani tu. Kwani kulikuwa kuna ulazima wa hicho kitu uniambie leo hii?” alongea Abdul huku akiwa amejawa na hofu kubwa kutokana na maamuzi hayo mazito aliyoyaamua mtoto wa bosi wake. “muda wenyewe ni mchache sana uliobakia kabla sijaondoka na kurudi tena chuo… isitoshe, kuonana na wewe ni ngumu sana na kupata muda kama huu.wa kuwa peke yetu… kwanini unakua sio muelewa Abdul?” aliongea Diana huku akionyesha wazi kuwa hataki kubadilisha mawazo yake.
“mimi ni muelewa sana Diana, ila wewe ndio huoni uzito uliopo kati yangu mimi kulala nje ya kambi yetu tena chumba kimoja na wewe. Hilo ndilo jambo ninalo lipinga mimi.” Aliongea Abdul kwa sauti iliyojaa huruma na kumuangalia Diana kama mtu aombaye msamaha kwa kosa Fulani hivi alilolomfanyia mpenzi wake.
“kwa hiyo wewe umeamuaje?” aliuliza kibabe Diana. “tuhairishe tu siku ya leo.. na ikiwezekana tukutane hata kesho.”
Aliongea Abdul na kumfanya Diana asimame kwa muda mrefu bila kuamua lolote. Alimuangalia Abdul na baadae akashusha pumzi na kumwambia Abdul waondoke maeneo yale.
Alipelekwa na gari mpaka kambini walipokuwa wanaishi wote kama makazi ya muda kwa ajili ya maandalizi ya shoo nyingine kubwa nchini Uturuki
Katika watu ambao hawakupata usingizi siku hiyo licha ya uchovu wa kazi nzito, alikuwa Sapna ambaye alikua anashuhudia kila kitu baada ya Abdul kushuka kwenye gari na Diana nae kushuka na kumbusu Abdul kwenye mashavu yake.
Sku ya pili yake, Diana alimpitia Abdul kambini mishale ya saa saba na kuondoka nae. Hali hiyo iliwafanya wana kikundi wote kuamini kuwa Abdul alikua anatembea na mtoto wa bosi wao. Wengi hawakukifurahia kitendo kile kwakua walijua kuwa ilikua ni dharau ya aina yake aliyoamua kumuonyeshea Mr. Zungu aliyewalea na kuwasomesha kwa gharama kubwa. Walijua kuwa lazima kitu kibaya kimtokee kama ukweli ukibainika kwa Mr.Zungu kuwa anatembea na mtoto wake wa pekee.
Diana alipaki gari kwenye hotel moja iliyopo pembeni kidogo ya jiji la Dar-es-salaam. Alipaki gari na kwenda na Abdul kwenda kupata chakula cha mchana. Walipomaliza kula, Abdul aliruhusu maongezi yao yaanze. “unajua toka siku ya kwanza kukuona, ulinishawishi niweze kukuona tena na tena. Yaani hata kama usingekuwa katika kundi hili, basi ningekutafuta kwa gharama yoyote ile.” Aliongea yule dada huku akionyesha kuwa alikua anafuraha kupita kiasi.
“nashukuru sana.” Alijibu Abdul huku na yeye akiachia tabasamu la wizi.
“unajua siku zote huwa nausikia tu moyo umempelekea mtu kufanya hivi, mara umempelekea mtu kufanya vile…. Ila siku hizi ndio nimeyajua mateso ya moyo pindi yatakapo kitu kwa mtu ambaye hana fikra za kukupa unachokihitaji.” Aliongea Diana na kumuacha Abdul njia panda. “una maanisha nini dada.. naona hilo fumbo ni tata kidogo kwangu.” Aliongea Abdul na kumuangalia Diana ambaye wakati huo hakuwa na ishara yoyote ya kucheka, aliashiria kuwa kile kitu ni kweli kinatoka moyoni.
“Abdul, sijawahi kupenda katika maisha yangu. Na wala sikujua nini maana ya upendo kutoka kwa mtu mwengine zaidi ya baba yangu kwakua ananipa kila nililolihitaji kutoka kwake. Ila kwa sasa nimegundua kuwa nampenda mtu mwengine mmbadala wa baba yangu. Tena huyu ni zaidi ya moto mkali umalizavyo kuni kwa jinsi alivyoingia moyoni mwangu kwa kasi na kunifanya nikae kwenye kipindi kigumu sana…. Mtu mwenyewe ninayemzungumzia hapa ni wewe Abdul. Una kila kitu ambacho nakihitaji mume wangu awe nacho. Kuanzia umbo, sauti na aina ya maisha yako unayoishi. Ni staa unayejiheshimu na unajua ufanye nini jukwaani ilimradi uwaridhishe mashabiki wako. Najua utakuwa unapendwa na wengi sana. Ila mpaka nimeamua kufunguka kwako tena ukizingatia sisi watoto wa kike tulivyokuwa wadhaifu na waoga wa kuongea hisia zetu juu ya wanaume tuwapendao ndio kabisaa… ila mpaka nimeongea basi ujue nimezidiwa mbaya Abdul… nakupenda, nakupenda sana Abdul.”
Maongezi ya Diana yaliendana na vitendo pamoja na hisia kali za mapenzi zilizomjia na kuanza kulia huku akimuangalia Abdul ambaye wakati ho alikua anamsoma Diana aliyekuwa mwekundu usoni akili lilia penzi lake.
Abdul alimuangalia Diana huku akiwa haamini alichokisikia kutoka kwa msichana huyo. Alimuangalia mrembo huyo aliyekuwa anabubujikwa na machozi huku sura yake ikibadilika rangi na kuwa nyekundu kutokana na kilio kilichoashiria uchungu utokao ndani ya moyo wake.
“unachokiongea ni kitu ambacho hakiwezekani Diana, hata kama nakupenda lakini utofauti wa madaraja kati yangu na yako ni kikwazo tosha katika mapenzi yetu. Mimi si tajiri kama baba yako. Mimi sina uwezo wa kulilinda penzi letu mbele ya baba yako. Yote tisa. Mimi naishi katika mgongo wa baba yako. Namtegemea kwa kla kitu. Sitakuwa na fadhila kama nitadiriki kutembea na wewe. Japo hatukuzaliwa tumbo moja, ila nimefunzwa kukuheshimu kama dada yangu. So, just forget about that issue.”
Aliongea Abdul na kumfanya huyo dada azidi kububujikwa na machozi. Ilimuuma sana kusikia maneno kama hayo yakitoka mdomoni mwa Abdul. Alimuangalia na kuanza kulia kwa sauti.
“noo… usilie Diana. Huo ndio ukweli ninaopaswa kukuambia, la sivyo nitakua najipalia mkaa kwa kukubali kuwa na wewe kimapenzi. Mimi ni nazi siwezi kushindana na jiwe, sana sana nitaumia mimi Diana. Nakuomba unielewe.” Aliongea Abdul na kummbembeleza Diana ambaye mpaka wakati huo alikua anali kwa kwikwi. “nakupenda abdul, usinifanyie hivyo.” Aliongea Diana huku akiendelea kulia “sio kwamba sikupendi. Nakupenda sana ila nahofia usalama wangu Diana.” Aliongea Abdul huku na yeye akionyesha ishara ya kulengwa lengwa na machozi.
Diana alimuangalia Abdul na kugundua kuwa alijawa na hofu kubwa. “mapenzi ni kitu kinachojitegemea Abdul. Hakuna anyeweza kuniingilia katika maamuzi yangu, hata baba yangu hawezi kunizuia kuwa na uhusiano na wewe kwa sababu anaziheshmu hisia zangu.” Aliongea Diana na kuonyesha ishara zote za kuwa katika hali ya kawaida baada ya kupata majibu yaliyo mpa uhai wa maamuzi ya kuwa na Abdul. “nipe muda nilifikirie kwa kina swala hili… maana maamuzi haya siyo ya kubeza wala kukurupuka.” Aliongea Abdul baada ya kujiona anazidiwa na maamuzi yake ambayo alishaanza kuweka wazi hisia zake juu ya mrembo huyo.
“nategemea majibu chanya kutoka kwako.” Aliongea Diana na kumuangalia Abdul.
Baada ya hapo hawakuona haja ya kuendelea kukaa pale, Abdul alirudishwa kambini na Diana akaenda nyumbani kwao.
Sapna alikua ni mmoja kati ya watu waliokuwa wanaumia bila sababu juu ya Abdul. Alikaa macho pima kutazama muenendo mpya wa Abdul kwa siku za hivi karibuni. Alikaa na kumuangalia Abdul ambaye alikua anaingia muda huo. Alikaa na kumtazama wakati Abdul alipokuwa anasalimiana na wenzake ambao walikua wanamshangaa pia. “mwanangu unapoelekea sio, unacheza makida kwenye nyaya za umeme.” Aliongea mmoja katika kundi la Dreams. “kwanini Adam?” aliuliza Abdul kwa mshangao. “we unaona uko sawa kabisa?” aliuliza mtu mwengine aliyekuwa pembeni. “ndio mnieleweshe sasa?” aliongea Abdul baada ya kukaa na wenzake. “usifikiri watu hawajui kama umeanzisha uhusiano na mtoto wa Mr. Zungu. Hivi hujifikirii hata wapi ulipotoka Abdul?” alionge Adam na kumuangalia Abdul ambaye alikuwa anawaangalia rafiki zake kwa zamu.
“jamani hizo hisia zenu wala hazina ukweli ndani yake. Mimi nina akili timamu na wala siwezi kufanya huo ujinga, najua ni wapi Mr. Zungu amenitoa hivyo siwezi kufanya huo ujinga kabisa.” Aliongea Abdul na kuwaangalia wenzake ambao hawakua na hisia za kumuamini. “mbona siku hizi umebadilika sana. Hupandi basi la bendi yetu. Unaletwa na kuchukuliwa muda wowote na Diana?.. hata kama sio kweli ila mzee akijua unafikiri atakufikiriaje?” aliongea Adam maneno yaliyomuingia sana Abdul na kumamfaya ajiinamie. “hilo nalo neno” aliongea Abdul na kukiri kuwa alikua anakosea.
Baada ya kuongea maneno yale, simu yake iliita. Aliichukua na kuangalia jina kwenye screen ya simu yake, na kugundua kuwa apigaye simu hiyo ni Diana. Alinyanyuka na kwenda chumbani kwake. Adam na wenzake wakabaki wanasikitika.
“niambie penzi wangu.” Alionge Diana baada ya Abdul kupoke simu yake. “sina usemi wangu. Niambie?” aliongea Abdul huku akitabasamu. “nimetokea kufurahi sana uwepo wako wa kuwa karibu na mimi kwa muda mrefu siku ya leo. Nakupenda sana Abdul na natamani kila nukta ya dakika isogeayo niwe ubavuni mwako mpenzi wangu.” Aliongea Diana na kumfanya Abdul kushusha pumzi ndefu. “Ahsante.” Aliitikia Abdul kiufupi.
“sasa, ni lini tena tutapata nafasi ya kuongea na kujadili juu ya issue yetu tuliyoonga, maana nahisi nachelewa kukuta mume wangu?” aliuliza Diana swali lililomfaya Abdul achelewe kujibu kwa sekunde kadhaa. “next week mine.” Alijibu Abdul baada ya muda. “naona mbali sana wangu… ila kwa ajili yako nitavumlia. Moyo wangu una nafasi moja tu kwa ajili yako. Usiniangushe Abdul, mwanaume wa ndoto zangu.” Aliongea Diana maneno ya mahaba yaliyomfanya Abdul ashindwe kutoka katika mitego ya msichana huyo ambaye ni hatari kuwa nae.
“sawa, nakutakia siku njema.” Aliongea Abdul na kusikilizia kitu atakachojibu Diana. “na wewe pia.” Alijibu Diana na kukata simu.
Abdul alijitupa kitandani na kuanza kufukiria kwa kina maneno yale matamu ya msichana Diana. Na muda huo huo aliyafikiria maneno ya marafiki zake walikuwa wanamtakia mema kila siku kwa kumtahadharisha si kuwa na uhusuiano nae wa kimapenzi tu, bali hata kuwa nae karibu kunaweza kumsababishia matatizo kutoka kwa Mr Zungu ambaye ndio tajiri wao aliyewapa mali na kila kitu wanachomiliki.
Alishindwa ni lipi aamue, alilala na kuwaza sana mpaka kiza kikaingia. Sapna aligonga hodi chumbani kwake na alipofungua tu mlango, alikutana na mrembo huyo alyekuwa amemletea chakula.
“ahsante sana.” Alijibu Abdul baada ya kukipokea kile chakula na Sapna akageuka na kuanza kuondoka.
“samahani Sapna,..na weza kuongea na wewe usiku huu?” aliuliza Abdul baada ya kumuona Sapna akizihesabu hatua zake kuelekea alikotoka, Sauti ile ya Abdul iliyokuwa imelitaja jina lake, Ilimfanya Sapna ageuze shingo yake haraka na kumsikiliza Abdul kitu alichtaka kumwambia. “hamna shida, ukimaliza kula utanikuta kwenye bustani nabembea.” Aliongea aliongea Sapna na kuendele na safari yake.
Abdul alikula haraka na baada ya kumaliza, alitoka nje na kwenda kwenye bustani na kumkuta Sapna anabembea. Alifika mpaka pale na kunza kumtazama mrmbo huyo aliyeachia tabasamu la nguvu baada ya kumuona yeye maeneo yale.
Ailmsogelea na yeye na kukaa kwenye bembea hiyo iliyowaruhusu watu wa tatu kukaa. Abdul alimuangalia Sapna ambaye wakati wote na yeye alikua hapepesi macho yake kumuangalia Abdul kama ishara ya kuwa na hamu ya kutaka kujua kitu alich Itiwa na yeye. “nimechelewa sana.” Abdul alifungua mjadala wao kwa style hiyo. “umewahi sana, au hukula kabisa?” aliuliza Sapna na kumuangalia Abdul. “nimekula ila kwa haraka sana kwa kuhofia kukuweka sana.” Aliongea Abdul huku akionyesha ni jinsi gani alivyokuwa ana hamu ya kuongea nae kitu alichokuwa anataka kumwambia Sapna kwa siku hiyo.
“lete mpya.” Aliongea Sapna na kumuangalia Abdul.
“samahani kama nitatokea kukukwaza kwa haya nitakayoongea mbele yako. Najua ni jinsi gani tunavyo heshimiana na kukubali kwa dhati kabisa kuwa sisi ni ndugu wa damu. Tumelelewa na watu waliotufundisha kuthaminiana na kila mmoja kumpa heshima mwenzake. Ila kwa upande mwengine wa shilingi hisia ni kitu kingine kabisa. Ni siri niliyokuwa nimeiweka kwa muda sasa. Na nafikiri huu ni wakati mzuri wa wewe kujua kile kilichopo moyoni mwangu. .. upo tayari?”
Aliongea Abdul maneno hayo bila ya kumuangalia usoni Sapna. Alipomaliza na swali hilo ndipo alipounyanyua uso wake na kumuangalia Sapna kwa kumkazia macho kidogo. Wakati wote huo, Sapna alikua makini kumsikiliza Abdul.
“nipo tayari.” Alijibu Sapna na kumuangalia Abdul aliyekuwa anaonyesha kuwa ameridhika na jibu lile.
“nikisemacho ni hisia zangu tu, na haimaanishi kuwa nimeamua kukutukana au kuvunja miiko ya umoja wetu. Ni ukwelii kutoka moyoni mwangu kabisa. …… NAKUPENDA SANA SAPNA.”
Aliongea Abdul na kumuangalia Sapna ambaye hakuwa na la kujibu zaidi ya kutumbua tu macho katika hali ya kutoamini alichokisikia kutoka kwa Abdul. Baada ya Abdul kuongea maneno yale, alimuangalia Sapna ambaye bado alikuwa amepigwa na butwaa, akaamua kunyanyuka na kumshika mkono wake wa kulia.
“uko huru kutoa jibu lolote na kwa wakati wowote,… usiku mwema Sapna.” Aliongea Abdul na kuuachia mkono wa Sapna na kuaza kupiga hatua kuelekea chumbani kwake.
Sapna alibaki ameshangaa pale pale bila kujibu chochote, mara machozi ya furaha yalianza kumtoka baada ya Abdul kutoweka katika upeo wa macho yake. Alitamani anyanyuke na kumfuata, ila staha ya kundi lao liliwabana vizuri. Maneno yale yalikuwa matamu na yenye faraja kama mfungwa aliyeambiwa kuwa amesamehewa na anaachiwa huru siku hiyo baada ya mateso ya miaka kadhaa. Sapna alimshukuru mungu kwa kumjaalia kupata mvulana ambaye ndio chaguo halisi la moyo wake.
Alinyanyuka pale alipokaa baada ya kupoteza muda ambao hata yeye mwenyewe hakuukumbuka. Akaenda chumbani kwake na kujilaza kitandani.
Usingizi haukupatikana zaidi ya kuusumbua ubongo kwa kufikiria maisha yao ya mbele yatakavyokuwa.
Abdul nae aliiporudi chumbani kwake alikaa kitandani na kuanza kuchuja mawazo yake, wakati huo alijaribu kuangalia upendo aliokuwa nao kwa Sapna na upande mwengine pia mtoto wa bosi wake naye alikua anamuhitaji kupita maelezo.
Alichekecha kichwa usiku kucha, lakini majibu aliyoyapata ni kwamba alikua anampenda sana Sapna kuliko Diana.
Mchana wa siku ya pili yake, Diana alienda tena kambini kuangalia mazoezi waliyokuwa wanafanya wakina Abdul. Alikaa mpaka yalipomalizika jioni, alipiga makofi na kumsogelea Abdul na kushika mkono. Sapna alimkata jicho la chuki lakini halikuweza kuwatenganisha mikono yao.
“twende sehemu tukaongee kidogo Abdul.” Aliongea Diana kwa sauti iliyosikika na kila mtu pale walipokuwepo. Abdul aligeuza shingo yake na kumuangalia Sapna ambaye naye aligeuza shingo yake na kujifanya yupo bize na ishu nyengine. Alimuangalia Diana ambaye wakati huo alishaanza kumvuta bila kusubiri jibu kutoka kwake kama amekubali au laa.
Abdul alivutwa na kupelekwa kwenye gari alilokuja nalo Diana na safari ya kuelekea sehemu ambayo Abdul hakuijua ilianzia hapo.
Walifika maeneo ya kibaha kwenye hotel moja iliyokuwa karibu na hospitali ya Tumbi na Diana akatafuta parking na kupaki gari yake. Alishuka na kuigia nae kwenye hotel hiyo. Hawakupita mapokezi kama alivyozoea kuona Abdul, alishangaa anapelekwa kwenye chumba kimoja wapo kwenye ile hotel yenye hadhi mkoa wa pwani.
“Surprise, .. hiyo suti ni yako. Unatakiwa ukaoge na ubadilishe nguo hizo.” Aliongea Diana na kumuangalia Abdul kwa mapozi ya hali ya juu. Abdul alishindwa kushangaa. Maana hakujua vitu vyote hivyo Diana aliviandaa muda gani.
Hakuwa na sababu ya ubishi, alinyanyuka na kwenda bafuni kuoga. Alipotoka kuoga hakumkuta Diana mule ndani, aliangaza huku na huko na kukikuta kikaratasi kidogo kilicho mfahamisha kuwa Diana alikua nje anamsubiri.
Alizivaa zile suti zilizo nakshiwa kwa ubunifu wa hali ya juu sana. Alipozivaa, zilikuwa kama ametengenezewa yeye toka kiwandani. Maana zilimkaa na kumpa muonekano tofauti kabisa. Pembeni ya ile Dressing table aliona kofia aina ya Cow boy. Akachukua na kuitinga kichwani kwake.
“woooooh”
Aalijikuta amejishangaa mwenyewe kwa jinsi alivyopendeza baada ya kutupa macho yake kwenye kioo kilichopo mbele yake. Viatu viliyokuwa na nakshi iliyofanana na hiyo suti, vilimkaa mpaka akshangaa upeo wa Diana katika kujua saize yake kabla ya kumpima.
Alitoka nje na kukutana na Diana aliyekuwa nje ya mlango akimsubiri.
“woooh… AMAZING!!!”
Alijikuta Diana akiongea maneno hayo baada ya kumuona Abdul akiwa tofauti kabisa. Alimfuata na kupitisha mkono wake katikati ya mkono wa Abdul na kuaza kumkokota. Walifika kwenye ukumbi mkubwa wa hiyo hotel ambao ulikuwa una watu wengi waliokuwa wapo wawili wawili.
Wazungu na mataifa mengine pia walikuwepo kwenye sherehe hiyo ambayo Abdul hakuwa na taarifa nayo hapo awali. Watu wengi waligeuza shingo zao kuwatazama wao walipokuwa wanaingia. Mara wakaanza kupiga makofi. Wakati wote huo walikua pamoja na walizidi kusonga mbele kwa kupitia capet jekundu lililotandiwa kuazia mlangoni mpaka stejini.
0 Comments